jinsi ya kuwasiliana na tume - des moines, iowa and human...• wakala wa mali yasiyohamishika...

2
Ikiwa unahisi kuwa umebaguliwa, tungependa kusikia kutoka kwako. Jinsi ya Kuwasiliana na Tume Unaweza kupiga simu: Simu: (515) 283-4284 Faksi: (515) 237-1408 Jumatatu hadi Ijumaa saa 8:00 asubuhi hadi 5:00 jioni. Mtandaoni: www.HumanRightsDSM.org www.facebook.com/DSMCivilHumanRights Barua pepe [email protected] Haki za Raia na Binadamu za Des Moines Kukuza Nafasi na Haki Kwa Wote 602 Robert D. Ray Drive Armory Building Des Moines, Iowa 50309 Wageni wanapokelewa kwa miadi au ziara za bila miadi. Je, Unabaguliwa? Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ni idara ya serikali ya jiji inayotekeleza sheria za nyumba sawa katika Jiji la Des Moines. Ikiwa unadhani kuwa umebaguliwa katika utoaji makao, unapaswa kuwasiliana na Tume. Tume itachunguza malalamishi yako bila malipo kuona ikiwa sheria ilivunjwa. Ikiwa kuna ukiukaji, Tume inaweza kukusaidia kupata masuluhisho ya kisheria ambayo ni haki yako. Ikihitajika, Tume inaweza kufanya vikao vya kesi au kuwasilisha kesi za ubaguzi mahakamani. Ubaguzi unaweza kuwa nyeti. Mara nyingi watu wanaweza kushuku kuwa wamebaguliwa, lakini wasiwe na uhakika wa kuuthibitisha. Wasiliana na Tume ikiwa unashuku kwamba umebaguliwa. Wasiliana nasi leo bila malipo na kwa usaidizi wa siri. 515-283-4284 Jua haki zako unapopangisha au kununua nyumba #JuaHakiZakoDSM M a e l e z o y a N y u m b a I n a y o f a a

Upload: others

Post on 31-Dec-2019

1 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Jinsi ya Kuwasiliana na Tume - Des Moines, Iowa and Human...• Wakala wa mali yasiyohamishika anajaribu kumshawishi mtu kutonunua wala kupangisha nyumba katika mtaa fulani. Huku kunaitwa

Ikiwa unahisi kuwa umebaguliwa, tungependa kusikia kutoka kwako.

Jinsi ya Kuwasiliana na Tume Unaweza kupiga simu:Simu: (515) 283-4284Faksi: (515) 237-1408

Jumatatu hadi Ijumaa saa 8:00 asubuhi hadi 5:00 jioni.

Mtandaoni:www.HumanRightsDSM.orgwww.facebook.com/DSMCivilHumanRights

Barua [email protected]

Haki za Raia na Binadamu za Des MoinesKukuza Nafasi na Haki Kwa Wote

602 Robert D. Ray DriveArmory Building

Des Moines, Iowa 50309 Wageni wanapokelewa kwa miadi au ziara za bila miadi.

Je, Unabaguliwa?

Tume ya Haki za Raia na Binadamu ya Des Moines ni idara ya serikali ya jiji inayotekeleza sheria za nyumba sawa katika Jiji la Des Moines.

Ikiwa unadhani kuwa umebaguliwa katika utoaji makao, unapaswa kuwasiliana na Tume.

Tume itachunguza malalamishi yako bila malipo kuona ikiwa sheria ilivunjwa. Ikiwa kuna ukiukaji, Tume inaweza kukusaidia kupata masuluhisho ya kisheria ambayo ni haki yako. Ikihitajika, Tume inaweza kufanya vikao vya kesi au kuwasilisha kesi za ubaguzi mahakamani.

Ubaguzi unaweza kuwa nyeti. Mara nyingi watu wanaweza kushuku kuwa wamebaguliwa, lakini wasiwe na uhakika wa kuuthibitisha. Wasiliana na Tume ikiwa unashuku kwamba umebaguliwa.

Wasiliana nasi leo bila malipo na kwa usaidizi wa siri.515-283-4284

Jua haki zako unapopangisha au kununua nyumba

#JuaHakiZakoDSM

Maelezo ya Nyumba Inayofaa

Page 2: Jinsi ya Kuwasiliana na Tume - Des Moines, Iowa and Human...• Wakala wa mali yasiyohamishika anajaribu kumshawishi mtu kutonunua wala kupangisha nyumba katika mtaa fulani. Huku kunaitwa

• Wakala wa mali yasiyohamishika anajaribu kumshawishi mtu kutonunua wala kupangisha nyumba katika mtaa fulani. Huku kunaitwa kuelekeza.

• Mwenye nyumba anakataa kupangisha ghorofa kwa mtu anayehitaji kwa sababu mtu huyo ana ulemavu wa akili.

• Mtu mweusi anajibu tangazo la gazeti lililo na ghorofa. Mwenye nyumba anamwambia kuwa ghorofa tayari imepangishwa. Baadaye inajulikana kuwa ghorofa haikupangishwa na mwenye nyumba baadaye anaipangisha kwa mtu mweupe anayejibu tangazo lilo hilo.

• Mwenye nyumba anamfurusha mpangaji mweupe kutoka kwenye nyumba yake kwa sababu marafiki zake weusi humtembelea hapo.

• Meneja wa makazi anakataa kupangisha ghorofa kwa familia yenye watoto, ataruhusu tu familia zenye watoto kuishi katika majengo fulani au kwenye ghorofa fulani, au anazitoza familia zenye watoto arbuni ghali za usalama.

• Meneja wa jengo anakataa kupangisha ghorofa kwa familia ya kigeni au Kiislamu, lakini ataipangisha kwa familia inayoonekana kuwa ya “Marekani.”

• Mwenye nyumba anaangalia rekodi za mikopo za watu wote waliotuma maombi ambao ni weusi na Wahispania na anatumia matatizo ya madogo ya mikopo kama sababu ya kukataa kuwapangishia; hata hivyo, mwenye nyumba huwa haangalii mara kwa mara rekodi za mikopo za watumaji ombi weupe au hupuuza matatizo madogo ya mikopo katika rekodi zao.

• Benki inakataa kukopesha hela kwa mnunuzi wa nyumba anayetaka kununua nyumba katika mtaa wa wachache. Huku kunaitwa kukataa.

• Meneja wa upangishaji anatoza watu wasio weupe au wapangaji wanawake arbuni ghali ya usalama, au kodi ya juu kuliko wapangaji weupe wanaume.

• Mpangaji wa kike na familia yake wanafurushwa kwenye ghorofa yao kwa sababu alikataa kutimiza haja za mapenzi za mwenye nyumba.

• Mwenye nyumba anakataa kupangisha ghorofa kwa mtu aliye na mnyama wa huduma. Mwenye nyumba anamchukulia mnyama kuwa mnyama kipenzi.

Ubaguzi wa Nyumba ni kinyume cha Sheria katika Jiji la Des Moines

Sheria inapiga marufuku vitendo vifuatavyo kwa msingi wa mbari, rangi, dini, jinsia, asili ya taifa, ulemavu wa mwili au akili, hadhi ya familia, imani, kizazi, mvuto wa jinsia, utambulisho wa jinsia na/ulipizaji kisasi.

• Kukataa kuuza au kupangisha nyumba • Kudanganya kuhusu uwepo wa nyumba • Kumfurusha mtu kwenye nyumba• Kubagua katika nyumba: kodi, usalama

wa vituo

Ikiwa unahisi kuwa umekumbana na hali zozote zilizoelezwa katika brosha hii, au chochote kinachofanana, tafadhali wasiliana na ofisi yetu leo ili upate usaidizi wa BILA MALIPO na wa SIRI.

Mifano ya Ubaguzi wa Nyumba:

515-283-4284