hali ya elimu tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya uhuru...ni kubwa. mwaka huu peke...

35
Hali ya Elimu Tanzania Miaka 50 Baada ya Uhuru Tufanye Nini Tuweze Kusonga Mbele? Mada za Kongamano La Elimu Kuadhimisha Miaka Hamsini ya Uhuru Lililoandaliwa na UDSTA kwa Kushirikiana na HakiElimu.

Upload: others

Post on 10-Jan-2020

35 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

Hali ya Elimu Tanzania Miaka 50 Baada ya Uhuru

Tufanye Nini Tuweze Kusonga Mbele?

Mada za Kongamano La Elimu Kuadhimisha Miaka Hamsini

ya Uhuru Lililoandaliwa na UDSTA kwa Kushirikiana na HakiElimu.

Page 2: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

2

Shukrani HakiElimu na UDSTA wanatoa shukrani za kuipekee kwa watoa mada Mh. Jackson makweta, Perofesa Herme Mosha, Dk. Hillary Dachi na Dk. Kitila Mkumbo kwa kukubali kuandaa na kuwasilisha mada katika Kongamano la "Kutathimini hali ya Elimu nchini: Miaka 50 Baada ya Uhuru" lililofanyika Chuo kikuu cha Dar es Salaam 26 Nov.2011.Pia tunapenda kuwashukuru watu wotawalioshiriki na kuchangia katika Kongamano hili.

Wakusanyaji Robert Mihayo Elisante Kitulo Annastazia Rugaba

Mhariri Elizabeth Missokia

Mchapishaji ©HakiElimu 2012 SLP 79401, Dar es Salaam, Tanzania Simu: (255 22) 2151852 au 3 Faksi: (255 22) 2152449 Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.hakielimu.org

ISBN: 978-9987-18-037-0 Unaruhusiwa kunakili sehemu yoyote ya kijitabu hiki kwa minajili isiyo ya biashara. Unachotakiwa kufanya ni kunukuu chanzo cha sehemu iliyonukuliwa na kutuma nakala mbili za chapisho kwa HakiElimu.

Page 3: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

3

Utangulizi ...............................................................................................................................4 Hotuba Ya Ufunguzi: Licha ya mafanikio changamoto bado nyingi .........................................7 Elizabeth Missokia Ubabaishaji wa viongozi ni kikwazo kwa elimu nchini ...............................................................9

Jackson Makwetta Miaka 50 ya Uhuru: Tanzania haina mengi ya kujivunia kielimu ..............................................15 Profesa Herme Mosha

Hadhi ya Ualimu Imeporomoka Nchini......................................................................................19 Dk. Hillary Dachi Dharau kwa Wataalamu Inaliangamiza Taifa..........................................................................24 Dk. Kitila Mkumbo

Hoja za Wachangiaji .................................................................................................................34

Yaliyomo

Page 4: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

4

Mnamo tarehe 26 Novemba mwaka 2011 shirika la HakiElimu kwa kushirikiana na Umoja wa walimu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSTA)waliandaa kongamano kubwa kuwahi kutokea nchini lenye lengo la kutathmini hali ya elimu nchini; miaka 50 tangu Tanzania Bara kupata uhuru wake mwaka 1961. Wazungumzaji wakuu walikuwa ni Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Mh Jackson Makweta na Wa-hadhiri wandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Herme Mosha, Dk Hillary Dachi na Dk. Kitila Mkumbo. Kongamano hilo lilidhamiria kutathmini Tumetoka wapi, tupo wapi na wapi tunaelekea:wapi katika sekta ya elimu hapa nchini. Aidha, Kongamano lilitakiwa kujadili kama taifa hapa tulipo tunaridhika napo? Je, nini kifanyike ili kuboresha zaidi hali hii? Pia kongamano hili lilitarajiwa kutathmini tumejifunza nini katika miaka hii 50 iliyopita? Kongamano hili pia lilitarajiwa kupima kuna nini na ni kwa kiasi gani tunajivunia elimu yetu na je imetoa mchango gani katika taifa letu? Hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo yalijadiliwa katika kongamano hilo la kusisimua lililohudhuriwa na walimu, wanafunzi kutokavyuo vikuu na shule mbalimbali za sekondari , Marafiki wa Elimu pamoja na wananchi mbali mbali kutoka sehemu mbalimbali za nchi yetu. Kwa ujumla washiriki wote walitambua mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania. Kongamano hilo liliithibitisha kwa takwimu ongezeko la idadi ya shule na vyuo, idadi ya uandikishwaji na usawa baina ya wanafunzi wa kike na kiume. Kwa mfano lilisifu mafanikio katika ongezeko la idadi ya shule za msingi kutoka shule 338 tu mwaka 1961 hadi zaidi ya 16,000. Pia lilisifu ongezeko la idadi ya shule za sekondari kutoka 41 tu mwaka 1961 tu mwaka 1961 hadi 4,367 zilizopo sasa. Hata hivyo pamoja na mafanikio haya washiriki wote walibaini changamoto mbalimbali ambazo zinaikabili sekta ya elimu. Baadhi ya changamoto hizi ni ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaoshindwa mitihani, na kuporomoka kwa ubora wa elimu . Washiriki walitoa mfano wa tafiti zinazoonesha kuwa kumekuwa na watoto wengi wanaohitimu darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika. Aidha,kumekuwa na uhaba mkubwa wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia pamoja na ukosefu wa waalimu. Na mwisho kila mmoja alitoa wito kwa wadau wa elimu nchini kuendelea kuikumbusha serikali juu ya changamoto hizo na namna ambavyo zinaweza kutatuliwa. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa mada zilizowasilishwa hapo na wataalamu hao pamoja na maoni yaliyotolewa na washiriki wa kongamano hili. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa mada zilizowasilishwa hapo na wataalamu hao pamoja na maoni yali-yotolewa na wa shiriki wa kongamano hili.Lengo lake ni kuhakikisha kuwa mawazo yaliyotolewa siku hiyo yanawafikia watu wengi zaidi ili waweze kuyafanyia kazi kwa lengo la kuboresha elimu nchini. Akifungua Kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu, Elizabeth Missokia alisema kumekuwa na mafanikio makubwa katika sekta ta elimu tangu nchi ilipopata Uhuru miaka 50 iliyopita. Alisema mathalani tulikuwa na shule za msingi takribani 3,238 lakini sasa tuna shule za msingi zipatazo 16,000.Aidha, mwaka huo wa 1961, tulikuwa na shule za sekondari 41 na wanafunzi 11,832 lakini mwaka huu tuna shule za sekondari 4,367 na wanafunzi 178,9547.Pia mwaka 1961 tulikuwa na vyuo vya ualimu vitatu na leo hii tunavyo 103. Haya alisema ni mafanikio makubwa. Lakini ali-bainisha kuwa bado kuna changamoto nyingi hususani kuhusu ubora wa elimu. Changamoto sugu ni uhaba wa vitendea kazi kwa walimu, ukosefu wa maabara, maktaba, uhaba wa nyumba za walimu, vyumba vya madarasa pamoja na mazingira mabovu ya kujifunzia ambavyo vimechangia kuporomoka kwa elimu yetu. Changamoto nyingine ni maslahi mabovu ya walimu na watumishi wa ngazi za kawaida mashuleni. Mtoa mada wa kwanza ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Elimukatika serikali ya kwanza, Jackson Makwetta alisema kuporomoka kwa elimu nchini kunatokana na Tanzania kuwa na viongozi wababaishaji, wasemaji wa maneno mengi, wasiotekeleza wanayoyasema na kukosa ufuatiliaji. Katika hotuba yake iliyopatikana kwa maandishi Mh. Makwetta al-isema, “Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefikia lakini, hajifungui.”Hivyo alisema kuwa Tanzania inahitaji kufanyiwa mabadiliko vinginevyo itaendelea kudidimia kiuchumi.

Utangulizi

Page 5: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

5

Lakini Makwetta alibainisha pia kuwa: “Tatizo kubwa la nchi hii ni serikali kutofuatilia, wala si tatizo la kukosekana kwa sera. Hili ni taifa la wasemaji maneno na siyo taifa la watekelezaji… kwa sababu wahusika hawataki kupata taabu” Naye Profesa Herme Mosha, akitoa mada katika kongamano hilo alisema kuwa, tatizo la Tanzania ni viongozi wake ku-tofuata sera za elimu zilizopo.Ali sema kuwa wakati wa kusherehekea Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yapo baadhi ya mambo ambayo watu wanapaswa kusema hapana, ikiwa ni pamoja na watoto kukaa chini madarasani, watoto kujazana madarasani na utekelezaji mbovu wa miradi na mipango ya elimu.n.k. Dk. Hillary Dachi yeye alizungumzia zaidi kuporomoka kwa hadhi ya ualimu tangu nchi ilipopata uhuru kiasi kwamba sasa hivi walimu wanaishi mauisha ya dhiki na wengi hawaipendi kazi hiyo. Dk. Dachi anaona kuwa taifa halitapata waalimu wa kutosha ikiwa hakuna juhudi za makusudi za kumfanya mwalimu aliyepo aendelee kufanya kazi yake kwani kwa sasa wengi hukimbia taaluma zao za ualimu na kuhamia katika taaluma zingine. Naye Dk. Kitila Mkumbo alisema kuwa, kwa sasa taifa lazima liamue kukubaliana na maoni ya wataalamu kuhusu lugha ya kufundishia kama iwe ni Kiswahili, hali aliyosema itawasaidia wanafunzi kuelewa vyema wanachofundishwa darasani. Kama sivyo basi Kiingereza kifundishwe vizuri ili wanafunzi wakielewe na waweze kukitumia ipasavyo. Kinachosisistizwa na watoa mada na washiriki wa Kongamano hili ni kuwa, pamoja na kwamba tunastahili kujivunia kuona watoto wetu tunao madarasani, na ni muhimu tuendelee kuwaandikisha zaidi, jambo la msingi: zaidi kuwa tuwape

watoto hao elimu bora! Elimu bora itawawezesha wa-toto wetu kuweza kukabiliana na chamgamoto zina-zowazunguka wao pamoja na jamii zao. Watanzania tunapaswa kutafakari sana mustakbali wa elimu yetu. Imefika wakati tuangalie kuwa labda badala ya kuendelea kujenga shule mpya, pengine sasa tuangalie zaidi namna ya kuboresha ufundishaji na ufundishwaji katika zile shule zilizopo ili wanafunzi wapate ujuzi wanaohitaji sasa na baadaye katika maisha yao. Ujuzi au uwezo huu ni pamoja na ule utakaomuwezesha mwanafunzi kujiamini na kujituma, kuweza kutatua matatizo na kukabiliana na changamoto kwa ufanisi na kuchambua na kutathmini taarifa kwa ufasaha na umakini zaidi. Elimu yetu inapaswa iwape wanafunzi uwezo wa kutumia mitazamo waliyojifunza kwenye eneo moja katika maeneo mengine. Aidha, elimu tunayowapa inapaswa iwape uwezo wa kuelewa na kuwa tayari kuchangia mahitaji ya jamii zao na taifa kwa ujumla.

Watoa mada wakuu katika Kongamano la kutathmini hali ya elimu

nchini, Miaka 50 baada ya uhuru wa Tanganyika. Kutoka kushoto ni

Prof Herme Mosha, Dkt Hillary Dachi na Dkt Kitila Mkumbo wote wa

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Page 6: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

6

HOTUBA YA UFUNGUZI: Licha ya mafanikio changamoto bado nyingi

Na Elizabeth Missokia* [Muhtasari: Pamoja kutambua mafanikio ya elimu yaliyofikiwa hapa nchini tangu 1961,

hususani upande wa kuongeza idadai tya shule na wanafunzi, mzungumzaji alionesha kuwa sekta hiyo bado imegubikwa na changamoto nyingi zinapaswa kuangaliwa ili watoto wote wa Tanzania wapate fursa ya kupata bora.] Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Bodi ya HakiElimu, Members wa HakiElimu, UDSTA, ninapenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wote mliofika siku hii ya leo ili kuweza kuzungumza na kutathmini mambo muhimu katika elimu ya nchi yetu na kuweza kutoka na mapendekezo ambayo yatakuwa yanatoa mwelekeo ni nini watanzania, hasa vijana, wanasema kuhusu elimu ya Tanzania. Miaka hamsini tumejitahidi, tumefanya mengi mazuri, na kwa kweli mafanikio ni mengi. Lakini bado kuna changamoto nyingi sana ambazo ziko mbele yetu na ni muhimu basi tuangalie na kutathmini tunayodhani yafanyike katika kuboresha elimu. Tumetoka mbali, miaka hamsini ni mingi na ukweli ukiangalia katika mwaka 1961 tulikuwa na shule za msingi takribani 3,238; leo tuna shule za msingi zipatazo 16,000. Haya ni mafanikio makubwa sana. Mwaka huo wa 1961, tulikuwa na shule za

sekondari 41 na wanafunzi 11,832 mwaka huu tuna shule za sekondari 4,367 na wanafunzi 178,9547 nchi nzima. Aidha, wakati nchi inapata

uhuru tulikuwa na vyuo vya ualimu vitatu na leo hii tunavyo 103.Haya pia dhahiri ni mafanikio makubwa sana.Lakini kama ilivyo kawaida, katika kila mafanikio, na hasa unapojaribu kupanua elimu, changamoto pia huwa zinaambatana na mafaniko hayo; h. asa katika nchi changa kama Tanzania. Wakati tumeongeza idadi ya shule na idadi ya wanafunzi, uwiano katika madarasa, kati ya wanafunzi na walimu, hapo awali ulikuwa 1:36; sasa hivi ni kama 1:75. Lakini tunajua hali halisi kwamba unapokwenda katika shule, kuna madarasa, hasa ya msingi, yana wanafunzi hata zaidi ya 100. Idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana. Mwaka 1961 shule za msingi tulikuwa na wanafunzi takribani 4,486 sasa hivi tuna

milioni 8 na kama laki tatu inakaribia laki nne!. Katika shule za sekondari mwaka 1961 tulikuwa na wanafunzi 11,832 lakini sasa hivi tuna zaidi ya wanafunzi milioni moja tunakaribia milioni mbili.

Changamoto zinakuja tena katika uwiano; bado tunaona

mpaka sasa hivi kwani wakati ule mwaka 1961 uwiano

ulikuwa 1:37. Lakini sasa hivi uwiano si mzuri sana

katika elimu ya sekondari na shule za msingi.Usawa wa

kijinsia, miaka ya sitini tulikuwa na tofauti ya kama asili-

mia 40 hivi sasa tunayo kama 50:50 usawa. Ukiangalia

uwiano katika sekondari pamoja na shule za msingi. Se-

kondari kidogo iko chini asilimia 48. Lakini changamoto

ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-

bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-

babu ya ujauzito.

Na tunapopanda juu, katika elimu ya juu, tunaona uwiano kati ya wavulana na wasichana, unapungua, wa wasichana una-

zidi kuwa mdogo. Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na elimu ya sekondari, ukizingatia na shule kata ambazo zimeon-

gezeka nyingi tu, kwa kweli imeongezeka kwa kiasi kikubwa sana; hadi kufikia asilimia 52.2 ukilinganisha na asilimia tano

ambayo ilikuwa mwaka 61. Lakini je hawa wanafaulu kweli? Kwa sababu ukiangalia kiwango cha kufeli kimeongezeka

toka asilimia 22.3 mwaka 1985 hadi asilimia 49.6 mwaka 2010 kwa kidato cha nne.

Idadi ya madarasa na vifaa vya kufundishia na kujifunzia

katika shule nyingi bado ni haba

Page 7: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

7

Hivyo ingwa ni kweli mafanikio ni mengi lakini changamoto vilevile ni nyingi. Je, tufanye nini? Wadau mbalimbali wa elimu wanapendekeza, taasisi mbalimbali, pamoja na chuo kikuu wamefanya utafiti wa kina ambao unaonesha changa-moto mbalimbali na mafanikio mbalimbali na kutoa mapendekezo mengi tu ambayo ni muhimu sana serikali ikayafanyia kazi. HakiElimu inapongeza juhudi hizi za serikali katika kupanua elimu, lakini changamoto katika kuboresha ubora wa elimu ya watoto ili kutoa wanafunzi au wahitimu ambao wanahitimu wakiwa na ujuzi unaowawezesha kupambana na changa-moto mbalimbali katika maisha yao, na katika kujiajiri au kuajiriwa, bado nyingi sana. Baadhi ya changamoto sugu ni uhaba wa vitendea kazi. Kama nilivyosema mwanzoni unapanua shule, unaongeza shule, idadi ya wanafunzi inaongezeka, madarasa yanaongezeka, lakini je, una vitendea kazi vya kutosha ambavyo vinaw-awezesha hawa walimu walioko kule darasani, ambao wanafundisha darasa moja ambalo lina wanafunzi 73 au zaidi ku-weza kumudu na kumwezesha kila mtoto aweze kusoma na kupata elimu? Tumesikia juzijuzi hapa utafiti ambao ume-fanywa na Uwezo, unaonesha dhahiri kwamba kiwango cha elimu kinashuka. Watoto wengi walioko shule za sekondari na shule za msingi na wale ambao wanahitimu shule za sekondari na msingi, wanahitimu wakiwa hawajui kusoma na kuandika au kufanya hesabu rahisi tu ambazo ziko katika level ya darasa la pili. Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2010 yalitushtua. Lakini si 2010 tu, kwa sababu ukiangalia mporomoko huu umeanza miaka sita, taribani kumi, iliyopita. Je, tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru tunatafakari haya yote?. Kuna utafiti uliofanywa na World Bank, ambao unaonesha walimu wanakaa darasani kwa muda wa saa labda moja na nusu au mbili tu Walimu wetu wengi wao wanakaa darasani na wanapokaa darasani haina maaana kwamba wanafundisha. Walimu wamekata tamaa; uwajibikaji umepungua; na uwajibikaji umepungua kwa wananchi. Kwa wazazi, tunajiona kwamba wajibu wetu ni kuwapeleka watoto shuleni na kuchangia tu na si kufuatilia matokeo yao. Unapoambiwa kwamba mtoto wako yuko darasa la saba hawezi kusoma na kuandika sawasawa unashituka!Unashangaa nini mzazi? Ina maana kwamba hukuwajibika. Lakini kama mtanzania unawajibika vipi kuiwaijibisha serikali na kuikum-busha na kuiambia kwamba tunataka elimu ambayo itawawezesha watoto wetu, waweze kutoka na ujuzi utakaoondoa taifa letu katika umaskini, katika ufisadi, rushwa na changamoto nyingine mbalimbali. Mwalimu unapokwenda shuleni ukakaa saa moja tu darasani au shuleni hujawajibika na humtendei haki yule mwanafunii ambaye anatakiwa kufundishwa. Bila shaka serikali inayatambua haya na kukubali kuwa hali ya elimu nchini si nzuri na tunasikia serikali na viongozi mbalimbali wa serikali wakikiri kushuka katika kiwango cha elimu au ubora wa elimu. Lakini tunapaswa na sisi kama wananchi tuendelee kuisukuma serikali kwa kushirikiana na si kuvunjana mioyo na kufikiri kwamba mtanzania anapozungumza anakuwa anakashifu tuu na kukejeli. Hatukashifu, hatukejeli. Tunaguswa na hali ya elimu na tunataka kuona maendeleo katika nchi yetu. Maendeleo katika nchi maskini kama hii, kama alivyosema Mwalimu Nyerere, yataletwa na elimu tu. “Ukitaka kumsaidia maskini mpemwanae elimu”, ndivyo alivyosema Mwalimu Nyerere. HakiElimu kuanzia mwaka ujao, pamoja na mambo mengi tunafikiria kufanya utafiti au tafiti za kina ili kuweza kutafuta majibu sahihi ya baadhi ya changamoto za sekta ya elimu. Na hatutaishia hapo tu, tutaendelea kushirikiana na jamii, wananchi pamoja na serikali, pamoja na Chuo Kikuu au vyuo vikuu vingine mbalimbali kutekeleza baadhi ya map-endekezo yanayotokana na tafiti zetu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mwanafunzi aliyeko darasani anaelimika. Tunapoingia katika nusu ya pili ya karne hii kama taifa inatupasa tusirudie makosa ambayo tumeyafanya nyuma. Tulenge kuandika his-toria mpya katika kuboresha elimu yetu, ambapo vizazi vijavyo vitanufaika na jitihada zetu. Ningependa kuchukua nafasi hii tena kuweza kuwashukuru Chuo Kikuu, cha Dar Es Salaam, hasa UDSTA na kuwa-karibisha tena. Kama alivyosema Rioba, pia nawakaribisha jopo la wataalamu liliopohapa mbele ili waweze kuchukua fursa hii kuweza kuchanganua na kutathmini kadri wanavyoweza. Lakini na sisi ambao tumefika hapa asubuhi hii ya leo tuweze kushirikiana ili tuweze kutathmini kwa pamoja na kutoka na majibu ambayo yatasaidia kuweka historia mpya katika nchi yetu. Asanteni na karibuni sana! * Elizabeth Missokia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la HakiElimu linalojihusisha na harakati za

kuboresha elimu nchini Tanzania

Page 8: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

8

Ubabaishaji wa viongozi ni kikwazo kwa elimu Tanzania Na Jackson Makwetta

[Muhtasari: Mwalisishaji anaiona Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifun-

gua zimefikia lakini, hajifungui. Kwake yeye kudorora kwa elimu nchini kunatokana na Tanzania kuwa na

viongozi wababaishaji, wasemaji wa maneno mengi, wasiotekeleza wanayosema na kukosa ufuatiliaji. Mtoa mada anaifananisha Tanzania na mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefikia lakini, hajifun-gui. Hivyo Tanzania inahitaji kufanyiwa mabadiliko vinginevyo itaendelea kudidimia kielimu na hivyo kiu-chumi. Anaona tatizo kubwa la nchi hii ni serikali kutofuatilia, wala si tatizo la kukosekana kwa sera na kwamba hili ni taifa la wasemaji maneno na siyo taifa la watekelezaji. Sera na mapendekezo mengi yapo lakini hayatekelezwi kwa sababu wahusika hawataki kupata taabu.]

Utangulizi Nikiangalia matatizo yanayoikabili sekta ya elimu nchini, machozi hunilengalenga hasa ku-tokana na kutambua ukweli kuwa ubora wa Taifa lolote lile hutegemea na ubora wa elimu itolewayo kwa watu wake. Maana yake ni kwamba, Watanzania tukitaka kuharibu ubora wa Taifa, letu njia nyepesi ni kuua au kuharibu misingi ya kupatia na kutolea elimu bora. Kwa hiyo Watanzania tukikiuka misingi ya kutolea na kupatia elimu bora misingi hiyo itatukiuka. Kuna wakati Tanzania ikisherehekea uhuru wake, hayati Mwalimu Julius K. Nyerere Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Tan-zania aliulizwa swali lifuatalo na waandishi wa habari kutoka nje ya nchi. “Kitu gani hasa kinawafanya Watanzania msherehekee siku hii ya Uhuru wenu?” Hayati Mwalimu Nyerere aliwajibu kuwa “Watanzania walikuwa wakishereekea siku ile kwa sababu ya kuwa hai hadi siku ile.” Huenda jibu lile lilikuwa sahihi. Hata sisi tungeulizwa swali kama lile leo bila shaka tungejibu kama alivyojibu hayati J.K. Nyerere. Je hali ya elimu nchini ikoje? Kuna wakati nchi yetu ilisifika sana kwa kufanikisha Elimu ya Msingi kwa kutumia njia za kimapinduzi chini ya ushauri wa mzee Nicholas Kuhanga. Wakati huo Tanzania ilitoa Elimu ya Msingi na Elimu ya watu wazima bure kwa watoto na watu wazima wote. Vilevile Serikali ilitoa elimu ya sekondari na ya vyuo vikuu kwa malipo kidogo. Elimu hiyo ilithaminiwa kote duniani. Dosari kubwa katika utoaji wa elimu ya sekondari na ya vyuo vikuu ni kwamba kwa muda mrefu hata baada ya Tanzania kupata uhuru iliendelea kutolewa kwa watu wachache sana. Kinacho-furahisha sasa ni kuwa leo elimu hiyo inatolewa kwa watu wengine zaidi na kwa gharama nafuu zaidi.

Vuguvugu La Ujenzi Wa Shule Na Vyuo Vikuu Na Matatizo Yake Lakini ni katika miaka ya hivi karibuni tu ndipo vuguvugu la ujenzi wa shule za sekondari za serikali, za binafsi na vyuo vikuu lilianza kujitokeza na kusababisha leo Tanzania kuwa na Vyuo vikuu na Vyuo vis-hiriki kufikia 40. Leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaota kama uyoga. Pongezi ziwaendee wanan-chi na wote waliohusika na ujenzi wa shule hizo. Kwa upande wa shule za sekondari watu binafsi wana-jenga shule hizi kwa kutegemea fedha zitokazo kwa wazazi wa watoto na kwa upande wa Vyuo vikuu watu binafsi wanajenga kwa kutegemea mikopo toka Bodi ya Mikopo. Kwa hiyo bila mikopo hiyo Bodi ya Mikopo baadhi ya vyuo vikuu haviwezi kudumu.

Hata hivyo mwamko wa wazazi kupenda elimu umesababisha elimu kupatikana kwa njia za ulanguzi. Shule za binafsi ni za watu wenye uwezo, kama zilivyo hospitali binafsi. Leo shule za serikali ndizo shule za watu wa kawaida. Tatizo jingine linatokana na wamiliki wa shule za binafsi ni kuwarubuni walimu wa shule za serikali ili wajiunge na shule zao na ili kuwapata huongeza mishahara na malupulupu mengine mengi. Matokeo ya kufanya hivyo ni shule za binafsi kufaulisha watoto vizuri kuliko shule za serikali. Leo baadhi ya wazazi wako tayari kupelekea watoto wao katika shule za binafsi hata kama wamecha-guliwa kwenda katika shule za serikali.

Wazazi hawaelewi kwa namna gani shule yenye wanafunzi zaidi ya 300 inaweza kuendelea kielimu wa-kati ikiwa na walimu watatu au wanne tu. Shule tunazo lakini zinakabiliwa na uhaba wa kila kitu (walimu, vitabu, maabara, vyumba vya madarasa, mabweni, matundu ya vyoo, nyumba za walimu, maktaba n.k.) Maneno ya kuzingatia hapa ni UHABA na UKOSEFU wa walimu wa masomo, huduma ya

Page 9: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

9

maji, umeme, zahanati, mabweni, viwanja vya michezo, vifaa vya michezo na kadhalika. Msamiati huu pia unatawala vyuo vikuu, vyuo vya ualimu, shule za elimu ya msingi, vyuo vya ufundi na kadhalika. Ni UHABA na UKOSEFU wa mahitaji katika kila ngazi ya elimu. Shule za sekondari za kata zote zi-nakabiliwa na uhaba na ukosefu wa mahitaji ya shule. Kutokana na UHABA NA UKOSEFU huo elimu inaporomoka KATIKA NGAZI ZOTE. Hii ndiyo hali ya elimu nchini. Watanzania wanaopenda ukweli wanajua ukweli huu. Kazi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni kutafuta ukweli wa mambo. Vyuo visipofanya hivyo vitapoteza umuhimu wa kuwepo kwake. Tume ya elimu ya 1982 inasisitiza suala hili. Naomba wale ambao hawajasoma ripoti ya TUME YA ELIMU ya mwaka 1982 na mapendekezo ya tume yake waisome. Sehemu kubwa ya mapendekezo yale ni muhimu zaidi leo kuliko mwaka 1982. Inasikitisha kuona kuwa Watanzania wengi hatuna muda wa kusoma vitabu au maandishi! Tuna muda wa kufanya mambo mengine! Binafsi naamini kuwa TUME ya 1982 ilifanya kazi nzuri. Wajumbe wa tume ile wengi wao wangali hai. Kwa namna gani wa-nashirikishwa katika kuboresha elimu nchini ni suala zuri la kujiuliza. Kwa tabia ya watanzaia si rahisi kuwashirikisha watu wengine katika mambo yetu. Kwa mfano, Mwalimu Nicholas Kuhanga aliyefanikisha UPE katika nchi yetu kwa nini tu-simshirikishe katika uboreshaji wa elimu nchini? Leo shule za sekondari na vyuo vikuu vinaon-gezeka wakati ubora wa elimu unazidi kupungua. Kwa mfano, katika matokeo ya mwaka 2010 nusu ya vijana wa Kidato cha Nne waliofanya mtihani wa Taifa hawakufaulu. Hata katika miaka mingine, vijana wengi wanafaulu kwa viwango vya chini yaani, divisheni 3 na 4 na idadi ya wale wanaoshindwa mitihani ya mwisho inazidi kuon-gezeka. Hii inaonesha kuwa ubora wa elimu nchini unaporomoka. Labda wengine hawapendi kusikia maneno, kushuka kwa ubora au kuporo-moka kwa elimu. Naomba watushauri tutumie maneno gani. Sisemi kuwa elimu imekufa bali nasema ubora wa elimu umepungua (Vijana wengi kushindwa mtihani wa kidato cha nne ni ishara moja wapo). Pia tathimini iliyofanywa hivi karibuni kuhusu hali ya elimu katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania imeonesha kuwa Tanzania inatoa elimu hafifu kuliko nchi za Uganda na Kenya. Ubishi kuhusu vigezo vilivyotumika katika zoezi hili unaweza kuendelea ila naomba tutenganishe utaalamu na siasa. Kwa mfano, kuna baadhi ya wanasiasa wanapendekeza kuwa mitihani ifutwe katika ngazi fulani za elimu. Lakini hawapendekezi njia gani zitumike katika kupima elimu itolewayo nchini. Hata hivyo sielewi lengo lao nini hasa. Watanzania tukikiuka misingi ya kutolea na kupatia elimu bora, misingi hiyo itatukiuka. Lazima tujiulize maswali yafuatayo kuhusu elimu itolewayo katika nchi yetu: Tunataka nini katika

elimu yetu. Tunataka elimu yetu itatue matatizo gani? Je elimu hii inatatua au inaongeza matatizo? Je,

tunataka elimu ya bure na ya lazima kwa watanzania wote na ifikie ngazi gani? (msingi au ya sekondari

au vyuo vikuu) Je kuna uhusiano gani kati ya maendeleo katika elimu na maendeleo yetu kiuchumi? Je,

kwa namna gani BODI YA MIKOPO itaweza kukidhi mahitaji ya vyuo bila kufanya mabadiliko ya

kimsingi katika sera ya elimu? Kwa nini watoto wa matajiri ambao tangu elimu ya awali, msingi na sekondari wa-

mekuwa wakisoma katika shule za binafsi kwa gharama kubwa leo wanaomba mikopo na serikali inawapa mikopo

hiyo. Tatizo hili halijatatuliwa.

Mmoja wa washiriki akichangia kwa hisis kali katika Kongamano hilo.

Page 10: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

10

Tanzania Imepiga Hatua Kubwa Katika Elimu Lakini Katika makala haya nazungumzia mafanikio na matatizo ya elimu katika miaka 50 ya uhuru wa Tanza-nia. Takwimu kuhusu idadi ya shule, vyuo, walimu, na wanafunzi zinapatikana kwa urahisi kutoka wizara husika. Takwimu hizo zinaonyesha kuongezeka kwa kila kigezo cha kutolea na kupatia elimu nchini. Nashauri tuzitumie vizuri taarifa hizo. Kwa mfano, idadi ya shule za sekondari za serikali ime-ongezeka sana. Halikadhalika, idadi ya walimu wa shule hizo nayo imeongezeka. Lakini vipi uwiano kati ya walimu na wanafunzi katika shule hizi? Ukweli ni kwamba idadi ya walimu ni ndogo kuliko idadi ya wanafunzi na uwezo wa kufundisha wa baadhi yao pia ni mdogo. Kutokana na uchache na uwezo wao mdogo wanafunzi katika ngazi zote za elimu nchini hawapati "dozi" kamili ya elimu wanayotakiwa kupata hali inayosababisha wanafunzi kumaliza elimu wakiwa hawajapata "dozi" kamili ya elimu wanayotarajia kuipata. Kwa hiyo Watanzania tusishangae kwa nini nchi yetu ni ya mwisho katika utoaji wa elimu bora katika Afrika ya Mashariki. Kamwe vijana wetu hawataweza kupata elimu bora ya Msingi au ya Sekondari au Vyuo Vikuu kwa kukaa tu katika majengo yaliyoandikwa "Shule" au Chuo Kikuu. Kamwe vijana hawa-taweza kupata elimu ya ngazi yoyote ile kwa njia ya OSMOSIS (kufyonza). Upatikanaji wa elimu bora una kanuni na misingi yake. Tukikiuka misingi ya utoaji elimu bora misingi itatukiuka. Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya.

Tunapitia Wakati Mgumu Katika Masuala Ya Elimu Watanzania tunapita wakati mgumu kiasi kwamba hata kubaki hapa tulipo ni kazi ngumu, kurudi

nyuma ni kazi rahisi, kwenda mbele ni kazi ngumu zaidi. Breki za gari tulilopanda hazishikiki. Kuna

hatari ya gari kurudi nyuma. Gari hili ni nchi yetu Tanzania. Nchi ikirudi nyuma tutapoteza hata

mafanikio kidogo tuliyoyapata katika miaka 50 ya uhuru. Hali inazidi kuwa mbaya. Vyanzo vya maji

vinakauka, nchi inakosa umeme, gharama za huduma muhimu zinazidi kupanda, vijana wanakosa ai-

jira na nguvukazi yao haitumiki.

Maana yake ni kwamba mapendekezo yoyote ya kuboresha elimu lazima pia yaonyeshe nchi itapata

wapi fedha ya kufanyia kazi hiyo? Kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa ushuru na kupunguza

rushwa, Tanzania ingeweza kupata fedha za kutosha kuboresha elimu yake. Fedha ipatikanayo kuto-

kana na ushuru wa misululu ya magari makubwa yaendayo Zambia, Malawi na Congo kila siku

inatumikaje? Aidha, watu wamepata wapi fedha ya kununua utitiri wa malori, magari madogo na

mapikipiki yanayosababisha barabara zisipitike katika miji yetu?

Pamoja na umaskini wetu lazima Watanzania tujue kuwa maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe

kwa bidii, maarifa, nidhamu, na kwa kuijitegemea. Ingawa Serikali ina uwezo mkubwa wa kutunga

sheria na kuweka taratibu za kusimamia uchumi lakini haina uwezo wa kusimamia taratibu zake. To-

fauti na nchi zenye serikali imara kama Marekani ambazo zimeweza kusimamia uchumi wake Tanza-

nia imeshindwa kufanya hivyo.. Kwa mfano serikali bila kupanga imekabidhi uchumi wa Tanzania

kwa watu wachache ambao inashindwa kuwatoza kodi. Kwa nini tusichukue hatua zifuatazo:-

Tulipe kodi na ada za shule kwani kujitawala ni kujitegemea.

Tufufue au kutilia mkazo siasa na Elimu ya Kujitegemea.

Tuchangie gharama za maendeleo kwa kufanya kazi ndogondogo za mikono.Mathalani kwaa nini kazi ya kufyeka nyasi katika shule isifanywe na wanafunzi?

Tusimamie vizuri shughuli zote za maendeleo ili kuzuia ufujaji wa fedha.

Serikali isimamie elimu itolewayo nchini ili kuondoa ulanguzi utapeli na uchakachuaji.

Tanzania Commision for Universities (TCU) iongezewe madaraka zaidi kuhusiana na vyuo vikuu. Tuongoze ufanisi katika kazi zetu na kupenda kufanya kazi.

Page 11: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

11

Tubane matumizi na kutumia vizuri kila senti tunayopewaau tunayoipata.

Tuache rushwa, ufujaji mali na uvivu.

Tupunguze sherehe, tafrija, mikutano, semina na kongamano zisizo na umuhimu kwa ustawi wa taifa letu. Mathalani tupunguze michango ya starehe kama vile inner party, send-off, bag party, kitchen party na wedding party. Badala yake tuanzishe michango ya maendeleo kama vile ya elimu n.k.

Aidha inatufaa tutumie vizuri wakati

Tupunguze migomo badala yake tujue kwa undani sababu ili kama ni uzembe hatua kali ziwe zinachukuliwa kwa wa-husika mapema.

Idadi ya wanafunzi wa kwenda vyuo vikuu ijulikane mapema. Kama idadi ya wanafunzi wa kwenda vyuo vikuu huwa haijulikani hadi mwezi mmoja kabla ya vyuo kufunguliwa tunategemea nini kama si migomo na tafrani nyingine?. Inatu-pasa tujisahihishe. Tubadili mwelekeo wetu au mtazamo wetu kuhusu umuhimu wa mambo (mind set). Kwa mfano itawezekanaje kuon-geza ubora wa elimu bila kuwashirikisha wananchi katika gharama hizo? Kama kuna wakati mzuri wa kubadili mambo au kufanya mapinduzi katika elimu basi wakati huo ni sasa. Hii ni kwa sa-babu mwamko wa watu wa kuelewa maana na umuhimu wa kutoa elimu kwa watoto wao umeongezeka. Matatizo ni mengi, na hakuna nchi isyo na matatizo.kilicho muhimu ni kuanza kuchukua hatua thabiti za kuanza kuyashughulikia

Elimu kwanza : Inaeleweka treni la elimu liko nje ya reli Inaeleweka kuwa treni la elimu liko nje ya Mifano iko mingi. Katika baadhi ya shule za Elimu ya Msingi bado baadhi ya

wanafunzi wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika na nusu ya wanafunzi wanaomaliza kidato cha

nne wanafeli mtihani wa mwisho. Hii ina maana wanamaliza elimu ya msingi bila elimu ya msingi wataendeleaje mbele?

Ni Elimu gani hii ambayo haimwezeshi mwanafunzi kuwaelezea watu kile anachokijua au kubuni na kuibua mambo, ku-

fikiri kisayansi, au kupeleleza na kuchambua mambo, kuumba vitu, kutafuta njia sahihi za kutumia katika kutatua matati-

zo yake. Tukubali kuwa elimu yetu ni butu. Tofauti na wenzao walioachwa nyuma baada ya kumaliza elimu ya Msingi

hawa hawawezi kulima, wala kupalilia mimea isipokuwa kupiga simu, kupiga stori, kukaa vijiweni, kuzurura mitaani na

kucheza disco. Lakini ajabu ni kwamba vijana hawa wanataka makuu, wanataka wakipanda mahindi asubuhi wavune jio-

ni. Mara wakianza kazi wanataka kuwa na simu pana, gari la kuendea kazini na nyumba nzuri ya kuishi. Pale wanapokosa

vitu hivi hupauka akili na huwafanya wafanye yasiyotegemewa. Vijana hawa ni wengi na wanaongezeka kila mwaka. Seri-

kali isipowatumia vijana hawa watu waovu watawatumia. Swali la kujiuliza ni je watanzania tunawezaje kulirudisha treni la

elimu yetu katika reli yake?

Haja Ya Kutumia Uzoefu Ulioko Nchini Duniani hakuna kidumucho isipokuwa mabadiliko. Watanzania wana haki ya kupata kilicho bora katika nchi yao ikiwa ni pamoja na kuwatumia watumishi bora waliostaffu na vijana wenye akili kwa faida ya nchi yao. Tabia ya kuwatenga au ku-towatumia watu hawa ni tabia mbaya inayodidimiza nchi yetu. Kuwatenga watu kwa sababu za kisiasa au kwa sababu ya kuwaogopa au kwa sababu ya roho mbaya ni ufisadi wa aina yake. Wenzetu huko Ulaya ambako tunaiga mambo mengi wanafanya hivyo. Si vema kwa baadhi ya Watanzania kuonekana hawatakiwi au wanaishi kwa hisani ya watu fulani. Wale wenye uwezo au madaraka wanaweza kumuua, kumtesa au kumtenga raia yeyote kwa sababu zozote zile ila hawawezi kumnyang‟anya utaifa na uraia wake.Hawawezi kumfukuza katika nchi yake. Tume ya Elimu ya Mwaka 1982 chini ya uenyekiti wangu ilichambua hali ya elimu iliyokuwa ikitolewa wakati ule hapa nchini. Pia ilitembelea nchi nyingi zilizoendelea na zisizoendelea ili kujifunza taratibu zao za utoaji elimu. Tume ilijifunza mengi na kutoa mapendekezo kwa serikali. Ni muda mrefu umepita (1982) tangu iwasilishe Ripoti yake. Kama serikali inatekeleza au haitekelezi mapendekezo ya Tume mimi sina la kufanya. Kinachonishangaza ni kuwa tangu nitoe Ripoti ile sijawahi kuitwa wala kuulizwa lolote na Wizara husika kuhusu elimu isipokuwa ninyi (HakiElimu) leo. Kwa maoni yangu hii ni kasoro kubwa katika nchi yetu. Nchi haifaidiki na utajiri wa uzoefu wa watu walio nje ya mkondo wa serikali kwa sababu zisizoeleweka (wastaafu wataalamu kama majaji, wanajeshi, walimu, mawaziri hawatumiki). Watu hawa ni hazina ya nchi na si tishio kwa yeyote. Nchi hii ni yetu sote. Tusiwaenzi watu waliostaafu baada ya kufa kwa kuhudhuria mazishi yao tu. Tusisubiri watu wafe ndiyo tuseme mazuri yao.

Page 12: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

12

Baadhi Ya Vikwazo Vilivyo Mbele Yetu

Huenda mapendekezo ya Tume ya MAKWETTA sasa yamepitwa na wakati. Hofu yangu ni kwamba kama nilivyokwishatamka hapo awali, tangu Tume ile itoe mapendekezo yake kwa serikali sijawahi kuitwa kutoa ushauri au ufafanuzi wowote kuhusu mapende-kezo ya Tume ile. Napendekeza iundwe Tume ny-ingine kwa madhumuni yaleyale ili kukidhi mazingira ya Karne ya 21. Tusichezee elimu madhara ya uharibifu yatakuja jitokeza miaka michache ijayo. Hapa chini natoa mapendekezo lakini mapendekezo haya yatafanikiwa tu kama baadhi ya mambo yaliyoko yatabaki kama yalivyo. Mabadiliko katika baadhi ya mambo yaliyoko leo yataathiri nguzo muhimu za ku-tolea na kupatia elimu. Kwa hiyo mapendekezo yoyote kuhusu mabadiliko katika mfumo wa elimu nchi nzima yazingatie mambo yafuatayo:-

Kuongezeka kwa idadi ya watu ambako kutasa-babisha kukua kwa umaskini.

Kuweko kwa watu wenye uzoefu na kutotumia uzoefu wao.

Kupungua au kukosekana kwa maji yanayohitajika na binadamu, wanyama na mimea (ukame) kutokana na sababu mbalimbali.

Kuongezeka kwa milipuko ya magonjwa ya hatari na vifo.

Kuharibika na kuchafuka kwa mazingira (mito na vijito vyote kukauka).

Kushuka kwa uchumi kutokana na kupungua kwa mafuta, gesi, maji, madini na kadhalika.

Uhaba au kukosekana kwa chakula (njaa).

Kukua kwa umasikini na kukosekana kwa amani.

Kukosekana kwa ajira na kutotumika kwa nguvu kazi.

Kustawi kwa rushwa na utawala mbovu.

Ubaguzi wa kipato (maskini na matajiri) na wa rangi. (Mathalani watu weusi kuzuiwa kwenda Ulaya).

Kurudi kwa ukoloni na utumwa mambo leo

Wenye navyo watashika uchumi i na utawala wa nchi

Kustawi kwa ukoloni mamboleo.

Nchi itageuka nchi ya ombaomba. Kesho ni leo na leo ni kesho. Kwa hivo kila jambo tufanyalo au tusilofanya leo linajenga au kubomoa misingi ya maendeleo yetu ya kesho. The future is now.

Hatua Za Kuchukua Ili Kuzuia Kasi Ya Kuporomoka Kwa Elimu Nchini Kobe kufanya maendeleo pale tu anapothubutu kutoa shingo yake nje ya gamba lake. Kwa hiyo pamoja na yote yanayo-semwa kuhusu elimu, ni vigumu sana kutabiri kuhusu mambo yatakavyokuwa kesho. Labda tutumie ujuzi na uzoefu wetu katika kuelezea baadhi ya viini vya matatizo katika shule na vyuo vyetu:- Wizara ya Elimu iunde haraka Tume ya Elimu ili kutizama matatizo ya elimu na mwelekeo wake kwa lengo la kuzuia

Tanzania kuachwa nyuma kielimu au kuzuia kuporomoka kwa elimu.Serikali isimamie na kuratibu elimu katika ngazi zote

ili kuzuia biashara na ulanguzi katika elimu chini.

Mazingira ya kuishi kwa walimu wengi bado ni changa-

moto kubwa

Page 13: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

13

Kutokana na uwezo mdogo wa walimu hasa walimu wa shule za sekondari, yaanzishwe mafunzo ya kuboresha elimu yao wawapo kazini yaani in service training for teachers (INSET)).Serikali itizame upya sera ya kugharamia elimu nchini ili kuhakikisha kuwa fedha ya umma inatumika vizuri na inatolewa mapema kwa wahusika. Hatua za kuboresha elimu zian-zie katika vyuo vya ualimu, vyuo vikuu na shule za msingi na mafunzo kazini. Sekta ya ukaguzi iimarishwe kwa kuongeza wakaguzi na vyombo vya usafiri. Migomo shuleni na vyuoni inaathiri sana maendeleo ya elilmu nchini pamoja na kuharibu mali ya umma. [Sera ya Mikopo bado hafifu] Wanafunzi washirikishwe katika kubana matumizi shuleni na vyuoni kwa kufanya kazi ndogondogo zisizopoteza muda wao mwingi. Wanafunzi wajihusishe na ubora na usalama wa mazingira ya shule na vyoo badala ya kubaki na ‘3Ks’ tu yaani KUSOMA, KULA NA KULALA. Wanafunzi washiriki katika masuala ya usafi, usalama na maendeleo ya shule au vyuo vyao. Taarifa kuhusu uwezo wa wazazi wa watoto kiuchumi zijulikane mapema. Wazazi wenye uwezo kiuchumi wanapaswa kulipa ada yote katika vyuo vikuu ili kupunguza kuelemewa kwa serikali katika suala hili.Udhaifu wa serikali usielezwe kwenye vyombo au taasisi zisizohusika (BODI YA MIKOPO) na utoaji wa huduma fulani muhimu. Ziundwe BODI ZA ELIMU katika ngazi za wilaya ili kusaidia Wizara ya Elimu kusimamia kwa kuwahusisha wadau wote wa elimu Wilayani.Serikali itizame upya sera kuhusu lugha ya kufundishia shuleni na vyuooni. Lugha ya “Kiswanglish ” inayo-tumika leo shuleni inaathiri elimu. Leo Kiingereza ni Kiswahili cha dunia! Serikali iwe na utaratibu wa kuendelea kuwatumia walimu waliostaafu (Sera au Mwongozo). Ili kukabiliana na tatizo la kumomonyoka kwa maadili shuleni, liingizwe somo la Maadili katika ngazi zote za kutolea elimu nchini.Itolewe tafsiri sahihi kuhusu maana ya shule na mahitaji ya lazima ya shule, au chuo. Shule au chuo ni pamoja na majengo, walimu bora na wa kuotsha, vifaa bora vya kutosha n.k. Sera ya elimu ya nchi iwe wazi katika ngazi zote. Je ni kutoa elimu ya bure kwa watoto wote kuanzia Elimu ya Awali, Msingi (UPE) elimu ya Sekondari (USE) na ya vyuo vikuu (UUE) na kadhali-ka ?

Hitimisho Hakuna kidumucho isipokuwa mabadiliko. Kama elimu bora ni ufunguo wa maisha bora basi elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya. Hebu tujiulize watanza-nia: Je, Elimu itolewayo nchini mwetu ni ufunguo wa maisha bora au ni ufunguo wa matatizo? Je, vijana wetu wanasoma kwa malengo? Je, elimu itolewayo nchini inakidhi malengo yao? Kama haikidhi kwa nini umma wa nchi hii uendelee kugharamia elimu isiyo na manufaa? Kama shule na vyuo vyetu havifundishi kufikiri, kudadisi haviumbi kazi bali vinaiba tamaa ya kupenda starehe na kazi nyepesi, chanzo ni nini?. Tatizo kubwa la nchi hii ni serikali kutofuatilia, wala si tatizo la kukosekana kwa sera. Hili ni taifa la wasemaji maneno na siyo taifa la watekelezaji. Mapendekezo ya Tume ya MAKWETTA ya mwaka 1982 licha ya kukubalika na serikali yame-wekwa kabatini. Hayatekelezwi kwa sababu wahusika hawataki kupata “taabu” ya kuyatekeleza mapendekezo yake. Baada ya kuyachambua tena Rapendekezo ya ripoti ya TUME hiyo mimi naona bado yana manufaa hadi leo. Sasa naelewa kwa nini Karl Marx. alisema matumizi ya nguvu ni lazima kwa mama aliyefikia siku za kujifungua. Kwa ma-

neno yake Lenin alisema „Force is the midwife of every old society pregnant with a new one” Kwa maoni yangu Tanza-

nia ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefika lakini hajifungui. Bila kumpasua mama, wote wa-

wili : mama na mtoto watakufa. Kwa hiyo : Mama akipasuliwa wote wawili wanaweza kuokolewa (au mmoja wao). Tan-

zania inahitaji kupasuliwa la sivyo itaendelea kudidimia kiuchumi milele.

Nchi ya Tanzania inahitaji kiongozi shupavu mwenye msukumo, mwenye akili na siyo mkusanyaji au mlafi, mwaminifu, mchapakazi mpenda haki na anayeona mbali (a visionary leader). Rushwa na utawala usiothubutu ni tatizo. Tanzania ni kama mjamzito: Inahitaji kuwa na kiongozi atakayethubutu kuipasua ili kuwaendeleza watanzania kiuchumi Jackson Makweta Waziri wa zamani wa Elimu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Tanzania.

Page 14: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

14

Miaka 50 ya Uhuru: Tanzania haina mengi ya kujivunia kielimu

Na Profesa Herme Mosha*

[Muhtasari: Kutokana na changamoto lukuki zina-

zoikabili sekta ya elimu hapa nchini Profesa Mosha anaona ha-kuna la kusherehekea katika miaka 50 ya elimu zaidi ya ongezeko la shule za kutoa elimu. Anaona kuwa Tanzania haina matatizo ya kisera katika sekta ya elimu. Shida iliyopo ni namna ambavyo sera hizo hutekelezwa. Anapendekeza kuwa Sera zinapoandaliwa watekelezaji nao waandaliwe ili kuweza kufikia malengo ya utekelezaji.]

Kama Mwenyekiti alivyosema mimi nina bahati mbili. Kwanza, nimefaidika kupata elimu ya kikoloni na elimu baada ya uhuru. Tulipata Lakini nataka kuanza kwa kusisitiza kwamba elimu ni jambo muhimu sana katika taifa lolote linaloendelea. Na napenda kuchukua elimu kama ndio muhimili mu-himu wa maendeleo kwa hivyo unavyochezea elimu au

unapotoa elimu isiyo bora basi mambo mengine yote katika nchi hayawezi kuwa bora. Kuanzia kilimo, siasa uchumi na vitu kama hivyo; na napenda kulisisitiza jambo hili. Pili napenda kueleza pia kwamba, kama alivyozungumza Mwenyekiti wenu, siku 13 tu zijazo tutakuwa tunasherehekea uhuru wa nchi yetu. Kweli kutakuwa na mlolongo wa mambo mengi mazuri ambayo tumefanikiwa katika elimu, na wa-nasiasa nadhani watatoa mlolongo mrefu sana wa mafanikio hayo. Lakini mimi ningependa niwashauri kwamba wanapo-tengeneza hotuba zao watumie pia data ambazo zinatengenezwa na Wizara yao pamoja na taasisi zao kwa sababu tunapozungumzia ubora, kuna mengi ambayo siyo bora kama tunavyodhani, na Mkurugenzi wa taasisi ya HakiElimu ali-yazungumzia baadhi ya hayo. Tutakapokuwa tunasherehekea miaka hiyo hamsini ya uhuru tutakuwa na mengi ya kusherehekea. Lakini mimi sina mengi sana ya kusherehekea katika upande wa elimu. Nina sababu zangu nyingi na baadhi ya hizo sababu zinapatikana hapa. Napenda nitofautishe kujenga shule na kutoa elimu. Kwa sababu unaweza ukajenga shule nyingi sana ukadhani umetoa elimu. Pia naomba nitofautishe ile dhana ya kwamba unapodahili tu watu basi unakuwa umetoa elimu. Asilimia 50 ya wanafunzi wanaomaliza shule za msingi wanafeli, data zipo. Asilimia chini ya kumi ya wanafunzi wanaomaliza O Level wanapasi katika daraja la kwanza na la pili. Ukiongeza na la tatu unabaki na asilimia 20. Wale wengine wako divisheni 4 na wengine wanapata divisheni zero. Ukiangalia katika uwanja wa elimu ya ualimu, karibu asilimia 80 ya walimu na zaidi wa shule za msIngi wamepata divish-eni 3, 4 na huenda ukakuta kuna wengine ambao wamechakachua . Ndiyo maana mimi nataka kusema kwamba sawa tumetoa, tumepanua elimu lakini katika kuelimisha taifa bado tupo nyuma sana. Hao watoto ambao tunawatoa wakiwa na nusu ya elimu wanapatarobo au kutokuwa na elimu kabisa.Hii ni kwa sababu unapokuwa na divisheni 2,3 na 4 ndiyo unaanza ule urobo au kutokuwa na elimu kabisa. Kwa sababau unapata maksi kati ya 30 na 40 ; au 20 na ngapi au wale wanaopata divisheni zero ndiyo hamna kitu kabisa.. Kwa hiyo lazima tuangalie huo upungufu. Lakini hatuwezu kuuelewa huo upungufu bila kwanza kujikita katika sera

mbalimbali za elimu. Na kutokana na bahati kwamba kuishi muda mrefu ni kuona mengi, basi nitajaribu kuangalia baadhi

ya sera za elimu ambazo zilipitishwa hapa nchini kuanzia mwaka 1961 mpaka 67 ambapo tulikuwa na ile sera ya kuondoa

ubaguzi katika nyanja mbalimbali za elimu pamoja na ubapanuzi.

Page 15: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

15

Hii sera ilikuwa ni nzuri sana; lakini tulifanya the first technical error katika elimu. Kosa hilo lilikuwa ni lile la kutupa jon-goo na mti wake. Ni kwamba tulikuwa na elimu ambayo ingeweza ikasaidia kijana akajua kusoma, kuandika kuzungumza na kujieleza na stadi zote za kazi. Mimi hapa nilipo hakuna civil engineer anayenibabaisha, hakuna field officer anay-enibabaisha. Wakati mwingine watu wananiuliza, “Profesa nadhani ungepaswa kuwa civil engineer na siyo mwalimu.” Lakini nawaambia pia wataalamu wa kilimo wanasema kuwa ningepaswa kuwa mwanakilimo na siyo mwalimu. Lakini pia katika ualimu nako natamba. Hii ni kutokana na elimu tuliyopewa wakati ule. Lakini tulibadilisha na tukaiweka pembeni na hasa tulipoingiza Education for Self-Reliance 1967. Lengo lilikuwa ni zuri sana lakini hatukuweka mazingira ya kufaa kwa walimu, madarasa na miundombinu ya kutekeleza elimu hiyo. Kwa sababu yale makosa tuliyofanya mwaka 1967. Walimu walianza kutawanyika, baadhi ya yale majengo tukabadilisha kuwa vitu vingine na vitu kama hivyo. Hata hivyo, sera nyingine ambazo zilifuata, ambazo ni muhimu kuzifahamu, ni ile sera ya mwaka 1974. Na katika hii sera kulikuwa na mambo matatu au manne ambayo yalizungumziwa. Kwanza, ni kutoa elimu ya msingi kwa wote. Wataalamu tulishapendekeza au walishapendekeza kwamba lengo hilo li-fikiwe mwaka 1989. Lakini Mwalimu (J.K. Nyerere) kwa nia nzuri kabisa akasema hapana watu wameanza kuishi pamoja vijijini ni lazima tulisogeze mbele lengo hili na elimu hiyo iweze ikapatikana ifikapo mwaka 1978. Kwa hivyo, kulikuwa na mipango ya haraka ambayo ilitusaidia Tanzania kuweza kufikia a hundred percent realization ya UPE. Lakini hiyo ilizaa mata-tizo kadha wa kadha tunayoyaona katika mfumo wa elimu siku hizi. Wale walimu wa Grade C waliongezeka sana na seri-kali haikuwa makini sana katika kuwachagua wakati huo. Japo sera zilizofuata, kama ilivyopendekezwa na Tume ya Elimu ya Rais ya Mheshimiwa Jackson Makweta ya mwaka 1982, kwamba hawa waondolewe lakini bado waliendelea kubaki katika mfumo wetu wa elimu. La pili, katika ile sera ya 1974 kuliingizwa pia kitu kinachoitwa kuoanisha elimu na vitendo. Kwa hivyo ilikonekana kwamba lazima elimu tunayotoa iendane na vitendo. Chuo Kikuu utaratibu wa kuwapokea watu moja kwa moja kutoka mashuleni ulisitishwa. Ikalazimika kwanza lazima ufanye kazi ndipo ujiunge na chuo kikuu ili ukija hapa uwe ni mtu mzima na siyo kijana tena. Lakini kutokana na matatizo yaliyojitokeza hapo baadaye, sera hii nayo ilibadilishwa. Kwa hivyo katika sera, Mheshimiwa Makweta yeye alipendekeza mambo mengi sana, hasa kubadilisha mfumo wa sasa wa elimu tulionao wa seven, four, two,three kuwa eight, four, four. Alipendekeza kwamba walimu wa daraja la chini waondolewe. Pia alipendekeza kwa mara ya kwanza kuwe na uchangiaji katika gharama za elimu na kuwe na partnership kati ya serikali, wazazi pamoja na wale wanaopata elimu. Pia ilipendekeza haja ya kuwa na ushirikishwaji katika elimu na mambo kadhaa wa kadhaa. Ukizungumza na Mzee Makweta anakueleza kwamba alitoa mapendekezo mazuri sana; na mimi nakubaliana naye. Lakini sisi wataalamu wa sera tunatamka wazi kwamba sera haiwezi ikajitekeleza yenyewe. Lazima kuwe na mikakati madhubuti ya kutekeleza sera hiyo. Kwa hivyo, ripoti yake bahati mbaya toka 1982 mpaka 1989 iliwekwa kwenye shelf, haikutekeelzwa. Bahati nzuri mwaka 1989 kukawa na waziri, marehemu Amran Mayaqgila, ambaye alikuwa ni mtaalamu wa mipango. Akaona kuna haja ya kuitekeleza lakini, siyo kuitekeleza ilivyokuwa bali iboreshwe na kuandaliwa sera ya elimu kwa karne ya ishirini na moja. Basi walidodosa na bahati nzuri au mbaya wakamnasa mzungumzaji wa sasa hivi. Wakamfanya kuwa mwenyekiti wa ku-fanya kazi hiyo. Tulikuwa wajumbe 14 na tulitoa mapendekezo kadhaa wa kadhaa. Na baadhi ya mapendekezo muhimu ambayo ningependelea kuyazungumzia hasa ni lile la kujaribu kutoa elimu ya msingi kwa wote. Hili tulitoa pendekezo linalohusiana na kuondoa vikwazo vyote vinavyowazuia wale wanaostahili kupata elimu wasipate elimu. Tulipendekeza pia kwamba, ugharamiaji wa serikali katika elimu uongezwe hadi kufikia asilimia 30 ya bajeti ya taifa au asilimia 2.5 ya Pato la Taifa. Na kuanzishwe aina nyingine za elimu. Lakini ilivyokuwa kuwa hii ripoti haingeweza ikajitekeleza. Kwa hiyo sisi tulishauri mambo mawili. Kwanza, kuwepo na sera mpya ya elimu, ambayo ni ile sera ya 1995. Baada ya sera hiyo kuwe na mpango kabambe wa elimu, ambayo ni ESDP ya 1997 ambayo ilifanyiwa tathmini mwaka wa 1999 na ilipofika mwaka 2001 wakati huo basi tukawa tuna mpango kabambe wa elimu.

Page 16: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

16

Napenda nitamke bayana kwamba mipango mingi ya elimu tunaiona sasa hivi imetokana na huu mpango kabambe. Kwa mfano MMEM, MMES, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ualimu na Mpango wa Elimu ya Juu. Basi niliendelea ku-shirikishwa katika baadhi ya hii mipango,na kuwa mwenyekiti katika mipango mitatu kati ya hiyo minne ambayo tunai-zungumzia. Sasa kitu ambacho ningependa kuzungumzia zaidi ni kwamba, Tanzania kisera hatuna matatizo. Matatizo katika elimu mengi yameshaainishwa. Lakini, tatizo lipo katika utekelezaji, na utekelezaji unatiwa dosari na mambo kadha wa kadha. Kwanza ni bajeti yetu. kiangalia katika kitabu hiki pia kinaonesha trend,; kuwa hakuna wakati wowote ambao tumevuka

asilimia mbili ya pato la taifa ambalo tunawekeza katika elimu.

Pili, ni tabia ya kuendelea kuzungumzia matatizo ya uchumi wetu bila kuyapatia ufumbuzi. Kwa mfano, kama bajeti ni finyu. Nakumbuka kuna kipindi fulani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitwataka viongozi wetu wahakikishe kwamba wanakusanya kodi kwani bila kodi huwezi ukapata maendeleo. Sasa swali la kwanza naelekeza kwa wasomi wenzangu, pamoja na wanamdahalo. Hapa chuo kikuu kuna schools mbalimbali. Nngekuwa katika school moja ningemuendea mheshimiwa rais wenu nimuambie naomba deal.i, Angeniuliza deal gani? Ningemwambia kwanza ukinipa ruhusa nikakusanya kodi , nikaongeza makusanyo ya kodi kutoka asilimia fu-lani kufikia asilimia fulani mimi utanipa retention gani?. Hizi siyo za kuweka mfukoni, isipokuwa za kuendesha shule yangu na pia kusaidia wale wanafunzi ambao hawana uwezo, wakawa na uwezo wa kuchangia elimu. Ukienda huko mjini utakuta kwamba kodi nyingi, nyingi sana hazilipwi; madukani, kodi za nyumba, kodi za bidhaa mbalimbali na vitu kama hivyo. Lakini wataalamu wote wa kodi tunawatoa hapa chuoni. Kitu kingine, ni kwamba kuna vitu vingine tunapaswa kusema hapana. Havipaswi ku-wepo tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru. Naomba nivitaje vitatu muhimu. Mimi sitasherehekea kukaa chini kwa wanafunzi katika shule zetu na hakuna sababu ya hao wanafunzi kukaa chini katika shule zetu, hiyo mosi. Ukitaka fedha zote hasa mjini ongeza bei ya petrol, ongeza bei ya bia ki-dogo wakishamaliza futa hiyo kodi. Pili, kitu ambacho sikisherehekei ni kuwa na madarasa yenye wanafunzi mia moja mijini hasa katika shule za misingi. Ukienda shule zile kubwa za sekondari, am-bazo baadhi ya walimu na wanafunzi wako hapa, staff hukaa kwenye korido. Mimi hilo silisherehekei. Tatu ni utekelezaji wa kiholela wa baadhi ya miradi ya elimu. Tuna fedha, lakini inapofika kutekeleza miradi, unakuta hii miradi inatekelezwa kiholela. Watu wanatengeneza matofali hamsini kwa mfuko mmoja wa saruji. Kwa hivyo, wanaingiza fedha nyingi sana lakini tunapaswa kujiuliza: je, fedha tunazowekeza katika elimu zinatumika ipasavyo ama vipi?. Jambo jingine ni kuhusu uongozi wa elimu. Nadhani kuna changamoto moja kubwa. Rais Kennedy alipoulizwa na

baadhi ya wananchi wake wewe ni Rais utatufanyia nini, yeye alibadilisha kibao akawauliza nyie kama mtu mmoja mmoja

mtalifanyia nini taifa?

Na mimi nataka kuwauliza swali hilo wote mlioko hapa sisi pamoja na uongozi wa elimu na wa kisiasa tutaifanyia nini

Tanzania ili iweze ikatoa elimu bora kwa wananchi wake?. Sina jibu lililoandikwa kwenye uso wangu lakini tunaweza tu-

kalipata. Kwa sababu kuna tabia siku hizi nadhani viongozi wengi hawajiulizi wanapokaa ofisini. ni alama zipi ama foot-

print zipi nitaziacha baada ya kutoka madarakani kama mchango wangu katika elimu. Badala yake wanaanza kujiuliza ni

nini nitakachopata kwa kuwa madarakani kwa kipindi fulani.

Page 17: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

17

Jambo jingine ni ubora wa elimu. Na hili nisingependelea kulizungumzia zaidi kwa sababu najua kwamba mmoja wetu atalizungumzia. Lakini pia kuna haja ya kufikiria ubora wa wanafunzi wanaochaguliwa kwenda sekondari, kwenda A level na kuja chuo kikuu. Ukiangalia hizi data, lile ziwa ama pool ambalo tunapaswa kuwavua hawa hawako wengi. Sasa tunapomchukua mtu ambaye ana sifa ambazo hazikutosheleza tumfanye nini ili aweze akafikia zile sifa ambazo tunazita-futa. Pia kuna suala la mitaala; nadhani tumekuwa tunachezea chezea mno mitaala yetu. Tunabadilisha mitaala katika mashule yetu bila ya maandalizi muhimu ya walimu, bila ya maandalizi ya vifaa na bila kuwatayarisha hao walimu, waweze ku-tekeleza vyema baadhi ya hii mitaala. Na mimi sitashangaa mwaka huu kwa sababu wanafunzi wameanza kutahiniwa katika utekelezaji wa mtaala mpya. Sitashangaa kama hali itakuwa mbaya zaidi kuliko mwaka jana. Kwa sababu viashirio vyote vipo vinaanza kujitokeza. Pia, kuna haya ambayo yameanza kujitokeza ambayo nadhani ni muhimu kuyaangalia, Ukiangalia katika ufaulu, wengi wa wanafunzi wanaofaulu sasa hivi wanatoka hasa katika shule za private. Kwa hivyo, tuwe makini tunakokwenda, tusipo-kuwa makini katika kusahihisha suala hili, tutakuta hii nchi inatawaliwa na watoto wale wale wa walio nacho; na hao wen-gine kuna kila dalili ya kuweza kuachwa bila kupata elimu ya kutosheleza. Mwenyekiti, napenda nisisitize mambo mawili kabla sijamaliza. Kwanza, lazima tuweze kutaja bayana, tunapozungumzia shule ni nini au chuo kikuu ni nini. Siyo majengo makubwa ya mihadhara wala sio majengo ya shule. Hiyo peke yake hai-toshelezi. Lazima tujiulize ili kitengo chochote kile kiweze kikaitwa shule kinapaswa kuwa na sifa gani? Walimu, mada-rasa, vifaa, maabara na kadhalika. Je, siku ya leo shule zina hadhi hizo? Ukipita katika nyingi ya hizi shule tunazoziita shule sio shule. Kwa nini tunaendelea kubaki na institutions kama hizi?. Mwisho mwenyekiti napenda kusema kwamba pale awali Mkurugenzi wa HakiElimu alitoa dukuduku moja ambalo ni muhimu. Nchi hii hatuwezi tukabadilika bila kuyakubali mabadiliko na mabadiliko yanahitaji ujasiri mkubwa. Mimi nime-sikia sana mambo ya kujivua gamba lakini mimi nisingependelea mambo ya kujivua gamba. Lakini tumekuwa na tabia ya ambayo nilipokuwa nazungumza na mzee Makweta aliniambia hili lazima ulizungumze. Tumekuwa na tabia ya kuwa kama kobe. Kobe akipata matatizo yeyote yeye mara moja anarudisha kichwa ndani. Tunapofanya hivi tunajinyima uhuru wetu wa kutafakazi na kuuliza maswali magumu pale ambapo mambo hayaendi sawasawa. Kwa hivyo, ningeomba tuache hizi tabia za kobe. Chuo hiki kilisifika sana katika miaka ya nyuma. Sababu chuo hiki kilikuwa na dini tatu kuu. Ijumaa Uislam; Jumamosi Usabato; Jumapili Ukristo na Ideological classes. Kulikuwa watu wanaaamini hata kama ni wakristu hawaendi kanisani isipokuwa wanakwenda kwenye vyumba vya mabwalo kama haya wanaanza kuchambua kila kitu na kukitolea mapende-kezo. Na hayo mapendekezo yalikuwa yanaifikia serikali na serikali inayasikia. Napenda kutumia pia mfano huu kwa sababu siku za karibuni niliona kuna tabia ambayo inaanza kujengeka ya woga.

Mimi nina ofisi pale karibu na Nkrumah. Vijana wawili wa FFU wananyanyua fimbo wanawakimbiza vijana mia mbili na

kuwaingiza katika crisis. Mi nasema tunapaswa kusema hapana. Kama ana nguvu ya hoja atueleze. Twende Revolutionary

square anibadilishe mawazo tukubali. FFU watano wanakuja watu elfu moja wanakimbia! Mna nafasi ya kuwaambia ha-

pana chuoni si mahali pa kupiga mabomu!

Pia katika siasa na serikalini kuna watu wachache wanadiriki kusema kwamba sisi ndio wenye kauli katika elimu na katika maendeleo ya elimu hata kama mawazo yao siyo sawa. Tuache vichwa vyetu nje. Sisi si kobe na katika baadhi ya mak-abila wanasema ukipata bahati ya kukuta kobe anatembea kichwa kiko nje basi siku hiyo ina bahati. Hivyo tuweze ku-hakikisha kwamba tunajadili kwa kutumia nguvu ya hoja matatizo yote yanayokabili elimu ya nchi yetu na kuweza kuya-patia ufumbuzi. Asanteni sana. *Profesa Herme Mosha ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ni mtaalamu aliyebobea katika masuala ya elimu. Pia ni amekuwa ni mshauri mkuu wa mipango ya elimu nchini aliyeshiriki katika kuunda sera ya elimu inayofuatwa hadi sasa.

Page 18: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

18

Hadhi ya Ualimu Imeporomoka Nchini Na Dkt. Hillary Dachi*

[Muhtasari: Dkt Dachi anafuatilia historia ya kuporomoka kwa hadhi ya ualimu nchini Anasema katika miaka ya 1960-70 walimu walipikwa

na kuiva vizuri na pia walilipwa vizuri,na kupewa mazingira mazuri ya kufanyia kazi mambo yaliyowahamasisha walimu kuipenda kazi yao. Baadaye mambo yalibadilika; walimu wakachukuliwa bila mfumo mzuri kiasi cha watu waliosomea taaluma zingine kupewa leseni za kufundishia. Mafunzo kazini yakawa hayatolewi tena na mishahara mibovu na mazingira mabovu ya kufanyia kazi na taabu nyingi zikawaandama walimu zilizowafanya wakate tamaa na thamani yao machoni pa jamii kushuka.Hivyo kwa sasa ualimu umepoteza sifa ya kuwa taaluma. Anaona kuwa taifa halitapata waalimu wa kutosha ikiwa hakuna juhudi za makusudi za kumfanya mwalimu aliyepo aendelee kufanya kazi yake badala ya kukim-bilia katika taaluma zingine.]

Labda ningeanza kwa kuongeza neno dogo tu kwenye mfano ule wa kobe. Kwamba kobe anachomoza kichwa na anaweza kukirudisha ndani ya gamba lake. Lakini mbaya zaidi ni kwamba kobe huwa akifa anakufa na gamba na lile gamba ndilo linakuwa kabuli lake. Mimi kwa sababu ni mwalimu na mwalimu wa walimu, ningependelea kutumia fursa hii kuzungumzia miaka hamsini ya walimu na ualimu na baadaye labda kuzungumzia mustakabali wa walimu na ualimu. Na mwalimu kwa tafsiri ya kawaida ni mtu anayesomesha wengine elimu au maarifa fulani kwa hiyo tafsiri hii ina maana wote wanaosomesha elimu au wanaosomesha maarifa katika kiwango chochote kile ni waalimu. Katika lugha ya kiaarabu huwa wanaitwa ustaadh maana yake ni mwalimu. Lakini katika jukwaa la leo mwalimu nitakayemzungumzia ni yule anayefundisha ngazi za elimu ya msingi na sekondari kwa sababu kubwa moja kwamba kwa ujumla wao hawa wanafundisha wanafunzi watoto wa Tanzania wasiopungua mil-ioni kumi, nafikiri ni zaidi ya milioni kumi. Kwa hiyo hawa wanashikilia maisha ya karibu ya asimia ishirini au zaidi ya watanzania. Siku hizi kuna msemo unaosema: Mnyonge nyongeni lakini haki yake mpeni. Walimu wamefanya makubwa sana ndani ya miaka hamsini. Wanafanya kazi kubwa sana sasa hivi na bado wana kazi kubwa sana mbele yao. Na hapa ninaposema mwalimu, dhana ya mwalimu ningeomba ieleweke kwamba ni yule mwenye sifa ya ualimu na ualimu. Maana kuvaa joho jeupe halafu ukawa na kifaa cha kupimia mapigo ya moyo shingoni hakikufanyi wewe kuwa daktari wa bi-nadamu. Au unapobeba ledger haikufanyi kuwa mhasibu. Na kama kuna makasisi hapa naomba msamaha: kuvaa joho la ukasisi hauna maana wewe umekuwa kasisi. Kwa hiyo hapa nazungumzia ualimu na sifa zake na hizo ni nyingi na nikitaja hapa sitazimaliza, nitazitaja chache tu. Kwanza, ni kulifahamiu vizuri sana somo lake au masomo anayoyafundisha.Hii ina maana yale aliyoyasoma shuleni na kuyafaulu vizuri. Hhhi ni kwa sababu huwezi kufundisha usichokijua; unapofanya hivyo inakuwa ni dhambi kwa Mungu. Pili, awe na uelewa mzuri katika saikolojia ya elimu ili aweze kuwafahamu vizuri sana wanafunzi wake; utayari wao wa kujifunza tabia na hata wale wenye mahitaji maalumu ya kujifunza ili aweze kuwasaidia. Aidha, awe na utaalamu wa kutosha kutumia njia bora za kufundishia kwa nadharia na vitendo. Kubwa zaidi awe anahudhuria shuleni na kuingia darasani kufundisha akiutumia huo muda kikamilifu. Awe tayari kuji-

funza pale mabadiliko katika somo analofundisha na katika taaluma ya ualimu kwa ujumla yanaotokea. Pia awe anafuata

maadili kikamilifu ya ualimu kwa haiba, tabia nidhamu na mwenendo.

Sasa walimu na ualimu katika muongo wa kwanza baada ya uhuru unaweza kutufanya tuweze kupata picha halisi ya kama

tulinganishe na sasa. Hizo sifa chache nilizotaja hapo juu wakati wa muongo wa kwanza baada ya uhuru katika miaka ya

1961 mpaka kwenye miaka ya mwanzo wa 1970. Bahati nzuri mimi nilikuwa mtoto wa shule katika kipindi hicho. Ingawa

mengi siyakumbuki lakini nakumbuka kiasi. Nakumbuka kwamba walimu walitayarishwa vizuri sana kitaaluma. Muda wa

kozi ya ualimu wa shule ya msingi kwa mfano ulikuwa si chini ya miaka miwili. Wakufunzi, siku hizi tunaita wanachuo,

walipikwa wakaiva katika maudhui ya masomo watakayofundisha na namna ya kufundisha kwa nadharia na vitendo

wakiwa chuoni, wakiwa darasani katika shule za mazoezi na wakiwa nje katika shule za vijijini na mijini.

Page 19: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

19

Baada ya kumaliza kozi waliajiriwa, lakini walipitia katika kipindi cha majaribio na uangalizi wa karibu sana wa walimu wakuu na idara ya ukaguzi. Kiliitwa kipindi cha probation, kabla hawajapata ajira kamili na kabla hawajasajiliwa kama walimu. Kwa hiyo palikuwa na mfumo mzuri wa ukaguzi na Idara ya Ukaguzi nayo ilitimiza wajibu wake kama ipasavyo. Walilipwa vizuri mishahara, wakati ule sisi tunakumbuka tulikuwa wadogo. Watumishi waliokuwa na magari kwa mfano walikuwa ni walimu. Waliweza kuyamudu madarasa; idadi ya wanafunzi ili-kuwa ni ya viwango vinavyokusudiwa; vifaa vya kufundishia na kujifunzia vilikuwepo. Waliendelezwa kitaalaamu na ki-taaluma kwa kuandaliwa mafunzio kazini yaliyogharamiwa na serikali. Mafunzo ya mwisho ninajayokumbuka yalikuwa ni yale yaliyoitwa ya MTUU Mpango wa TanzaniaUnicef na Unesco, miaka ya sabini. Baada ya hapo hapajawahi kuwa na mpango wowote ule wa mafunzo kazini unaoeleweka uliopangwa vizuri kama ule MTUU. Na kwa ujumla kazi ya ualimu iliheshimiwa katika jamii. Mwalimu alitambuliwa kwa mchango wake katika kusomesha na kufundisha. Walitambuliwa kama wataalamu na kazi yao ilitambuliwa kuwa ni ya kitaalamu. Waalimu waliipenda kazi yao. Palikuwa na msemo unaosema „ualimu ni wito‟. Ulikuwa maarufu, sasa hivi unachukiwa sana na ukiusema mbele ya walimu unaweza ukapigwa mawe. Katika muongo wa pili, hii miaka ya sabini mpaka themanini, hapo nilikuwa tayari na akili kidogo kwa sababu nilikuwa shule ya msingi na baadaye sekon-dari. Shule zilikuwa zikitekeleza Azimio la Arusha na Elimu ya Kujitegemea kwa vitendo kwa kufyeka misitu, kulima mashamba , ufugaji, bustani, kuvuna mazao kwa malipo vijijini. Wanafunzi wakawa viba-rua wakisimamiwa na walimu kama manyapara; na mimi kuna kipindi nilifanya hiyo kazi kusimamia wanafunzi wakati wanavuna mazao kwenye mashamba ya wanavijini kwa ajili ya malipo. Kilikuwa vilevile kipindi cha walimu kushiriki katika kampeni za kufuta ujinga na kampeni za Elimu ya Watu Wazima; Mtu ni Afya, Misitu ni Mali, Siasa ni Kilimo. Shule zikawa ni vituo vya Elimu ya Watu Wa-zima; walimu wakawezesha na kuratibu elimu ya watu wazima. Vilevile kilikuwa ni kipindi cha Operesheni Vijini; shule zikawa kambi za muda na vituo vya kuratibu operesheni. Baadhi ya walimu wakafanya kazi za umeneja wa vijiji. Na kilikuwa kipindi cha utekelezaji wa sera ya elimu ya msingi kwa wote, Universal Primary Education (UPE). Shule zikajengwa kwa wingi. Sijui kama zilikuwa ni shule; lakini kama tukichukulia kwamba wanafunzi walikuwa wanakusanyika wanasomeshwa na wanafundishwa basi zilikuwa ni shule. Idadi ya shule ilikua ikazidi elfu sita, wanafunzi wakazidi milioni 3. Kubwa tunaloliona kwa upande wa walimu kipindi hicho ni utaratibu wa kutayarisha walimu kubadilika. Muda wa kozi ya ualimu kwa mfano wa shule za msingi na Diploma ya ualimu ukapunguzwa na kuwa chini ya mwaka mmoja; na kwa ukamilifu nafikiri ni kwa miezi tisa. Wakufunzi walijifunza mbinu za kufundishia tu. Sababu za mabadiliko zilizotolewa na wakubwa zilikuwa mbili: Kwanza, kwamba palikuwa na uhaba wa walimu kwa hiyo ilibidi muda wa kujifunza upunguzwe ili kupata walimu wa kutosha katika kipindi kifupi. Hii sababu inaweza kukubalika na madhara yake kuvumilika pale linapokuwa suluhisho la muda mfupi tu. Lakini pale inapokuwa tabia ya kudumu uharibufu wake ni mkubwa sana Sababu ya pili, wakubwa walisema utaratibu wa kutayarisha walimu ulikuwa ni mbovu. Walidai kwamba ulirithiwa toka

kwa wakoloni; kwamba umepitwa na wakati; kwamba ni ghali;na kuwa hakuna sababu ya kumweka mwalimu miaka mi-

wili. Wataalamu wanasema hii ilikuwa ni sababu ya kisiasa zaidi kwa sababu haikuwa na mshiko kitaaluma na kitaalamu.

Page 20: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

20

Na katika kipindi hiki, serikali ilibuni, ikaanzisha na kutekeleza mpango wa kufundisha walimu kwa ajili ya shule za vijijini kwa njia ya masafa, nje ya chuo. Enzi hizo ukawa maarufu kama walimu wa UPE. Wale wenzangu na mimi nafikiri mna-kumbuka. Hao walikuwa wakifundisha madarasa ya chini mpaka darasa la tatu la nne; na wengine mpaka darasa la tano. Wakufunzi waliodahiriwa ni wale waliomaliza darasa la saba walioshindwa mitihani ya kumaliza darasa la saba na wale ambao walifaulu lakini hawakuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kwa sababu nafasi zilikuwa hazitoshi. Lakini inasemekena kuna wengine ambao walidahiliwa na walikuwa hawakumaliza darasa la saba. Na hao walichukuliwa kutoka kila pahala. Wengine walikuwa wakifanya kazi na shughuli za kila aina; nyingine ambazo zilikuwa hazithaminiwi na kudharaulika katika jamii. Kwa ujumla jamii na wananchi walitambua udhaifu na athari za baadaye za mpango huu. Enzi hizo wananchi waliukebehi mpango huu na kuuita „Walimu Pasipo Elimu‟ na kuwakejeli walimu na kuwaita „Walimu wa UPE‟ na kadhali na kadhalika. Si vizuri sana kuyakumbusha haya lakini kama tunaangalia tulipotoka ni vizuri tuangalie historia na kuyakubali baadhi ya makosa. Kwa hiyo mpango huu ulizalisha walimu kiasi cha 40,000. Hii ina mana kuwa wastani wa asilimia 20 na kuzidi kidogo ya walimu tulionao na wanaofundisha sasa hivi walipitia katika mpango huu wa UPE. Katika muongo wa tatu, miaka ya themanini mpaka tisini, hiki kilikuwa ni kipindi cha mabadiliko makubwa sana katika sera za nchi hii za uchumi na maendeleo ya uchumi na kisiasa. Nisingependa kuzungumzia sana muongo huu lakini tuta-kumbuka sana kuwa kila kitu kilikuwa ruksa. Muongo wanne, miaka ya tisini mpaka elfu mbili, kipindi hiki walimu waliongezeka sana kwa sababu vyuo binafsi viliru-husiwa. Lakini cha kusikitisha ni kwamba, kwa mara ya kwanza walimu walikosa ajira serikalini. Sababu zilizotolewa na wakubwa ni kwamba bajeti ilikuwa finyu. Huwa kuna msemo ambao si mzuri sana unasema „Palipo na udhia penyeza rupia‟. Msemo huu si mzuri sana kwa sababu unaashiria kama rushwa hivi kwa sababu unapenyeza rupia. Lakini palipo na bajeti finyu unaweza ukautumia vilevile kwamba palipo na udhia wa bajeti finyu ondoa rupia sekta ya elimu. Ndivyo ilivyokuwa kwamba unaweza kupunguza bajeti ya sekta ya elimu kwa sababu ina udhia ina walimu wengi na ma-hitaji yake ni makubwa. Vilevile hii ilikuwa kwa sababu ya masharti ya wakubwa, Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia, kusitiza ajira katika sekta ya umma kama sharti mojawapo la kukopa kwa ajili ya kufufua uchumi ambao uli-kuwa umedorora. Lakini kuna sababu ambayo huwa haitajwi sana; ambayo ilikuwa ni ushauri mwingine wa wakubwa, kwamba uhaba wa walimu uliopo ni feki. Hakuna tatizo la walimu, kwamba walimu wapo isipokuwa tatizo ni mgawanyo mbovu wa walimu usiojali uwiano ulio sawa kati ya shule na shule; kati ya wilaya za mijini na vijijini; kati ya mikoa na mikoa. Kwa hiyo, mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 palikuwa na walimu zaidi ya 25,000, ambao hawakuwa na ajira.

Baadhi walijiajiri wenyewe kwa kufungua vituo vya tuisheni, wengi walifanya umachinga, kama mamantilie, wengine wa-kawa wahudumu wa baa, migahawa, nyumba za kulala wageni, wakawa wapiga debe, wengine wakaanza kupiga madisko na kuonesha sinema za video kwenye vibanda vilivyojengwa vijijini. Hiyo ndiyo ilikuwa hali halisi katika kipindi hicho.Kwa mara ya kwanza tuliona walimu wana- kosa ajira na taaluma ikaanza kuparaganyika. Tukaingia muongo wa tano, miaka ya 2000 mpaka 2010 hadi sasa. Hiki ni kipindi ambacho, kama profesa alivyosema, kimekuwa cha mpango kabambe wa elimu ambao ukazaa mipango mingi ikiwamo MMEM na MMES. Shule nyingi zika-jengwa, idadi imefikia zaidi ya 15,000 kama alivyosema Mkurugenzi wa HakiElimu, Sekondari zaidi ya 4,000. Walimu wa-mefikia zaidi ya 180,000 na maelfu bado wanahitajika. Shule za msingi zipo kila kijiji na za sekondari kila kata; ingawa madarasa hayatoshi, walimu hawatoshi, vitabu havitoshi, hakuna maabara, shule zingine mwalimu mmoja, viranja na wao ni walimu. Lakini tukubali tu kwamba kipindi hiki walimu wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa wote, wa mijini na vjijini. Kwa sababu tafsiri ya mazingira magumu kwa siku hizi inaleta matatizo na nafikiri kuna namna ya ubaguzi fulani. Kwa sababu ninaposema mazingira magumu haina maana ya umbali toka mahali fulani kwenda mahali fulani tu, lakini vilevile mazingira magumu pale shuleni, mazingira magumu pale anapoishi.

Page 21: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

21

Kwa hiyo hata walimu wa mijini na wao wana mazingira magumu. Wakati mwingine ni magumu sana hata kuliko wale wa vijijini. Kwa hiyo katika kipindi hiki walimu wameajiriwa kwa maelfu. Hata waliokosa ajira kwa miaka mitano na zaidi wakati ule wameajiriwa pia angalau wamepata mafunzo ya kuondoa kutu na ugutu. Mitaala ikabadilika. Kuna dhana- maarufu sana siku hizi katika mitaala unaitwa „Mhamo wa ruwaza‟, walimu wanaifa-hamu kwa kiingereza unaitwa paradigm shift. Kwamba wanafunzi wanabidi waijue wenyewe, walimu wasaidie wanafunzi kujifunza. Lakini hii haikwenda sambamba na mafunzo kazini ili walimu waweze kupigwa msasa kutekeleza mitaala mipya kama inavyotakiwa. Muda wa kozi za walimu vyuoni ukapunguzwa tena, tukarudi kama zamani. Wakafundishwa njia za kufundishia tu, kisha

wakaajiriwa. Sera ya elimu ikawekwa kando wakaanza kudahiliwa wanafunzi waliopata alama za chini, daraja la nne.

Lakini daraja na nne lina alama vilevile; wakaenda mpaka

alama 28 ambacho sio kitu kizuri. Wakachukua vijana waliomaliza kidato cha sita wakapewa mafunzo ya wiki nne ya njia

ya kufundishia; wakapewa leseni za kufundisha wakaajiriwa. Wananchi wakawabandika majina ya kejeli kama ilivyokuwa

walimu wa UPE wakati ule; wakaitwa „[Voda Fasta‟ sehemu zingine wanawaitwa „Yeboyebo‟ na kadhalika. Kwa hiyo uka-

ingia udhalilishaji mwingine katika taaluma ya ualimu. Na

walimu wenye shahada ya taaluma yoyote wakapewa le-

seni za kufundishia wakaajiriwa bila mafunzo ya aina

yeyote, angalau hata ya wiki moja. A fadhali hata wale

waliopewa ya wiki nne; kwamba baadaye watasoma sta-

shahada ya ualimu. Kwa hiyo, kwa ujumla kipindi hiki

tunaona kwamba walimu walipata mafunzo na kuajiriwa

kwa mifumo tofauti. Kwa hiyo kwa ubaguzi wa namna

fulani kwa sababu wana mafunzo tofauti, wanaajiriwa

tofauti kwa hiyo ajira zao zina masharti tofauti, misha-

hara tofauti. Kwa kilugha huwa tunasema walibananga,

yaani serikali na wadau na elimu , sisi ambao hatukup-

inga hili kwa ujumla tulibananga.Kwa hiyo

ningependelea kuangalia mustakabali wa walimu na taa-

luma hii ya ualimu katika kipindi kijacho kwamba iweje.

Ukisoma Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 na ile ya ma-badiliko yake ya mwaka 1995, vilevile ukiangalia Teacher Services Scheme ya 2008, hivi vyote vinatambua ualimu kwamba ni taaluma. Ni kazi ambayo ina miiko na maadili yake. Lakini ukifikiri sana wakati mwingine unajiuliza, je, ualimu katika nchi hii unakidhi vigezo vya kuitwa kwamba hii ni taaluma? Yaani ukiweka katika mizani na taaluma nyingine kama she-ria, uhandisi na udaktari. Kwanza, hatuna Bodi ya taaluma ya ualimu ambayo ingeweza kutusajili na kusimamia maadili na mambo mengine

yanayohusiana na taaluma ya ualimu. Hatuna vyama vya kitaaluma vya walimu. Zamani kilikuwepo chama kinaitwa

Chama cha Kitaalamu cha Walimu Tanzania yaani (CHAKWATA) profesa sijui bado kipo au? Sina uhakika. Tuna

Chama cha Walimu Tanzania (CWT). Lakini hiki ni chama kama vilivyo vyama vingine vya wafanyakazi, kinatetea

maslahi ya walimu na haki za walimu katika ajira.

Vituo vya walimu vipo vipo tu, idadi yake sasa hivi ni kama 600 lakini vinafanya nini nafikiri ni suala ambalo nadhani

tunapaswa kulifanyia kazi. Mafunzo kazini hakuna, kila kitu kinaenda mzobemzobe, shagala bagala sio lugha nzuri lakini

ndio hivyo. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema mwaka 1966, nafikiri wakati anazindua Chuo cha Ualimu cha Dar es Sa-

laam Chang‟ombe, ambacho sasa hivi ni chuo kikuu kishiriki cha chuo hiki. Na hii naomba niweke wazi kuwa ni tafsiri

yangu mwenyewe ni Kiingereza lakini nimetijahidi kutafsiri kwa Kiswahili alisema: “Wale wenye wajibu ya kuwaandaa vijana

wana nguvu kubwa ambayo huwezi kuilinganisha na nyingine yeyote ile.

Mazingira ya kufanyia kazi kwenye baadhi ya shule yanawakatisha tamaa walimu

Page 22: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

22

Fikra kwamba walimu hawana nguvu kwa umoja wao ni moja ya makosa makubwa tunayoyafanya, kwani walimu wanaweza kuijenga au kuiobomoa jamii. Siyo nguvu ya mtu mwenye bunduki, sio nguvu inayoweza kutambuliwa na mpumbavu; ni nguvu ya kuamua tuwe na taifa la namna gani, miaka ya 1990 na baada ya hapo.” mwisho wa kunukuu. Leo hii nimesema ualimu umepoteza hadhi na heshima yake katika jamii. Ni kazi ambayo kwa vijana wengi ni chaguo lao la mwisho. Kwa wazazi wenzangu walio hapa nafikiri maneno haya nitakayotamka mnayatumia sana kwa mtoto asipo-fanya vizuri. Kwa maneno mengine akifeli akapata madaraja ya chini sana mnasema mtafutie angalau kozi ya ualimu. Wakimkuta pale nyumbani ukasema bado nahangaika unajua hakufanya vizuri wanasema ina maana umekosa hata kozi ya ualimu? Hata ualimu umekushinda? Sasa hii hali nafikiri inasikitisha sana. Kwa sababu katika muongo wa kwanza na kidogo katika muongo wa pili kuna ma-hali nilisoma nafikiri kwenye maandiko yaliyoandikwa na Profesa Mosha, kwamba miaka hiyo walimu walikuwa wana-heshimiwa hata kanisani walikuwa wanawekewa viti vya mbele kama ambavyo tunawawekea wanasiasa siku hizi. Lakini sasa hivi mimi vijana wangu ninaokutana nao waliomaliza shahada ya kwanza wakati mwingine hata shahada ya uzamili wanaponiambia mwalimu shikamoo nasema marahaba hujambo kijana wangu. Swali la pili ambalo huwa napenda kufahamu ni kwamba wako wapi? Kwa hiyo nitamuuliza uko wapi? Jibu ninalopata kwa wengi husema mwalimu nipo mtaani tu. Lakini kumbe si kweli kwamba wako mitaani. Ukweli ni kwamba wamea-jiriwa kama walimu shule fulani lakini hawataki watambuliwe kama wao ni walimu. Hataki kabisa kujihusisha na ualimu. Lakini kama atakuwa ameajiriwa benki, kuna mwanafunzi wangu yupo CRBD hapahapa chuoni, atakuambia haraka kuwa mwalimu mimi nipo CRDB. Lakini kama ni mwalimu anakuwa mzito kukuambia shule gani anafundisha. Walio wengi, taaluma ya ualimu ni kama suluhisho la maisha kwamba unapokosa kila kitu, anakuwa hana jinsi ila ni kukimbilia kujifunza ualimu. Kwa hiyo wengi wako katika mpito tu. Na kwa sababu ukiwa katika ualimu ni rahisi sana kujiendeleza, kwa hiyo walio wengi wanabadilisha taaluma wanaenda katika taaluma nyingine. Na ndiyo maana itakuwa ni kazi sana kuweza kupata walimu wa kutosheleza kwa sababu hakuna namna yeyote tunayoifanya kama serikali kuhakiki-sha kwamba walimu wanaipenda kazi yao, wanaendelea kufundisha na wanapenda kufahamika kama walimu. Walimu wamekata tamaa kwa sababu ukiwauliza wao, si maneno yangu, ni kwamba serikali haiwathamini. Kelele tuna-zisikia za madai, wanadai kila siku na mwalimu usipommotisha, usipompa ile morali ya kufanya kazi, hasa mwalimu anayefanya kazi katika mazingira magumu. Narudia kwamba ninaposema mazingira magumu sina maana lazima awe ni yule anayefundisha mbali sana vijijini, mazingira magumu nasema ni pale shuleni, darasa lina wanafunzi mia ishirini. Kwa wale wenyeji wa Dar es Salaam wanafahamu kwamba wanafunzi wamekuwa wengi mpaka shule zimezaaa shule. Siku hizi tuna shule mama, shule zinazaa shule. Shule ya msingi Mbagala kwa wale wanaoifahamau ina watoto kama saba; Mbagala Kizuiani, sijui Annex n.k.!Lakini ile ilikuwa shule moja, sasa hivi wanafunzi zaidi ya elfu sita, walimu mia na hamsini, ikawa shule kubwa kuliko shule yoyote Tanzania. Lakini iko mjini. Lakini pia kuna sera za ubaguzi; kwamba mwalimu anaanza kazi huyu apewe laki tano, huyu anyimwe kwa kigezo kimoja au kingine. Nafikiri hiyo nayo ndiyo inayosababisha mpaka walimu vijana wanaendelea kuchukia kazi za ualimu kwa kuwa sera zingine ni za kibaguzi na hazifai kabisa kutumika. Kwa hiyo waalimu wanapokata tamaa wanapoteza uwezo wa kufundisha, na taaluma inabadilika kabisa kwa sababu walimu wasipoingia darasani au wakaingia darasani lakini wasifun-dishe hiyo ni kwenda kinyume kabisa na taaluma yao. Lakini kwa sababu wamekata tamaa, mwalimu mwenye digrii mbili, Kiswahili tunasema huyu ana shahada ya Uzamili,

anapopata mshahara nusu ya mshahara wa katibu muktasi wa baadhi ya mashirika ya umma, hivi jamani inaingia akilini?

Hii ni kwa sababu tunasema elimu ni kuwekeza, huyu amewekeza kwa ajili yake na faida ya taifa. Lakini unapomlipa

mshahara wa kudhalilisha kiasi hicho halafu asifundishe darasani nafikiri utakuwa huna maneno mengi ya kujitetea.

Kwa hiyo tunapoangalia mustakbali wa walimu na ualimu nafikiri imefikia wakati tuangalie upya taaluma ya ualimu na kazi ya ualimu. Kwamba irudi katika hali yake ya zamani na hadhi inayostahiki kwa sasa na kwa hali ya sasa. Mwenyekiti asante sana. *Dk. Hillary Dachi ni Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam na pia ni mwalimu wa

siku nyingi.

Page 23: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

23

Dharau kwa Wataalamu Inaliangamiza Taifa Dk. Kitila Mkumbo*

[Muhtasari: Dk Mkumbo anatambua hatua zilizopigwa katika sekta ya elimu tangu mwaka 1967-2011 nchini hususani uandikishaji na udahili

wa wanafunzi. Hata hivyo katika katika mizani ya kujifunza na kuelewa, ujuzi wa kufikiri, kiwango cha kustarabika na kupambanua mambo ina-saliti maendeleo ya elimu kwani inaonyesha kuwa taifa halijapiga hatua. Anapendekeza kuwekeza katika ubora wa elimu, kuchagua Lugha moja

itakayotumika katika kufundishia kati ya Kiingereza au Kiswahili, kuboresha maslahi ya walimu na kutatua migomo katika vyuo.]

Nashukuru sana Mwenyekiti wa Kongamano hili. Natambua kuna faida na hasara ya kuwa mzungumzaji wa mwisho; hasa wazungumzaji wa mwanzo wakiwa ni walimu wako. Profesa Mosha na Dkt Dachi wote wamenifundisha. Faida ya kuzungumza mwisho ni kwamba hata ukikosea hawana fursa ya kukukosoa kwa hiyo itabidi wamezee tu. Hasara yake ni kwamba wanakuwa wamekutia hofu kwa kuwa mambo mengi ambayo ulikuwa uongee wanakuwa wameshayaongea. Lakini nitajitahidi kudonoa. Nilipewa kazi pia ya kuunganisha na paper ya Mheshimiwa [Jackson] Makweta kitu ambacho sitakifanya.Hii ni kwa sa-babu ngazi ya Makweta ni ngazi nyingine kabisa na mimi nisingependa kujiingiza kwenye kusema maneno yake; na bahati nzuri mmegawiwa karatasi yake. Lakini nianze tu kwa kusema kwamba katika ukurasa wa pili wa karatasi ya Mheshimiwa Makweta ana mu- quote Mwalimu Julius Kambarage. Nyerere kwamba kuna wakati Tanzania ikisherehekea uhuru wake, hayati Mwalimu Nyerere, Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, aliwahi kuulizwa swali lifuatalo na waandishi wa habari toka nje ya nchi. Swali lilisema „Kitu gani hasa kinawafanya watanzania msherehekee siku hii ya uhuru wenu?‟ Na Mwalimu aliwa-jibu kuwa, watanzania walikuwa wakisherehekea siku ile kwa sababu ya kuwa hai hadi siku ile ya uhuru. Walikuwa wa-nasherehekea uhuru sababu kubwa ni kwamba walikuwa wanamshukuru Mungu kwa sababu walikuwa hai hadi siku ile wakisherehekea uhuru. Hilo ndilo Mwalimu Nyerere aliona ni jambo la maana la kusherehekea. Ninahisi hizi zilikuwa ni siku za mwanzo sana za uhuru. Bahati mbaya Mheshimiwa Makweta hajasema ilikuwa ni tarehe ngapi, lakini nafikiria ilikuwa ni siku za mwanzo kabisa za uhuru na alikuwa anakebehi serikali ya kikoloni ambayo ilikuwa imeondolewa tu madarakani. Sasa na sisi tunawajibu wa kujiuliza tunaposherehekea miaka hamsini ya uhuru leo, tunasherehekea nini? I hope kwamba tutakuwa tunasherehekea zaidi ya kuwa hai. Natumaini hivyo. Kama tunasherehekea tu kwa kuwa tuko hai basi tuko hoi kwelik-weli. Baada ya kusema hayo niseme tu kwamba katika mawasilisho yangu nitaangalia, nitapitia, kwa sababu ni miaka hamsini, ntajaribu kuangalia mafanikio yetu katika elimu, katika miaka hii hamsini, na nitajitahidi kukwepa yale ambayo wenzangu wamekwishaeleza ili isiwe ni marudio. Na katika kufanya hivyo nimechagua vigezo vitano vya kaungalia mafanikio yetu katika elimu.

Kuangalia kiwango cha uandikishaji na udahili katika ngazi mbalimbali za elimu

Kuangalia kiwango cha ufaulu katika mitihani ya kitaifa ya kimataifa

Kiwango cha ufahamu ama uelewa (literacy rate)

Kiwango cha ujuzi, kufikiri na kupambanua mambo Kiwango cha kustaarabika (civil competence)

Sitajikita sana kwenye kiwango cha uandikishaji na udahili, kwa sababu wakati Mkurugenzi wa HakiElimu akitoa neno la ufunguzi alieleza vizuri mafanikio ambayo tumeyapata. Kwa kiwango chochote kile tumepiga hatua sana katika suala zima la kuwapa fursa watu wetu waweze kuingia katika zile taasisi za elimu; iwe ni shule ama vyuo. Kama nilivyosema takwimu zimeonesha, ukiangalia hata ile elimu ambayo haisemwi sana; ile elimu ya awali, na yenyewe

kwa siku za karibuni tumepiga hatua sana. Sasa hivi angalau karibu asilimia 40 ya watoto wetu wana nafasi ya kuweza ku-

hudhuria madarasa ya elimu ya awali kabla hawajaanza shule za ya msingi. Na wale ambao wako katika elimu wanafa-

hamu kwamba elimu ya awali inatoa msingi muhimu sana kwenye elimu ya baadaye. .

Page 24: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

24

Of course tunatofautiana mkoa hadi mkoa. Kwa bahati mbaya mkoa wa Dar es Salaam ndio wa mwisho. Mkoa wa Dar es

Salaam ni asilimia 13 tu ya watoto ndio wanaoweza kuingia katika elimu ya awali kabla ya kuanza shule ya msingi. Na on-

gezeko kubwa liko katika shule za watu binafsi au mashirika binafsi.

Na ukipiga takwimu, katika hali ya kawaida tulipaswa kuwa na shule za msingi, kama tungeenda kwa kasi ile ya wakati wa uhuru, tulipaswa kuwa na shule za msingi 14,300 tu; lakini tuna shule za msingi 16,000. Kwa hiyo tumeenda zaidi ya asili-mia mia. Kwa hiyo tumepiga hatua kubwa sana. Katika shule za sekondari, kama tungeenda kwa kasi iliyokuwepo wakati wa uhuru, tungekuwa na shule za sekondari

chini ya 200 katika nchi nzima leo tunaposherehekea miaka 50 ya uhuru. Lakini leo tuna shule zaidi ya 4,000 kama alivyosema Mkurugenzi wa HakiElimu. Kwa vyovyote vile kwa maana ya kuwapa watu fursa ya elimu tumepiga hatua ya ajabu sana kwa kiwango kile cha Tsunami! Kwa hiyo, kwenye shule kama ukitaka kuweka maksi, kwa sisi walimu tunapenda sana ku-weka maksi. Katika vile vigezo vitano, kama kila kigezo kina maksi mbili, katika hiki kigezo cha kwanza huna ujanja utabidi ukipe maksi mbili zote kwa sababu kwa kweli tumepata mafanikio kwa kila kiwango. Ukija kwenye kigezo cha pili, kwa maana ya kiwango cha ufaulu katika mitihani; hii pia nafikiri Mkurugenzi wa HakiElimu aliligusia. Kiwango cha kufaulu kimeshuka sana hilo tu-nalijua. Na kwa wastani kimeshuka kutoka

asilimia 90 kwenye miaka ya tisini mpaka asilimia 50 hivi leo. Kwa hiyo katika watoto kumi ni watano peke yao ndio wanaofaulu. Ukiingia katika sekondari kiwango cha kufeli ni kiwango cha Tsunami. Nafahamu matokeo ya mwaka jana yalivyokuwa mabovu na kuna kitu kimoja ambacho hakielezwi vizuri kuhusu matokeo ya mwaka jana. Ukweli ni kwamba katika wa-toto karibu 550,000 waliofanya mitihani, wanafunzi 177,000, ambao ni asilimia karibu hamsini, walipata sifuri!. Lakini kuna wengine kama asilimia thelethini ya hao walipata daraja la nne, Division 4. Na watu wote mnafahamu maana ya Di-vision 4 ni nini ndani ya nchi hii. Ukishapata Division 4 ndiyo itabidi uingie kwenye yale aliyokuwa anasema Dkt. Dachi, siku hizi Division 4 hata ualimu huendi. Huko Polisi walishaacha siku nyingi. Nasikia walimu nao wameacha. Kwa hiyo ukijumlisha Division 4 na Division zero kwa mwaka jana asilimia 80 walipata division zero na division four.Kwa maana ya kitaalamu, asilimia 80 walifeli mitihani ya kidato cha nne mwaka jana. Kwa hiyo, kwa maana ya ufaulu kwa kweli habari ni habari mbaya. Na kwa maana ya ualimu ukiniambia nitoe maksi kwenye hapa nitatoa maksi chini ya sifuri. Lakini kwa sababu mara nyingi hatutoi chini ya sifuri, basi na hapa naweka si-furi katika miaka hiyo hamsini ya uhuru. Na wewe uwe unajumulisha ili mwishoni tujumulishe kwa pamoja tuone ni maksi ngapi tumepata. Naenda kwenye kigezo cha tatu, kwa maana ya kiwango cha ufahamu/ uelewa. Miaka ya themanini wale ambao wana-

fuatilia mambo ya elimu, nchi hii iliweza kupata tuzo ya UNESCO kwa kuwa nchi ya kwanza katika barani Afrika ku-

weza kufikia kile kiwango cha asilimia 80.

Dk. Kitila akiwa na mmoja wa washiriki kwenye Kongamano la miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania na Elimu

Page 25: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

25

Katika watu kumi, watu wanane na kuendelea walikuwa wanaweza kusoma, kuandika na kufanya mahesabu ya kimaisha

yaani ukimpa shilingi mia tano au shilingi elfu moja akaenda kununua soda ya shilingi mia tano anajua anatakiwa arud-

ishiwe shilingi mia tano. Hayo ndiyo mahesabu ya kimaisha, ya kawaida katika maisha ya kila siku. Kwa hiyo zaidi ya

watu wanane katika watu kumi walikuwa wanaweza kusoma kuandika na mahesabu ya kimaisha.

Juzi nilikuwa kwenye mkutano wa UNESCO pale mjini, tulikuwa tunapitia maendeleo ya mambo ya elimu katika miaka

hamsini na tukawa tunabishana. Takwimu za kimataifa zinaonesha kwamba ni asilimia 60 mpaka 63 ya watanzania ndio

wanaojua kusoma kuandika na mahesabu ya kimaisha. Kwa hiyo tumeshuka kutoka asilimia 80 miaka ya themanini

mpaka asilimi 60 miaka hii. Watu wa Wizara ya Elimu walikataa. Wao figure walionayo ni asilimia 70. Haya ngoja tuwaku-

balie, asilimia 70 ya watanzania ndio wanaojua kusoma na

kuandika. Hata kwa kiwango hicho tumeshuka, kwa hiyo

katika watu kumi ni watu saba peke yao au chini ya hapo

ndio wanaoweza kusoma, kuandika na kufanya mahesabu

ya kimaisha.

Wale waliosimamia uchaguzi wa mwaka jana wanakum-buka. Kiwango cha watu waliokuwa wanaomba kupigiwa kura mwaka jana kimeongezeka sana. Katika wapiga kura kumi wapiga kura kati ya watatu mpaka wanne walikuwa wanaomba kupigiwa kura. Maana yake hawajui kusoma na kuandika. Kwa hiyo hata katika maisha ya kawaida unaweza ukaona. Na siku hizi imekuwa jambo la kawaida kukutana na mtu ambaye hajui kusoma na kuandika. Wale ambao wanaajiri

watoto wa kazi; mnawaita ma-house girl, ambao mimi sipendi kuwaita hivyo, siku hizi uwezekano wa kukutana

na house girl ambaye hajui kusoma na kuandika umeongezeka sana. Kwa hiyo tuna tatizo kubwa sana katika kigezo hiki. Sasa ukijumulisha kiwango cha kujifunza na uelewa nafikiri Mku-rugenzi wa HakiElimu pia alieleza hapa kwamba kwa tafiti ambazo zimefanyika miaka miwili mfululizo, zimeonesha kwamba vijana wetu wa kitanzania walioko shule za msingi uwezo wao unashuka. Kwa mfano, katika vijana kumi ni wa-tatu peke yao, wanafunzi wa darasa la tatu, ndio wana uwezo wa kusoma sentensi ya Kiswahili ya darasa la pili. Sijui kama tunaelewana katika hicho. Maana yake ni kuwa mtoto yupo darasa la tatu, mpe sentensi ya Kiswahili, ya darasa la pili asome; . ni watoto watatu peke yao kati ya kumi ndio wanaweza kusoma! Kenya ni watoto wanne mpaka watano. Hii ni Kiswahili, siongelei Kiingereza, Kiingereza ni biashara nyingine. Sasa twende kwenye Kiingereza, katika watoto kumi ni mtoto mmoja peke yake ana uwezo wa kusoma hadithi ya Ki-ingereza aya moja; Tena hiyo hadithi ni ya Kiingereza ya kiwango cha darasa la pili! Hao ndio tulionao. Sasa katika wa-toto kumi, kwa maana ya mahesabu, ni watoto watatu peke yao ndio wenye uwezo wa kufanya mahesabu ya kujumuisha, kutoa na kuzidisha ya kiwango cha darasa la pili katika nchi yetu. Kwa hiyo hitimisho la utafiti huu ulikuwa ni kwamba watoto wa kitanzania na wa Afrika Mashariki kwa ujumla, lakini

wanaingia madarasani, wanaingia katika majengo yanayoitwa madarasa, na mkusanyiko wa madarasa unaoitwa shule,

lakini hawajifunzi. Lakini wa kwetu ndio walikuwa na hali mbaya zaidi. Hiyo ndiyo ilikuwa hali.

Kwa hiyo ukitaka kutoa maksi kwa hapa, na mimi nimekuwa very kind nimeona kwamba kwa hapo kwa kweli tumejitahidi

tutatoa maksi tu kwa sababu wameweza kusoma soma hizo sentensi. Basi hebu tuwape 0.75. Naona wanafunzi wangu

ninaowafundisha wanajua. Huwa si vigumu sana kwa mimi kutoa maksi za namna hii! Kwa hiyo 0.75 katika kile kigezo

cha tatu.

Mazingira ya kusomea katika shule nyingi ni magumu sana

Page 26: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

26

Twende kwenye kigezo cha nne ambacho nakiita kiwango cha ujuzi, kufikiri na kupambanua mambo. Kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya elimu. Ukipita katika elimu tunatarajia uweze kufikiri vizuri zaidi kuliko mtu ambaye hajaenda katika mfumo wa elimu. Uweze kupambanua mambo vizuri zaidi.Moja ya kazi za shule zetu, na hii ipo kwenye karatasi ya Mheshimiwa Makweta, yeye anaeleza kwamba shule zetu na taasisi zetu za elimu ya juu zimekuwa zinafanya kazi moja tu yenye kuwakilishwa na herufi „K‟ tatu kwa maana ya kula, kulala na kusoma. Yaani kitu kinachoendelea katika shule zetu na katika vyuo vyetu ni hizo K tatu. Vijana wetu wanakula, kulala na kusoma basi. Alisahau tu zingine angeweza kuon-geza K nyingine ya kustarehe! Kwenda kujirusha disko, club, ndiyo maana siku hizi klabu ni nyingi sana sehemu ambazo kuna vyuo! Hawafanyi kazi nyingine zaidi ya hizo. Hawawezi kufagia hata kama kuna karatasi, hapa sasa hivi wakimaliza kunywa maji labda kwa sababu nimesema, wakimaliza kunywa maji wataacha chupa hapohapo, hawatazitoa. Wakiona karatasi hapo nje hawataweza kuzito. Kuna kipindi tulipokuwa kwenye serikali ya wanafunzi,

tukaamua kuandika proposal kwa utawala wa chuo,

kuomba kwamba kazi za hapa chuo kikuu zianze ku-

fanywa na wanafunzi kama njia ya kuwafanya waji-

ingizie kipato. Tukaomba kwamba badala ya kuajiri

makampuni ya usafi kwa nini wanafunzi wasifagie wao

na walipwe ka ujira kidogo. Utawala wakapokea suala

hili kwa furaha sana. Tulipolipeleka pendekezo hili kwa

wenzetu tulizomewa ile mbaya. Yaani sisi tuanze kufa-

gia? Lakini wale ambao wamesoma nje kama mimi

kwenye shahada zao baadhi wanafahamu.

Mimi nimesoma nje. Kazi mojawapo niliyokuwa nafanya ilikuwa ni kuosha masufuria kafteria ndio iliyo-kuwa inanipatia kipato cha ziada. Lakini hapa ukitaka kugombana na wanafunzi wetu waambie wafanye kazi hizo! Tulitaka pale UDASA Club, tulitaka kufanya uta-ratibu kwamba ile club badala ya kumpa mtu, tuajiri wanafunzi wetu wawe ndio ma-bar maids pale; lakini wakatucheka sana. walitucheka sana; yaani mimi nikauze soda? Lakini huko Ulaya baada ya mwaka mmoja au miwili ndiyo unaweza ukapata kazi ya kufanya baa, yaani we huwezi kupata kazi ya kuuza baa ukienda. Lazima waku-train ndiyo uweze kufanya kazi baa! Library pale tuna wafanyakazi, tumeajiri chungu nzima.Lakini sehemu nyingine wanaofanya kazi library ni wanafunzi wanapeana zamu mchana na usiku, na ndiyo maana wanaweza wakafundishwa mpaka saa sita hadi saa nane. Lakini hebu jaribu kumwambia mwanafunzi wa hapa akafanye kazi library! Kwa hiyo nakubaliana kabisa na kabisa na Mheshimiwa Makweta kwamba kazi yetu katika taasisi hizi imekuwa ni kula kulala na kusoma. Matokeo yake ni nini? Vijana wetu wanamaliza vyuo vikuu, shule za msingi, shule za sekondari hawajui chochote zaidi ya kusoma, kuandika na mahesabu basic. Bahati mbaya siku hizi hata kuandika a good, convinving application letter, Mkurugenzi wa HaliElimu yuko hapa yeye anaajiri watu kila siku,waambie wakuandikie barua nzuri ya kukushawishi uwaajiri; hawa-taweza!. Kwa hiyo tuna hali mbaya sana katika level ya ujuzi; hatutoi watu wenye ujuzi, tunajifanya tunatoa taaluma kwa sababu taaluma ni rahisi kujitetea. Lakini level ya pili ambayo ni kitaaluma zaidi ni uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo na ni rahisi sana kupima hili.

Kimojawapo cha kupima ni kuangalia kwanza uvumilivu na ustahimilivu. Uvumilivu na ustahimilivu wa kusikiliza hata

mambo usiyoyapenda hata mambo ambayo unafikiri ni ya kijinga na ya hovyo. Unamsikiliza mtu na unamjibu kwa hoja.

Hili limepotea. Sasa hivi vijana wetu wanapenda ukienda sehemu uhubiri lugha wanayotaka kuisikia wao. Ole wako

useme kitu ambacho hawakitaki; watakuzomea na ukiendelea watakurushia hata chupa! Hii inaonesha kuwa hakuna to-

fauti ya hapa na sehemu zingine

Wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vikuu pia wal-ishiriki kikamilifu kwenye Kongamano

Page 27: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

27

Hili limepotea. Sasa hivi vijana wetu wanapenda ukienda sehemu uhubiri lugha wanayotaka kuisikia wao. Ole wako useme kitu ambacho hawakitaki; watakuzomea na ukiendelea watakurushia hata chupa! Hii inaonesha kuwa hakuna to-fauti ya hapa na sehemu zingine. Lakini sehemu ambapo kuna watu wanaofikiri na wanapambanua mambo watu wana-vumiliana. Na ukisoma hapa huko miaka ya nyuma walikuwa wanabishana; wapo ambao walikuwa wanatetea ujamaa na wapo ambao walikuwa wanapinga ujamaa. Wapo ambao walikuwa wanatetea mifumo mingine lakini walikuwa wana-vumiliana na kusikilizana. Katika kigezo hiko kwa kweli tumeshuka sana kwa maana ya kiwango hiki cha ujuzi… Kwa mnaofuatilia habari mtakumbuka Mbunge wa Chalinze, aliwaomba ma-contractors wa Kichina wanaojenga barabara, wasilete wafanyakazi kutoka Dar es Salaaam wala wachina. Aliomba wawachukue vijana wake pale Chalinze kwenye hiyo barabara ili wajipatie ujira. Alipowaendea alitaka kusababisha achukiwe. Wakamshukia, yaani unataka sisi tu-kafanye kazi kwenye mitaro? Are you serious? Tupo tayari tuchange mia tano mia tano waajiri wengine sisi hatuwezi kufanya kazi kwenye mitaro! Hii ndio jamii tuliyo nayo ya watanzania; wanataka kufanya kazi fulani hawataki kazi fulani. Kwa hivo ni tatizo kubwa sana. Sasa baada ya yote haya nafikiri kwamba kuna mambo matatu ambayo ni lazima tuyashughulikie haraka sana katika nchi yetu. Mambo matatu ni ya msingi kabisa kabisa. Suala la kwanza ni lile ambalo wenzangu wame-lieleza; ni suala zima la kuwekeza kwenye ubora wa elimu. Na uwekezaji wa maana kabisa katika nchi yoyote ile iliyoendelea ni pale ilipoamua kuwekeza katika elimu. Iwe ni China iwe ni Korea, iwe ni Malaysia tunafahamu ukitaka kujua kwa nini Malaysia wameendelea, miaka arobaini walikuwa kama sisi, ukiwauliza watakuambia ni kwa sababu waliamua kuwekeza katika elimu. Kwa hiyo, hiyo ni hatua ya msingi kabisa kabisa ambayo lazima tuchukue. Na hatuna njia ya mkato na kwa sababu tumeona mafaniko makubwa ambayo tumeyapata kwenye enrollment ni kwa sababu kuongeza idadi ni kazi rahisi sana. Na watanzania sisi ni mabingwa wa kufanya mambo rahisi, mambo rahisi ambayo yanatupa mafanikio ambayo sasa hivi tunayaona. Hatutaki kufanya mambo magumu na ya muda mrefu. Mtanzania anataka afanye jambo sasa hivi alione ma-tokeo yake, ukimwambia eti baada ya miaka ishirini ijayo hawezi kukubali. Ndiyo maana hiyo Ripoti ya Makweta waliitupa kwa sababu Ripoti ya Makweta ilikuwa ni miaka ishirini kutoka miaka ya 80 hadi miaka ya 2000. Yaani miaka ishirini yote hiyo! Tunataka kufanya mambo watu wayaone! Watu walimshangaa kwa kuwa wanataka kufanya jambo sasa hizi. Tuanze kujenga shule za kata sasa hivi na watoto waingie sasa hivi. Ni kama kwenye kuzaa tu; kuzaa watoto wengi wakati mwingine kama Mungu amekujaalia afya ya kibaiolojia kuzaa watoto wengi siyo tatizo. Unaweza kuzaa watoto kumi, kumi na watano, ishirini hiyo si tatizo kubwa. Tatizo kubwa ni pale utakapoa-mua kuwalea wale watoto sawa sawa. Kwa hiyo duniani hapa kuongeza idadi haijawahi kuwa tatizo! Kwa hiyo tunapojivunia mafanikio ya elimu tujue kwamba tumefanikiwa yale mambo rahisi mambo magumu yametu-

shinda. Na mtu mwenye akili hapimi mafanikio yake kwa kufanikiwa kufanya mambo rahisi. Hatuwezi kumsifia baba eti

kanunua nepi, atakuwa baba wa ajabu, kwa sababu kununua nepi! Hilo ni jambo la msingi la baba. Mambo magumu

ndiyo tunataka tupime ufanisi wake. Lazima tuwekeze katika kupata na kubakisha walimu bora bila kujali kada ya ualimu

kama alivyosema Dkt Dachi. Hata Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, hakisifiki wala hakijawahi kusifika kwa sababu kina

majengo mengi; bali kinasifika kwa sababu kwa muda mrefu chuo hiki kiliamua kuwekeza katika suala zima la wafanya-

kazi, walimu.

Ingawa shule nyingi zimejengwa walimu wenye sifa wa ku-

tosha bado ni tatizo kubwa

Page 28: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

28

Kuna vyuo vingi sasa hivi vinatuzidi sisi majengo. Lakini kitu ambacho sisi tumebakiza ni kwamba hatujayumba katika suala zima la kada hiyo ya ualimu. Of course tuwekeze katika mazingira hii ni story ya kila siku mazingira ya kujifunza na kufundishia. Na kwenye paper ya Mzee Makweta anasema kwamba kama elimu ni ufunguo wa maisha, elimu mbaya ni ufunguo wa maisha mabaya! Kwa hiyo tulijue hilo. Kama tunaendelea kuwa na mfumo mbovu wa elimu tusitarajie mambo ya ajabu, tutatoa watu ambao ni wabovu. Jambo la pili ambalo lazima tulishughulikie haraka sana na hili limesemwa miaka yote ni suala zima la lugha. Kwenye Ri-poti ya Makweta kuna karibu page tatu zinazoongelea suala zima la lugha. Ukitaka kujua mtu kama anafikiri sawasawa, msikilize anavyotumia lugha. Matumizi ya lugha fasaha ndiyo njia rahisi kabisa kisaikolojia kutambua uwezo wa mtu wa kufikiri na kupambanua mambo. Kama huwezi kutumia lugha sawasawa, hatuwezi kujua kile ambacho unakifikiri. Sasa tumebishana miaka mingi sana juu ya lugha gani itumike katika suala zima la kufundishia na mimi sitaki sitaki kuendeleza mabishano hayo. Ninachotaka kusema hapa ni kwamba hatuna option. Lazima watu wetu wajue lugha. Sasa hivi, mimi nafundisha hapa, walimu tunaenda kufundisha madarasani na wanafunzi wetu wanaenda kwenye semina. Wote tunatoka majasho, wakati mwingine unakuta mtu anatoka jasho unafikiri ni kwa sababu ya joto, lakini mateso ya lugha aliyokuwa anahangaika nayo darasani. Unampa mwanafunzi ku present semina anazunguka, ukimpa nafasi ya Kiswahili saa hiyohiyo utaona atakachokifanya! Kwa hivyo kwa sababau nyie nyie ambao mnasoma si ndio nyie mtakuwa walimu? Kama leo hukijui Kiingereza hakuna muujiza eti utakuja kukijua Kiingereza utakapokuwa mwalimu! Wewe kama hujui utakuwa hujui tu. Utaongeza vocabulary kidogo lakini lugha utakuwa huijui. Sasa tunafundisha, tunasoma bila raha mmekunja nyuso. Mambo ya kufundisha ni ya raha, ufundishe watu wacheke watu wafurahi. Sasa kama tunaona hili suala la kutumia Kiswahili limeshindikana basi jamani tujitahidi tufundishwe Kiingereza tukijue sawasawa. Kwa sababu hili jambo tumebishana watu wametoa mapendekezo, watu wameandika tafiti nyingi, watu wengi wamekubali isipokuwa mtu mmoja tu. Serikali peke yake ndiyo haijakubali kwamba tunaweza kwenda kwenye Kiswahili. Mimi nikisoma makala yoyote hakuna hata mtu mmoja ambaye amesema hakuna Kiswahili; sana sana walimu wawili wa-tatu, na wenyewe kwa sababu zao. Sasa tutaendelea kubishana mpaka lini suala la lugha hili? Basi kama limeshindikana tuwafanye, na mimi naamini watan-zania ni kama watu wengine wanauwezo wa kujifunza, wapewe fursa ya kujifunza Kiingereza wakijue. Na watanzania wanakipenda sana Kiingereza! Si unaona hata hapo mmeandika Reserve Seat! Kwani kulikuwa na ugumu gani kuandika Kiswahili hapo. Nenda kwenye restaurant kule Kariakoo ndani kabisa, chukua menu wameitwanga Kiingereza hata kama kimekosewa lakini Kiingereza: maharage and rice, wanakuwekea hapo bei! Angalia malori haya angalia nyuma lime-andikwa lugha gani? Kwa hiyo watanzania wanakipenda kiingereza lakini ukweli ni kwamba hawakijui. Sasa lazima tufanye mambo mawili: moja ama tukubaliane na mapendekezo ya wataalamu wote ambao wamekwisha

kueleza tuachane na, na tunaposema tuachanae hatumaanishi tukitupe Kiingereza. Ukienda Norway watu wanakijua Ki-

ingereza kuliko sisi lakini wanatumia kinorway, wanatumia Norwegian. Tukubaliane na mapendekezo ya wataalamu, tu-

rudi kwenye Kiswahili, tutafanya kazi of course ili Kiswahili kikamilike kuwa lugha ya kisayansi. Tukihamishe, kuna mtu

mmoja alisema itoke kuwa lugha ya mashairi, iwe lugha ya kisayansi. Lakini mimi siamini kuwa Kiswahili ni lugha ya

mashairi tu Kiwahili kimebobea kimeiva na tuna kitengo kizima cha Kiswahili hapa.

Kama tunaendelea kuyakataa mapendekezo ya wataalamu wanafunzi wetu ni wazuri sana, maadamu tu awe anajua kwamba atafaulu ndilo taifa hilo tulilonalo. Yaani shida kubwa tuliyo nayo ni qualifications. Sifa za kitaaluma, siyo ujuzi. Kuna watu ukimwambia kwamba bwana wewe usiwe na wasiwasi utapata A, yupo tayari akalala aka-relax! “Sasa mimi nina shida gani, nimeshaahidiwa „A‟ ! Sasa katika utaratibu huu hatuoni hasara za kupoteza muda wa kusoma kupitia mi-gomo na migogoro inayoendelea katika vyuo vyetu kwa hiyo lazima tuimalize.

Page 29: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

29

Na migogoro na migomo katika chuo hiki kwa mfano imekuwepo miaka yote. Imekuwepo miaka yote na ni mikongwe kama ambavyo chuo ni kikongwe. Na tusitoe majibu rahisi kwa sababu kuna watu wanatoa majibu rahisi sana. Kwamba hawa wanafunzi wanachochewa na vyama vya siasa. Na vyama vya siasa ambavyo wanavyoviongelea ni vyama vya upin-zani. Haya ni majibu rahisi kwa sababu migomo ilikuwepo hata kabla ya vyama vingi. Mgomo wa kwanza mkubwa wa chuo hiki ulikuwa ni mwaka 1966, ukiongozwa na akina Samuel Sitta, walikuwa wanapinga sera ya JKT. Sasa mwaka 1966 kulikuwa na vyama vingi? Hamna. Migomo miaka ya sabini imetokea sana na baadaye miaka ya tisini. Tofauti kubwa iliyopo katika ya migomo ya wakati ule na ya sasa ni kwamba kipindi hicho wanafunzi walikuwa wana-gomea sera. Walikuwa wakigoma kupinga sera fulani. Miaka ya tisini, migomo iliyokuwepo ilikuwa inapinga sera ya uchangiaji wa gharama za elimu ya juu. Bahati nzuri kwa watawala, wanafunzi wetu wa siku hizi hawapingi sera. Ni bahati nzuri sana kwa sababu ni vigumu sana kupambana na mtu anayepinga sera. Kwa sababu maana yake ita-involve kubadili sera. Wanafunzi wa siku hizi kwa kweli wanapinga mambo rahisi. Wanataka na wenyewe wawe sehemu ya mgawanyo wa keki, waongezewe boom, sasa kwani kuongeza boom ni ngumu? Ngumu ni kubadilisha sera. Wanataka kujua kwa nini sijapewa mkopo, ukimpa mkopo yanai-sha; siyo? Kwa hiyo, sasa hivi, kwa maoni yangu, ni rahisi kushughulikia migomo ya sasa hivi kama watawala wakiwa thabiti na thubutu. Na migomo yote iliyotokea miaka ya elfu mbili na kuja huku chanzo chake ni mikopo tu ya wanafunzi. Wala wanafunzi hawa kwa bahati nzuri hawapingi Bodi ya mikopo, hawapingi sera ya kuchangia, wanachopinga ni kwamba kwa nini mimi nipate huyu asipate. Tena wakiangalia, kama juzi nilikuwa naongea na mwanafunzi mmoja mgomo wa juzi, wakaja wanafunzi wanne wamesoma shule moja. Mmoja amepata mkopo, watatu hawajapata. Very logically akaniam-bia, “Dokta hebu angalia, hawa watatu tumesoma shule moja, sitaitaja hiyo shule, mimi nimepata division three, huyu ka-pata division one hao wawili division two, wamekosa mikopo!” Mimi nina wazazi huyu hata wazazi hana. Sasa katika hali ya kawaida kwa mazingira hayo, mimi nimefaulu chini zaidi kuliko wewe, nina wazazi nawajua. Huyu ambaye amefaulu hajapata mkopo. Sasa unataka wanafunzi wasilalamike kwa nini? It is logical. Kwa hiyo unakuta kwamba hakuna sababu ya msingi ya huyu kunyimwa mkopo na huyu kupewa. Kwa hiyo tatizo kubwa tulilonalo katika vyuo vikuu sasa hivi ni suala zima la Bodi ya Mikopo kwa sababu BBodi hiyo imeshindwa kabisa kufanya kazi na nafikiri haina uwezo huo ambao imepewa kufanya kisheria. Na sababu kubwa sana ambayo imeifanya ishindwe ni kitu ni kwamba imeshindwa kabisa kuainisha vigezo vya kupata mikopo vilivyo bayana. Kwa sababu, tazama ile sheria iliyounda BBodi ya Mikopo. Ukienda kwenye sehemu ya 17 ya hiyo sheria inaanisha vigezo vya mtu vya kupata mkopo. Vipo vitano visikilize uone kama ni vigezo vya maana: Kigezo cha kwanza, uwe mtanzania. Is that a problem? wanafunzi waliopo katika shule zetu za sekondari zaidi ya asilimia 99.9 ni watanzania. Kwa hiyo hapa kila mtu ata-fit sio? Hili siyo tatizo. Cha pili, uwe umedahiliwa katika chuo kilichosajiliwa. Hiyo ni ngumu na yenyewe? Yaani upate admission kwenye vyuo vikuu siyo kazi ngumu siku hizi ambapo vyuo vikuu ni vingi. Kwa hiyo hii haiwezi kutenganisha. Cha tatu, uwe umeandika barua ya maombi. Sasa hii na lenyewe litakushinda? Ipo kwenye sheria, msome hiyo sheria ya BBodi ya Mikopo. Ya nne sasa, usiwe na chanzo cha fedha za kulipa gharama za masomo. Sasa si nitasema sina, kwani watanzania ambao hawana chanzo ni wachache si wengi sana hao. Na cha mwisho, uwe ni mwanafunzi anayeendelea na masomo na ambaye amefaulu masomo yake katika mwaka husika. Kwa maana kwamba ukifeli somo uka-sup au uka-disco, hutapewa mkopo. Sasa niambie katika hivi nani atakayekosa mkopo? Katika vigezo hivi kuna mtu wa kukosa mkopo?

Page 30: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

30

Kwa hiyo utakuta kwamba BBodi kimsingi haina vigezo bayana vya kuweza kutenganisha nani apate na nani asipate. Na

kwa nini BBodi imekuwa hivyo? Imekuwa hivyo kwa maoni yangu kwa sababu nyingi lakini nitaje chache.

Moja ni suala zima la mtazamo mkanganyiko kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wanaotoa mikopo au hawajui ama ha-waamini kama wanachokitoa ni mikopo. Sijui kama mnanielewa? Serikali, BBodi na vyombo vingine ama hawajui au ha-waamini kwamba kile wanachokitoa ni mikopo. Na kumbukeni kwamba suala la cost sharing lilishinikizwa na Benki ya Dunia, ilikuwa ni moja ya masharti. Kwa hiyo hakuna hata mtu mmoja ambaye kimsingi alikubaliana kwa dhati toka moyoni mwake kwamba ni sera sahihi. Tukaamua kufanya mambo ili waone kwamba tumekwisha kukubalina na masharti yao. Mkanganyiko wa pili, wanaopokea au kuomba mikopo nao ama hawajui au hawaamini kama wanachokipewa ni mikopo. Hakuna, hawa wanafunzi wengi wanaochukua mikopo, hakuna hata mmoja ukiongea nae anasema atalipa.Sisi wenyewe tunakatwa kwa sababu tupo katika taasisi za serikali. Basi wamenikata wala hawajawahi kuniambia, nimeona tu kwenye salary slip yangu kwamba hela inakatwa wala hawajawahi kuniandikia barua kwamba Kitila Mkumbo unadaiwa shilingi hizi, tutakukata kwa muda huu, saini hapa, hakuna. Na bahati nzuri sisi wakati tukisoma hatukuwahi kusaini ile mikataba ambayo mnasaini nyie. Kwa hiyo kimsingi ni huruma tu ya kwangu. Kama tungeamua kuwa serious tungeenda mahaka-mani na tungeishinda BBodi kwa kukata mishahara yetu kwa kuwa hawana kigezo cha kukata mishahara! Kwa hiyo Bodi haina mikakati, watu wengi sana ambao wamepokea mikopo hawarudshi. Pili, waliokopa hawana mpango wowote wa kulipa hilo deni wala sio kitu ambacho kinawahangaisha. Hakuna mtu am-baye anakaa anafikiri kwamba anadaiwa deni, hakuna. Kwa sababu tunafahamu kabisa kwamba deni ni liability. Ukiwa na

deni unafikiria ukimuona aliyekukopesha unahan-gaika nimwambieje leo. Leo waliokopa hawa ha-kuna hata mmoja anayefikiria eti kwamba mimi nadaiwa na Bodi. Kwa hiyo huo mtazamo ni ta-tizo kubwa sana. Kwa hiyo uwezo hafifu wa uten-daji wa Bodi unatuweka hapa tulipo. Na tatu, ni tatizo kubwa sana kutoa mikopo ku-toka Dar es Salaam. Huwezi kuwa na ufanisi wa nchi kubwa kama ya Tanzania kwa kutoa mikopo kutokea Dar es Salaam. Ndiyo maana hawawezi kuwa na vigezo. Utanijua vipi mimi niliyetokea huko Iramba ndani sana, utanijua vipi? Na watan-zania hawa leo anaweza kujifanya tajiri kesho maskini wa kutupa. Tajiri tu kwa sababu eti ana hela kidogo kwa sababu eti nimeajiriwa kesho seri-kali ikininyang‟anya ajira kwisha habari yangu. Itabidi nikapige magoti kwa Betty kwamba naomba kazi hapo HakiElimu. Kwa hiyo in the next six months kama sina ajira niko hoi. Sasa utaniambia mimi ni tajiri? Kwa hiyo hakuna kitu cha maana hapo.

Sasa tufanye nini kuhusu hili, mimi nina mapendekezo matatu muhimu sana, ambayo nafikiri tukiweza kuyatekeleza

yanaweza ikatusaidia kwenye suala hili.

Kwanza, inabidi tukubaliane kwa dhati kabisa kwamba tulipofika haiwezekani kwa serikali peke yake kugharamia elimu

ya juu asilimia 100. It is impssible. Na mimi nimejiridhisha hivyo. Gharama za chuo kikuu ni kubwa kumsomesjha mwana-

fuzi mmoja katika level ya chuo kikuu. Nilikuwa nasoma utafiti mmoja kuhusu kuwasomesha wanafunzi zaidi ya mia

kwenye level ya shule ya msingi

Dk. Kitila Mkumbo kushoto pamoja na Mwenyekiti wa

Kongamano Ayub Rioba wakifurahia jambo na mmoja wa

washiriki.

Page 31: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

31

Gharama ya kumsomesha chuo kikuu ni gharama kubwa. Na kwa nchi hizi maskini tutajidanganya kwamba eti kuna seri-kali yoyote itakayokuja kuweza kutoa elimu ya juu bure. Inaweza ikiamua kuwa na chuo kikuu kimoja tu, kama Chuo Ki-kuu cha Dar Es Salaam. Lakini kama tukitaka kwenda sambamba na wenzetu wakenya, waganda kwa maana ya kupanua fursa ya elimu ya juu,hatuwezi. Sasa hivi tumefikia asilimia 3 ya wahitimu wa sekondari. Wenzetu wanaongelea zaidi ya asilimi 10. Ni aibu katika nchi kubwa kama hii. Kwa hiyo lazima upanuzi wa elimu ya juu uendelee, na kama utaendelea haiwezekani kabisa serikali yeyote itakayokuja ikawa na miujiza ya kusomesha watu wote bure kabisa asilimia 100. Kwa hiyo hicho ni kitu cha kwanza ambacho lazima tushawishiane kwa ushahidi wa dhati na kila mtu akaelewa hivyo. Tukisha kuelewana hapo then tukubaliane ni namna gani ya kuweza ku-finance elimu ya juu. Ili kila mtu awe na fursa. Na mimi nina mapendekezo matatu katika hilo. Pendekezo la kwanza, nafikiri kwanza lazima serikali iwe na scholarship kwa wanafunzi wanaofanya vizuri sana. Hawa ni lazima wapate scholarship ya serikali masomo yale yalipiwe asilimia mia. Hiyo lengo lake ni moja tu, ni kuzawadia bidii. To reward efforts. Mfumo wetu uliopo sasa hivi hauzawadii bidii. Ndiyo maana mtu ana division three na mwingine ana divi-sion one, division three anapata mkopo division one hapati. Na ukiangalia socio- economic status yao haitofautiani sana. Hatuzawadii bidii. Ukishatoa scholarship ili mtoto aliyepo shule kule Iramba ajue ukombozi wangu peke yangu ni mimi kupata division one.…Hivyo mkombozi peke yake niliye nae ni mimi kusoma kwa bidii. Sasa hivi hakuna incentive yoyote kwa mwanafunzi kusoma kwa bidii. Anachotakiwa ni kupata kiwango cha ufaulu cha kawaida ili aweze kuchaguliwa chuo kikuu. Pili, lazima tuendelee kugharamia masomo kwa wale wanaosoma taaluma za huduma ambazo mafanikio binafsi huchu-kua muda mrefu. Taaluma zinatofautiana na hazitakuja kufanana. Ili taaluma inayoitwa ualimu duniani kote motivation yake siyo fedha. Hakuna nchi yeyote ambayo utaenda ukakuta kwamba eti taaluma ya ualimu inalipwa vizuri zaidi kuliko zingine. Ni kwa sababu motivation ya kuwa mwalimu cha kwanza kabisa siyo fedha. Na hata sisi tuliojiunga hapa na wen-zetu waliojiunga kule commerce. Mmoja alikuwa anasema mwenzangu ameenda BoT kama mimi nilikuwa namzidi na amelipwa hivi. Nikamwambia ungeenda BoT. Kwa sababu sisi hapa kuna vitu vinatu-motivate kubaki kufundisha chuo kikuu, sio fedha. Ingekuwa ni fedha hakuna ambaye angebaki hapa. Sasa zile taaluma ambazo kwa kweli private returns zinapatikana baada ya muda mrefu lazima ziweze kupewa kipaumbele. Na hizi taaluma tunaongelea taaluma za ualimu, udaktari na zile ambazo zinahusiana na hizo. Hizi ni taaluma muhimu sana katika jamii kwa sababu ni za utumishi; ni taaluma za huduma. Mtu mwingine akitoka hapa akaenda kule anaanza kupata faida yeye haraka kabla hata serikali haijaanza kupata faida.

Lakini kwenye ualimu anayeanza kupata faida kwanza ni jamii na serkali kabla ya wewe kuanza kupata faida. Wakati taa-

luma zingine, kama sheria, likely utaanza kupata faida wewe uliyesoma kabla ya jamii iliyokusomesha haijaanza kupata

faida. Sasa taaluma kama hizi lazima zipewe kipaumbele ama wanafunzi wanaosomea haya masomo wapate scholarship

au wapewe kipaumbele katika kupata mikopo.

Na ya mwisho ni hiyo ya mikopo. Lakini mikopo itolewe katika ngazi ya wilaya na kupitia taasisi ambazo zinafahamu shughuli za kibenki na kifedha. Kwa mfano, kama tungeingia mkataba na NMB, benki ambayo ipo katika kila wilaya, wale wakipewa motisha maalumu na serikali, wakasamehewa baadhi ya mambo fulani ikiwemo kodi, wana uwezo wa ku-jua Kitila Mkumbo anatoka wapi, kijiji gani, na wazazi wake kina nani, na wana nini, kiasi kwamba wakimpa mtu mkopo wanaingia naye mkataba usipolipa ndani ya miaka fulani baada ya kumaliza chuo anafahamu kwamba kale kashamba ka bibi yake kanakwenda kufilisiwa, kwa sababu kila mtu ana ka mali fulani. Ninapotoka mimi tunathamini sana mashamba. Na ungemwambia bibi yangu kwangu shamba lake linakuja kuuzwa kwa

sababu ya mkopo, asingekubali angefanya jitihada aanze kulipa kidogo kidogo. Vigezo lazima viainishwe vizuri na ukitoa

katika ngazi ya wilaya, wanauwezo wa kuweza kujua nani ana uwezo kiasi gani. Pi na watu wajue kwamba wanachochu-

kua ni mkopo na lazima kuna njia kabambe za kuwafanya warudishe hiyo mikopo, na lazima utoe mifano kama umesema

baada ya miaka mitano tangu uliposoma hujanza kulipa mkopo wako ni kosa la jinai. Na ukiwakamata watu sita Mbeya,

saba Singida, nane Pwani, kumi Kagera, unawafunga kwa kushindwa kulipa deni walilosomea. Uta-send message.

Page 32: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

32

Nchi za wenzetu zinazotoa mikopo mzazi anafanya bidii kuhakikisha kwamba anamuepusha mtoto wake kupata mkopo wa elimu ya juu kwa sababu ni kifungo cha ajabu. Ukishakuwa na mkopo wa elimu ya juu una miaka ishirini ya kuulipa. Kwa hiyo wazazi wote wenye akili wanafanya kazi ya bidii kuhakikisha watoto wao hawaingii kwenye mnyororo wa mkopo wa elimu ya juu. Matokeo yake ni kwamba wanaopata mikopo ni wale tu ambao kwa kweli wanastahili na hawana uwezo kwa namna yeyote kuweza kulipa elimu ya watoto wao. Lakini hapa kwetu wenye uwezo na aliye nao anakimbilia mikopo kwa sababu ni cha bure. Na Makweta ameonesha kwenye paper yake kwamba mtu amesomesha watoto wake tangu nursery mpaka sekondari kwa kulipa mahela mengi, akija Chuo Kikuu cha Dar es Salaam milioni 1.6 kwa mwaka anakuambia hana huku alikuwa analipa dola 6,000 kwenye nursery school; hapa chuo kikuu hana! Sasa huyu mzazi ili aweze kuendelea kumlipia mtoto wake muoneshe kwamba mtoto wako kwa kuchukua mkopo anaji-ingiza kwenye kifungo cha kulipa deni miaka ishirini ijayo. Wazazi wenye uwezo, wenye akili zao watawaepusha watoto wao kuchukua mikopo. Na kwa utaratibu huo basi, miaka mingi ijayo tutakuwa na a very big revolving fund kama ilivyo kwa National Health Insurance Fund. Leo, wana mafedha mengi mpaka wanashindwa wayatumie vipi. Kwa sababu tunalipa na siyo lazima uugue. Na kwa utaratibu huo tunakuwa na fedha za kusomesha kizazi kijacho bila matatizo yoyote. Mimi nafikiri kwamba kwa mapendekezo haya matatu tukiyatekeleza, yakaboreshwa, yakafanyiwa tafiti, tunaweza tukajitoa katika mkanganyiko mkubwa wa namna ya kuboresha elimu. Nimalizie kwa sentensi za Mheshimiwa Makweta ili nimtendee haki. Ukurasa wake wa 12 anaeleza “sasa naelewa kwa nini V.I Lenin alisema matumizi ya nguvu ni lazima kwa mama aliyefikia siku za kujifungua. Kwa maneno yake Lenin alisema: “Force is the midwife of any society pregnant of a new one”. Kwa maoni yangu, Tanzania ni kama mama mjamzito ambaye siku zake za kujifungua zimefika lakini hajifungui. Bila kumpasua mama huyu wote wawili, yaani mama na mtoto wanaweza kufa, na tukimpasua, wote wawili wanaweza kuokolewa au angalau mmoja wao. Tanzania inahitaji, si maneno yangu, kupasuliwa. La sivyo itaendelea kudidimia kiu-chumi milele. Na mwisho anamalizia tafuteni kwanza maendeleo katika elimu na mengine yote yatafuata. Sasa shida moja ambayo nchi hii inayo ni utekelezaji. Wataalamu watasema, kila mtu atasema lakini hakuna kitakachofanyika. Profesa [Abdallah] Safari alinifundisha maneno matatu. Tulikuwa tunajadili jambo fulani akaniambia, “Kitila usihangaike haya majamaa ni mafed-huli”. Unajua maana ya ufedhuli? Ufedhuli ni kiwango cha juu cha ujeuri na ujeri ni kiwango cha juu cha kiburi. Kwa hiyo akaniambia kuna maneno matatu, kiburi, jeuri na ufedhuli. Ufedhuli ni kiwango cha juu kabisa cha ujeuri. Mimi ushauri wangu ni kwamba tubadilike. Ufedhuli wa kutokusikia wanayoyasema wataalamu utatuangamiza. Asanteni sana.

*Dk. Kitila Mkumbo, ni mwalimu aliyebobea katika masuala ya saikolojia. Pia ni Mkuu wa Kitengo cha Saiko-

lojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

.

Page 33: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

33

.

Hoja za Wachangiaji Mara baada ya wazungumzaji wote kuhitimisha hotuba wachangangiaji wengine walipata fursa ya kuchangia mambo mbalimbali katika kongamano hilo. Michango hiyo imeainishwa hapa chini: Mchangiaji wa kwanza alikuwa ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliyeuliza maswali na kutoa

michango ifuatayo:- Kwa nini HakiElimu haijihusishi na elimu ya juu ingawa kuna matatizo chungu nzima? Pia alitofau-

tiana na pendekezo la Dkt Kitila la kuwapatia mishahara mizuri taaluma zinazohusika na kutoa huduma kwani ni kama

kuwapendelea na inaweza kuchochea mapambano. Mwisho alipendekeza kuwa ni muhimu kuwasomesha wanafunzi

katika vyuo vya umma bure kwani kuna fedha nyingi bali hutumika katika masuala yasiyo ya msingi.

Ndugu Mutembei- ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili alitoa mapendekezo yafuatayo: Mawaziri wasiwe wabunge ili kuepuka suala la kuchanganya taaluma na siasa. Alisema suala la mawaziri kuwa wanasiasa ndilo linafanya mapende-kezo mazuri ya watalaamu yasifanyiwe kazi. Pia ali-washukia watalaamu nchini kwa kupingana wao kwa wao na hivyo kushindwa kuwa wajasiri kuishauri seri-kali juu ya sera ya elimu kuhusu lugha ya kufundishia. Alisema kushindwa kuruhusu lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia ni sawa na kuhalalisha mauaji ya halaiki na kwamba historia itatusuta.Aidha, alitoa an-galizo kwa wasomi kuwa na msimamo katika masuala ya kisera pindi wanapotoa ushauri kwa serikali kwani wengi husaliti ukweli. Ndugu Ramadhani Uda, Rafiki wa Elimu kutoka Tanga anasema: Maamuzi ya serikali katika suala la

elimu yazingatie tafiti kwani athari zake ni kubwa kwa jamii. Akirejerea miaka ya 1990 serikali ilipositisha kuwapa nafasi za kusoma wanafunzi wenye uwezo na wengi wao waliangukia katika biashara haramu kama madawa ya kulevya. Mwalimu Clara: Alinaunga mkono hoja ya kuchagua Lugha moja kwa ajili ya kufundishia.Lakini pia anatoa angalizo kwa watunga sera na wahamasishaji kuwa wanapoondoa jambo fulani katika elimu wajaribu kutafuta mbadala wake. Kwa mfano walipoondoa adhabu ya viboko wangekuja na mbadala wake. Dk. Martha Qorro, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliuliza maswali mengi: Ili elimu iwe mu-himu tunahitaji vigezo vipi? suala la sera kutokuwa na tatizo lina ukweli? Nini misingi ya elimu yetu? Hivi sisi ni nani na tumetoka wapi na tunataka kwenda wapi? Baada ya maswali hayo alitoa mapendekezo yake ambayo ni pamoja na kuwa tuvunje mfumo wa elimu ya kukariri ambao alisema umewekwa na watawala ili waendelee kututawala. Alisema jambo hilo limejenga matabaka kwa kuwatenga wasomi na jamii na kuwafanya wataalamu wetu kuwa wabinafsi na kujiona kuwa ni watawala.Hivyo alisema elimu ya sasa ilenge kutatua matatizo ya jamii ili isitofautiane na mazingira ya kawaida.Pia ali-pendekeza Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia na Kiingereza kifundishwe tu kama somo. Ndugu Charles Nchimbi toka kikundi cha sanaa na ufundi cha watu wenye ulemavu. aliyeuliza kwa nini shule za wale-mavu hazipo na zilizopo hazina waalimu? Alipendekeza kuwepo shule za kufundisha lugha za alama ili kuwasaidia wale-mavu viziwi na wasiosikia.Aidha, alishauri kuwa tushirikiane ili tuweze kutatua matatizo ya mtanzania. Kevin kutoka KISUVITA alipendekeza katika katiba mpya liiingizwe suala la umuhimu wa kufundisha na kuwa alama za viziwi.

Kila mshiriki alitamani kupata fursa ya kuchangia hoja

kwenye Kongamano hilo.

Page 34: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

34

. Buyobe John Buyobe mwanafunzi wa shahada ya pili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikubaliana na mapendekezo kuwa ni muhimu kuwepo na taarifa za kutosha pamoja na uelewa wa kutosha miongoni mwa wanotarajiwa kutekeleza sera. Halima Mengele ambaye ni Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania,TENMET, alipendekeza kuwa tuishawishi seri-kali kwamba nchi ina rasilimali za kutosha. Alisema masharti magumu ya elimu mfano yale tuliyopewa na taasisi za kifedha za kimataifa kama IMF na Benki ya Dunia ni matokeo ya kutojitegemea katika bejeti. Pia suala la Lugha ya Kiswahili lipewe nafasi katika sera zetu. Pia jamii nzima ishirikiane katika suala la elimu; siyo kuiachia serikali pekee. Pia alisisitiza umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia kwa vile ni vizuri kumfikirisha mtu kiutalamu na kuwa mbunifu kwa lugha yake ya asili. Richard Damasi: kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yeye aliona kuwa matokeo mabaya katika elimu ni zao la kuge-uza sekta hiyo kama bidhaa ambayo hata hivyo asilimia kubwa ya viongozi ndiyo wamiliki wa shule hizo. Hivyo aliona mfumo wa elimu hauwezi kubadilishwa na viongozi kwani wana maslahi binafsi katika mfumo uliopo. Mongere, mwalimu kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini alitoa tahadhari juu ya suala la kuingia katika Lugha moja ya kufundishia yaani Kiswahili kama ilivyopendekezwa na baadhi ya wadau. Bahati kutoka chama cha waandishi wa habari za ukimwi aliona ni muhimu mitaala ikaongezewa somo la ukimwi kutoka ngazi za awali. Prudensi alisema uundwaji wa sera za elimu na watu wachache ndiyo unaozaaa sera mbovu.Hivyo ni muhimu uundwaji

wa sera za elimu uhusishe watu wengi zaidi.

Mwalimu kutoka Kisarawe alisema waalimu wanaojiendeleza wapandishwe madaraja ya mishahara kwa wakati. John John wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipendekeza kuwa elimu, ikiwa na ile ya kijima (informal education), ina-paswa kuangaliwa upya ili wale wasiopata elimu ya shuleni waweze kukabiliana na mazingira yao. Pia alipendekeza ku-wepo ukaribu baina ya wasomi na serikali. Mchangiaji amabaye hakutambulika kwa jina: alishauri kuwepo kwa taasisi za elimu zisizo za kiserikali pamoja na maafisa sera wa wilaya ili kuhakikisha kuwa sera zinazowekwa zinatekelezwa. Mwalimu Kisati Makwaya kutoka Msalato sekondari alishauri siasa zisiingilie masuala ya elimu. Mwanafunzi Azania Sekondari, aliona hakuna sababu ya kusherehekea miaka hamsini ya elimu tangu uhuru kwani changamoto zilizopo ni kubwa mno. Alipenda kuona wanasiasa wakizungumzia masuala muhimu ya elimu. Akitoa mfano alisema, ”Nilitegemea kuona NEC ikijadili kuhusu kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana lakini hakuna wana-chofanya zaidi ya kujadili magamba”

Page 35: Hali ya Elimu Tanzaniahakielimu.org/files/publications/miaka 50 ya Uhuru...ni kubwa. Mwaka huu peke yake tuna wasichana takri-bani 5,346 ambao wamekatisha masomo yao kwa sa-babu ya

35

.

HakiElimu inawezesha wananchi kuleta mabadiliko katika elimu na demokrasia.

SLP 79401 · Dar es Salaam · Tanzania. Simu (255 22) 2151852/3 · Faksi (25522) 2152449

[email protected] · www.hakielimu.org