ibada za leo

Post on 24-Jan-2016

369 Views

Category:

Documents

0 Downloads

Preview:

Click to see full reader

TRANSCRIPT

SOMOMAISHA NA IBADA ZA

LEO.

Fungu Kuu: Warumi 7:24

“Ole Wangu, Maskini Mimi! Ni Nani

Atakayeniokoa Na Mwili Huu Wa Mauti?”

{1T 457} Niliona taratibu za Mungu zimekwishwa geuzwa, na maagizo yake maalumu kupuuzwa, na wale wanaoiga mitindo ya marekani. Nilirejesha katika kitabu cha Torati 22:5: “mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume wala mwanamume asivae mavazi yampasayo mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.” Mungu asingelikuwa na watu wake wanaoitwa warekebisha mavazi. Ni kukosa haya ….. Kabisa kusikowafaa watu wasiojivuna, wanyenyekevu wafuasi wa Kristo.

{1T 462} Kwa mawazo yao yaliyo haribika juu ya jambo hili wamejadiri swala la ufupishaji wa nguo hadi mtazamo wao wa kiroho umechanganyikiwa kiasi kwamba wanawaona wanaume kama miti inayotembea.

{4T 629}Shetani amevumbua mitindo ya mavazi kwa dhumuni la kuzamisha fikra za wanawake katika swala la mavazi ili waweze kulifikiria hata angalau kidogo.

{4T 628}Kadri tunavyoona wakina dada wanajitenga kwenye mavazi rahisi, na kuendeleza upendo kwenye mitindo ya ulimwengu, tunapata shida. Kwa kuchukua hatua katika mwenendo huo wanajitenga wenyewe kwa Mungu, na kukataa kujipamba kwenye mioyo yao. Hawapaswi kuhisi uhuru kwa kutumia muda waliopewa na Mungu kwenye urembo usio maana wa mavazi yao. Ni kiasi gani kizuri muda huu ungeweza kutumika katika kutafakari maandiko, hatimaye kupata maarifa kamilifu ya unabii na masomo juu ya maisha ya Yesu .

{1T 521} Ningependa kwa dhati uswa wa urefu wa nguo, na ningesema kwamnba inchi tisa kwa kulingana na mawazo yangu kuhusu jambo hili kama ninavyoweza kulielezea jambo hili katika inchi

1 TIMOTHEO 4:12 Mtu awaye yote

asiudharauujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika

usemi mwenendo, upendo imani na usafi.

{4T 630} Wengi huangalia haya makatazo kama mitindo iliyopitwa na wakati kuangaliwa kwa uthamani, lakini yeye aliyewapatia wanafunzi wake unaelewa hatari inayopatikana kwa kupenda mavazi katika wakati wetu na ametuma kwetu ujumbe wa onyo. Je tutatilia maanani maonyo haya na kuwa na hekima? Maonyesho ya mavazi yanaendelea kuongezeka. Mwisho bado haujafika. Mitindo hudumu kubadilika, na dada zetu hufuata mkondo wake, bila kujali muda wala gharama. Kuna kiasi kikubwa kinachotumiwa katika mavazi, wakati kingelipaswa kurudishwa kwa Mungu mtoaji.

{4T 641} Maneno yetu, matendo, yetu mavazi yetu ni ni wahubiri hai wa kila siku, hutukusanya kwa Kristo au kututenga mbali naye. Hili siyo jambo la kipuuzi la kukwepwa kwa masihara. Somo la mazavi linahitaji tafakari makini na maombi mengi.

{4T 641} Ni aibu kwa dada zetu kusahau tabia zao takatifu na wajibu wao kwa Mungu na kuiga mitindo ya dunia. Siyo kwamba hatufahamu bali ni ukaidi wa mioyo yetu. Hatuwezi kuendeleza mivuto yetu kwa mwenendo huo. Ni kukinzana na taaluma ya imani yetu inayopelekea sisi kudhalauliwa katika macho ya ulimwengu.

{5 T 498} Mara nyingi nimeumia ninapoingia katika nyumba ya Mungu anayoabudiwa, kuona mavazi machafu ya wanaume na wanawake. Kama moyo na tabia vingekuwafunuliwa , katu kusingekuwa na chochote juu yao kuhusu mbingu. Hawana wazo la kweli kuhusu utaratibu, jambo lakuvutia na mwenendo uliotakaswa ambao Mungu anahitaji kila anayekuja mbele zake kumuabudu awenao. Mambo haya hutoa msisitizo gani kwa wasioamini na kwa vijana, ambao hufahamu haraka na kufanya maamuzi?

KICHO NDANI YA KANISAHABAKUKI 2:20

Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.

{5T 495} Ni kweli kwamba heshima katika nyumba ya Mungu karibia imetoweka kabisa. Mambo matakatifu na mahali patakatifu hapatambuliwi , matakatifu na yaliyotukuka hayatambuliwi… lakini shetani amekuwa kazini kuharibu imani yetu katika ibada ya wakristo watakatifu.

{5T 491} Moyo mnyenyekevu na wenye kuamini, nyumba ya Mungu duniani ni mlango wa kuingia mbinguni. Wimbo wa sifa, maombi, maneno yanenwayo na wawakilishi wa Krtisto, ni mawakala waliochaguliwa na Mungu, kuwaandaa watu kwa ajili ya kanisa la mbinguni, kwa ibada ya juu ambayo ndani yake hakiwezi kuingia kilicho najisi/kichafu.

{5T 491} Wakristo wanaweza kujifunza jinsi gani wanapaswa kupajali mahali ambapo Mungu hukutana na watu wake. Kumekuwa na mabadiliko makubwa, siyo kwa uzuri bali kwa ubaya, kwa matendo na desturi za watu ukirejea kwenye ibada ya kidini. Vitu vya thamani, vitakatifu, vinavyotuanganisha sisi na Mungu kwa haraka vinakosa nafasi yake moyoni na akilini mwetu, na kushushwa chini katika nafasi sawa na vitu vya kawaida.

{5T 492}Wakati watu wa Mungu wanapoingia kwenye ibada, wanapaswa kufanya hivyo kwa kicho, wakitembea kimya kuelekea kwenye viti vyao. … mazungumzo ya kawaida, minong’ono na vicheko havipaswi kuwepo katika nyumba ya ibada, wenda kabla au hata baada ya ibada.

{5T 493} Na wote watoke nje bila kusukumana au kuongea kwa sauti kubwa, wajisikie kwamba wako mbele za Mungu, kwamba macho yake yako juu yao, na kwamba imewapasa kutenda kama vile wako mbele zake wakimtazama. Pasiwepo na mtu anayesimama kutoa umbeya mahali watu wanapopita. Maeneo ya kanisa yanapaswa kupambwa na heshima takatifu. Haipaswi kufanywa mahali pa kukutana na kutembelea marafiki wa zamani, na kutambulisha mawazo ya kawaida na mapatano ya biashara za kidunia. Haya yanapaswa kuachwa nje ya kanisa. Mungu na Malaika wamekuwa wakidharauliwa na wasiojali, kelele za vicheko na kuburuzwa kwa miguu vikisikika mahali fulani.

. {5T 498} Kwa sababu ya kukosa heshima katika tabia, mavazi na mwenendo na kukosekana kwa ibada yenye akili, Mungu mara nyingi amegeuza uso wake asiwatazame wale waliokusanyika kumwabudu.

{5T 499} Mawazo ya watu wengi mara nyingi yamekuwa yakifuatilia nyaraka zinazohusu mavazi, na hivyo mawazo mengi ambayo yasingepaswa kuingia mioyoni mwa watu wa Mungu sasa yanaingia. Mungu anapaswa kuwa kiini cha mawazo ya watu na ibada. Na chchote kile kinachovuta fikra kutoka katika utaratibu, huduma takatifu ni hatia kwake. Maswala yote ya mavazi yanapaswa kuongozwa kwa umakini sana, na kufuata kwa ukaribu taratibu za Biblia. Mitindo imekuwa miungu inayoongoza ulimwengu wa nje, na mara nyingi hujipenyeza ndani ya kanisa. Asiwepo mtu yeyeto atakayedharau hekalu la Mungu kwa muonekano wake. Kwa maana Mungu na Malaika wake wako pale.

WITOWarumi 12:1-21.Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. 2. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza na ukamilifu

Mungu na

Akubariki

sana

top related