ijtihad na taqlid - al mustakshif abu manal danah

927
1 IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM : MAIMAMU NA MADHHAB KATIKA UISLAM. TOLEO LA TATU. KIMETAYARISHWA NA AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH. KIMECHAPISHWA NEW DELHI, INDIA RAMADHAN 1438 Al Hijr, 2017

Upload: chadmcrash

Post on 10-Jan-2021

23 views

Category:

Education


2 download

DESCRIPTION

Ijtihad Na Taqlid - Al Mustakshif Abu Manal Danah. Historia ya Uislamu, Maimamu na Madhhab Yao Katika Uislam

TRANSCRIPT

  • 1

    IJTIHAD NA TAQLID HISTORIA YA UISLAM : MAIMAMU

    NA MADHHAB KATIKA UISLAM.

    TOLEO LA TATU.

    KIMETAYARISHWA NA

    AL MUSTAKSHIF ABU MANAL DANAH.

    KIMECHAPISHWA NEW DELHI, INDIA

    RAMADHAN 1438 Al Hijr, 2017

  • 2

    ﴾اهللَِّ الرَّْمحَـِن الرَِّحيمِ ِبْسِم ﴿ ُفِسَنا َوِمْن إنَّ اْحلَْمَد هللَِِّ َحنَْمُدُه وَنْسَتِعيُنُه َوَنْستَـْغِفرُُه َونـَُعوُذ اِبهللَِّ ِمْن ُشُروِر أَنْـ

    ُ َفَال ُمِضلَّ َلُه َوَمْن َال َهاِدَي َلُه ُيْضِلْل فَ َسيَِّئاِت أَْعَمالَِنا، َمْن يـَْهِدِه اهللًَّدا َعْبُدُه َوَرُسوُلهُ ُ َوْحَدُه َال َشرِيَك َلُه َوأْشَهُد أنَّ حمَُمَّ َوأْشَهُد أْن َال ِإَلَه ِإالَّ اهللَّBismillahi Rahman Rahim, Inna Al-hamda Lillaahi nahmaduhu wanasta’eenahu wa nastaghfiruhu, wa na’oodhu billaahi min shuroori anfusinaa wa min sayi’aati aA’maalinaa. Man yahdih - Illaahu falaa mudhilla laahu wa man yudhlil falaa haadiya lahu. Wa ashhadu an laa ilaaha ill-Allaahu wahdahu laa shareekallahu, wa ashhadu anna Muhammadan ‘abduhu wa rasooluhu.

    Tafsir: Kwa jina la Allah, ambae anastahiki shukrani zote, tunaemuomba msaada na msamaha wake. Tunajilinda kwa Allah na kila maovu ya Nafsi zetu na mambo mabaya yetu. Kwani kwa hakika mtu yeyote yule alieongozwa na Allah basi hakuna atakaempotoa, na aliepotoshwa na Allah basi hakuna atakaemuongoa. Nnashuhudia kua hakuna anaepaswa kuabudiwa isipokua Allah pekee asiekua na mshirika, na nnashuhudia kua Muhammad (Salallahu A’layhi wa Salam) ni Mtume wake.

    يـَُقوُل هللاُ َعزَّ َوَجلَّ

    ﴾الَّ َوأَنُتم مُّْسِلُمونَ إِ ُقواْ اهللََّ َحقَّ تـَُقاتِِه َوالَ َمتُوُتنَّ �َيـَُّها الَِّذيَن َءاَمُنواْ اتـَّ ﴿ Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha haqqa tuqatihi wala tamootunna illa waantum muslimoona (Surat Al Imran 3:102)

    Tafsir: Enyi mlioamini! Muogopeni Allah (kwa kutekeleza maamrisho yake na kuachana na makatazo yake) kama anavyotahiki kuogopewa. [Mtiini, mshukuruni na daima mkumbukeni], na msife isipokua katika hali ya kua ni Waislam.

  • 3

    َها نـَّْفٍس َوِحَدٍة َوخَ ِمنْ يَـأَيـَُّها النَّاُس اتـَُّقواْ رَبَُّكُم الَِّذى َخَلَقُكمْ ﴿ َلَق ِمنـَْ الَِّذى َتَسآَءُلوَن بِِه ُهَما رَِجاًال َكِثرياً َوِنَسآًء َواتـَُّقواْ اهللَّ َزْوَجَها َوَبثَّ ِمنـْ

    َ َكاَن َعَلْيُكْم َرِقيباً اْألَ وَ ﴾ْرَحاَم ِإنَّ اهللَّ Ya ayyuha alnnasu ittaqoo rabbakumu alladhi khalaqakum min Nafsin wahidatin wakhalaqa minha zawjaha wabaththa minhuma rijalan kathiran wanisaan waittaqoo Allaha alladhii tasaaloona bihi waal-arhama inna Allaha kana AAalaykum raqeeban (Surat An Nisaa 4:1)

    Tafsiri: Enyi Watu! Mcheni Mola wenu aliekuumbeni kutokana na Nafsi moja (Adam), na kutokana nae (Adam) akamuumba mke wake (Hawwa), na kutokana na wao akawaumba wanaume na wanawake wengi na muogopeni Allah ambae ana haki juu yenu, na msivinje udugu, kwani kwa Hakika Allah ni mwenye uangalifu juu yenu.

    َ َوُقوُلواْ قـَْوًال َسِديداً ﴿�َيـَُّها الَّ ِلْح َلُكْم َأْعَمـَلُكْم ُيصْ -ِذيَن َءاَمُنواْ اتـَُّقواْ اهللَّ﴾اً َعِظيماً فـََقْد فَاَز فـَْوز َويـَْغِفْر َلُكْم ُذنُوَبُكْم َوَمن ُيِطِع اهللََّ َوَرُسوَلهُ

    Ya ayyuha alladhina amanoo ittaqoo Allaha waqooloo qawlan sadeedan, Yuslih lakum aAAmalakum wayaghfir lakum dhunoobakum waman yutiAAi Allaha warasoolahu faqad faza fawzan AAadhiman (Al Ahzab 33:70-71)

    Tafsir: Enyi Mlioamini! mcheni na mumuogope Allah, na (daima) semeni kweli, atakuongozeni kufanya mema na kukusameheni dhambi zenu. Na kwa hakika yeoyote yule ambae anaemtii Allah na Mtume wake (Salallahu A’layhi wa Salam) atakua ni miongoni mwa waliofuzu.

    Allahuma J’alna minna al faizin fawzan A’adhimah…Aamin

  • 4

    YALIYOMO IJTIHAD NA TAQLID........................................................................................ 1 YALIYOMO ....................................................................................................... 4 UTANGULIZI. ................................................................................................. 15 SURA YA KWANZA ....................................................................................... 18 ASILI NA MAANA YA NENO DINI. ..................................................... 18 KUUMBWA KWA ULIMWENGU. ........................................................ 23 KUUMBWA KWA MALAIKA NA MAJINI. ............................................ 28 KUUMBWA KWA NABII ADAM. ......................................................... 31 BANI ADAM NA AL AMANAH. ............................................................... 43 KUUMBWA KWA HAWA ..................................................................... 48 KUSHUKA DUNIANI KWA ADAM NA HAWA. .................................. 51 ASILI YA UISLAMU. ............................................................................. 59 MITUME NA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QUR’AN. ............... 63 MAANA YA MIUJIZA. ........................................................................... 70 KHALILU ALLAH IBRAHIM A’LAYHI SALAAM ..................................... 84 ASILI YA MJI WA MAKKAH NA UKOO WA QURAYSH. ................... 89 ASILI YA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM.. 101 KUZALIWA KWA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM ................................................................................................... 108 MAISHA YA UTUME WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. ............................................................................................ 112 WAKE WA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM. ............................................................................................................... 128 SURIYYAH NA MILK AL YAMIN KATIKA UISLAM ........................... 137 MFUMO WA UTUMWA NA MATEKA WA VITA KATIKA UISLAM. ............................................................................................................... 142 AAL, AHL, ZAWJ NA QAWWAM KATIKA UISLAM. ............................ 150 SURA YA PILI ............................................................................................... 171 MAANA YA TAQLID ............................................................................ 172 MAANA YA FIQH. ............................................................................... 172 MAANAYA USUL UL FIQH NA MIFUMO YA USUL. ....................... 172 TAKLIF NA MUKALLAF KATIKA UISLAM. ....................................... 175 MAANA YA SHARIA’H NA TASHRI’I ................................................. 176 AL HUKMU AL SHARI’I. ....................................................................... 182 MAQASID ASH SHARIA’H – MAKUSUDIO YA SHARIA’H ................. 184 UHUSIANO BAINA YA MAQASID ASH SHARIA’H NA FIQH. ...... 191

  • 5

    AINA ZA HUKMU AL TAKLIFI ............................................................ 193 MAQASID ASH SHARIA’H NA USUL UL FIQH .................................... 196 MAANA YA IJTIHAD. .......................................................................... 198 SIFA ZINAZOHITAJIKA KATIKA KUFANYA IJTIHAD. .................. 198 UMUHIMU WA SANAD KATIKA KUFANYA IJTIHAD. ................... 199 HISTORIA YA ISNAD KATIKA UISLAM............................................ 202 DARJA ZA HADITH KULINGANA NA ISNAD ZAKE. ....................... 205 AINA ZA MUJTAHID. ........................................................................... 212 WANAZUONI NA TAQLID .................................................................. 213 TAQLID KATIKA IMANI NA AQIDA. .................................................. 215 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA QUR’AN NA SUNNAH. ...................... 216 SURA YA TATU ............................................................................................ 226 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA WAKATI WA MASAHABA. ............ 226 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA UONGOZI WA ABU BAKR AS SIDDIQ (11-13 A.H) ............................................................................................ 235 ABU BAKR NA JEMEDARI KHALID IBN WALID (SAIFU ALLAH). 238 HISTORIA YA MAISHA YA KHALID IBN WALID KABLA YA UISLAM ................................................................................................ 238 KHALID IBN WALID NA VITA VYA UHUD. .................................... 241 KUSILIMU KWA KHALID IBN WALID. ............................................ 245 KHALID IBN WALID NA VITA VYA MUTAH .................................. 250 MATAYARISHO YA VITA VYA TABUK ........................................... 254 KHALID IBN WALID NA VITA VYA YAMAMAH............................ 255 KHALID IBN WALID NA VITA VYA YARMOUK ............................ 264 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA UONGOZI WA UMAR IBN AL KHATTAB R.A (13-24 A.H). ................................................................. 270 KHALID IBN WALID NA KUSALIMU AMRI KWA MJI WA JERUSALEM ......................................................................................... 270 KHALID IBN WALID NA VITA VYA QINNASIRIN (ALLEPO)........ 274 KUFARIKI KWA KHALID IBN WALID (SAIF ALLAH)...................... 275 UMAR IBN AL KHATTAB NA ABD ALLAH IBN ‘ABBAS .............. 278 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA UONGOZI WA UTHMAN IBN AFFAN (24-35 A.H) ............................................................................................ 294 IJTIHAD NA TAQLID KATIKA UONGOZI WA ALI IBN ABI TALIB (35-40 A.H). ........................................................................................... 299 VITA VYA MWANZO BAINA YA WAISLAMU: VITA VYA NGAMIA. ............................................................................................................... 303

  • 6

    VITA VYA PILI BAINA YA WAISLAMU: VITA VYA SIFFIN .......... 304 ABD ALLAH IBN ‘ABBAS NA AL MUHAKKIMAH. .......................... 306 SURA YA NNE ............................................................................................... 310 UTAWALA WA BANU UMAYYAD WA DAMASCUS. .................... 310 ABD ALLAH IBN ABBAS NA MUAWWIYAH. ................................. 311 UTAWALA WA UMAR IBN ABD AL ‘AZIZ (99-101 A.H). .............. 315 UTAWALA WA AL ‘ABBAS WA BAGHDAD. ................................... 328 NIZAM AL MULK NA UTAWALA WA SELJUQ ............................... 331 MUJADDID IMAM AL GHAZAL NA MADRASAT AL NIZAMIYYAH. 333 UTAWALA WA SALAH AD DIN YUSUF IBN AYYUB..................... 338 WAMONGOLIA KATIKA HISTORIA YA UISLAMU. ....................... 343 UMUHIMU WA MJI WA JERUSALEM KWA DINI YA KIISLAM .... 344 USTAARABU WA KIISLAMU KIUTAMADUNI NA UVUMBUZI WA KISAYANSI KATIKA HISTORIA YA DUNIA. ................................... 351 BAADHI YA MANENO YA KIZUNGU YENYE ASILI YA KIARABU. ............................................................................................................... 358 SURA YA TANO ............................................................................................ 361 KALIMAT TAWHID – KALIMAT TAYYIBA - LA ILAHA ILA ALLAH NA MASHARTI YAKE................................................................................ 361 MADHHAB KATIKA HISTORIA YA UISLAM. ................................... 370 KUFUNGWA KWA MILANGO YA IJTIHAD. ..................................... 373 MFUMO WA KUTOA HUKMU KATIKA MADHHAB. ....................... 373 HISTORIA YA MAIMAM NA MADHHAB YAO. ................................ 374 IMAM JABIR IBN ZAID, ABD ALLAH IBN IBADHI NA MADHHAB YA IBADHI (22-93 Al Hijr). .................................................................. 377 MAKUNDI YALIYOTOKA NDANI YA MADHHAB YA IBADHI. ..... 383 VYANZO VYA MSINGI WA FIQH YA IBADHI. ................................ 386 WANAZUONI MAARUFU WA MADHHAB YA IBADHI. .................. 387 IMAM JAFAR AS SIDDIQ NA MADHHAB YA SHIA (80-148 Al Hijr) ............................................................................................................... 388 MAKUNDI YA WAFUASI WA MADHHAB YA SHIA. ....................... 394 MTAZAMO WA MADHHAB YA SHIA JAFARI KUHUSIANA NA SHUTMA JUU YA SHAHADA, TAHRIF, UCHANGANYAJI SALA, KUWATUSI MASAHABA, TURBAH, N.K ........................................... 396 VYANZO VYA MSINGI WA FIQH YA SHIA JAFARI. ..................... 404 WANAZUONI MAARUFU WA MADHHAB YA SHIA ........................ 404 IMAM ABU HANIFA NA MADHHAB YA HANAFI (80-150 Al Hijr) 405

  • 7

    VYANZO VYA MSINGI WA FIQH YA HANAFI................................ 418 WANAZUONI MAARUFU WA MADHHAB YA HANAFI .................. 419 IMAM MALIK NA MADHHAB YA MALIK (93-179 Al Hijr) .............. 420 VYANZO VYA MSINGI WA FIQH YA MALIK................................. 426 WANAZUONI MAARUFU WA MADHHAB YA MALIK. .................. 427 IMAM MUHAMMAD IDRIS AL SHAFI’I NA MADHHAB YA AL SHAFI’I (150-204 Al Hijr) ..................................................................... 427 MAISHA YA IMAM AL SHAFI’I NCHINI YEMEN (179-184 Al Hijr) 434 MAISHA YA IMAM AL SHAFI’I NCHINI IRAQ (184-186 Al Hijr) .... 435 MAISHA YA IMAM AL SHAFI’I ALIPORUDI MAKKAH (186-195 Al Hijr)........................................................................................................ 436 TOFAUTI BAINA YA IMAM AL SHAFI’I NA MAIMAM WALIOMTANGULIA. .......................................................................... 438 WANAFUNZI WAKUBWA WA IMAM AL SHAFI’I ALIOWAACHA MAKKAH. ............................................................................................. 439 MAISHA YA IMAM AL SHAFI’I ALIPORUDI BAGHDAD (195-199 Al Hijr)........................................................................................................ 439 AL RISALA MIN USUL UL FIQH YA IMAM AL SHAFI’I .................... 441 MPANGILIO WA AL RISALA YA IMAM AL SHAFI’I. ....................... 442 WANAFUNZI WAKUBWA WA IMAM AL SHAFI’I ALIOWAACHA IRAQ (NGUZO ZA AL QAWL AL QADIM) ........................................... 454 MAISHA YA IMAM AL SHAFI’I ALIPOHAMIA MISRI (199-204 Al Hijr)........................................................................................................ 455 IMAM AL SHAFI’I NA SAYYIDA NAFISA (NAFISAT AL I’LM) ....... 464 KUFARIKI KWA IMAM AL SHAFI’I .................................................. 466 YANZO VYA MSINGI WA FIQH YA AL IMAM AL SHAFI’I .......... 467 WANAFUNZI WAKUBWA WA IMAM AL SHAFI’I ALIOWAACHA MISRI (NGUZO ZA AL QAWL AL JADID). .......................................... 470 AL QAWL AL QADIM NA AL QAUL AL JADID KATIKA FIQH YA IMAM AL SHAFI’I. ............................................................................... 470 AL QAWL AL MASHHUR NA AL QAWL ALA AL MUTAMAD KATIKA MADHHAB YA IMAM AL SHAFI’I...................................................... 478 KUENEA KWA MADHHAB YA IMAM AL SHAFI’I ........................... 481 UMAARUFU WA WANAZUONI WA MADHHAB YA IMAM AL SHAFI’I.................................................................................................. 482 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA I’LM MCHANGANYIKO. ..................................................................... 483

  • 8

    WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA HADITH. ................................................................................................ 483 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA TAFSIR. ................................................................................................. 484 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA FIQH. ..................................................................................................... 484 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA UTAALAM WA LUGHA YA KIARABU. ............................................ 484 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA AQIDAH. ............................................................................................... 485 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA TASAWWUF. ........................................................................................ 485 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KATIKA FANI YA UTAWALA. ........................................................................................... 485 WANAZUONI WA MADHHAB YA AL SHAFI’I WALIO KATIKA KARNE YETU. ...................................................................................... 486 IMAM AHMAD IBN HANBAL NA MADHHAB YA HANBAL (164-241 Al Hijr) ................................................................................................... 487 SHAYKH AHMAD IBN TAYMIYYAH NA AHLU SUNNA WAL JAMAAH ............................................................................................... 493 UTAWALA WA DOLA LA OTTOMAN............................................... 497 UTAWALA WA OTTOMAN-SULTAN MUHAMMAD AL FATIH. ... 497 UTAWALA WA OTTOMAN-SULTAN SULAIMAN SALIM (AL QANUN). ................................................................................................ 500 UTAWALA WA OTTOMAN-SULTAN ABDÜLHAMID II (1842-1918) ............................................................................................................... 502 FITNAT UL WAHABBIYYAH.................................................................. 507 NJIA ALIZOZITUMIA ABDUL WAHAB ............................................ 509 SALAFI NA MADHHAB YA IMAM HANBAL. ................................... 516 TAHADHARISHO LA WANAZUONI WA KARNE YETU JUU YA JITIHADA ZA UPANDIKIZWAJI WA MITIZAMO YA KIWAHABI NA KISALAFI KATIKA TAFSIRI NA VITABU VYA ASILI VYA KIISLAM. .............................................................................................. 518 VYANZO VYA FIQH YA MADHHAB YA HANBAL: ......................... 525 WANAZUONI MAARUFU WA MADHHAB YA IMAM HANBAL. .... 526 BAADHI YA WANAZUONI MAARUFU WA KISALAFI. .................. 526

  • 9

    AL NAKBA - NAMNA PALESTINA ILIVYOGEUZWA KUA ISRAEL. ............................................................................................................... 528 MAENEO WANAYOISHI WAFUASI WA MADHHAB KWA UJUMLA DUNIANI. .............................................................................................. 534 SURA YA SITA .............................................................................................. 536 KAULI ZA MAIMAMU WA MADHHAB KUHUSU KUFANYA TAQLID. ................................................................................................. 536 KUTOFAUTIANA KWA WANAZUONI. ............................................. 540 KANUNI ZINAZOTUMIKA ILI KUTATUA TOFAUTI BAINA YA WANAZUONI. ...................................................................................... 551 BAADHI YA TOFAUTI NA UFANANO BAINA YA MADHHAB KATIKA SALA...................................................................................... 560 JITIHADA ZA WANAZUONI KATIKA KUTAFUTA UMOJA WA WAISLAM BAINA YA MADHHAB YA IBADHI, SHIA NA AHLU SUNNAH W AL JAMAA. ......................................................................... 566 BAADHI YA TOFAUTI NA UFANANO WA MITIZAMO BAINA YA MADHHAB YA IBADHI, SHIA NA AHLU SUNNAH W AL JAMAA. ..... 571 DAR AL TAQRIIB BAYNA MADHAHIB AL ISLAMIYYAH – KITENGO CHA USHIRIKIANO WA MADHHAB YA KIISLAM KATIKA CHUO CHA AL AZHAR CHA MISRI .............................................................. 577 TAFSIR YA FATWA YA SHAYKH AL AKBAR AL SHALTUT YA DAR AL TARQIIB BAYNA MADHAHIB AL ISLAMIYYAH ..................... 580 TOFAUTI YA AQIDA ZA ASHARIYYAH, MATURIDDIYAH NA ATHARIYYAH, KATIKA AHL SUNNA WAL JAMAA. ............................ 581 ASILI YA AQIDAH YA ASHARRIYAH .............................................. 590 ASILI YA MATURRIDIYAH ................................................................ 593 ASILI YA ATHARRIYAH..................................................................... 594 SURA YA SABA ............................................................................................. 595 HISTORIA YA UISLAMU BARANI AFRIKA. .................................... 596 HISTORIA YA UISLAMU KATIKA AFRIKA MASHARIKI............... 600 UTAWALA WA SULTAN BARGHASH KATIKA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI. ......................................................................... 603 QUTB UL IMAMI - IMAM MUHAMMAD YUSUF AL ATFAYYISH. 607 QADHI AHMAD IBN ABU BAKAR IBN SUMAYT AL SHAFI’I ....... 611 UHUSIANO WA NCHI ZA MAGHARIBI KWA NCHI ZA KIISLAM. 616 BARUA YA MALCOLM X KUTOKA MAKKAH. .............................. 621 ZANZIBAR CHINI YA MWAMVULI WA WAINGEREZA ................ 625

  • 10

    KUANGUKA KWA AL ANDALUS YA AFRIKA MASHARIKI ......... 628 BAADHI YA MADHARA YALIYOTOKEA BAADA YA KUFIFIA KWA NURU YA UISLAM KATIKA AFRIKA MASHARIKI. ............. 644 SURA YA NANE ............................................................................................ 660 JEE NI NANI ADUI WA NDANI KWA NDANI YA UISLAM. ........... 661 FITNA – KULINGANA NA MTIZAMO WA WANAZUONI. ............... 662 BIDA’A – KULINGANA NA MTIZAMO WA WANAZUONI. ............. 665 AINA ZA BIDA’A .................................................................................. 672 MAKUNDI YA SALAFI - KULINGANA NA UFAFANUZI WA SHAYKH YASIR QADHI. .................................................................... 674 SIFA NZURI ZA SALAFI. ..................................................................... 684 MAKOSA NA KASORO ZA SALAFI. .................................................. 686 HITIMISHO KUHUSIANA NA SALAFI. ............................................. 693 HADITH DHAIF KATIKA FADHA'IL Al A’MAL – KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. ................................................................... 696 FATWA, MUFTI, QADHA NA QADHI – MAANA NA TOFAUTI ZAKE. ............................................................................................................... 699 GHULUW NA TATARRAF (MISIMAMO MIKALI) NA MADHARA YAKE KATIKA UISLAM. .................................................................... 702 AL WASATIYYAH (MSIMAMO WA KATI) NA UMUHIMU WAKE KATIKA UISLAM. ................................................................................ 707 TALFIQ - KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI...................... 718 BARUA YA IMAM ABU BAKR IBN AL ARABI KWA IMAM AL GHAZAL KUHUSU TAQLID NA TALFIQ. .......................................... 719 MASWALI YA QADHI ABU BAKR IBN AL ‘ARABI AL MALIKI: .. 719 MAJIBU YA MUJADDID UD DIN IMAM AL GHAZALI AL SHAFI’I: ............................................................................................................... 721 TASAWWUF (SUFI) - KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. . 724 TASAWWUF KATIKA IBADA. ............................................................. 727 A’RIFIN NA AWLIYAH KATIKA TASAWWUF................................ 732 TARIQAH KATIKA TASAWWUF ....................................................... 733 WANAZUONI MAARUFU WENYE KUFANYA TASAWWUF KATIKA KIZAZI CHETU. .................................................................................... 739 TAWASSUL – KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. .............. 740 TAKFIR – KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI . ................... 754 MUFTI AHMAD AL KHALIL NA FATWA YA TAKFIR .................... 757 MUFTI MUHAMMAHD TAQI USMAN NA FATWA YA TAKFIR .... 758

  • 11

    FATWA YA WANAZUONI DUNIANI KUHUSU TAKFIR .................. 761 JIHAD NA MAANA YAKE KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. ...................................................................................... 766 FATWA YA SHAYKH UL ISLAMI DR. MUHAMMAD TAHIR UL QADRI KUHUSIANA NA JIHAD NA MAUAJI YA KUJITOLEA MUHANGA. .......................................................................................... 771 FATWA YA MUFTI AFIFI AL AKITI KUPINGA MSIMAMO MKALI WA MAUAJI YA KUJITOLEA MUHANGA. ....................................... 772 RU’YAT UL HILAL - MUONEKANO WA MUANDAMO MWEZI KATIKA UISLAM. ................................................................................ 801 MATLA MAHAL AL RUÝAH – ENEO LA MUONEKANO WA MUANDAMO WA MWEZI - KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. ...................................................................................... 805 SAUDIA NA KALENDA YA UMM UL QURA ..................................... 809 EID AL ADHHA – HUKMU NA HISTORIA YAKE. ............................. 810 FATWA YA DAR UL ULUM DEOBAND JUU YA KUTOAMINIKA KWA MUANDAMO WA MWEZI WA SAUDI ARABIA (MWEZI JANUARY 2015). .................................................................................... 812 FATWA YA KIARABU YA AZIMIO LA NNE LA RABITA AL’ALAM AL ISLAMIYA KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI. ...................... 816 TAFSIRI YA KIINGEREZA YA FATWA YA RABITA L’ALAM AL ISLAMIYA KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI KATIKA AZIMIO LA NNE. ................................................................................................ 819 TAFSIRI YA KISWAHILI YA FATWA YA RABITA L’ALAM AL ISLAMIYYAH KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI KATIKA AZIMIO LA NNE .................................................................................. 821 FATWA YA SHAYKH MUHAMMAD IBN SALIH AL UTHAYMEEN KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI KATIKA TAREHE 28/8/1420 (2000) (MTAZAMO WA MADHHAB YA IMAM HANBAL NA WA KISALAFI). ........................................................................................... 824 FUNGA YA ARAFAH KULINGANANA NA FATWA YA SHAYKH MUHAMMAD IBN SALIH AL UTHAYMEEN. ................................... 825 MUFTI TAQI USMANI KUHUSU KUUNGANISHA MWANDAMO WA MWEZI MMOJA DUNIANI KOTE (MADHHAB YA HANAFI ). ........ 827 NINI MAANA YA UMOJA WA KIISLAMU? ...................................... 828

  • 12

    FATWA YA AYATOLLAH SAYYID AS SISTANI KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI YA MWAKA 2012 (MADHHAB YA SHIA). ............................................................................................................... 830 UFAFANUZI WA SHAYKH YASIR QADHI KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI. .......................................................................................... 830 UFAFANUZI WA KINA WA SHAYKH MUHAMMAD AFIFI AL AKITI KUHUSU MWANDAMO WA MWEZI : MADHHAB YA AL IMAM AL SHAFI’I. ................................................................................................. 831 MISIKITI KARIBU NA ENEO LENYE MAKABURI........................... 843 FATWA YA MUFTI MKUU WA CHUO KIKUU CHA AL AZHAR CHA MISRI MUFTI ALI JUMAH. ................................................................. 843 UTHIBITISHO WA MTIZAMO WA MADHHAB YA IMAM AL SHAFI’I KUHUSIANA NA KUTENGUKA KWA UDHU KUNAKOTOKANA NA KUGUSANA BAINA YA MWANAMME NA MWANAMKE - MUFTI TAHA KARAN ...................................................................................... 851 QUNUT KATIKA SALA YA AL FAJIR – KULINGANA NA MTIZAMO WA MADHHAB YA AL IMAM AL SHAFI’I ........................................ 858 UTHIBITISHO WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KUHUSIANA NA QUNUT KATIKA SALA YA ALFAJIR. ................................................ 862 TALQIN NA IS A’L THAWAB – KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI. ...................................................................................... 867 TAFSIRI YA KISWAHILI YA TALQIN AL RUH BAADA JAFN AL JASAD KUISOMEA ROHO BAADA YA KUINGIA KATIKA NGOME ............................................................................................................... 886 NISF SHAABAN – NUSU YA MWEZI SHAABANI NA UTUKUFU WAKE. ................................................................................................... 889 SALAT NISF SHAABAN KATIKA MADHHAB YA AL IMAM AL SHAFII – FATWA YA MUFTI AFIFI AL AKITI. ................................. 893 FATWA YA MUFTI AFIFI AL AKITI KUHUSIANA NA 'AMAL ZA WALIO HAI, PIA HUWAFAA WALIOTANGULIA AKHERA. .......... 899 MAWLID AN NABAWI – KULINGANA NA KAULI ZA WANAZUONI ............................................................................................................... 911 HISTORIA YA IMAM AL BARZANJI. ................................................ 916 HITIMISHO. .................................................................................................. 917 MARUDIO YA VITABU VILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI ............................................................................................................... 925

  • 13

    MARUDIO YA MITANDAO ILIVYOTUMIKA KATIKA KITABU HIKI ............................................................................................................... 927

    PICHA NA MICHORO ILIYOMO NDANI YA KITABU

    ASILI YA MANABII WALIOTAJWA KATIKA QUR’AN…………….. 74 ASILI YA UKOO WA QURAYSH……………………………………….. 107 FAMILIA YA RASUL ALLAH SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM….. 124 AINA ZA MIFUMO YA USUL UL FIQH…………………………………… 174 DARJA ZA MASLAHI YA MSINGI YA MAQASID ASH SHARIA’H… 187 MUKHTASAR, ASILI NA MAANA YA MAQASID ASH SHARIA’H… 190 JADWELI INAYOTOFAUTISHA BAINA YA SHARIA’H NA FIQH….. 191 UHUSIANO WA MAQASID ASH SHARIA’H NA HUKMU TAKLIFI… 192 SEHEMU ZINAZOJUMUISHA HADITH………………………………. 200 MFANO WA SANAD…………………………………………………… 201 ASILI YA HADITH KUTOKANA NA SIFA ZAKE……………………. 206 DARJA YA HADITH NA SIFA ZAKE………………………………….. 208 RAMANI YA ENEO ALILOTAWALA ABU BAKR…………………... 268 RAMANI YA ENEO ALILOTAWALA UMAR IBN AL KHATTAB….. 290 RAMANI YA ENEO ALILOTAWALA UTHMAN IBN AFFAN……… 296 RAMANI YA ENEO LILILOTAWALIWA NA UTAWALA WA BANU UMMAYAD……………………………………………………...

    322

    ASILI YA UTAWALA WA BANU UMAYYAD NA AL ABBAS…….. 324 RAMANI YA ENEO LILILOTAWALIWA NA UTAWALA WA AL ABBAS…………………………………………………………………...

    328

    ENEO LA ARDHI TAKATIFU YA BAYT AL MAQDIS (AL QUDS)…… 349 JADWELI YA UVUMBUZI WA KISAYANSI KATIKA HISTORIA YA KIISLAM…………………………………………………………….

    357

    ASILI YA UISLAMU KUTOKA KWA NABII MUHAMMAD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM HADI KUFIKIA KATIKA MADHHAB YA AHL SUNNAH WAL JAMAA, IBADHI NA SHIA……

    370

    SILSILA YA ILM YA MUJTAHID IMAMU WA FIQH WA MADHHAB………………………………………………………………

    374

    ASILI YA MAKUNDI YA MADHHAB YA IBADHI…………………… 384 ASILI YA MAIMAMU 12 WA MADHHAB YA SHIA………………… 391 ASILI YA MAKUNDI YA MADHHAB YA SHIA……………………… 394 ASILI YA MADHHAB YA AHLU SUNNAH W AL JAMAAH………….. 406

  • 14

    ASILI YA UKOO WA QURAYSH, UKOO ULIOTOA BANU HASHIM AMBAO PIA NI ASILI YA IMAM MUHAMMAD IDRIS AL SHAFI’I

    429

    ISNAD YA I’LM YA AL IMAM AL SHAFI’I KUANZIA KWA NABII MUHAMMD SALALLAHU A’LAYHI WA SALAM………………………

    456

    SILSILA YA BAADHI YA WANAZUONI WA MADHHAB YA AL IMAM AL SHAFI’I KUANZIA KWA IMAM AL SHAFI’I HADI KWA IMAM IBN HAJAR AL ASQALANI……………………………………

    468

    SILSILA YA ILM YA FIQH YA MADHHAB YA IMAM AL SHAFII.. 475 ENEO LILILOTAWALIWA NA DOLA LA OTTOMAN EMPIRE........ 498 SILSILA YA WANAZUONI WA MAARUFU WA MADHHAB YA AL SHAFI’I KUANZIA KWA IMAM AN NAWAWI HADI KWA SHAYKH UL ISLAMI AHMAD ZAYN AD DAHLAN..........................

    505

    MAELEZO KWA UFUPI YA MAIMAMU WA SKULI ZA MADHHAB NA VYANZO VYA FIQH VINAVYOTUMIWA KATIKA SKULI ZA MADHHAB YAO........................................................................................

    526

    MAENEO YA WAFUASI WA MADHHAB TOFAUTI YA DINI YA KIISLAM DUNIANI……………………..................................................

    534

    BAADHI YA TOFAUTI NA UFANANO BAINA YA MADHHAB KATIKA SALA…………………………………………………………..

    559

    BAADHI YA TOFAUTI ZA MITIZAMO BAINA YA MADHHAB YA IBADHI, SUNNI NA SHIA. ..................................................................

    569

    FATWA YA CHUO CHA AL AZHAR CHA MISRI YA KUYALETA KARIBU MADHHAB YA KIISLAM - DAR AL TAQRIIB AL MADHAHIB AL ISLAMIYYAH...................................................................

    577

    ASILI YA AQIDA ZA ASHARI, MATURIDI NA ATHARI KATIKA AHLU SUNNA WAL JAMAAH………………………………………..

    582

    TOFAUTI BAINA YA AQIDA ZA ASHARI NA MATURIDI………… 586 SILSILA YA WANAZUONI WA AFRIKA MASHARIKI WA MADHHAB YA AL IMAM AL SHAFI’I KUANZIA KWA MUFTI ZAYN AD DAHLAN HADI KWA SHAYKH ALI AL BARWAN, ABDALLAH SALEH AL FARSY NA HASAN IBN AMEIR…………..

    611

    SILSILA YA BAADHI YA TARIQAH ZA I’LM YA TASAWWUF ………. 733 FATWA YA RABITA AL A’ALAM ISLAMIYYAH KUHUSU MUANDAMO WA MWEZI……………………………………………..

    816 820

    TALQIN AL RUH BAADA JAFN AL JASAD………………………… 884

  • 15

    UTANGULIZI.

    ﴾احلَْقَّ َوأَنُتْم تـَْعَلُمونَ ﴿َوَال تـَْلِبُسواْ احلَْقَّ اِبْلَبـِطِل َوَتْكُتُمواْ Wala talbisoo alhaqqa bialbatili wataktumoo alhaqqa waantum taAAlamoona

    (Surat Al Baqara 2:42)

    Tafsir: Na msichanganye haki na batil, na wala msifiche ukweli wakati mkiujua.

    Ningependa kumshukuru Allah Subhanahu wa Ta’ala na kumtakia Rehma na Amani Mtume wake Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam kwa kuniwezesha kuifanya kazi hii kwa mara ya tatu. Namuomba Allah Subhanahu wa Ta’ala atunufaishe kwa yale mambo yenye manufaa ndani ya kitabu hiki na pia yale yaliyokuwemo katika maisha yetu na pia atuepushe na yale yasiyokua na manufaa nasi, kama ikiwa yamo ndani ya kitabu hiki ama katika maisha yetu, kwani ni Allah pekee ndie mjuzi wa kila kitu..Aamiin.

    Kusudio la kuchapisha kitabu hiki ni kuelimisha jamii ya Kiislam kwa kifupi kwa wale wanaopendelea kufahamu kuhusu Uislam, Taqlid na Ijtihad katika Historia ya Uislam tangu kuanzia wakati wa Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, wakati wa Makhalifah wanne wa Kiislam, kuijua historia ya kuenea kwa Dini ya Kiislamu na njia walizotumia katika kueneza Uislam katika maeneo tofauti ulimwenguni, tofauti na tulivyokua waislamu wa leo.

    Vile vile kuielimisha jamii ya Kiislamu kuijua historia ya Maimamu wa Madhhab ya Kiislam, kujua kwa nini Waislam huwafuata Maimamu wa Maadhhab tofauti duniani, kujua tofauti za Maimamu hao katika baadhi ya mambo na makubaliano yao katika baadhi ya mambo, na kujua Madhhab ya Maimamu hao yalienea vipi katika maeneno mbali mbali Ulimwenguni tangu yalipoanzia hadi kufikia hapa tulipofikia leo.

    Ingawa mada kuu ya kitabu hiki ni kuhusu Ijtihad na Taqlid, lakini pia nimeangalia mambo mengine ambayo hua yanaenda sambamba na mada hiyo. Kitabu hiki kimegawika katika sura nane tofauti ambazo zinazungumzia mambo mbali mbali katika historia ya Uislam, kama vile Asili ya dini ya Kiislam, Asili na kusudio la kushushiwa Mitume na Allah Subhanah wa Ta’ala, Historia ya mji wa Makkah na pia ya ukoo wa Quraysh na asili ya Nabii Muhammad Salallahu A’layhi wa Salam, Maqasid ash Sharia’h, asili ya Ijtihad na Taqlid na historia ya uongozi wa Amir ul

  • 16

    Mu’minin wote wanne wa Uislam na watawala mbali mbali wa Kiislam waliofuatia baada ya Amir ul Mu’minin hao, kama vile tawala za Banu Umayyad wa Damascus, Banu Umayyad wa Al Andalus, Al Abbas wa Baghdad, Utawala wa Seljuq, Al Ayyub wa Misri, Dola la Ottoman la Uturuki, Dola la Al Bu Said wa Oman na Zanzibar na kuangalia mafanikio yao katika kuendeleza, kuonesha na kudumisha sifa sahihi na za asili za dini ya Kiislamu.

    Katika kitabu hiki pia nimezungumzia maana na asili ya Madhhab ya Kiislam, Historia za Maimamu wa Madhhab hayo ikiwemo Madhhab ya Ibadhi, Shia, Hanafi, Malik, Shafi’i na Hanbal. Na kuzungumzia tofauti za wanavyuoni wa Madhhab hayo na pia mitizamo yao kuhusiana na tofauti zao, na vile vile sikuwacha kuzungumzia historia za Wanazuoni wakubwa wa Afrka Mashariki na pia mitihani waliyokutana nayo na namna walivyoshirkiana na kua na umoja baina yao na Wanazuoni wengine wa Kiislam Duniani dhidi ya wale wanaoipiga vita Dini ya Kiislam, na namna Wanazuoni hao walivyokabiliana na mitihani hiyo.

    Nimeangalia na pia mitizamo ya wanazuoni juu ya baadhi ya mitihani ya ndani inayosababishwa na baadhi ya wafuasi wa Dini ya Kiislam, mitihani ambayo inayotutatiza, kutuchanganya na kutuletea mgawanyiko miongoni mwa Waislam wa leo ambayo hutokana na kutokujua maana, asili na uhalali wa Ijtihad, Taqlid, Bida’a, Talfik, Tasawwuf, Takfir, Kufr, Tawassul, Jihad, Ru`yatul Hilal, Talqin na mengineyo, nimeyaangalia mambo hayo si kwa ajili ya kuunga mkono ama kupinga mambo hayo, bali kwa ajili ya kuonesha misingi ya mambo hayo kwa wale wasiojua lakini wakawa wanafuata ama kufanya mambo hayo na pia kwa wale wasiojua lakini wakawa wanayapinga mambo hayo ili kujaribu kujenga mandhari ya ustahmilivu katika jamii ya Kiislam.

    Kwa kua dhumuni la kitabu hiki ni kuelimisha jamii, inawezekana kua kuna baadhi ya watu wakafahamu ama kutafsir sivyo maelezo yaliyokuwemo ndani yake, hivyo ningependa kutilia mkazo kua dhumuni la kitabu hiki si kukosoa, kuwalazimisha wale wasiofuata mitizamo iliyokuwemo ndani yake kuifuata, kuanzisha mjadala, kusomesha somo la Fiqh ama kuchochea uhasama miongoni mwa Waislam, kwani dini ya Kiislam inapinga chuki, fitna, hasad, uhasama na mijadala isiokua na faida ya kuelimisha ndani yake n.k, bali ni kujenga mazingira ya kuheshimiana, kufahamiana na kustahmiliana katika Ummah wa Kiislam.

    Katika ulimwengu wa leo wa Kiislamu kuna migawanyiko ya makundi tofauti, na inaonekana kua Waislamu wengi wako katika hali hii kwa sababu ya kutofahamu ukweli na undani wa dini ya Kiislam ulivyo, hawaijui Historia ya Uislam, hawawajui Maimamu wa Madhhab yao, wala tofauti za Maimamu wa Madhhab hayo, na pia

  • 17

    Maimamu hao walikua wanazichukulia vipi tofauti zao, ili kujua uhalisi wa mitizamo ya Madhhab ya Kiislamu juu ya tofauti baina ya Madhhab na kua mstahimlivu juu ya tofauti hizo, inabidi mtu ajue historia ya Uislamu na historia ya Madhhab hayo, kanuni zao na njia wanazozitumia katika kutoa hukmu.

    Kwa kua Waislam wengi wa Afrika Mashariki ni wafuasi wa Imam Al Shafi’i, basi nimeamua kutumia kurasa nyingi zaidi kumuelezea Imam Al Shafi’i na Madhhab yake, kuliko Maimamu wengine katika kitabu hiki ili Waislamu hao wapate kujua zaid kuhusu Imam Al Shafi’i na Madhhab yake wanayoyafuata na misimamo ya Madhhab ya Imam Al Shafi’i kuhusiana na mambo mbali mbali katika dini ya Kiislamu.

    Ningependa kuomba samahani, kwa wale wasiofuata Madhhab ya aina yeyote, kwa wale wanaofuata Madhahab mengine yasiyokua ya Ahlu Sunnah wal Jamaah na pia kwa wale wasiofuata Madhhab ya Al Imam Al Shafi’i kwani mambo mengi ambayo yameelezewa ndani ya kitabu hiki yameegemea zaidi katika upande mmoja wa Madhhab Ahlu Sunnah wal Jamaa na zaid katika mitazamo ya Madhhab ya Imam Al Shafi’i, hata hivyo katika baadhi ya mambo ambayo nimepata vithibitisho vya Madhhab mengine basi pia sikuwacha kuweka wazi vithibitisho vyao katika kuweka wazi mitizamo yao katika mambo yaliyozungumziwa ndani yake.

    Vile vile ningelipenda kuomba samahani pale itakapoonekana kua nimeteleza katika kuzungumzia kuhusiana na Madhhab ya Ibadhi kwa sababu miongoni mwa maelezo yanayoelezea Madhhab ya Ibadhi niliyoyapata basi mengi yametokana na vyanzo vilivyotofautiana vya wafuasi wa Madhhab ya Ibadhi wa Afrika ya Kaskazini ambayo hua ni rahisi kupatikana na baadhi yametokana na vyanzo vya wafuasi wa Madhhab ya Ibadhi wa Oman ambayo hua ni vigumu sana kupatikana. Jambo ambalo linaweza kuwasababishia baadhi ya wasomaji kufaham sivyo, kwani kidogo kuna kutofautiana kuhusiana na uhalisi wa maelezo ya historia ya Madhhab hayo, baina ya pande hizo mbili na pia baina ya Wanazuoni wa Madhhab hayo wa karne zilizotangulia na Wanazuoni wa karne za hivi karibuni.

    Inshaallah Allah atunufaishe na kila lenye manufaa ndani ya kitabu hiki na atuepushe na kila lenye shari na walakin na hivyo kutokua na manufaa yeyote

    ndani yake…Aamiin.

  • 18

    SURA YA KWANZA

    ُ أَنَُّه الَ ِإلَـَه ِإالَّ ُهَو َواْلَمَلـِئَكُة َوأُْوُلواْ اْلِعْلِم َقآِئَماً اِبْلِقْسِط الَ إِ لَـَه ﴿َشِهَد اهللَّ﴾يَن ِعنَد اهللَِّ اِإلْسلَـمُ ِإنَّ الدِّ -احلَِْكيُم ِإالَّ ُهَو اْلَعزِيُز

    Shahida Allahu annahu la ilaha illa huwa waalmala-ikatu waoloo alAAilmi qa-iman bialqisti la ilaha illa huwa alAAazeezu alhakeemu, Inna alddeena

    AAinda Allahi al-islamu. (Surat al Imran 3:18-19).

    Tafsir: Allah anashuhudia kua Lâ ilâh illa Huwa (Hakuna mwenye kustahiki kuabudiwa isipokua yeye), na Malaika (wanashuhudia hilo), na wenye Ilm (pia

    wanashuhudia hilo). Yeye ni mwenye kusimamisha haki kwa viumbe wake Lâ ilâh illa Huwa (Hakuna mwenye kustahiki kuabudiwa isipokua yeye), Yeye ni

    mwingi wa uwezo na mwingi wa hikma. Hakika ya dini mbele ya Allah ni Uislam.

    ASILI NA MAANA YA NENO DINI.

    Neno Dini ni moja kati ya maneno muhimu na yanayotumika sana ulimwenguni, kwani neno hili hua ni muongozo wa mfumo wa maisha ambao ndio unaowapelekea viumbe kujali wanayoyafanya katika maisha yao na hivyo kuwapelekea kufuzu katika maisha ya hapa Duniani na kesho Akhera.

    Tukiangalia maana ya neno hili kwa lugha ya kiarabu, lugha ambayo ndio asili ya neno hilo, basi tunaona kua neno Dini lina na Tafsir nyingi zikiwemo miongoni mwao pamoja na:-

    Kutiishwa, Kunyenyekea, Kuwa chini ya Mamlaka, Kua chini ya uangalizi, Njia, Tabia na Mazoea ya kitu fulani, na vile vile Adhabu, Sharia’h, Malipo na Hukmu kama vile wanavyosema waarabu wenyewe : Kama tadinu tudan ambapo maana yake kwa Kiswahili tunasema Kama uwafanyiavyo wengine basi nawe ndivyo hivyo hivyo utakavyofanyiwa.

    Kutokana na maana ya tafsir hizo tunaona kua maana ya neno hilo linapotumika katika mfumo wa maisha ulimwenguni basi mfumo huo hua unafafanulika kama ifuatavyo:

  • 19

    Mfumo wa maisha ulio chini ya Mamlaka, uangalizi na utiifu unaofuata njia zilizowekwa na mwenye Mamlaka kamilifu ya maisha hayo ambamo ndani yake mna hukmu za Malipo kwa watiifu wa Mamlaka hayo na Adhabu kwa waasi wa Mamlaka hayo.

    Tunapouzungumzia mfumo huo wa njia ya maisha ya viumbe vinavyoishi Ulimwenguni basi pia hua tunamzungumzia yule mwenye mamlaka juu ya viumbe hivyo, yaani Muumbaji wa viumbe hivyo. Na hakuna mwengine mwenye uwezo wa kuumba isipokua ni Allah Subhanahu wa Ta’ala, ambae anapotaka kitu kiwe basi huamrisha ‘kua’ na kinakua, kama inavyosema Qur’an tukufu:

    َآ أَْمرُُه ِإَذآ أَرَاَد َشْيئاً َأن يـَُقوَل َلُه ُكن فـََيُكوُن ﴿ بَِيِدِه ٱلَِّذىْبَحـَن سُ فَ -ِإمنَّ ﴾َشْىٍء َوِإلَْيِه تـُْرَجُعونَ َمَلُكوُت ُكلِّ

    Innama amruhu idha arada shay-an an yaqoola lahu kun fayakoonu; Fasubhana alladhi biyadihi malakootu kulli shay-in wa-ilayhi turjaAAoona (Surat Yasin 36:82-83)

    Tafsir: Hakika amri yake, anapokikusudia kitu basi hua ni kukiambia ‘Kua’ na kitu hicho hua. Ametukuka yeye ambae katika mikono yake kuna umiliki wa kila kitu na kwake yeye mtarudishwa.

    Kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala ni mwenye uwezo wa kuumba kitu chochote, vyovyote atakavyo, bila ya kutokana na kitu chengine au kuwepo kwa kitu chengine chochote iwe kwa ghafla moja tu, kun fayakun ( ُكُن فَیَكُون) (kua na kinakua), na pia ni mwenye uwezo wa kuumba kitu na kukiumbia kitu hicho mahitaji yake yote bila ya kuwepo kwa kitu chengine, au kuumba vitu au viumbe kwa kuchukua muda fulani yaani kukitoa kiumbe akiumbacho kutoka katika hatua moja hadi nyengine, na pia bila ya kuwepo utofauti wa uwezo wake juu ya kuumba kwake huko iwe kwa ghafla au kwa kuchukua muda fulani.

    Na hii ni moja kati njia za Allah Subhanahu wa Ta’ala za kuonesha busara zake, ukamilifu wake na kudhihirisha maana na sifa zilizomo katika majina yake kwa viumbe wake kama alivyosema katika Qur’an:

  • 20

    ٰى َوٱَألْرِض َوَما َبثَّ ِفيِهَما ِمن َدآبٍَّة َوُهَو َعلَ َوِمْن آَ�تِِه َخْلُق ٱلسََّماَواِت ﴿﴾َمجِْعِهْم ِإَذا َيَشآُء َقِديرٌ

    Wamin ayatihi khalqu alssamawati waal-ardhi wama baththa feehima min dabbatin wahuwa AAala jamAAihim idha yashao qadeerun (Surat Ash Shuraa 42:29). Tafsir: Na miongoni mwa dalili zake ni kuumba mbingu na ardhi, na viumbe hai vilivyotawanyika ndani yake, na yeye ana uwezo wa kuwakusanya pamoja atakapo.

    Ili kufahamu zaid kuhusiana na kun fayakun ( ُكُن فَیَكُون) (kua na kinakua), inabidi kufahamu maana ya umoja wa vitendo na wa viumbe vyote vilivyoumbwa kutokana na matakwa kamilifu ya Allah Subhanahu wa Ta’ala. Umoja huu unatoka na namna anavyoumba bila ya kuhitaji msaada wa yeyote au msaidizi yeyote zaidi yake.

    Tunaposema kun fayakun ( فَیَكُونُ كُن ) (kua na kinakua), basi haina maana kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anatumia maneno na kuamrisha kitu kiwe, la! Bali maana yake ni kua anapotaka kitu kiwe kinakua bila ya kuchukua hata sekunde baina ya kutokuwepo kwa kitu hicho na kuwepo kwake. Hivyo hapa imetumika kun fayakun ( ُكُن فَیَكُون), ili kuwa kama ufafanuzi kwa waliokusudiwa kufikishiwa ujumbe huo ambao ni Bani Adam (Kizazi cha Adam) kutokana na uwezo wa ufaham wao wa kibinaadam.

    Kwa sababu uwezo huo wa kun fayakun ( ُكُن فَیَكُون), kamwe hauwezi kutafsirika unavyotakiwa utafsirike kwa maneno au kwa ufaham wa Bani Adam.

    Kauli hii ya Kun fayakun imetajwa tena na Allah Subhanahu wa Ta’ala pale aliposema:

    َا قـَْولَُنا ِلَشْىٍء ِإَذآ أََرْدَ�ُه أَ ﴾ن نـَُّقوَل َلُه ُكْن فـََيُكونُ ﴿ِإمنَّ Innama qawluna lishay-in idha aradnahu an naqoola lahu kun fayakoonu (Surat An Nahl 16:40)

  • 21

    Tafsir: Kwa hakika! Kauli yetu juu kitu tunachokikusudia, ni kukiambia Kua na kinakua

    Anasema Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al Ghazal kuhusiana na ‘Kun fayakunu’ kua: ‘Aya hii kamwe haiwezi kutafsirikia kwa juu juu kwa sababu kama ikiwa kauli ya Allah ‘Kun’ iliamrishwa kwa kitu ambacho hakijawa, basi itakua ni jambo lisilowezekana kwa sababu, kitu ambacho hakijawa hua hakiwezi kufahamu kilivyoamrishwa na hivyo hakitoweza kutii amri hiyo, na ikiwa amri hiyo iliamrishwa wakati kitu hicho kishakua basi amri hiyo hua hai hitajiki, kwa sababu kitu hicho tayari kishakua. Lakini pale kilipotumika ‘Kinaya’ (kukielezea kitu kupitia kwa mfano wa kitu chengine) hiki, basi kimetumika ili kuelezea kwa kina Ufahamu wa viumbe, ili kuonesha mfano wa Uwezo Mkubwa wa kupita kiasi wa Allah ambao hakuna njia nyengine ya kuuelezea ukafahamika isipokua kwa njia hii’

    Miongoni mwa vitu vilivyoumbwa mwanzo na Allah Subhanahu wa Ta’ala ni pamoja na Nuru, Maji, Arshi, Kursi na Kalamu. Kwani kabla ya kuumbwa kwa Ulimwengu, kila kitu kilikua kipo katika kiza cha kutokuwepo. Hivyo kutokana na Neema na Ukarimu wa Allah Subhanahu wa Ta’ala akaondoa kiza hicho na kuumba Nuru ambayo ilikua ni asili au kiini cha kuwepo kila kitu kilichokuwepo. Kuna aina mbili za Nuru. Aina ya kwanza ni Nuru iliyoumbwa ambayo ndio inayopatikana Duniani, Akhera na Peponi. Nuru hii imegawika makundi mengi na inajumuisha Muangaza, I’lm, Uongofu, Imani n.k. kwani kazi ya kila aina ya Nuru hua ni kumurika aina fulani ya kiza cha kitu kisichokuwepo na kuonesha ukweli halisi ulivyo wa kitu hicho kwa kukifanya kiwepo.

    Aina ya pili ya Nuru ni Nuru ambayo haikuumbwa na hii hua inajulikana kama moja kati ya Majina ya Sifa Takatifu za Allah Subhanahu wa Ta’ala. Hii ni Sifa ambayo Allah Subhanahu wa Ta’ala mwenyewe anaielezea katika Qur’an kama ifuatavyo:

    ُ نُوُر ٱلسََّماَواِت َوٱَألْرِض َمَثُل نُورِِه َكِمْشكَ ﴿ ٱْلِمْصَباحُ اٍة ِفيَها ِمْصَباحٌ و ٱهللَِّىف ُزَجاَجٍة ٱلزَُّجاَجُة َكأَنـََّها َكوَْكٌب ُدّرِيٌّ يُوَقُد ِمن َشَجَرٍة مَُّبارََكٍة زَيـُْتونٍَة الَّ

    يـَْهِدى َشْرِقيٍَّة َوالَ َغْربِيٍَّة َيَكاُد زَيـْتُـَها ُيِضۤيُء َوَلْو َملْ َمتَْسْسُه َ�ٌر نُّوٌر َعَلٰى نُورٍ ُ لُِنورِِه َمن َيَشآءُ َويَ ُ ِبُكلِّ َشيْ ٱهللَّ ُ ٱَألْمثَاَل لِلنَّاِس َوٱهللَّ ﴾ٍء َعَلِيمٌ ْضِرُب ٱهللَّ

  • 22

    Allahu nooru alssamawati waal-ardhi mathalu noorihi kamishkatin feeha misbahun almisbahu fee zujajatin alzzujajatu kaannaha kawkabun durriyyun yooqadu min shajaratin mubarakatin zaytoonatin la sharqiyyatin wala gharbiyyatin yakadu zaytuha yudee-o walaw lam tamsas-hu narun noorun AAala noorin yahdee Allahu linoorihi man yashao wayadribu Allahu al-amthala lilnnasi waAllahu bikulli shay-in AAaleemun.(Surat Al-Noor 24: 35).

    Tafsir: Allah ni Nuru ya Mbingu na Ardhi, mithli ya Nuru yake ni kama Mishkat (Mishkat ni sehemu kama kidirisha ambacho hujengwa maalum kwa ajili ya kuwekea taa ukutani na hivyo kufanya muangaza wa taa hiyo uwe mkubwa zaid kuliko taa hiyo ikikaa katika sehemu iliyo wazi), na ndani yake mna taa, na taa hiyo imo ndani ya kioo. Kioo ambacho kinang’ara kama nyota ya Durriyun (aina ya nyota yenye kung’ara sana kama lulu), (taa) ambayo imewashwa kutokana na mti mtakatifu wa Mzaituni usio wa Mashariki wala Magharibi, ambao mafuta yake hutoa mwangaza bila ya kuguswa na moto wowote (kuwashwa). Nuru juu ya Nuru! Allah humuongoza katika mwangaza wake yeyote yule amtakae. Na Allah anaweka wazi mifano kwa Bani Adam, Na hakika Allah ni mwenye kujua kila kitu.

    Aya hii imetumia kiunganishi ‘ka’ kinachotafsirika kwa lugha ya Kiswahili kama ‘kama’ ambacho hujulikana kama Kaf at tashbih ambayo inayoleta maana ya kushabihisha kitu kimoja kua kinafanana tu na kitu chengine lakini hata hivyo, kitu hicho si kitu chenyewe kilichokusudiwa. Kutumika kwa kaf at tashbih katika aya hii kunaonesha kutokuwepo uwezekano wa kuelezea sifa za Majina ya Allah Subhanahu wa Ta’ala hata kupitia kwa njia za kufananisha kwani yeye mwenyewe anasema kua:

    ﴿لَْيَس َكِمْثِلِه َشْىٌء﴾Laysa kamithlihi shay-un (Surat Ash Shuraa 42:11) Tafsir: Hakuna kitu chochote chenye mithli yake. Na vile vile akasema:

    ﴾ َيُكْن لَُّه ُكُفواً َأَحدٌ ﴿َوملَْ Walam yakun lahu kufuwan ahadun (Surat Al Ikhlas 112:4)

  • 23

    Tafsir: Hakuna anaefanana nae.

    Hivyo ufananisho huu wa Sifa ya ‘Nuru ya Allah’ hauwezi kuonesha ukweli halisi ulivyo, bali ufafanisho huu umetumika ili kufafanua kimaana kutokana na ufahamu wa walengwa waliokusudiwa, kwa sababu ukweli halisi wa ‘Nuru ya Allah’ ni ukweli ambao hauwezi kufikirika kwa hali yeyote ya kiumbe yeyote yule na wala hauwezi kuelezeka kwa lugha ya kiumbe chochote.

    Imam Abu Hamid Ibn Muhammad Al Ghazal katika kuielezea maana ya Al Nur anasema kua: Al Nur ni yule anaeonekana kutokana na kuvifanya vitu vyote vionekane, kwani kila kitu kinachoonekana chenyewe na kusababisha vitu vyengine vionekane hua kinaitwa Nuru. Tukiangalia kwa mtazamo wa kua kila kilichokuwepo hupingana na kisichokuwepo, basi kile kinachoonekana hakiwezi kulinganishwa na kitu chengine isipokua tu na kile kilichokuwepo. Kwani hakuna kiza kilichokua cheusi zaidi kuliko kile kiza cha kitu kisichokuwepo.

    Kile kilichokua huru kutokana na giza la kutokuwepo, na kua na uwezekano wa kutokuwepo, na huondoa kila kitu kutoka katika kiza cha kutokuwepo na kukiingiza katika udhihirisho wa kuwepo, basi hua kinastahiki kuitwa Nuru. Kuwepo ni Nuru iliyohuru isiyotegemea kitu inayomurika kila kitu kutokana na asili ya Nuru yake Allah Subhanah wa Ta’ala, kwani Allah Subhanahu wa Ta’ala ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Na kama ilivyokua hakuna hata chembe moja pekee ya muangaza wa jua ambayo huonesha kua ndio chanzo cha muangaza wa jua hilo, basi vile vile hakuna hata chembe moja ya kitu kutoka katika vitu vilivyomo ndani ya mbingu na ardhi, ambacho hakimpelekei mtu kukosa uhakika wa kutokana na uwezekano wa kuwepo kwake bila ya kuhitaji kuwepo kwa yule aliesababisha kuwepo kwa kitu hicho.

    Hivyo kutokana na Nuru, hususan Nuru ya Allah, basi kila kitu hua kiko wazi, chenye kuonekana, chenye kufahamika na hivyo kua ni chenye uhakika na chenye kua na yakini.

    KUUMBWA KWA ULIMWENGU.

    Baada ya Allah Subhanahu wa Ta’ala kuumba Nuru na kuonesha kila kinachotakiwa kuonekana na wale ambao kutokana na Hikma za Allah Subhanahu wa Ta’ala mwenyewe kutaka wavione, basi akauumba Ulimwengu unaojumuisha Mbingu na Ardhi, kama Surat Fatir inavyosema:

  • 24

    ﴾ٱلسََّماَواِت َوٱَألْرضِ فَاِطِر ٱْحلَْمُد هللَِِّ ﴿ Alhamdu lillahi fatiri alssamawati waal-ardhi (Surat Fatir 35:1)

    Tafsir: Sifa zote na Shukrani anastahiki Allah, alieanzisha kwa kuumba (bila ya kutokana na kitu chochote) mbingu na ardhi.

    Ulimwengu ambao ndani yake mna sehemu mbili tofauti, sehemu ya Ash Shahada (wenye kuonekana) ambao tunaoishi sisi na vile vile kuna sehemu ya Al Gahyb (usioonekana). Allah Subhanahu wa Ta’ala anatuthibitishia kuwepo kwa ulimwengu unaoonekana na usionekana pale aliposema katika Qur’an:-

    َهاَدِة ُهَو ٱلرَّْمحَـُٰن ٱلرَِّحيمُ ُهَو ﴿ ُ ٱلَِّذى َال ِإلَـَٰه ِإالَّ ُهَو َعاِملُ ٱْلَغْيِب َوٱلشَّ ﴾ ٱهللَّ Huwa Allahu alladhi la ilaha illa huwa AAalimu alghaybi waalshshahadati huwa alrrahmanu alrraheemu; (Surat Al Hashr 59:22)

    Tafsir: Yeye ni Allah, ambae hakuna Mola isipokua yeye, yeye ni mwenye kujua yasiyoonekana na yenye kuonekana. Yeye ni mwingi wa Rehma na mwingi wa kurehemu.

    Na akasema tena kua

    ْؤِمُنوَن اِبْلَغْيِب يُـ ٱلَِّذينَ -َذِلَك اْلِكَتاُب الَ َرْيَب ِفيِه ُهًدى لِّْلُمتَِّقَني - املۤۤ ﴿﴾ِممَّا َرَزقْـَنـُهْم يُنِفُقونَ وَ َويُِقيُموَن ٱلصَّالةَ

    Alif-Lâm-Mîm. Dhalika alkitabu la rayba feehi hudan lilmuttaqeena; Alladhina yu/minoona bialghaybi wayuqeemoona alssalata wamimma razaqnahum yunfiqoona (Surat Al Baqara 2:1-3)

    Tafsir: Alif lam Mim. Hiki ni kitabu ambacho hakina shaka ndani yake, ambacho ni muongozo kwa wenye Taqwa. Wale ambao wenye kuamini al Ghayb (Ulimwengu usioonekana), na wakasimamisha Sala na wakanufaika na kile tulichowaruzuku.

  • 25

    Al Ghayb, Ulimwengu usioonekana unajumuisha kila kisichoweza kuonekana, kusikika na kuhisika kwa hisia za Bani Adam kama vile: Muumbaji ambae ni Allah Subhanahu wa Ta’ala na kila kitu ambacho amekiumba yeye lakini hakiwezi kuonekana, kusikika au kuhisika, kwa mfano kama vile Malaika, Maandiko, Wahy, Pepo, Jahannam, Akhera, Roho, Majini n.k.

    Allah Subhanahu wa Ta’ala ameelezea kuhusiana na uumbwaji wa Al Ghayb na pia Ash Shahada unaoonekana ambao upo baina ya mbingu na ardhi, kwa kusema kua:

    ا َوَجَعْلَنا َأنَّ ٱلسََّماَواِت َوٱَألْرَض َكانـََتا رَْتقاً فـََفتَـْقَنامهَُ أََوَملْ يـََر ٱلَِّذيَن َكَفُرۤواْ ﴿َواِسَى َأن َمتِيَد ْرِض رَ اْألَ َوَجَعْلَنا ِىف - ِمَن ٱْلَمآِء ُكلَّ َشْيٍء َحيٍّ أََفَال يـُْؤِمُنونَ

    َنا السََّمآَء َسْقفاً َوَجَعلْ -هِبِْم َوَجَعْلَنا ِفيَها ِفَجاجاً ُسُبالً لََّعلَُّهْم يـَْهَتُدوَن نـََّهـَر َوالشَّْمَس َخَلَق الَّْيَل َوال ٱلَِّذىَوُهَو -حمَُّْفوظاً َوُهْم َعْن َءايَـِتَها ُمْعِرُضوَن

    ﴾فـََلٍك َيْسَبُحونَ َر ُكلٌّ ِىف َواْلَقمَ Awa lam yara alladhina kafaroo anna alssamawati waal-ardha kanata ratqan fafataqnahuma wajaAAalna mina alma-i kulla shay-in hayyin afala yu/minoona; WajaAAalna fee al-ardhi rawasiya an tameeda bihim wajaAAalna feeha fijajan subulan laAAallahum yahtadoona; WajaAAalna alssamaa saqfan mahfoodhan wahum AAan ayatiha muAAridhoona; Wahuwa alladhi khalaqa allayla waalnnahara waalshshamsa waalqamara kullun fee falakin yasbahoona (Surat Al Anbiya 21:30-33)

    Tafsir: Jee wale wasioamini hawajui kua Mbingu na Ardhi vilikua ni kitu kimoja, na baadae tukavibagua, na tukaumba kila kitu kutokana na Maji? Jee hawaamini?; Na tukaweka katika Dunia, Milima iliyoimarika ili isitikisike pamoja nayo, na tukaweka ndani yake njia kwa ajili yao ili wapite bila kupotea. Na tukaifanya mbingu kua paa lililo salama na lenye kudhibitiwa vizuri sana. Lakini hata hivyo wanageukia upande wa pili wa dalili zetu; Na ni yeye alieumba usiku na mchana, jua na mwezi, na kila kimoja kinaelea katika njia yake.

    Aya hiyo inaweka wazi kua katika kuumbwa kwa ulimwengu unaonekana, basi kwanza mbingu na ardhi vilikua ni kitu kimoja kilichoungana lakini baadae

  • 26

    vikatenganishwa na kila moja kikawa mbali na mwenzake, zikawekwa Ardhi saba na Mbingu saba, kisha ikawekwa hewa baina ya ardhi ya mwisho ya juu na mbingu ya mwisho ya chini na ikasababiswha mvua kunyesha kutoka mbinguni na baada ya hapo miti ikaota ardhini.

    Qur’an imethibitisha mara mbili kua baina ya vitu viwili hivi, yaani mbingu na ardhi, kua Ardhi iliumbwa mwanzo kuliko Mbingu, katika aya zifuatazo:

    يعاً ُمثَّ اْستـََوى ِإَىل السََّمآِء َفسَ اْألَ ﴿ُهَو الَِّذى َخَلَق َلُكم مَّا ِىف وَّاُهنَّ ْرِض مجَِ﴾َوُهَو ِبُكلِّ َشْىٍء َعِليمٌ َسْبَع َمسَـَواتٍ

    Huwa alladhii khalaqa lakum ma fee al-ardhi jamiAAan thumma istawa ila alssama-i fasawwahunna sabAAa samawatin wahuwa bikulli shay-in Aaaleemun (Surat Al Baqarah 2:29)

    Tafsir: Ni yeye alieumba kila kitu kwa ajili yenu ardhini, na kisha akasimama na kuzielekea mbigu na akaziweka sawa mbingu saba, yeye ni mjuzi wa kila kitu.

    Na vile vile katika aya ya pili inayosema:

    َوَجتَْعُلوَن َلُه أَنَداداً ْرَض ِىف يـَْوَمْنيِ اْألَ َخَلَق بِٱلَِّذى﴿ُقْل أَِءنَُّكْم لََتْكُفُروَن َر ِفيَهآ َوَجَعَل ِفيَها َرَواِسَى ِمن فـَْوِقَها َوبَـَرَك ِفي - ِلَك َربُّ ٱْلَعاَلِمنيَ ذٰ َها َوَقدَّ

    ٍم َسَوآًء لِّلسَّآئِِلَني ِيفۤ أَقْـَوتـََها َوِهَى ُدَخاٌن تَـَوٰى ِإَىل ٱلسََّمآءِ ٱسْ ُمثَّ -أَْربـََعِة أَ�َّنَ َطْوعاً أَْو َكْرهاً قَالََتآ أَتَـ َوِلَألْرِض ٱْئِتَيافـََقاَل َهلَا فـََقَضاُهنَّ َسْبَع -ا طَآئِِعَني يـْ

    نـَْيا ِمبََصـِبيَح لسََّمآءَ ٱِىف ُكلِّ َمسَآٍء أَْمَرَها َوَزيـَّنَّا يـَْوَمْنيِ َوأَْوَحىَمسَاَواٍت ِىف الدُّ ﴾ِلَك تـَْقِديُر ٱْلَعزِيِز ٱْلَعِليمِ ذٰ َوِحْفظاً

    Qul a-innakum latakfuroona bialladhii khalaqa al-ardha fee yawmayni watajAAaloona lahu andadan dhalika rabbu alAAalameena; WajaAAala feeha

  • 27

    rawasiya min fawqiha wabaraka feeha waqaddara feeha aqwataha fee arbaAAati ayyamin sawaan lilssa-ileena; Thumma istawa ila alssama-i wahiya dukhanun faqala laha walil-ardhi i/tiya tawAAan aw karhan qalata atayna ta-iAAeena Faqadahunna sabAAa samawatin fee yawmayni waawha fee kulli sama-in amraha wazayyanna alssamaa alddunya bimasabeeha wahifdhan dhalika taqdeeru alAAazeezi alAAaleemi (Surat Fusilat 41:9-12)

    Tafsir: Sema (Ewe Muhammad) Hakika nyinyi mnamkufuru yule ambae ameiumba Ardhi kwa siku mbili na mmetengeneza washirika wengine (kumshirikisha) pamoja nae? Yeye ndie ambae, ni Mola wa kila kitu kilichopo. Ameweka (ardhini) milima imara juu yake na akaibariki, na akakadiria ndani yake rizki (kwa watakaoishi ndani yake) kwa siku nne sawia, kwa wote wale wanaouliza (kuhusiana na uumbwaji wake). Kisha akasimama kuielekea mbingu wakati ikiwa katika hali ya moshi, na akaiambia (hiyo mbingu) na ardhi: ‘Njooni nyote wawili iwe kwa hiari au bila hiari.’ Vyote vikasema: ‘Tunakuja kwa hiari’. Kisha akazimalizia kua mbingu saba katika siku mbili, na akaipangia kila mbingu yake jambo lake. Na tukaipamba mbingu ya karibu (ya chini) kwa taa ili ziwe pambo na pia kama ulinzi (kutokana na Shaytan). Hayo ndio makadirio ya mwenye uwezo na mwenye kujua.

    Tafakkar kwani aya hii kamwe haipingani na zile aya za Surah Al-Nazi’at zisemazo:

    َلَها َوأَْغَطَش -َرَفَع َمسَْكَها َفَسوَّاَها -ُء بـََنـَها ٱلسََّمآ﴿أَءَنُتْم َأَشدُّ َخْلقاً أَِم لَيـَْها َمآَءَها َوَمْرعَ -َدَحـَها ِلكَ ذٰ ْرَض بـَْعَد اْألَ وَ -َوَأْخرََج ُضَحـَها ـَها َأْخرََج ِمنـْ

    ﴾نـَْعاِمُكمْ َوِألَ َمَتـعاً لَُّكْم -أَْرَسـَها َوٱْجلَِبالَ - Aantum ashaddu khalqan ami alssamao banaha; RafaAAa samkaha fasawwaha; Waaghtasha laylaha waakhraja dhuhaha; Waal-ardha baAAda dhalika dahaha; Akhraja minha maaha wamarAAaha; Waaljibala arsaha; MataAAan lakum wali-anAAamikum (Surah Al Nazi’at 79:27-33)

    Tafsir: Jee nyinyi ni wagumu zaidi kuwaumba, au ni mbingu alizoziumba? Aliinyanyulia urefu wake, akaiamrisha ikakaa sawa sawa, akaufunika kwa kiza usiku wake, na huuleta kwa muangaza mchana wake. Na baada ya hapo akaitandaza ardhi, na akatoa ndani yake maji yake na malisho yake. Na majabali akaimarishia, (ili kua) malisho na manufaa kwenu na wanyama wenu.

  • 28

    Kwani kutokana na aya hizo tatu tulizoziangalia tunaona kua mbingu na ardhi vilikua ni kitu kimoja, halafu vikatenganishwa kila kimoja peke yake, kwa kwanza kuumbwa kwa ardhi lakini bila ya kutandazwa kisha ndio ikaumbwa mbingu na kupambwa na kujaaliwa usiku na mchana na kila kitu chake. Na baada ya hapo ndio ardhi ikatandazwa na kuwekewa majabali (milima) ambayo uimara na urefu wake kwenda chini ya ardhi ni mara mbili zaid ya vile inavyoonekana milima kutokana na muonekano wake wa juu ya ardhi namna ulivyoelekea juu hewani, na hii ni kwa sababu ya kuiimarisha Ardhi itulie bila ya kuyumba. Baada ya kuimarishwa huko, ardhi ikakadiriwa matumizi ya viumbe vyote vitakavyokuja kuishi juu yake na kisha ikatoa maji yake ambayo ni pamoja na mito na maziwa na pia ikatoa malisho yake ambayo ni pamoja na majani na miti yenye kutoa vivuli, vyakula, matunda n.k.

    KUUMBWA KWA MALAIKA NA MAJINI.

    Baada ya uumbwaji wa ulimwengu, mbingu na ardhi ndio vikaumbwa viumbe vyengine vilivyotawanyika Ulimwenguni humo wakiwemo Malaika. Allah Subhanahu wa Ta’ala anasema katika aya inayofuatia ya Surat Fatir:

    فَاِطِر ٱلسََّماَواِت َوٱَألْرِض َجاِعِل ٱْلَمالَِئَكِة ُرُسالً أُْوِيلۤ َأْجِنَحٍة ٱْحلَْمُد هللَِِّ ﴿﴾ َشْيٍء َقِديرٌ ٱْخلَْلِق َما َيَشآءُ ِإنَّ ٱهللََّ َعَلٰى ُكلِّ مَّثـَْىنٰ َوُثَالَث َوُراَبَع يَزِيُد ِىف

    Alhamdu lillahi fatiri alssamawati waal-ardhi jaAAili almala-ikati rusulan ulee ajnihatin mathna wathulatha warubaAAa yazeedu fee alkhalqi ma yashao inna Allaha AAala kulli shay-in qadeerun (Surat Fatir 35:1)

    Tafsir: Sifa zote anastahiki Allah, Muumba wa Mbingu na Ardhi, ambae aliewaumba Malaika wajumbe wenye mbawa mbili au tatu au nne. Huongeza miongoni mwa viumbe vyake atakavyo. Hakika Allah ni muweza wa kufanya kila kitu.

    Neno Malaikah linatokana na neno ‘Malak’ ambalo maana yake ni kua na uwezo mkubwa sana wa kinguvu, kwani Malaika ni viumbe wenye uwezo mkubwa sana kinguvu ambao hua unawapelekea kufanya yale waliyoamrisha bila ya kuchoka na hivyo kutojiskia kutaka kupata mapumziko ijapokua hawali wala hawalali na wala hawapunguzi kasi katika kumtukuza Allah Subhanah wa Ta’ala. Kama inavyosema Qur’an:

  • 29

    ﴾ُيَسبُِّحوَن ٱْللَّْيَل َوٱلنـََّهاَر َال يـَْفتُـُرونَ ﴿ Yusabbihoona allayla waalnnahara la yafturoona (Surat Al Anbiyah 21:20)

    Tafsir: Wao (Malaika) wanamtukuza (Allah Subhanahu wa Ta’ala ) mchana na usiku na kamwe hawapunguzi (kasi katika kumtukuza huko).

    Vile vile miongoni mwa sifa za Malaika ni kutofanya dhambi na kutokua na khiari ya kufanya mambo, na hivyo hua hawaasi katika utekelezaji wa mambo waliyoamrishwa kufanya na Allah Subhanah wa Ta’ala, kama inavyoelezea Qur’an:

    ُروَن﴾َمآ أََمَرُهْم َويـَْفَعُلوَن َما يـُْؤمَ ٱهللََّ الَّ يـَْعُصوَن ﴿َملَـِئَكٌة ِغَالٌظ ِشَدادٌ Mala-ikatun ghiladhun shidadun la yaAAsoona Allaha ma amarahum wayafAAaloona ma yu/maroona (Surat At Tahrim 66:6)

    Tafsir:..Malaika wakubwa na wakali, ambao kamwe hawaasi amri wanazopewa na Allah, bali hutekeleza kile wanachoamrishwa.

    Ingawa Malaika wako wengi sana kiidadi, lakini kila mmoja hua na kazi yake maalum, hua hawana jinsia, wanao uwezo wa kujigeuza katika hali na maumbo mbali mbali na vile vile wametofautiana ki hadhi na kidarja. Malaika mwenye hadhi ya juu kabisa ni Malaika Jibril A’layhi Salaam ambae ni Kiongozi Mkuu wa Malaika wote.

    Baada ya kuumbwa viumbe Malaika, wakafuatia kuumbwa viumbe wajulikanao kama Majini au Jinn. Neno Jinn linatokana na neno Jannah ambalo maana yake ni kutoonekana au kufichika. Viumbe hawa wao waliumbwa kabla ya kuumbwa kwa kiumbe Mtu au Adam, kama inavyoelezea Surat Al Hijr:-

    ْن َمحٍَإ مَّْسُنوٍن ٱِإلنَسانَ ﴿َوَلَقْد َخَلْقَنا َلْقَناُه ِمن َوٱْجلَآنَّ خَ -ِمن َصْلَصـٍل مِِّر ٱلسَُّمومِ ﴾قـَْبُل ِمن �َّ

  • 30

    Walaqad khalaqna al-insana min salsalin min hama-in masnoonin - Waaljanna khalaqnahu min qablu min nari alssamoomi (Surat Al Hijr 15:26-27).

    Tafsir: Na kwa hakika, tumemuumba Mtu kutokana na udongo wenye kutoa sauti wa mfinyanzi; Na Majini, tumewaumba kabla yake kutokana na moto usiokua na moshi.

    Kama inavyosema aya hiyo kua kitu kinachowatofautisha viumbe Majini na Watu ni asili ya maumbile yao kwani wao kutokana na kuumbwa na moto usiokua na moshi basi wamekua na nguvu na uwezo wa kutoonekana na baadhi ya viumbe wengine na pia hua na uwezo wa kujibadilisha katika maumbo wayatakayo yakiwemo maumbo ya viumbe wengine pia. Majini wanao uwezo wa kuteka nyara na kuzitawala akili, ufahamu na miili ya viumbe wengine, na wamejaaliwa uwezo huo katika hali ya kua ni mtihani dhidi yao, ili kuangaliwa namna watakavyoutumia uwezo huo Ulimwenguni na kubeba majukumu yanayotokana na matumizi hayo.

    Ingawa Majini wameumbwa kwa moto, lakini katika hali fulani hua wanafanana na Bani Adam na kufanana kwao kunatokana na maumbile ya kua wao pia hua na sifa kama walizonazo Watu kwani hua wanafahamu, wanakula, wanakunywa, wanoana, wanazaana na kupata watoto, wanakufa, n.k. Majini wamegawika katika makundi yafuatayo:-

    1. Afriit: Hawa hua ni Jinni mkubwa na mwenye nguvu sana na hua ni waharibifu sana na husababisha madhara makubwa kwa Bani Adam .

    2. Arwaah: Hawa hua ni wale ambae huwaathiri na kuwadhibiti Bani Adam vijana.

    3. Aamar: Hawa hua ni Majini ambao wanaoishi majumbani pamoja na watu. 4. Shaytan: Hawa hua ni wale ambao ni wafuasi wa Iblis.

    Ndani ya makundi hayo kuna Majini wa aina mbili, kuna Majini wanaotii amri za Allah na pia wapo wasiotii, kama vile inavyoelezea Qur’an katika Surat Al Jinn pale Majini hao waliposema:

    نـَنَّآ َأن لَّن َوَأ�َّ ظَ -ُكنَّا طََرآِئَق ِقَدداً ِلكَ ذٰ ﴿َوأَ�َّ ِمنَّا الصَّـِلُحوَن َوِمنَّا ُدوَن ْعَنا -ْرِض َوَلن نـُّْعِجَزُه َهَرابً اْألَ ِىف ٱهللََّ نـُّْعِجَز ا مسَِ ءَاَمنَّا ِبِه ْهلَُدىٰ ٱَوَأ�َّ َلمَّ

    َفَمن يـُْؤِمن بَِربِِّه َفالَ َخيَاُف َخبْساً َوالَ َرَهقًا﴾

  • 31

    Waanna minna alssalihoona waminna doona dhalika kunna tara-iqa qidadan; Wanna dhananna an lan nuAAjiza Allaha fee al-ardhi walan nuAAjizahu haraban; Waanna lamma samiAAna alhuda amanna bihi faman yu/min birabbihi fala yakhafu bakhsan wala rahaqan (Surat Al Jinn 72:11-13)

    Tafsir: Hakika miongoni mwetu kuna baadhi ambao ni wacha Mungu, na wengine hua ni kinyume chake. Sisi tuna makundi yenye njia tofauti. Sisi ni wenye kufikiri kua kamwe hatutoweza kumkimbia Allah ardhini wala kumkimbia kwa kuruka hewani; Na kwa hakika tumeusikia uongofu, na tumeuamini, na yeyote yule atakemuamini Mola wake kamwe hawezi kua na khofu ya kupunguziwa malipo ya amali zake njema au ya kuzidishiwa adhabu za makosa yake.

    Majini wasiotii amri za Allah Subhanahu wa Ta’ala hua wanajulikana pia kama Shaytan neno ambalo kwa kiarabu humaanisha sifa ya kiumbe alieasi, aliepotoka na hivyo kukaa mbali na ukweli na wakati huo huo kufanya kila anachoweza ili kuwapotosha viumbe wengine kuhusiana na ukweli huo.

    KUUMBWA KWA NABII ADAM.

    Baada ya kuumbwa viumbe hivyo kikafuatia kuumbwa kwa Bashar au Mtu. Neno la kiarabu Bashar linatokana na mzizi wa neno ‘Ba-Shin-Ra’ ambalo si lenye kumaanisha tu bashirio, furahio, habari muhimu yenye kubadilisha muonekano wa mtu aliepokea habari hiyo aliyopewa na mgusano wa maingiliano lakini pia mzizi wa neno hilo ‘Ba-Shin-Ra’ lina maana ya uwezo na uzuri wa muonekano wa umbo la nje la Bani Adam, na hii ndio maana ambayo imetumika katika kulielezea ‘Umbo bora la kiumbe hai lenye kila sifa bora na iliyokamilika kikamilifu’ la kiumbe Mtu katika aya ifuatayo:

    ْن محََ ِإىنِّ َخـِلٌق َبَشًرا مِّن صَ لِْلَمآلِئَكةِ ﴿َوِإْذ قَاَل رَبَُّك ﴾ٍإ مَّْسُنونٍ ْلَصـٍل مِّ Wa-idh qala rabbuka lilmala-ikati innee khaliqun basharan min salsalin min hama-in masnoonin (Surat Al Hijr 15:28).

    Tafsir: Na (kumbuka) wakati Mola wako alipowaambia Malaika. Hakika mimi nitamuumba Bashar kutokana na udongo wa mfinyanzi wenye asili ya weusi.

    Kiumbe hiki chenye sifa ya kua na umbo la ‘Bashar’ ni kiumbe Adam, ambae aliumbwa kwa kuchanganywa kwa udongo maalum mlaini na maji, matokeo ya

  • 32

    mchanganyiko ambao ulikua ni udongo wenye kunata kama mfinyanzi na baada ya kumalizwa kufinyangwa, Adam akawa katika Jism (mwili) kubwa zuri na bora lililokua na urefu wa takriban mita 27.5 na upana wa mita 3.5, umbo hilo liliumbwa na kukaa bila ya kua na roho kwa muda wa miaka 40, katika kipindi hiki umbo hilo lilishikamana na kua ni lenye kutoa sauti linapogongwa kama vile sauti ya mtungi wa udongo usiokua na maji na lilikua ni lenye kutoa harufu fulani. Malaika pamoja na Iblis (ambae alikua ni Jini) walikua kila wanapopita katika sehemu iliyosimamishwa Jism la Adam hukishangaa kiumbe hicho. Baada ya miaka 40, Allah Subhanahu wa Ta’ala akampulizia Adam roho yake.

    Ingawa Allah Subhanahu wa Ta’ala anao uwezo wa kuumba vitu au viumbe kwa ghafla moja kun fayakun ( ُكُن فَیَكُون) (kua na kinakua), lakini kutokana na busara zake, ikiwemo kutufunza sisi Bani Adam kutokua na papara katika vitendo vyetu na busara nyengine ambazo anazozijua yeye mwenyewe, basi aliamua kumuumba Adam kwa kuchukua muda fulani kutoka hatua moja hadi nyengine, kwa kuufinyanga udongo katika umbo la Adam, na kisha akakiumba kizazi cha kiumbe huyo ndani ya kiumbe hicho, kizazi ambacho kinajulikana kama Bani Adam, na kisha akalipulizia roho umbo hilo la Adam kama yeye mwenyewe Allah Subhanahu wa Ta’ala anavyotufahamisha kwa kusema:

    ﴾ِمن ِطنيٍ ٱلَِّذۤي َأْحَسَن ُكلَّ َشْيٍء َخَلَقُه َوبََدأَ َخْلَق ٱِإلْنَسانِ ﴿ Alladhi ahsana kulla shay-in khalaqahu wabadaa khalqa al-insani min teenin; (Surat As Sajda 32:7) Tafsir: Yeye ndie ambae alieumba kila alichokiumba katika umbo bora: Alianza kwa kumuumba al'l-insāni' (mtu) kutokana na udongo.

    Katika kumuelezea kiumbe Adam, tunaona kua pia aya hii na nyenginezo zimetumia neno ‘Insan’ linalotokanana mzizi wa neno ‘Alif-Nun-Siin’ lenye kumaanisha sifa za kua na hisia mbali mbali za ufahamu, kua na sifa ya urafiki wa kuzungumza na kusikiliza, kua na mazoea ya kuishi kijamii, sifa ya kua na ukaribu, kua na upendo, na ucheshi n.k.

    Na ndio maana Allah Subhanahu wa Ta’ala akasema:

    ﴾َأْحَسِن تـَْقِوميٍ ٱِإلنَساَن ِيفۤ ﴿َلَقْد َخَلْقَنا

  • 33

    Laqad khalaqna al-insana fee ahsani taqweemin(Surat Tinn 95:4)

    Tafsir: Kwa hakika tumemuumba Insan katika Taqwim bora kabisa.

    Tukiangalia tunaona kua aya hii mbali ya kutumia neno Insan lakini pia imetumia neno Taqwim, na kusisitiza kua ni Taqwim bora kabisa, neno Taqwim linatokana na mzizi wa neno QA-MA ambalo kwa kiarabu lina maana ya kua katika hali ya kusimama, kua thabiti, madhubuti, kamilika, sawia bila kua na kasoro yeyote, kua na thamani, hali ya usimamizi, hali ya ulinzi, hali ya mpangilio ulokamilika, hali ya mfumo kamili, hali ya umbo lililokamilika n.k

    Hivyo basi tunaweza kusema kua neno ‘Bashar’ linazungumzia mfumo uliokamilika wa mwili au hali ya umbo bora la nje la Bani Adam na ufanyaji kazi wa viungo mbali mbali vya mwili wake kama vile ngozi, kichwa, mdomo, masikio, macho, pua, mikono, kifua, miguu n.k umbo ambalo pia viumbe wengine kama Malaika hulitumia, pale wanapotumwa na Mola wao kuwaletea ujumbe Bani Adam walioteuliwa kupokea ujumbe na Allah Subhanah wa Ta’ala.

    Lakini neno ‘Insan’ hua linazungumzia mfumo wa umbo uliokamilika kiubora usiokua na kasoro yeyote wa umbo la Bani Adam unaojumuisha pamoja mfumo wa ‘Bashar’ na mfumo wa viungo vya ndani ya mwili wake unaogusia roho, Nafsi, moyo, ubongo, akili, mfumo wa fahamu, mfumo wa damu, mfumo wa hisia n.k na pia ufanyaji kazi wa mifumo hiyo na viungo hivyo vya ndani vikishirikiana na viungo vya nje kunakompelekea kiumbe mtu kua na hisia mbali mbali za kimwili kama kuona, kusema, kusikia, kupenda, kuchukia, kutamani, kutimiza mahitaji mbali mbali ya kinafsi, kiroho, kimwili, n.k.

    Ubora, ukamilifu na uzuri wa Insan unaelezewa zaidi katika aya zinazofuatia:-

    ُمثَّ َجَعَل - َن ُكلَّ َشْيٍء َخَلَقُه َوبََدأَ َخْلَق ٱِإلْنَساِن ِمن ِطنيٍ ٱلَِّذۤي َأْحسَ ﴿َجَعَل َلُكُم ُمثَّ َسوَّاُه َونـََفَخ ِفيِه ِمن رُّوِحِه وَ -َنْسَلُه ِمن ُسالََلٍة مِّن مَّآٍء مَِّهٍني ﴾َدَة قَِليًال مَّا َتْشُكُرونَ ْفئِ اْألَ وَ ٱلسَّْمَع َوٱألَْبَصارَ

    Alladhee ahsana kulla shay-in khalaqahu wabadaa khalqa al-insani min teenin, Thumma jaAAala naslahu min sulalatin min ma-in maheenin; Thumma sawwahu wanafakha feehi min roohihi wajaAAala lakumu alssamAAa waal-absara waal-af-idata qaleelan ma tashkuroona (Surat As Sajda 32:7-9)

  • 34

    Tafsir: Ni yeye aliekifanya kizuri kila kitu alichokiumba, na akaanza kumuumba Insan kutokana na udogo. Kisha akakijaalia kizazi chake kutokana mfano bora wa maji yanayo dharaulika, kisha akamtengeneza katika hali iliyokamilika, na akampulizia ndani yake sehemu ya roho yake, na akakupeni uwezo wa kusikia na kuona na kuhisi: lakini mnashukuru kidogo tu!

    Aya hizi zinamuelezea Insan alivyoumbwa na kukamilishwa kwake kwa kutumia kauli isemayo ‘Kisha akampulizia ndani yake Ruhi yake’ ambayo inamaanisha kua Allah Subhanahu wa Ta’ala alimpulizia Adam ndani yake Roho yake iliyoumbwa na Allah Subhanah wa Ta’ala. Hivyo neno hili Ruh ambalo kwa Kiswahili tunasema ‘Roho’ ambayo Adam amepuliziwa hua halimaanishi kua ni kama sehemu ya Allah Subhanahu wa Ta’ala ambayo imeingizwa ndani ya Adam. La hasha! kwani kusema, kufikiri au kufahamu hivyo hupelekea kuinga katika Kufr.

    Allahuma nsurna Aa’la al Kafirin…Aamin

    Imam Fakhr Ad Din al Razi anasema katika kufafanua maana kauli hiyo kua: ‘Kwa sababu Qur’an imeweka wazi kua Allah Subhanahu wa Ta’ala ni Ahad (mmoja), yaani umoja uzioweza kugawika katika sehemu nyengine, na tafsiri inasema kua hii ‘Ruh’ imeumbwa moja, basi sifa ya kujumuishwa kwake Ruh hii na Allah Subhanahu wa Ta’ala aliposema ‘Ruh’ yangu hua ni kule kunakoelezeka kwa kiarabu kama Idhafat at Tashrif yaani ‘kupewa sifa ya kutukuzwa’, inayoonesha kua Ruh au Roho iliyomo ndani ya mtu huyu wa kwanza na kizazi chake chote kua ni ‘Tukufu, yenye Hadhi na Thamani kubwa sana’’.

    Ruh hiyo imeumbwa katika hali ya asili ya Fitra kama anavyosema Allah Subhanahu wa Ta’ala:

    َها َال تـَْبِديَل ٱهللَِّ ٱلَِّىت َفطََر ٱلنَّاَس َعلَ ﴿فََأِقْم َوْجَهَك لِلدِّيِن َحِنيفاً ِفْطَرَة يـْ﴾ِلَك ٱلدِّيُن ٱْلَقيُِّم َولَـِٰكنَّ َأْكثـََر ٱلنَّاِس َال يـَْعَلُمونَ ِخلَْلِق ٱهللَِّ ذٰ

    Faaqim wajhaka lilddeeni haneefan fitrata Allahi allatee fatara alnnasa AAalayha la tabdeela likhalqi Allahi dhalika alddeenu alqayyimu walakinna akthara alnnasi la yaAAlamoona (Surat Ar Rum 30:30)

  • 35

    Tafsir: Hivyo uelekeze uso wako katika dini, kama Hanifa (Hali ya kutoabudu yeyote isipokua Allah tu) wa Fitra ya Allah, ambayo (hali ya kimaumbile) aliyowaumbia Watu. Hamna kubadilika katika viumbe vya Allah, hiyo ndiyo dini iliyosimama sawa sawa lakini watu wengi hawajui. Hivyo kutokana na hali ya uasili wa Ruh ni kua ina Fitra, basi hua ni jambo la maumbile kwa Bani Adam kujua na kufahamu kua yeye ameumbwa na kwa kua ameumbwa basi pia vile vile atakuwepo aliemuumba, na pale inapotokea kua Bani Adam akafikiria vyenginevyo basi hua ametoka katika uasili wa maumbile yake. Kwani anasema Allah Subhanahu wa Ta’ala kua:

    َوِإْذ َأَخَذ رَبَُّك ِمن َبِينۤ آَدَم ِمن ُظُهورِِهْم ُذرِّيـَّتـَُهْم َوَأْشَهَدُهْم َعَلٰى أَنُفِسِهْم ﴿ا ِبَربُِّكْم قَاُلواْ بـََلٰى َشِهْدَ� َأن تـَُقوُلواْ يـَْوَم ٱْلِقَياَمِة ِإ�َّ ُكنَّا َعْن َهـٰذَ أََلْستُ

    ﴾َغاِفِلنيَ Wa-idh akhadha rabbuka min banee adama min dhuhoorihim dhurriyyatahum waashhadahum AAala anfusihim alastu birabbikum qaloo bala shahidna an taqooloo yawma alqiyamati inna kunna AAan hadha ghafileena.(Surah Al-A'raf, 7:172)

    Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wako, alipowatoa watoto wa Adam (Bani Adam) katika sehemu za siri za wazee wao, wakiwa katika hali ya mbegu na akawashuhudisha katika Nafsi zao kwa kusema ‘Jee mimi si Mola wenu?’, nao wakajibu, ‘Naam tunakushuhudia’, hivyo msije mkasema katika siku ya Malipo kua, ‘Tulikua tumeghafilika’.

    Tukio hili hua linajulikana kama tukio la kula kiapo cha Ahadi, ambayo ni ahadi ya kumshuhudia Allah Subhanahu wa Ta’ala kua ndie Muumbaji wa viumbe vyote, ambapo Ruh za kizazi chote cha Adam kabla ya kuja ulimwenguni zilitolewa katika sehemu za siri za Adam, na kulishwa kiapo hicho, kisha zikarejeshwa na kuwekwa katika mfumo wa hali ya pazia la kiza iliyohifadhi vizazi na vizazi vya Bani Adam kimoja baada ya chengine, kwa makadirio na majaaliwa maalum ya maelfu na maelfu ya miaka na miaka, vizazi na vizazi, kiasi ya kua kila mmoja hawezi kuingia ulimwenguni kupitia katika sehemu za siri za mzazi wake au kuondoka ulimwenguni baada ya kuingia kwake kabla ya kufika mda wake maalum wa kuingia na kutoka ulimwenguni kama inavyosema Qur’an:

  • 36

    ﴾َما َتْسِبُق ِمْن أُمٍَّة َأَجَلَها َوَما َيْسَتْأِخُرونَ ﴿ Ma tasbiqu min ommatin ajalaha wama yasta/khiroona (Surat Al Mu’minun 23:43) Tafsir: Hakuna Ummah (Kizazi) utakaoweza kuyaharakisha majaaliwa yake wala utakaoweza kuyachelewesha. Allah Subhanahu wa Ta’ala anaweka wazi kua kati ya viumbe vyote hivyo alivyoviumba, basi hakuwaumba Majini na Watu kwa ajili ya kumsaidia yeye kitu fulani au wamfanyie kitu fulani ambacho anakihitaji kutoka kwao, bali ameviumba viumbe hivyo ili vipate kumuabudu kwa kumpenda, kwa kumuogopa, kumnyenyekea na kumtegemea Allah Subhanahu wa Ta’ala tu peke yake, hakika yeye ni mwenye kuvipatia rizki zao viumbe vyote hivyo kutokana na uwezo wake, kama alivyosema katika Qurán:

    ُهم مِّن ّرِْزقٍ -ِإالَّ لِيَـْعُبُدوِن ٱجلِْنَّ َوٱِإلنسَ ﴿َوَما َخَلْقُت َوَمآ َمآ أُرِيُد ِمنـَْ ُهَو ٱلرَّزَّاُق ُذو ٱْلُقوَِّة ٱْلَمِتنيُ -أُرِيُد َأن يُْطِعُموِن ﴾ ِإنَّ ٱهللَّ

    Wama khalaqtu aljinna waal-insa illa liyaAAbudooni; Ma oreedu minhum min rizqin wama oreedu an yutAAimoon; Inna Allaha huwa alrrazzaqu dhoo alquwwati almateenu (Surat Adh Dhariyat 51:56-58).

    Tafsri: Sikuwaumba Majini na Bani Adam isipokua waniabudu mimi. Sitafuti rizki kutoka kwao wala sijataka wanilishe. Kwa hakika Allah ni mwenye kutoa rizki, mwenye uwezo na nguvu juu ya kila kitu.

    Baina ya viumbe vitatu hivyo vyenye hadhi alivyoviumba Allah Subhanah wa Ta’ala, yaani Malaika, Majini na Watu, basi wa kwanza kuumbwa na Allah Subhanahu wa Ta’ala walikua ni Malaika ambao waliumbwa katika siku ya Jumatano, na miaka baadae wakaumbwa Majini lakini katika siku ya Al Khamis na pia miaka baadae akaumbwa Adam na pia katika siku ya Ijumaa, na kati ya viumbe vyote, Adam alikua ni kiumbe bora mwenye hadhi ya juu zaid miongoni mwao, hivyo ulipofika wakati wa kuumbwa kwake Allah Subhanahu wa Ta’ala aliwaambia viumbe hao waliomtangulia katika kuumbwa kwa kusema kama inavyosema Qur’an:

  • 37

    ًة قَاُلواْ َأَجتَْعُل ِفيَها َمن َخِليفَ ٱَألْرضِ ﴿َوِإْذ قَاَل رَبَُّك لِْلَملَـِئَكِة ِإّينِ َجاِعٌل ِىف ۤ ُس َلَك قَاَل َوَحنُْن ُنَسبُِّح ِحبَْمِدَك َونـَُقدِّ ٱلدَِّمآءَ يـُْفِسُد ِفيَها َوَيْسِفُك أَْعَلُم ِإّينِ

    ﴾َما الَ تـَْعَلُمونَ Wa-idh qala rabbuka lilmala-ikati innee jaAAilun fee al-ardhi khaleefatan qaloo atajAAalu feeha man yufsidu feeha wayasfiku alddimaa wanahnu nusabbihu bihamdika wanuqaddisu laka qala innee aAAlamu mala taAAlamoona (Surat Al Baqara 2:30)

    Tafsir: Na kumbuka wakati Mola wako aliposema kuwaambia Malaika: ‘Hakika mimi nitajaalia Khalifah katika ardhi kizazi baada ya kizazi’, nao wakasema ‘Utajaalia wale ambao watafanya ufisadi na kumwaga damu ndani yake?, wakati sisi tunakusifu kwa sifa zako, tunakushukuru na kukutukuza’ Allah akasema : ‘Mimi nnajua kile msichokijua’

    Anasema Imam Fakhr ad Din Al Razi kua: ‘Kauli ya Malaika ya kusema kua ‘Utajaalia wale ambao watafanya ufisadi na kumwaga damu ndani yake?, wakati sisi tunakusifu kwa sifa zako na kukushukuru na kukutuza’ ilikua ni kama maombi kutoka kwao kua haina haja ya kuumbwa viumbe wengine kwani wao wanaweza kukaa pia duniani na kuendelea kumtukuza Allah Subhanah wa Ta’ala, lakini hata hivyo Allah Subhanahu wa Ta’ala akawaambia, ‘Mimi nnajua kile msichokijua’, akimaanisha kua Allah Subhanahu wa Ta’ala anajua vizuri zaidi ni lipi bora kwao wao Malaika, baina ya kukaa Duniani ama Mbinguni.’ Kisha Allah Subhanahu wa Ta’ala akasema katika Qur’an:

    أبَِْمسَآِء نِْبُئوِىن أَ ﴿َوَعلََّم ءَاَدَم اَألْمسَآَء ُكلََّها ُمثَّ َعَرَضُهْم َعَلى اْلَمَلـِئَكِة فـََقاَل لَّْمتـََنآ إِنََّك قَاُلواْ ُسْبَحـَنَك الَ ِعْلَم لََنآ ِإالَّ َما عَ -َهـُؤَالِء ِإن ُكنُتْم َصـِدِقَني

    ُهم أبَِْمسَآِئِهْم فـََلمَّآ - ٱْلَعِليُم ٱحلَِْكيمُ أَنَت أبَِْمسَآِئِهم نـَْبَأُهمْ أَ قَاَل يَـاءَاَدُم أَنِبئـْ

  • 38

    ُدوَن َوَما ُكنُتْم ُم َما تـُبْ َوأَْعلَ ٱلسََّماَواِت َوٱَألْرضِ َغْيَب أَْعَلُم أَُقْل لَُّكْم ِإّينِ قَاَل ﴾َتْكُتُمونَ

    WaAAallama adama al-asmaa kullaha thumma AAaradahum AAala almala-ikati faqala anbi-oonee bi-asma-i haola-i in kuntum sadiqeena; Qaloo subhanaka la AAilma lana illa ma AAallamtana innaka anta alAAaleemu alhakeemu; Qala ya adamu anbi/hum bi-asma-ihim falamma anbaahum bi-asma-ihim qala alam aqul lakum innee aAAlamu ghayba alssamawati waal-ardhi waaAAlamu ma tubdoona wama kuntum taktumoona; (Surat Al Baqara 2:31-33)

    Tafsir: Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, Kisha akavionesha vitu hivyo kwa Malaika, na kuwaambia ‘Nitajieni majina ya vitu hivi ikiwa nyinyi ni wakweli’, Wao (Malaika) wakasema: ‘Utukufu ni wako, Sisi hatuna I’lm isipokua ya kile ulichotufundisha, hakika wewe ni mjuzi wa kila kitu na mwingi busara’. (Allah) Akasema: ‘Ewe Adam watajie majina yake’, na alipowatajia majina ya vitu hivyo (Allah akasema): ‘Jee sikukwambieni kua mimi najua mambo ya Ghayb (yaliyofichika) mbinguni na ardhini, na nnajua kile mnachokiweka wazi na kile mnachokificha’.

    Hivyo Adam akafundiswa majina ya vitu vyote viliopo mbele yake yeye na viumbe hivyo vyengine, kisha akaviuliza viumbe vyengine majina ya vitu hivyo, nao wakashindwa kuvijua, Allah Subhanahu wa Ta’ala akamuuliza Adam ambae nae akataja majina ya vitu hivyo, baada ya kutaja majina ya vitu hivyo Malaika wakajua kua Adam yuko juu zaid yao ki I’lm na kiheshima, hivyo Allah Subhanahu wa Ta’ala akawaamrisha kwa pamoja wote Malaika na Iblis waliopo mbele yake kumsujudia Adam.

    وََكاَن َوٱْسَتْكبَـرَ َأَىبٰ الًَّدَم َفَسَجُدواْ ِإالَّ إِْبِليَس ٱْسُجُدواْ ﴿َوِإْذ قـُْلَنا لِْلَمَلـِئَكِة ﴾ٱْلَكاِفرِينَ ِمَن

    Wa-idh qulna lilmala-ikati osjudoo li-adama fasajadoo illa ibleesa aba waistakbara wakana mina alkafireena (Surat Al Baqara 2:34)

  • 39

    Tafsir: Na (Kumbuka) wakati tulipowaambia Malaika: ‘Msujudieni Adam’. Na wakasjudu isipokua Iblis, akakataa na kua na kibri, na akawa ni miongoni mwa waliokufuru.

    Hikma iliyomo katika tokeo hili ni kuwaonesha Malaika na Iblis kua darja ya Adam iko juu kuliko darja yao, kumuonesha Adam kua yeye ni kiumbe bora zaid kuliko viumbe wawili hao, na pia kumuwekea wazi Adam kua Iblis ni Adui yake mkubwa ambae aliekataa kua chini yake.

    Ingawa Malaika na Iblis walipewa amri inayotakiwa kutekelezwa lakini Iblis alikataa kuitii amri hiyo, si kutokana na kua yeye hakua Malaika, kwa sababu ingawa kweli hakuwa miongoni mwa Malaika, lakini amri iliyotolewa ilikua ni ya jumla kwa wote waliokuwepo sehemu hiyo, nae alijumuishwa katika amrisho hi