chama cha maendeleo ya vijiji na …...4 chama cha maendeleo ya vijiji na mazingira cha kibale...

15
Kesi Tafiti za Mradi wa Equator Ufumbuzi wa maendeleo endelevu ya mtaa kwa ajili ya watu asili na jamii shujaa Uganda CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA MAZINGIRA CHA KIBALE (KAFRED) Empowered lives. Resilient nations.

Upload: others

Post on 08-Jan-2020

14 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

Kesi Tafiti za Mradi wa EquatorUfumbuzi wa maendeleo endelevu ya mtaa kwa ajili ya watu asili na jamii shujaa

Uganda

CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA MAZINGIRA CHA KIBALE (KAFRED)

Empowered lives. Resilient nations.

Page 2: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

MFULULIZO WA KESI TAFITI ZA MRADI WA EQUATOR WA UNDP Jamii asili na wazawa jamii kote nchini wanaendeleza ufumbuzi wa ubunifu wa maendeleo endelevu ifanyayo kazi kwa ajili ya watu asili. Sio machapisho mengi au kesi tafiti inayosema hadithi kamili ya jinsi juhudi kama hizo ufuka, upana wa athari zake, au jinsi yanayobadilika kwa muda.Wachache zaidi wamejitahidi kusimulia hadithi hizi kupitia kwa uelekezi wa watendaji wa jamii wenyewe wakielekeza hadithi.

Katika kuadhimisha miaka kumi ya utendaji kazi, Mradi wa Equator unalenga kujaza pengo hili. Kesi tafiti lifuatalo ni moja katika mfululizo wa kesi zinazohadithia kazi ya washindi watuzwa wa taji la Equator – zilizochunguzwa na kufanyiwa mapitio rika na kuambatana na mbinu bora katika uhifadhi wa kijamii na mazingira na maisha endelevu. Kesi hizi zina lengo la kuhamasisha mjadala wa sera zinazohitajika ili kupeleka mafuniko ya jamii asili kufikia kilele, kuboresha maarifa msingi ya kimataifa kwa ufumbuzi wa mazingira na maendeleo asili na kutumika kama mifano ya kuigwa. Masomo ya kesi ni bora kutazamwa na kueleweka na rejea kwa ‘Nguvu za Matendo ya Jamii Asili: Mafunzo ya Miaka 10 ya Taji la Equator’, maandishi ya masomo ya kujifunza na mwongozo wa sera ambazo huchota kutoka kwa kesi nyenzo.

Bonyeza kwenye ramani kutembelea Mradi wa Equator na kutafuta kesi tafiti

WahaririMhariri Mkuu: Joseph CorcoranMhariri Mtendaji: Oliver HughesWahariri wa Kuchangia: Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Erin Lewis, Whitney Wilding

Waandishi wa kuchangia Edayatu Abieodun Lamptey, Erin Atwell, Toni Blackman, Jonathan Clay, Joseph Corcoran, Larissa Currado, Sarah Gordon, Oliver Hughes, Wen-Juan Jiang, Sonal Kanabar, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Rachael Lader, Patrick Lee, Erin Lewis, Jona Liebl, Mengning Ma, Mary McGraw, Gabriele Orlandi, Juliana Quaresma, Peter Schecter, Martin Sommerschuh, Whitney Wilding, Luna Wu

MuundoOliver Hughes, Dearbhla Keegan, Matthew Konsa, Amy Korngiebel, Kimberly Koserowski, Erin Lewis, John Mulqueen, Lorena de la Parra, Brandon Payne, Mariajosé Satizábal G.

ShukraniMradi wa Equator anakubali kwa shukrani KAFRED, na hasa uongozi na juhudi za Tinka John Amooti na George Owoyesigire. Shukrani zote za picha in kwa hisani ya KAFRED. Ramani ni kwa hisani ya CIA World Factbook na Wikipedia. Kesi Tafiti hii ilitafsiriwa na Alex Kimanzi na Kusahihishwa na George Oloo (Wajitoleaji wa Umoja wa Mataifa).

Uelezeaji UnaopendekezwaUnited Nations Development Programme. 2012. Kibale Association for Rural and Environmental Development (KAFRED), Uganda. Equator Initiative Case Study Series. New York, NY.

Page 3: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

MUHTASARI WA MRADIJamii ya kijiji Bigodi, karibu Fort Portal, magharibi mwa Uganda, yapata kilomita nane za ardhi oevua ya mafunjo ambayo ni nyumbani kwa wingi wa wanyamapori. Aina nane za nyani na zaidi ya aina 200 za ndege huteka watalii kutoka kwa pori jirani ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu, ambayo kinamasi Bigodi hutengenezea ukanda muhimu wa wanyamapori. Kupitia kwa kazi ya Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED), jamii ilifaidika sana kutoka kwa biashara hii ya utalii wa ikolojia kwa kuanzisha matembezi ya kuongozwa kupitia oevu, zikisaidiwa na uuzaji wa hila mikono wa kikundi cha wanawake kijijini. Usimamizi endelevu wa eneo iliungwa mkono na utungaji wa sheria ndogo katika mwaka wa 1995, iliyoundwa kwa mtindo shirikishi na mamlaka ya serikali za mitaa. Utaratibu huu ulitoa msingi wa kisheria kwa ajili ya kazi ya kikundi katika uhifadhi wa wanyamapori na kuongeza mapato ambayo iliyofaidi Hifadhi ya Taifa na wadau wa ndani kwa kipimo sawa.

HABARI TENDETIMSHINDI WA TUZO LA EQUATOR: 2004, 2010

ILIANZISHWA: 1992

MAHALI: Wilayani Kamwenge, magharibi mwa Uganda

WALENGWA: Takriban familia 300

BAYOANUWAI: Hifadhi ya Ardhi Oevu la Bigodi

3

CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA MAZINGIRA CHA KIBALE (KAFRED)Uganda

YALIYOMO

Usuli na Muktadha 4

Shughuli muhimu na Ufumbuzi 6

Athari za Bioanuwai 8

Athari za Kijamii na kiuchumi 10

Athari za Sera 11

Uendelevu 12

Uigaji 14

Washirika 14

Page 4: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

4

Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda. Kundi hili lilianzishwa mwaka 1992, na linatumia utalii ikolojia na biashara nyingine za mazingira endelevu ili kukuza bayoanuwaina maendeleo ya jamii katika ardhi oevu ya Bigodi. Ardhi oevu hili huunda ukanda muhimu wa wanyamapori na ni nyumbani kwa tajiri utofauti za kibayolojia: kinamasi, inaomea nyasi aina ya ‘papyrus’, iko kilomita nane tu kwa urefu, lakini inasaidia zaidi ya aina 200 za ndege na aina nane za nyani. Pamoja na ushiriki kutoka jamii mitaa ya kilimo, wanachama wa asili wa KAFRED waliweza kusitisha kushambuliwa kwa eneo ardhi oevu na kujenga njia za wanyamapori kuongoza watalii. Mapato kutokana na utalii yametumika katika ujenzi wa shule ya sekondari na kukuza elimu ya mazingira katika eneo hilo, kuanzisha mradi wa mkopo kwa ajili ya familia za wakulima, na kusaidia kundi la wanawake inayozalisha kazi za mikono na mikono hila.

Ukanda muhimu wa wanyamapori

Ukanda wa ardhi oevu ya ikolojia ya Bigodi inajumuisha maeneo mawili ya hifadhi ya kitaifa ya msitu wa Kibale, na hatimaye hupeleka maji katika Ziwa George, sehemu muhimu ya Ramsar, kwa njia ya mto Dura. Katika nusu ya mwisho ya karne ya ishirini, nyasi ya papyrus ndani ya ardhi oevu ilipungua kwa kiwango kikubwa, kuonyesha hasara ya uaribifu wa misitu unaofunika ardhi oevu kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa idadi ya watu inayo ongezeka katika sehemu hiyo. Licha ya upotevu huu wa makazi, ardhi oevu bado hutembelewa na ndege wa aina ya Grey Crowned Cranes, ilhali masokwe mara kwa mara hupitia kwa ukanda huo wa misitu. Miongoni mwa aina nyingi za nyani asili ni nyani na kima punju; Duniani, hifadhi ya kitaifa ya msitu wa Kibale ndiko tu wanapatikana kikundi kidogo cha punju nyekundu wa Uganda (Procolobus rufomitratus tephrosceles). Sehemu hii pia ni nyumbani kwa Great Blue Turaco ambayo ni nadra sana.

Kabla ya miaka ya 1990, kulikuwa hakuna utalii katika kanda ya msitu ya Kibale. Hifadhi ya taifa lenyewe lilitumiwa hasa kwa ajili ya utafiti wa masokwe. Hata hivyo, baada ya masokwe kuzoeshwa mahala pale, watalii walianza kutembelea eneo hilo, na hii ikasababisha ufunguzi wa tovuti ya utalii katika sehemu jirani ya Kanyanchu mwaka wa 1991. Wajitoleaji kutoka Marekani na Uingereza walifanya kazi na mradi huu, na mmoja wao alikuwa muhimu katika kuhimiza wakazi wa Bigodi kuanzisha shughuli zao wenyewe za utalii. Kichocheo kilikuwa maoni ya mtalii juu ya idadi ya aina ya nyani na ndege aliowaona akitembea kijijini: Kwa hivyo utalii huu wa mazingira wa Bigodi ulichangiwa na mahitaji. Malengo ya awali ya KAFRED yalikuwa kutumia utalii wa mazingira kama chombo cha kukuza uhifadhi. Lengo hili lilipanuka na likajumuisha kutumia mapato kutokana na utalii kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii. Eneo ardhi oevu lilitengwa kwa madhumuni ya utalii, na sheria za kijiji zinazosimamia uhifadhi wake zilitungwa mwaka wa 1995 katika mchakato shirikishi.

Usuli na Muktadha

Page 5: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

55

Chimbuko la hatua za pamoja kwa ajili ya uhifadhi.

Hii ilifanyika dhidi ya historia ya miradi ya kijamii kushindwa kufaulu katika Bigodi. Mradi wa shule ya sekondari ilikuwa imefungwa baada ya kujengwa juu ya ardhi inayomilikiwa na kanisa, na kusababisha mvutano wa kidini na kikabila. Wakati huo huo, mradi wa mikopo na akiba ulikuwa umevunjika baada ya usambazaji usiokuwa wa usawa wa fedha wamkopo, na ukosefu wa uwazi katika kutoa pesa hizo kwa matumizi. KAFRED hivyo basi ilijiepusha na kujenga kwenye ardhi iliyohusishwa na makabila fulani au makundi ya kidini, badala yake kutumia ardhi ya jumuiya iliyotolewa na mamlaka ya eneo hilo. Pia ilihakikisha kwamba sekta mbalimbali za jamii ziliwakilishwa vya kutosha katika uanachama wake. Awali kulikuwa wanachama waanzilishi sita, ingawa wengi zaidi walishirikishwa katika mikutano iliyopelekea kuundwa kwake. Kufikia mwaka wa 1996 kulikuwa na zaidi ya wanachama 30 wa kikundi; katika mwaka wa 2012 kulikuwa na zaidi ya 120. Hizi ni wakilishi dhati wa vikundi mbalimbali ndani ya kijiji, ingawa KAFRED awali ilikabiliwa na matatizo na uanachama

wa wanawake. Hii ilisababisha uanzilishi wa Kundi la Wanawake la Bigodi, ikiungwa mkono na KAFRED; jimbo hili inawakilisha moja ya vikundi kadhaa zinazohusishwa na KAFRED, ikiwa ni pamoja na kikundi cha Enyange cha Ngoma na Michezo ya kuigiza, kikundi cha wanawake cha Kiyoima, Kikundi cha Siagi ya Karanga cha Bigodi, na kikundi cha Mikopo na Akiba cha Bigodi. Mikutano mikuu ya mwaka hufanywa katika lugha ya wenyeji ya Rutooro: Ngazi hii ya ushiriki wa jamii imekuwa msingi wa mafanikio ya mipango ya KAFRED. KAFRED pia ilikuwa mwanachama mwanzilishi wa UCOTA, Jumuiya ya Chama cha Utalii wa Kijamii huko Uganda, ambayo imechangia kuhamasisha sera za serikali juu ya jukumu la jamii katika mipango ya utalii. Katika mwaka wa 2010, KAFRED ilipata kuwa mradi wa kwanza kupewa tuzo la UNDP la mradi waEquator kwa mara ya pili, kufuatia mafanikio yao katika mwaka wa 2004. Mradi huu umeonyesha kwa mfululizo faida na uwezo wa uvumbuzi wa kijamii kwa utalii wa mazingira, uhifadhi na maendeleo, na inatumika kama mfano wa kuigwa nchini Uganda na kimataifa.

“Watunga sera wanapaswa kuelewa umuhimu wa jamii na ushiriki wa jamii katika uhifadhi. Lazima wajenge mazingira ya sera muhimu kuruhusu hii.”

Tinka John Amooti, Mkurugenzi, KAFRED

Page 6: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

6

Shughuli na Ubunifu Kuu

Shughuli za utalii wa ikolojia katika Bigodi ni pamoja na matembezi ya kuongozwa kupitia kwa kinamasi na kijiji. Matembezi kupitia kwa kinamasi inafanywa na kuendeshwa na waelekezi wenye mafunzo, na hufanyika kupitia njia za mbao zilizojengwa kupitia kwa ardhi oevu. Njia hizi huruhusuwatalii kuona wanyamapori kwa karibu, ikiwa ni pamoja na aina 200 ya ndege na aina nane ya nyani. Wakati huo huo, matembezi kwa kijiji yalianzishwa ili kuwaruhusu watalii kuona njia za jadi za maisha ndani ya kijiji. Shughuli ni pamoja na kutembelea shule ya msingi, kanisa, na mganga wa jadi, na kusikia juu ya jukumu la wanawake katika kijiji, sherehe za jadi, na hadithi ya “Kijiji cha Makabila mbili”. Hadithi hii inahusu historia ya Bigodi, ambapo wabatooro kiasili waliungana na wabakiga wakihama kutoka kusini-magharibi mwa Uganda katika miaka ya 1950. Mpango wa kitalii nyumbani pia unaanzishwa na mwanachama mwanzilishi wa KAFRED, ili kupima kama kuna mahitaji ya kutosha ya huduma hii kwa kiwango kikubwa.

Uwekezaji Katika Elimu

Kuwekeza mapato kutoka utalii wa mazingira katika elimu imekuwa wasiwasi mkuu kwa KAFRED tangu kuanzishwa kwake. Ingawa eneo hili lilikuwa makao ya shule tano za serikali za msingi, watoto walilazimika kusafiri hadi Fort Portal, mji ulio umbaliwa kilomita 35, kuhudhuria shule ya sekondari. Majaribio ya awali ya kuanzisha shule katika jamii yalikabiliwa na changamoto ya mvutano wa kidini. Hata hivyo, kufuatia mikutano shirikishi ya mpangilio katika mwaka wa1992, iliamuliwa kuwa msimamo wa KAFRED wa kutounga mkono upande wowote utawawezesha kushinda vikwazo hivyo. KAFRED ilianzisha elimu ya sekondari mwaka wa1993, ikitumia jengo jamii iliokopwa kutoka kwa shirika la wakulima. Jengo la kwanza la ziada lilijengwa mwaka wa 1994, na shule hilo sasa linajumuisha wanafunzi mpaka kidato cha nne (kawaida umri wa miaka16.) Hivi sasa lina wanafunzi zaidi ya 200. Hadi hivi karibuni, KAFRED iliruzuku ada zote za shule na mshahara. Tangu serikali ya Uganda kufutilia mbali ada ya masomo katika shule za sekondari za serikali mwaka wa 2007, wingi wa ada zote za shule zinalipwa na serikali. KAFRED hulipa

ada zinazosalia, kumaanisha kwamba familia hazihitaji kuchangia. KAFRED pia hulipa mishahara ya walimu katika shule.

Hii imekuwa ikisaidiwa na mipango ya elimu ya mazingira ya KAFRED. Moja ya mipango hii imeanzishwa kwa kushirikiana na Mradi wa Kuni wa Kibale ambayo imesaidia uendeshaji wa kituo cha sayansi kwa majengo ya KAFRED, wakati makundi ya wanawake hutumia ngoma na maigizo ili kufikisha ujumbe kuhusu uhifadhi. Mara nyingi, matumbuizo haya hufanywa katika makanisa na mashule. Filamu pia huonyeshwa katika sehemu za umma kwa ajili ya elimu ya mazingira, kwa kuzingatia mradi sawa huko Tanzania ulioanzishwa na shirika isiyo ya serikali kutoka Uholanzi, iitwayo “Hali kwa Watoto”. Wakati huo huo, KAFRED imesaidia mafunzo ya waalimu kupitia ushirikiano wake wa kimataifa na UNITE (Uganda and North Carolina International Teaching for the Environment). Awali, huu ilikuwa mradi wa kubadilishana maarifa mashuleni, ulioanzishwa na North

Page 7: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

7

Carolina Zoo, kupitia UCOTA. UNITE sasa inasaidia huo mradi wa mafunzo ya ualimu kupitia mtaalam wa mazingira nchini Uganda. Katika mwaka wa 2010, mafunzo kwa walimu ililenga mandhari ya viumbe hai.

Kuboresha ustawi wa jamii na usawa wa kijinsia

KAFRED ina mipango ya kuwekeza zaidi mapato ya utalii katika miradi ya afya Bigodi, ambayo itawezekana mara tu serikali ikilipia ada za shule ya sekondari kikamilivu. Hadi sasa, hiki kikundi kimeshajenga nyumba ya wakunga katika kitengo cha afya humu, kuongeza upatikanaji wahuduma za afya kwa wajawazito katikajamii. Kundi la Wanawake la Bigodi liliunda chama ili kusaidia wanawake katika eneo hilo kuendeleza kazi za mikono na bidhaa ndogondogo kwa ajili ya kuuza kwa watalii. Kikundi hiki kinahusishwa na KAFRED, na kimepokea msaada kutoka kwao katika mfumo was mafunzo ya kitaalam katika maendeleo ya bidhaa na masoko. Pia wamepewa nafasi ili kuonyesha kazi zao za mikono. 90% ya mapato kutoka kwa utalii huenda kwa mwanamke binafsialiyefanyaufundi, ilhali 10% huendakwa mfuko wa jumuiya. Mfuko huu hutumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya jamii, ambayo kwa hivi sasa ina wanawake 40: hadi sasa wametumia faida walizopatakuanzisha shule ya awali huko Bigodi. Hatimaye, KAFRED imesaidia kuanzisha mradi mkopo kwa ajili ya familia wanaoishi pembeni mwa ardhi oevu. Hawa ni wakulima ambao wanabeba mzigo mkubwa wa migogoro baina ya binadamu na wanyamapori kutoka eneo hifadhi kwa njia ya nyani wenye kupora mazao. Wakulima hawa pia hufuatilia na kulinda eneo hilo, kuhakikisha kwamba hakuna binadamu wanaingilia kwenye misitu

au maeneo oevu. Mfuko wa dola 2,000 ulitolewa kwa wawakilishi kutoka familia 120 katikamwaka wa 2005, hukusheria kuhusu kukopeshana kwa pesa hizo zikianzishwa na familia zenyewe. Walichagua kamati ya kusimamia mikopo, ikiwa inajumuhisha mwakilishi kutoka KAFRED, na ikaanzisha mkopo was kuzunguka bila riba kwa ajili ya familia.

Ramani: Muundo wa uongozi wa KAFRED

Kamati Tendaji

Meneja wa Mradi

Mpokeaji

Wafanyikazi wasaidizi

Kitengo cha Fedha

Usimamiz i waShuleMwelekezi mkuu

Waelekezi

Chanzo: KAFRED

Page 8: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

8

Matokeo

MATOKEO YA BAYOANUWAIMatokeo muhimu zaidi kwa viumbe hai yaliyopatikana na KAFRED imekuwa kupunguza kiwango cha kushambulia ardhi oevu na wanakijiji. Hatua ya kwanza ilikuwa kupewa mamlaka ya kusimamia ardhi oevu Bigodi kwa niaba ya jamii pana na mamlaka ya serikali ya eneo hilo.

Kuhifadhi mipaka ya ardhi oevu

Uhifadhi wa ardhi oevu ulianzishwa na warsha shirikishi ya kupangilia iliofanyika huko Bigodi katika mwaka wa 1995. Mkutano huuulihusisha wanachama wa KAFRED, wakuu wa familia zinazoishikatika mipaka yaardhi oevu, viongozi wa wanawake, wawakilishi wa baraza za eneo hilo, na viongozi wa wilaya. Wawezeshaji kutoka Mradi wa Taifa ya Ardhi Oevu (NWP) na mradi wa uhifadhi na maendeleo wa Kibale na Semliki (KSCDP) walisaidia kwa kuanzisha sheria za kuongoza matumizi ya ardhi oevu Bigodi. Hii ilihusisha mambo kama umbali

wa shughuli za binadamu kutoka pembeni mwa kinamasi, kuzuia isipite kiwango kilichokuwa kimefikia. Pia walitilia mipakaukusanyaji wa kuni, mazoea ya malisho, na ukusanyaji wa matunda, na wakati huo huo kupiga marufuku kuchimba mahandaki ili kutoa maji kwa ardhi oevu na uchomaji katika eneo hifadhi. Sheria hizi zilikubaliwa na jamii na zimesaidia sana katika kuhifadhi ardhi oevu iliyobaki eneo hilo. Bila sheria hizi ardhi oevu hii haingekuwepo leo.

Jitihada hiari zaidi zimelenga upandaji wa miti aina ya mikaratusi kuzunguka eneo la ardhi oevu. Ingawa inakua haraka na kwa hiyo nzuri kwa ajili ya mbao, miti hii ina athari haribifu kwa kutoa maji kutoka nchi kavu, na kuacha udongo na asidi nyingi zinazozuia mimea nyingine kukua. Shughuli zimefanywa tangu mwaka wa 2008 ilikupunguza miti aina ya mikaratusi, na kuhamasisha wanakijiji wasipande zaidi. Katika kesi moja, hii ilihusisha afisa wa mazingira wilayani, ambaye aliletwa ili kushawishi mtu mmoja kuyang’oa mikaratusi; alifidiwa na pesa za kununua miche ya miti asilia.

Jedwali: Aina zilizo hatarini na pia nadra zinazo patikana katika ardhi oevu ya Bigodi

Aina yandege Sehemuya Orodha Nyekunduya IUCN

Crowned Hawk-eagle (Stephanoaetus coronatus) Hatari Ndogo

Grey Crowned Crane (Balearica regulorum) Iiko Hatarini

African Grey Parrot (Psittacus erithacus) Karibu Kutishwa

Papyrus Gonolek (Laniarius mufumbiri) Karibu Kutishwa

White-winged Swamp Warbler (Bradypterus carpalis) Hatari Ndogo

Chimpanzees (Pan troglodytes) Hatarini

Ugandan Red Colobus (Procolobus rufomitratus tephrosceles) Hatarini

L'Hoest's monkey (Cercopithecus lhoesti) Yawezekana kuwahatarini

Chanzo: KAFRED

Page 9: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

Mradi wa KAFRED wa miche ya miti umehimiza upandaji wamiti asili ya cordia na prunus Africanus kama kilimo mseto, ikiwa na anga la umiche 5,000 iliyokuzwa katika mwaka wa 2010. Miche hizi hutolewa kwa wanajamii bila malipo. Kwa kushirikiana na Mradi wa Kuni wa Kibale, KAFRED pia inaunda mradi wa kukuza Sesbania sesban aina ya mti asili unaokua kwa haraka. Mti huu unasifiwa kwa ajili ya matumizi yake kama kuni na kumaliza gasi ya naitrojeni, na unaweza kukua na kufikia urefu wa futi 15 mwaka moja baada ya kupanda. Mradi huu pia unauza vifaa vya kutengeneza majiko ufanisi ya kuni, yanayotumia miti chache na hivyo basi kupunguza shinikizo kwenye msitu.

Ufuatiliaji uliolengwa kwa aina za wanyamapori

Ufuatiliaji wa bioanuwai katika eneo oevu imekuwa bila mpangilio na kuongozwa na watu mbalimbali. Watafiti wa nyani kutoka kituo cha nyanjani cha Biolojia cha Chuo Kikuu cha Makerere wamewaelimisha viongozi wa KAFRED juu ya aina mbalimbali ya nyani na mara kwa mara kufanya utafiti juu ya aina hiyombalimbali ya nyani. Hawa ni pamoja na punju weusi na weupe, punju nyekundu, Nyani, tumbili wa shavu ya kijivu, tumbili mwenye mkia mwekundu, tumbili wa samawati, na tumbili wa aina ya “hoest”. KAFRED sasa inasimamia zoezi la kuhesabu aina hizi katika eneo la utalii na sehemu ambapo bodi ya kutembea imepangwa, ili kutathmini athari ambayo shughuli za binadamu huenda ikawa nayo kwa idadi ya nyani. Aina ya ndege ni zaidi ya 200, na ni pamoja na Great Blue Turaco ambayo in nadra, na yenya kupitishwa na KAFRED kama alama yao. Aina kama warbler, kurea, crane, na flycatcher pia hukaa katika kinamasi Bigodi na kuvutia idadi kubwa ya watazamaji wa ndege.

Kupunguza migogoro ya binadamu na wanyamapori

Migogoro ya binadamu na wanyamapori, imeleta tatizo kubwa ya kijamii kwa wakazi wa Bigodi, hasa kwa wale wanaoishi pembeni mwa eneo hifadhi. Uporaji wa mazao umekuwa changamoto kuu, ingawa utafiti umeonyesha kwamba wanyama wa nyumbani huaribu zaidi mazao kuliko wanyama pori. Hifadhi ya Taifa ya Msitu Kibale imetumiamitaro na ua ili kuzuia tembo kuvuka na kuingia katika maeneo ya makazi ya binadamu, ingawa juhudi hizi mara nyingi haziimarishwi, au wenyewe huingilia ardhi ya wakulima. Kinyume chake, KAFRED imewahimiza wanakijiji kutumia mbinu za jadi kama vile kupanda wigo mwiba na kufuatilia ili kuzuia nyani kupora mazao yao.

Hiki kikundi kwa sasa kinafanya kazi na UNITE na pia mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Msitu Kibale ili kuongeza maarifa miongoni mwa jamii kuhusu jinsi ya kupunguza migogoro baina ya binadamu na wanyamapori. Kutumia dola 3,000 ruzuku kutoka Cleveland Zoo, KAFRED inasaidia kufanya mafunzo manne juu ya migogoro baina ya binadamu na wanyamapori kwa ajili ya wanachama 200 wa vyama vya wazazi na waalimu na Kamati simamizi za shule katika eneo la kilomita tano kutoka kwa hifadhi. Hatimaye, jitihada za kukabiliana na migogoro baina ya binadamu na wanyamapori zitawekwa katika kamati tisaza shule. Mikakati ni pamoja na kuongeza matumizi ya “mazao shikilishi” kwenye mashamba ilikuzuia wanyama tatizo; kuanzisha na kudumisha mitaro kusitisha uvamizi wa tembo; kutumia pilipili kali kama njia ya kuzuia wanyama; kupunguza matumizi ya sumu kwakuua wanyama; ushirikiano zaidi kati ya jamii ya Bigodi na Mamlaka ya Wanyamapori ya Ugana (UWA), na wito kwa uwajibikaji zaidi katika jinsi maafisa wa serikali ya eneo hilo hukabiliana na maswala haya.

9

Jedwali: Walengwa wa KAFRED, 2011

Aina Idadi

Wanachama wa KAFRED wanaopigakura 117

Wanachama wa KAFRED wasiopigakura 37

Wafanyakazi (viongozi, mameneja, walimu, na wafanyakazi wengine wasaidizi)

33

Wazazinawatoto wa shuleyasekondari 500

Wanachama wa vikundi vya wanawake 110

Watumiaji rasilimali ya ardhi oevu Takribani familia 300 inakadiriwa kwa wastani wa watu 8 kila moja, kufanya jumla ya 2400

Watalii Wastani wa 4,000 kila mwaka

Wekezaji katika biashara ya uchukuzi wa utalii Makampuni zaidi ya 20 yakuelekeza ziara pamoja na makampuni na wakurugenzi wao, wafanyakazi na familia inakadiriwa kuwa watu 250

Watoaji huduma(malazi, chakula na upishi) Angalau 15 watoa huduma wafanyakazi wao inakadiriwa kuwa watu 225

Wakina mama wenye kusaidiwa na wakunga / mwaka Takribani 100

Chanzo: KAFRED

Page 10: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

MATOKEO YA KIJAMII NA KIUCHUMIMatokeo ya kijamii na kiuchumi kwa KAFRED katika kituo cha biashara cha Bigodi yamedhihirika hasa kupitia uwekezaji katika elimu ya sekondari. Hii ni pamoja na ujenzi wa majengo ya shule na kusaidia ada na mishahara ya wanafunzi na walimu. Miradi ya afya pia imeanzishwa, ilhali faida za kiuchumi zimepatikana kwa jumuiya husika kwa njia ya msaada kwa Kikundi cha Wanawake cha Bigodi na mradi wa mkopo kwa ajili ya familia zinazofanyaukulima.

Walengwa wa moja kwa moja

KAFRED inaajiri moja kwa moja wanakijiji 11 katika ofisi zake na kama waelekeziwa ziara. Walimu na wafanyakazi ishirini wameajiriwa na KAFRED katika shule ya sekondari, na pia wapishi wawili. Kituo cha Sayansi pia kinaajiri mfanyikazi mwingine zaidi. Katika nyakati mbalimbali, miradi ya ujenzi ya KAFRED pia imezalisha mapato kwa ajili ya wafanyakazi wa sehemu hiyo, kama vile katika maktaba ya shule, nyumba ya wakunga katika kitengo cha afya, na katika kudumisha njia za utalii. Faida ya kazi ya KAFRED imedhihirika miongoni mwa watu wengi, pamoja na wale wanatoa huduma kuhusiana na utalii na wale wanaotumia rasilimali za ardhi oevu.

Faida nyingine ya kijamii kwa jamuiya ya Bigodi imekuwa mradi wa maji safi ulioanzishwa na KAFRED kupunguza utegemeaji wa maji chafu kutoka kwa vyanzo vilivyoko katika ardhi oevu. Hii pia ilipunguza kutolewa kwa maji kutoka eneo la ardhi oevu. KAFRED imetumia michango kutoka kwa utalii na ufadhili kutoka kwa washirika kusukuma maji safi kutoka kwa chanzo cha maji kilichoko katika eneo hifadhi iliyo karibu. Wakati huo huo, bodi za kutembea kupitia ardhi oevu hutumiwa na wanajumuiya ili kuvuka kutoka eneo moja ya kijiji hadi nyingine. Ushirikiano wa KAFRED na Mradi wa Kuni wa Kibale pia umesababisha ujenzi wa majiko ya mafuta ya ufanisi

kwa ajili ya familia za Bigodi, kupunguza shinikizo juu ya misitu kwa ajili ya kuni na kuboresha hali ya afya ya washiriki.

Hiki kikundi kimehimiza shughuli badala za riziki ambazo zimesaidia kuongeza mapato kwa familia na kuhimiza wakulima wa Bigodi kujiepusha kuingilia maeneo ardhi oevu. Hizi biashara ikolojia ni pamoja na ufugaji nguruwe, ufugaji mbuzi, na kupanda mboga kwa ajili ya kuuza, na zimefadhiliwa na mfuko wa mikopo unaozunguka. Hadi sasa, angalau 90 miongoni mwa nyumba 120 zinazopakana na ardhi oevu zimepokea mkopo. Familia hizi ziko na wastani wa wanachama nane, zikitoa zaidi ya walengwa 700 wa moja kwa moja kutoka kwa mradi badala wa riziki wa KAFRED.

10

Chanzo: KAFRED

Ulishaji wambuzi/kondoo

Ulishaji wanguruwe

Uzalishaji Mazao

Biashara/uwekaji duka

Ukulima wangombe

Ukulima wamboga

Upandaji wamiti

Mengine

Kielelezo: Jinsi mfuko wa fedha umetumika (2011)

Page 11: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

11

MATOKEO KATIKA SERAShughuli nyingi za KAFRED zimehusisha uhusiano wa karibu na serikali za mitaa katika ngazi mbalimbali. Hizi ni pamoja na halmashauri za mitaa katika kijiji, parokia, kata ndogo, na ngazi ya wilaya. Mamlaka ya serikali za mitaa walikuwa muhimu hasa katika kutengeneza sheria za kijiji kusimamia matumizi ya ardhi katika ardhi oevu, na katika kuhimiza kushiriki kwa jumuiya katika miradi ya KAFRED

Katika ngazi ya kitaifa, KAFRED alisaidia kuanzisha Chama cha Utalii wa Jumuiya cha Uganda (UCOTA) ikiwa na lengo la kutetea kwa niaba ya miradi ya jumuiya katika ngazi ya kitaifa. KAFRED ilikuwa mojawapo wa takribani vikundi thelathini zilizoshirikikatika uundaji wake, ambayo iliungwa mkono na mradi wa hifadhi wa USAID. Wazo hili lilikuzwa mwaka 1995 wakati wa warsha ya mafunzo juu ya usimamizi wa utalii kwa vikundi jumuiya vinavyokaa maeneo ya hifadhi za kitaifa za Uganda. Nyingi katika hivi vikundi viliendelea

kuwasiliana kwa karibu, na KAFRED pamoja na Kundi la Wanawake la Bigodi walikuwa muhimu katika kuanzishwa kwa chama hicho mwaka wa 1998. Tinka Yohana Amooti, mwanachama mwanzilishi wa KAFRED, alihudumu kama katibu wa kitaifa wa kwanza, na uhusiano wa karibu uliokuzwa ulimaanisha kwamba KAFRED ilichangia pakubwa katika shirika hili la kitaifa. UCOTA imeweza kufanikiwa kushawishi sera ya utalii ya Uganda, na kukuza msisitizo zaidi kwa miradi ya jamii. Wamekaa katika kamati za kupanga kwa ajili ya kuandaa sheria za utalii za kitaifa, na kuchangia kuandaa sera ya utalii mwaka wa 2003.

Katika mwezi wa Februari 2012, bunge la Uganda liliandaa kwa mara ya kwanza nchini humo “ wiki ya utalii “. Tinka Yohana Amooti aliwasilisha mafanikio ya KAFRED moja kwa moja kwa bunge - kama mmoja wa wawakilishi wawili tu wa mipango ya utalii jamii. Hili tukio la kihistoria, ambalo lengo lake lilikuwa kujadili uwezo wa Uganda katika utalii wa mazingira, lilihudhuriwa na spika wa bunge, mawaziri wa utalii, wanyamapori na urithi, wabunge, na wawakilishi wa sekta ya utalii binafsi.

Page 12: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

12

Uendelevu na Uigaji

UENDELEVUUendelevu kishirika na kifedha wa KAFRED umewezeshwa na mbinu zao za uhifadhi, utalii wa mazingira, na shughuli za maendeleo. La muhimu kwa mafanikio ya mipango ya maendeleo ya jamii yao imekuwa ushiriki wa jamii. Hii ilikuwa muhimu mwaka wa 1992, wakati wanachama waazilishi wa KAFRED waliweza kujifaidi na mafunzo kutoka kushindwa kwa mashirika ya kijamii hapo awali, na mwakani 1995, wakati KAFRED iliwezesha kuchora sheria ndogo za kijiji za kutawala matumizi ya ardhi katika maeneo ya ardhi oevu.Pia ilitekeleza jukumu katika uanzilishi wa Kundi la Wanawake la Bigodi kama chombo tofauti, na kuepuka mvutano ambao ungetokana na ushiriki wa wanawake katika KAFRED yenyewe. Michakato shirikishi ya jamii, ilisaidia kuanzisha mradi mkopo kwa ajili ya familia zinazohusika na ukulima, ilhalivipengele vyote vya kijiji cha Bigodi vinawakilishwa katika wanachama wapigao kura wa KAFRED. Hiki kikundi kinaongozwa na kamati teule ya wajumbe saba, ambao huchaguliwa tena kila miaka miwili. Wanachama wengi wa kikundi wanatoka kwa jumuiya ya vijana wa Bigodi.

Katika suala la uendelevu wake kifedha, KAFRED hufanya bajeti ya mapato yake, 90% ambayo hutoka kwa utalii utembeaji wa bodi, ili kufidia mishahara ya wafanyakazi wake. Miradi ya maendeleo ya jamii ambayo si endelevu, au inayotegemeafedha za wafadhili kutoka

Jedwali: Chanzo cha fedha Kwa Mwaka 2010/11

Chanzo cha Fedha Asilimia ya jumla ya mapato

Matembezi yaliyoongozwa(katika kinamasi na kijiji) (karibu dola 50,000) 90.5%

Michango na misaada ndogo 8%

Ada ya mafunzo kwa waelekezi 0.9%

Uuzaji wa zawadi 0.6%

Chanzo: KAFRED

Page 13: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

1313

nje huepukwa; badala yake KAFRED imeweza kulipia gharama za shughuli hizi kutumia mapato ya utalii wa mazingira na misaada isiyo ya kurudiwa, kama iliyopokewakatika mwaka 2004 kutoka kwa Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) inayotekelezwa na UNDP kupitia mradi wake wa ruzuku ndogo.

Kuepuka kutegemea zaidi utalii mazingira

Ushirikiano wa KAFRED na UWA kupitia Hifadhi ya Taifa ya Msitu Kibale, imehakikisha kwamba KAFRED imebakia kujulikana kwa uwazi na wageni, na inaendelea kukua kivutio cha utalii katika eneo hilo. Hata hivyo, shirika hili linatambua kwamba kujitegemea zaidi kwa utalii mazingirakutadhoofisha uendelevu wa kifedha wa mradi huo.. Hii ilikuwa dhahiri mwaka 1999-2001, wakati idadi ya watalii katika magharibi mwa Uganda ulishuka baada ya watalii wanane kuuwawa katika Hifadhi ya Taifa Fungamana ya Msitu Bwindi mnamo Februari 1999. Athari ilihisika huko Bigodi, kupunguza idadi ya utalii - na hivyo mapato – kwa takriban 60% kwa miaka mitatu.

Ili kushughulikia suala hili, mpango mkakati wa KAFRED unahusisha lengo la kukusanya angalau 20% ya jumla ya mapato kutokana na shughuli zisizotegemea utalii wa mazingira na zinazozingatia mazingira kufikia mwaka wa 2016, wakati ikidumisha ongezeko la wastani katika mapato ya jumla ya 10%. Mpango mkakati pia inaeleza haja ya kuongeza kuelewa kwa mazingira miongoni mwa jamii inayopakana na ardhi oevu angalau kwa 60%; kupunguza zaidi kuingiliwa na upandaji mikaratusi katika ardhi oevu; kudumisha kiwango kikubwa cha fedha za KAFRED kuchangia kwa afya, elimu na mahitaji ya miundomsingi ya jamii katika Bigodi; kuongezea zaidi shughuli za kuwaingizia mapato jamii inayopakana na ardhi

1,401

578 525 504

2,373

0

500

1000

1500

2000

2500

1994 1995 1996 1997 1998 1999 2000 2001 2002 2003 2004 2005 2006

Kielelezo: Idadi ya Wageni ya KAFRED, 1994-2006

Chanzo: KAFRED

Page 14: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

14

oevu; na kuwekeza 20% ya mapato ya kila mwaka katika ujenzi wa miundombinu ya kutosha kwa ajili ya shughuli zausimamizi wa KAFRED. Huu mpangilio wa kimbele unaweka mradi huu katika hali nzuri yakukabiliana na changamoto zinazoikumba.

UIGAJIKAFRED imewapokea wageni kutoka kwa makundi mengine inayoshiriki katika kuendeleza utalii wa jamii, uhifadhi, au miradi ya maendeleo; mfano wao wa ushiriki wa jamii na miaka 18 ya uzoefu zimefanya mradi huu kuwa mfano wa kuigwa kwa taratibu hizi. Mashirika yasiyo ya kiserikali pia hukaribia KAFRED ili kupewa mafunzo na ushauri, ilhali kazi uigaji umefanywa katika milima ya Rwenzori na maeneo ya Msitu Bwindi. Hii ni pamoja na kuendeleza matembezi kijiji katika maeneo ya utalii wa mazingira changa, kwa mfano.

Mwaka wa 2003, kazi ya KAFRED ilishirikishwa kama mfano wa utalii wa kijamii unaochangia kupunguza umaskini na uhifadhi katika jarida la Shirika la Utalii Duniani ya Umoja wa Mataifa. Jopo la wataalamu wa kimataifa walichagua KAFRED kama mojawapo ya uhudi mbili za Uganda zilizoonyeshwa, baada ya Halmashauriya Utalii yaUganda kualikwa kuwasilisha kesi za masomo mafanikio za utalii wa mazingira. Kwa upande wake, UCOTA iliiomba KAFRED

kutoa masomo ya njia bora kuhusu fedha zao na ufadhili, uendelevu na udhibiti wa shughuli za utalii wa mazingira. Mfano wa KAFRED ilichapishwa katika ‘Maendeleo Endelevu ya Utalii Ikolojia - Mkusanyiko wa Mazoea Bora katika SMEs’ (WTO, 2003).

Ni lazima ikubaliwe, hata hivyo, kuwa kikwazo kimoja cha kubadilishana maarifa nchini Uganda imekuwa lugha nyingi za kikabila zinazozungumzwa. Jamii au mienendo kundi inaweza kuwa tofauti kabisa katika maeneo mengine ya nchi, na hii mara kwa mara imefanya “kupandikiza” mfano wa KAFRED iwe ngumu. Hata hivyo, KAFRED imeweza kuwa mfano wa kuigwa katika ngazi ya kitaifa n kimataifa.

WASHIRIKAWashirika mbalimbali wamekuwa muhimu sana kwa kazi ya KAFRED. Zifuatazo ni baadhi, ingawa si zote, ya makundi ambayo yamechangia mafanikio yao.

• Asili ya Uganda• Chama cha Utalii wa Jamii Uganda (UCOTA) kimesaidia kutoa

mafunzo bora katika maeneo kama vile uelekezi, usimamizi wa utalii, masoko, utengenezaji was bidhaa za mikono, na upatikanaji wa soko kwa ajili ya kazi za mikono za wanawake.

• Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA) imetoa mafunzo ya uelekezi na ya fedha na kwa njia ya kugawana mapato ya hifadhi

• IUCN imetoa mafunzo ya kujenga uwezo katika usimamizi wa ardhi oevu na imetoa vifaa vya ofisi.

• North Carolina Zoo ilitoa fedha kwa ajili ya shule ya sekondari, na imeshirikiana na KAFRED kupitia UNITE; Cleveland zoo pia imefadhili mradi huu.

• Chuo Kikuu cha nyanjani cha Chuo Kikuu cha Makerere huko Kibale hutoa watafiti wasaidie katika kuendesha ufuatiliaji katika ardhi oevu.

• Mradi wa kuni wa Kibale ushiriki katika usimamizi wa kituo cha sayansi cha Bigodi na husaidia kuelimisha jamii jinsi ya kuhifadhi kuni.

• Wakfu wa Maendeleo ya Rwenzori imetoa fedha na vifaa vya nyanjani kwa ajili ya utalii wa mazingira.

• Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) inayotekelezwa na UNDP kupitia mradi wake wa ruzuku ndogo imetoa msaada wa kifedha kwa ajili ya kuandika masomo na kushiriki kwao na jumuiya nyingine nchini na kimataifa.

• Mradi wa Equator ya UNDP imeongeza hadhi ya kitaifa na kimataifa ya KAFRED, pamoja na kutoa fursa ya kupata washiriki zaidi nakujulikana na wanahabari.

“Uhifadhi hauwezi kufanikiwa bila ushiriki thabiti wa jamii. Wanahitaji kushirikishwa katika mchakato. Kufanya kazi na mashule ni njia muhimu kwa ajili ya elimu ya mazingira. Katika Rutooro, lugha ya mama, hakuna neno kama “hifadhi”. Elimu ni muhimu kwa ajili ya jamii

kuelewa na kushiriki.”Tinka John Amooti, Mkurugenzi, KAFRED

Page 15: CHAMA CHA MAENDELEO YA VIJIJI NA …...4 Chama Cha Maendeleo ya Vijiji na Mazingira Cha Kibale (KAFRED) ni asasi ya kijamii ifanyayo kazi katika Wilaya ya Kamwenge, magharibi mwa Uganda

Equator InitiativeEnvironment and Energy GroupUnited Nations Development Programme (UNDP)304 East 45th Street, 6th Floor New York, NY 10017Tel: +1 646 781-4023 www.equatorinitiative.org

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ni matandao wa maendeleo ulimwenguni wa Umoja wa Mataifa, kwa ajili ya kutetea mabadiliko na kuunganisha nchi kwa uzoefu, ujuzi na rasilimali ili kusaidia watu kujenga maisha bora.

Mradi wa Equator huleta pamoja Umoja wa Mataifa, serikali, mashirika ya kiraia, mashirika ya biashara, na mashirikaya mitaa ili kutambua na kuendeleza ufumbuzi wa maendeleo endelevu kwa ajili ya watu, asili na jamii shujaa. © 2012 na Mradi wa EquatorHaki zote zimehifadhiwa

REJEA ZAIDI

• Lepp, A., Holland, S. 2006. A Comparison of Attitudes Toward State-Led Conservation and Community-Based Conservation in the Village of Bigodi, Uganda. Society & Natural Resources, Vol. 19, Iss. 7.

• Mulindwa, D. 2007. Rethinking Community Participation in Ecotourism Management: The Case of KAFRED in Bigodi, Uganda. PhD The-sis, Ashcroft International Business School, Anglia Ruskin University.

• KAFRED tovuti: bigodi-tourism.org/1701.html

Bonyeza picha hapachini ili kusoma masomo ya kesi zaidi kama hii.