annuur 1101

Upload: annurtanzania

Post on 04-Jun-2018

571 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    1/12

    ISSN 0856 - 3861 Na. 1101 MUHARRAM 1435, IJUMAA , NOVEMBA 29-DES. 5, 2013 BEI TShs 500/=, Kshs 50/=

    Sauti ya Waislamu

    www.annuurpapers.co.tz

    Uk. 6

    Soda!

    Hujuma, changamoto

    kwa Dr. Shein, MaalimWanaohujumu SUK wanajulikana....Kigugumizi cha nini kuwakemea? Sheikh Chambuso RajabuAndha Kanoon nyingine

    Polisi, DC wasifanye kazi kwa chuki

    Sensa, kosa la mauwaji wapi na wapi?

    Operesheni Madinah, hatari tupu!

    Tukisema tusije kuambiwa wachochez

    NIANZE kwa kusemakuwa kutokana na habarizinazoibuka na kuchukahivi sasa, yapo madai kuwakulikuwa na ukiukwajimkubwa wa sheria nah a k i z a b i n a d a m uk a t i k a o p e r e s h e n ii l i yof a n yi k a k a t i k avijiji kadhaa wilayaniKilindi. Inawezekanakulikuwa na sababu zamsingi kabisa kufanyaoperesheni hiyo, lakininamna ilivyoendeshwana madai yanayotolewa

    hivi sasa na mashuhudawa operesheni hiyo, nahasa waathirika, inaachamaswali mengi kulikokutoa majibu. Uk. 7

    WAKATI wa kadhia yamabucha ya nguruwemwaka 1993, sikumabucha yanavunjwa,w a h a d h i r i w aKiislamu, akiwemoU s t a d h H a b i b u

    Mazinge, walikuwTemeke wakifanymuhadhara. Mabuchyanavunjwa Manzesna Magomeni, wawananguruma katik

    Inaendelea Uk.

    WAHITIMU katikaShule za Sekondariza Kiislamu nchiniw a m e t a k i w a

    Kuweni Waislamu popote mlipoWahitimu sekondari wapewa nasaha

    Na Bakari Mwakangwale kudhihirisha Uislamuwao sambamba nakusimamisha swalapopote watakapokuwa.

    Hayo yamesemwa na

    Alhaj Hassan Mjenja,akiongea na wanafunzipamoja na Waislamukatika mahafali ya kumi

    Inaendelea Uk. 3

    Sheikh Chambuso Rajab

    Alhaj Hassan Mjenja, akiongea na wanafunzi pamoja na Waislamu katika mahafaliya kumi na sita ya kidato cha nne katika Seminari ya Ridhwaa, yaliyofanyikaShuleni hapo Novemba 24, 2013.

    Na Juma Kilaghai

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    2/12

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    3/12

    3 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Habari

    Kuweni Waislamu popote mlipoInatoka Uk. 1na sita ya kidato channe katika Seminari yaRidhwaa, yaliyofanyikaShuleni hapo Novemba24, 2013.

    Mjenja aliwaelezawahitimu hao kuwa

    elimu ni amana na neemaambayo wataulizwanamna walivyoitumiana kuwataka kuiwekakatika vitendo elimuhiyo waliyoipata wakiwakatika shule zao.

    Z i n g a t i e n imafundisho ya dini yaKiislamu mliyoyapatam k i w a S h u l e n i n ayawekeni katika vitendohuku mkishikamana naswala popote mtakapokuwa, na dhihirisheniUislamu wenu popote ilimpate kufaulu.

    El imu mliyoipatani amana na ni neemamtakayoulizwa namnamlivyoitumia, alisemaAlhaj Mjenja.

    Alhaj Mjenja, alisemahuko nyuma Waislamunchini hawakuwa nafursa sawa ya elimu nawatu wa dini nyingine,hali iliyowafanya kuwawachache sana katikavyuo vikuu.

    A l i s e m a , v i j a n awanaohitimu hivi sasakupitia Shule mbalimbali

    za Kiislamu wamekiak i w a n g o a m b a c h ow a n a w e z a k u t o amchango mkubwa kwaumma wa Kiislamu na

    jamii kwa ujumla pamojana kuingia kwa wingikatika ngazi ya vyuo.

    Aliwataka wahitimuhao kufahamu kuwa,elimu waliyoipata nisehemu ndogo kwak u z i n g a t i a u s e m iusemao elimu ni baharina kwa hatua waliyokiani katika hatua ya awalikabisa katika kuingiandani ya bahari hiyo.

    Hivyo, Alhaj Mjenja,a l i w a t a n a b a i s h aw a h i t i m u h a ok u t o r i d h i k a a ukubweteka na kiwangocha elimu walichokipatana kuepukana na kibrikutokana na kiwangocha elimu walichokia,

    badala yake wajiendelezezaidi.

    Naye Mkuu wa Shulehiyo Mwalimu Ahmed

    Yahya, akiongea mbeleya mgeni rasmi, alisemakwa Muislamu kutafutaelimu ni faradhi na yeyoteanayejishughulisha nahilo anakuwa katika

    ibada jambo ambalohumpandisha darajambele ya Allah (sw).

    M w l . Y a h y a ,al isema pamoja nakuwa wanafunzi hao

    wanaagwa kwa kumalizaelimu watambue kuwaElimu ni Bahari naElimu haina mwishoh i v y o a k a w a t akutoridhika na elimu

    waliyoipata hapo.Aliwataka wahitim

    hao kuitumia elimu hiykwa manufaa ya yawenyewe na jamii.

    Jumla ya wanafunz77, wa kidato cha nnwamehit imu katikShule ya Ridhiwaakatika michepua ySanaa, Biashara nSayansi.

    Hivi karibuni tumekuatukisikia na kuonanamna umoja wa vijanawa CCM ama UVCCM,unavyoelekeza nguvu

    zake katika uwekezajina ufunguzi wa miradiya kibiashara. Lengolao moja wapo likiwani kujaribu kuuendeshaumoja wao kupitiamiradi hio na ni wazipia kulenga katikakujijengea umaarufumiongoni mwa vijana.

    Huu ni mkakati mmojawapo ambao ChamaCha Mapinduzi kupitiaumoja huo wa vijanawao wanaweza, iwapo

    nia na madhumuni yamalengo yao yatakua nisa kujijengea heshimamiongoni mwa vijana,iwapo ni kweli watawezakuisimamia miradi hiokatika kuwafaidishavijana katika ngazi yaajira. Mkazo ni hapokwenye siasa safi nauongozi bora.

    Nguvu kazi ya vijanawa CCM ambayo kwasasa inatumika katikakuendeleza siasa zamaj i taka, inaweza

    kubadilika na kuwam f a n o w a k u i g w akatika wanayoyakusudiakuyafanya, iwapo kwelilengo ni kuwainua vijanana si mradi wa mtuama kikundi cha watuwachache.

    Vijana hawa ambaowanatumika zaidi mudahuu katika kuvurumishamatusi kwa viongozi waupinzani na wapinzaniwao wa siasa kwa ujumla,na uendelezaji wa siasa za

    UVCCM waonyesha njia tunawasubiri Vijana-CUFNa Mwandishi Wetu mipasho kwa mtindo wa

    kidole jichoni, mipashoambayo haileti zaidiya mifarakano katika

    jamii, wanaweza kuwani mfano kwa vijana wachama pinzani na umojawa vijana wa CUF kuanzanao kukiria mbinu zaushindani wa kisiasakwa vitendo katikakujiletea maendeleo, nasio maneno matupu.

    M k o n o m t u p uhaurambwi. Ni msemowenye kulenga shabahakwamba mwenye kitucha kutoa, si sawa naasie na kitu mkononi.UVCCM wakifanikiwakuendeleza miradi mfanowa jengo walilolijenga

    na kutoa milango yabiashara liliopo darajani,maarufu Youth Leaguena mengineyo ambayowanakusudia kuwekeza,

    basi hio itakua ni hatuamoja kubwa na karataya kisiasa inayowezakuwavutia vijana kutakakujisogeza karibu nao.Hakuna anaependaumasikini na manenomatupu.

    Na kwa nini badalaya vijana hawa wa CCM

    kuekwa majukwaaniw a k a t u k a n a w a t uwazima na viongoziw a u p i n z a n i k w amatusi ya nguoni hukuwakiendeleza farka,wasiwe ni mfano wakuigwa kwa vitendo vyakimaendeleo na siasa saza ushindani!

    Viongozi wa siasa navijana wao washindanekwa kasi ya kuletamaendeleo katika jamii.Wewe umefungua mradi

    wa maduka basi miminakupiga kwa kufunguamradi wa kiwanda changuo. Mambo yawekama hivi, na matokeo

    b i l a ya k us u g uan an a k u s u k u m a n ayataonekana dhahirikatika jamii, na kawaidaya binadamu hufuatapale panapongara. Nifuata nyuki ule asali, japoanaweza kukuuma pia.Lakini maadhali asaliumepata, utavumiliamaumivu!

    M o j a t u a m b a l on i m u h i m u k a t i k amuktadha wa jambo hilini namna gani miradihii imeanzishwa, nawanaofaidika ni nani?

    Je uhalali wake tokeau a n z i s h w a j i w a k eupo? Ni jengo ambaloamenyanganywa mtu?Ni ardhi iliyopatikanakwa unyanganyi amauvamizi?

    Ni jambo moja kuwana miradi tofauti yakujiongoza na jenginetofauti iwapo miradih i o i m e p a t i k a n akatika mazingira yaudanganyifu na uonevu.

    N a i t i z a m a p i c h ahii inayoendelea kwam t i z a m o h u u w aushindani wa vyama vyakisiasa kivitendo katikakuwapelekea vijana waomaendeleo. Je, umoja wavijana CUF wamejipangavipi katika hili? Je, Vijanawa CUF watakua niwapiga makofi wazurimikutanoni ama uongoziwao nao wataanzakubuni mbinu kama hizi

    za kujiendesha.Enzi za vyama kuomb

    ruzuku na kutegemew a n a c h a m a w a kwawe ndio wachangiazimepitwa na wakat

    V y a m a v i t u m i k iwanachama wake badaly a k i n y u m e c h a kwanachama kukitumikichama kwa kubunmiradi tofauti.

    Uwezo wa chama kamCUF kufungua viwandvidogo vidogo kamvya ushoni na kuchongama miradi ya ufugajsidhani kama haupo, hisi kwa kukisia na walhalihitaji CUF iwe nmadaraka ya uraisi.

    Tutapokutana tenkatika majukwaa ys i a s a U V C C M i wimebadilisha sera ymatusi na badala yakiisute CUF kwa kukoskuwaandalia vijana wakmikakati ya kimaendelena vijana wa CUF nawajibu mapigo kwmifano bora zaidi yaoHuu ndio ushindanninaoutarajia wa ipi timnzuri katika maendele

    na sio uhodari wa matusTutapokia hatua kam

    hio hakutokua na hajya kudanganyana kwsera. Sera zitajionyeshkwa vitendo badala ymaneno matupu.

    Ikiwa lengo ni hilo nUVCCM wameanza, Jumoja wa vijana wa CUwataiga? Kuna maenemengi tu ya kuanzii l a tus ubi r i tuone(Mzalendo net)

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    4/12

    4 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Makala/Tangazo

    T U K I W A k a t i k akusheherekea miakamitatu ya SUK kunamambo yamejitokeza na

    hayapaswi kupuuzwa.I n a w e z e k a n a n ichangamoto, lakinimimi nadhani kunab aad h i ya mamb oy a n a h a r u f u y ahujuma. Kwanza hapatuelewane kwambakatika mfumo wowotempya, changamoto nisuala lisiloepukika.Hili nikiri lakini kilakitu kina MUKTADHAw a k e n a n i h u omuktadha unaoashiriau c h a n g a m o t o w akitu,ama umakusudi

    na taabani huwa nihujuma.Hebu tufikirie haya

    m a c h a c h e a m b a y okwangu mimi nayaonakwa j i cho l engi ne .Tukianza na milingoy a s i a s a t u m e o n awadau wakuu wa hioS U K w a k i n y u k a n am a j u k w a a n i . L akushangaza na kutisha,hata MATUSI SASAIMEKUWA ndio silaha

    baina ya pande mbilijambo ambalo halikuwal inatara j iwa kabisa

    katika hii inayoitwazama ya maridhiano,maelewano na umojawa kitaifa. Ubaya wamambo, hata viongoziwakuu wameshindwakukemea na imeonekanasasa kuwa ndio desturi,na zaidi kundi mojala siasa kutoka kwawahadhina wakongwewa Chama tawala. Sualila kujiuliza ni hil i ,inakuwaje wewe iweunajenga nyumba kwa

    bidii, halafu unapita kwanyuma kuja kuibomoa?

    J e e , h i i i t a k u w achangamoto au hujuma?Katika hili inaonekanakuna kundi limepangwana juhudi hizi kwa zaidizinajulikana kutokachama gani.

    W a c h a m b u z iwananasibisha harakatihizi na watu waliokataaumoja wa kitaifa nawanatumia mwavuliwa kichama kubomoaSUK huku wakijifanyawanaipenda. Wadadisiw a n a f i k a m b a l i

    Hujuma, changamoto kwa Dr. Shein, Maalim

    w a k i a m i n i k u w al engo l ao n i kut i aMTAFARUKU ndaniya GNU ili yao yatimiem a a n a h i i G N Uimekuwa kisiki kwao.

    Kwa up ande waWatendaji serikalini,nako kuna harufu namimi naiona si njemasana wala hainukii yalemawanda ya umoja.

    T a z a m a y a l emalalamiko kutokammoja ya viongoziwakuu wa GNu kuwailika wakati viongozifulani wa mikoa naw i l a y a h u m p i g achenga katika ziarakatika maeneo yao.Hivi tuseme nayo hii nichangamoto kweli aukuna harufu ya hujuma?K a m a i t a k u w a n ichangamoto, basi KAZITUNAYO maana itabidituandae WAVU wakuwazuwiya viongozi

    h a w a w a s i o n d o k ewanapokuja viongoziwakuu katika maeneoyao!

    Fikiria lile tukio lawamachinga na ziaraya V1 pale darajani nalokama ni changamoto.M p a k a l e o w a t uwanajiuliza nafasi yakiongozi wa kitaifa hatakama haiheshimiwi, jee,inafaa kupuuzwa kiasicha hata kuvunjianaheshima wazi wazi? Hiinayo ni changamoto

    kweli? Mimi naona kunakitu kimejicha na ikosiku kitachuka.

    Yale matusi na lughaza kuwatenga watukatika zama hizi mpyaza SUK, nazo huendani changamoto. Lakini

    je, hao viongozi ambaowanachama na viongoziw a v y a m a v y a ovinavyoshabikia haya,tuseme hawayaoni?

    Hawasikii? Jee, hii nayoni changamoto kiasicha hata kukemewakushindikana?

    H a y a n i b a a d h iya mambo ambayokwangu mimi naonay a n a w a l a k i n i n akunahitajika wataalamusasa wa kutenganishac h a n g a m o t o n ahujuma maana hapaZ a n z i b a r m u d a s i

    mrefu tutaongoza kwkuwa na aina nyingza CHANGAMOTOkuliko sehemu yoyotile duniani.

    Mwisho tutafakahaya tukijuwa kuwa kilmmoja ana wajibu wkuhimiza mshikamanna umoja wa kitaifa.

    (Makala hii ni kwhisani ya mtandao wkijamii-Mzalendo net

    UDHAMINI WA WANAFUNZI WA SEKONDARI

    Al-farouq Islamic SeminaryP.O.BOX 9211, Tell 2807843, Dar es salaam

    Uongozi wa Alfarouq Islamic Seminary unawatangazia nafasi za udhamini wamasomo wazazi wa Kiislamu wenye watoto wa kiume waliomaliza darasa la sabamwaka 2013 na kupata wastani wa Grade A au B, utaratibu wa kufuata ni huuufuatao;-

    Kuja kuchukua fomu ya kujiunga na shule Al-farouq Islamic SeminaryTabata- Bima.

    Kuja na nakala ya matokeo ya mtoto husika kutoka kwenye mtandao Internet)

    Kuwa tayari kufanya usaili (Interview) tarehe 14/12/2013 shuleni Al- farouqIslamic Seminary.

    NB:Fursa itatolewa kwa wale watakaofaulu vizuri katika usaili wa shuleni Alfarouq Islamic Seminary.Udhamini unaotolewa ni kwa kulipiwa ada tu kwa mwanafunzi wa kutwa(day) na mwanafunzi anayedhaminiwa na akataka kukaa bweni itabidi alipekiasi cha pesa kilichobaki kutimiza ada ya mwanafunzi bweni.

    Karibuni Al- farouq Islamic Seminary kwani tumejipangakuwahudumia.

    Kwa mawasiliano zaidi tafadhali piga simu namba.0717 176262, 0712 164208,0782 023033.

    Wabillah Taufq

    RAIS mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume (kushoto) akizungumza na Rais wa sasa Dkt. AMohamed Shein (katikati) na makamu wake, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia)

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    5/12

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    6/12

    6 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Makala/Tangazo

    KAMA wewe ni teja wavitu vitamu, bila shakahabari hii itakukera.Itakukera kwa sababuinashambulia moja yavitu ambavyo ni vitamusana katika dunia yetuya leo - soda. Soda nitamu kweli kweli, hakuna

    ubishi. Itaacha vipi kuwatamu wakati kiasi charobo lita ya kinywajihicho kimebeba wastaniwa vijiko tisa vya chai vyasukari?

    Madhara ya sukariy a n a e l e w e k a . K w akukumbushana tu, sukariina madhara mengi yakiafya ikiwa ni pamoja na:

    1. Kus hus ha sanakinga za mwili za mtumiaji;

    2. Kupunguza uwezowa seli nyekundu za damukusambaza gesi ya oksijenimwilini;

    3 . Kumharakishia

    mtumiaji kasi ya kuzeeka;4 . K u m w o n g ez eamtumiaji kiasi kikubwacha uric acid mwilini, nahivyo kumweka katikahatari ya kukabiliwa nashinikizo la damu, maradhiya moyo, na ugonjwa wajongo (arthritis);

    5. K u c h o c h e aongezeko la uzito wamwili; na

    6. kuchochea kasi yakukua na kusambaa kwaseli za saratani.

    Wa t en g en ez a j i w asoda, kwa kuona kuwawateja wao wanaanzakujanjaruka, na wanahojiusalama wa kinywajihicho, wamebuni njia yakuendelea kuwashikilia,huku wenyewe wakijihisikuwa wako salama! Njiahiyo ni kuja na aina yasoda wanazodai kuwahazina sukari, maarufukama calorie free sodasau d iet sodas . Hatahivyo ukweli ni kwambas o d a h i z i z i n a k i d h imatakwa ya ule msemomaarufu wa Kiswahiliu n a o s em a U m er u k amkojo ukakanyaga !au umeruka maj ivuukakanyaga kaa la moto.

    Soda!

    Na Juma Kilaghai

    Sababu ya kusema hivini kuwa soda hizi huwaz i n a n o g e s h w a k w avinogesho (sweeteners)bandia ambavyo aghalabuni hatari kuliko hata hiyosukari halisi. Vinogeshohivi ni kama Nutrasweet,Equal na Spoonful.

    Ubaya wa vinogeshohivi ni kwamba vyote

    v i n a t e n g e n e z w a n ak e m i k a l i a i n a y aASPARTAME. Taf i t imbalimbali zinaituhumukemikali hii kuwa inamadhara makubwa kiafya.Kemikali hii imekuwaikituhumiwa tangu miakaya 1970 kuwa ilikuwainasababisha saratani yaubongo. Tuhuma hizizilikuja baada ya matokeoya tati nyingi zilizofanyikakupitia panya wa maabarakuonyesha hivyo.

    Pamoja na tuhuma hizi,Taasisi ya Chakula naDawa ya Marekani (FDA)iliidhinisha matumizi yakekama kinogesho mbadala

    wa sukari, kwa majumbanina migahawani, mnamoJuly 1981. Miaka miwiliba ad ay e, mn am o July1983, FDA iliidhinishamatumizi ya kemikali hiikwa matumizi mapanazaidi, pale ilipoidhinishaitumike kama kinogeshobandia cha v inywaj iv i n a v y o t e n g e n e z w av i w a n d a n i . Wa t a f i t iw a n a s e m a k u w amwaka mmoja baadaya idhini hii kutolewaidadi ya Wamarekaniwalioathiriwa na ainambalimbali za saratani yaubongo iliongezeka kwaasilimia kumi (10%)!

    Kemikali ya Aspartamehuundwa kwa uwianoufuatao: Asilimia kumi(10%) kemikali ya ainaya methanol, asilimiaarobaini (40%) kemikaliya aina ya aspartic acid,na as i l imia hamsini(50%) kemikali ya ainaya phenylalanine. Wakatikemikali ya methanolinajulikana wazi kuwahusababisha uharibifu waneva ya kuonea (opticalnerve) na kupelekeamuathirika kukumbwa naupofu; kupitia majaribioyaliyofanyika kwenyep a n y a w a m a a b a r a ,kemikali ya aspartic acid

    imethibit ishwa kuwainatoboa matundu kwenyeubongo. Kwa upandewake, phenyla lanineinapoingia mwilini hupitiamabadiliko yanayopelekeakuzaliwa ndani ya mwilikwa kemikali aina yadiketopiperazine (DKP).DKP ni miongoni mwavichocheo vianzilishivikubwa vya ugonjwa wasaratani.

    Madhara ya Aspartamekama kisababishi chasaratani hayaishii kwenyekutengenezwa kwa DKPpekee ndani ya mwili.A s p a r t a m e p i a i n a

    uwezekano mkubwa wakusababisha saratani palemtumiaji atakapotumiabidhaa zenye kemi ka lihiyo, ambazo zimewekwakwa muda mrefu, kwenyehali ya hewa yenye jotozaidi ya nyuzi joto 30 katikakipimo cha centigrade.Hali hii hujitokeza kwamfano, kwenye maghalayasiyo na viyoyozi, auwakati wa kusafirishwakwa bidhaa hizo kwenyemalori yasiyo na majokofu.

    K a t i k a m a z i n g i r aya aina hii kemikali yamethanol iliyomo katikaAspartame hubadilikana kuwa kemikali ainaya formaldehyde; na

    kisha kemikali aina yaformic acid. Zote mbili,formaldehyde na formicacid, ni vichocheo vianzilishi vikubwa vya

    ugonjwa wa saratani.Kitaalamu formaldehydeinawekwa kundi moja nasumu hatari kama vilekemikali za aina ya cynidena arsenic.

    T a f i t i m b a l i m b a l iz i m e b a i n i s h a k u w au k i o n d o a a i n ambalimbali za sarataniya ubongo, Aspartamepia inasababisha sarataninyingine kadhaa zikiwemozile za viungo vya uzazikwa jinsia zote, na sarataniza damu aina ya leukemia

    na lymphoma. Hizi nsaratani zinazoathirchembe nyeupe za damuambapo katika leukemikunakuwa na ongezekkubwa la seli nyeupe zdamu zinazoshindwkupevuka, wakati katikl y m p h o m a k a s i ykugawanyika kwa senyeupe za damu inakuw

    kubwa sana ukilinganishna seli za kawaida, au uhwa seli hizo unakuwa nmrefu ukilinganisha nseli za kawaida.

    Kukaa mbali na sodni moja ya njia mujarabza kuilinda afya yakkwa ujumla, lakini kukambali na soda zinazotumvinogesho bandia nmoja ya njia za kujikingdhidi ugonjwa hatari wsaratani.

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    7/12

    7 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Makala

    Sheikh Chambuso RajabuAndha Kanoon nyingine

    NIANZE kwa kusemak u w a k u t ok a n a n ahabari zinazoibuka nakufichuka hivi sasa,y a p o m a d a i k u w akulikuwa na ukiukwajim k u b w a w a sh e r i a

    na haki za binadamuk a t i k a o p e r e s h e n ii l iyofanyika kat ikavijiji kadhaa wilayaniKilindi. Inawezekanakulikuwa na sababu zamsingi kabisa kufanyaoperesheni hiyo, lakininamna ilivyoendeshwana madai yanayotolewahivi sasa na mashuhudawa operesheni hiyo, nahasa waathirika, inaachamaswali mengi kulikokutoa majibu.

    Miongoni mwa madaini kuwa watu wameuliwa,wamejeruhiwa, mal ikuporwa na nyumba zao

    kuteketezwa kabisa kwamoto. Hadi sasa baadhiya watu hawajulikaniwalipo na ndio maanakuna watoto bado wapomikononi mwa serikalimjini Tanga.

    Inadaiwa pia kuwahadi hivi sasa hali sishwari kwa watu wenyendevu au kuvaa kanzu,k w a k u t u h u m i w akwamba ni magaid iambapo hufanyiwa visambalimbali. Kama madaihaya ni kweli, tunasemahii si sahihi kabisa.

    T a a r i f a k w a m b a

    viongozi wa taas is iz a K i i s l a m u T a n g a ,wanakusudia kuonana naMkuu wa Mkoa ili kupatakibali kwenda kufanyauchunguzi na kujuakwa uhakika yaliyojiri,ni jambo la kupokewakwa mikono miwili kwanihuenda likasaidia sanakatika kujua ukweli nakusawazisha mambo.

    Katika siku za nyumaniliwahi kuandika makalaikiwa na kichwa cha habari:Andha Kanoon, SMZ nayale ya UAMSHO.

    Kichwa kidogo cha

    habari kikisema: DPPUnguja, msikilize AmitabhBachchan.

    Kat ika makala h i iningependa nirejee yaleniliyosema katika makalaile, ila hapa niseme kuwaDC Halima Dendegua m s i k i l i z e A m i t a b hBachchan.

    Nilianza makala ilekwa kueleza kisa chamama na binti yakemdogo wanamchunguliakwa uchungu mtu aliyekorokoroni. Mtu yuleanayeonekana kuchokaakiwa na huzuni kubwa

    Na Omar Msangi

    kwa masaibu ya kuwa jela.Anawafuata taratibu nakuongea nao wakitizamanakupitia lango la chuma.Baina ya vyuma vyamlango (iron bars) panauwazi ambapo wanawezakuonana na kupitishamkono kushikana.

    Hawa ni mke na mumena binti yao Neelo. Mkeanalia na mume machoziyanatiririka akijaribukumfariji mkewe.

    S i s i k i t i k i n akuhuzunika kuwa jela,huzuni na uchungu wanguni juu yenu. Mtaishijemke wangu na binti yetumpenzi Neelo.

    Anapomwona babaanatoa machozi, Neelo,bi nti md og o wa kia simiaka 5 anaimba wimbowa kumtoa huzuni babayake:

    Learn to laugh whilecrying. Learn to cry whilelaughing. As much life as GodHas given us, we will live thatmuch.

    We are two and we havea lile girl. That is our smallworld. With happiness isfi lle d every corner of ourhome.

    There are big joys insmall things. Like shiningstars in long nights.

    Huo ni wimbo ambao,Jan Nissar Akhtar Khan,al ipenda kumwimbiamwanawe huku akichezanaye anaporejea kutokakazini. Ufupi wa maneno

    akionyesha jinsi wawiliyeye na mkewe pamoja namtoto wao, walivyokuwawakiishi maisha ya furaha.

    Katika wimbo huubaba anampa nasaha bintiyake akimwambia awena furaha muda wote.Asipende kuwa mtu wa

    majonzi na kulia bilampango. Acheke hataanapokuwa na jambo lakumtoa machozi.

    Leo ni zamu ya bintikumfari j i baba yakealiyeko jela anapolia kwauchungu wa namna mbili:

    Kwanza kufungwaje la kw a kos a am ba lohakutenda. Pili, kuonafamilia yake ikiteseka kwakukosa huduma, hurumana mapenzi ya mume nababa.

    Wakiwa bado wanahamu ya kuongea, anakujaaskari na kuwaambiamuda umekwisha wakuongea na mfungwa.Inabidi mke aondoke hukuwakitizamana kwa huzunina mumewe.

    Wa k a t i a k i o n d o k abi nt i anab ub uj ik wa namachozi huku akiimbarote rote., anageukanyuma na kumtizama babayake, mtoto analia kwakwikwi hali inayomfanyaba ba na ye ku shi nd wakuhimili na kuelemewana uchungu, anashindwakabisa kumtizama Neelo.

    (Nakushauri msomajitafuta filamu Andha

    kanoon uitizame kwamakini. Kama unajuaKiingereza, tafuta yenyeEnglish sub-tile)

    Haikupita siku nyingibaada ya kutembel ewana mkewe, mfungwaJan Nissar Akhtar Khan(Amitabh Bachchan)

    anapokea barua kutokakwa mkewe ikimfahamishakuwa ameamua kujiuwayeye na kumuuwa bintiyao kwa sababu hatawezakuhimili tabu ya maishabila mume wake mpenzialiyeko jela. Anasemaamebakwa na watu wanne.Na hivyo haoni sababu yakuishi tena katika maishahayo ya fedheha.

    Anasema: Akijiuwa,Nini itakuwa hatmaya Neelo ambaye babayake yupo jela na ambayemama yake anakaribiakujiuwa?.

    Neelo atabakia pekeyake Awe nani akiwahana elimu kwa sababuhana baba wala mama wakumsomesha? Kibaka,mwizi, ombaomba aumalaya changudoa?

    Mimi ni mama, siwezikukubali kuona mtotowangu akiwa katika halihiyo.

    That is why I am takingher along with me. May Godforgive me.

    K w a m a a n a h i y o ,nimeamua kuondokanaye. Namnyonga kishanamimi najiuwa. Wako

    mkeo mpenzi ZakhiyMungu wangu nisamehe

    M f u n g w a K h aanatolewa jela na kwendkushiriki mazishi ymkewe na mwanaweAnapowalaza kat ikmwanandani, inamjip i c h a w a l i v y o k u wwakiishi kwa furaha huk

    sauti ya kuimba rote rotWe are two and w

    have a little girl. That our small world. Withappiness, is lled evercorner of our home.

    Kwa vile alikuwa kazoekumletea binti yake zawadya chokleti, anaonekanakiweka chokleti ndani ysanda ya binti yake azikwnayo.

    Hiki ni kisa ambachkipo katika filamu yKihindi (Bollywood filmya mwaka 1983 iitwayAndha Kanoon(Blind LawKatika filamu hii kijan

    Pankaj Sonker (Jan NissaAkhtar Khan ) anaajiriwkama asa misitu baadya kumaliza masomyake. Anaonekana akiishkwa furaha na mkewZakhiya pamoja na binyao Neelo. Siku mojakiwa kazini , Sonkeanakutana na majangili wmbao wakiwa wamevunna kuchukua magogkutoka katika moja ymisitu anayoisimamia biya kibali. Anaonekanakiwakabili na kadirwalivyotaka kumhonga k a g o m a a k i s i m a mkatika sheria.

    M w e n y e k a m p u nile iliyokuwa ikivunmagogo kinyume chsheria akamwambia kuwal ikuwa amemwekedau a f i sa mwenzakaliyekuwepo kabla yakKila mwezi akimpa Rup1,000. Sasa yeye atampRupia 1,500 mpaka 2,00kwa mwezi. Hata hivykijana mchapakazi akiwna hamu ya kufanya kazkwa mujibu wa sheria nkama mzalendo mtetemasilahi ya nchi, akakata

    S i k u m o j a a k i wnyumbani na mkew

    akajiwa na kikosi chaskari waliomkamatw a k i m w a b i a k u wa n a t u h u m i w a k wm a u w a j i - k w a m balimuuwa mtu mmojaki i twa Ram GuptaH u y u n i m m o ja ww a t u a l i o p a m b a nnao wakivuna magogkinyume cha sheria.

    K e s i i k a n g u r u mmahakamani. Mashahidn a v i d h i b i t i ( v yuwongo) vikaletwa. JaNissar Akhtar Kha

    Inaendelea Uk.

    SHEIKH Chambuso Rajab (katikati)

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    8/12

    8 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Makala

    Sheikh Chambuso RajabuAndha Kanoon nyingine

    Inatoka Uk. 7

    akahukumiwa kutumikiakifungo miaka 20 jela.

    Mwishowe, alitoka kwamsamaha wa Rais katikasherehe za kila mwakaza Mahtma Gadhi. Hatahivyo, hiyo ni baada yakukaa jela kwa miaka 11na miesi 6.

    S i k u m o ja a k i p i t am i t a a n i , a k a m w o n aRam Gupta, akihutubiamkutano wa hadhara wakampeni za uchaguzi.A k a g u n d u a k u w akumbe mtu aliyedaiwakumuuwa yupo hai. Lakinialishagundua pia kuwamkewe hakuwa amejiuwa,ba li yeye na bi nt i yaowaliuliwa na huyu huyuRam Gupta. Alipomwonatu akaanza kumfukuza.Ram akakimbia mwishowea k a j i k u t a a n a i n g i andani ya mahakama ileile ambapo Jan Nissar

    Akhtar Khan alihukumiwakifungo na Jaji alikuwayule yule. Khan akaingiana kumuuwa mbele yaJa ji yu le yu le ak ie le zaalivyohukumiwa kwadhulma na jinsi mkewe nabinti yake walivyouliwa naRam halafu ikasingiziwakuwa wamejiuwa.

    Je, unanikumbuka,Mheshimiwa Jaji? Mi niyule yule Jaan-E-Nissarambaye miaka kumi namoja na nusu iliyopitakatika koti kama hii hii,ulinihukumu kwendajela miaka 20 kwa kos ala kumuuwa mtu huyu,au niseme mnyama huyu(maana hastahiki kuitwabinadamu) Ram!

    U n a n i k u m b u k asasa? Unakumbuka sasaile hukumu yako yakifungo cha miaka 20jela ambapo Sheria yakokipofu haikuweza kuonakuwa sikuwa na hatia namtu aliyedaiwa kuuliwaalikuwa hai?

    N i m e m u u w a l e ombele ya macho yakob aa da ya k u t u m i k i akifungo. Sasa huwezikunihukumu tena maanahuwezi kumwadhibu

    mtu mara mbili kwa kosamoja. Na kama utatakakuniadhibu, basi nilipe.Nirejeshee miaka yangu11 na miezi 6 niliyokaaje la ni ki wa si na ha ti a.Nirudishie mke wanguZakhiya na mwananguNeelo waliouliwa naRam (ambapo Sheriayako kipofu haikumuonamuuwaji) mkasingiziakuwa mke wangu kajiuwamwenyewe.

    Mheshimiwa Ja j i ,acha sarakasi na usaniihuu wa Sheria kipofu.

    Kitie moto kiti chakocha mamlaka ambachoukikikalia unawahukumuna kuwaadhibu watuwasio na hatia. Vunja naitupilie kwa mbali kalamuyako iliyoandika hukumuya dhulma dhidi yangu.

    Kabla ya hapo, Jan NissarAkhtar Khan anaonekanaakipita mitaani akiimbaAndhaa Kanoon.

    Sheria Kipofu. Inawezakukusaliti muda wowote.Inaweza kuadhibu watuwasio na hatia. Haisaidiiwanyonge. Ni rafiki wawezi. Ni mchezo wa hojana sarakasi za maneno namisamiati ya wanasheria.Haitoi haki. Inachukiakusamehe. Kama watuwangeiogopa sheria ,uhalifu ungekoma (lakinih a w a i o g o p i ) . W a t uwanauliwa na kuteswa,

    lakini Sheria inachapausingizi. Sheria inawezakuwa na mkono mrefu,inaweza kuwa na nguvu,lakini kipofu, haioni!Inaandika bila ya kuona.Kwa sababu hiyo, wengiwanaozea jela wakiwahawana hatia. Wengiwameumia na kutesekamikononi mwa sheria(ambayo) ni rafiki wamajambazi, watoa rushwana masadi.

    K a t i k a m a k a l a i l enilieleza kuwa Masheikhw a U a m s h o w a p orumande kwa zaidi ya

    mwaka ikidaiwa kuwawametenda kosa ambaloinabidi dhamana zaozizuiwe. Tujaaliye kuwasheria kama hiyo ipo.Kwamba mtu anawezakunyimwa haki yake yadhamana kutokana na kosa

    alilofanya. Kwa hiyo DPPanaweza kuitumia bila yakulaumiwa kuwawekaMasheikh hao mwakamzima bila ya dhamanana asilaumiwe kwa sababuhoja itakuwa kuwa si yeyeni sheria. Lakini nikasema,swali la msingi ni je, hayomakosa wanayodaiwakufanya yamethibit i?Kama upo ushahidi wawazi kuwa wametendamakosa hayo, kitu ganikinaleta kigugumizi hatakesi zao zisisikilizwe?

    Kisha nikahoji, iwapoSheikh Azzan na Masheikh

    wenzake wa UAMSHOwatakuwa wamewekwandani kwa dhulma, kwamaana kuwa ni yale yaleya Andha Kanoon (BlindLaw), Sheria Kipofu, naniatalipa dhulma hii?

    K a t i k a k a d h i a y aSheikh Chambuso RajabRamadhani, tunaambiwakuwa alikamatwa wakatiaki fanya j i t ihada zakuwapatia msaada wakibinaadamu wahangawa kadhia ya Kilindi.Kutokana na maelezoya Sheikh Chambusomwenyewe, amri ya

    k u k a m a t w a k w a k eilitolewa na Mkuu waWilaya ya Tanga.

    Suala hapa si kuhojimamlaka ya Mkuu waWilaya, bali mazingirayaliyopelekea kutolewaamri. Kwa mujibu wam a e l e z o y a U s t a d hAhmad Mustafa ambayeni Katibu wa Shirikishola Taasisi za KiislamuTanga (SHITTA), kupitiakwa Sheikh Chambuso,Mkuu wa Wilaya alitoaamri kukamatwa SheikhChambuso kama namnaya kutaka kumkomoaau kulipiza kisasi kwa

    ki le a l i chodai kuwaalimsumbua sana wakatiwa sensa. Hili ndio tunalohoji. Hapa ndio penyetatizo.

    H i v i s a s a S h e i k hChambuso anakabiliwa nakesi ya kushawishi kuuwa.Lakini tunaambiwa msingiw a k u k a m a t w a ; D CHalima anadaiwa kusemaalimsumbua sana wakatiwa sensa!!!

    Kama Sheikh Chambusoalitenda kosa, alimsumbuaMkuu wa Wilaya wakatiwa zoezi la sensa, basiakamatwe kwa kosa hilona litajwe wazi. Lakinikil ichojiri , ni SheikhChambuso kukamatwa nakudhalilishwa, kuwekwabila ya chakula na maji kwamuda mrefu mpaka apigekelele, ndio polisi waliopozamu wamhurumie nak u m p a m s a a d a n amwishowe amefunguliwakesi ya kushawishi kuuwahuko Handeni.

    Kwa mujibu wa maelezoya Sheikh Chambuso, tokamwezi wa sita ambapoalisafiri kwenda Dar es

    Salaam, hajawahi kutokanje ya Wilaya ya Tanga.Na hilo hapana shakaPolisi na vyombo vya dolawanalijua kwa sababutunajua wana timu zawatendaji mahiri ambaowanajua kazi zao nawajibu wao. Zana wanazona muda wa kufuatilia nakujua mambo kama hayo.

    S a s a h a p a n d i ot u n a j i u l i z a , h i z im b w e m b w e z ak u m k a m a t a S h e i k hChambuso kumfunga

    pingu mikono nyumna kumfunga kitambac h eu s i u s o n i a s i o nanakopelekewa mpakanaingizwa rumandHandeni za nini? Andio katika kutekelezyale anayodaiwa kusemDC, kwamba ametoamri Sheikh Chambusoakamatwe kwa sababalimsumbua sana katiksensa?

    N i n a a n d i k a h a yniki jua kuwa tayarSheikh Chambuso ankesi mahakamani, nsifanyi hivi kutaka kuhokesi au kuathiri kazi zmahakama, lakini hojhapa ni kutaka kutizamhaki na kuona kuwa hakinatendeka. Na ni imanyangu kuwa mahakamitatenda haki.

    Hata hivyo nisem

    jam bo ji ng ine . Ka ti km a h o j i a n o y a k e nMohamed Said, SheikChambuso ametaja kiskilichowahi kumkutanishyeye na Mkuu wa Upelelewa Wilaya aliyemtaja kwjina la Jum anne. Katikkisa hicho kilichotokesiku za nyuma kidogoChambuso anasema kuwMkuu huyo wa Upelelewa Wilaya alimtishaAlimwambia: kwa hiumeshinda, lakini ipo sikutaingia katika anga zangNitakuficha (Waislam

    hawatakuona).K w a m b a s i kakimkamata atamfichmaana akikamatwa TangWaislamu wanajazanPolisi.

    Sasa maneno kama hayukiunganisha na maelezya Sheikh Chambuso kuwhajawahi kuka Handenmwaka huu wala Kilindlakini anakamatwa Tangm j i n i n a k u p e l ek whadi Handeni. Akifikm a h a k a m a n i k e sanayosomewa inadak u w a k a k a m a t i w

    Handeni akishawishi watkufanya mauwaji; inatiwasiwasi kuwa huendyote haya yanafanyiksi kisheria, lakini kwchuki na nia za visaswalizokwishajiwekebaadhi ya watendaj i wPolisi na Serikali.

    Kama hivi ndivyo, kwhakika hii sio katika sherikanuni na utaratibu wutendaji kazi wa Polik a t i k a n c h i a m b a yinaongozwa kwa sheria nmaadili ya utawala bora

    Amitabh Bachchan.

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    9/12

    9 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Habari/Tangazo

    Bodi ya Hajj Trust SACCOS, inawaalika

    wanachama wote katika mkutanomkuu wa Mwaka utakaofanyikaJumapili 01-12-2013 saa 3 AsubuhiUkumbi: wa Starlight Hotel Jijini Daes salaam

    Mwanachama atakae liona tangazohili amwaarifu na mwenzake.

    Wote mnakaribishwa

    MKURUGENZI wa hospitaliya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dk. Malik Abdala Juma,ambaye amejeruhiwa vibaya

    na watu wanaosadikiwakuwa ni majambazi mjiniNairobi Kenya, anawezakusafirishwa nje ya nchikwa matibabu zaidi.

    H a y o y a m e b a i n i k aba ada ya Na ib u Wazi riwa Ushirikiano wa AfrikaMashariki, Dk. Abdala JumaSadala, kunukuliwa nakituo cha redio cha ZenjiFm Zanzibar, akieleza kuwaatazungumza na serikali ilikuangalia uwezekano wa Dk.Malik kupelekwa India kwaajili ya kupatiwa matibabuzaidi.

    Dk. Sadala alisema kuwaDk. Malik aliumizwa vibaya

    C H A M A C h aW a n a n c h i C U Fkimesema kitaendeleakutekeleza dhamirayake ya kuwaunganishawananchi ili kuhakikishak u w a W a z a n z i b a r iwanakuwa kitu kimoja.

    K a t i b u M k u u w aChama hicho, Maalim SeifSharif Hamad, amesemai w a p o w a z a n z i b a r iwataondosha tofauti zaona kusimamia maslahi yanchi, maendeleo makubwayanaweza kupatikanaikiwa n i pamoja nak u w a k o m b o a v i j a n akutokana na ukosefu waajira.

    Maalim Seif ambayeni Makamu wa Kwanzawa Rais wa Zanzibar,ameeleza hayo katikamkutano wa hadharauliofanyika Fumba wilayaya Magharibi Unguja,wakati akihitimisha ziarayake ya kichama kwamajimbo tisa ya wilayahiyo.

    A l i s e m a k u t a f u t a

    suluhisho la ukosefuwa ajira kwa vijana, nikipaumbele chake nambambili katika uongoziwake wa kisiasa, baada yakuwaunganisha wananchikuishi kwa umoja namashirikiano.

    A m e f a h a m i s h akuwa zipo njia nyingiza kuwakomboa vijanak u t o k a n a n a t a t i z ohilo, ikiwa ni pamojana kuwajengea uwezoil i waweze kuajiriwakatika viwanda vidogov i d o g o n a v y a k a t ikupitia kwa wawekezaji

    wa sekta ya viwanda,pamoja na kuwaelekezakujishughulisha na uvuviwa bahari kuu.

    Eneo jengine alilolitajak u w ez a k u w a s a i d i avijana kuondokana naukosefu wa ajira, ni sektaya kilimo ambayo alisemaitawasaidia wananchiwengi kwa wakati mmojakuondokana na tatizo hilo.

    A m efa fa n u a k u w ajambo la msingi ni vijanakuwajengea uwezo katikamaeneo hayo yenye fursaza kiuchumi, ili kuweza

    Wanaokosa vitambulisho vya ukaazi

    Zanzibar ushahidi wakusanywaMaalim Seif ahitimisha ziara Magharibi UngujaNa Mwanishi Wetu kukidhi ushindani wa

    soko la ajira, sambamba nakuwawezesha kuwekezakatika kilimo cha kisasaambacho kitakuwa na tijazaidi kwa wakulima.

    Akizungumzia kuhusuuhai wa Chama hicho,Maalim Seif alisema haliya chama katika wilayahiyo inaridhisha, hasakutokana na maendeleo

    mazuri katika chaguzi

    za chama katika ngazi zamatawi.Amewataka wanachama

    kuwachagua viongoziwazuri watakaowezakusimamia maslahi yachama hicho kuelekea

    uchaguzi mkuu wa mwak

    2015.Katika hatua nyenginMaalim Seif amekemetabia ya baadhi ya viongokuendeleza chuki nuhasama miongoni mwwananchi, jambo ambalamesema halitoisadia nchkutimiza malengo yake yamani na maendeleo.

    Kwa upande wakMkurugenzi wa HabarU e n e z i n a H a k i zB i n a d a m u w a C U FSalim Bimani, amesemwanakusanya ushahidi wwatu wanaonyimwa hakya kupatiwa vitambulishvya Mzanzibari Mkaaz(ZAN ID), ili kuupelek

    kwa Rais wa Zanzibar DAli Mohamed Shein.Amesema lengo l

    kukusanya ushahidi huni kuthibitisha madayao kwa Mhe. Ra iskuwa bado baadhi ywananchi wananyimwv i t a m b u l i s h o h i v yk i n y u m e n a s h er i ai l i hatimaye wawezkupatiwa vitambulishhivyo na kuandikishwkuwa wapiga kura.

    Naye Mwakilishi wJimbo la Mji MkongwIsmail Jussa Ladhu (CUFalisema kuwa uzalendo wkweli unahitajika katikkuondoa kero za kimaishzinazowakabili vijana ntaifa kwa ujumla.

    Katika mkutano huCUF kilivuna wanachamwapya 144, sambambna kukabidhiwa kadi 1kutoka kwa wanachamwa NCCR Mageuzi nkadi 7 kutoka Chama ChMapinduzi (CCM).

    SMZ kumpeleka Dk. Malik India?Na Mwandishi Wetu sehemu ya kichwani na

    kuathirika jicho na ubongokiasi kwamba hata zungumzayake ni kwa shida.

    Hata hivyo amesemakuwa Dk. Malik tayari

    ameshafanyiwa opereshenikubwa na vipimo vilimeneshakuwa hali si mbaya.

    Imeelezwa kuwa Dk.Malik, ambaye alikuwa jijiniNairobi nchini Kenya kikazi,alipotezana na wenzakewaliokuwa wakishiriki katikamkutano wa masuala yaafya, uliohusisha Wakuu wahospitali na Wataalamu waAfya tangu Ijumaa ya wikiiliyopita.

    B a a d a e a l i k u t w aamejeruhiwa vibaya na kitukinachosadikiwa ni chenyemakali na kulazwa katikahospitali ya Jomo Kanyaajijini Nairobi.

    MKURUGENZI wa hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Dk. Malik Abdala Juma.

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    10/12

    10 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Mashairi/Matangazo

    Sina la kusema sina, naitengua kauliSito washutumu tena,ninasema bilikuliSito fanya kama jana, kuwatungia methaliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina sababu ya mana, kuugubika ukweliKweli mpo juu sana, wacheni niwakubaliMme bawabu kwakina, kuanzisha jambo hili

    Sina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina kibaya kuona, nimeziona daliliNjema tena zimenona, zisibebeke kwa meliUkasomee Uchina, daraja la uzamiliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina tena la kunena, MUM siyo wabahiliWanafundisha Kichina,wameanza kudahiliUsiseme sifa huna,zipo ngazi mbali mbaliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina mfundo moyoni, wacheni leo nikiliMUM chumvi mchuzini, ninapinga si bizaliKwenye kundi la madini, haziye iwe MetaliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina matongo machoni, nimefutwa ujahiliUnafanana na nini, nisiipate mithaliKama mti wa porini, wewe mkaajabali

    Sina lakusema sina,naitengua kauliSina hila mtimani, msinione dalaliWanafunzi wa vyuoni, nanyi pia wa skuliMwakaribishwa chuoni, kichina mkiamiliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Sina wino kalamuni, kaditama naghailiNakuomba Rahmani,kiondoshee thakiliMUM siyo Madrasani, chenyewe chuo kamiliSina lakusema sina,naitengua kauli

    Isihaka Hemed Mzuzuri(Sauti ya Mkutubi)MUM-MOROGORO

    SINA

    Kalamu nimeishika, kutoa yangu indhari,Lengo ipate kuka, Bara nako Zanzibari,

    Kwa kila anohusika, na haya ajihadhari,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Mambo haya kwa hakika, chimbuko la nyingi shari,Sahali kubanangika, umma kwa kuyakhitari,Aula kuyaepuka, mambo haya ni hatari,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Umimi ebu kumbuka, ya ibilisi fakhari,Baidi livyomuweka, na rehema za Qahari,Kwa sijida kukiuka, kisa umbole la nari,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Ruwazaye kuishika, twahisi ni ufakhari,Kumbe ni kujahilika, na za dunia ghururi,Nadra kuyumkinika, sote kuwa Maamiri,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Hata nyumbayo mulika, mu wangapi Maamiri,Ummoja kwa hakika, ulo Mkuu wa dari,

    Kulikoni kukiuka, wa taifa Uamiri,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Fulusi mbele kuweka, jingo kutaliathiri,Malengo tuloyaweka, sahali kuyahajiri,Kwa mwake ndani kusaka, ghawazi na utajiri,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Uluwa pia kutaka, kwa sasa tumekithiri,Kwa hili twahangaika, huku na kule kujiri,Kwa mioyo kutoridhika, jengo kutalidamiri,Umimi, mali na vyeo, ni sumu ya harakati.

    Haya tusipoepuka, wenyewe twajisihiri,Tujaribu kuridhika, bado tawili safari,Kwa hili kulikiuka, hatutaka dahari,Umimi, mali na vyeo, hilaki ya harakati.

    ABUU NYAMKOMOGI - MWANZA

    SUMU YA HARAKATI !

    Inawaalika Waislamu wote katika mkutano wa Vijana wa Kiislamuwa Afrika Mashariki, utakao fanyika Jijini Mwanza.

    Tarehe 12-16/Desemba/2013.

    Taasisi za Kidini, Vyuo pamoja na Misikiti pia wanaalikwa kushiriki katikaMkutano huo, Jijini Mwanza.

    Katika Mkutano huo wajumbe watajigharamikia nauli isipo kuwachakula, malazi na machapisho ni bure.

    Kwa mawasiliano na maelezo zaidi Piga Simu Namba:- Mwanza 0782170 607/0752 721 486,

    0654 355 420 /0654 064 215/ 0713 495 992/ 0718 476 527.

    KARIBU MWANZA

    Kamati ya Maandalizi

    Jumuiya ya Vijana wa Kiislamu Jijini Mwanza

    Jumuia ya wataalam wa Kiislamu wa Tanzania (TAMPRO)inatoa taarifa ya kuwepo mkutano mkuu wa kumi nan ne wawanachama wake.

    Mkutano utafanyika siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 25-26 Desemba 2013 kuanzia saa 3:00 asubuhi kwenye ukumbi waHoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam .

    Jumatano kutakuwa na mhadhara mfupi, salama za viongoziwa matawi na wageni waalikwa.

    Alhamis mkutano mkuu utajikita katika agenda zifuatazo:UfunguziKuthibitisha akida (Quorum) na uanachamaKupokea agenda

    Kuthibitisha kumbukumbu za kikao kilichopitaYatokanayo na kumbukumbu za kikao kilichopitaTaarifa ya utendaji ya mwaka 2013Taarifa ya fedha 2013Mpango wa wazi na bajeti ya mwaka 2014Taarifa ya mchakato wa mabadiliko ya katiba ya TAMPROKuthibitisha wajumbe wapya wa Tume ya uchunguziKuthibitisha wanachama wapyaMengineyoKufungaWanachama wote mnakaribishwa

    Pazi M. SemiliKATIBU MKUU

    TAARIFA YA MKUTANO WA MWAKA 2013

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    11/12

    11AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 201Tangazo

    Waislamu kote Nchini mnatangaziwa nafasi za darasa la kwanza katika shule ya kiislamu kirinjiko. Shule hii ni ya bwenkwa wavulana na wasichana

    1. Shule hii ni ya kiislamu yenye lengo la kuwapa watoto elimu bora na kuwalea kwa malezi ya kiislamu.Mwisho wa kuchukua fomu ni tarehe 10/12/2013. Fomu hii italipiwa Tsh.10,000/=

    2. Masomo yanayofundishwa ni haya yafuatayo:-Elimu ya dini ya kiislamu, Usomaji wa Quran na mafunzo yake, Lugha ya kiarabu, English, Kiswahili, MathematicsScience, History, Geography, Civics, Computer (ICT), Michezo (PDS).

    3. Muombaji awe amemaliza elimu ya awali

    Fomu za maombi zinapatikana katika vituo vilivyoorodheshwa hapa chini.

    Arusha - Osi ya Islamic Education Panel Jambo Plastic Ghorofa ya 2 mkabala na msikiti Mkuu Bondeni - 0763 282 371/ 0784 406 610

    Kilimanjaro - Moshi: Msikiti wa Riadha 0654 723 418 - Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0655 697 075

    Tanga - Twalut Islamc Centre Mabovu Darajani 0715 894111/0789 410914 - Uongofu Bookshop: - 0784 982525/

    - Korogwe: SHEMEA SHOP 0754 690007 - Mandia Shop - Lushoto: 0782257533 Mwanza - Nyasaka Islamic Secondary School 0717 417685/0786 417685- Osi ya Islamic Education Panel Mtaa wa Ruji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770 Musoma - Osi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05, -0784721015/0765024623 Kagera - Bukoba: Alhuda Caf Kwa mzee Kinobe karibu na osi za TRA. - 0688 479 667

    Shinyanga - Masele com: Osi za NSSF Shinyanga Mjini mkabala na bank ya CRDB - 0752180426 - Kahama osi ya AN NUUR Karibu na msikiti wa Ibadhi: 0753 993930

    Dar es Salaam - Ubungo Islamic High School 0754 260 241/0712033556 - Osi ya Islamic Ed. Panel Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin 0655144474

    Morogoro - Wasiliana na Ramadhani Chale :0715704380

    Dodoma - Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0712 325086

    Singida - Osi ya Islamic Ed. Panel karibu na Nuru snack Hotel 0714285465/0784 928039

    Manyara - Babati: Shule ya Msingi Hangoni: 0784 667575 - Osi ya Islamic Ed. Panel Masjid Rahma: 0764 469870/0789 174902 Kigoma - Msikiti wa Mwanga Kigoma: 0753 355224 - Kibondo Islamic Nursery School: 0784 442860

    - Kasulu: Murubona Isl.SS. 0714710802 Lindi - Wapemba Store: 0784 974041/0786 959663 Mtwara - Amana Islamic S.S 0715 465158/0787 231007 Songea - Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU 0715 681701/0716791113

    - Mkuzo Islamic High School. 0716 791113 Mbeya - Duka la vifaa vya Kiislamu nje ya Msikiti wa Uyole 0713 200209

    - Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209 Rukwa - Sumbawanga: Masjid TAQWA 0717082 073 Tabora - Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566 Iringa - Madrastun Najah: 0714 522 122 Pemba - Wete: Wete Islamic Education Center: 0777 432331 Unguja - Madrasatul Fallah: 0777125074- Maa - Osi ya ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu 0653705627

    USIKOSE NAFASI HII ADHIMU WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

    KIRINJIKO ISLAMIC ENGLISH MEDIUM PRIMARY SCHOOLP. O. Box 62 SAME Tel: 0784 833982/ 0784 435336

    E-mail [email protected]

    NAFASI ZA DARASA LA KWANZA 2014

  • 8/13/2019 ANNUUR 1101

    12/12

    12 AN-NUU

    MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 20112MAKALA

    AN-NUUR12 MUHARRAM 1435, IJUMAA NOV. 29 - DES. 5, 2013

    Mimi Muhusin Machemba (0659 954 010), ni Mzazi wMwanafunzi Ruqayah Muhsin, anayesoma Kidato cha Tatu (FormThree) katika Shule ya Sekondari ya Chamazi Islamic Seminary.

    Naomba msaada kwa yoyote au Taasisi yoyote kumalizia adya kijana wangu kiasi cha Tsh.400,000/= tu, nimekwama kutokanna mitihani ya kimaisha.

    Yoyote atakayejaaliwa kunusuru mustakabali wa kielimu wmwanafunzi huyo, aelekeze msaada wake moja kwa moja katikAkaunti ya Shule, kwa jina la CHAMAZI ISLAMIC SEMINARY, A/No. 054137000033-NBC.

    Au awasiliane na Uongozi wa Shule (Mkuu wa Shule) kwa No0713 989 309 au 0783 419 659.

    Maombi ya msaada wa kulipiwa ada ya Shule

    AFRIKA ya Kusini naZanzibar zimeanzishasafari za ndege zamoja kwa moja kutokaJohannesburg AfrikaKusini hadi Zanzibar.

    Akizungumza katikauzinduzi wa usari huouliofanyika katika hoteliya LAGEMA Nungwi,Makamu wa Kwanzawa Rais wa ZanzibarMhe. Maalim Seif SharifHamad, alilipongezashir ika la ndege laMANGO la Afrika Kusinikwa kuamua kuanzishasafari hizo.

    Maalim Seif alisemasafari hizo zitasaidiakuongeza idadi ya wataliikutoka Afrika ya Kusini,hasa ikizingatiwa kuwawatalii wa nchi hiyotayari wameruhusiwakuingia Zanzibar bila

    Chama cha wananchiCUF, kimewatakaw a f u a s i w a k ekujiandaa na ushindik at ik a U ch ag u ziMkuu wa mwaka2015, kutokana na kileilichokiita kuwa niwombi la mabadilikoya uongozi katikanchi za Afrika.

    Akihutubia mkutanowa hadhara wa chamah i c h o u l i o f a n y i k akatika jimbo la Dimanimwishoni mwa wikiiliyopita, Katibu Mkuuw a c h a m a h i c h o ,ambaye pia ni Makamowa Kwanza Rais waSMZ, Malim Seif SharifHamad, alisema serikaliya Umoja wa Kitaifa

    i taendelea kuwepolakini kigezo cha chamani kupata Urais.

    Aidha alisema kuwachama hicho kitaendeleakupata ushindi katikamajimbo 18 ya visiwaniPemba na yale manneya Unguja, na kudaikwamba ushindi huoutaifanya CUF kuwa naviti 34 vya Ujumbe waBaraza la Wawakilishisawa na asilimia 70 ya

    Mawaziri.Katika mkutano huo,

    Maalim Seif ameongeza

    kuwa hata kama baadhi

    ya vyama vitafanya

    ghilba katika upigaji

    wa kura, lakini katika

    uchaguzi ujao wapigakura wao watakipigiakura chama cha CUF.

    Maalim Seif amedaikuwa ushindi wa chamahicho 2015 utatokana na

    Maalim Seif atamba CUF kushinda Uchaguzi Mkuu 2015Na Mwandishi Wetu mabadiliko ya uongozi

    katika nchi za Afrikayalioanzia Kaskazini

    Usafri wa ndege Johannesburg-Zanzibar wazinduliwaNa Mwandishi Maalum viza.

    Amefahamisha kuwaZanzibar inategemeasana sekta ya utalii katikakukuza uchumi wake nakwamba, kwa sasa sektahiyo ndio inayoongozapato la fedha za kigenikwa asilimia 72.

    Alisema serikali kwaupande wake itafanyakila juhudi kushirikianana shirika hilo pamoja nawawekezaji wengine, ilikuhakikisha kuwa sektaya utalii na uwekezajiz inapata maendeleomakubwa.

    Aidha Maalim Seifamewataka waongozajiwatalii pamoja na vyombovya habari kuwa mabaloziwazuri wa kuitangazaZanzibar kwa wageni,ili kuvutia watalii nawawekezaji wengi zaidi.

    A l i s e m a l e n g o l aserikali ni kufanya kazi

    kwa karibu zaidi na Afrikaya Kusini katika sektazote za maendeleo, ilikunyanyua hali za maishakwa wananchi wa pandehizo mbili.

    Kwa upande wake,Balozi wa Afrika yaKusini nchini TanzaniaBw. Thamduycse Chilliza,alisema wananchi waAfrika ya Kusini marazote wamekuwa wakisiaukarimu wanaoupatakutoka kwa ndugu zao waTanzania na kwamba, halihiyo imekuwa ikiwavutiawawekezaji wengi kutokanchi hiyo.

    Alisema uzinduzi wasafari za moja kwa moja zandege utarahisisha safariza watalii na wawekezajiwengine, sambamba nakukuza uhusiano wamuda mrefu uliopo katiya nchi hiyo na Zanzibar.

    A l i o n g e z a k u w aTanzania imeendelea

    mwa bara hilo.Katika mkutano huo

    chama hicho kimepata

    wanachama wapya144 waliokabidhiwakadi za CUF ambapo

    kadi saba za Chamcha Mapinduzi (CCMzilirejeshwa.

    k u w a n c h i m u h i mbarani Afr ika kutokanna uwepo wa amani nusalama, tofauti na ilivykwa nchi nyingi za Afrikhal i inayoipa nafaskubwa zaidi ya kuvutiwawekezaji kutoka nchmbalimbali duniani.

    Naye Waziri wa HabarUtamaduni, Utalii n

    Michezo Bw. Said AMbarouk, amepongezjuhudi zinazochukuliwna Afrika ya Kusini katikkuimarisha vitega uchumvyake Zanzibar.

    Alisema hatua hiyinadhihirisha ukwekuwa Zanzibar ni mahapazuri na salama kwuwekezaji na wagenna kul i takia sh ir ikhilo la ndege mafanikim a k u b w a k a t i kkutekeleza majukumyake ya kutoa huduma zusari wa ndege nchini.

    MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) akiwa katika moja ya ziara zak

    za kikazi visiwani humo.