WAZAZI NIPENDENI
NI MPANGO WA KITAIFA WA
UJUMBE MFUPI WA SIMU NA
VYOMBO VINGINE VYA HABARI
•Kuboresha afya ya mama, mtoto na familia
SABABU ZA MSINGI ZA KUSHIRIKI
Kuunga mkono mpango wa kitaifa wa eMTCT wa
kuondosha maambukizi ya VVU kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto ifikapo 2015.
Kuwafikia wanawake wote wanaohitaji uzazi wa
mpango
Malengo mahususi
Kuongeza idadi ya akina mama kuhudhuria kliniki mara tu anapojihisi mjamzito (kuanzia wiki ya 12)
Kuongeza idadi ya akina mama wajawazito na wenzi wao kupima maambukizi ya VVU na kupata huduma endelevu.
Kuongeza utumiaji wa huduma za kuzuia malaria kwa akina mama wajawazito.
Kuhamasisha familia matumizi ya lishe bora
Kuongeza idadi ya akina mama wanaojifungua katika vituo vya kutolea huduma.
Kuhamasisha familia kuandaa mpango binafsi wa kujifungua
Kuhamasisha huduma endelevu kwa mtoto.
UTEKELEZAJI WA MPANGO HUU
Kushirikisha kamati ya afya Mkoa, Wilaya
na watoa huduma katika mpango huu.
Kuwaelekeza watoa huduma wa afya ya uzazi na mtoto ili kuwasaidia akina mama na familia kutumia huduma hii.
Kushirikisha wilaya na mikoa katika kusimamia, kutekeleza na kuendeleza huduma hii.
Huduma ya ujumbe mfupi wa simu kwa Afya ya mama
Huduma ya bure ya ujumbe mfupi wa
simu wenye kuboresha afya ya
mama mjamzito na familia
Kampeni ya Wazazi nipendeni katika matangazo ya vyombo vya habari.
Kuanzia Novemba 2012 hadi Juni 2013
Vyombo vya habari ni pamoja na:
LUNINGA
Matangazo zaidi ya 6,000 ya luninga yatarushwa kupitia
vituo 7 vya habari
1. Luninga i. Dawa tahadhari ya malaria (SP)
Bofya hapa uone sinema
1 2 3
4 5 6
Bofya hapa uone sinema
1.Luninga
iii. Mkakati wa Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT)
1 2 3
6 4 5
Matangazo ya redio zaidi ya 28,000 yatarushwa kupitia vituo 21.
2. RADIO
Bofya hapa kusikiliza redio
Ujauzito
PMTCT
SP
Malaria
Kujifungua
3. Mabango: Bango la ukutani - Poster Kuna aina 2 ambayo yatagawiwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. 5 hospitali, 4 Kituo cha Afya, 2 Zahanati kwa kila aina ya bango.
4. Mabango: 3,000 yanayohamishika yatasambazwa kupitia wadau. 2 kila wilaya na yatawekwa mahali penye mikusanyika ya watu wengi
5. Vipeperushi
Zaidi ya vipeperushi milioni 1.2 vya mpango binafsi wa kujifungua salama vitagawiwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. 2,500 hospitali, 500 Kituo
cha Afya na 125 Zahanati
5. Vipeperushi: Mpango binafsi wa kujifungua salama
• Kipeperushi cha mpango binafsi wa kujifungua salama ni kwa ajili ya mjamzito na mwenzi wake kujaza wakiwa na mhudumu wa afya kwa maandalizi ya kujifungua salama. • Kipeperushi hiki si cha kugawiwa kwa kila mtu bali ni kwa ajili ya walengwa tu ambao ni wajawazito wanaofika kliniki
6. Gurudumu la ujauzito – pregnancy wheel
•Gurudumu la kukokotoa umri wa ujauzito ni kitendea kazi cha watoa huduma wa afya. Gurudumu hili litakusaidia kukadiria tarehe ya kujifungua kutokana na tarehe ambayo mimba imetungwa. •Mtoa huduma atatumia gurudumu hili kujua taarifa muhimu kama tarehe ya kupata SP, tarehe ya kliniki na lini mtoto ataanza kucheza tumboni nk. Mgawanyo wake ni 2 hospitali, 2 kituo cha afya na zahanati 1
& WheelCalendar months Back
7. Kadi ya kukumbusha kurudi kliniki kupata dozi ya SP Kadi hii ni kwa ajili ya kuwapatia wajawazito, mtoa huduma huijaza na kumpa mjazito ikionyesha jina na tarehe atakayokuja tena kwa dozi ya pili ya SP. Mgawanyo ni, 2,500 hospital, 500 kituo cha afya na 125 zahanati
8. Bumper Sticker
• Stickers zinazohamasisha kampeni ya Wazazi Nipendeni zinaweza kugandishwa kwenye magari yakiwemo daladala, malori, mabasi, bajaj, pikipiki, kwenye majengo na sehemu za wazi zenye mikusanyiko ya watu. •Kila mdau atapewa sticker 100 kwa kila wilaya.
9. Bango la nyuma ya gari
Mabango 3 makubwa na 3 madogo yatagawiwa kwa wadau
Wheel Cover
Tuma SMS neno “mtoto” BURE kwenda
15001 kwa taarifa zaidi
Tuma SMS neno “m toto” BURE kwenda
15001 kwa taarifa za idi
Fomu ya kufuatilia ugawaji wa vitendea kazi
Huduma ya ujumbe mfupi wa simu kwa Afya ya mama
SMS neno “mtoto” kwenda 15001 Huduma hii ni bure kwa mitandaoo yote
Mtumiaji wa huduma hii atapokea ujumbe kumkumbusha kuhusu huduma anazotakiwa kupata kwa wakati huo, dondoo za afya zinazohusu hali yake na muda wa ujauzito. Una weza kujisajili kama:
Mama mjamzito ukizingatia umri wa uja-uzito, kwa miezi au wiki Msaidizi wa mama mjamzito Mama mwenye mtoto mchanga mpaka wiki 16 Msaidizi wa mama mwenye mtoto mchanga Mdau au mtu uliyeguswa kuhusu Afya ya ujauzito na uzazi salama
Usaidizi muda wa kujifungua kwa kupitia ujumbe mfupi wa simu utakaosisitiza umuhimu wa kujifungulia kliniki, unyonyeshaji salama na kadhalika.
Ujumbe mfupi wa simu atakaotumiwa mjamzito utahusu: kumkumbusha muda wa kwenda kliniki; utumiaji sahihi wa dawa; usalama wake na ushauri kuhusu lishe, taarifa zote zikimfikia kwa kuzingatia hatua ya ujauzito aliyoifikia.
Huduma baada ya kujifungua: kutoa taarifa kuhusu uzazi wa mpango, lishe, chanjo, na malezi bora ya kifamilia.
Ahsanteni