darasa vii kazi ya nyumbani kiswahili jina la … · kuwa makini na covid-19 nawa mikono yako kila...

17
KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020 WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI DARASA VII KAZI YA NYUMBANI KISWAHILI JINA LA MWANAFUNZI: _____________________ MAELEKEZO 1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi. 2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo. 3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu. SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098 Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com) “Quality Education for the New Generation”

Upload: others

Post on 04-Jul-2020

161 views

Category:

Documents


1 download

TRANSCRIPT

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

WIZARA YA ELIMU SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI

DARASA VII – KAZI YA NYUMBANI

KISWAHILI

JINA LA MWANAFUNZI: _____________________

MAELEKEZO

1. Kumbuka kuandika majina yako matatu kwa usahihi.

2. Jibu maswali yoe kulingana na maelekezo.

3. Soma maswali kwa ufasaha kabla ya kuyajibu.

SHULE YA MSINGI MARTIN LUTHER S. L. P 1786 Dodoma. Simu. +255 26 2395029, +255 784 449098

Fax +255 26 2395030 (www.martinlutherschooldodoma.com)

“Quality Education for the New Generation”

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

SEHEMU “A” SARUFI Chagua herufi ya jibu sahihi.

1. Wiliam na Omega wanatembea kivivu. Neno “kivivu” limetumika kama aina ipi ya maneno?................ A. kionyeshi B. kiwakilishi C. kielezi D. kivumishi E. nomino [ ]

2. Umoja wa sentensi “Ng’ombe wetu wanatoa maziwa mengi” ni upi? A. Ng’ombe yangu inatoa maziwa kidogo B. Ng’ombe yangu anatoa maziwa kidogo C. Ng’ombe lenu linatoa maziwa kidogo

D. Ng’ombe wangu inatoa maziwa kidogo E. Ng’ombe wangu anatoa maziwa kidogo [ ] 3. Ili nifaulu mtihani wangu vizuri…................nijifunze kwa umakini.

A. bidii B. ni budi C. sina budi D. siyo budi E. si budi [ ] 4. Viongozi wanatuhimiza tufanya utundu wa kisayansi. Neno “utundu” limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. nomino B. sifa C. kivumishi D. kiwakilishi E. kielezi [ ]

5. Neno lipo linakamilisha sentensi hii? “Waziri aliwataka wananchi waudhibiti uchumi wao ili……na mabepari” A. usiasiliwe B. usiadhiriwe C. usiashiriwe D. usiathiliwe E. usiathiriwe [ ]

6. Sentensi ifuatayo ipo katika kauli ipi? Shule yetu imeharibiwa na upepo. A. kutenda B. kutendeana C. kutendana D. kutendwa E. kutendea [ ]

7. Ipi ni sentensi iliyo katika kauli taarifa? A. Tafathali nichinjie kuku wangu B. Nichinjie kuku wangu C. Aliniomba nimchinjie kuku wake D. Mchinje kuku huyo tafadhali E. Kwa nini unanichinjia kuku wangu? [ ]

8. Alisema yeye hatakwenda, sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo inabadili kauli taarifa kuwa kauli halisi

A. Alisema haendi B. Alisema yeye hataenda C. Mimi sitaenda D. Kuwa sitaenda E. Alisema mimi nitaenda [ ] 9. “Tunasoma” katika neno tunasoma kiambishi cha wakati ni kipi? A. tu- B. –na- C. –so- D. –ma E. –nas- [ ] 10. Kilichomfanya……….ni woga. A. alikimbia B. angekimbia C. akakimbia D. akimbie E. tukakimbia [ ] 11. Nilikutana na rafiki yangu nimpendaye akitembea barabarani. Katika sentensi hii ni neno lipi limetumika kama

kielezi?.............. A. barabarani B. yangu C. nilikutana D. na E. nimpendaye [ ] 12. Kama John angalisoma kwa bidii……… A. angefaulu mtihani B. angalifaulu mtihani

C. angelifaulu mtihani D. angifaulu mtihani E. angalifaulishwa mtihani [ ] 13. Wewe ni kijana mdogo. Neno wewe katika sentensi hii lipo katika nafsi gani? A. nafsi ya kwanza umoja

B. nafsi ya pili wingi C. nafsi ya tatu wingi D. nafsi ya kwanza wingi E. nafsi ya pili umoja [ ] 14. Sara na Sofia ni wanafunzi wa darasa la saba. Neno “na” limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. nomino B. kiunganishi C. kielezi D. kitenzi E. kisifa [ ]

15. Alisema yeye hana ubaya na mtu. Neno lililotumika kama kiwakilishi katika sentensi hii ni lipi?

A. yeye B. mtu C. ubaya D. hana E. alisema [ ]

16. Sudi na Selina “wanapigana” Neno lililopigiwa mstari lipo katika kauli ipi? A. kutendwa B. kutendana C. kutendewa D. kutendea E. kutendeana [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

17. Kamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi. Ingawa walipata shida nyingi njiani……….walifika salama. A. hatimaye B. ingawaje C. ingawa D. hitima E. yatimaze [ ]

18. Neno lipi lina kamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi kati ya haya yafuatayo? …….. Jumatatu tulipoanza mtihani”

A. itakuwa B. ilikuwa C. ifikapo D. ifikiapo E. ilikuwepo [ ] 19. Tukitaka kupata mazao mengi…………….…tutumie mbolea.

A. ni budi B. si budi C. tuna budi D. budi E. hatuna budi [ ] 20. “Kiranja wetu wa darasa alikwenda dukani……….alikatazwa na mwalimu. Neno lipi linakamilisha sentensi hiyo?

A. ila B. lakini C. ingawa D. isipokuwa E. kwa [ ] 21. “Kitabu ulichonipa kina kurasa chache” katika sentensi hii maneno yaliyopigiwa mstari yana wakilisha nini?

A. kishazi tegemezi B. kishazi huru C. kishazi ambatano D. kirai E. kielezi [ ] 22. “Kobe anatembea taratibu” Neno taratibu ni aina ipi ya maneno?

A. kivumishi B. Nomino C. kiwakilishi D. kielezi E. kitenzi [ ] 23. Vibaya pia vimenunuliwa. Neno “vibaya” katika sentensi hii limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. kivumishi B. kiwakilishi C. Nomino D. kitenzi E. kielezi [ ] 24. “Mama anaendesha gari”. Herufi iliyopigiwa mstari inawakilisha kiambishi cha aina gani katika kitenzi anaendesha?

A. Tamati B. Tendo C. Wakati D. Rejeshi E. Nafsi [ ] 25. Sentensi isemayo “Ukinisaidia nitakusaidia” ni aina ipi ya sentensi?

A. changamano B. sahihi C. ambatano D. shurutia E. mseto [ ] 26. Huyu si ndugu yangu. Katika sentensi hii neno “si” ni aina ipi ya maneno?

A. kitenzi kikuu B. kelezi C. ketenzi kisaidizi D. kitenzi kishirikishi E. kelezi kivumishi [ ] 27. Alitembea…………..miguu kutoka shuleni hadi nyumbani. A. kwa B. na C. wa D. cha E. pa [ ] 28. Mtoto huyu alikuwa na bidii darasani……….hakufaulu mtihani.

A. hivyo B. hata lau C. walau D. angalau E. hata hivyo [ ] 29. Watu wale……….waliomsimamisha Sofia. A. ndiye B. ndiyo C. ndo D. ndio E. nd [ ] 30. Kama ungaliniomba kitabu kile…………… A. ningalikupa B. ningelikupa C. ningekupa D. nitakupa E. nakupa [ ] 31. Hadi sasa hakuna mtu……………..aliyekamatwa kuhusika na wizi ule.

A. yoyote B. wowote C. yeyote D. yote E. vyovyote [ ] 32. Mwalimu aliwataka wanafunzi wamsikilize kwa makini sentensi hii ipo katika kauli ipi?

A. taarifa B. halisi C. kutendwa D. kutendana E. kutendewa [ ] 33. Tulimkuta rafiki yetu amelewa chakari. Katika sentensi hii neno chakari limetumika kama aina gani ya maneno?

A. Nomino B. kielezi C. kiunganishi D. kiwakilishi E. kitenzi [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

34. Katika neno “sikujua” kiambishi kipi ni kikanushi? A. -siku- B. -jua- C. -a D. -ku- E. si- [ ] 35. Jeni amenunua gari: Hii ni aina gani ya sentensi?

A. fupi B. changamano C. sahili D. ambatano E. shurutia [ ]

36. Tangu tupate uhuru hatunyanyaswi tena kama……….kabla ya kujitawala.

A. inavyokuwa B. iliyokuwa C. itakavyokuwa D. ilivyokuwa E. ilivyo [ ]

37. Wingi wa maneno “mtoto huyu hana adabu” ni upi? A. watoto wale hawana adabu B. watoto hawa hawana adabu C. watoto huyu hana miadabu D. watoto vyote havina adabu E. watoto wote hawana adabu [ ]

38. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo ipo katika kauli taarifa?

A. Mzee amesema kwamba nimechoka kusikiliza mazungumzo B. Mzee amesema nimechoka kusikiliza mazungumzo C. Mzee amesema kuwa tumechoka kusikiliza mazungumzo D. Mzee amesema kwamba amechoka kusikiliza mazungumzo E. Mzee amesema nimechoka mazungumzo [ ]

39. “Twendeni nyumbani sasa” sentensi hii ipo katika kauli ipi?

A. taarifa B. shurutia C. ulizo D. mshangao E. halisi [ ] 40. Kitenzi kutokana na neno msomaji ni…………..…. A. kulima B. kusoma C. kupekua D. kuhariri E. kutangaza [ ] 41. Mvua kubwa ilinyesha lakini watoto waliendelea kucheza mpira. Neno “lakini” limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. kiunganishi B. nomino C.kitenzi D. kivumishi E. kiwakilishi [ ] 42. “Kichwa kinaniuma” alisema Ana. Sentensi ipi kati ya hizi zifuatazo inabadili kauli hii kuwa kauli taarifa? Alisema kuwa

kichwa…………. A. kinaumwa B. kinamuumiza C. kinauma D. kinaumia E. kinamuuma [ ] 43. Mkutano mkuu wa chama………………mwaka kesho.

A. ulifanyika B. utafanyika C. umefanyika D. unafanyika E. ungefanyika [ ] 44. Niliwanunulia watoto wangu vitabu safi. Neno “wangu” limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. nomino B. kiungo C. kitenzi D. kiwakilishi E. kivumishi [ ] 45. Habari gani ndugu?............hujapata nafuu bado? A. ebu B. la C. Je, D. Eti E. au [ ] 46. Majambazi na polisi walikuwa wanatupiana risasi. Sentensi hii ipo katika kauli ipi?.........

A. kutendana B. kutendeana C. kutenda D. kutendeka E. kutendwa [ ] 47. Kaa anakimbia upande upande. Neno lililo pigiwa mstari limetumika kama aina ipi ya maneno?

A. kitenzi B. kivumishi C. kiwakilishi D. kiunganishi E. kielezi [ ]

48. Farida na dada yake wanapendana sana. Katika sentensi hii ni kauli ipi ya utendaji imetumika? A. kutenda B. kutendewa C. ktendea D. kutendana E. kutendwa [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

49. ………….kusoma kwa bidii ili tupate maarifa mengi. Neno lipi linakamilisha sentensi hii? A. Tunapasiwa B. Tunapashwa C. Tunapaswa D. Tunapasua E. Tunapasha [ ]

50. Kutokuwa na uvumilivu kumemfanya Chale aache kazi. Neno “uvumilivu” hapa limetumika kama aina ipi ya maneno? A. kivumishi B. kisifa C. kiungo D. nomino E. kiwakilishi [ ]

51. Ni nomino ipi inatokana na kitenzi “nakili”………… A. nakala B. kunakili C. kula D. lika E. nauli [ ] 52. Haaa! Unakula udongo. Neno haaa! Limetumika kama aina gani ya maneno?

A. kihisishi B. kitenzi C. kivumishi D. kielezi E. nomino [ ] 53. “Kamba ya mbuzi imeliwa na mchwa” sentensi hii ipo katika kauli ipi?

A. kutendana B. kutendwa C. kutendeana D. utenda E. kutendewa [ ] 54. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo kwa ushaihi? Mjumbe wetu………mchango wetu kwa mwenyekiti.

A. aliahirisha B. aliwakilisha C. aliwasilisha D. aliasilisha E. aliwasirisha [ ] 55. Sipendi uongo. Sentensi hii ipo katika nafsi ipi?

A. ya kwanza wingi B. ya tatu umoja C. ya kwanza umoja D. ya pili umoja E. ya tatu wingi [ ] SEHEMU “B”: MSAMIATI Chagua herufi ya jibu sahihi.

56. …………kwamba wananchi wengi wanajua kusoma na kuandika. Neno linalokamilisha sentensi hii ni lipi? A. Imedhirika B. Imedhihirika C. Emethihilika D. Imesihirika E. Imezihirika [ ]

57. Neno lipi lina maana sawa na mwanamke mzee? A. shabibu B. ajuza C. shaibu D. kigori E. kigego [ ] 58. Upepo mkali uwezao kuezua nyumba na hata kuharibu vyombo vya baharini huitwa………..

A. karakana B. gharika C. tufani D. ghasia E. kaidi [ ] 59. Lipi kati ya maneno yafuatayo halilandani na mengine? A. paa B. kipeto C. ukuta D. dari E. sakafu [ ] 60. Neno lipi linajumuisha maneno bunduki, sime, rungu, mkuki, mshale……………..….

A. vyuma B. madini C. dhahabu D. silaha E. kifo [ ] 61. Mahakama itabidi………….matokeo ya uchaguzi baada ya mlalamikaji kushinda kesi.

A. ibainishe B. isitokee C. lainishe D. ibadhilishe E. ibatilishe [ ] 62. Kinyume cha neno ahirisha ni kipi?.......... A. tekereza B. agiza C. simamisha D. tekeleza E. telekeza [ ] 63. Tendo la mtu kurudi kutoka mahali Fulani huitwaje?

A. kulegea B. kuelekea C. kurejea D. kupwekea E. kuelea [ ] 64. Ingawa mzee Maganga aliharibiwa vitu vyote hakutaka kudai…………………..

A. fidia B. rushwa C. faida D. hongo E. sheria [ ] 65. Kinyume cha neno TAWANYA ni………. A. punguza B. anua C. changanya D. kusanya E. eneza [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

66. ...................................ni aina ya wavu wakuvulia samaki. A. mgono B. jarife C. ndoano D. dema E. chambo [ ]

67. Kisawe cha neno SURIAMA ni ....... A. zeruzeru B. albino C. mkimbizi D. chotara E. mzungu [ ]

68. Maneno yapi yanaonyesha kuacha tabia nzuri na kufuata tabia mbaya?.... A. geuka nyuma B. kosa adhabu C. utovu wa nidhamu D. kengeuka E. kuwa na nidhamu [ ]

69. Hali inayoridhisha ni hali..... A. makini B. fasaha C. adimu D. adimika E. maridhawa [ ]

70. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi, Kitu...... ni kitu cha thamani. A. dhahili B. dalili C. pomoni D. azizi E. kitenge [ ]

71. Maendeleo hayawezi kuja nchini kama hakuna.......... A. utengano B. udhaifu C. mafarakano D. ubadhilifu E. utengamano [ ]

72. Mtu asiye na huruma wala asiyetenda haki ni mtu A. mdhalilishaji B. dhalimu C. mdanganyifu D. kachero E. mzuri [ ]

73. Sara alijitoa…....kumwokoa ndugu yake. A. mhanga B. kifafa C. ndimi D. uuguzi E. kirumi [ ]

74. Nondo ni kipande chembamba cha chuma, pia ni..... A. aina ya ndege B. ugonjwa wa ngozi C. kupinda mgongo D. mdudu kama kipepeo E. mti wa matunda [ ]

75. Chukua ……utwange hiyo mihogo kwenye kinu. A. mcha B. miche C. mchi D. mchwe E. machu [ ]

76. Rais, Wabunge, Madiwani, huitwa waheshimiwa. Je Meya huitwaje? A. kadhi B. bosi C. mfadhili D. mgeni E. mstahiki [ ]

77. Sina nasaba na Pendo. Maana yake ni nini? A. si rafiki B. simfahamu C. sina undugu D. simpendi E. toinyo [ ]

78. Alijifanya .... kwa kuvua nguo mbele za watu. A. hayawani B. upatu C. punde D. mkutubi E. mhunzi [ ]

79. Sitakuwa na “soni” kuwaadhibu wanafunzi watoro. Neno soni lina maana ya.... A. uongo B. haya C. imani D. ukweli E. uwongo [ ]

80. Neema alilala huku akiwa amejifunika gubigubi. Neno “gubigubi” maana yake ni.... A. kujifunika kuanzia kichwani hadi miguuni B. kujifunika ukiwa umelala chali C. kujifunika mgongo wazi D. kujifunika rubega E. kujifunika kucha tu [ ]

81. Tulitia nanga salama kwani…………wetu alikuwa mzoefu. A. Dereva B. Nahodha C. Mwendeshaji wa semina D. Utingo E. Rubani [ ]

82. Ingawa kulikuwa na nuru ya kutosha tayari ilikwishatimia saa moja kamili. Neno “nuru” maana yake ni………. A. giza B. mawingu C. mwanga D. taa E. umeme [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

83. Vifaa hivi vitakidhi lengo la kumalizia jengo letu. Neno “vitakidhi” lina maana gani?

A. vitaongeza B. vitatosheleza C. vitaharibu D. vitaleta E. vitahamasisha [ ] 84. Ni fungu lipi la maneno yafuatayo lenye maana sawa na samani?

A. vikombe, bakuli, kabati B. vitanda, viti, meza, kabati C. godoro, meza, kitanda D. meza, gauni, shati, kiti E. koroboi, kabati, kibiriti [ ]

85. Neno lililo kinyume cha neno “duni” ni lipi? A. bora B. dogo C. bichi D. hafifu E. baya [ ] 86. Serikali imetoa ilani juu ya unywaji wa pombe za kienyeji vilabuni. Neno ilani lina maana gani?

A. laana B. ruhusa C. onyo D. leseni E. matengenezo [ ] 87. Neno lenye maana sawa na ufukara ni lipi kati ya haya?

A. ukwasi B. usawa C. ukurutu D. ukata E. ugonjwa [ ] 88. Kinyume cha neno “takasa” ni kipi? A. takata B. chafua C. chanua D. tandika E. taabika [ ] 89. Mahali panapochimbwa madini panaitwaje? A. mgodini B. shimoni C. mererani D. porini E. madinini [ ] 90. Furah alishikwa na “fadhaa” alipobaini ameuziwa mali ya wizi. Neno “fadhaa” katika sentensi hii lina maana ipi?

A. aibu B. mshangao C. hofu D. chuki E. nderemo [ ] 91. Fundi seremala alinihadaa aliponiambia angenipa kabati langu juzi. Neno “alinihadaa” lina maana gani?

A. alinisingizia B. alinidanganya C. aliniahidi D. alinizawadia E. alinipa [ ] 92. Kinyume cha neno “okota” ni kipi? A. dokoa B. gusa C. nyakua D. dondosha E. daka [ ]

93. Mtu hodari asiye ogopa kwa neno moja huitwaje? A. mkaidi B. jambazi C. mgomvi D. jasiri E. mjinga [ ] 94. Omani amekwenda kubarizi. “kubarizi” maana yake ni nini?

A. kuogelea B. kumsengenya C. kupunga upepo D. kuchukua mzigo E. kubeba meli [ ] 95. Kutokana na maumivu makali Maria hakupata hata………. A. punje la usingizi B. lepe la usingizi

C. patio la usingizi D. madhara ya usingizi E. kulala usingizi [ ]

96. Neno lipi kati ya maneno yafuatayo lina maana sawa na neno “tamati”? A. mwanzo B. awali C. ufupisho D. kikomo E. tunza [ ]

97. Nimetuma ujumbe lakini sijapata mwitiko wowote. Neno mwitiko katika sentensi hii lina maana sawa na neno lipi? A. mwito B. mwangi C. mwaliko D. utata E. jibu [ ]

98. Pendo alinikera sana kwa maneno yake. Neno kukera lina maana ipi katika sentensi hii?

A. kulia B. kupumzika C. kuudhi D. kuogelea E. kucheka [ ] 99. Masanja ni mtoto wa mjukuu wangu. Kwa hiyo Masanja ni nani?

A. mpwa wangu B. binamu yangu C. kilembwe wangu D. kitukuu changu E. kining’ina changu [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

100. John alinitembelea kwa…………….kunijulia hali.

A. dhumuni la B. madhumuni ya C. zumuni la D. udhumuni wa E. dhumuni ya [ ] 101. Maana ya neno aghalabu ni ipi? A. angalau B. mara chache C. mara mbili D. nadra E. mara nyingi [ ] 102. Kinyume cha “nuka” ni kipi? A. nukia B. nukanuka C. harufu D. uozo E. fukiza [ ] 103. “Matona alioa msichana wa hirimu yake” Neno hirimu lina maana gani katika sentensi hii?

A. nasaba B. rika C. kabila D. jinsi E. dini [ ] 104. Mtaalamu wa elimu ya nyota huitwaje? A. mpiga ramli B. mganga wa kienyeji

C. mkataba D. mnajimu E. mshirikina [ ] 105. Neno moja linalojumuisha dhahabu, shaba, chuma, almasi, bati na rubi ni lipi?

A. silaha B. vipuli C. madini D. migodi E. ala za muziki [ ] 106. Neno lipi ni kinyume cha neno adili? A. wema B. uovu C. ujasiri D. ujanja E. ujinga [ ] 107. Mtu msafi wa mwili na mavazi huitwaje? A. nadhifu B. mng’avu C. shupavu D. mwadilifu E. mtukufu [ ] 108. Kati ya maneno yafuatayo ni lipi lenye maana sawa na neno ukwasi? A. umaskini B. ufukara C. upungufu D. ukondefu E. utajiri [ ] 109. Nini maana ya neno faraghani? A. ukumbini B. mafichoni C. furahini D. hadharani E. mkutanoni [ ] 110. Kipindi cha miaka mia moja huitwa? A. muhula B. zama C. msimu D. karne E. majira [ ] 111. Mtu anayeshukiwa kuwa ametenda kosa huitwaje? A. askari B. mtuhumiwa C. jaji D. wakili E. diwani [ ] 112. Mtu anayeipenda nchi yake huitwaje?................ A. mzaliwa B. mwananchi C. shujaa D. raia E. mzalendo [ ] 113. Mshitakiwa alipofika mahakamani aliomba mahakama impe………………… A. dhamini B. mdhamini C. mdhamana D. dhamana E. amana [ ] 114. Neno lipi linakamilisha sentensi ifuatayo kwa usahihi? A. Nilipofika Morogoro nilipata………wa kutembelea eneo la

viwanda. A. wasaa B. washa C. washia D. warsha E. wasia [ ] 115. Mtu anayetengeneza vitu kama vile meza, viti, kabati na vitanda kwa kutumia mbao huitwaje?...................

A. mwashi B. sonara C. seremala D. rubani E. mhunzi [ ] 116. Mahali anaposimama mshtakiwa mahakamani huitwa ……....

A. jela B .mahabusu C. kizimbani D .gerezani E. mahakamani [ ] 117. Mzee Musa amekuwa kibogoyo. Maana yake ni ………

A. hana pua B. hana meno C. hana fedha D. hatafuni vizuri E. kazeeka sana. [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

118. Neno lenye maana sawa na “mawio” ni lipi kati ya haya?

A. machweo B. macheo C. mchana D. magharibi E. alasiri. [ ]

119. Kazi yako ina walakini. Neno walakini lina maana sawa na ………………….…. A. ubora B. maridadi C. umakini D. kasoro E. sifa zinazotakiwa. [ ]

120. Mtu anayetumwa kushughulikia masuala ya posa wakati wa kuoa au kuolewa ni ……. A. mshenga B. mpatanishi C. mzushi D. mtumwa E .mtu hodari. [ ]

121. Wazazi wanashauriwa kuongea ………..kuhusu suala la UKIMWI. A. kwa siri B. baina C. chumbani D .sawasawa E. bayana. [ ]

122. Kaka …..kwa matumizi ya dawa za kulevya. A. amezidiwa B .amekithiri C. ameoza D .amepitiliza sanasana E. amependekeza. [ ]

SEHEMU “C”: LUGHA YA KIFASIHI

123. Anna ni mtoto wa nasaba bora. Mtoto wa nasaba bora ina maana gani?...... A. mtoto wa pekee kuzaliwa B. mtoto wa ukoo bora C. mtoto wa kutumwatumwa D. mtoto mwenye akili E. mtoto wa binadamu [ ]

124. Nahau “pata jiko” ni kinyume cha nahau ipi? .................................................

A. pata mzungu B. kupata mke C. pata nasaha D. Kupata naizisheni E. kupata amana [ ]

125. Babu kafa, kaniachia pete. Jibu la kitendawili hiki ni.................................................

A. Tairi B. jogoo C. jongoo D. njia E. yai [ ]

126. Malizia methali hii “kipenda roho, .................................................

A. Hula na nduguye B. humrudia mwenyewe C. Hula nyama mbichi

D. hukimbiza ubawa wake E. huenda kicheko [ ]

127. Mtaka yote kwa pupa, hukosa yote. Methali hii ina fanana na ipi kati ya hizi? .................................................

A. Ukipata chungu kipya, usisahau cha zamani B. Kamba hukatikia, pabovu C. Mali bila daftari huisha bila kujua D. Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba E. Heri kenda shika, kuliko kumi nenda rudi. [ ]

128. Ng’ombe wangu nikitaka anywe maji sharti kumshika mkia. Jibu la kitendawili hiki ni lipi? .....................................

A. Mkanda B. barabara C. kivuli D. mbariko E. kata [ ]

129. Neno “Jua” ni jibu la kitendawili gani kati ya hivi? .................................................

A. Juu mboga, chini ugali, katikati kuni B. Huku tamu na huku tamu, katikati chungu C. Huku ng’o na huko ng’o D. Bibi kizee ana kazi milele, asubuhi na jioni. E. Rafiki yangu ni mharibifu lakini bado namhitaji [ ]

130. Matapeli wale waliingia mitini walipowaona askari. Nahau iliyopigiwa mstari maana yake ni ipi? .........................

A. Toa hongo B. pata tabu C . kamatwa D. Kutoweka E. kutembea huku na huko [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

131. Kuwa mfupi halafu ukasifiwa kuwa ni mrefu sana. Nahau inayofaa maelezo hayo ni ipi?

A. ameupara B. vishwa kilemba cha ukoka C. ona fahari D. fyata mkia E. vimba kichwa [ ]

132. ................................................. na wewe mgomeke. Malizia methali hii.

A. Audi wa mtu B. Mtenda jamala C. Mwana wa ndugu D. Akugomaye E. Mtoto mkaidi [ ]

133. Familia yetu hujitunzia mazao waliyovuna kwa ajili ya matumizi ya baadae wakati wa njaa. Methali gani inafaa maelezo

hayo.

A. Jungu kuu halikosi ukoko B. akiba haiozi C. Hisani hulipwa D. kinga ni bora kuliko tiba E. Undugu kufaana si kufanana [ ]

134. Jibu lipi linakamilisha methali ifuatayo? “Chaka la simba” … A. halilali nguruwe B. ni chafu sana C. lina ubaya D. lina mifupa mingi E. linatisha sana [ ]

135. Rushwa imeota mizizi, neno “kuota mizizi” lina maana gani? ……

A. kuanza B. kushamiri C. kuibuka D. kuendelea E. kupotea [ ]

136. Wanafunzi wa darasa la saba wanafanya kazi kwa kushirikiana. Nahau ipi inafaa kutumika katika sentensi hii? A. bega kwa bega B. nyama ya ulimi C. kuuponda wa fisi D. unga mkono E. kuvaa miwani [ ]

137. Jibu sahihi la kitendawili hiki ni lipi? “nina kitanda changu cha mkangashale mwana wa halali aende akalale” A. mvua B. maji C. nyumba D. bahari E. jua [ ]

138. Fulani hana faragha. Maana ya maneno “hana faragha” ni ipi?...........…. A. hana siri B. hana moyo C. hana hasira D. hana utu E. hana dharau [ ]

139. Daima namsikia tu, lakini simuoni nini maana ya kitendawili hiki…….…

A. upepo B. mchawi C. mvua D. mwanga E. giza [ ] 140. Methali ipi ina maana sawa na methali ifuatayo. Upele humwota siye na kucha.

A. penye miti hakuna wajenzi B. wingi si hoja na raha C. mkataa kwao mtumwa D. kujikwaa si kuanguka E. Kiingiapo mjini si haramu [ ]

141. Methali isemayo”usiache mbachao kwa msala upitao” maana yake ni…………… A. usiamini mambo yajayo ukasahau yaliyopita B. Tamani vitu vya mwenzako acha vyako C. unapopika chakula lazima uwe mwangalifu D. usimwamini kila mtu ukafuata mambo yake E. kipya kinyemi ingawa kidonda [ ]

142. Jibu sahihi la kitendawili hiki ni lipi? Ngilingili huingia kwa ngilongilo lakini ngilongilo haingii kwa ngilingili

A. kijiko na sufuria B. kijiko na mwiko C. sufuria na beseni D. penseli na rula E. daftari na kalamu [ ]

143. Mzee Kipanya alipata tabu sana katika kuhangaikia shamba lake, baada ya mahangaiko ya muda mrefu hatimaye mzee huyo alivuna mazao mengi sana na sasa hana shida ya chakula. Je, hapo ni methali gani inafaa kumpa mzee huyo? A. jasiri haachi asili B. baada ya dhiki faraja

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

C. dawa ya moto ni moto D. maji hufuata mkondo E. mwenda pole hajikwai [ ] 144. Tegua kwa usahihi kitendawili kifuatacho” kondoo wangu kachafua njia nzima”

A. jogoo B. konokono C. kinyonga D. tandu E. mjusi [ ]

145. Kinyume cha nahau katisha tamaa ni kipi? …. A. pata chungu B. ona fahari C. kata maini D. tia moyo E. pata chungu [ ]

146. Kamilisha kwa usahihi kitendawili kifuatacho. Mtemi hafi…. A. chali chali B. wima wima C. fofofo D. kifudifudi E. usingizini [ ]

147. Moja kati ya methali zifuatazo haihimizi watu kujiendeleza kielimu …………. A. kuuliza si ujinga B. kuishi kwingi kuona mengi C. penye nia pana njia D. elimu ni bahari E. akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki [ ]

148. Upele humuota asiye na kucha. Methali ipi kati ya hizi ina maana sawa na hiyo? A. mwenda pole hajikwai B. penye miti hakuna wajenzi C. damu nzito kuliko maji D. mchumia juani hulia kivulini E. haba na haba hujaza kibaba. [ ]

149. Kuwa na ulimi wa upanga manaa yake ni …… A. kutoa maneno ovyo ovyo B. kutoa maneno makali C. kupayuka D. kuwa na uolimi mrefu E. kukata kata maneno [ ]

150. Malizia methali ifuatayo; Mla ni mla leo ………

A. mla mla leo kala nini B. mla baadae kala nini C. mla jana kala nini D. mla kesho kala nini E. asiyekula hali tena [ ]

151. Nini jibu la kitendawili hiki, ‘mbwa mwitu wamemzunguka kumlinda’ A. kucha na vidole B. mdomo na meno C . ulimi na meno D. kichwa na nywele E. mkono na vidole. [ ]

152. Watu walimtaka yule mwizi kusalimu amri. “Kusalimu amri” ni usemi wenye maana ya ….. A. ahame mtaa B. akubali kwenda jela C. asikubali kabisa D. akubali kushindwa E. asalimie watu wote. [ ]

153. Methali “Bandu bandu humaliza gogo” inafanana na …… A. mwenda pole hajikwai B. pole pole ndio mwendo C. haraka haraka haina Baraka D. chovya chovya humaliza buyu la asali E. aliye juu mngoje chini [ ]

154. Wazazi walikata shauri kumpeleka kaka shule “Kukata shauri” maana yake ni ….. A. kumpeleka kwa mkuu B. hakuna jibu C. kuamua D. kumchapa E. kupeleka shauri. [ ]

155. Usinivike kilemba cha ukoka ina maana ya ……………………..…

A. usinidharau B. usinikasirishe C. usinibembeleze D. usinipe sifa nisizostahili [ ]

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

156. Nikitembea waliowafu huniamkia na waliohai hukaa kimya. Maana ya kitendawili hiki ni…..….. A. yai na kifaranga B. majani makavu na mabichi C. kulala na kukesha D. alfajiri na jioni E. usiku na mchana. [ ]

157. Wana wa mfalme ni wepesi kujificha. Maana ya kitendawili hiki ni ……

A. macho B. ulimi C. pua D. masikio E. ini [ ] 158. Kamilisha methali ifuatayo. “Mwacha asili ni… A .mkunga B. mtumwa C. mgeni D. mtalii E. mzalendo [ ]

159. Tegua kitendawili kifuatacho. “Kondoo wetu ana ngozi ndani na nyama nje.………

A.Nanasi B. Katani C. Firigisi D. Nazi E. Siafu [ ] 160. Heri kufa macho kuliko ……………………..…

A. kufa mwili B. kufa moyo C. kufariki dunia D. kufa masikio E. kufa mdomo [ ]

161. Manahodha wengi chombo huenda mrama. Ni methali gani kati ya hizi zifuatazo inapingana na hii? …… A. Kwenye watu wengi haliharibiki neno B. Jungu kuu halikosi ukoko C. Mchimba kisima huingia mwenyewe D. wingi si hoja E. Wengi wape [ ]

162. Tegua kitendawili kifuatacho. Ajihami bila silaha. …… A. Askari B. Shujaa C. Fisi D. Mwizi E. Kinyonga [ ]

163. Jibu la kitendawili: “Nikimpiga mwanagu nalia mwenyewe” ni …….

A. Ngoma B. Pilipili C. kitunguu D. Shoka E. Muhogo [ ]

164. Maana ya nahau “Kupiga chuku” ni ipi? …………….. A. kutoa maneno machafu B. kutoa maelezo ya uongo C. kuchukia jambo Fulani D. kusema ukweli E. kutunza siri [ ]

165. Samahani ndugu umenitoka. Maana ya neno umenitoka ni ipi? ………………………..… A. umeniacha B. umenikimbia C. nimekusahau D. umenichoka E. umenifia. [ ]

SEHEMU “D”: UTUNGAJI (i) Umepewa insha yenye sentensi tano zilizoandikwa bila kufuata mtiririko wa mawazo. Zipange sentensi hizi

ili zilete mtiririko wenye mantiki kwa kutumia herufi A, B, C, D, E. 166. Lilipigwa tena la mgambo watu walijipanga kila upande wa msitu ili wamshambulie simba huyo [ ]

167. Ilikuwa yapata saa tisa za usiku la mgambo lilipolia [ ] 168. Baada ya kukuru kakara nyingi, wananchi walifanikiwa kumuua simba kwa kutumia silaha zao za jadi [ ] 169. Kumbe ilikuwa ishara ya kuonyesha kuwa simba alikuwa ameingia kijijini kwao. [ ] 170. Watu waliposikia walizinduka na kuanza safari ya kuelekea kule yowe lilkokuwa limetokea [ ]

(ii) Umepewa habari yenye sentensi nne (4) zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

ziwe na matiririko wenye mantiki kwa kutumia herufi A, B, C, D.

171. Kwa njia hii, vizazi vilivyofuata viliweza kujua uvumbuzi uliofanywa kabla yao. [ ] 172. Jambo muhimu lililofanywa na mababu zetu ni kuhifadhi kumbukumbu za uvumbuzi wao wa kuchora kila kifaa

walichovumbua. [ ] 173. Kwa kutumia vizazi vilivyotangulia, nasi pia tunaweza kuvumbua vitu vipya ambavyo vitaweza kutuleta

maendelea zaidi. [ ] 174. Hivyo maisha ya binadamu yakaendelea kuwa bora na yenye manufaa kila siku. [ ]

(iii) Umepewa habari yenye sentensi 4 zilizoandikwa bila mtiririko sahihi wa mawazo. Zipange sentensi hizo ili ziwe

na mtiririko wenye mantiki kwa kutumia herufi A, B, C, D.

175. Ukataji miti kwa wingi kwa ajili ya ujenzi na shughuli zingine huweza kusababishia nchi yetu ya Tanzania kuwa jangwa. [ ]

176. Kutokana na miti watu hujenga nyumba nzuri za kila namna zinazopendeza na za kudumu. [ ]

177. Hivyo ni muhimu kwa kila mtu kupanda miti kila anapokata mti kwani nchi isiyo na miti ni sawa na mtu ambaye amevuliwa nguo. [ ]

178. Miti ina faida nyingi sana kwa binadamu. [ ]

SEHEMU “E”: USHAIRI (i) Soma kwa makini shairi lifuatalo kisha jibu swali la 179 – 184 kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi.

Msituni nikakuta, nyuki wamo mzingani. Kwa juhudi wanakita, mara nje mara ndani, Husuda wameukata, hata hawasengenyani, Nyuki ni wadudu duni, wanashinda kwa umoja.

Mchwa nao nikaona, wamejenga maskani, Wafanya bidii sana, uvivu hawatamani, Wao husaidiana, tena hawadanganyani, Mchwa wadudu wa chini, wanaishi kwa umoja.

Nalo jeshi la siafu, hutaduwaa njiani, Laenda bila ya hofu, maana lajiamini, Silaha zao dhaifu, meno tena hawaoni, Wa kuwatadia nani, kwani wanao umoja.

Nao chungu wachukuzi, nyamarima wa njiani, Maskini wapagazi, mizigo yao kichwani, Ingawa si wachokozi, wakali ukiwahini, Katu hawafarakani, wanadumu kwa umoja.

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

MASWALI. 179. Mwandishi wa shairi hili anasisitiza kuhusu nini? A. uzalishaji B. maarifa

C. ushirikiano D. urafiki E. undugu [ ]

180. Shairi hili lina mizani mingapi kwa kila mstari?

A. sita B. kumi na sita C. tano D. saba E. thelathini na moja [ ] 181. Neno “husuda” kama lilivyotumika katika shairi hili lina maana gani?

A. uhasama B. hisani C. hiana D. wivu E. huzuni [ ] 182. Kisawe cha neno “Tadi” ni kipi? A. uchokozi B. tishio C. kemea D. ukombozi E. umbua [ ]

183. Kina cha kati katika ubeti wa pili ni kipi? A. wa B. na C. ja D. u E.ni [ ]

184. Kichwa cha habari kinachofaa kwa shairi hili ni kipi? A. Upekee wa wadudu B. Umuhimu wa wadudu

C. Uhatari wa wadudu D. uchunguzi wa wadudu E. Umoja wa wadudu [ ]

(ii) Soma shairi lifuatalo kwa usahihi kisha jibu maswali kwa kuchagua herufi ya jibu sahihi. Ninaye ndege mzuri,mrembo wa kupendeza, Rangi zake mashuhuri, ni nne nawaeleza, Ndizo rangi za fahari, urembo kuutimiza, Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania?

Anayo rangi nyeusi, sote tunaitukuza, Nami nilipodadisi, kumbe nimemwambukiza, Nayo ni rangi halisi, ambayo imenikuza, Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania?

Rangi ya pili kijani, kwenye mbawa katimiza, Nzuri isiyo kifani, kwenye mwanga hung’ariza, Jamani niambieni, ndege amenipendeza, Ndege huyu ndege gani, hapa kwetu Tanzania?

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

MASWALI 185. Shairi ulilosoma lina jumla ya beti ngapi? A. saba B. kumi C. tatu D. nne D. tano [ ]

186. Katika shairi hilo kila ubeti una jumla yamishororo mingapi? A. 6 B. 4 C. 2 D. 1 E. 8 [ ] 187. Kina cha mwisho katika ubeti wa tatu ni kipi? A. a B. ze C. nde D. za E.ki [ ] 188. “Ndege huyu ndege gani hapa kwetu Tanzania?” katika shairi ulilosoma maneno hayo huitwaje?

A. kibwagizo B. kusini na kaskazini C.mwana kutanda chini D. nyeusi zapendeza E. sitomuuza [ ] 189. Ubeti wa kwanza una jumla ya mizani mingapi? A. 16 B. 8 C. 64 D. 28 E. 17 [ ] 190. Kulingana na shairi ulilosoma, ndege aliyetajwa ana rangi ngapi? A. tano B. nne C. tisa D.kumi na moja E. ishirini [ ] SEHEMU E: UFAHAMU

(i) Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata

Miongoni mwa mashujaa ambao hawawezi kusahaulika katika historia ya nchi yetu ni Mtwa Mkwawa.

Huyu alikuwa kiongozi wa kabila la wahehe mkoani Iringa. Baba yake Mkwawa aliitwa Munyigumba.

Mkwawa aliongoza mapambano makali dhidi ya wajerumani kuanzia mwaka 1891 hadi mwaka 1898.

Alifanikiwa kuwaua wajerumani wengi akiwemo aliyekuwa kamanda wa kikosi cha Kijerumani aliyejulikana

kwa jina la Emili Zelwiski.

Mara baada ya kuuawa kwa kamanda Zelwiski mnamo mwaka 1891, Gavana wa Ujerumani aliwaamuru

wanajeshi wake wamtafute Mkwawa kwa nguvu zote hadi wamkamate. Baada ya Mkwawa kugundua kuwa

amezidiwa sana na Wajerumani akaamua kujiua kwa kujipiga risasi yeye na mlinzi wake kwa kuhofia asikamatwe

na Wajerumani.

MASWALI

191. Kwa mujibu wa kifungu hiki cha habari, ni shujaa gani hawezi kusahaulika kirahisi katika historia ya nchi yetu?

192. Mkwawa alipambana na wajerumani kwa muda wa miaka mingapi?...................................................................

193. Kiongozi wa Kijerumani aliyeuliwa na jeshi la Mkwawa mwaka 1891 alikuwa nani? ............................................

194. Baba yake mkwawa aliitwa nani? ............................ ............................................ .................................................

195. Kwanini Mkwawa aliamua kujiua mwenyewe? ............................................ ............................................

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020

Soma kwa makini kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.

Katika nchi ya Tanzania kuna baadhi ya vijiji ambavyo vimepiga hatua kubwa kimaendeleo. Maendeleo

hayo hayakuja kama ndoto bali yametokana na maarifa na juhudi za wakazi wa vijiji hivyo. Miongoni mwa vijiji vilivyopiga hatua

kimaendeleo ni kijiji cha Kwabosa kilichopo wilaya ya Lushoto mkoani Tanga. Ukifika Kwabosa utawakuta wanakijiji wakifanya

kazi zao bega kwa bega ili kukamilisha mipango yao ya maendeleo. Wanakijiji wa Kwabosa wengi wao hujishughulisha na

kilimo na ufugaji. Hulima mazao ya biashara na mazao ya chakula.

Zao kuu la biashara kijijini hapo ni chai. Mbali na chai, pia hulima kahawa kama zao lingine la biashara. Kwa upande wa

mazao ya chakula wanakijiji wa Kwabosa hulima mahindi, maharage, matunda na mboga mboga. Mbali na kushirikiana katika

kilimo na ufugaji, wanakijiji wa Kwabosa pia hushirikiana katika ujenzi wa miundombinu na huduma mbalimbali za kijamii kama

vile barabara, shule na Zahanati. Kijijini Kwabosa kuna shule mbili za msingi na shule moja ya sekondari. Shule hizi zote

zimejengwa kwa ushirikiano mkubwa wa wananchi wakiungwa mkono na serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo.

MASWALI:

196. Kijiji cha Kwabosa kinapatikana katika mkoa gani?............................................................................................

197. Kuna aina ngapi za mazao yanayolimwa na wananchi wa Kijiji cha Kwabosa?...................................................................

198. Ukiachilia mbali chai, Zao lingine la biashara linalolimwa na wakazi wa Kijiji cha Kwabosa ni lipi?.....................................

199. Je, kuna jumla ya shule ngapi katika kijiji cha Kwabosa? ...................................................................................

200. Wanakijiji wa Kwabosa hufanya kazi zao bega kwa bega. Nahau kufanya kazi bega kwa bega

kama ilivyotumika katika kifungu cha habari hapo juu ina maana gani? .............................................................

“Elimu ni uzima wangu” (Methali 4:13)

KUWA MAKINI NA COVID-19 NAWA MIKONO YAKO KILA MARA MACHI 2020