hotuba ya waziri wa ardhi...• kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya arusha,...

80
1 HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI, MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI, (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2007/08 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa leo ikiwa ni Bunge la Bajeti la Pili kwa Serikali ya awamu ya nne. Naipongeza Serikali na Bunge lako Tukufu kwa kusimamia kwa mafanikio majukumu ya Serikali. Nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa ushirikiano ambao Kamati ya Kilimo na Ardhi imekuwa ikinipatia katika kutimiza majukumu ya uendelezaji wa Sekta ya Ardhi. Kwa ujumla ninawashukuru waheshimiwa wabunge kwa kutunga Sheria tatu zinazohusu uendelezaji wa makazi na matumizi bora ya ardhi vijijini katika kikao cha nane cha Bunge Mwezi Aprili, 2007. 2. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo ada, Bunge lako Tukufu limepokea na kuzingatia misingi ya Jumla ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2007/08, kupitia Hotuba za Mheshimiwa Waziri

Upload: others

Post on 30-Dec-2019

30 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

1

HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO

YA MAKAZI, MHESHIMIWA JOHN POMBE MAGUFULI,

(MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO

NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA

2007/08

UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, naomba kumshukuru Mwenyezi

Mungu kwa kutuwezesha kukutana hapa leo ikiwa ni Bunge la

Bajeti la Pili kwa Serikali ya awamu ya nne. Naipongeza Serikali

na Bunge lako Tukufu kwa kusimamia kwa mafanikio majukumu

ya Serikali. Nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa

ushirikiano ambao Kamati ya Kilimo na Ardhi imekuwa ikinipatia

katika kutimiza majukumu ya uendelezaji wa Sekta ya Ardhi. Kwa

ujumla ninawashukuru waheshimiwa wabunge kwa kutunga

Sheria tatu zinazohusu uendelezaji wa makazi na matumizi bora

ya ardhi vijijini katika kikao cha nane cha Bunge Mwezi Aprili,

2007.

2. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo ada, Bunge lako Tukufu

limepokea na kuzingatia misingi ya Jumla ya Bajeti ya Serikali kwa

mwaka wa fedha 2007/08, kupitia Hotuba za Mheshimiwa Waziri

Page 2: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

2

wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Mheshimiwa Waziri wa

Fedha na Mheshimwa Waziri Mkuu. Nawapongeza na

kuwashukuru wote kwa Hotuba zao nzuri. Kufuatia misingi hiyo

ya jumla, Hoja yangu itajielekeza katika kuainisha malengo na

mikakati ya utekelezaji katika Sekta ya Ardhi, Nyumba na

Maendeleo ya Makazi.

3. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza

shughuli zake kulingana na miongozo ya Serikali kama vile

Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania

(MKUKUTA), Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Ilani ya CCM ya

uchaguzi ya mwaka 2005 pamoja na maagizo mbalimbali

yanayotolewa na viongozi wa kitaifa, wakiwemo wabunge.

4. Mheshimiwa Spika, ardhi ni mojawapo ya rasilimali za

msingi kwa uhai wa binadamu na viumbe vyote juu yake. Ardhi

hubeba raslimali zingine zote asili na miundo mbinu. Kwa bahati

mbaya ardhi haiongezeki lakini wategemezi wa ardhi na mahitaji

yao huongezeka kila siku. Mbaya zaidi, baadhi ya mahitaji hayo

hukinzana. Mkulima anahitaji ardhi yenye rutuba kuzalisha

mazao, wakati huo huo mfugaji anahitaji ardhi hiyo kwa malisho

ya mifugo yake na mwanamazingira anahitaji kilimo na mifugo

Page 3: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

3

katika hali ambayo hifadhi ya mazingira inazingatiwa ambayo pia

ni muhimu kwa uhai wa binadamu na viumbe vinginevyo.

Mkanganyiko huu hauna jibu sahihi na la haraka. Njia muafaka ya

kushughulikia mkanganyiko huu ni kuhakikisha kuwa kila kipande

cha ardhi nchini kinapimwa, kinapangwa na kusajiliwa. Hii ndiyo

dhana madhubuti ya uendelezaji endelevu wa ardhi kwa faida ya

kizazi kilichopo na kijacho.

5. Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo

hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo na Ardhi,

naomba kutoa Hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa likubali

kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara

ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha

2007/08.

UTEKELEZAJI WA BAJETI KATIKA MWAKA 2006/07

Ukusanyaji wa Mapato

6. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekuwa ikitekeleza

mikakati mbalimbali kwa lengo la kuboresha ukusanyaji wa

mapato, utaona kwamba Wizara imeweza kuongeza makusanyo

ya kodi ya pango la ardhi toka Shilingi milioni 230 kwa mwaka

Page 4: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

4

1993/94 hadi Shilingi bilioni 8.37 kwa mwaka 2006/07. Mikakati

hiyo ni pamoja na kuboresha kumbukumbu za ardhi za wamiliki

wa viwanja na mashamba na kuhamasisha ukusanyaji wa kodi

kwa njia ya matangazo ya televisheni, radio na magazeti.

7. Mheshimiwa Spika katika mwaka wa fedha 2006/07,

Wizara ilikuwa na lengo la kukusanya jumla ya Shilingi

10,747,833,000 kutokana na vyanzo mbalimbali. Hadi kufikia

Juni 2007, Wizara imekusanya jumla ya Shilingi 10,087,865,007

ambazo ni sawa na asilimia 94 ya lengo. Kati ya makusanyo

hayo, Shilingi 8,598,450,357 ambazo ni sawa na asilimia 85

ya makusanyo, ni kodi ya pango la ardhi itokanayo na viwanja

pamoja na mashamba.

8. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2007/08

Wizara yangu ina lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi

11,091,832,000; Maduhuli haya yatakusanywa kwa kutumia

mikakati ifuatayo:- Kuelimisha wananchi kwa kutumia matangazo

kwa njia ya televisheni, radio na magazeti; kufuatilia kwa karibu

vituo vya makusanyo katika Halmashauri za Miji na Wilaya ili

kuthibiti mapato na sheria za fedha; kujenga uwezo na kuboresha

vituo vya makusanyo kwa kuvipatia vifaa mbalimbali zikiwemo

Page 5: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

5

Kompyuta na programu ya kukadiria kodi na kuboresha hazina ya

kumbukumbu za ardhi. Aidha, kuanzia mwaka wa fedha 2007/08

kituo cha Dar es Salaam kitatoa huduma ya ukadiriaji na ulipaji

kodi ya pango la ardhi katika sehemu moja, badala ya utaratibu

uliopo sasa unaowalazimu wateja kupita ofisi zaidi ya moja. Hatua

hiyo itapunguza msongamano na kuongeza ufanisi. Natoa wito

kwa Halmashauri kutoa kipaumbele katika suala la

ukusanyaji na udhibiti wa kodi ya pango la ardhi kwani

hayo ni mapato ya Serikali.

Matumizi

9. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07,

Wizara yangu iliidhinishiwa jumla ya Shilingi 16,208,689,000

kwa ajili ya matumizi ya kawaida, kati ya hizo Shilingi

3,666,109,000 zilitengwa kwa ajili ya mishahara na Shilingi

12,542,580,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo. Miradi ya

maendeleo ilitengewa Shilingi 2,065,994,000.

Page 6: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

6

10. Mheshimiwa Spika, kazi muhimu zilizotekelezwa na

Wizara yangu katika mwaka wa fedha 2006/07 ni pamoja na:-

• Kupima mipaka ya vijiji 2,668 katika mikoa tisa ya Pwani, Lindi,

Iringa, Mbeya, Rukwa, Kigoma, Kagera, Shinyanga na Tanga;

• Kufanya mawasiliano ya kuimarisha mipaka ya Kimataifa kati

ya Tanzania na; Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na

Comoro.

• Kuchora na kuhakiki ramani za miji 41 ya Kanda ya Ziwa;

• Kusambaza Government Notices (GN) zinazoonyesha mipaka

ya Wilaya kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa yote nchini;

• Kusimamia upimaji wa viwanja katika miji ya Dar es Salaam,

Mwanza, Mbeya na Morogoro. Hadi sasa jumla ya viwanja

49,228 katika miji hiyo vimepimwa.

• Kusajili hatimiliki na nyaraka nyingine za kisheria 24,647 na

kutoa vyeti vya ardhi ya vijiji 211 na Hatimiliki za kimila 3,940.

• Kutwaa ardhi kwa manufaa ya umma na kubatilisha miliki 637

katika mikoa mbalimbali hapa nchini;

• Kutoa vibali vya uwekaji rehani hakimiliki 594 na uhamisho wa

miliki 1,352;

• Kutoa elimu kwa umma juu ya Sera na Sheria za ardhi katika

wilaya 23 na vijiji 172;

• Kuhakiki miliki na kutatua migogoro ya ardhi;

Page 7: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

7

• Kufanya Uthamini wa nyumba na mali 2800 kutoka sehemu

mbalimbali nchini

• Kuandaa mipango ya muda mrefu ya miji miwili ya Mwanza na

Mtwara/Mikindani na mipango ya muda mfupi ya Miji minane

ya Tandahimba, Tunduru, Namtumbo, Masasi, Babati,

Mererani, Ushirombo na Misungwi;

• Kutayarisha miswada ya Sheria ya Mipangomiji na Vijiji, na

Sheria ya kusimamia maadili ya Maafisa Mipangomiji;

• Kuandaa mipango ya uendelezaji upya maeneo ya kati ya miji

ya Tanga na Singida, na maeneo ya Upanga na Kurasini Jijini

Dar es salaam;

• Kutambua miliki 10,842 kwenye maeneo yaliyojengwa kiholela

na kupanga maeneo ya pembezoni mwa jiji la Dar es salaam.

Hadi sasa jumla ya miliki 230,000 zimetambuliwa na leseni za

makazi 75,000 zimetolewa;

• Kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Nyumba;

• Kutayarisha Mpango wa Taifa wa Matumizi ya Ardhi, Mipango

ya Matumizi ya Wilaya 13 na Mipango ya Matumizi ya Vijiji 172

nchini;

• Kusikiliza na kuamua mashauri ya ardhi na nyumba 4180;

• Kuunda mabaraza ya ardhi na nyumba katika wilaya 10;

Page 8: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

8

• Kukarabati majengo kwa ajili ya ofisi za mabaraza katika wilaya

5;

• Kutoa elimu ya Sheria ya Mahakama za Ardhi kwa kusambaza

Mwongozo wa Sheria hiyo katika mikoa 8 ya Mara, Mwanza,

Morogoro, Tanga, Ruvuma, Arusha, Manyara na Dar es

Salaam;

• Kufanya utafiti kuhusu vifaa vya ujenzi wa nyumba za gharama

nafuu, teknolojia rahisi za ujenzi na kusambaza matokeo yake

kwa kuendesha semina katika wilaya 4 na mafunzo kwa

vitendo katika wilaya 7;

• Kukusanya kodi ya pango la nyumba za Shirika la Nyumba la

Taifa(NHC) ambapo jumla ya Shilingi 19.8 bilioni

zilikusanywa

• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa

ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa

kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

nyumba zilizopo;

• Kuimarisha ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi na maduhuli

yatokanayo na huduma za ardhi katika vituo 117;

• Kurudisha asilimia 20 ya makusanyo kwenye Halmashauri za

miji na Wilaya na kukagua vituo 73 vya makusanyo;

Page 9: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

9

• Kuingiza kwenye kompyuta viwanja 300,820 na mashamba

5,233 katika Halmashauri 85 nchini ili kurahisisha utoaji wa

huduma katika Halmashauri husika;

• Kukamilisha ujenzi wa mfumo wa masjala ya Ardhi unaotumia

teknolojia ya kompyuta (Computerised Movable Shelves);

• Kukamilisha Mfumo wa Menejimenti ya Habari za ardhi

(Management of Land Information Systems (MOLIS);

• Kukamilisha ujenzi wa tovuti ya Wizara (www.ardhi.go.tz);

• Kukamilisha ujenzi wa mtandao wa mawasiliano ya Wizara

unaounganisha Ofisi za Usajili wa Hati za Kanda katika miji ya

Mwanza, Mbeya, Dodoma, Moshi na Ofisi za Ardhi katika

Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke;

• Kuboresha mazingira ya kazi na kuwezesha watumishi 272

kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi na mrefu ndani na nje ya

nchi. Pia, kuajiri watumishi wapya 93 na kupandisha vyeo

watumishi 109 ambapo kati ya hawa wanawake ni 37;

• Kukamilisha ujenzi wa jengo la Idara ya mifumo ya habari

(Management Information Systems);

• Kuimarisha na kujenga nidhamu na uadilifu kwa lengo la kuleta

ufanisi katika kazi; na,

• Kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI.

Page 10: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

10

MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2007/08

11. Mheshimiwa Spika, mwelekeo wa bajeti ya Wizara kwa

mwaka wa fedha 2007/08 unalenga katika kutekeleza MKUKUTA,

Ibara ya 42 na 68 za Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi

ya Mwaka 2005, na Mkakati wa Kurasimisha Rasilimali na

Biashara Tanzania (MKURABITA). Hivyo kazi zifuatazo zitapewa

kipaumbele katika utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka

huu wa fedha.

• Upimaji wa mipaka ya vijiji na uimarishaji wa mipaka ya

Kimataifa;

• Utoaji wa hati za kumiliki ardhi kimila na uhamasishaji wa

ujenzi wa masjala za ardhi kwa ajili ya usajili wa hati katika

ngazi za vijiji na wilaya;

• Uchoraji wa ramani za msingi;

• Uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya miji ya muda

mrefu na mfupi;

• Ujenzi wa nyumba kwa ajili ya uuzaji na upangishaji;

• Uandaaji wa Kanuni na utekelezaji wa Sheria za Kupanga Miji

na Vijiji na Sheria ya Maadili ya Maafisa Mipango Miji;

• Uelimishaji wa umma kuhusu Sera na Sheria za Ardhi, na

• Uongezaji wa mapato yatokanayo na pango la ardhi.

Page 11: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

11

HUDUMA ZA MAENDELEO YA ARDHI

12. Mheshimiwa Spika, Ardhi ni rasilimali muhimu katika

kuwapunguzia wananchi umasikini. Kwa kutambua hilo, Wizara

yangu imeendelea na utoaji wa hatimiliki, utwaaji ardhi kwa

manufaa ya umma, ukaguzi na uhakiki wa miliki kwa ajili ya

utatuzi wa migogoro kiutawala, usajili wa hatimiliki pamoja na

nyaraka mbalimbali, utoaji vibali vya uwekaji rehani hakimiliki za

ardhi na uhamisho wa miliki, uthamini wa mali, uasisi wa masjala

za Wilaya na Vijiji sambamba na utoaji elimu kwa umma kuhusu

Sheria za Ardhi. Vile vile Wizara imeendelea na jukumu lake la

kuchapisha na kusambaza fomu za aina mbalimbali za kisheria

kwa ajili ya umilikishaji ardhi katika Halmashauri zote nchini.

Pamoja na kutoa huduma hizo, Wizara iliendelea na ukusanyaji

wa maduhuli kutoka vyanzo mbalimbali vinavyohusiana na

huduma za ardhi hususan kodi ya ardhi, ushuru, na ada za

miamala ya ardhi kama vile uhamisho na uwekaji rehani wa milki

za ardhi.

Page 12: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

12

Utoaji Milki

13. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa Fedha

2006/07, jumla ya hati 9,107 zilitayarishwa. Kati ya hizo 6,610

zilitoka Halmashauri na 2,497 ziliandaliwa na Wizara chini ya

mradi wa viwanja 20,000 Dar es Salaam (Jedwali Na. 1).

Vilevile mashamba 87 yako katika hatua mbalimbali za

uhawilishaji kwa mujibu wa Sheria ya ardhi ya Vijiji Na. 5 ya

mwaka 1999 (Sura 114).

14. Mheshimiwa Spika, ili kuongeza uhakika wa Watanzania

kumiliki ardhi yao na kuitumia kujipatia mitaji, Wizara katika

mwaka wa fedha 2007/08 itaendelea kuweka mazingira bora ya

utayarishaji hati ikiwa ni pamoja na kuboresha uwekaji wa

kumbukumbu za umilikaji ardhi ambapo lengo litakuwa ni

kutayarisha hati zipatazo 8,000. Kwa lengo hili Wizara itaendelea

kuhakikisha nyaraka muhimu za kutayarisha hati zinapatikana

hadi kwenye Halmashauri kwa wakati.

Page 13: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

13

Ukaguzi na Uhakiki Miliki kwa Ajili ya Utatuzi wa

Migogoro ya Ardhi

15. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2006/07,

Wizara yangu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kinondoni

ilibuni mkakati maalum wa kuhakiki miliki na maendelezo katika

maeneo yasiyoendelezwa kwa muda mrefu. Malengo ya mkakati

huu ni kujenga hazina ya kumbukumbu sahihi na salama,

kuboresha ukusanyaji kodi na kuandaa hatimiliki. Mkakati huo

unatekelezwa katika maeneo ya Mbezi, Jangwani Beach, Tegeta,

Ununio na Boko yenye jumla ya viwanja 14,531 vilivyopimwa.

Licha ya viwanja hivyo kumilikishwa kuanzia mwaka 1986 idadi

kubwa ya viwanja hivyo havijaendelezwa kikamililifu. Mpaka sasa

viwanja 10,031 vimehakikiwa kwa kutumia picha za anga na

ukaguzi. Kati ya hivyo, viwanja vilivyoendelezwa ni 5,014,

vyenye maendelezo hafifu ni 2,497 na ambavyo havijaendelezwa

kabisa ni 2,520. Uhakiki huu umesaidia Wizara kutatua migogoro

ya muda mrefu na kuchochea kasi ya uendelezaji wa maeneo

hayo.

Page 14: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

14

16. Mheshimiwa Spika, Aidha, napenda kuwakumbusha na

kuwatahadharisha wavamizi wa viwanja kuwa, kwa mujibu wa

kifungu cha 175 cha Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999,

kufanya maendelezo kwenye kiwanja chenye miliki halali ya mtu

bila ridhaa yake ni kosa. Hivyo, mvamizi anatakiwa ama abomoe

jengo lake ili kumpisha mmiliki halali au afanye makubaliano ya

kisheria na mmiliki halali wa kiwanja husika. Hii ndiyo Sheria ni

lazima ifuatwe na itekelezwe.

17. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha

2007/08 Wizara inakusudia kukamilisha uhakiki wa miliki za

viwanja 4,500 vilivyobaki; na kuendelea kubadilisha hati katika

viwanja husika toka hati ya miaka 33 hadi kufikia miaka 99.

Aidha, katika mwaka 2007/08 Wizara yangu kwa kushirikiana na

Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itatengeneza baadhi ya

barabara katika maeneo husika. Natoa wito kwa Halmashauri

zote nchini kuendelea kuhakiki miliki za viwanja na

mashamba katika maeneo yao ili kupunguza migogoro

ambayo inaweza kuepukika.

18. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha

2006/07 Wizara yangu imebatilisha miliki za viwanja na

Page 15: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

15

mashamba 637 katika mikoa mbalimbali hapa nchini,

imeidhinisha vibali vya uhamisho wa miliki 1,352 na vibali vya

rehani 594. Pia katika kipindi hicho mashauri 61 yanayohusu

ardhi yalishughulikiwa na Mahakama. Katika mwaka wa fedha wa

2007/08 Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini

itaendelea kuwahamasisha wamiliki kuendeleza viwanja na

mashamba yao. Hata hivyo pale ambapo watashindwa

kufanya hivyo Wizara yangu itachukua hatua za

kupendekeza kwa Mheshimiwa Rais kufuta miliki hizo na

kisha kumilikisha wananchi wengine.

Usajili wa Hatimiliki na Nyaraka za Kisheria

19. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha

2006/07, Wizara ilikuwa na lengo la kusajili hatimiliki na nyaraka

za kisheria 12,000. Lengo hilo limevukwa kwa kusajili hatimiliki

na nyaraka za kisheria zipatazo 24,647. Kati ya hizo, hatimiliki na

nyaraka 18,598 zimesajiliwa chini ya Sheria ya Usajili Hati (Sura

334). (Jedwali Na. 2); Nyaraka 5,423 zimesajiliwa chini ya

Sheria ya Usajili wa Nyaraka (Sura 117) (Jedwali Na. 3); na

dhamana 626 zimesajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Dhamana

zihamishikazo (Sura 210).

Page 16: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

16

20. Mheshimiwa Spika, kutokana na mwamko wa wananchi

kusajili hati na nyaraka mbalimbali, katika kipindi cha mwaka wa

fedha 2007/08 Wizara yangu itaendelea kuongeza kasi na idadi

ya kutoa hatimiliki kwa wananchi kwa kuimarisha Ofisi ya Msajili

wa Hati ili kuwezesha kusajili hatimilki za ardhi na nyaraka za

kisheria ambapo lengo ni kusajili hati na nyaraka 20,000. Pia,

kufanya mapitio ya Sheria za usajili ardhi na nyaraka kwa lengo la

kuziboresha ili kwenda na wakati na kutoa huduma kwa ufanisi

zaidi.

Utekelezaji wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji

21. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inawajibika kusimamia

utekelezaji wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji ya mwaka 1999

inayohusika na umilikishaji wa ardhi vijijini. Chini ya Sheria hiyo

Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri imekuwa ikitoa elimu

kuhusu miliki ya ardhi vijijini, ujenzi na ukarabati wa Masjala za

Ardhi za Wilaya na za Vijiji, kutoa vyeti vya Ardhi ya Kijiji na

kusajili Hatimiliki za Kimila. Tangu zoezi lilipoanza mwaka 2003/04

jumla ya Masjala 7 za ardhi za Wilaya na Masjala 37 za Vijiji za

mfano zimeanzishwa. Katika mwaka wa fedha 2006/07 Masjala za

Wilaya 7 na Vijiji 14 ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Page 17: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

17

Ukaguzi wa wilaya 53 na vijiji 412 umefanyika kwa lengo la

kuhamasisha ujenzi wa masjala. Aidha, Vyeti vya Ardhi ya Vijiji

211 na Hati za Hakimiliki za Kimila 3,940 zimetolewa kwa

wanavijiji na hivyo kufanya idadi kamili ya vyeti ambavyo

vimetolewa kuwa 402 na Hati za Hakimiliki za Kimila kuwa

5,202.

22. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kwamba hati za

kumiliki ardhi zinamwezesha mwananchi katika kujiletea

maendeleo yake Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri

kuhakikisha wananchi wengi zaidi vijijini wanamilikishwa ardhi

yao. Katika mwaka wa fedha 2007/08 Wizara ina lengo la

kuendelea kutoa elimu, kuhamasisha ujenzi, ukarabati na uzinduzi

wa masjala za Ardhi za Wilaya 16 na Vijiji 78.

23. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kutoa elimu

ya Sera, Sheria za Ardhi na matumizi bora ya ardhi katika Wilaya

mbalimbali. Kwa mfano, Wizara imekuwa ikisisitiza kwa mujibu

wa Sera ya Ardhi ya Mwaka 1995 kuwa kila kipande cha ardhi

kina thamani na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji

Na. 5 ya Mwaka 1999 kifungu cha 3(g) na kwa mujibu wa Sheria

ya Ardhi Na.4 ya Mwaka 1999 kifungu cha 3(g) ardhi yote

Page 18: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

18

inayotwaliwa kwa mtu yeyote kwa ajili ya matumizi yoyote ni

lazima mhusika wa ardhi hiyo alipwe fidia. Katika mwaka 2006/07

Wizara imeendesha mafunzo katika wilaya 23 na Vijiji 172.

Utayarishaji wa vipindi na makala ya elimu ya Sera na Sheria za

Ardhi kupitia Television, radio na magazeti ulifanyika. Aidha,

nakala 2,012 za Sheria ya Ardhi ya Vijiji na kanuni zake na

vijarida 5,270 vya Mwongozo wa kutoa Elimu ya Sheria ya Ardhi

ya Vijiji zilisambazwa sehemu mbalimbali nchini.

24. Mheshimiwa Spika, utaona kuwa utekelezaji wa Sheria ya

Ardhi ya Vijiji bado unaenda kwa kasi ndogo sana. Hii inatokana

na Halmashauri kutotimiza majukumu yao katika kutekeleza

Sheria hii. Pia, Halmashauri hazitumii fursa zilizopo za asasi zisizo

za kiserikali katika kutekeleza sheria hii. Ningependa kusisitiza

kuwa jukumu la utekelezaji wa Sheria hii ni la Halmashauri. Hivyo

Wizara yangu inazikumbusha Halmashauri kutimiza wajibu wao

na kutumia fursa zilizopo kuanzisha Masjala za Ardhi za Vijiji na

Wilaya na kuendelea kutoa elimu ya Sera na Sheria ya Ardhi ya

Vijiji kwa wananchi na watendaji katika maeneo yao. Katika

mwaka wa 2007/08 Wizara yangu itaendelea kushirikiana na

Halmashauri zote nchini kutoa elimu ya mafunzo ya sera na

Page 19: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

19

sheria za ardhi. Aidha, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa umma

kupitia vyombo vya habari.

Uthamini wa Mali

25. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na majukumu ya

kuthamini nyumba na mali nyinginezo kwa madhumuni ya kulipa

fidia, kutoza kodi ya ardhi, mauzo (transfer), mizania (balance

sheet), kuweka rehani, kuomba mikopo, mirathi na bima. Katika

mwaka wa fedha 2006/07 Wizara iliweka lengo la kuthamini

nyumba na mali nyinginezo 2000. Hadi kufikia Juni 2007 jumla

ya nyumba na mali nyinginezo zipatazo 5,519 zilithaminiwa na

kuingizia serikali jumla ya Shilingi 240,825,800. Wizara kwa

mwaka 2007/08 itaendelea kutoa huduma za uthamini ambazo

zinakadiriwa kuingizia serikali jumla ya Shilingi 200,000,000.

Pamoja na kazi za kutoa huduma za uthamini, Wizara inaandaa

sheria ya kusimamia kazi za Uthamini na Wakala wa Miliki (Real

Estate Agency).

26. Mheshimiwa Spika, Wizara ina wajibu wa kuandaa

kumbukumbu ya viwango vya uthamini (Valuation Data Bank)

kwa lengo la kuwezesha uthamini wa mali mbalimbali kufanyika

Page 20: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

20

kulingana na bei ya soko. Kazi ya kuingiza kumbukumbu za

viwango vya thamani wa mali kwenye kompyuta inaendelea. Hadi

Juni 2007 idadi ya kumbukumbu za taarifa za uthamini wa mali

mbalimbali imefikia 821,973. Kwa vile thamani ya ardhi na

nyumba kimsingi hupanda kutokana na mabadiliko ya hali ya

uchumi, zoezi hili litaendelea kuwa la kudumu ili kuwa na viwango

vinavyoendana na thamani ya soko.

KUMBUKUMBU ZA ARDHI NA MAWASILIANO.

27. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imetoa kipaumbele

katika kuboresha mifumo ya habari na mawasiliano kwa lengo la

kuboresha huduma kwa wananchi. Katika jitihada za kuimarisha

hazina ya kumbukumbu, kazi ya kuingiza kumbukumbu kwenye

kompyuta inaendelea. Hadi kufikia mwezi Mei 2007, taarifa za

viwanja 300,820 na mashamba 5,233 zilibainishwa na

kuingizwa kwenye kompyuta. (Jedwali Na. 4.) Pamoja na

juhudi za kuimarisha matumizi ya kompyuta na kuboresha

mawasiliano Makao Makuu na ofisi za Kanda za Usajili wa Hati,

Wizara yangu imeazimia kuendelea kusambaza taaluma na

matumizi ya kompyuta katika Ofisi za Ardhi za Halmashauri. Hadi

sasa Wizara, imepeleka taaluma na kompyuta katika Halmashauri

Page 21: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

21

5 ambazo ni Manispaa za Morogoro, Moshi na Arusha, na Jiji la

Mwanza na Mbeya.

28. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2007/08

Wizara itaendelea kuboresha kumbukumbu za ardhi pamoja na

mkakati wa kuziwezesha Ofisi za Ardhi za Halmashauri nyingine 6

kupata taaluma na kompyuta ili kuimarisha matumizi ya teknolojia

ya habari na mawasiliano. Lengo ni kuboresha huduma na

kupanua wigo wa makusanyo. Natoa wito kwa Halmashauri

zote nchini kuwasilisha takwimu za viwanja na

mashamba ili ziweze kuingizwa kwenye Hazina ya

kumbukumbu za Wizara na hivyo kuboresha huduma kwa

wananchi.

MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA

29. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ina jukumu la

kusimamia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa mujibu

wa Sheria ya Ardhi Na. 2 ya mwaka 2002. Baada ya kuanza

kutumika kwa sheria hiyo mwaka 2003 kumekuwa na ongezeko la

mashauri yanayofunguliwa katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba

ya Wilaya kutokana na wananchi kuelewa thamani ya ardhi. Hadi

Page 22: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

22

kufikia Mei 2007, kulikuwa na jumla ya mashauri 10,382 ambapo

kati ya hayo, 6,872 yalifunguliwa katika mwaka 2006/07.

Ongezeko hili limesababisha kuwepo kwa mlundikano wa kesi. Ili

kukabiliana na tatizo hili Wizara katika mwaka 2006/07

imeendelea kuunda Mabaraza mengine katika wilaya 10 zenye

migogoro mingi ya Ardhi. Napenda kuchukua fursa hii

kuwashukuru viongozi wote wa mikoa na wilaya waliotoa

majengo/ofisi kwa ajili ya Mabaraza hayo. Pamoja na kuunda

Mabaraza mapya, Wizara imejitahidi kupata ufumbuzi wa tatizo la

mlundikano wa kesi kwa kuongeza idadi ya vikao katika Mabaraza

ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Jitihada hizo zimewezesha kuamua jumla ya mashauri 4,180

katika mwaka 2006/07. (Jedwali Na. 5). Aidha, Baraza la Rufaa

la Ardhi ambalo liliongezewa muda, limeamua jumla ya rufaa 61.

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/08 Wizara

itaendelea kuunda Mabaraza mengine katika wilaya 5 kwa

kujenga na kukarabati majengo ambayo yanatolewa na Wilaya ili

kuongeza idadi ya Mabaraza kulingana na fedha iliyotengwa

katika mwaka huu. Pia, utaratibu uliotumika Dar es Salaam wa

kuongeza idadi ya vikao utatumika katika mikoa mingine yenye

mlundikano wa kesi. Natoa wito kwa uongozi wa Mikoa na

Page 23: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

23

Wilaya kutoa majengo yatakayotumika kwa uendeshaji

wa Mabaraza hayo.

31. Mheshimiwa Spika, mfumo mpya wa utatuzi wa migogoro

ya Ardhi na Nyumba unaoanzia ngazi ya Kijiji na Kata una lengo

la kuwapunguzia wananchi gharama za kusafiri umbali mrefu

kupata haki zao. Katika mwaka 2006/07 kumekuwa na jitihada za

kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Kata katika Halmashauri

mbalimbali nchini. Pamoja na kuanzishwa Mabaraza hayo kuna

upungufu katika uendeshaji wake. Kwa sababu hiyo, katika

mwaka wa fedha 2007/08 Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi

ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, itaandaa

mkakati wa kuimarisha utendaji wa kazi katika Mabaraza ya Ardhi

ya Vijiji na Kata ili mashauri yasiyo na ulazima wa kwenda ngazi

za juu yasikilizwe na kutolewa uamuzi katika ngazi hizo. Natoa

wito kwa viongozi wa Halmashauri za Wilaya ambazo

hazijaunda mabaraza ya Ardhi ya vijiji na Kata wayaunde

ili kutatua migogoro mingi ya ardhi na nyumba katika

maeneo yao.

Page 24: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

24

HUDUMA ZA UPIMAJI NA RAMANI

32. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendelea na

utekelezaji wa majukumu yake ya upimaji ardhi na utayarishaji

wa ramani za msingi kwa nchi nzima ambazo huonyesha hali

halisi ya sura ya nchi na maendelezo yaliyo juu yake. Ramani hizo

ni chanzo muhimu cha taarifa zinazohitajika katika kubuni na

kutayarisha mipango ya matumizi mbalimbali ya ardhi.

Utayarishaji wa ramani za msingi ni ghali na zinachukua muda

mrefu kwa kuwa huhitajika ndege maalumu ya kupiga picha za

anga. Vile vile utayarishaji wa ramani unahitaji vifaa vya kisasa

ambavyo ni ghali.

Utayarishaji wa Ramani

33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara yangu ilipanga kupiga picha za anga na kutayarisha digital

orthophotos za miji ya Mbeya na Morogoro kwa ajili ya

kuendeleza Mradi wa kupima viwanja na kudhibiti ujenzi holela.

Pia, Wizara yangu iliahidi kupiga picha za anga katika Kanda ya

Mashariki inayojumuisha miji 128 katika Mikoa ya Pwani, Tanga,

Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Singida, Dodoma na Morogoro.

Page 25: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

25

Kazi hizo hazikufanyika kutokana na mawingu kuendelea kutanda

angani katika maeneo hayo. Upigaji wa picha za anga na

utayarishaji wa digital orthophoto katika Jiji la Dar es Salaam, nao

umeendelea kusitishwa kutokana na hali ya mawingu kuendelea

kutanda angani. Inatarajiwa kazi hizo kufanyika katika mwaka wa

fedha 2007/08 kutegemea hali ya hewa.

34. Mheshimiwa Spika, uchoraji na uhakiki uwandani wa

ramani za miji 41 Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya

Mwanza, Shinyanga, Kagera na Mara umekamilika. Aidha,

uchoraji wa ramani za miji 47 Kanda ya Magharibi inayojumuisha

mikoa ya Kigoma, Tabora, Rukwa, Mbeya na Iringa uko katika

hatua mbalimbali za utekelezaji baada ya kazi ya uwianishaji wa

ardhi (Ground Photo Control) na picha za anga za mwaka 2006

kukamilika.

35. Mheshimiwa Spika, Ili kuhakikisha kuwa miji yetu

inatayarishiwa mipango bora ya kuiendeleza kabla haijajengwa

kiholela hatuna budi kuandaa ramani za msingi mapema. Katika

mwaka wa 2007/08 Wizara yangu imepanga kupiga picha za anga

na kuchora ramani za msingi katika miji ya Mbeya na Morogoro.

Vile vile kwa lengo la kuwezesha mipango mingine ya maendeleo,

Page 26: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

26

ramani za uwiano wa 1:50,000 zitahuishwa kwa kutumia satellite

images na kuingizwa kwenye mfumo wa kompyuta.

Upimaji Majini (Hydrographic Surveying)

36. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu ina jukumu la kupima

na kuandaa ramani za maeneo ya ardhi kwenye maji ndani ya

Bahari na Maziwa makubwa kwa nia ya kuimarisha usalama wa

vyombo vya usafiri majini pamoja na kuainisha rasilimali zilizomo.

Ili kufanikisha azma hiyo Wizara kwa kushirikiana na Shirika la

“International Hydrographic Organisation – IHO” imeendelea na

hatua ya kujenga uwezo wa kitaalamu na vifaa. Katika ushirikiano

huo Wizara imepokea ramani za majini (Hydrographic Charts) za

baadhi ya bandari zilizopo mwambao wa bahari ya Hindi kwa ajili

ya uhuishwaji.

37. Mheshimiwa Spika, Serikali imeridhia mkataba wa

Kimataifa wa Sheria za Bahari (The United Nations Convention on

the Law of the Sea - UNCLOS) wa kutambua na kudai eneo la

nyongeza nje ya eneo la ukanda wa kiuchumi (Exclusive

Economic Zone) lijulikanalo kitaalam kama Extended Continental

Page 27: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

27

Shelf. Eneo hilo ni muhimu kwa maliasili zilizopo baharini

kutokana na ongezeko la miliki ya nchi. Tafiti zilizofanyika na

taasisi mbalimbali katika maeneo kama hayo zinaashiria

upatikanaji wa raslimali mbalimbali. Ili Serikali iweze kumiliki eneo

hilo ni lazima lipimwe na ramani zake kuwasilishwa kwenye

Umoja wa Mataifa kabla ya mwaka 2009. Katika kazi hii, Wizara

yangu inahusika na masuala ya Haidrografia (Hydrography) na

Jiodesia (Geodesy). Wadau wengine ni Wizara ya Mambo ya Nchi

za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Nishati na Madini,

Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Maendeleo ya

Petroli ambao wanahusika na Jiofizikia (Geophysics) na Jiolojia

(Geology). Hivyo, Wizara yangu itashirikiana na wadau wengine ili

tusipoteze fursa hii.

Upimaji Miliki

38. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu katika mwaka 2006/07

iliendelea kushirikiana na Halmashauri mbalimbali ili kuzijengea

uwezo wa kutoa huduma za upimaji miliki na kuweka

kumbukumbu za ardhi kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Mikoa ya

Mwanza, Arusha, Shinyanga, Iringa, Mbeya na Ruvuma imeanza

kuhifadhi kumbukumbu za upimaji katika kompyuta. Pia mikoa hii

Page 28: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

28

imepatiwa software kwa ajili ya kurahisisha kazi za upimaji ardhi

na uandaaji ramani. Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam

zimepatiwa plani pepe (digital survey plans) ili zisaidie katika

kuandaa plani za hati (deed plans). Warasimu ramani kutoka

Halmashauri hizo wamepata mafunzo ya kutumia plani pepe na

namna ya kuandaa plani za hati.

39. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara yangu imeidhinisha plani za upimaji zenye jumla ya

viwanja 16,312 na mashamba 712 kutoka kwenye Halmashauri

mbalimbali. Kasi ya upimaji viwanja na mashamba ni ndogo

ukilinganisha na mahitaji kutokana na Halmashauri nyingi

kutokuwa na wataalamu na vifaa vya kutosha. Ili kuimarisha

shughuli za upimaji nchini natoa wito kwa Halmashauri

kuajiri wataalamu na kutenga fedha kwenye bajeti zao

kwa ajili ya kununulia vifaa vya kisasa.

40. Mheshimiwa Spika, Miji yetu inaendelea kukua hivyo

mahitaji ya viwanja mijini nayo yanaongezeka. Kwa kutambua

mchango wa ardhi katika maisha, wananchi wengi wanajitokeza

kuchangia gharama za upimaji wa viwanja na mashamba. Hati

miliki za ardhi zimewasaidia wananchi kwa shughuli mbalimbali

Page 29: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

29

ikiwa ni pamoja na dhamana kwa mikopo. Haya ni mafanikio ya

utekelezaji wa dhati wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na

Kupunguza Umasikini Tanzania. Katika mwaka 2007/08 Wizara

yangu itasimamia upimaji miliki wa viwanja 18,000 na

mashamba 1,000 katika Halmashauri mbalimbali nchini.

Mradi wa Upimaji Viwanja Mijini

41 Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendelea kutekeleza

Mradi wa Upimaji wa Viwanja katika miji ya Dar es Salaam,

Mwanza, Morogoro na Mbeya. Hadi sasa jumla ya viwanja

49,228 katika miji hii vimepimwa. Katika Jiji la Dar es Salaam,

jumla ya Viwanja 34,314 vimepimwa kwa gharama ya Shilingi

bilioni 30.31 tangu mradi ulipoanza mwaka 2002/03. Katika Jiji

la Mwanza jumla ya viwanja 9,800 vimepimwa kwa Shilingi

milioni 830. Halmashauri ya Jiji la Mbeya imepima viwanja

2,350 kati ya viwanja 5,000 kwa Shilingi. milioni 600. Vile

vile Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imepima viwanja

2,764 kati ya viwanja 4,000 kwa gharama ya Shilingi milioni.

400. Hali hii inaonyesha kuwa dhana ya uchangiaji

gharama za upimaji imeeleweka vizuri kwa wananchi na

hivyo kuufanya Mradi huu kuwa endelevu. Wizara yangu

Page 30: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

30

itaendelea kuziwezesha Halmashauri zilizo tayari

kuanzisha na kutekeleza miradi ya upimaji viwanja mijini.

42. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2006/07

nililitaarifu Bunge lako tukufu juu ya Mfuko Maalum wa Kupima

Viwanja (Plot Development Revolving Fund - PDRF) ulioanzishwa

mwaka 1993. Hadi Juni, 2006 Asasi mbili na Halmashauri 30

zilikopeshwa jumla ya Shilingi. 399,112,613. (Jedwali Na.6).

Hadi kufikia Julai 2007, Halmashauri 14 za Ileje, Nkasi, Mpanda,

Sumbawanga, Kibaha, Hanang, Kondoa, Njombe, Hai, Bukoba

Manispaa, Kigoma Vijijini, Manispaa ya Mtwara na Jiji la Mbeya na

Tanga zilikamilisha marejesho yenye jumla ya Shilingi

216,801,167. Nazipongeza sana Halmashauri hizi, hata hivyo

bado Halmashauri 16 na Asasi 2 hazijakamilisha marejesho yenye

jumla ya Shilingi. 182,311,446. Halmashauri hizo ni pamoja na

Monduli, Babati, Kondoa, Maswa, Tarime, Iringa (V), Mufindi,

Mbalali, Mwanga, Songea (V), Tunduru, Masasi, Newala,

Ruangwa, Liwale, Bagamoyo. Asasi ambazo hazijarejesha ni CDA

na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika. Katika mwaka 2007/08

Halmashauri 19 zitakopeshwa jumla ya Shilingi 416,002,381

kwa ajili ya upimaji viwanja mijini. Bado nasisitiza kuwa lengo

la Wizara ni kuufanya Mfuko uwe endelevu ili

Page 31: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

31

kuziwezesha Halmashauri kupima viwanja mijini.

Kutorejesha kunazinyima fursa halmashauri nyingine

kunufaika na Mfuko huu. Napenda kutoa wito kwa

wahusika wote kurejesha fedha walizokopa mapema

Upimaji wa Vijiji

43. Mheshimiwa Spika, Upimaji wa mipaka ya vijiji ni hatua

ya kwanza ya utekelezaji wa Sheria ya Ardhi ya vijiji namba 5 ya

mwaka 1999 (sura 114). Sheria hii iliandaliwa ili kuwezesha

upangaji wa matumizi endelevu ya ardhi na uhifadhi wa

mazingira. Idadi ya vijiji nchini inakadiriwa kufikia 13,000. Hadi

Juni 2006 vijiji 6,000 vilikuwa vimepimwa. Katika mwaka 2006/07

Wizara yangu iliahidi kupima mipaka ya vijiji 3,104. Hadi Juni

2007 jumla ya Vijiji 2,668 sawa na asilimia 86 (Jedwali Na. 7)

vimepimwa mipaka yake katika mikoa ifuatayo:- Pwani, Lindi,

Iringa, Mbeya, Rukwa, Kigoma, Kagera, Shinyanga na Tanga.

44. Mheshimiwa Spika, kutokana na tengeo la fedha la

mwaka 2006/07 kazi iliyofanyika ni kubwa ikilinganishwa na

upimaji uliofanywa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 iliyopita. Ni

dhahiri kuwa Wizara ikiendelea kutengewa fedha za kutosha

Page 32: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

32

itawezekana kukamilisha kazi iliyobakia katika muda wa miaka

mitatu hadi minne. Katika mwaka 2007/08, Wizara yangu

itaendelea na upimaji wa mipaka ya vijiji katika Mikoa sita. Natoa

wito kwa mamlaka za Mikoa, Halmashauri za Wilaya na

Serikali za Vijiji ambako vijiji vimepimwa, kuchukua

hatua za makusudi na kujenga tabia na utamaduni wa

kulinda na kutunza mipaka yao ili idumu na kuzuia

kuzuka kwa migogoro ya mipaka hapo baadae. Mipaka ya

vijiji ni msingi wa mipaka ya Wilaya, Mikoa na kitaifa,

kwa hiyo uimara wake unachangia kuimarisha amani na

utulivu na ni ufumbuzi wa migogoro ya mipaka yote

nchini. Ni vema ilindwe na kutunzwa wakati wote kwani

imeigharimu Serikali fedha nyingi kuipima.

45. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa wananchi

wanaoishi katika maeneo yaliyo na madini hawabughudhiwi,

Wizara yangu itaendelea kupima maeneo yanayotumiwa na

wachimbaji wa Makampuni makubwa ili kuondoa migogoro

inayojitokeza kati ya Makampuni hayo na wananchi katika

maeneo husika. Kwa kushirikiana na Tanzania Investment Centre

-TIC na Mikoa, Wizara itapima maeneo yanayofaa kwa kilimo cha

Page 33: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

33

mashamba makubwa na kuwa na Land Bank katika Mikoa yote.

Hatua hii itasaidia wawekezaji wanaohitaji mashamba makubwa

kuyapata bila usumbufu. Aidha, Wizara imepanga kupima eneo la

Kigamboni kwa nia ya kuanzisha mji wa kisasa ndani ya Jiji la Dar

es Salaam.

46. Mheshimiwa Spika, kwa kushirikiana na Wizara ya

Maliasili na Utalii Wizara itaandaa mpango utakaowezesha kupima

Hifadhi za Taifa zote na hivyo kupunguza migogoro inayojitokeza

kati Mamlaka za Hifadhi hizo na wananchi. Aidha, Wizara

itaendelea kutoa hati kwa mashamba na ranch zilizokuwa mali ya

Serikali ambazo kwa sasa ranch hizo zimemilikishwa kwa watu

binafsi.

Mipaka ya Kimataifa

47. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inalo jukumu la

kukagua na kupima mipaka ya kimataifa. Ili kutekeleza jukumu

hili, Wizara yangu ilifanya mawasiliano na nchi jirani za Kenya,

Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Comoro kwa lengo la

kupanga ukaguzi na uimarishaji wa mipaka hiyo. Katika mwaka

wa fedha 2006/07 Tanzania na Msumbiji zilifanya ukaguzi wa

Page 34: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

34

pamoja wa mpaka wa nchi kavu kutathmini gharama za

kuimarisha mpaka huo kwa kusimika mawe ya ziada. Pia,

mikutano kati ya Tanzania, Uganda na Kenya ilifanyika kujadili

jinsi ya kurudishia baadhi ya mawe ya mipaka yaliyoharibiwa na

kuandika upya protokali za mipaka.

48. Mheshimiwa Spika, kutokana na uamuzi wa Viongozi wa

nchi zinazounda Umoja wa Afrika (African Union) kuwa mipaka ya

kimataifa ya nchi hizo iwe imetambuliwa, kuainishwa, kuhakikiwa

na kupimwa ifikapo mwaka 2012, Wizara yangu itahakikisha

kwamba mipaka yote na nchi jirani inashughulikiwa ipasavyo

kabla ya muda huo. Natoa wito kwa wadau wote katika

suala hili kushirikiana kukamilisha jukumu hili. Katika

kipindi cha mwaka 2007/08, Wizara yangu itaendeleza juhudi za

kufanya mashauriano ya pamoja kati ya Tanzania, Comoro na

Msumbiji ili kukamilisha mpaka katika Bahari ya Hindi. Aidha,

Mawasiliano na serikali za Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya

Congo na Rwanda yatafanyika ili kuanza kushughulikia mipaka

hiyo ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa programu inayohusu

mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika bonde la Mto Songwe.

Page 35: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

35

Mipaka ya Ndani ya Nchi.

49. Mheshimiwa Spika, Mwaka jana nililitaarifu Bunge lako

Tukufu kuwa chanzo kikubwa cha migogoro ya mipaka ni

mamlaka za utawala za Wilaya kutokufahamu wala

kujishughulisha na mipaka rasmi ya maeneo yao. Ili kutatua

migogoro hiyo, Wizara yangu imesambaza nakala za Tangazo la

Serikali (GN) la mipaka ya Wilaya kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya

nchini kote. Pia, nilitoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa,

mara wakipata nakala ya GN ya mipaka ya wilaya zao, wafanye

mikutano ya ujirani mwema ili kujifahamisha na kutambua mipaka

rasmi ya Wilaya zao na kujiridhisha na tafsri zake. Kama GN ni ya

zamani na haitafsiriki, hoja ijengwe na kuwasilishwa Ofisi ya

Waziri Mkuu-TAMISEMI, yenye dhamana ya GN, kuomba

zihuishwe ili ziendane na hali halisi na kurahisisha tafsiri.

50. Mheshimiwa Spika, ninafurahi kuliarifu Bunge lako kuwa

katika mwaka 2006/07 baadhi ya wilaya zimeanza kushughulikia

utatuzi wa migogoro yao. Kwa mfano, taarifa rasmi ya kumalizika

kwa mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Bukombe na

Biharamulo iliwasilishwa. Ninaupongeza uongozi wa Mikoa ya

Shinyanga na Kagera kwa hatua hiyo na ninaomba Mikoa na

Page 36: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

36

Wilaya nyingine kuiga mfano huo. Vile vile Wizara imepokea

nakala za barua kutoka Mikoa na Wilaya kadhaa za kuiarifu

TAMISEMI upungufu katika maelezo ya GN hasa za zamani na

kuomba zihuishwe. Wizara yangu itaendelea kushirikiana na

Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI kushughulikia GN hizo.

MAENDELEO YA MAKAZI

51. Mheshimiwa Spika, pamoja na majukumu mengine ya

Wizara niliyoyazungumzia awali, Wizara ina jukumu la kusimamia

uendelezaji wa makazi hapa nchini kwa kuzingatia Sera ya

Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 na Sheria ya Mipangomiji

na Vijiji (Sura 378) ya mwaka 1956 ambayo imerekebishwa na

kupitishwa na Bunge lako tukufu mwezi Aprili 2007.

52. Mheshimiwa Spika, miji ya Tanzania inakua kwa kasi.

Idadi ya watu katika miji yetu imekuwa ikiongezeka kwa wastani

wa asilimia 4.5 kwa mwaka. Kwa mujibu wa sensa ya mwaka

2002, Tanzania ilikuwa na watu 34,443,603 kati ya hao asilimia

23 walikuwa wanaishi mijini. Hivi sasa nchi yetu inakadiriwa kuwa

na watu 37,000,000 kati ya hao asilimia 27 wanaishi mijini.

Inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2025, nusu ya Watanzania

Page 37: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

37

watakuwa wanaishi mijini. Kutokana na ongezeko kubwa la watu

mijini, mahitaji ya makazi yaliyopangwa yataongezeka. Hii ni

changamoto kwa mamlaka za miji. Natoa wito kwa

halmashauri zote chini kuliona suala hili kwa mtazamo

chanya na kuchukua hatua za makusudi za kuhakikisha

kwamba miji inapimwa na kupangwa ili kuzuia upanukaji

wa maeneo yasiyopangwa mijini. Pia nawaasa wananchi

kuacha tabia ya kujenga katika maeneo yasiyopimwa na

badala yake waombe viwanja vilivyopimwa kutoka

kwenye halmashauri zao. Wizara yangu kwa kushirikiana

na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za

Mitaa itahakikisha kwamba Halmashauri zinaandaa

mikakati ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Maendeleo ya Miji

53. Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza mwaka jana Wizara

yangu inaandaa mipango ya aina mbili ya kuongoza uendelezaji

wa miji. Mipango ya muda mrefu ambayo utekelezaji wake

huchukua miaka ishirini (Master Plans) na mipango ya matumizi

ya ardhi ya muda mfupi ambayo huchukua miaka mitano hadi

kumi (Interim Land Use Plans). Katika mwaka wa fedha uliopita

Page 38: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

38

Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri husika ilikamilisha

mipango ya matumizi ya ardhi ya muda mfupi ya miji ya

Tandahimba, Tunduru, Namtumbo, Masasi, Babati, Mererani,

Ushirombo na Misungwi. Pia katika kipindi hicho Wizara ilianza

maandalizi ya mipango ya namna hiyo kwa miji ya Mvomero,

Kibaigwa, Bunda na Chato. Katika mwaka wa fedha 2007/08

Wizara yangu itakamilisha mipango hiyo na kuandaa mipango

kwa ajili ya miji ya Kasulu, Kibondo, Maswa na Kyela.

54. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri husika ilianza maandalizi

ya Mipango ya Muda Mrefu (Master Plans) kwa Jiji la Mwanza na

Manispaa ya Mtwara/Mikindani. Katika mwaka wa fedha 2007/08

Wizara yangu itakamilisha mipango hiyo na kuandaa mpango wa

namna hiyo kwa miji ya Dar es Salaam na Kigoma. Napenda

kuhimiza Halmashauri ambazo zina mipango ya muda

mrefu au mfupi kuandaa Mipango ya Kina (Detailed

Layouts), ili kuweza kupata viwanja vya kupima na

kuendeleza.

55. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na

Halmashauri husika imekuwa inaandaa mipango ya kuendeleza

upya maeneo ya kati ya miji (Redevelopment Schemes). Mipango

Page 39: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

39

hii inaandaliwa ili kuwezesha uwekezaji mpya na kuyafanya

maeneo hayo yenye thamani kubwa ya ardhi yaweze kuchangia

ipasavyo katika uchumi wa miji hiyo na Taifa kwa ujumla. Katika

mwaka wa fedha 2006/07, Wizara ilikamilisha mipango ya namna

hiyo kwa Jiji la Tanga, mji wa Singida na eneo la Upanga Jijini

Dar es Salaam. Katika mwaka 2007/08 mipango ya namna hiyo

itaandaliwa kwa eneo la kati la mji wa Lindi na kwa maeneo ya

Magomeni, Oysterbay na Msasani Peninsular/Masaki katika Jiji la

Dar es Salaam. Ili kutekeleza Sera ya Makazi ya Mwaka

2000 na kuongeza thamani ya ardhi, napenda nitoe wito

kwa wananchi kujenga nyumba za maghorofa katika

maeneo yaliyokamilika kupangwa upya.

56. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekuwa inatekeleza

Mradi wa Kuendeleza Upya Eneo la Kurasini tangu mwaka

2006/07 ili liweze kutumika kwa shughuli zinazohusiana na

Bandari na kuwa kitega uchumi kikubwa kwa Taifa. Wizara

inaendelea kulipa fidia kwa wakazi wanaohamishwa hatua kwa

hatua kulingana na upatikanaji wa fedha, ili kuweza kupatikana

kwa maeneo huru ya kupima viwanja vikubwa na kumilikisha

viwanja hivyo kwa njia ya zabuni. Katika Mwaka wa fedha

2006/07 jumla ya viwanja vitatu vilipimwa na jumla ya shillingi

2.284 bilioni zilipatikana kutokana na mauzo ya viwanja hivyo.

Page 40: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

40

Aidha jumla ya shilingi 2.762 bilioni zilitumika kulipa fidia kwa

nyumba zipatazo 183. Wizara imekamilisha kufanya uthamini na

kupima viwanja vingine sita ambavyo tayari vimetangazwa

kuuzwa kwa njia ya zabuni. Katika mwaka wa fedha 2007/08

Wizara itaendelea na utekelezaji wa Mradi huo.

57. Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya mwaka jana

nililieleza Bunge lako Tukufu kuwa Wizara ilikuwa inahuisha

Sheria ya Mipangomiji na Vijiji (Sura 378) ya mwaka 1956 pamoja

na Sheria ya Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Na. 3 ya

mwaka 1984 na kuandaa Sheria ya kusimamia taaluma ya

Mipangomiji. Napenda kuchukua nafasi hii kulishukuru Bunge lako

Tukufu kwa kutunga Sheria Mpya ambazo ni Sheria ya

Mipangomiji, Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi na Sheria

ya Kusajili Wataalam wa Mipangomiji. Katika mwaka 2007/08

Wizara itaandaa Kanuni na Miongozo ya kutekeleza Sheria hizi.

Utekelezaji wa Sheria hizo utaboresha hali ya makazi hapa nchini.

58. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara ilishiriki katika mkutano wa 21 wa Shirika la Umoja wa

Mataifa linaloshughulikia Makazi (UN-Habitat) na Mkutano wa

Shirika la Afrika linalotoa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba

kwa nchi za Afrika (Shelter Afrique). Shirika la Umoja wa Mataifa

Page 41: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

41

linaloshughulikia Makazi (UN-Habitat) limewezesha vikundi vya

akina mama visivyokuwa vya Kiserikali kupata eneo katika

Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa zaidi

ya tano kwa njia ya ubia. Katika mwaka wa fedha 2007/08 Wizara

itaendelea kushirikiana na Mashirika ya Kimataifa kama UN-

Habitat, UNEP, Shelter Afrique pamoja na sekta binafsi kubuni

njia mbalimbali za kuboresha makazi nchini.

Mradi wa Kutambua Miliki Katika Maeneo Yaliyojengwa

Kiholela.

59. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inaendelea na

utekelezaji wa Mradi wa Kutambua miliki katika Jiji la Dar es

Salaam kwa kushirikiana na Halmashauri zote. Katika mwaka

2006/07 Wizara ilianza kutekeleza awamu ya pili ya Mradi

ambayo inahusu kutambua miliki na kuendeleza maeneo ya

pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam. Katika utekelezaji huo miliki

10,842 zilitambuliwa katika maeneo ya Kimara na Mbezi

Luguruni pamoja na kuandaa Mpango wa Kina wa eneo la Mbezi

Luguruni kuwa kitovu cha huduma (Satelite urban centre). Ili

kuhakikisha maeneo hayo yanaendelezwa kwa mpangilio, katika

mwaka 2007/08 Wizara itaendelea kushirikiana na Halmashauri

Page 42: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

42

kutambua na kuandaa mipango shirikishi ya kuendeleza maeneo

hayo ili kuzuia uendelezaji holela, kuwezesha upimaji wa maeneo

hayo na kuweka huduma muhimu za kijamii na kiuchumi.

Maendeleo ya Nyumba

60. Mheshimiwa Spika, kama inavyoeleweka nyumba ni moja

ya mahitaji matatu muhimu ya mwanadamu ikiwa ni pamoja na

chakula na mavazi. Nyumba bora huchangia katika kuwa na afya

nzuri na hivyo kumwezesha mwananchi kujiendeleza kiuchumi.

Vile vile shughuli za uendelezaji nyumba huleta ajira na hivyo

huchangia katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

61. Mheshimiwa Spika hali ya nyumba hapa nchini siyo ya

kuridhisha kwani katika maeneo mengi ya mijini kuna uhaba wa

nyumba za kuishi na nyingi ni duni. Watu wengi huishi katika hali

ya msongamano na mazingira yasiyoridhisha. Inakadiriwa katika

maeneo ya mijini peke yake kuna upungufu wa nyumba milioni

tatu. Katika maeneo ya vijijini nyumba nyingi ni duni na hudumu

kwa wastani wa miaka 7 tu, hali ambayo hufanya watu wa vijijini

kutumia muda wao mwingi katika kukarabati nyumba badala ya

kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.

Page 43: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

43

62. Mheshimiwa Spika, Ili kuimarisha sekta ya nyumba,

Wizara ilianza kuandaa Sera Mpya ya Maendeleo ya Nyumba

katika mwaka 2006/07. Kazi hii itaendelea katika mwaka wa

fedha 2007/08. Sera hii itakuwa ndiyo dira ya kuendeleza

nyumba hapa nchini na itaandaliwa Sheria husika ‘Housing Act’

ambayo itarahisisha utekelezaji wake.

Mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa Serikali.

63. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea na jukumu

la kusimamia Mfuko wa Mikopo ya Nyumba kwa Watumishi wa

Serikali. Lengo ni kuwakopesha watumishi ili waweze kukarabati,

kujenga au kununua nyumba za kuishi na hivyo kujipatia makazi

ya uhakika. Mfuko huu ni wa mzunguko (Revolving Fund) na

marejesho yake huzingatia kipindi cha mtumishi kuwa katika ajira.

Katika mwaka wa fedha 2006/07 waombaji wapya 390

waliidhinishiwa mikopo yenye thamani ya Shilingi

1,646,277,979 na kufanya idadi ya watumishi walioidhinishiwa

mikopo tangu mfuko huu uanzishwe kufikia 1,169 yenye

thamani ya Shilingi 4,484,457,515. Hadi kufikia mwezi Juni,

2007 marejesho halisi yalifikia Shilingi 761,008,608. Katika

Page 44: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

44

mwaka wa fedha 2007/08 Wizara yangu itaendelea kuboresha

kumbukumbu za wakopaji na kutumia mfuko huo kukopesha

wafanyakazi ili waweze kupata makazi bora (Jedwali Na. 8).

MIPANGO YA MATUMIZI BORA YA ARDHI

64. Mheshimiwa Spika, Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ni

nyenzo mahsusi katika kuhifadhi mazingira, kuwezesha uzalishaji

endelevu katika ardhi na raslimali zake, kuondoa migogoro ya

ardhi, kunusuru wananchi katika majanga mbalimbali na

kugawanya ardhi kisayansi kwa watumiaji mbalimbali. Katika

mwaka wa fedha 2006/07, Tume ya Taifa ya Mipango ya

Matumizi Bora ya Ardhi imeendelea kusimamia na kuratibu

uandaaji na utekelezaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi

katika ngazi ya Vijiji, Wilaya na Taifa. Kufuatia kutangazwa kwa

Mkakati wa Taifa wa Kuhifadhi Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya

Maji, Tume iliweza kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi

katika Wilaya 13 na Vijiji 150.

65. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2007/08 Tume kwa

kushirikiana na Halmashauri na Wizara ya Maliasili na Utalii

itaendelea kuandaa na kutekeleza mipango ya matumizi bora ya

ardhi katika wilaya 6 za mpakani, wilaya 4 zenye hifadhi za

Page 45: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

45

wanyamapori na mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji 40.

Aidha Tume itaratibu mipango yote inayoandaliwa na wadau

wengine na kuhakikisha inatekelezwa kisheria.

WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI WA NYUMBA BORA NA VIFAA VYA UJENZI (NHBRA)

66. Mheshimiwa Spika, Wakala wa Taifa wa Utafiti wa

Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi unalo jukumu la kutafiti,

kukuza, kushauri, kuhamasisha na kusambaza matokeo ya utafiti

na utaalam wa ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu. Vile

vile Wakala huelimisha na kuhamasisha wananchi kuanzisha

vikundi vya ushirika vya uzalishaji na vya ujenzi wa nyumba bora

na za gharama nafuu kwa kutumia vifaa vilivyotafitiwa na Wakala

katika ngazi zote nchini.

67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07,

Wakala uliendesha semina za uhamasishaji kwa viongozi, maafisa

maendeleo ya jamii, madiwani, wahandisi na wananchi, katika

wilaya za Tabora Vijijini na Mjini, Morogoro Vijijini na Mkoa wa

Pwani, jumla ya washiriki 800 walihudhuria. Mafunzo kwa vitendo

yamefanyika katika Wilaya za Namtumbo, Kinondoni, Ilala,

Temeke, Tabora Vijijini na Mjini, na Iringa Vijijini ambako vikundi

Page 46: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

46

vya ujenzi vilifundishwa mbinu za kufyatua matofali ya udongo

saruji au ya mfinyanzi ya kuchoma pamoja na ujenzi kwa kutumia

matofali yanayofungamana. Shirika la Taifa la Nyumba kwa

kushirikiana na Wakala linatumia teknologia hiyo katika ujenzi wa

maduka 76 huko Ipogolo – Iringa, pia Wakala wa Majengo ya

Serikali wanatumia teknolojia hiyo kujenga nyumba za serikali

katika baadhi ya mikoa nchini. Wananchi wameanza kuvutiwa na

teknolojia hii, hivyo kuitumia katika ujenzi wa nyumba zao. Pia

utafiti wa mashine za kufyatulia matofali yanayofungamana

unaendelea kuboreshwa.

68. Mheshimiwa Spika, ili matokeo ya tafiti yaweze kuwafikia

watumiaji, Wakala hutumia fursa mbalimbali kujitangaza. Katika

mwaka 2006/07, Wakala ulijitangaza kwa kushiriki katika

maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Maonyesho ya

Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam na Mkutano wa Kimataifa

wa Hakimiliki uliofanyika nchini. Pia Wakala ulijitangaza kupitia

vyombo mbalimbali vya habari, magazeti na vipeperushi. Katika

mwaka wa fedha 2007/08, Wakala utaendelea kujitangaza kwa

kutumia fursa mbalimbali zitakazojitokeza.

Page 47: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

47

69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2007/08

Wakala utaendelea na utafiti na utaimarisha Maabara yake ya

utafiti kwa kununua vifaa vipya ili kuingia katika ushindani na

kwenda pamoja na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Pia utaelimisha na kuhamasisha wananchi kuanzisha vikundi vya

ushirika vya ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu na vya

uzalishaji wa vifaa vya ujenzi vilivyotafitiwa. Yote hayo

yatafanyika kwa njia za semina na mafunzo kwa vitendo. Aidha,

Wakala utashiriki katika maonyesho mbalimbali ya Kitaifa na

kimataifa. Napenda kurudia tena wito nilioutoa mwaka

uliopita kwa Halmashauri zote nchini na Wananchi

kuwasiliana na Wakala na kutumia teknolojia zake ili

kuboresha nyumba na makazi.

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

70. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Bunge Na. 2 ya mwaka

1990 iliyorekebishwa mnamo Juni, 2005, inalitaka Shirika la

Nyumba la Taifa liendeshe majukumu yake kibiashara.

Majukumu haya ni pamoja na kujenga nyumba kwa madhumuni

ya kupangisha na kuuza, kusimamia miliki, kusimamia majengo

kama wakala, kuendesha miradi ya ujenzi itakayoidhinishwa na

Serikali na kufanya shughuli za ukandarasi wa majengo.

Page 48: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

48

71. Mheshimiwa Spika, nyumba za kupanga ndiyo raslimali

kubwa ya Shirika, kwani zaidi ya asilimia 88 ya mapato yake

hutokana na kodi ya pango ya nyumba zake 16,021. Nyumba hizi

zipo kwenye miji mbali mbali ya mikoa ya Tanzania Bara. Kiasi

kingine cha mapato ya Shirika hutokana na ujenzi wa nyumba za

kuuza na shughuli za ukandarasi. Aidha napenda kuliarifu Bunge

lako tukufu kuwa kutokana na marekebisho ya Sheria Na. 2 ya

Shirika la Nyumba la Taifa yaliyofanywa na Bunge hili mwezi Juni

2005, yamewafanya wapangaji wengi kulipa kodi zao za pango

kwa wakati kulingana na mikataba yao ya pango. Katika kipindi

cha mwaka 2005/06 Shirika liliweza kukusanya kiasi cha Shilingi

19,227,412,873 ambacho ni makusanyo makubwa katika

historia ya Shirika. Ongezeko hilo lilitokana na wapangaji wengi

kulipa malimbikizo ya nyuma. Katika kipindi cha kuanzia mwezi

Julai 2006 hadi mwezi Juni 2007, kiasi cha Shilingi

19,775,538,668 kilikusanywa.

72. Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha

ukusanyaji wa mapato, Shirika lilirekebisha kodi za pango kwa

nyumba zake nchini kote kuanzia mwezi Machi 2007. Kodi hiyo

mpya itaongeza mapato kutoka shilingi 15,000,000,000 hadi

Page 49: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

49

22,600,000,000 kwa mwaka. Nawashukuru na kuwapongeza

wapangaji wote waliotimiza wajibu wao wa kulipa kodi

zao za pango kwa wakati. Pia nachukua fursa hii

kuwataka wapangaji wenye malimbikizo kulipa mara

moja ili kuliwezesha Shirika kutekeleza wajibu wake

ipasavyo.

73. Mheshimiwa Spika, katika zoezi la kuuza nyumba ndogo

na za kati, jumla ya nyumba 4,900 kati ya 4,992 ambazo ni

sawa na asilimia 98 ya nyumba zilizokusudiwa kuuzwa zimelipiwa

kikamilifu na kulipatia Shirika jumla ya Shilingi 7,516,654,526.

Ni matarajio ya Shirika kuwa wapangaji wa nyumba 92 waliobaki

watakamilisha kulipa madeni yao kulingana na mikataba ya

mauziano. Sanjari na hilo, Shirika liliendelea kupokea malipo

kutoka kwa wanunuzi wa nyumba mpya 314 zilizojengwa kwa

ajili ya kuuzwa. Hadi kufikia Juni 2007, kiasi cha Shilingi

5,738,312,116 kilikusanywa ikilinganishwa na matarajio ya

Shilingi 8,818,961,114. Hata hivyo, kasi ya kulipia nyumba

hizi bado ni ndogo. Ninatoa wito kwa wanunuzi wote

waliopewa fursa hii kukamilisha malipo yao ifikapo mwezi

Desemba 2007. Baada ya muda huo kupita nyumba hizo

zitauzwa kwa wananchi wengine.

Page 50: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

50

74. Mheshimiwa Spika, mapato hayo yameliwezesha Shirika

kushughulikia majukumu yake mbali mbali kama vile ujenzi wa

nyumba za makazi, majengo makubwa ya biashara, gharama za

uendeshaji, matengenezo ya nyumba na malipo ya kodi mbali

mbali kwa mujibu wa Sheria. Katika mwaka wa fedha 2006/07

Shirika limelipa Serikalini jumla ya Shilingi 2,201,655,661 hadi

Juni 2007, zikiwa ni kodi za mapato, ongezeko la thamani,

majengo na viwanja. Katika kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita

Shirika limeweza kulipa Shilingi 8,180,399,028 kama kodi

mbalimbali ambazo zimechangia katika kuwaletea wananchi

maendeleo.

75. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha jukumu la

usimamizi wa nyumba zilizopo, Shirika linatenga asilimia 25 ya

mapato yatokanayo na kodi ya pango kila mwaka kwa ajili ya

kugharamia matengenezo. Hatua hii imeliwezesha Shirika

kuzifanyia matengenezo makubwa baadhi ya nyumba zilizokuwa

katika hali mbaya na kupunguza kero kwa wapangaji. Katika

mwaka wa fedha 2006/07 jumla ya nyumba 2,306

zilitengenezwa pamoja na majengo 418 kwa gharama ya

Shilingi 4,914,814,949 (Jedwali Na. 9). Aidha, ili kuwa na

Page 51: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

51

mpango wa matengenezo endelevu na wenye ufanisi, Shirika

limeandaa programu ya miaka mitano (5) ya matengenezo kama

sehemu ya Mpango Mkakati wa Shirika (Corporate Plan). Katika

mpango huo, Shirika limepanga kuyafanyia matengenezo

makubwa majengo yapatayo 478 kila mwaka ili ndani ya kipindi

cha miaka mitano ijayo majengo yote yawe yamefanyiwa

matengenezo makubwa.

76. Mheshimiwa Spika, Shirika limeendelea kujenga majengo

makubwa ya vitega uchumi kwa kutumia mtaji wake na kwa

kushirikiana na sekta binafsi. Katika mwaka 2006/07 Shirika

lilikamilisha jengo 1 la ghorofa Kigoma, majengo 2 yenye maduka

15 Arusha na maghorofa 2 ya makazi yenye nyumba 24 Dodoma

kwa kutumia mtaji wake. Shirika limekamilisha majengo 3

makubwa na linaendelea na ujenzi wa majengo mengine 16 kwa

njia ya ubia. Katika mwaka 2007/08 Shirika linatarajia kujenga

majengo makubwa 29 ya makazi na biashara na maduka 87

katika Jiji la Dar es Salaam na Arusha na miji ya Kigoma, Iringa,

Shinyanga na Tabora kwa kutumia mtaji wake na kwa

kushirikiana na wabia.

Page 52: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

52

77. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Shirika lilikamilisha ujenzi wa nyumba 64 za kuuza na

kupangisha, zilizojengwa maeneo ya Boko, Mbezi Beach na

Mbweni JKT katika Mikoa ya Dar es Salaam na maeneo ya Kijenge

na Mwandamo katika Mkoa wa Arusha. Katika mwaka wa fedha

2007/08 Shirika linatarajia kujenga nyumba 222 kwa ajili ya

kuuza na kupangisha katika Mikoa ya Dar es Salaam, Arusha,

Pwani, Lindi na Kagera. Pamoja na hili, Shirika litafanya

upembuzi yakinifu wa kujenga nyumba katika miji midogo ya

Mikoa na Wilaya. Nia na madhumuni ya kufanya upembuzi huu,

ni kutaka kubaini mahitaji na aina ya nyumba zinazohitajika katika

miji hiyo. Utekelezaji wa jukumu hili unalenga kulipatia Shirika

sura ya kitaifa. Shughuli hizi zinalenga katika utekelezaji wa Ilani

ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ibara 68(g).

78. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake,

Shirika linakabiliwa na matatizo mbali mbali yakiwa ni pamoja

na:- mtaji mdogo kwa ajili ya ujenzi; ukosefu wa soko la uhakika

la nyumba zinazojengwa kutokana na kukosekana kwa mfumo

rasmi wa kutoa mikopo ya ujenzi na ununuzi wa nyumba; na kesi

zilizoko mahakamani zinazohusu wapangaji wanaopinga

uendelezaji wa viwanja vyenye majengo chakavu au yaliyopitwa

Page 53: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

53

na wakati katikati ya miji zinazochukua muda mrefu bila

kumalizika.

79. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza ufanisi, Shirika

limejiwekea mikakati ya kutatua matatizo hayo kama ifuatavyo:

• kuendelea na usimamizi wa rasilimali za nyumba zilizopo

ambapo msukumo zaidi utawekwa katika matengenezo

makubwa na ya kina ya nyumba na majengo;

• kupanua wigo wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya

kuuza na kupangisha;

• kuendelea na mkakati wa uendelezaji upya wa viwanja

vilivyoko katikati ya miji kupitia Sera ya ubia iliyobuniwa na

Shirika;

• kuendelea kuiomba mahakama ione umuhimu wa

uendelezaji wa viwanja vyenye majengo chakavu au

yaliyokusudiwa kuendelezwa ili itoe maamuzi ya kesi

mapema;

• kuendelea kuhimiza ushirikiano baina ya Serikali, Shirika na

vyombo vya fedha kwa ajili ya uanzishaji wa mfumo rasmi

wa kutoa mikopo ya ununuzi na ujenzi wa nyumba kwa raia

na taasisi mbali mbali.

Page 54: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

54

Natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge kutoa msukumo

katika uanzishaji wa mfumo wa kutoa mikopo kwenye

sekta ya nyumba.

HUDUMA ZA UTAWALA NA RASILIMALI WATU

80. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeendelea kuboresha

utoaji wa huduma kwa ufanisi wa hali ya juu. Dhamira hii

inathibitishwa na jitihada mbalimbali zilizofanywa na

zinazoendelea za kuboresha mifumo ya utendaji kazi na

usimamizi wa rasilimali watu. Wizara yangu imeendelea kutoa

mafunzo, kuboresha mazingira ya ofisi, kutoa stahili kwa

watumishi zinazoendana na ajira zao pamoja na kudumisha

Utawala Bora. Aidha, msisitizo umelenga katika kutumia dhana

shirikishi ya kupanga, kujenga uwezo, kutekeleza, kusimamia na

kutathmini utekelezaji ili kuboresha utendaji kazi na kudhibiti

nidhamu. Pia Wizara yangu imeendelea kupiga vita RUSHWA,

kutoa huduma kwa waathirika wa UKIMWI waliopo na kuongeza

kasi ya mapambano ya maambukizi mahali pa kazi.

81. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara yangu imeboresha utendaji kazi kwa kununua vitendea

Page 55: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

55

kazi, ikiwa ni pamoja na kompyuta, samani za ofisi na magari kwa

ajili ya kutoa huduma kwa ufanisi. Wizara imeajiri watumishi

wapya 93, kati yao 69 ni ajira mpya na 24 ni ajira mbadala,

watumishi 109 wamepandishwa vyeo kati yao wanawake ni 37 na

watumishi 8 wamechukuliwa hatua za kinidhamu (Jedwali Na.

10). Katika mwaka wa fedha 2007/08, Wizara yangu itaendelea

kuboresha mazingira ya kazi, kutoa stahili mbalimbali za

watumishi pamoja na kuajiri watumishi wengine 246 wa fani

tofauti.

82. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara yangu ilikamilisha hatua ya pili ya ukarabati wa jengo la

Ardhi. Licha ya ukarabati huu kuleta mandhari nzuri ya jengo,

utaboresha mpangilio wa ukaaji wa wazi unaosaidia kuleta ufanisi

zaidi katika utendaji pamoja na kusaidia kuzuia mianya ya

Rushwa. Ukarabati wa jengo la Menejimenti ya Mifumo ya Habari

(Management Information System) umekamilika ambapo huduma

za kukadiria malipo ya kodi ya pango la ardhi itatolewa ndani ya

jengo hilo ili kuwaondolea wananchi kero ya kusongamana na

usumbufu wa kuhudumiwa katika majengo mawili tofauti. Aidha,

michoro ya ubunifu na usanifu wa jengo la Upimaji na Ramani

imekamililka katika mwaka wa fedha 2006/07. Wizara itakamilisha

Page 56: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

56

maandalizi kwa kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi, nyaraka

za zabuni na mikataba ya ujenzi katika mwaka wa fedha 2007/08.

83. Mheshimiwa Spika, watumishi wa Sekta ya Ardhi

wameendelea kupelekwa kwenye mafunzo ya aina mbalimbali.

Katika mwaka 2006/07 jumla ya Watumishi 272 wa Wizara na

Halmashauri walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na mfupi

ndani na nje ya nchi. Kati ya hao watumishi 57 walikuwa

wanawake. (Jedwali Na. 11 (a) na 11 (b)). Katika mwaka wa

fedha 2007/08, Wizara yangu inatarajia kuwapatia mafunzo jumla

ya watumishi 50 kati yao 5 ni kutoka katika Halmashauri.

84. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha na kudumisha

utendaji kazi, Wizara yangu imeendelea kutoa mafunzo juu ya

utoaji wa huduma bora kwa mteja (customer care service) kwa

waajiriwa wapya na watumishi wa vituo vya nje. Mafunzo haya

yamesaidia kuwafanya watumishi kuelewa wajibu wao na

matarajio ya wateja ya kupatiwa huduma bora. Aidha, kwa

kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma,

Wizara yangu imeboresha utaratibu uliokuwepo wa kushughulikia

malalamiko ya wananchi. Katika mwaka 2007/08, Wizara yangu

Page 57: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

57

itaendelea kutoa mafunzo ya utoaji wa huduma bora kwa mteja

kwa waajiriwa wapya.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi

85. Mheshimiwa Spika, wiki ya Utumishi wa Umma

huadhimishwa kila mwaka katika wiki ya tatu ya mwezi Juni,

ambapo mwaka huu iliadhimishwa tarehe 17.6.2007 hadi

23.6.2007. Katika maadhimisho hayo Wizara na Taasisi za Serikali

hushiriki maonyesho kwa lengo la kuelimisha umma juu ya

huduma zitolewazo na Wizara/Taasisi hizo. Mwaka huu jumla ya

Wizara na Taasisi 77 zimeshiriki maonyesho hayo na kauli mbiu

ilikuwa ni “Zingatia Maadili, Pambana na Rushwa ili

kuimarisha Utawala Bora”. Kamati ya Maonyesho hayo iliteua

jopo la majaji ambalo lilitumia vigezo vifuatavyo kuwapata

washindi:- Iwapo Wizara inafanya juhudi zozote katika kuboresha

utoaji huduma; Iwapo Wizara ina utaratibu wa kushughulikia kero

mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupunguza mzunguko wa utoaji

huduma. Aidha, mawasilisho katika mabanda ya maonyesho

yalizingatia uwezo wa washiriki kufafanua maswala mbalimbali,

kufikisha ujumbe na vielelezo, uwezo wa washiriki kujieleza na

Page 58: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

58

kufikisha ujumbe, tabia na mwenendo wa washiriki, muonekano,

bidhaa zilizoonyeshwa na uwezo wa kuhudumia, lugha iliyotumika

kufikisha ujumbe na wingi wa wateja wanaoingia na

kuhudumiwa.

86. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu katika maadhimisho

hayo ililenga kuufahamisha umma, mikakati inayotekelezwa na

Wizara kulingana na kauli mbiu hiyo. Nafurahi kulijulisha Bunge

lako Tukufu kuwa kati ya Washiriki hao 77, Wizara yangu imepata

ushindi wa pili, ambapo kwa upande wa Wizara zote zilizoshiriki

imekuwa mshindi wa kwanza. Ushindi huu wa Wizara yetu ni

changamoto kubwa kwetu na umetokana na michango na ushauri

mkubwa tunaoupata toka kwa waheshimiwa wabunge na

wananchi kwa ujumla. Ninawashukuru sana.

87. Mheshimiwa Spika, ili kupambana na janga la UKIMWI

katika sehemu ya kazi, Wizara yangu imeendelea kuhamasisha

watumishi ili waweze kupima afya zao kwa kuwaleta wataalam

wa huduma ya ushauri nasaha na kupima kwa hiari mahali pa

kazi kila baada ya miezi mitatu. Vilevile, katika uhamasishaji huo

watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI walisaidia kuhamasisha

kwa kutoa uzoefu wa kuishi kwa matumaini. Kutokana na

Page 59: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

59

hamasa hiyo, jumla ya watumishi 219 wamepima kwa hiari. Zoezi

hili limeongeza hamasa ya watumishi kwa kupima afya zao.

Wizara imekuwa ikiwapatia watumishi walioathirika huduma za

dawa na lishe. Katika mwaka wa fedha 2007/08 Wizara yangu

itaendelea kuhamasisha upimaji wa afya na kutoa huduma kwa

waathirika.

88. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imeanzisha Kitengo cha

Elimu, Habari na Mawasiliano ambacho kina jukumu la kutoa

taarifa zinazoihusu Wizara kwa wananchi. Katika mwaka wa fedha

2006/07 Kitengo hiki kiliratibu vipindi vya Elimu, Habari na

Mawasiliano ndani na nje ya Wizara. Utaratibu huu umesaidia

kuelimisha umma juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa. Katika

mwaka wa fedha 2007/08 Wizara yangu itaendelea kuboresha

mawasiliano, kutoa elimu na habari kwa wadau mbalimbali.

Vyuo vya Ardhi

89. Mheshimiwa Spika, Wizara ina vyuo viwili vya Ardhi vya

Tabora na Morogoro ambavyo vinatoa mafunzo ya Astashahada

(Ordinary Diploma) katika fani za Urasimu Ramani na Upimaji

Ardhi, na Cheti katika fani za Umiliki Ardhi na Uthamini na

Page 60: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

60

Uchapaji Ramani. Fani hizi ni muhimu kwa ajili ya kukidhi mahitaji

ya soko la wataalam wa ardhi nchini. Katika mwaka wa fedha

2006/07 idadi ya wahitimu ilikuwa 124 kati yao 44 walitoka Chuo

cha Ardhi Morogoro na 80 walitoka Chuo cha Ardhi Tabora

(Jedwali Na. 12). Katika mwaka 2007/08, vyuo hivyo vitaandaa

programu ya mafunzo ya muda mfupi ili wataalam wa Sekta ya

Ardhi waliopo katika Halmashauri waweze kupatiwa mafunzo.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa maombi maalum. Natoa wito

kwa Halmashauri kutumia fursa hii kuwapeleka wataalam

wao kujifunza ili waende sanjari na mabadiliko ya

teknolojia.

SHUKRANI

90. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati

kwa Mheshimiwa Rita Louise Mlaki (Mb), Naibu Waziri, Bibi

Salome T. Sijaona, Katibu Mkuu, Wakuu wa Idara na Taasisi na

Wafanyakazi wote wa Wizara yangu kwa juhudi na mshikamano

wao katika kufanikisha malengo ya Wizara na Taifa kwa ujumla.

Itakuwa ni ukosefu wa fadhila kama sitaishukuru Kamati ya Kilimo

na ardhi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kushauri na kutoa maoni

Page 61: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

61

ya kuboresha Sekta ya Ardhi. Pia, natoa shukrani kwa Benki ya

Dunia, Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Denmark, Uingereza,

Sweden na Uholanzi kupitia Mradi wa “Business Environment

Strengthening for Tanzania” (BEST) na Mkakati wa Kurasimisha

Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA), ambazo

zimeisaidia Wizara katika kutekeleza Mkakati wa Utekelezaji wa

Sheria za Ardhi, natoa shukrani kwa UN-Habitat kwa kuendelea

kushirikiana na Sekta ya Ardhi na Makazi katika kuboresha makazi

nchini. Aidha, nazishukuru Asasi zisizo za Kiserikali zilizoshirikiana

na Wizara katika kutoa elimu ya Sheria za Ardhi na Mipango

Shirikishi ya Matumizi ya Ardhi Vijijini. Msaada wao tunauheshimu

na kuuenzi na nawaomba wadau wengine zaidi kujitokeza

kusaidia jitihada za Serikali kuboresha huduma za ardhi na makazi

kwa wananchi. Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wapiga kura

wangu wa Jimbo la Biharamulo Mashariki katika Wilaya mpya ya

Chato kwa ushirikiano wao mkubwa wanaoendelea kuutoa

kwangu.

Page 62: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

62

HITIMISHO

91. Mheshimiwa Spika, Sera na Sheria zilizopo zinawalinda

kikamilifu wananchi wetu, lakini tatizo kubwa lililopo kwa sasa ni

baadhi ya Wananchi, Mamlaka na Taasisi mbalimbali kutozingatia

matakwa ya Sheria katika suala zima la utwaaji ardhi pindi ardhi

hiyo inapohitajika kwa shughuli za maendeleo. Sera ya Ardhi ya

Mwaka 1995 inatamka wazi kuwa kila kipande cha ardhi kina

thamani na kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5

ya Mwaka 1999 kifungu cha 3(g), Sheria ya Ardhi Na.4 ya Mwaka

1999 kifungu cha 3(g) na Sheria ya Utwaaji ardhi Na. 47 ya

Mwaka 1967 zinatambua kwamba ardhi yote inayotwaliwa kwa

mtu yeyote kwa ajili ya matumizi yoyote ni lazima mhusika wa

ardhi hiyo alipwe fidia. Kutofuatwa kwa Sheria hizi kunawaletea

usumbufu mkubwa wananchi katika kudai haki zao. Ni vizuri

Mamlaka zote zinazohusika na usimamizi wa ardhi nchini kuwa

mstari wa mbele kuwaelimisha wananchi juu ya haki ya ardhi

wanayoimiliki. Natoa rai kwa Mamlaka na Taasisi mbalimbali

zinazotwaa ardhi za wananchi hao kuheshimu Sheria, Kanuni na

Taratibu za utwaaji ardhi ili wananchi walipwe fidia kwa mujibu

wa Sheria hizo.

Page 63: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

63

92. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua kuwa ardhi ni mali ni

ukweli usiofichika kwamba Watanzania hatuwezi kushinda vita

dhidi ya umaskini kwa silaha ambayo hatuna. Silaha ya uhakika

aliyonayo kila Mtanzania, ni ardhi. Kwa kutumia ardhi kama ardhi,

na ardhi kama mtaji, tunaweza kuushinda umaskini tulionao.

Hivyo basi, njia pekee ya kuhakikisha ardhi inamwondolea

mwananchi umaskini ni kwa Serikali kupima kila kipande cha

ardhi yetu na kummilikisha mwananchi kwa kumpa hatimiliki iwe

ya kimila au ya Serikali ili aweze kuitumia kama dhamana ya

kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za fedha.

BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2007/08

93. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/07

Wizara yangu ilitengewa shilingi 18,274,683,000. na katika

mwaka wa fedha 2007/08 Wizara inaomba Bunge lako Tukufu

likubali kupitisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Ardhi,

Nyumba na Maendeleo ya Makazi ya jumla ya Shilingi

14,691,991,000 kama ifuatavyo:-

(i) Shilingi 11,091,832,000 kama Makusanyo ya Mapato

ya Serikali.

Page 64: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

64

(ii) Shilingi 3,909,653,000 kwa ajili ya mishahara ya

Watumishi .

(iii) Shilingi 8,806,338,000 kwa ajili ya matumizi

mengineyo.

(iv) Shilingi 1,976,000,000 kwa ajili ya Matumizi ya Miradi

ya Maendeleo.

Hivyo, jumla ya fedha yote ninayoomba ambayo

inajumuisha Mishahara, Matumizi Mengineyo na Matumizi

ya Miradi ya Maendeleo ni Shilingi 14,691,991,000.

94. Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana wewe, na pia

waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.

95. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Page 65: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

65

Jedwali Na. 1

HATI ZA KUMILIKI ARDHI ZILIZOSAJILIWA MWAKA 2006/07 SN KANDA ZA

USAJILI MIKOA WILAYA IDADI

Ilala 467 Kinondoni 994

DSM Temeke 446

Mradi 2497 Wizara ya Ardhi Jumla Ndogo 4404

Bagamoyo 33 Kibaha 168 Kisarawe 16 Mafia 19 Mkuranga 30 Rufiji 4

PWANI Jumla Ndogo 270

Kilosa 9 Morogoro(M) 86 Morogoro(V) 60 Mvomero 0 Jumla Ndogo 155

1

DAR ES SALAAM

MOROGORO Jumla Ndogo Kanda 4,829

Dodoma (M) 36 Dodoma (V) 57 Kondoa 18 Mpwapwa 1 Kongwa 0

DODOMA Jumla Ndogo 112

SINGIDA Iramba 2 Manyoni 16 Singida 90 Jumla Ndogo 108

2

DODOMA

Jumla Ndogo Kanda 220

Geita 17 Ilemela 963 Magu 19 Misungwi 26 Nyamagana 116

3

MWANZA

MWANZA Sengerema 14

Page 66: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

66

Ukerewe 5

Jumla Ndogo 1160

Bunda 45 Musoma (M) 30 Musoma (V ) 35 Tarime 48

MARA Jumla Ndogo 158

Kigoma (M) 42 Kigoma (V) 28 Kibondo 4 Kasulu 6

KIGOMA Jumla Ndogo 80

Bukoba (M) 42 Bukoba (V) 35 Biharamulo 53 Karagwe 25 Muleba 11 Ngara 1

KAGERA Jumla Ndogo 167

Bariadi 12 Kahama 47 Maswa 32 Shinyanga (M) 59 Shinyanga (V) 27

SHINYANGA

Jumla Ndogo 177 Igunga 14 Nzega 36 Tabora (M) 60 Urambo 4 Uyui 0 Jumla Ndogo 114

TABORA

Jumla Ndogo Kanda 1,856Ileje 30 Kyela 52 Mbeya (M) 17 Mbeya (V) 172 Mbozi 99 Mbarali 13 Rungwe 22

MBEYA Jumla Ndogo 405

4

MBEYA

IRINGA Iringa (M) 86

Page 67: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

67

Iringa (V) 5

Kilolo 9

Makete 10 Mufindi 76 Njombe 54

Jumla Ndogo 240

Mpanda 4 Nkasi 16 Sumbawanga (M) 34 Sumbawanga (V) 13 Jumla Ndogo 67

RUKWA Jumla Ndogo Kanda 712

Hai 75 Moshi (M) 129 Moshi (V) 116 Mwanga 10 Rombo 12 Same 47

KILIMANJARO Jumla Ndogo 389

Arusha 426 Arumeru 212 Karatu 45 Monduli 15 Ngorongoro 3

ARUSHA Jumla Ndogo 701

Babati 9 Hanangi 5 Mbulu 9 Kiteto 9 Simanjiro 18

MANYARA

Jumla Ndogo 50 Handeni 7 Korogwe 10 Lushoto 11 Muheza 26 Pangani 8 Tanga (J) 133 Jumla Ndogo 195

5

MOSHI

TANGA Jumla Ndogo Kanda 1,335

Page 68: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

68

Mtwara (M) 19 Mtwara ( V) 18 Masasi 5

MTWARA Newala 6

Tandahimba 2 Jumla Ndogo 50 Kilwa 2 Lindi (M) 22 Lindi (V) 9 Nachingwea 3

LINDI

Jumla Ndogo 36 Mbinga 11 Songea Urban 46 Songea Rural 11 Tunduru 1 Jumla Ndogo 69 Jumla Ndogo Kanda 155

6

MTWARA

RUVUMA Jumla Kuu 9,107

Page 69: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

69

Jedwali Na. 2

USAJILI WA HATI/NYARAKA CHINI YA SHERIA YA USAJILI WA HATI SURA NA.334

JULAI, 2006

HADI

MEI, 2007

Hat

i za

kum

iliki

ard

hi z

ilizo

sajil

iwa

Nyu

mba

zili

zouz

wa

(Tra

nsfe

r)

Mik

atab

a ya

upa

ngis

haji

nyum

ba z

aidi

ya

mia

ka m

itano

(le

ases

)

Milk

i zili

zow

ekw

a re

hani

(M

ortg

ages

)

Reh

ani

ziliz

omal

iza

deni

(D

isch

arge

&

Rel

ease

s)

Nya

raka

za

kuw

ekes

ha H

ati

(Not

ice

of D

epos

it)

Nya

raka

za

ku

wek

esha

H

ati

ziliz

oond

olew

a (W

ithdr

awal

of

Not

ice

of

Dep

osit)

Hat

i za

m

arej

esho

ya

m

ilki

na

milk

i zi

lizof

utw

a

Hat

i nyi

ngin

ezo

*

Uha

mis

hjaj

i w

a m

ilki

unao

toka

na

na

maa

muz

i ya

Bun

ge a

u sh

eria

mba

limba

li (T

rans

mis

sion

by

Ope

ratio

n of

Law

)

Nya

raka

za

Taha

dhar

i na

Vizu

izi (

Cave

ats

& I

njun

ctio

ns)

Upe

kuzz

i wa

Daf

tari

la H

ati (

Sear

ch)

JUMLA KUU

JUMLA

9,107

957

53

832

350

131

74

143

702

149

186

5,914

18,598

* Maombi ya kuandikishwa wasimamizi wa Mirathi * Maombi ya kuandikishwa warithi wa marehemu * Mabadiliko ya majina ya wamiliki wa Hati za kampuni au mashirika mbalimbali

Page 70: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

70

Jedwali Na: 3

NYARAKA ZILIZOSAJILIWA CHINI YA SHERIA YA USAJILI WA NYARAKA (SURA 117)

Nyaraka ambazo ni Lazima

Zisajiliwe (Compulsory Registration)

Nyaraka ambazo ni Muhimu Kusajiliwa Lakini Siyo Lazima

(Optional Registration)

Jumla

Kuu

KIPINDI KUANZIA

JULAI 2006 HADI

MEI,

2007

Uha

mis

ho/m

auzo

ny

umba

/mas

ham

ba a

mba

yo y

ana

baru

a ya

tol

eo

Mik

atab

a ya

upa

ngis

haji

Reh

ani

Ufu

taji

wa

Reh

ani z

ilizo

lipiw

a Ba

rua

za t

oleo

zili

zoto

lew

a kw

a m

aene

o am

bayo

hay

ajap

imw

a (o

ffer

of

Rig

ht o

f O

ccup

ancy

)

Nya

raka

zin

azot

upa

mam

laka

(P

ower

of

Atto

rney

)

Mab

adili

ko y

a jin

a (D

eed

Poll)

Nya

raka

za

uteu

zi (

Dee

d of

A p

poin

tmen

t)

Nya

rka

za m

aele

wan

o (M

emo

of

Und

erst

andi

ng)

Wos

ia (

Will

)

Mik

atab

a ya

mau

zo

Baru

a za

utw

aaji

wa

mal

i (Le

tter

of

Hyp

othe

catio

n of

goo

ds)

Hat

i ya

dham

ana

(Ind

emni

ty

Bond

s)

Mik

atab

a ya

kui

ngia

ubi

a (P

artn

ersh

ip D

eed)

Mka

taba

wa

kuto

a hu

dum

a za

ki

taal

uma

(Pro

fess

iona

l ser

vice

Nya

raka

nyi

ngin

ezo

*

Taar

ifa z

a up

ekuz

i (Se

arch

Re p

orts

)

JUMLA

22

48

41

24

3

1049

1180

36

65

49

60

110

79

127

15

1703

812

5423

* Mikataba ya makabidhiano * Maombi ya kuvunja ubia * Viapo * Mikataba ya Ukopeshaji * Maombi ya kubacdilisha mikataba * Makubaliano ya kuondoa madai * Mikataba ya kuwekesha Hati * Vizuizi * ‘Debenture’ * Mikataba ya ajira

Page 71: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

71

Jedwali Na. 4

VIWANJA NA MASHAMBA YALIYOINGIZWA KWENYE KOMPYUTA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2006/07

Na. Mkoa Viwanja Mashamba 1 Arusha 3,748 511 2 Dar es Salaam 38,011 - 3 Dodoma 6,690 66 4 Iringa 4,760 325 5 Kagera 6,824 - 6 Kilimanjaro 19,160 500 7 Kigoma 6,788 1,989 8 Lindi 4,658 - 9 Manyara 8,777 31 10 Mara 16,239 103 11 Mbeya 15,875 179 12 Morogoro 4,477 261 13 Mtwara 3,972 48 14 Mwanza 44,962 26 15 Pwani 5,533 217 16 Rukwa 7,538 11 17 Ruvuma 33,710 839 18 Shinyanga 19,285 3 19 Singida 20,177 18 20 Tabora 15,188 - 21 Tanga 14,448 106

Jumla 300,820 5,233

Page 72: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

72

- Jedwali Na. 5

Mashauri Yaliyoamuliwa Katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Mwaka 2006/07

Na. BARAZA MASHAURI YALIYOKUWEPO

MASHAURI YALIYOFUNGULIW

A

MASHAURI YALIYOAMULIW

A

MASHAURI YANAYOENDELEA

1 Arusha 202 371 187 386

2 Dodoma 137 143 161 119

3 Ilala 280 789 523 546

4 Iringa 72 211 166 117

5 Kagera 211 511 207 515

6 Kigoma 22 122 72 72

7 Kilimanjaro 220 353 357 216

8 Kinondoni 756 868 629 995

9 Lindi 14 34 28 20

10 Manyara 171 255 140 286

11 Mara 165 363 204 324

12 Mbeya 102 457 180 379

13 Morogoro 114 305 155 264

14 Mtwara 25 96 85 36

15 Mwanza 230 533 143 620

16 Pwani 35 152 53 134

17 Rukwa 76 105 96 85

18 Ruvuma 58 142 39 161

19 Shinyanga 50 102 58 94

20 Singida 73 145 93 125

21 Tabora 53 32 39 46

22 Tanga 50 242 167 125

23 Temeke 394 541 398 537

JUMLA 3510 6872 4180 6202

Page 73: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

73

Jedwali Na. 6

HALI YA MIKOPO NA MAREJESHO KUTOKA MFUKO WA PDRF

Na Halmashauri Kiasi cha Mkopo

kiliotolewa Tarehe ya

kutolewa MkopoKiasi cha Mkopo kilichorejeshwa

Kiasi cha deni anachodaiwa

1 Nkasi 900,000.00 Julai 1999 900,000.00 0.00

2 Mpanda 1,368,000.00 Julai 2000 1,368,000.00 0.00

3 Sumbawanga 1,566,000.00 Julai 2000 1,566,000.00 0.00

4 Jiji la Mbeya 16,700,000.00 Julai 2000 16,700,000.00 0.00

5 Ileje 6,632,000.00 Julai 1997 6,632,000.00 0.00

6 Mtwara Manispaa 4,322,615.00 Julai 2000 4,322,615.00 0.00

7 Kibaha Wilaya 36,618,500.00 Julai 2000 36,618,500.00 0.00

8 Hanang 2,500,000.00 Julai 2000 2,500,000.00 0.00

9 Kigoma Vijijini 600,000.00 Julai 2000 600,000.00 0.00

10 Jiji la Tanga 53,588,000.00 Julai 2000 53,588,000.00 0.00

11 Kondoa mjini 5,295,000.00 Julai 2002 5,295,000.00 0.00

12 Njombe 592,000.00 Julai 2000 592,000.00 0.00

13 Hai 10,000,000.00 Feb. 2002 10,000,000.00 0.00

14 Bukoba Manispaa 2,915,000.00 Julai 2002 2,915,000.00 0.00

15 Monduli 2,228,898.00 Julai 1993 0.00 2,228,898.00

16 Mwanga 25,825,000.00 Oct., 2004 24,173,750.00 1,651,250.00

17 Babati 4,443,000.00 Julai 2000 2,006,485.00 2,436,515.00

18 Kondoa Wilaya 4,118,400.00 Julai 2002 0.00 4,118,400.00

19 Maswa 6,000,000.00 Feb. 2002 1,925,317.00 4,074,683.00

20 Tarime 4,586,000.00 Julai 2002 3,802,236.00 783,764.00

21 Iringa Vijijini 5,000,000.00 Julai 2000 3,312,670.00 1,687,330.00

22 Mufindi 8,206,000.00 Feb. 2002 0.00 8,206,000.00

23 Mbarali 13,880,000.00 Feb. 2002 526,177.00 13,353,823.00

24 Songea Manispaa 43,109,000.00 Julai 2000 7,277,445.00 35,831,555.00

25 Tunduru 2,900,000.00 Julai 2000 1,486,985.00 1,413,015.00

26 Masasi 34,806,000.00 Julai 2000 12,667,955.00 22,138,045.00

27 Newala 3,007,400.00 Julai 2000 434,555.00 2,572,845.00

28 Ruangwa 2,130,000.00 Julai 2000 0.00 2,130,000.00

29 Liwale 8,324,000.00 Julai 2000 5,244,626.00 3,079,374.00

30 Bagamoyo 68,450,000.00 Julai 2000 6,666,851.00 61,783,149.00

31 CDA 5,279,000.00 Julai 2000 3,679,000.00 1,600,000.00

32 W/Kilimo na Mifugo

13,222,800.00 April 1999 0.00 13,222,800.00

399,112,613.00 216,801,167.00 182,311,446.00

Page 74: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

74

Jedwali Na. 7

ORODHA YA VIJIJI VILIVYOPIMWA MIPAKA KWA MWAKA 2006/07

NA. Mkoa Wilaya Idadi ya Vijiji

Kisarawe 75 Bagamoyo 82

Kibaha 25 Mkuranga 88

Rufiji 68

1 Pwani

Jumla Ndogo 338 Chunya 70

Ileje 68 Kyela 94 Mbeya 120

Rungwe 152 Mbarali 65

2 Mbeya

Jumla Ndogo 569 Kilwa 94 Liwale 28

Nachingwea 81 Ruangwa 75

Lindi 125

3 Lindi

Jumla Ndogo 403 Mpanda 78 Nkasi 82

Sumbawanga 173

4 Rukwa

Jumla Ndogo 333 Makete 97 Mufindi 71 Njombe 134

Iringa/Kilolo 87 Ludewa 76

5 Iringa

Jumla Ndogo 465 Kibondo 67 Kasulu 84 Kigoma 55

6 Kigoma

Jumla Ndogo 206 Bukombe 112 7 Shinyanga

Jumla Ndogo 112 Biharamulo/Chato 91 8 Kagera

Jumla Ndogo 91 Muheza 102 Korogwe 49

9 Tanga

Jumla Ndogo 151 Jumla Kuu 2668

Page 75: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

75

Jedwali Na 8

MIKOPO YA NYUMBA ILIYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO YA NYUMBA KWA WATUMISHI WA SERIKALI NA MAREJESHO YAKE KUANZIA MWAKA

1993/94 HADI 2006/07

S/N Mwaka wa Idadi ya Jumla ya Fedha Kiasi Kilichorejeshwa

Fedha Watumishi Iliyotumika 1 1993/1994 30 62,800,000.00 02 1994/1995 23 39,173,750.00 03 1995/1996 107 228,665,687.50 2,148,986.154 1996/1997 0 0 8,410,126.905 1997/1998 0 0 20,529,520.506 1998/1999 116 297,344,244.20 8,665,603.507 1999/2000 0 0 35,983,460.358 2000/2001 0 0 38,798,185.809 2001/2002 110 517,725,439.10 43,405,463.4010 2002/2003 31 116,758,000.00 58,346,644.6011 2003/2004 85 310,918,445.45 78,139,443.0512 2004/2005 17 77,078,610.00 98,371,414.2013 2005/2006 260 1,187,715,360.00 140,172,057.9614 2006/2007 390 1,646,277,979.60 228,037,702.09

JUMLA 1169 4,484,457,515.85 761,008,608.50

Page 76: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

76

Jedwali Na.9

IDADI YA MAJENGO NA NYUMBA ZILIZOTENGENEZWA NA GHARAMA ZAKE KUANZIA JULAI 2006 HADI JUNI 2007

MAJENGO NYUMBA (APARTMENTS)

Idadi ya nyumba katika Tawi

S/N

Tawi

Idadi ya majengo

Katika Tawi

Majengo yaliyo

tengenezwa Gharama

(TShs) Zilizopo ZilizotengenezwaGharama

(TShs)

JUMLA YA GHARAMA

ILIYOTUMIKA TShs

1 ARUSHA 183 59 102,344,577 988 340 109,670,360 212,014,9372 BUKOBA 47 9 62,172,242 251 18 11,550,920 73,723,1623 DODOMA 15 4 55,200,450 132 28 5,306,300 60,506,7504 ILALA 403 84 488,500,962 3,579 573 379,526,305 868,027,2675 IRINGA 31 6 64,304,755 201 86 27,960,500 92,265,2556 KIGOMA 24 4 39,453,688 97 49 8,031,600 47,485,2887 KINONDONI 173 32 259,196,735 774 117 397,846,856 657,043,5918 LINDI 28 1 7,288,710 122 20 5,639,600 12,928,3109 MBEYA 34 2 39,293,740 252 72 19,820,280 59,114,020

10 MOROGORO 60 11 138,477,083 579 37 86,801,945 225,279,02811 MOSHI 148 15 219,750,451 722 118 85,217,095 304,967,54612 MTWARA 65 3 3,350,940 227 28 12,785,700 16,136,64013 MUSOMA 37 8 37,315,905 147 21 6,127,090 43,442,99514 MWANZA 140 26 282,723,955 1,005 98 51,757,672 334,481,62715 SHINYANGA 45 11 71,208,521 197 17 19,311,391 90,519,91216 SINGIDA 28 85 12 6,706,409 6,706,40917 TABORA 28 4 41,377,800 182 23 26,822,059 68,199,85918 TANGA 166 10 71,472,670 787 70 55,492,287 126,964,95719 TEMEKE 190 29 180,712,990 856 89 146,921,710 327,634,70020 UPANGA 547 92 440,338,620 4,838 469 422,809,217 863,147,83721 Makao Makuu 0 8 105,753,226 0 21 318,471,633 424,224,859

JUMLA 2392 418 2,710,238,020 16021 2306 2,204,576,929 4,914,814,949

Page 77: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

77

Jedwali Na. 10

WATUMISHI WALIOPANDISHWA VYEO JULAI 2006 – JUNI 2007 Idara Cheo Idadi

Mipangomiji Mkuu I 1 Mipangomiji Mkuu II 2 Mipangomiji Mwandamizi 3

Maendeleo ya Makazi

Msanifu Majengo Mwandamizi 1

Mpima Ardhi Mkuu II 2 Mpima Ardhi Mwandamizi 3

Fundi Sanifu Mkuu 9 Upimaji na Ramani

Fundi Sanifu Mwandamizi 48

Afisa Ardhi Mkuu1 2 Afisa Ardhi Mkuu II 4 Afisa Ardhi Mwandamizi 2 Mchapa Hati Mwandamizi 1

Maendeleo ya Ardhi

Mthamini Mkuu II 1 Afisa Ugavi Mkuu II 1 Afisa Utumishi Mkuu II 1 Afisa Tawala Mwandamizi 2

Msaidi wa Mtendaji Mkuu 1 1

Mwandishi Mwendesha Ofisi 3

Katibu Mahsusi II 2 Dereva Mwandamizi 2

Utawala na Rasilimali Watu

Dereva I 3 Mchumi Mkuu II 1 Idara ya Mipango Mchumi I 3 Mhasibu Mwandamizi 1 Mhasibu I 3 Mhasibu II 5

Idara ya Uhasibu

Mhasibu Msaidizi 2 Jumla 109 Wanawake 37 Wanaume 72

Page 78: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

78

Jedwali 11(a)

WATUMISHI WALIOHUDHURIA MAFUNZO YA MUDA MFUPI – 2006/07

Na. Aina ya kozi Idadi 1 Computer Course 14 2 Advanced Drivers Course 1 3 Office Management 2 4 Security Course 1 5 Records Management 1 6 Customer Care Course 77 7 Procurement Course 1 8 Auto CAD 1 9 Retirement Course 1

10 Fleet Management 1 11 Fire Fighting Training 50 12 Project Management 1 13 Advance Management Course 2 14 CPA Review 9 15 Professional Enhancement 1 16 Higher Standard Government Accounting 2 17 Integrated Urban Planning 1 18 Coastal Area Management 1 19 Toponomy Workshop 1 20 Digital Photogrametry 1 21 Global Navigation Satellite System 1 22 Monitoring & Evaluation 1 23 Operational Project Planning 1 24 Ethics of Good Government 1 25 Effective Management 1 26 Environmental Planning and Design 1 27 Housing & Urban Development 1 28 Remote Sensing Application & Mapping 3

29 Study Tour of village Development and Certification 4

30 Refresher Course in Implementation of New land Laws and Registry 1

31 Computer Skills and Database 14 32 Computer Skills and Record Management 9 33 Monitoring & Evaluation & Reporting 3 34 Data base and Data warehousing 1 35 Short Course in Accountancy 1 36 Project Procurement Contract 3 37 Management Skills Stage II 3 38 Office Practices 1

Jumla 219

Page 79: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

79

Jedwali Na.11 (b)

WATUMISHI WALIOHUDHURIA MAFUNZO YA MUDA MREFU – 2006/07

Na. Aina ya kozi Idadi

1 Certificate in Records Management 2 2 Certificate in Law 1 3 Diploma in Law 8 4 Diploma in Cartography 1 5 Diploma in Secretarial 4 6 Diploma in Geo-informatics 4 7 Advanced Diploma in Accountancy 5 8 BSc in Urban Planning Management. 7 9 Bachelor in Law 4

10 Postgraduate Diploma in Housing 1 11 Post Graduate Diploma in Scientific Computing 2 12 Post Graduate Diploma in Hydrograph 1 13 Masters in Public Administration 2 14 Masters in Real Estate 5 15 Masters in Economics 1

16 Masters in Business Administration 2 17 Masters in Geometric 3

Jumla 53

Jedwali Na.12

IDADI YA WANACHUO WALIOHITIMU VYUO VYA ARDHI 2006/07

Na. Aina ya Kozi Chuo cha Tabora

Chuo cha Morogoro

1. Diploma in Cartography 14 - 2. Certificate in Cartography 21 - 3. Certificate in Land Mgt. Valuation &

Registration 24 -

4. Certificate in Graphics Arts and Printing 21 - 5. Diploma in Land Survey - 24 6. Certificate in Land Survey - 20 Jumla 80 44

Page 80: HOTUBA YA WAZIRI WA ARDHI...• Kujenga nyumba mpya za kuuza au kupangisha katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma kwa kushirikiana na sekta binafsi na kuzifanyia matengenezo

80

Matofali ya udongo saruji yanayofungamana kwa ajili ya kujenga

Nyumba za gharama nafuu

Nyumba iliyojengwa kwa matofali yanayofungamana