al-barjas

79
al-Mu´taqad as-Swahiyh Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas 1 www.firqatunnajia.com ح امعتقد الصحǽعتقادسلم ا كل م اجب عل الal-Mu´taqad as-Swahiyh [I´tiqaad sahihi wajibu kwa kila Muislamu kuiamini ] Mwandishi: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Upload: iddi-shaabani-mwaluko

Post on 11-Jul-2016

94 views

Category:

Documents


7 download

DESCRIPTION

salafy

TRANSCRIPT

Page 1: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

1

www.firqatunnajia.com

امعتقد الصحيح الواجب على كل مسلم اعتقاد

al-Mu´taqad as-Swahiyh

[I´tiqaad sahihi wajibu kwa kila Muislamu kuiamini]

Mwandishi:

Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym

Tarjama:

Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Page 2: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

2

www.firqatunnajia.com

00. Dibaji ya kitabu al-Mu´taqad as-Swahiyh .................................................................................. 3

01. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ................................................................... 8

02. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat ...................................................... 13

03. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah .................................................................... 16

04. ´Aqiydah sahihi juu ya nguzo za imani sita ............................................................................. 24

05. ´Aqiydah sahihi juu ya imani ..................................................................................................... 51

06. Msimamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya Takfiyr ........................................................................... 55

7. ´Aqiydah sahihi juu ya muislamu mtenda dhambi ................................................................... 57

08. ´Aqiydah sahihi juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) .................................................................................................................................................. 61

09. ´Aqiydah sahihi juu ya watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) .................................................................................................................................................. 66

10. ´Aqiydah sahihi juu ya karama za mawalii .............................................................................. 69

11. ´Aqiydah sahihi juu ya watawala wa waislamu ...................................................................... 71

12. Msimamo sahihi juu ya mijadala katika dini ........................................................................... 74

13. Matahadharisho ya kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´ .......................................................................... 77

14. Hitimisho ya kitabu ..................................................................................................................... 79

Page 3: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

3

www.firqatunnajia.com

00. Dibaji ya kitabu al-Mu´taqad as-Swahiyh

Himdi zote anastahiki Allaah. Swalah na salaam ziwe juu ya Mtume wa

Allaah, kizazi chake na Maswahabah zake.

Amma ba´d:

Hakika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ndio dini ya haki ambayo

ni wajibu kwa kila muislamu aiitakidi, kwani ndio ´Aqiydah ya Mtume wa

Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake watukufu

(Radhiya Allaahu ´anhum). Atakayechagua ´Aqiydah nyingine, basi

ameipelekea nafsi yake katika adhabu, khasira na ghadhabu za Allaah kali.

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu

mapote ambayo yatazuka katika Ummah wake na akataja mapote sabini na

tatu:

"Yote yatakuwa Motoni isipokuwa moja tu ambalo ni al-Jamaa´ah."1

Hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesifu mkusanyiko huu

ambao umesalimika kutokamana na matishio ya Moto pale aliposema:

"Ni wale wataokuwemo katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na

Maswahabah."2

Hiki ndio kidhibiti cha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hakika wao ni wenye

kushikamana na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa

1 Ahmad na Abu Daawuud kutoka kwa Mu´aawiyah na ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim, adh-Dhahabiy, ash-

Shaatwibiy na wengineo. Ahmad, Ibn Maajah na Ibn Abiy ´Aaswim kutoka kwa Anas.

2 Ameipokea al-Aajurriy katika "ash-Shariy´ah" kutoka ´Abdullaah bin ´Amr na at-Twabaraaniy katika "as-

Swaghiyrah" na katika "al-Awsatw" kutoka kwa Anas bin Maalik.

Page 4: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

4

www.firqatunnajia.com

sallam) na Sunnah za makhaliyfah wake waongofu. Ni wenye kuziuma kwa

magego. Kwa ajili hio ndio maana wakawa ni pote lililookoka (Firqat-un-

Naajiyah). Ni wenye kuokoka na Moto siku ya Qiyaamah. Ni wenye

kusalimika na Bid´ah hapa duniani. Vilevile wao ni kundi lililonusuriwa

(Firqat-ul-Mansuurah). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Hakutoacha kuwepo kipote katika Ummah wangu kuwepo katika haki

wazi wazi mpaka itapowajia amri ya Allaah ilihali wako wazi wazi."

"Hakutoacha kuwepo kipote kwenye Ummah wangu katika ushindi mpaka

itapowajia amri ya Allaah ilihali ni washindi."3

Maana ya kuwa wazi hapa ni nusura (Ta´ala):

فأيدنا الذين آموا على عدوهم فأصبحوا ظاهرين

"Tukawatia nguvu wale walioamini dhidi ya maadui zao, wakapambaukiwa wakiwa washindi." (61:149)

م الغالبون دنا وإن ج

"Na hakika jeshi Letu ndilo litakaloshinda." (37:173)

Wao ni wenye kushinda kwa panga na mikuki au kwa hoja na dalili. Inahusu

kundi moja na sio mengi. Kwa ajili hiyo ndio maana wameitwa ´mkusanyiko`.

Amesema (Ta´ala):

ل ق إ الض فماذا ب عد ا

"Na kuna nini baada ya haki ila upotofu." (10:32)

Hawatambuliki kwa jina lingine zaidi ya Uislamu na Sunnah na majina

mengine yenye dalili. Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

3 Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa al-Mughiyrah bin Shu´bah.

Page 5: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

5

www.firqatunnajia.com

"Ahl-us-Sunnah hawana jina lingine wanalotambulika kwalo, si Jahmiyyah,

Qadariyyah wala Raafidhwah."

Aliulizwa vilevile kuhusu as-Sunnah ambapo akajibu kwa kusema:

"Hawana jina lingine zaidi ya as-Sunnah."

Bi maana Ahl-us-Sunnah hawana jina wanalojinasibisha nalo zaidi yalo.

Kumetiliwa umuhimu mkubwa juu ya kuipa nguvu ´Aqiydah ya wema

waliotangulia (Salaf-us-Swaalih) na kubainishwa dalili zake. Imewekwa wazi

na maimamu wengi wakubwa katika vitabu vingi, vya kibinafsi na vya kwa

pamoja. Miongoni mwa vitabu hivyo kuna vinavyoitwa "as-Sunnah", bi

maana "´Aqiydah". Ni zaidi ya vitabu mia mbili na khamsini. Baadhi yavyo ni:

1 – ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy ´Aaswim

2 – ”as-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Imaam Ahmad

3 – ”as-Sunnah” ya al-Khallaal

4 – ”as-Sunnah” ya Ahmad bin al-Furaat Abiy Mas´uud ar-Raaziy

5 – ”as-Sunnah” ya Ismaa´iyl bin Usayd al-Madiyniy

6 – ”as-Sunnah” ya Ibn-ul-Qaasim – mwanafunzi wa Maalik

7 – ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Salaam al-Baykandiy

8 – ”as-Swifaat wa ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” ya Nu´aym bin Hammaad

9 – ”as-Sunnah” ya al-Athram

10 – ”as-Sunnah” ya Harb bin Ismaa´iyl al-Karmaaniy

11 – ”as-Sunnah” ya Ibn Abiy Haatim

12 – ”as-Sunnah” ya Ibn Jariyr at-Twabariy

13 – ”at-Tabasswur fiy ´Alam-id-Diyn” vilevile ni ya Ibn Jariyr

Page 6: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

6

www.firqatunnajia.com

14 – ”as-Sunnah” ya at-Twabaraaniy

15 – ”as-Sunnah” ya Abush-Shaykh al-Aswbahaaniy

16 – ”as-Sunnah” ya Abul-Qaasim al-Laalakaa’iy

17 – ”as-Sunnah” ya Muhammad bin Naswr al-Marwaziy

18 – ”´Aqiydat-us-Salaf wa Asw-haab-il-Hadiyth” ya as-Swaabuuniy

19 – ”al-Ibaanah” ya Ibn Battwah

20 – ”at–Tawhiyd” ya Ibn Khuzaymah

21 – ”at-Tawhiyd” ya Ibn Manda

22 – ”al-Iymaan” ya Ibn Abiy Shaybah

23 – ”al-Iymaan” ya Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Salaam

24 – ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Muzaniy – mwanafunzi wa ash-Shaafi´iy

25 – ”Sharh-us-Sunnah” ya al-Baghawiy

26 – ”Sharh Madhaahib Ahl-is-Sunnah” ya Ibn Shaahiyn

27 – ”al-Hujjah fiy Bayaan-il-Mahajjah wa Sharh ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah” ya

Abul-Qaasim al-Aswbahaaniy

28 – ”Usuul-us-Sunnah” ya Abu Abdullaah Ibn Abiy Zamaniyn

29 – ”ash-Shariy´ah” ya al-Aajurriy

30 – ”I´tiqaad Ahl-is-Sunnah” ya Abu Bakr al-Ismaa´iyliy

31 – ”as-Sunnah” ya al-Barbahaariy

32 – ”al-Iymaan” ya Ibn Manda

33 – ”al-Iymaan” ya al-´Adaniy

34 – ”al-´Arsh” ya Ibn Abiy Shaybah

Page 7: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

7

www.firqatunnajia.com

35 – ”al-Qadar” ya Ibn Wahb

36 – ”al-Qadar” ya Abu Daawuud

37 – ”ar-Ru’yah” ya ad-Daaraqutwniy

38 – ”as-Swifaat” ya ad-Daaraqutwniy

39 – ”an-Nuzuul” ya ad-Daaraqutwniy

40 – ”Jawaab Ahl Dimashq fiys-Swifaat” ya al-Khatwiyb al-Baghdaadiy… na vitabu vinginevyo vingi.

Vivyo hivyo inahusiana na vitabu vilivyoandikwa baada ya waandishi hawa.

Miongoni mwao ni Ibn ´Abdil-Barr, Ibn Qudaamah al-Maqdisiy, Ibn

Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, adh-Dhahabiy, Ibn Kathiyr, Muhammad bin

´Abdil-Wahhaab na wengineo. Humo mmebainishwa ´Aqiydah sahihi.

Vinasimamisha hoja na kufichua utata wa Ahl-ul-Ahwaa´.

Tutataja sehemu katika ´Aqiydah ya watu hawa vigogo.

Sipati kuwezeshwa haya isipokuwa na Allaah. Kwake Yeye ninategemea na

kwake Yeye naelekea.

Page 8: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

8

www.firqatunnajia.com

01. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini kuwa Allaah (Ta´ala) amepwekeka

juu ya kuumba, uola na uendeshaji wa mambo. Allaah (Ta´ala) amesema:

است وى على العرش ي غشي الل إن رض ستة أيام وم ربكم الل ه الذي خلق السماوات وا والقمر والج ياا والشم لبه ار ي يل المر مسخرات بأمر لق وا ت بارك الل ه ربج العالمي أ له ا

"Hakika Mola wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita kisha akalingana juu ya ´Arshi. Anafunika usiku kwa mchana, unaufuatia upesi upesi na [ameumba] jua na mwezi na nyota vyote vimetiishwa kwa amri Yake. Tanabahi! Ni Vyake Pekee uumbaji na amri. Amebarikika Allaah, Mola wa walimwengu." (07:54)

رض لق ما يشاء لل ه ملك السماوات وا

"Ni wa Allaah Pekee ufalme wa mbingu na ardhi. Anaumba Atakavyo." (42:49)

رض له ملك يت السماوات وا وهو على كل شيء قدير يي و

"Ni Wake Pekee ufalme wa mbingu na ardhi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu ni Muweza." (57:02)

Tawhiyd hii inaitwa Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na imekita katika nafsi ya kila

mwanaadamu. Hakuna mwanaadamu yeyote anayepingana nayo, sawa awe

muislamu au kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu makafiri:

رض لي قولن الل ه م من خلق السماوات وا ولئن سألت

"Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah." (31:25)

وما ي ؤمن أك رهم بالل ه إ وهم مجشركون

Page 9: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

9

www.firqatunnajia.com

"Na wengi kati yao hawamwamini Allaah isipokuwa wao ni wenye kufanya shirki." (12:106)

Mujaahid amesema:

"Wanaamini kuwa Allaah ndio Muumbaji na Mruzukaji wao anayewafisha.

Hii ndio imani yao pamoja na kuwa wanamshirikisha na wengine."

Washirikina walikuwa hawaitakidi kuwa waungu wao wana sehemu katika

uumbaji wa Allaah. Walikuwa wakiamini kuwa Allaah ndiye mwenye

kuendesha hayo peke yake. Pamoja na hivyo walikuwa wakidai kuwa

wanawatumia waungu wao kwa kujikurubisha kwa Allaah na wawashufaie

Kwake. Amesema (Ta´ala):

الص الل ه زلفى أ لل ه الدين ا ذوا من دونه أولياء ما ن عبدهم إ لي قربونا إ والذين ا

"Tanabahi! Ni ya Allaah Pekee dini iliyotakasika. Na wale waliojichukulia badala Yake walinzi [husema]: “Hatuwaabudu isipokuwa ili watukurubishe kwa Allaah ukaribio."" (39:03)

م ش رض أم م على قل أرأي تم شركاءكم الذين تدعون من دون الل ه أرو ماذا خلقوا من ا اهم كتاباا ف ب ي ت رك السماوات أم آت ي م ب عضاا إ غروراا مه بل إن يعد الظالمون ب عض

"Sema: “Je, mnawaona washirika wenu ambao mnawaomba badala ya Allaah? Nionyesheni ni nini walichoumba katika ardhi au wana ushirika wowote mbinguni au Tumewapa kitabu chochote kile, kisha wao kwa hicho wakawa na hoja bayana?” Hapana! Bali hawaahidiani madhalimu wao kwa wao isipokuwa uongo." (35:40)

تا ون وي قولون أئا لتاركو آ م إل ه إ الل ه يستك م كانوا إذا قيل ون ل إن شاعر

"Hakika wao walipokuwa wakiambiwa: "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" wanatakabari na wanasema: “Je, sisi kweli tuache miungu yetu kwa ajili ya mshairi mwendawazimu?"" (37:35-36)

ا دا ا وا ا ة إل اب إن ه ذ أجعل ا ا لشيء ع

Page 10: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

10

www.firqatunnajia.com

"Amewafanya miungu wote kuwa ni mungu mmoja? Hakika hili ni jambo la ajabu mno!" (38:05)

Allaah (Ta´ala) aliasisi Tawhiyd hii ili ihakikishwe, ithibitike na kumwelekeza mtu katika uwajibu wa Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah, kwa sababu Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah ni yenye kulazimisha mtu asimuabudu yeyote isipokuwa Allaah (Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:

ا الاس اعبدوا ربكم الذي خلقكم والذين من ق بلكم لعلكم ت ت قون يا أي ج

"Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu Ambae Amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kuwa na taqwa." (02:21)

لكم الل ه ربجكم له الملك تصرفون إل ه إ هو ذ فأ

"Huyo Ndiye Mola wenu Pekee Ana ufalme, hakuna mungu wa haki mwingine asiokuwa Yeye, basi vipi mnageuzwa?" (39:06)

م من خوف م من جوع وآم ف لي عبدوا رب ه ذا الب يت الذي أطعم

"Basi wamuabudu Mola wa nyumba hii. Ambaye Anawalisha kutokana na njaa na Akawapa amani kutokana na khofu." (106:03-04)

Allaah (Ta´ala) amesema kwamba Yeye peke yake ndiye Mwenye kuwaumba

na Mwenye kuwaruzuku, jambo ambalo hawana shaka nalo. Amefanya hilo

kuwa ni hoja dhidi yao ili iwe ni wajibu kumuabudu yeye peke yake, hali ya

kuwa hana mshirika. Allaah (Ta´ala):

مد لل ه وس الذين اصفى قل ا رض وأنزل لكم من السماء ماءا فأنبت م على عباد ر أما يشركون أمن خلق السماوات وا ا به آلل ه خي رها بتوا ش ة ما كان لكم أن ت دائق ذات ب اراا وجعل ع الل ه أإل ه م ا أن رض ق راراا وجعل خ بل هم ق وم ي عدلون أمن جعل ا

اجزاا ا رواسي وجعل ب ي البحرين يب الم أإل ه مع الل ه ويكشف السجوء وعلكم خلفاء بل أك رهم ي علمون أمن ر إذا دعا ضرض ديكم ظلمات الب ر والبحر ومن ي رسل الرياح بشراا ب ي يد أإل ه مع الل ه ا ا ما تذكرون أمن ي ته قلي ه مع أإل ي ر

الل ه الل ه عما يشركون ت عا

"Sema: "Sifa zote kamilifu na tukufu anastahiki Allaah na amani kwa waja Wake ambao Amewachagua. Je, Allaah ni bora au wale wanaowashirikisha? Au nani Aliyeumba mbingu na ardhi na Akakuteremshieni kutoka

Page 11: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

11

www.firqatunnajia.com

mbinguni maji, kisha Tukaotesha kwayo mabustani anisi za kupendeza kabisa, nyinyi hamna uwezo wa kuotesha miti yake. Je, yuko mungu mwengine pamoja na Allaah? Bali wao ni watu wanaosawazisha. Au nani Aliyeijaalia ardhi kuwa mahali pa matulio na Akajaalia baina yake mito na Akaiwekea milima na Akajaalia baina ya bahari mbili kizuizi. Je, yuko mungu mwengine pamoja na Allaah? Bali wengi wao hawajui. Au nani Anayemuitika aliyedhikika anapomwomba, na Akamuondoshea dhiki, na Akakufanyeni makhalifa wa ardhi? Je, yuko mungu mwengine pamoja na Allaah? Ni machache mno mnayokumbuka. Au nani Anayekuongozeni katika viza vya nchi kavu na bahari na nani anayetuma pepo za bishara kabla ya Rahmah Yake. Je, yuko mungu mwengine pamoja na Allaah? Ametukuka Allaah kutokana na yale wanayomshirikisha."" (27:59:63)

Katika Aayah zote hizi Allaah (Ta´ala) anawakemea washirikina wanaokiri kuwa Allaah (Ta´ala) peke yake ndiye muumbaji wa mbingu na ardhi na mwenye kunufaisha na kudhuru. Pamoja na hivyo kukiri kwao huku hakukuwanufaisha kitu, kwa sababu walimshirikisha Allaah pamoja na waungu wengine ambao walikuwa wakiwaabudu kama wanavyomuabudu Allaah. Hakika nadharia hii inaenda kinyume na Shari´ah na akili. Ambaye amepwekeka katika mambo yote haya - kama kuumba, kuruzuku, kuhuisha na kufisha - ndiye mwenye haki ya kutekelezewa utiifu aina yote. Ndio maana Allaah (Ta´ala) amewakemea pale aliposema:

أإل ه مع الل ه

"Je, yuko mungu mwengine pamoja na Allaah?"

Hata hivyo hakusema:

"Je, kuna muumbaji mwengine pamoja na Allaah," kwa sababu walikuwa ni

wenye kuthibitisha hili.

Allaah (Ta´ala) amebainisha ni ubatilifu uliyoje kuwa na mshirika katika uola.

Lau angelikuwepo mwengine aliye na sehemu katika hilo, basi mbingu na

ardhi vingeharibika. Hili ni lenye kufahamika pia kwa akili ya kimaumbile.

Allaah (Ta´ala):

ذ الل ه من ولد وما كان معه من إل ه م على ب عض إذاا لذهب ك ما ا ب عض ا خلق ولع سبحان الل ه عما يصفون لج إل ه

Page 12: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

12

www.firqatunnajia.com

"Allaah Hakujifanyia mwana yeyote na wala hakukuwa pamoja Naye mungu yeyote - hapo bila shaka kila mungu angelichukua vile alivyoviumba na bila shaka baadhi yao wangeliwashinda wengineo. Utakasifu ni wa Allaah kutokana na yale wanayoyaelezea." (23:91)

ة إ الل ه لفسدتا ما آ لو كان في

"Lau wangelikuweko humo miungu mingi asiyekuwa Allaah, bila shaka zingelifisidika." (21:22)

Page 13: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

13

www.firqatunnajia.com

02. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat

Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamoja na

kwamba wanathibitisha majina mazuri na sifa tukufu ambazo Allaah (Ta´ala)

amejithibitishia katika nafsi yake na ambazo Mtume Wake (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) amemthibitishia. Hawavuki Qur-aan na zile Hadiyth

zilizothibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Wanathibitisha hayo kimatamshi na wanatambua maana yake katika lugha ya

kiarabu ambayo Qur-aan imeteremshwa kwayo. Hata hivyo namna yake

wanamwachia Allaah (Ta´ala), kwa kuwa ni maalum kwa Allaah (Ta´ala) na

hakuna mwengine yeyote mwenye ujuzi kwazo.

Katika mlango huu wa khatari wanapita kutokamana na misingi ya Kishari´ah

iliyothibiti; yule mwenye kushikamana nayo basi amesalimika na upindaji.

Wa kwanza: Kuthibitisha yale ambayo Allaah (Ta´ala) amejithibitishia nayo

katika nafsi yake na yale ambayo Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amemthibitishia. Haya yanatakiwa kufanyika pasi na kuongeza wala

kupunguza, kwa kuwa hakuna yeyote ambaye ni mjuzi wa kumtambua

Allaah (Ta´ala) kuliko Allaah Mwenyewe:

قل أأنتم أعلم أم الل ه

“Je nyinyi mnajua zaidi au Allaah?" (02:140)

Hakuna mwanaadamu yeyote ambaye ni mjuzi wa kumtambua Allaah kuliko

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah (Ta´ala)

amesema:

ى ي يو وى إن هو إ و ق عن ا وما ي

"Na wala hatamki kwa matamanio yake. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake." (53:03-04)

Page 14: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

14

www.firqatunnajia.com

Wa pili: Mtu amtakase Allaah (Ta´ala) na kushabihiana na sifa za viumbe. Allaah (Ta´ala):

كمله شيء وهو السميع البصي لي

"Hakuna chochote kinachofanana Naye - Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona." (42:11)

د يكن له كفواا أ و

“Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye." (112:04)

Wa tatu: Mtu asijaribu kufikiria sifa Zake. Allaah (Ta´ala):

ا يون به علما و

"Na wala wao hawawezi kuzunguka elimu Yake." (20:110)

يا هل ت علم له

"Je, unamjua mwengine mwenye Jina kama Lake?" (19:65)

Miongoni mwa sifa hizi ni pamoja na maneno Yake (Ta´ala):

ن على العرش است وى الر

"Mwingi wa Rahmah amelingana juu ya ´Arshi." (20:05)

Haya yametajwa sehemu nyingi katika Qur-aan. Hapa mtu anatakiwa

kuelewa ya kwamba kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi ni kulingana

kihakika. Tunaelewa maana yake na hatujui namna yake. Maana yake ni kuwa

juu na kungatika. Haya ndio yenye kufahamishwa na lugha ya kiarabu. Ahl-

us-Sunnah wal-Jamaa´ah wamekubaliana juu ya maana hii. Kuhusiana na

namna ya kulingana huku, hakuna yeyote anayeijua isipokuwa Allaah peke

yake - hali ya kuwa hana mshirika.

Hali kadhalika Allaah (Ta´ala) anasema:

Page 15: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

15

www.firqatunnajia.com

كموا با كمتم ب ي الاس أن ا وإذا أهل مانات إ يعاا إن الل ه نعما يعظكم به لعدل إن الل ه يأمركم أن ت ؤدجوا ا إن الل ه كان بصياا

"Hakika Allaah Anakuamrisheni kurudisha amana kwa wenyewe na mtakapohukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika uzuri ulioje wa mawaidha Anayokuwaidhini nayo Allaah! Hakika Allaah daima ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona." (04:58)

Hapa kunathibitishwa usikizi wa Allaah. Kwa mujibu wa lugha ya kiarabu

usikizi maana yake ni "kufikia sauti".

Tunamthibitishia Allaah (Ta´ala) usikizi ambao anafikia kwao sauti. Usikizi

huu haufanani na usikizi wa viumbe vya Allaah. Kuhusu namna yake,

tunamwachia Allaah (Ta´ala). Hivyo hatusemi: "Anasikia vipi?" Hatujiingizi

katika hilo, kwa kuwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hakutufanya tujue hilo.

Bali ni katika mambo ambayo Allaah (Jalla wa ´Alaa) peke yake ndiye

mwenye ujuzi kwayo.

Vivyo hivyo inahusu uoni; kufikia vyenye kuonwa. Imethibiti katika "as-

Swahiyh" ya Muslim kutoka kwa Abu Muusa al-Ash´ariy ya kwamba Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Hakika Allaah halali na wala haimstahikii Yeye kulala. Huteremsha

uadilifu na huupandisha. Kwake kunanyanyuliwa matendo ya usiku kabla

ya matendo ya mchana na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku.

Pazia Yake ni nuru; lau ataiondosha basi nuru ya uso na enzi Yake

ingeliunguza kila kiumbe Chake ambapo unafikia uoni Wake."

Tunamthibitishia Allaah uoni wa kihakika ambao kwao anafikia vyenye

kuonwa. Pamoja na kwamba hatuna ujuzi wowote kuhusu namna ya uoni

huu.

Hii ni baadhi ya mifano ya namna ambavyo Ahl-us-Sunnah wanaamini majina

na sifa za Allaah.

Page 16: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

16

www.firqatunnajia.com

03. ´Aqiydah sahihi juu ya Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah

Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamoja na mtu

kumpwekesha Allaah (Ta´ala) katika ´ibaadah. Hawaabudu mwengine

pamoja na Allaah. Badala yake wanamtekelezea aina zote za ´ibaadah za

wajibu na za mapendekezo Allaah, hali ya kuwa hana mshirika.

Hawamsujudii yeyote isipokuwa Allaah. Hawamfanyii Twawaaf yeyote

isipokuwa Allaah. Hawachinji kwa ajili ya yeyote isipokuwa Allaah.

Hawamuwekei nadhiri isipokuwa Allaah. Hawaapi kwa yeyote isipokuwa

kwa Allaah. Hawategemei isipokuwa kwa Allaah. Hawamuombi yeyote

isipokuwa Allaah. Hii ndio Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah:

واعبدوا الل ه و تشركوا به شيئاا

"Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote." (04:36)

وقضى ربجك أ ت عبدوا إ إيا

"Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu yeyote isipokuwa Yeye."" (17:23)

او دا ا وا ا ما أمروا إ لي عبدوا إل

"Hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu mungu wa haki Mmoja." (09:31)

لصي له الدين وما أمروا إ لي عبدوا الل ه

"Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Yeye dini." (98:05)

إ لي عبدون ن ن وا وما خلقت ا

"Na Sikuumba majini na wanadamu isipokuwa waniabudu." (51:56)

Waniabudu maana yake ni "wanipwekeshe mimi tu".

Page 17: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

17

www.firqatunnajia.com

Kinyume chake ni shirki - Allaah atukinge nayo. Shirki ndio dhambi kubwa

ambayo Allaah ameasiwa kwayo. Amesema (Ta´ala):

لك لمن يشاء ومن يشرك بالل ه ف قد اف ت رى إاا عظيماا إن الل ه ي غفر أن يشرك به وي غفر ما دون ذ

"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amebuni dhambi kuu." (04:48)

لك لمن يشاء ا ومن يشرك بالل ه ف قد ضل إن الل ه ي غفر أن يشرك به وي غفر ما دون ذ ا بعيدا ض

"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali." (04:116)

ر مشركي به فاء لل ه غي وي به الريح مكان سحيق ومن يش ر أو ت ا خر من السماء ف تخفه الي رك بالل ه فكأ

"Muelemee haki kwa Allaah bila ya kumshirikisha. Na yeyote anayemshirikisha Allaah basi kama kwamba ameporomoka kutoka mbinguni, wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno." (22:31)

تشرك بالل ه به وهو يعظه يا ب إن الشرك لظلم عظيم وإذ قال لقمان

"Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: “Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kuu!"" (31:13)

Amebainisha (Ta´ala) ya kwamba shirki inabatilisha matendo yote na inamtoa

mtu katika Uislamu. Amesema (Ta´ala):

م ما كانوا ي عملون بط ع ولو أشركوا

"Na kama wangemshirikisha bila shaka yangebatilika yale waliyokuwa wakitenda." (06:88)

اس ن عملك ولتكونن من ا الذين من ق بلك لئن أشركت ليحب ي إليك وإ رين ولقد أو

Page 18: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

18

www.firqatunnajia.com

"Kwa yakini umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako: “Ukifanya shirki bila shaka zitabatilika ‘amali zako na bila shaka utakuwa miongoni mwa waliokhasirika."" (39:65)

Katika "as-Swahiyh" ya Muslim kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya

Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) amesema:

"Mwenye kukutana na Allaah pasi na kumshirikisha Yeye na chochote,

ataingia Peponi, na mwenye kukutana Naye ilihali anamshirikisha Yeye na

chochote, ataingia Motoni."

Katika "as-Swahiyh" ya al-Bukhaariy kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya

Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) amesema:

"Mwenye kufa ilihali ni mwenye kuomba mwenza asiyekuwa Allaah,

ataingia Motoni."

Yule mwenye kufanya aina yoyote ile ya ´ibaadah akamfanyia asiyekuwa

Allaah, basi huyo ni mshirikina kafiri.

Kwa mfano du´aa ni moja miongoni mwa ´ibaadah ambazo Allaah

ameamrisha. Hivyo basi, yule mwenye kumuomba Allaah peke yake, huyo ni

mpwekeshaji. Upande mwingine, yule mwenye kumuomba asiyekuwa

Allaah, ameshirikisha. Amesema (Ta´ala):

فعك و يضرجك فإن ف علت فإنك إذاا من الظالمي و تدع من دون الل ه ما ي

“Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa na wala asiyekudhuru. Endapo utafanya hivo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu." (10:106)

د ربه سابه ع ا ا آخر ب رهان له به فإ ا إنه ي فلح الكافرون ومن يدع مع الل ه إل

"Na yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake - hakika hawafaulu makafiri." (23:117)

Page 19: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

19

www.firqatunnajia.com

ا وأنه لما قام عبد الل ه يدعو كادوا ي دا تدعوا مع الل ه أ ا أدعو ر و أشرك به وأن المساجد لل ه ف ا قل إ دا كونون عليه لبدا أ

"Na kwamba mahala pote pa kuswalia ni kwa ajili ya Allaah Pekee, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah. Na kwamba mja wa Allaah aliposimama kumwomba, walikaribia kumzonga. Sema: “Hakika mimi namuomba Mola wangu Pekee na wala simshirikishi na yeyote."" (72:18-20)

ق لغ فا له دعوة ا الماء ليب م بشيء إ كباسط كفيه إ يبون وما دعاء الكافرين وما هو ببالغه والذين يدعون من دونه يستل إ ض

"Kwake ndiko kuna maombi yote ya haki. Na wale wenye kuomba badala Yake hawawaitikii kwa chochote isipokuwa kama anayenyosha viganja vyake viwili vya mikono kwenye maji ili yafikie kinywani mwake, wala hayafikii - na du’aa za makafiri hazipo ila katika upotofu." (13:14)

ياء و ر أ لقون أموات غي لقون شيئاا وهم عون الذين يدعون من دون الل ه وما يشعرون أيان ي ب

"Na wale wanaowaomba badala ya Allaah hawaumbi kitu chochote, bali wao wanaumbwa. Ni maiti si wahai na hawatambui lini watafufuliwa." (16:20-21)

ا آخر ف تكون من المعذبي ا تدع مع الل ه إل ف

"Basi usiombe pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa." (26:213)

ار ويولج ال جل مجسمىيولج الليل ال ري والقمر كل ار الليل وسخر الشم لكم الل ه ربجكم له الملك والذين تدعون ذمي لكون من ق ع من دونه ما ابوا لكم إن تدعوهم يسمعوا دعاءكم ولو و ي بئك وي وم القيامة يكفرون بشرككم وا ما است

مل خبي

"Anauingiza usiku katika mchana na Anauingiza mchana katika usiku na Anaitisha jua na mwezi - kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Huyo Ndiye Allaah Mola wenu, ufalme ni Wake Pekee. Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba, hawasikii maombi yenu na hata wakisikia, hawatakuitikieni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu na wala hakuna atakayekujulisha kama Mjuzi." (35:13-14)

Page 20: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

20

www.firqatunnajia.com

رض لي قولن الل ه م من خلق السماوات وا الل ه بضر هل هن كاشفات ضر أو ولئن سألت قل أف رأي تم ما تدعون من دون الل ه إن أراد سكات ر ة هل هن الل ه ته أراد بر س عليه ي ت وكل المت وكلون قل

"Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Allaah." Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah ikiwa Allaah Atanikusudia dhara, je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinikusudia Rahmah, je, wao wataweza kuizuia Rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake wategemee wenye kutegemea."" (39:38)

رض أم م شرك السماوات قل أرأي تم ما تدعون من دون الل ه أرو ماذا خلقوا من ا ائ تو بكتاب من ق بل ه ذا أو أثارة من علم إن ي وم القيامة وه يب له إ تم صادقي ومن أضلج ن يدعو من دون الل ه من يست م غافل ك م م عن دعائ شر الاس كانوا ون وإذا

م كافرين أعداءا وكانوا بعباد

"Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi au wana ushirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kabla ya hiki au alama yeyote iliobakia ya elimu mkiwa wakweli". Na nani aliyepotoka zaidi kuliko ambaye anayeomba asiyekuwa Allaah ambaye hamuitikii mpaka Siku ya Qiyaamah nao kuhusu du’aa zao ni wenye kughafilika. Na [siku ya Qiyaamah] watakapokusanywa watu [miungu ya uongo] watakuwa maadui wao na watakuwa kwa ‘ibaadah zao ni wenye kuzikanusha." (46:04-06)

Imethibiti katika "as-Sunan" kutoka kwa an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

"Du´aa ndio ´ibaadah."

Tawhiyd hii - Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah - ndio ambayo kulitokea magomvi kati

ya Mitume na watu wao. Tawhiyd hii ndio sababu ya Allaah kuwatuma

Mitume kwa ajili ya kuibainisha na kulingania kwayo. Hali kadhalika

Akateremsha Vitabu kwa ajili ya kuihakikisha, kuiweka wazi na kutumia hoja

kwayo. Amesema (Ta´ala):

ولقد ب ع ا كل أمة رسوا أن اعبدوا الل ه واجتبوا الاغوت

Page 21: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

21

www.firqatunnajia.com

"Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na miungu ya uongo." (16:36)

ي إليه أنه إل ه إ أنا فاعبدون وما أرسلا م ن ق بلك من رسول إ نو

"Na Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mungu wa haki ila Mimi, basi Niabuduni."" (21:25)

زل الم أن أنذروا أنه إل ه إ أنا فات قون ي ئكة بالرجوح من أمر على من يشاء من عباد

"Anateremsha Malaika na Roho kwa amri Yake juu ya Amtakaye miongoni mwa waja Wake, kwamba: “Onyeni: Hakika hapana mungu wa haki ila Mimi basi Nicheni."" (16:02)

Hii ndio ambayo Mitume kwanza walikuwa wakianza kuwaamrisha watu

wao pindi walipokuwa wakiwalingania katika dini ya Allaah. Kila Mtume

alikuwa akiwaamrisha watu wake:

ر يا ق وم اعبدوا الل ه ما لكم من إل ه غ ي

“Enyi watu wangu! Mwabuduni Allaah, hakika hamna mungu mwingine wa haki asiokuwa Yeye." (07:59,65,73,85)

Nuuh alisema hivyo na hali kadhalika Huud, Swaalih, Shu´ayb na Mitume wengine wote - swalah na salaam ziwashukie wote.

Allaah (Ta´ala) amesema:

ا ت عبدون من دون الل ه أوثاناا ولقون إفكاا وإب راهيم إذ قال لقومه اعبدوا الل ه وات قو تم ت علمون إ ر لكم إن ك لكم خي إن الذين ذلكون د الل ه الرزق واعبدو واشكروا له ت عبدون من دون الل ه إليه ت رجعون لكم رزقاا فاب ت غوا ع

"Ibraahiym alipowaambia watu wake: “Mwabuduni Allaah na mcheni. Hivyo ni kheri kwenu mkiwa mnajua. Hakika mnaabudu badala ya Allaah masanamu na mnazua uzushi. Hakika wale mnaowaabudu badala ya Allaah hawakumilikiini riziki, basi tafuteni riziki kwa Allaah na mwabuduni Yeye na mshukuruni, Kwake mtarejeshwa." (29:16-17)

Page 22: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

22

www.firqatunnajia.com

Vilevile amesema (Ta´ala) kuhusu Mtume Wake Yuusuf (´alayhis-Salaam):

ا اءا يا صا ار ما ت عبدون من دونه إ أ د الق ر أم الل ه الوا ن أأرباب مجت فرقون خي ا من لس يتموها أنتم وآباؤكم ما أنزل الل ه كم إ لل ه سلان لك الدين القيم ول كن أك ر الاس ي علمون بدوا إ إيا أمر أ ت ع إن ا ذ

“Enyi masahibu wangu wawili wa jela! Je, waungu wengi wanaofarakana ni bora au Allaah ambaye ni Mmoja Pekee, Mwenye nguvu? Hamuabudu badala Yake isipokuwa majina [ya masanamu] mmeyaita nyinyi na baba zenu - hakuyateremshia Allaah kwayo ushahidi wowote. Hakuna hukumu isipokuwa ya Allaah. Ameamrisha kwamba msimwabudu yeyote isipokuwa Yeye Pekee - hiyo ndio dini iliyonyooka, lakini watu wengi hawajui." (12:39-40)

Washirikina hawana mashiko yoyote kwa ushirikina wao. Hawawezi kupata

mashiko yoyote kutoka katika akili sahihi wala andiko kutoka kwa Mitume.

Amesema (Ta´ala):

ةا ي عبدون ن آ واسأل من أرسلا من ق بلك من رجسلا أجعلا من دون الر

“Na waulize wale Tuliowatuma kabla yako miongoni mwa Mitume Wetu, je, Tulifanya badala ya Mwingi wa Rahmah miungu mingine iabudiwe?" (43:45)

Maana yake ni kwamba hakuna Mtume yeyote ambaye alimwita mtu

kuabudu chochote pamoja na Allaah. Bali wote, kuanzia wa kwanza wao hadi

wa mwisho wao, walikuwa ni wenye kuita katika kumuabudu Allaah Mmoja

wa Pekee, hali ya kuwa hana mshirina. Amesema (Ta´ala):

م شرك السماوات ق رض أم ائ تو بكتاب من ق بل ه ذا أو أثارة من علم إن ل أرأي تم ما تدعون من دون الل ه أرو ماذا خلقوا من اتم صادقي ك

"Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah! Nionyesheni nini wameumba katika ardhi au wana ushirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kabla ya hiki au alama yeyote iliobakia ya elimu mkiwa wakweli." (46:04)

Page 23: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

23

www.firqatunnajia.com

Kutokana na yaliyotangulia, inapata kufahamika kuwa Tawhiyd hii ndio wajibu wa kwanza, jambo la kwanza la wajibu na ndio dini pekee ambayo Allaah anaikubali.

Page 24: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

24

www.firqatunnajia.com

04. ´Aqiydah sahihi juu ya nguzo za imani sita

Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kumuamini

Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, kufufuliwa baada ya

kufa na kuamini Qadar.

Imani ya kumuamini Allaah ni kuthibitisha Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah,

Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na Tawhiyd al-Asmaa´ was-Swifaat, jambo ambalo

tumeshatangulia kulitaja.

Imani ya kuamini Malaika ni kuthibitisha na kuamini uwepo wao, majina yao

yaliyotajwa na matendo yao yaliyotajwa. Amesema (Ta´ala):

ا أنزل إليه من ربه والمؤمون د من رجسله آمن الرسول ئكته وكتبه ورسله ن فرق ب ي أ كل آمن بالل ه وم

"Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini. Wote wamemwamini Allaah, na Malaika Wake, na Vitabu Vyake, na Mitume Wake. [Nao husema:] Hatutafautishi baina ya yeyote kati ya Mitume Wake."" (02:285)

من آمن بال أن ت ولجوا وجوهكم قبل المشرق والمغرب ول كن ال ال ئكة والكتاب والبيي لي خر والم ل ه والي وم ا

"Wema haina maana ya kuwa mnaelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, lakini wema khasa ni mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii." (02:177)

Katika "as-Swahiyh" ya Muslim ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu

´anh) amepokea katika Hadiyth yake ndefu kuhusu swali la Jibriyl

alipomuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya imani. Akajibu

ifuatavyo:

"Imani ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya

Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake."

Allaah (Ta´ala) amewasifu katika Kitabu Chake ifuatavyo:

رض ار ي فت رون وله من السماوات وا ون عن عبادته و يستحسرون يسبحون الليل وال يستك د ومن ع

Page 25: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

25

www.firqatunnajia.com

"Na ni Vyake Pekee vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi na wale walio Kwake hawatakabari na ‘ibaadah Yake na wala hawachoki. Wanasabihi usiku na mchana wala hawazembei." (21:19-20)

ا ن ولدا ذ الر بل عباد مجكرمون يسبقونه بالقول وهم بأمر ي عملون سبحانه وقالوا ا

"Na wakasema: “Mwingi wa Rahmah Amejichukulia mwana. Utakasifu ni Wake! Bali [hao Malaika] ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii kwa kauli nao kwa amri Yake wanafanya." (21:26-27)

ون عن عبادته ويسبحونه وله يس د ربك يستك دون إن الذين ع

"Hakika wale walioko kwa Mola wako hawatakabari kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabihi na Kwake Pekee wanasujudu." (07:206)

Wao ni waja na viumbe miongoni mwa viumbe vya Allaah (Ta´ala) wakubwa. Malaika hawastahiki chochote katika ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):

ء إياكم كانوا ي عبدون قالوا سبحانك ئكة أه ؤ ي قول للم يعاا شرهم ن أنت ولي جا من دوم وي وم أك رهم بل كانوا ي عبدون ا م مجؤمون

"Na Siku Atakayowakusanya wote kisha Atawaambia Malaika: “Je, hawa ndio waliokuwa wakikuabuduni?” Watasema: "Utakasifu ni Wako! Wewe ni mlinzi wetu sio hao. Bali walikuwa wakiabudu majini, wengi wao wakiwaamini."" (34:40-41)

ئكة و أيأمركم بالكفر ب عد إذ أنتم مجسلمون البيي أربابااو يأمركم أن ت تخذوا الم

"Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miungu. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa waislamu?" (03:80)

Katika "as-Swahiyh" ya Muslim ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amepokea

ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Malaika wameumbwa kutokamana na nuru, majini wameumbwa

kutokamana na moto na Aadam ameumbwa kutokamana na kile

kilichosifiwa kwenu."

Page 26: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

26

www.firqatunnajia.com

Miongoni mwa sifa zao ni kwamba wana mbawa. Katika wao kuna ambao

wana mbawa mbili, wengine wana mbawa tatu, wengine wana mbawa nne na

kadhalika. Amesema (Ta´ala):

ث ور وث ا أو أجحة م ئكة رس رض جاعل الم مد لل ه فاطر السماوات وا لق ما يشاء باع ا إن الل ه على كل يزيد ا شيء قدير

"Himidi zote Anastahiki Allaah muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbilimbili, tatutatu na nnenne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo. Hakika Allaah juu ya kila kitu ni Muweza." (35:01)

Katika "as-Swahiyh" ya al-Bukhaariy kumepokelewa kutoka kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba:

"Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Jibriyl akiwa na

mbawa mia sita."

Allaah (Ta´ala) amewapa uwezo wa kuweza kujigeuza katika maumbile

mazuri. Kama ambavyo Jibriyl (´alayhis-Salaam) alivyojigeuza kwa Maryam

katika umbile la mtu wa sawa. Vivyo hivyo kama walivyojidhihirisha kama

wageni wawili watukufu pindi walipomtembelea Ibraahiym (´alayhis-

Swalaatu was-Salaam) na hali kadhalika wakafanya pindi walipomjia Luutw

(´alayhis-Salaam) ili kuwaadhibu watu wake na mfano wa hivo.

Allaah amewakemea washirikina ambao wamedai kuwa Malaika ni mabanati

wa Allaah - Allaah ametakasika na yale ambayo madhalimu wanasema.

Amesema (Ta´ala):

ا ن ولدا ذ الر م وما خ سبحانه وقالوا ا م و يشفعون بل عباد مجكرمون يسبقونه بالقول وهم بأمر ي عملون ي علم ما ب ي أيدي لف مشفقون إ لمن ارتضى وهم من خشيته

"Na wakasema: “Mwingi wa Rahmah Amejifanyia mwana. Utakasifu ni Wake! Bali [hao Malaika] ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii kwa kauli nao kwa amri Yake wanafanya. Anajua yale yaliyoko mbele yao, na yale yaliyoko nyuma yao na wala hawamuombei uombezi yeyote yule

Page 27: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

27

www.firqatunnajia.com

isipokuwa kwa yule ambaye Amemridhia. Nao kutokana na kumkhofu, ni wenye kutahadhari." (21:26-28)

Baada ya hapo amesema (Ta´ala) kuhusu Malaika:

ئكة إ م الب ون أم خلقا الم م ألربك الب ات و م لكاذبون أصفى فاست فت م لي قولون ولد الل ه وإن م من إفك ناثاا وهم شاهدون أ إن تذكرون أم لكم سلان مجبي فأتوا بكت كمون أف تم صادقي ابكم إ الب ات على البي ما لكم كيف ن ك

"Waulize: “Je, Mola wako ndio ana mabanati na wao ndio wana watoto wa kiume au Tumewaumba Malaika kuwa wanawake nao wameshuhudia? Tanabahi! Hakika wao kwa uzushi wanasema: “Allaah Amezaa." Na hakika wao bila shaka ni waongo kweli kweli. Je, Amechagua mabanati kuliko wana wa kiume? Mna nini! Vipi mnahukumu? Je, hamkumbuki? Je, mna hoja bayana? Basi leteni kitabu chenu mkiwa ni wakweli." (37:149-157)

حن المسبحون وما ما إ له مقام معلوم وإنا لحن الصافجون وإنا ل

"Na hakuna miongoni mwetu isipokuwa ana mahali maalumu. Na hakika sisi bila shaka tutajipanga safu. Na hakika sisi bila shaka ni wenye kumsabihi." (37:164-166)

Miongoni mwao ni Jibriyl (´alayhis-Salaam). Kazi yake ni kupeleka Wahy. Amesema (Ta´ala):

يل فإنه ن زله على ق لبك بإذن الل ه قل من كان عدوا

"Sema: “Yeyote aliyekuwa adui wa Jibriyl, basi hakika yeye ameiteremsha Qur-aan katika moyo wako kwa idhini ya Allaah."" (02:97)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona juu na mbawa zake mia

sita na umbile lake kubwa limefunika upeo wa juu. Kisha baada ya hapo

akamuona mbinguni usiku wa safari ya mbinguni. Amesema (Ta´ala):

دها ى ع ت د سدرة الم ن زلةا أخرى ع جة المأوى ولقد رآ

"Na kwa yakini amemuona katika uteremko mwingine. Kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa. Karibu yake ndio ipo bustani inayokaliwa." (53:13-15)

Page 28: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

28

www.firqatunnajia.com

Hakumuona katika umbile lake isipokuwa mara hizi mbili tu. Kuhusiana na mara nyinginezo, alijionyesha katika muonekano wa mtu na mara nyingine katika muonekano wa Dihyah al-Kalbiy. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Jibriyl:

ون بكم أمي وما صا د ذي العرش مكي ماع فق المبي إنه لقول رسول كرم ذي ق وة ع با ولقد رآ

"Hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu, Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye ´Arshi, Anayetiiwa, tena muaminifu. Na wala huyu mwenzenu hana wazimu. Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho uliosafi." (81:19-23)

Malaika mwingine ni Mikaaiyl. Kazi yake ni mazao na namna

itakavyogawiwa. Yote hayo yanatokamana na maamrisho ya Allaah (´Azza

wa Jall). Imaam Ahmad amepokea kutoka kwa Anas ya kwamba Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Jibriyl:

"Ni kwa nini sijapatapo kumuona Mikaaiyl akicheka?" Akasema: "Mikaaiyl

hajapatapo kucheka tangu uumbwe Moto."

Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Mikaaiyl:

يل وميكال فإن الل ه عدو للكافرين ئكته ورسله وج من كان عدوا لل ه وم

"Yeyote aliyekuwa adui wa Allaah na Malaika Wake, na Mitume Wake, na Jibriyl, na Miykaal, basi hakika Allaah ni adui kwa makafiri." (02:98)

Miongoni mwao kuna mwingine ambaye ni Israafiyl. Kazi yake ni kupuliza

baragumu ambalo atalipuliza mara tatu baada ya kuamrishwa na Mola Wake

(´Azza wa Jall); mara ya kwanza itakuwa ya mfazaiko, ya pili ya kufa na ya

tatu kwa ajili ya kusimama kwa ajili ya Mola wa walimwengu. Malaika

watatu hawa ndio wale waliotajwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) katika du´aa yake ya swalah ya usiku:

"Ee Allaah, Mola wa Jibraaiyl, Mikaaiyl na Israafiyl. Muumba wa mbingu

na ardhi. Mjuzi wa yenye kujificha na yenye kuonekana. Hakika Wewe

utahukumu baina ya waja Wako katika yale yote waliyotofautiana.

Page 29: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

29

www.firqatunnajia.com

Niongoze katika yale yaliyotofautiana kwayo kwa idhini Yako. Hakika

Wewe unamuongoza Umtakaye katika njia iliyonyooka."

Imepokelewa na Muslim.

Katika "Sunan" ya an-Nasaa´iy imepokelewa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya

Allaahu ´anhaa) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema:

"Ee Allaah, Mola wa Jibraaiyl, Mikaaiyl na Israafiyl. Ninajilinda Kwako

kutokamana na vuke la Moto na adhabu ya kaburi."

Kadhalika kuna Malaika wa mauti. Kazi yake ni kutoa roho. Amesema

(Ta´ala):

ربكم ت رجعون إ قل ي ت وفاكم ملك الموت الذي وكل بكم

"Sema: “Atakufisheni Malaika wa mauti ambaye amewakilishwa kwenu kisha kwa Mola wenu mtarejeshwa."" (32:11)

Vilevile kuna Malaika ambao kazi yao wamewekwa ili kumhifadhi mwanaadamu katika hali zake zote; asipokuwa safarini, anapokuwa safarini, anapokuwa amelala na anapokuwa macho. Amesema (Ta´la):

كم من أسر القول ار له معقبات من ب ي يديه ومن خل سواء م ر به ومن هو مستخف بالليل وسارب بال فظونه من أمر ومن ج فه م الل ه ي غي روا ما بأنفس مرد له وإذ إن الل ه ي غي ر ما بقوم م من دونه من وال ا أراد الل ه بقوم سوءاا ف وما

"Ni sawasawa kwenu anayefanya siri kauli yake au anayeisema kwa juu na anayenyemelea usiku na anayetembea huru mchana. Ana [Malaika] wanaofuatana mfululizo mbele yake na nyuma yake wanamhifadhi kwa amri ya Allaah. Hakika Allaah Habadilishi yale yaliyoko kwa watu mpaka wao wenyewe wabadilishe yale yaliyomo katika nafsi zao. Na Allaah Akiwatakia watu uovu basi hakuna wa kuurudisha. Na wala hawana mlinzi yeyote badala Yake " (13:10-11)

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amefasiri Kauli Yake (Ta´ala) "Ana

wanaofuatana mfululizo" ifuatavyo:

Page 30: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

30

www.firqatunnajia.com

"Ni Malaika wenye kumlinda mbele yake na nyuma yake. Pindi wakati

wake wa kueshi unapofika, wanamwacha."

Malaika wengine ni waandishi Watukufu. Ni wale wenye kuandika matendo

mema na maovu ya waja. Amesema (Ta´ala):

افظي كراماا كاتبي ي علمون ما ت فعلون وإن عليكم

"Na hakika juu yenu bila shaka mmewekewa wenye kulinda. Watukufu wanaoandika. Wanajua yale myafanyayo." (82:10-12)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Nyumba yenye kuamiriwa mbinguni wanaingia - na katika upokezi

mwingine "wanaswali" - kila siku Malaika elfu sabini na baada ya hapo

hawarejei tena."

Yule mwenye kupinga kuwepo kwa Malaika ni kafiri kwa mujibu wa

maafikiano ya waislamu. Amesema (Ta´ala):

ا ا بعيدا خر ف قد ضل ض ئكته وكتبه ورسله والي وم ا ومن يكفر بالل ه وم

"Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake na Vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali." (04:136)

Kuhusu kuamini vitabu vilivyoteremshwa, Allaah (Ta´ala) amemteremshia

kitabu kila Mtume. Amesema (Ta´ala):

م الكتاب والميزان لي قوم الاس بالقسط لقد أرسلا رسلا بالب ي ات وأنزلا مع

"Kwa yakini Tuliwapeleka Mitume Wetu kwa hoja bayana na Tukateremsha pamoja nao Kitabu na shariy‘ah ili watu wasimamie kwa uadilifu." (57:25)

م الكتاب با ذرين وأنزل مع دةا ف ب عث الل ه البيي مبشرين وم وما اخت لف فيه يحكم ب ي الاس فيما اخت لفوا فيه ق ل كان الاس أمةا وام م الب ي ات ب غياا ب ي ق بإذنه إ الذين أوتو من ب عد ما جاءت دى الل ه الذين آموا لما اخت لفوا فيه من ا دي من يشاء والل ه ف ي

صراط مجستقيم إ

Page 31: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

31

www.firqatunnajia.com

"Watu walikuwa Ummah mmoja kisha Allaah Akatuma Manabii wabashiriaji na waonyaji na Akateremsha pamoja nao Kitabu kwa haki ili kihukumu baina ya watu katika waliyokhitilafiana kwayo. Na hawakukhitilafiana katika hayo isipokuwa wale waliopewa hicho baada ya kuwajia hoja bayana kwa uhusuda baina yao. Allaah Akawaongoza wale walioamini kuendea haki katika yale waliyokhitilafiana, kwa idhini Yake. Na Allaah Humwongoza Amtakaye kuelekea njia iliyonyooka." (02:213)

Tunaviamini vitabu hivi, tunatambua kuwa ni vyenye kutoka kwa Allaah na

kujisalimisha kwa maneno Yake (Ta´ala):

اعيل وإسحاق وي عقوب و إب راهيم وإ ا وما أنزل إ م قولوا آما بالل ه وما أنزل إلي البيجون من ر موسى وعيسى وما أو سباط وما أو ام ون د م ن له مسلمون ن فرق ب ي أ

"Semeni: “Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quub na al-Asbaatw na aliyopewa Muusa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni mwao nasi Kwake tunajisalimisha."" (02:136)

ا الذين آموا آموا بالل ه ورسوله والكتاب الذي ن زل على رسوله والكتاب ال ئكته ذي أنزل من ق بل يا أي ج وكتبه ورسله ومن يكفر بالل ه وما ا بعيدا خر ف قد ضل ض والي وم ا

"Enyi mlioamini! Mwaminini Allaah na Mtume Wake na Kitabu Alichokiteremsha kwa Mtume Wake na Kitabu Alichokiteremsha kabla. Na atakayemkufuru Allaah na Malaika Wake, na Vitabu Vyake na Mitume Wake na Siku ya Mwisho, basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali." (04:136)

ا أنزل الل ه من كتاب ت وقل آم

"Na sema: “Nimeamini yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu." (42:15)

لك الكتاب ريب فقون والذين ي ؤ هدا فيه ا ذ ا رزق اهم ي ة و ا أنزل إليك وما ى للمتقي الذين ي ؤمون بالغيب ويقيمون الص مون خرة هم يوقون أنزل من ق بلك وبا

Page 32: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

32

www.firqatunnajia.com

"Alif Laam Miym. Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake, ni Mwongozo kwa wenye taqwa. Ambao huamini ya ghayb na husimamisha swalah na katika vile Tulivyowaruzuku hutoa. Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah." (02:01-04)

Tunaamini kuwa vitabu hivi ni maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) na si ya

mwingine. Allaah (Ta´ala) amezungumza kwavyo kihakika kama

Alivyopenda na Kutaka. Katika maneno haya kuna yenye kusikika kutoka

Kwake nyuma ya pazia pasi na mkati kati. Kama Allaah alivyozungumza na

Muusa kihakika pasi na mkati kati. Amesema (Ta´ala):

ولما جاء موسى لميقاتا وكلمه ربجه

"Na alipokuja Muusa katika miadi Yetu na Mola wake Akamsemesha." (07:143)

اصفيتك على الاس برسا ميقال يا موسى إ وبك

"Akasema: “Ee Muusa hakika Mimi Nimekuteua juu ya watu kwa ujumbe Wangu na maneno Yangu." (07:144)

Maneno mengine ni yale ambayo Allaah (Ta´ala) anamsikilizisha mjumbe

Malaika na anamuamrisha amfikishie mjumbe mwanaadamu. Amesema

(Ta´ala):

ي بإذ اب أو ي رسل رسوا ف يو ياا أو من وراء كيم نه ما يشاء وما كان لبشر أن يكلمه الل ه إ و إنه علي

"Na wala haikuwa kwa mtu yeyote kwamba Allaah Amsemeze isipokuwa kwa njia ya Wahy au kutoka nyuma ya kizuizi au Hutuma Mjumbe, kisha Anamfunulia Wahy kwa idhini Yake Ayatakayo. Hakika Yuko juu, Mwenye hikmah." (42:51)

Imani ya kuamini vitabu kunajumuisha kuamini zile Shari´ah zilizomo katika vitabu vyote na kwamba ilikuwa ni wajibu kwa nyumati walioteremshiwa navyo kujisalimisha navyo na kuhukumu kwa yale yaliyomo ndani. Vitabu hivi vinasadikishana na havikadhibishani. Vitabu vyote kimoja kufutwa na

Page 33: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

33

www.firqatunnajia.com

chenye kuteremshwa baada yake ni jambo la haki. Kwa mfano baadhi ya Shari´ah katika Tawrat zilifutwa na Injiyl. Amesema (Ta´ala) kuhusu ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam):

رم عليكم ل لكم ب عض الذي ومصدقاا لما ب ي يدي من الت وراة و

"Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu." (03:50)

Vivyo hivyo Qur-aan ilifuta vitabu vya kimbingu vilivyotangulia. Amesema

(Ta´ala):

يماا عليه مصدقاا لما ب ي يديه من الكتاب وم

"Kinachosadikisha yale yaliyokuja katika Vitabu vilivyokuwa kabla yake na ikivilinda." (05:48)

وما هو إ ذكر للعالمي

"Na haikuwa isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu." (68:52)

Imani ya kuamini vitabu ni jambo linalotakiwa kuwa la kijumla kwa yale

yaliyotajwa kwa jumla na kwa ufafanuzi kwa yale yaliyotajwa kwa ufafanuzi.

Kuna baadhi ya majina ya vitabu ambavyo Allaah (Ta´ala) amevitaja kwa

ufafanuzi. Kitabu ambacho Allaah amemteremshia Muusa kinaitwa "Tawrat",

kitabu alichoteremshiwa ´Iysaa kinaitwa "Injiyl", kitabu alichoteremshiwa

Daawuud kinaitwa "Zabuur" na kitabu alichoteremshiwa Muhammad

kinaitwa "Qur-aan". Hali kadhalika ametaja (Ta´ala) suhuf ya Ibraahiym na

Muusa - Swalah na salaam ziwaendee. Tunaamini vitabu hivi kwa mujibu wa

ufafanuzi uliyoelezwa.

Allaah ametaja vitabu vingi kwa njia ya ujumla bila ya kutaja kitu juu yake.

Vivyo hivyo tunaviamini kwa ujumla huu. Amesema (Ta´ala):

ا أنزل الل ه من كتاب ت وقل آم

Page 34: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

34

www.firqatunnajia.com

"Na sema: “Nimeamini yale Aliyoyateremsha Allaah katika Kitabu."" (42:15)

Qur-aan Tukufu ambayo Allaah amemteremshia Mtume wetu Muhammad

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio kitabu cha mwisho cha mbinguni na

hakuna kitabu kingine baada yake. Kimefuta vitabu vyote vilivyotangulia na

ni chenye kutumika kwa wanaadamu na majini. Amesema (Ta´ala):

وما هو إ ذكر للعالمي

"Na haikuwa isipokuwa ni ukumbusho kwa walimwengu." (68:52)

Ni chenye kuyazunguka mambo yote ambayo watu wanayahitajia katika dini

na dunia yao. Amesema (Ta´ala):

مت ع م ديااالي وم أكملت لكم ديكم وأ س ليكم نعم ورضيت لكم ا انف ر مت مصة غي ر فإن الل ه غفور فمن اضيم ر

"Leo Nimekukamilishieni dini yenu na Nimekutimizieni neema Yangu na Nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu. Basi atakayefikwa na dharura na kushurutishwa kutokana na njaa kali pasipo kuelekea dhambi; basi hakika Allaah ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (05:03)

Qur-aan ni miujiza na hakuna yeyote ambaye anaweza kuja na mfano wake.

Amesema (Ta´ala):

نج على أن يأتوا ل ه ذا القرآن يأتون له ولو ك وا ن يااقل لئن اجتمعت ا م لب عض ظ ان ب عض

"Sema: “Ikiwa watajumuika wanadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan hawatoweza kuleta mfano wake, japokuwa watasaidiana wao kwa wao." (17:88)

Kadhalika amesema (Ta´ala):

يد يأتيه الباطل من ب ي يديه و من خلفه كيم زيل من ت

"Haitokifikia ubatili mbele yake na wala nyuma yake - ni uteremsho kutoka kwa Mwenye hikmah, Mwenye kustahiki kuhimidiwa kwa yote." (41:42)

Page 35: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

35

www.firqatunnajia.com

Kimehifadhiwa na kuzidishwa na kupunguzwa. Amesema (Ta´ala):

افظون إنا نن ن زلا الذكر وإنا له

"Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaouhifadhi." (15:09)

Kuhusu imani ya kuwaamini Mitume, inatakiwa iwe kwa usadikishaji wa

kukata kabisa ya kwamba Allaah ameutumia kila Ummah Mtume ambaye

aliwalingania katika kumuabudu Allaah Pekee na kukufuru vile vyote

vinavyoabudiwa badala Yake.

Katika hili kunaingia pia ya kwamba wote ni wakweli, wenye kusadikishwa,

wema, wasafi, wachaji Allaah, waaminifu na waongofu na wenye kuongozwa.

Wote wamefikisha ujumbe wa Allaah.

Allaah alimfanya Ibraahiym kuwa kipenzi wa hali ya juu na kadhalika

akamfanya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kipenzi wa

hali ya juu. Allaah alimzungumzisha Muusa kihakika na akamnyanyua Idriys

nafasi ya juu. ´Iysaa ni mja na Mtume wa Allaah, ni neno Lake tu

alilompelekea Maryam na ni roho iliyotoka Kwake.

Allaah amewafadhilisha baadhi juu ya wengine na akawanyanyua daraja

baadhi juu ya wengine.

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio bwana wa wanaadamu

siku ya Qiyaamah na ni jambo litapitika pasi na ufakhari.

Ulinganizi wa Mitume wote ulikuwa ni wenye kuafikiana katika msingi wa

dini, nako ni kumpwekesha Allaah (Ta´ala) katika uungu Wake, uola Wake na

majina na sifa Zake. Amesema (Ta´ala):

م س د الل ه ا إن الدين ع

"Hakika dini mbele ya Allaah ni Uislamu." (03:19)

ر ا اسرين ومن ي بتغ غي خرة من ا م دياا ف لن ي قبل مه وهو ا س

Page 36: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

36

www.firqatunnajia.com

"Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika." (03:19)

Amesema (Ta´ala) kuhusu Nuuh:

أكون من المسلمي وأمرت أن

"Sitaki ujira isipokuwa kwa Allaah na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu." (10:72)

Kadhalika amesema (Ta´ala) kuhusu Muusa:

تم تم بالل ه ف عليه ت وكلوا إن ك تم آم مي مجسل وقال موسى يا ق وم إن ك

“Enyi watu wangu! Ikiwa mmemwamini Allaah; basi Kwake mtegemee, mkiwa ni Waislamu." (10:84)

Vivyo hivyo amesema (Ta´ala) kuhusu Sulaymaan pindi Balqiys aliposema:

ظلمت ن فسي وأسلمت مع سليمان لل ه رب العالم ي رب إ

"Mola wangu! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu na sasa nimesilimu pamoja na Sulaymaan kwa Allaah Mola wa walimwengu." (27:44)

Amesema (Ta´ala):

ا به ا إليك وما وصي ي ا والذي أو ا كب ر أن أقيموا الدين و ت ت فرقوا فيه إب راهيم وموسى وعيسى شرع لكم من الدين ما وصى به نودي إليه من ييب على المشركي ما تدعوهم إليه ت إليه من يشاء وي الل ه

“Amekuamuruni katika dini yale Aliyomuusia kwayo Nuuh, na ambayo Tumekufunulia Wahy na Tuliyomuusia kwayo Ibraahiym, na Muusa na ‘Iysaa kwamba: “Simamisheni dini na wala msifarikiane humo." Yamekuwa makubwa kwa washirikina yale unayowalingania. Allaah Anamteua Kwake Amtakaye na Anamuongoza Kwake anayerudia rudia kutubia." (42:13)

Page 37: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

37

www.firqatunnajia.com

Mitume walikuwa 315 na Manabii 124.000. Haya yamethibiti katika Hadiyth

kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka

katika Hadiyth ya Abu Umaamah na ya Abu Dharr4.

Tofauti kati ya Mtume na Nabii, ni kwamba Nabii ni yule ambaye anapokea

Wahy kutoka kwa Allaah. Akitumwa vilevile kwa wale wenye kwenda

kinyume na maamrisho ya Allaah ili afikishe ujumbe wa Allaah, anahesabika

kuwa Mtume. Ama yule ambaye anatendea kazi Shari´ah ya kabla yake na

asitumwe kwa yeyote ili kufikisha ujumbe kutoka kwa Allaah, anahesabika

kuwa Nabii na sio Mtume5. Mujaahid (Rahimahu Allaah) amesema:

"Mtume ni yule anayezungumzishwa na kupokea Wahy kutoka kwa Allaah

na wala hatumwi [kwa watu]."

Kujengea juu ya haya ni kwamba kila Mtume ni Nabii na sio kila Nabii

anakuwa Mtume.

Allaah (Ta´ala) ametaja wengi katika wao. Kwa mfano Aadam, Nuuh, Idriys,

Huud, Swaalih, Ibraahiym, Ismaa´iyl, Ish-aaq, Ya´quub, Yuusuf, Luutw,

Shu´ayb, Yuunus, Muusa, Haaruun, Ilyaas, Zakariyyah, Yahyaa, al-Yasaa´,

Dhul-Kifl, Daawuud, Sulaymaan, Ayyuub, asbaatw (makabila), ´Iysaa na

Muhammad - Swalah na salaam ziwaendee wote. Allaah ametueleza khabari

zao ambazo ndani yake mna mafunzo na mazingatio na mawaidha:

م عليك ن قصص ا ا قد قصصاهم عليك من ق بل ورس ا ورس وكلم الل ه موسى تكليما

"Na Mitume Tuliokwishakusimulia habari zao kabla na Mitume [wengine ambao] Hatukukusimulia habari zao - na bila shaka Allaah Alimsemesha Muusa maneno ya kikweli." (04:164)

Kwa hivyo tunawaamini kwa ufafanuzi pale wanapotajwa kwa ufafanuzi na kwa jumla pale wanapotajwa kwa jumla.

4 Tazama ”Silsilah al-Ahaadiyth as-Sahiyhah” (6/358/2668) ya Imam Muhammad Naaswir-ud-Dîn al-Albaaniy.

5 ”an-Nubuwwaat” ya Shaykh-ul-Islaam, uk. 255.

Page 38: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

38

www.firqatunnajia.com

Tunaamini kuwa Mitume na Manabii wote ni wanaadamu walioumbwa na

hawana sifa yoyote ile ya kiungu. Amesema (Ta´ala):

د كم إل ه وا ا إل أ ى إ ا أنا بشر م لكم يو ا قل إ دا اا و يشرك بعبادة ربه أ ا صا فمن كان ي رجو لقاء ربه ف لي عمل عم

"Sema: “Hakika mimi ni mtu kama nyinyi Isipokuwa tu nafunuliwa Wahy kwamba: "Hakika mungu wenu wa haki ni mungu Mmoja Pekee". Hivyo anayetaraji kukutana na Mola wake na atende ‘amali njema na wala asishirikishe katika ‘ibaadah za Mola wake yeyote." (18:110)

م إن نن إ بش م رسل نج على من يشاء من عباد قالت وعلى وما كان لا أن نأتيكم بسلان إ بإذن الل ه ر م لكم ول كن الل ه الل ه ف ليت وكل المؤمون

"Mitume wao wakawaambia: “Sisi si chochote isipokuwa ni watu kama nyinyi, lakini Allaah Anamfadhilisha Amtakaye miongoni mwa waja Wake. Na haikutupasa sisi kukujieni kwa hoja mnazotaka isipokuwa kwa idhini ya Allaah. Na kwa Allaah Pekee wanategemea waumini." (14:11)

لك من المرسل سواق وما أرسلا ق ب م ليأكلون العام وشون ا ون ي إ إن ةا أتص وكان ربجك بصياا وجعلا ب عضكم لب عض فت

"Na Hatukupeleka kabla yako Mitume wowote isipokuwa bila shaka walikuwa wanakula chakula na wanatembea masokoni. Na Tumejaalia baadhi yenu nyinyi kwa nyinyi kuwa ni majaribio je mtavumilia? Na Mola wako daima ni Mwenye kuona." (25:20)

ملك دي خزائن الل ه و أعلم الغيب و أقول لكم إ إن قل أقول لكم ع ى إ عمى أتبع إ ما يو قل هل يستوي ا ت ت فكرون والبصي أف

"Sema: “Sikuambieni kuwa mimi nina hazina ya Allaah na wala kwamba najua ya ghayb na wala sikuambieni kuwa mimi ni Malaika. Sifuati ila yale nilofunuliwa Wahy". Sema: “Je, analingana sawasawa kipofu na mwenye kuona - basi hamtafakari?"" (06:50)

فسي ن فعاا و ضرا إ ما شاء الل ه ال قل أملك ل ي وما مس ستك رت من ا ت أعلم الغيب وء ولو ك إن أنا إ نذير وبشي سج لقوم ي ؤمون

Page 39: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

39

www.firqatunnajia.com

"Sema: “Siimilikii nafsi yangu manufaa yoyote wala dhara yoyote isipokuwa Apendavyo Allaah na lau ningekuwa najua ya ghayb, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri na wala lisingelinigusa ovu. Mimi si chochote isipokuwa ni mwonyaji na mbashiriaji kwa watu wanaoamini."" (07:188)

Tunaamini kuwa ni waja miongoni mwa waja wa Allaah ambao Allaah amewaheshimisha kwa Ujumbe. Amewasifu kuwa ni waja pindi zinapotajwa nafasi zao kuu na pindi Anapowasifu.

Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) amekhitimisha Ujumbe kwa Ujumbe wa

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba Alimtuma kwa

walimwengu wote majina na wanaadamu:

يعاا رسول الل ه إليكم ا الاس إ قل يا أي ج

"Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote."" (07:158)

ةا للعالمي وما أرسلاك إ ر

"Na Hatukukutuma isipokuwa uwe ni Rahmah kwa walimwengu." (21:107)

وما أرسلاك إ كافةا للاس بشياا ونذيراا ول كن أك ر الاس ي علمون

"Na Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui." (34:28)

Ameeleza (Ta´ala) kuwa amechukua ahadi kwa Mitume endapo wataishi zama za Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi wamfuate. Hapa kuna dalili ya wazi kabisa ya kwamba Ujumbe wake ndio wa mwisho na kuwa unafuta nyujumbe zingine zote zilizotangulia. Amesema (Ta´ala):

جاءكم رسول مجصدق لما وإ كمة صرنه ذ أخذ الل ه مياق البيي لما آت يتكم من كتاب و معكم لت ؤمن به ولت قال أأق رر وأخذلكم إصري لك فأول ئك هم الفاسقون ق قالوا أق ررنا على ذ ب عد ذ دوا وأنا معكم من الشاهدين فمن ت و ال فاش

"Na pale Allaah Alipochukua ahadi kwa Manabii: Nikisha kupeni Kitabu na hikmah, kisha akakujieni Mtume mwenye kusadikisha mliyo nayo, ni juu yenu mumuamini na mumsaidie. Akasema: "Je, mmekiri nammekubali

Page 40: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

40

www.firqatunnajia.com

kushika agizo langu juu ya hayo?" Wakasema: "Tumekubali." Akasema: "Basi shuhudieni na Mimi nipamoja nanyi katika kushuhudia. Watakaogeuka baada ya haya basi hao ndio mafusaki." (03:81-82)

Mitume walikuja na bishara njema juu ya Ujumbe wa Muhammad (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) - swalah na salaam ziwe juu yao wote. Amesema

(Ta´ala):

رسول الل ه إليكم مجصدقاا لما ب ي يدي إسرائيل إ ه وإذ قال عيسى ابن مرم يا ب من الت وراة ومبشراا برسول يأ من ب عدي اد سحر مجبي ف لما جاءهم بالب ي ات قالوا ه ذا أ

"Na pale ´Iysaa mwana wa Maryam aliposema: “Enyi wana wa Israaiyl! Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake "Ahmad." Basi alipowajia kwa hoja bayana, walisema: “Huu ni uchawi wa wazi." (61:06)

خرة إنا هدنا إليك سةا و ا ن يا الدج وسعت كل شيء قال عذا أصيب به من أشاء واكتب لا ه ذ ا ور فسأكتب م للذين ا يل ي ت قون وي ؤتون الزكاة والذين هم بآياتا ي ؤمون الذين ي تبعون الرسول ال دهم الت وراة وا دونه مكتوباا ع ي الذي

“Na Tuandikie katika dunia hii mazuri na katika Aakhirah. Hakika sisi tumerudi kutubu Kwako. Akasema: “Adhabu Yangu Nitamsibu nayo Nimtakaye na Rahmah Yangu imeenea kila kitu. Basi Nitawahukumia wale wenye taqwa na wanaotoa zakaah na ambao wao wanaziamini Aayaat Zetu. Wale wanomfuata Mtume, Nabii asiyejua kuandika na kusoma, wanamkuta ameandikwa kwao katika Tawraat na Injiyl." (07:156-157)

Katika "as-Swahiyh" ya Muslim imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi Mwake.

Hatosikia kuhusu mimi sawa awe myahudi au mnaswara kisha asiamini

yale niliyotumwa kwayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni."

Page 41: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

41

www.firqatunnajia.com

Yule mwenye kukanusha Ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) kwa walimwengu wote, amewakanusha Mitume wote hata yule

Mtume ambaye anadai kuwa anamuamini na kumfuata. Amesema (Ta´ala):

كذبت ق وم نوح المرسلي

"Watu wa Nuuh walikadhibisha Mitume." (26:105)

Amefanya kuwa waliwakadhibisha Mitume wote pamoja na kuwa Nuuh ndiye alikuwa Mtume wa kwanza.

Tunaamini kuwa hakuna Nabii yoyote baada ya Muhammad (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam). Yule mwenye kudai kuwa kuna Nabii mwingine baada

yake, amekufuru. Allaah (Ta´ala) amesema:

د من رجالكم ول كن رسول الل ه وخا البيي مد أبا أ ما كان

"Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii." (33:40)

Katika "as-Swahiyh" ya Muslim imepokelewa kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Nimefadhilishwa juu ya Mitume wengine kwa mambo sita: nimepewa

maneno ambayo ni machache lakini yenye maana pana, nimenusuriwa kwa

woga [unaotiwa kwenye nyoyo za maadui], nimehalalishiwa mateka,

nimefanyiziwa ardhi yote kuwa safi na mahali pa kuswalia, nimetumwa

kwa viumbe wote na mimi ndiye Nabii wa mwisho."

Mwenye kukanusha Ujumbe wa Nabii au Mtume yoyote, amekufuru kwa

maafikiano ya waislamu. Amesema (Ta´ala):

ا ن بب إن الذين يكفرون بالل ه ورسله ويريدون أن ي فرقوا ب ي الل ه ورسله وي قولون ن ؤم لك سبي عض ونكفر بب عض ويريدون أن ي تخذوا ب ي ذقا د م أول ئك هم الكافرون ي فرقوا ب ي أ ياا والذين آموا بالل ه ورسله و م أول وأعتدنا للكافرين عذاباا مج م ئك سوف ي ؤتي

ا أجورهم يما وكان الل ه غفوراا ر

Page 42: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

42

www.firqatunnajia.com

"Hakika wale waliomkufuru Allaah na Mitume Wake na wanataka kufarikisha baina ya Allaah na Mitume Wake na wanasema: “Tunaamini baadhi [ya Mitume] na tunawakanusha wengine”, na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo - hakika hao ndio makafiri wa kweli na Tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha. Na wale waliomwamini Allaah na Mitume Wake na hawakumfarikisha yeyote baina yao, hao Atawapa ujira wao na Allaah daima ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu." (04:150-152)

Kuhusu kuamini siku ya Mwisho, ni siku ya Qiyaamah na yale mambo na hali

zitazopitika ndani yake.

Ahl-us-Sunnah wanaamini hilo kwa yakini. Amesema (Ta´ala):

خرة هم يوقون ا أنزل إليك وما أنزل من ق بلك وبا والذين ي ؤمون

"Na ambao huamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako na ni wenye yakini na Aakhirah." (02:04)

ي وم القيامة ريب فيه الل ه إل ه إ هو معكم إ دياا لي ومن أصدق من الل ه

"Allaah, hakuna mungu wa haki ila Yeye. Bila ya shaka Atakukusanyeni Siku ya Qiyaamah haina shaka ndani yake. Na nani mkweli zaidi katika maneno kuliko Allaah?" (04:87)

تية وإن الساعة

"Hakika Saa bila shaka itafika." (15:85)

Katika hilo kunaingia vilevile kuamini Ufufuliwaji, nayo ni ile Siku maiti

watahuishwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

رض إ من شاء الل ه ونفخ الصجور فصعق من السماوات وم ظرون ن ا نفخ فيه أخرى فإذا هم قيام ي

"Na itapulizwa katika baragumu watazimia wale walioko mbinguni na ardhini isipokua Amtakaye Allaah. Kisha litapulizwa humo jengine tahamaki hao wanasimama wakitazama." (39:68)

Page 43: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

43

www.firqatunnajia.com

ا كما بدأنا أول خلق نجعيد ا علي إنا كا فاعلي وعدا

"Kama Tulivyoanza uumbaji umbo la awali Tutalirudisha. Hiyo ni ahadi juu Yetu - hakika Sisi ni Wafanyao." (21:104)

Katika haya kunaingia pia kuamini madaftari ya matendo ambayo

yatagawiwa kwa mkono wa kulia au wa kushoto nyuma ya mgongo. Allaah

(Ta´ala) amesema:

سابيه ق م ت أ ظ كتابه بيميه ف ي قول هاؤم اق رءوا كتابيه إ و فأما من أو ا دانية كلوا ف وف عيشة راضية جة عالية ق كتابه بشماله ف ي قول ي الية وأما من أو يام ا ا أسلفتم ا ساب واشربوا هيئاا أدر ما أوت كتابيه و ا كانت القاضية ا ليت يه يا ليت

ماليه ع عون ذراعاا ف ما أغ ا سب سلسلة ذرع حيم صلجو ا سلانيه خذو ف غلجو اسلكو إنه كان ي ؤمن بالل ه هلك عيم و طعام إ من غسلي ي العظيم له الي وم هاها ضج على طعام المسكي ف لي اطئون و أكله إ ا

"Ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: “Hebu chukueni someni kitabu changu! Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu". Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Kwenye Pepo ya juu. Matunda yake ya kuchumwa ni karibu. [Wataambiwa]: “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita." Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: “Ee, laiti nisingelipewa kitabu changu na wala nisingelijua hesabu yangu! Ee, laiti yangelikuwa mauti ndio kumalizika kwangu. Haikunifaa mali yangu. Ufalme wangu umeangamia." [Itasemwa]: “Mchukueni na mfungeni pingu kisha kwenye [Moto wa] al-Jahiym muingizeni aungue. Halafu katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini mtieni pingu. Hakika yeye alikuwa hamuamini Allaah Mkuu na wala hahamasishi kulisha masikini. Basi leo hapa hatokuwa na rafiki wa dhati, na wala [hawatopata] chakula isipokuwa maji ya vidonda vilooshwa [vya walio Motoni]. Hawakili [chakula] hicho isipokuwa wenye hatia. (69:19-37)

Vilevile kuamini Mizani itayowekwa siku ya Qiyaamah na hivyo hakuna yoyote atayedhulumiwa. Amesema (Ta´ala):

م خالدون فمن ث قلت موازيه فأول ئك هم المفلحون م ج ومن خفت موازيه فأول ئك الذين خسروا أنفس

Page 44: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

44

www.firqatunnajia.com

"Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, hao ndio wenye kufaulu. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu, basi hao ni wale ambao wamekhasirika nafsi zao watakuwa katika [Moto wa] Jahannam ni wenye kudumu." (23:102-103)

Kadhalika kunaingia kuamini uombezi katika kisimamo hicho. Kuna aina nne za uombezi:

Uombezi mkubwa [ash-Shafaa´ah al-´Udhwma]: Hii ni kwa Muhammad

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake na itapitika pindi watu

wanasubiri wahukumiwe.

Uombezi ili milango ya Peponi ifunguliwe: Aina hii pia ni kwa Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake.

Uombezi wa kukhafifishiwa adhabu yule mwenye kuiistahiki: Kadhalika

aina hii ni kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake pindi

atapomuombea ami yake Abu Twaalib akhafifishiwe adhabu ya Moto. Haya

ni malipo kwa kuwa alikuwa akimlinda na kumchunga.

Uombezi ili baadhi ya watu zinyanyuliwe daraja zao Peponi: Aina hii

imesemekana kuwa ni kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke

yake na imesemekana pia kuwa si yeye pekee.

Uombezi kwa wenye madhambi makubwa: Hawa ni wale wapwekeshaji

watenda madhambi. Wametumbukia Motoni kwa sababu ya madhambi yao

na wataombewa ili watoke humo. Uombezi huu Mtume wa Allaah (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam), Mitume na Malaika na waja wema wana haki juu

yake.

Kadhalika Qur-aan na swawm vitawaombea watu wake siku ya Qiyaamah.

Vilevile watoto wa waumini watawaombea wazazi wao.

Vilevile inahusiana na kuamini hodhi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam). Maji yake ni maeupe kushinda maziwa, matamu kushinda asali na

yenye harufu nzuri kushinda ya miski. Atayekunywa humo mara moja, basi

hatohisi kiu tena kamwe.

Page 45: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

45

www.firqatunnajia.com

Ni lazima pia kuamini Njia itayowekwa juu ya Moto. Watu watapita juu yake

kwa mujibu wa matendo yao. Mtu wa kwanza atapita kama umeme, halafu

kama upepo na halafu mwingine kama ndege. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) amesimama kwenye Njia akisema:

"Ee Mola! Salimisha, salimisha!"

Baada ya hapo matendo ya waja yatapungua mpaka atapokuja mtu ambaye

atatambaa kwa sababu hawezi kutembea. Kwenye ncha ya Njia

kumetundikwa ndoano zilizoamrishwa kumchukua wenye wastahiki. Hivyo

mwenye furaha ataokoka na mla khasara atatumbukia Motoni.

Tunaamini yale yote yaliyokuja katika Qur-aan na Sunnah juu ya siku hiyo na

hali zake - Allaah atulinde nazo.

Kuhusu kuamini Qadar kheri na shari yake, inahusiana na kuthibitisha kwa

kukata kabisa ya kwamba Allaah alikadiria makadirio ya viumbe na kwamba

yale yote yaliyopitika, Allaah aliyataka, na yale yote ambayo hayakupitika,

Allaah hakuyataka. Allaah (Ta´ala) amesema:

بقدر eإنا كل شيء خلقا

"Hakika sisi Tumekiumba kila kitu kwa makadirio." (54:49)

وكان أمر الل ه قدراا مقدوراا

"Na amri ya Allaah daima ni majaaliwa yaliyohukumiwa." (33:38)

Qadar ina daraja nne:

Ya kwanza: Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) anakijua kila kitu. Anakijua kila

kilichokuwepo, kilichopo na vipi kitakuwa kwa elimu Yake ya milele. Hajiwi

na elimu mpya baada ya kutokujua na wala hasahau baada ya kujua.

Ya pili: Tunaamini kuwa Allaah aliandika katika Ubao uliohifadhiwa kila

kitachokuwepo mpaka Qiyaamah kisimame. Amesema (Ta´ala):

Page 46: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

46

www.firqatunnajia.com

رض ت علم أن الل ه ي علم ما السماء وا لك كتاب أ لك على الل ه يسي إن ذ إن ذ

"Je, hujui kwamba Allaah Anajua yale yote yaliyomo katika mbingu na ardhi? Hakika hayo yamo katika Kitabu. Hakika hayo kwa Allaah ni mepesi." (22:70)

د ر كتاب ا ع قال علم و سى قال فما بال القرون ا يضلج ر و ي

"Akasema: "Basi nini hali ya karne za awali?" Akasema: "Ujuzi wake uko kwa Mola wangu katika Kitabu. Hapotezi Mola wangu na wala Hasahau."" (20:51-52)

إمام مجبي ا صي وكل شيء أ

"Kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari bayana." (36:12)

Katika nukta hii kunaingia vilevile makadirio ya milele kabla ya kuumba

mbingu na ardhi. Amesema (Ta´ala):

نا قل لن يصيب ا إ ما كتب الل ه لا هو مو

"Sema: “Halitusibu lolote isipokuwa lile Alilotukidhia Allaah - Yeye ni mlinzi Wetu."" (09:51)

Kadhalika inahusiana na Siku makubaliano yalipoandikwa:

ألست بربكم

“Je, Mimi siye Mola wenu?” (07:172)

Amesema (Ta´ala):

م ألست بربكم دهم على أنفس م وأش ورهم ذري ت آدم من ظ قالوا ب لى وإذ أخذ ربجك من ب

"Na pindi Mola wako Alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao na Akawashuhudisha juu ya nafsi zao: “Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndiye." (07:172)

Page 47: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

47

www.firqatunnajia.com

Kuhusu makadirio ya maisha, yanapitika pale tone la mbegu linapotumbukia

kwenye kifuko cha uzazi. Ndipo hutumwa Malaika anayepulizia kipande cha

nyama roho na anaamrishwa mambo mane; riziki yake, muda atakaoeshi,

matendo yake na kama atakuwa mwenye furaha au mla khasara.

Ama kuhusu makadirio ya hali, yanapitika katika usiku wenye Cheo.

Amesema (Ta´ala):

كيم ا ي فرق كلج أمر في

"Humo hupambanuliwa kila jambo la hikmah." (44:04)

Ibn ´Abbaas amesema:

"Katika usiku wenye Cheo kunaandikwa kwenye mama wa Kitabu

yatayokuwepo katika mwaka mauti, uhai, riziki, mvua na mahujaji.

Kunasemwa: "Atahiji fulani, atahiji fulani.""

Kuhusu makadirio ya kila siku, amesema (Ta´ala):

كل ي وم هو شأن

"Kila siku Yeye Yumo katika kuleta jambo." (55:29)

Makadirio ya kila siku ni upambanuzi wa makadirio ya hali, makadirio ya hali

ni upambanuzi wa makadirio ya maisha pindi kinapoumbwa kipomoko,

makadirio ya maisha ni upambanuzi wa makadirio ya maisha ya kwanza

pindi ilipopitika Siku ya makubaliano ambapo pia ni upambanuzi wa

makadirio ya milele ambayo Kalamu iliandika kwenye Kitabu

kinachobainisha. Kitabu hichi chenye kubainisha ni katika elimu ya Allaah

(´Azza wa Jall). Kadhalika kikomo cha makadirio kinaishia katika elimu ya

Allaah (´Azza wa Jall).

ى ت ربك الم وأن إ

"Na kwamba kwa Mola wako ndio kikomo." (53:42)

Page 48: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

48

www.firqatunnajia.com

Ya tatu: Utashi. Tunaamini kuwa Allaah (Ta´ala) ametaka kila kilichomo

mbinguni na ardhini. Hakukuwi kitu isipokuwa kwa kutaka Kwake.

Anachokitaka, huwa, na asichokitaka, hakiwi. Amesema (Ta´ala):

ا أمر إذا أراد شيئاا أن ي قول له كن ف يك ون إ

"Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!" nacho huwa." (36:82)

تت لوا ول كن الل ه ي فعل ما يريد ولو شاء الل ه ما اق

"Na lau Angelitaka Allaah wasingelipigana lakini Allaah Anafanya Ayatakayo." (02:253)

دى ولو م على ا مع شاء الل ه

"Na kama Angetaka Allaah Angeliwakusanya katika uongofu." (06:35)

دةا عل الاس أمةا وا ولو شاء ربجك

"Na kama Angetaka Mola wako, basi Angejaalia watu wote kuwa ni ummah mmoja." (11:118)

ول ق القول م هداها ول كن ا كل ن ف ت ي ا و شئ

"Na Tungelitaka, Tungeliipa kila nafsi mwongozo wake, lakini imethibiti kauli kutoka Kwangu." (32:13)

ز من شيء السماوات و ا رض وما كان الل ه لي ع

"Na hakuna lolote limshindalo Allaah mbinguni na wala ardhini." (35:44)

Ya nne: Uumbaji. Hakika Yeye (Ta´ala) ndiye ameumba kila mtendaji na matendo yake, kila mwenye kufanya harakati na harakati zake na kila mwenye kutulia na utulivu wake. Amesema (Ta´ala):

والل ه خلقكم وما ت عملون

Page 49: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

49

www.firqatunnajia.com

"Allaah Amekuumbeni na yale mnayoyatenda." (37:96)

وهو على كل شيء وكيل الل ه خالق كل شيء

"Allaah ni Muumbaji wa kila kitu, Naye juu ya kila kitu ni mdhamini Anayetegemewa kwa yote." (39:62)

Pamoja na hivyo tunaamini kuwa waja wana uwezo, utashi na matakwa juu

ya matendo yao. Allaah (Ta´ala) ndiye amewaumba wao na matakwa yao,

uwezo wao, maneno yao na matendo yao. Maneno na vitendo vinavyotoka

kwao, vinanasibishwa kwao kihakika na kwavyo ndivyo ima watalipwa

thawabu au adhabu. Hata hivyo wao hawawezi isipokuwa yale ambayo

Allaah (Ta´ala) amewawezesha na wala hawatotaka isipokuwa Allaah akitaka

kwanza. Amesema (Ta´ala):

تذكرة رب إن ه ذ ذ إ ا فمن شاء ا كيماا وما تشاءون إ أن يشاء الل ه ه سبي ا إن الل ه كان عليما

"Hakika huu ni ukumbusho, basi anayetaka achukue njia ya Mola wake. Na hamtoweza kutaka chochote isipokuwa Atake Allaah - hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye hikmah." (76:29-30)

كم أن يستقيم وما تشاؤون إ أن يشاء الله ربج ا لعالمي إن هو إ ذكر للعالمي لمن شاء م

"Haikuwa huu ila ni Ukumbusho kwa walimwengu wote - kwa yule miongoni mwenu anayetaka anyooke. Wala nyinyi hamtataka isipokuwa atake Allaah, Mola wa walimwengu." (81:27-29)

ا ا إ وسع ا ما اكتسبت يكلف الل ه ن فسا ا ما كسبت وعلي

"Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake. Itapata [thawabu] iliyoyachuma na ni dhidi yake [kwa dhambi] iliyojichumia." (02:286)

تم ت عملون ا ك أورث تموها ة ال وتلك ا

"Na hiyo ni Pepo ambayo mmerithishwa kwa yale mliyokuwa mkitenda." (43:72)

Page 50: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

50

www.firqatunnajia.com

ا ك لد تم ت عملون وذوقوا عذاب ا

"Onjeni adhabu yenye kudumu kwa yale mliyokuwa mkiyatenda." (32:14)

راا ي ر ومن ي عمل م قال ذرة شرا ي ر فمن ي عمل م قال ذرة خي

"Basi yule atakayetenda kheri sawa na uzito wa chembe ya atomu, ataiona, na yule atakayetenda shari sawa na uzito wa chembe ya atomu, ataiona." (99:07-08)

Tunaamini kuwa makadirio hayamzuii mtu na kutenda kama ambavyo

vilevile hayamfanyi mtu akayategemea. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) alipowaeleza Maswahabah zake juu ya Qadar, na kwamba

yameanza kufanya kazi na kwamba kalamu imekauka, wakamwambia:

"Tusitegemee yaliyopangwa kwetu na tukaacha kutenda?"

Akasema:

"Hapana. Tendeni, kila kitu kimewepesishwa."

Halafu akasoma:

ى وات قى وصدق ب فأما من أع س يسر للعسرى ا فس س وكذب با ل واست غ يسر لليسرى وأما من فس

"Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema, basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema, basi Tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu." (92:05-10)

Makadirio yana sababu zinazomfanya mtu akayafikia. Kama ambavyo kuoa ni

sababu inayopelekea kupata kizazi na kilimo ni sababu inayopelekea katika

mavuno, kadhalika matendo mema ni sababu inayopelekea kuingia Peponi na

matendo mabaya ni sababu inayopelekea katika Moto.

Page 51: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

51

www.firqatunnajia.com

05. ´Aqiydah sahihi juu ya imani

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamona na kuonelea

kuwa imani ni kutamka shahaadah ya upwekeshaji ya kwamba hakuna

mungu wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa

Allaah, kuyaamini yakini maneno haya na matendo ya viungo vya mwili.

Imaam ash-Shaafi´iy amesema:

"Maswahabah, Taabi´uun na wale tuliokutana nao walikuwa ni wenye

kuafikiana kwa kusema kwamba imani ni maneno, matendo na nia. Mtu

halipwi kwa kuacha moja katika hivyo vitatu."

Imepokelewa na al-Laalakaa´iy katika "as-Sunnah".

Imani inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Allaah (Ta´ala) amesema:

انااالذي عوا لكم فاخشوهم ف زادهم إ م الاس إن الاس قد ن قال

"Wale walioambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni" yakawazidishia imani." (03:173)

م م آياته زادت م ي ت وكلون وإذا تليت علي اناا وعلى ر إ

"Wanaposomewa Aayaat Zake huwazidishia imani na kwa Mola wao wanategemea." (08:02)

اناا إ م من ي قول أيجكم زادته ه ذ اناا وهم يستبشرون فأما الذين آموا ف زا وإذا ما أنزلت سورة فم م إ دت

"Na inapoteremshwa Suurah, basi miongoni mwao wako wanaosema: “Nani kati yenu [Suurah] hii imemzidishia imani? Ama wale walioamini huwazidishia imani nao wanafurahia." (09:124)

ا زاب قالوا ه ذا ما وعدنا الل ه ورسوله وصدق الل ه ورسوله ولما رأى المؤمون ا اناا وتسليما وما زادهم إ إ

"Basi waumini walipoona yale makundi, walisema: “Haya ndio yale Aliyotuahidi Allaah na Mtume Wake na Amesema kweli Allaah na Mtume Wake - na haikuwazidishia isipokuwa imani na kujisalimisha." (33:22)

Page 52: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

52

www.firqatunnajia.com

م ا اناا مع إ هو الذي أنزل السكية ق لوب المؤمي لي زدادوا إ

"Yeye Ndiye Aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za waumini ili Awazidishie imani pamoja na imani zao." (48:04)

اناا وي زداد الذين آموا إ

"Na iwazidishie imani wale walioamini." (74:31)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Ibn ´Umar ya kwamba

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwatolea mawaidha wanawake

na akawaambia:

"Sijaona walio na akili punguani na dini pungufu wanaomghalibu mtu

mwenye busara kama nyinyi [wanawake]."

Hii ni dalili juu ya kupungua kwa imani. Vilevile amesema (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam):

"Muumini aliye na imani kamilifu zaidi ni yule aliye na tabia njema zaidi."

Ameipokea Ahmad na wengineo kutoka kwa Abu Hurayrah.

Ikiwa ambaye yuko imani kamilifu zaidi ana tabia njema zaidi, basi aliye na

tabia mbaya ana imani pungufu zaidi.

Imani sio maneno na matendo peke yake pasi na kuamini, kwa kuwa hii ni

imani ya wanafiki. Amesema (Ta´ala):

ؤمي خر وما هم ومن الاس من ي قول آما بالل ه وبالي وم ا

"Na miongoni mwa watu wako wasemao: ”Tumemuamini Allaah na Siku ya Mwisho" hali ya kuwa si wenye kuamini."" (02:08)

Wala imani sio kule kuwa na utambuzi peke yake, kwa kuwa hii ni imani ya

makafiri na wakanamungu. Amesema (Ta´ala):

ا وعلوا م ظلما ا أنفس قت ا واست ي وجحدوا

Page 53: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

53

www.firqatunnajia.com

"Wakazikanusha na hali kuwa nafsi zao zimeziyakinisha kwa dhulma na majivuno." (27:14)

حدون م يكذبونك ول كن الظالمي بآيات الل ه فإن

"Hakika wao hawakukadhibishi wewe lakini madhalimu wanakanusha Aayaat za Allaah." (06:33)

اهم الكتاب ي عرفونه كما ي عرفون أب اءهم الذين آت ي

"Wale Tuliowapa Kitabu wanatambua kama wanavyotambua watoto wao." (02:146)

م وكانوا من ق بل يست فتحون على الذين د الل ه مصدق لما مع ف لعة الل ه ما عرفوا كفروا به كفروا ف لما جاءهم ولما جاءهم كتاب من ع على الكافرين

"Na kilipowajia Kitabu kutoka kwa Allaah kisadikishacho yale yaliyo pamoja nao na japokuwa hapo kabla walikuwa wakiomba ushindi dhidi ya wale waliokufuru, basi yalipowajia yale waliyokuwa wakiyatambua waliyakanusha, basi laana ya Allaah iwe juu ya makafiri." (02:89)

م ود وقد ت ب ي لكم من مساك م فصدهم عن السبيل وكانوا مستبصرين وعاداا و م الشيان أعما وزين

"Na [Tuliwaangamiza pia kina] ‘Aad na Thamuud na yamekwishakubainikieni masikani yao; na shaytwaan aliwapambia ‘amali zao akawazuia na njia, na walikuwa ni wenye kumaizi." (29:38)

Kadhalika imani sio maneno na kuamini pasi na matendo. Allaah ameyaita

matendo kuwa ni imani. Amesema (Ta´ala):

انكم وما كان الل ه ليضيع إ

"Na Allaah Hakuwa Mwenye kupoteza imani zenu." (02:143)

Bi maana swalah zenu kuelekea Yerusalemu. al-Bukhaariy na Muslim

wamepokea kutoka kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya

Page 54: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

54

www.firqatunnajia.com

kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuuambia

msafara wa ´Abdul-Qays:

"Ninakuamrisheni mambo mane; kumuamini Allaah na hivi mnajua ni nini

kumuamini Allaah? Ni kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki

isipokuwa Allaah, kusimamisha swalah, kutoa zakaah, kufunga

Ramadhaan na kutoa khumusi ya mateka yenu."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea vilevile kutoka kwa Abu Hurayrah

(Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema:

"Imani ni tanzu sabini na kitu - au ni tanzu sitini na kitu. Bora yake ni

kushuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na ya

chini yake ni kuondosha chenye kudhuru njiani na hayaa pia ni tanzu

katika imani."

Page 55: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

55

www.firqatunnajia.com

06. Msimamo wa Ahl-us-Sunnah juu ya Takfiyr

Hakuna kitendo chochote kukiacha kwake ni kufuru isipokuwa swalah peke

yake. Yule mwenye kuiacha pasi na kifungamanishi basi amekufuru.

Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

wameafikiana juu ya hilo. ´Abdullaah bin Shaqiyq amesema:

"Hakuna kitu Maswahabah wa Mtume wa Allaah ambacho walikuwa

wakionelea kukiacha kwake ni kufuru isipokuwa swalah."

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Takfiyr ni haki ya Allaah. Asiwepo atayemkufurisha yeyote isipokuwa tu yule

ambaye amekufurishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) au mtu ambaye waislamu wameafikiana juu ya kumkufurisha.

Ambaye atamkufurisha mtu kwa kitu kisichokuwa ukafiri ambacho

kimesimama juu ya hoja zilizo wazi kutoka katika Qur-aan tukufu, Sunnah

Swahiyh au maafikiano, basi mtu huyo anastahiki adhabu kali na kuaziriwa.

Kwa sababu al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Thaabit bin adh-Dhwahhaak

(Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenye kumtuhumu muumini ukafiri basi ni kama kumuua."

Kufuru inaweza kupatikana kwa kutamka neno, kufanya kitendo na kuitakidi

imani fulani ya kufuru ambayo hakuna tofauti yoyote inayozingatiwa.

Miongoni mwa mambo vilevile yanayoshurutisha ukafiri ni mtu kuhalalisha

[kitu au jambo la haramu].

Tofauti kati ya kukufurisha kwa jumla na kumkufurisha mtu maalum:

kukufurisha kwa jumla ni kama makemeo ya jumla. Mtu anatakiwa kusema

vile ilivyo kama ambavyo haikufungamana na kwa ujumla wake. Mfano wa

hilo ni kama walivyosema maimamu:

"Mwenye kusema Qur-aan imeumbwa ni kafiri."

Page 56: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

56

www.firqatunnajia.com

Ibn Khuzaymah (Rahimahu Allaah) amesema:

"Ambaye hathibitishi kuwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi na yuko juu ya

mbingu saba ni kafiri ambaye damu yake ni halali. Mali yake inakuwa fai."

Kuhusu kumkufurisha mtu maalum ni lazima masharti yatimie na kusiwepo

vikwazo. Kukufurisha kwa jumla ambako hakufungamana hakupelekei

kumkufurisha mtu maalum mpaka yatimie masharti ya kukufurisha na

vikwazo viondoke.

Page 57: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

57

www.firqatunnajia.com

7. ´Aqiydah sahihi juu ya muislamu mtenda dhambi

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa hakuna dhambi, mbali na

shirki, inayomtoa muislamu katika Uislamu isipokuwa pale atapoihalalisha.

Ni mamoja akawa ni mwenye kuifanya na huku anaona kuwa ni halali au

akawa anaamini kuwa ni halali pasi na kuifanya. Kwa sababu hii ina maana

ya kwamba atakuwa ni mwenye kuikadhibisha Qur-aan na Mtume (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo ni kufuru kwa mujibu wa Kitabu,

Sunnah na maafikiano.

Hakuna dhambi inayomfanya mwenye nayo kudumu Motoni milele

isipokuwa tu shirki. Allaah (Ta´ala) amesema:

لك لمن يشاء إن الل ه ي غفر أن يشرك به وي غفر ما دون ذ

"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae." (04:48)

Aayah imefahamisha kuwa mtenda dhambi yuko chini ya matakwa ya Allaah;

Akitaka (Ta´ala) kumsamehe atamsamehe kwa fadhila na ukarimu Wake, na

Akitaka atamuingiza Motoni kwa kiasi cha dhambi yake ili umsafishe na

madhambi halafu baada ya hapo atamtoa kutokana na Tawhiyd yake kisha

amwingize Peponi.

Allaah ametaja baadhi ya madhambi makubwa katika Kitabu Chake. Baadhi

yake ni kuua na manyanyaso. Hata hivyo Amethibitisha imani kwa wenye

nayo. Mtu kama huyo ni muumini kwa imani yake, mtenda dhambi kwa

dhambi zake. Amesema (Ta´ala):

ا الذين آموا كتب عليكم القصاص ا لىيا أي ج نى لقت نى با ر والعبد بالعبد وا رج با فمن عفي له من أخيه شيء فات باع اسان بالمعروف وأداء إليه بإ

"Enyi mlioamini! Mmeandikiwa shariy’ah kisasi waliouawa. Muungwana kwa muungwana na mtumwa kwa mtumwa na mwanamke kwa

Page 58: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

58

www.firqatunnajia.com

mwanamke, na anayesamehewa na nduguye kwa lolote basi kufuatilizwa kwake kuwe kwa wema na kumlipa kwake iwe kwa wema." (02:178)

Amemthibitishia (Ta´ala) imani yule muuaji na muuliwaji kama ambavyo amethibitisha kuwa ni wandugu katika imani. Hakuna mgongano wa kutumia neno "dhambi" katika kitendo au yule mtendaji, kumwita yule mtendaji muislamu na kumpitishia zile hukumu za Kiislamu juu yake. Kitu kinachoweka hilo wazi, ni kile kisa cha ´Abdullaah bin Himaar ambaye alikuwa anakunywa pombe. Pindi alipoletwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Swahabah mmoja akasema:

"Allaah akulaani. Ni wingi uliyoje unaletwa!"

Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

"Usimlaani; hakika anampenda Allaah na Mtume Wake."

Dhambi hii haikumtoa katika Uislamu. Bali uhakika wa mambo ni kuwa

alimthibitishia imani, pamoja na kutumbukia katika dhambi hii kubwa. Kitu

kinachobainisha hilo, ni kuwa kufuru, shirki, dhuluma, dhambi na unafiki

vimegawanyika aina mbili katika Shari´ah:

Aina kubwa: Aina hii ni ile inayomtoa mtu katika Uislamu.

Aina ndogo: Aina hii inapingana na ukamilifu wa imani wa yule mwenye

nayo pasi na kumtoa katika Uislamu.

Mgawanyiko huu umebainishwa na Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Mmoja

katika wabingwa wa Ummah na mfasiri wa Qur-aan, Ibn ´Abbaas (Radhiya

Allaahu ´anhumaa), amesema kuwa kuna kufuru ndogo, dhuluma ndogo,

dhambi ndogo na unafiki mdogo. Allaah amemwita yule mwenye kuomba

badala Yake kwamba ni "kafiri", "mshirikina" na "dhalimu". Allaah (Ta´ala)

amesema:

د ربه سابه ع ا ا آخر ب رهان له به فإ ا إنه ي فلح الكافرون ومن يدع مع الل ه إل

Page 59: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

59

www.firqatunnajia.com

"Na yeyote yule anayeomba pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo, basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake - hakika hawafaulu makafiri." (23:117)

ا دا ا أدعو ر و أشرك به أ قل إ

"Sema: “Hakika mimi namuomba Mola wangu Pekee na wala simshirikishi na yeyote."" (72:20)

فإن ف علت فإنك إذاا من الظالمي فعك و يضرجك و تدع من دون الل ه ما ي

“Wala usiombe badala ya Allaah asiyekufaa na wala asiyekudhuru. Endapo utafanya hivo, basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu." (10:106)

ن ف كان من ا فسق عن أمر ربه إ إبلي

"Isipokuwa Ibliys alikuwa miongoni mwa majini akaasi amri ya Mola wake." (18:50)

Haya yote yanahusiana na kufuru kubwa, shirki kubwa, dhuluma kubwa na dhambi kubwa ambavyo haviwezi kukusanyika na imani. Allaah (Ta´ala) amesema:

ا أنزل الل ه فأول ئك هم الكافرون و كم من

"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri." (05:44)

ا أنزل الل ه فأول ئك هم الظالمون كم ومن

"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio

madhalimu." (05:45)

ا أنزل الل ه فأول ئك هم الفاسقون كم ومن

"Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio mafasiki." (05:47)

Page 60: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

60

www.firqatunnajia.com

وم نارااإن الذين ي ا يأكلون ب وسيصلون سعياا أكلون أموال اليتامى ظلماا إ

"Hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa dhulma hapana shaka kwamba wanakula katika matumbo yao moto na watauingia [Moto wa] Sa’iyraa." (04:10)

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Kumtukana muislamu ni dhambi na kumpiga vita ni kufuru."

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Mwenye kuapa kwa mwengine asiyekuwa Allaah amekufuru au

ameshirikisha."

Haya yanahusiana na kufuru ndogo, shirki ndogo, dhuluma ndogo na dhambi

ndogo ambavyo vinaweza kukusanyika na imani, kama ilivyokuja katika Qur-

aan, Sunnah na maafikiano ya Salaf. Mambo haya yanafanya imani kupungua

na kupingana na ukamilifu wake.

Page 61: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

61

www.firqatunnajia.com

08. ´Aqiydah sahihi juu ya Maswahabah wa Mtume wa Allaah

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Miongoni mwa ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kuwapenda

Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),

kujenga urafiki nao, kuwatakia radhi na kuwaombea msamaha na kuwasifia.

Allaah (Ta´ala) amesema:

سان رضي الل ه ع نصار والذين ات ب عوهم بإ اجرين وا ولون من الم ار والسابقون ا ن ا ا ت ري م جات م ورضوا عه وأعد ا أب اخالدين في لك الفوز العظيم دا ذ

"Na wale waliotangulia awali miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito - ni wenye kudumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa." (09:100)

Allaah (Ta´ala) amewaridhia waliotangulia awali pasi na kushurutisha wema.

Kuhusu wale waliokuja nyuma, hayuko radhi na wao endapo hawatowafuata

kwa wema. Amesema (Ta´ala):

رة لقد رضي الل ه عن المؤمي إ ت الش ذ ي بايعونك

"Kwa yakini Allaah Amewawia radhi waumini walipofungamana nawe ahadi ya utiifu chini ya mti." (48:18)

Yule ambaye Allaah ameridhika naye basi hatomkasirikia maishani. Imethibiti

katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

amesema:

"Hakuna yeyote aliyetoa kiapo cha usikivu na utiifu chini ya mti atayeingia

Motoni."

Allaah amewaelezea Muhaajiruun na kuwasifu ya kwamba ni wakweli.

Amesema (Ta´ala):

اجرين الذين أخرجوا صرون الل ه ورسوله للفقراء الم ا من الل ه ورضواناا وي م ي بت غون فض أول ئك هم الصادقون من ديارهم وأموا

Page 62: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

62

www.firqatunnajia.com

"Kwa ajili ya mafuqara Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [zikataifishwa] mali zao wanatafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake - hao ndio wakweli." (59:08)

Halafu Akawataja Answaar na kusema:

دون م و بجون من هاجر إلي م ان من ق بل م ولو كان م والذين ت ب وءوا الدار وا ا أوتوا وي ؤثرون على أنفس اجةا صدورهم ومن يوق شح ن فسه فأول ئك هم المفلحون خصاصة

"Na wale waliokuwa na makazi na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohajiri kwao na wala hawapati kuhisi choyo yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa, na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe wameshikwa na ufukara. Na yeyote anayeepushwa na ubakhili na tamaa ya uchu wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu." (59:09)

Kisha Akataja (Ta´ala) hali za waumini baada yao wenye kuwafuata

Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa

wema na kusema:

خوانا الذين سب قونا ب يم والذين جاءوا من ب عدهم ي قولون رب ا اغفر لا و عل ق لوبا غ للذين آموا رب ا إنك رءوف ر ان و ا

"Na wale waliokuja baada yao wanasema: “Mola wetu! Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo ya chuki kwa wale walioamini. Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu." (59:10)

م جمد رسول الل ه اء ب ي ا من ا والذين معه أشداء على الكفار ر ا ي بت غون فض دا سيماهم لل ه ورضواناات راهم ركعاا سود م من أثر السج م الت وراة وجوه لك م ل ب ذ فآزر فاست غلظ فاست وى على سوقه ي ع أ يل كزرع أخرج ش م ا وم ل

م مغفرةا وأجراا عظيماا الكفار الزجراع ليغيظ م ات م وعد الل ه الذين آموا وعملوا الصا

"Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na Radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu. Huo ni mfano wao katika Tawraat na mfano wao katika Injiyl kama mmea umetoa chipukizi lake, likautia nguvu kisha likawa nene, kisha likasimama

Page 63: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

63

www.firqatunnajia.com

sawasawa juu ya shina lake liwapendezeshe wakulima ili kuwakasirisha makafiri. Allaah Amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na ujira mkubwa." (48:29)

Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

"Yule ambaye moyoni mwake mna chuki dhidi ya mmoja katika Maswahabah

wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi anaingia ndani

ya Aayah:

ق والذين آموا وهاجروا وجاهدوا سبيل الل ه والذين آووا ونصروا أول ئك هم المؤمون م مغفرة ورزق كرم ا

"Na wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah na wale waliotoa makazi na wakanusuru - hao ndio waumini wa kweli. Watapata msamaha na riziki tukufu." (08:74)

Amesema (Ta´ala) juu ya Maswahabah akibainisha fadhila za wale

waliojitolea na kupigana kabla ya Ushindi - mkataba wa Hudaybiyah - juu ya

wale waliojitolea na kupigana baada ya Ushindi - lakini makundi yote mawili

yameahidiwa Pepo na Allaah:

كم من أنفق من ق أول ئك أعظم درجةا من الذين أنفقوا من ب عد وقات لوا بل الفتح وقاتل يستوي م س ا وك وعد الل ه ا والل ه ت عملون خبي

"Na mna nini hata hamtoi katika njia ya Allaah na hali urithi wa mbingu na ardhi ni wa Allaah Pekee. Hawi sawa miongoni mwenu aliyetoa kabla ya Ushindi na akapigana. Hao watapata daraja kuu kabisa kuliko wale waliotoa baada [ya ushindi] na wakapigana - na wote Allaah Amewaahidi Pepo. Na Allaah kwa yote myatendayo ni Mjuzi." (57:10)

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Sa´iyd al-Khudriy

(Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) amesema:

"Msiwatukane Maswahabah zangu."

Katika matamshi ya Muslim imekuja:

Page 64: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

64

www.firqatunnajia.com

"Msimtukane yeyote katika Maswahabah zangu. Lau atakuwepo mtu

atayetoa dhahabu mfano wa [mlima wa] Uhud, basi hautofikia Mudd wala

nusu ya mmoja wao."

Mudd ni robo ya Swaa´ [chini ya gramu mia sita] na nusu yake ni nusu ya

Mudd.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa ´Imraan bin Huswayn

(Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema:

"Watu bora ni karne yangu, kisha wataofuatia, kisha wataofuatia." ´Imraan

amesema: "Sijui alisema karne mbili au tatu baada ya karne yake." Halafu

baada ya hapo watakuja watu wataotoa ushuhuda pasi na kuombwa

kushuhudia, watafanya khiyana pasi na kuaminiwa, wataweka nadhiri pasi

na kutimiza na kutadhahiri kwao kuipenda dunia."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Anas (Radhiya Allaahu

´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya

Answaar:

"Alama ya imani ni kuwapenda Answaar. Alama ya unafiki ni kuwachukia

Answaar."

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa al-Baraa´ bin ´Aazib

(Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema kuhusu Answaar:

"Hakuna anayewapenda isipokuwa muumini tu na hakuna anayewachukia

isipokuwa mnafiki tu. Allaah anampenda yule mwenye kuwapenda na

Allaah anamchukia yule mwenye kuwachukia."

Muslim amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd al-Khudriy

(Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema:

"Hakuna mtu anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho anayewachukia

Answaar."

Page 65: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

65

www.firqatunnajia.com

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib

(Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) amesema kuhusu kisa cha Haatwib bin Abiy Balt´ah:

"Ameshuhudia [vita vya] Badr. Allaah aliwatazama watu wa Badr na

kusema: "Fanyeni mtakalo, hakika Nimekusameheni.""

Muslim amepokea kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anh)

ambaye amesema kuwa Umm Mubashshir alimsimulia ya kwamba alimsikia

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema kwa Hafswah:

"Hakuna yeyote katika wale waliokula kiapo cha usikivu na utiifu

atayeingia Motoni - Allaah akitaka."

Walikuwa watu zaidi ya 1400 na miongoni mwao alikuwa Abu Bakr, ´Umar,

´Uthmaan na ´Aliy.

Ahl-us-Sunnah wanaitakidi kuwa mbora wa Ummah huu baada ya Manabii

wake ni Abu Bakr as-Swiddiyq. Kisha ´Umar al-Faaruq. Haya ni kwa

maafikiano ya Maswahabah na Taabi´uun. Hakuna yeyote katika wao

aliyepingana na hili.

Kumepokelewa mapokezi tele kutoka kwa kiongozi wa Waumini ´Aliy bin

Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba amesema:

"Wabora wa Ummah huu baada ya Manabii wake ni Abu Bakr na ´Umar."

Ahl-us-Sunnah wanaonelea kuwa watatu ni ´Uthmaan na wanne ni ´Aliy bin

Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Page 66: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

66

www.firqatunnajia.com

09. ´Aqiydah sahihi juu ya watu wa nyumba ya kwa Mtume

(Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

Katika ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni pamoja na kuwapenda

watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutambua

fadhila na utukufu wao. Katika hali hii mtu anatakiwa kutendea kazi wasia

wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya Ghaadiyr Khumm.

Alimhimidi Allaah na akamsifu, akawaidhisha na kukumbusha. Kisha

akasema:

"Amma ba´d: Enyi watu! Hakika mimi si mwingine isipokuwa ni

mwanaadamu tu. Anakaribia mjumbe kutoka kwa Mola wangu kunijia

[kunichukua] na hapo itabidi niitikie. Nimekuachieni vitu viwili. Cha kwanza

ni Kitabu cha Allaah ambacho ndani yake mna uongofu na nuru. Hivyo basi

kichukueni Kitabu cha Allaah na shikamaneni nacho."

Akasisitiza juu ya Kitabu cha Allaah halafu akasema:

"Na familia yangu. Ninakukumbusheni juu ya Allaah kwa familia yangu.

Ninakukumbusheni juu ya Allaah kwa familia yangu. Ninakukumbusheni juu

ya Allaah kwa familia yangu."

Ibn Kathiyr amesema katika Tafsiyr yake:

"Hatuukatai wasia wa watu wa nyumba ya kwa Mtume na kuwatendea

wema, kuwaheshimu na kuwatukuza. Hakika wanatokamana na kizazi kisafi

na familia tukufu kabisa iliyopo katika uso wa ardhi kifakhari, kiukoo na

kinasabu. Hili khasa pale ambapo watakuwa ni wenye kufuata Sunnah ya

kinabii, sahihi na ilio wazi. Hali kama hii ndio waliokuwa nayo wahenga wao

kama al-´Abbaas na watoto wake na ´Aliy na familia yake na dhuriya yake -

Allaah awawie radhi wote."

Miongoni mwa watu wa familia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni

wakeze. Amesema (Ta´ala) kuhusu wao:

Page 67: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

67

www.firqatunnajia.com

اهلي و وق رن ب يوتكن و ت ب رجن ت ب رجج ا ة وآتي الزكاة وأطعن الل ه ورسوله ة ا وأقمن الص كم الرج ا يريد الل ه ليذهب ع إلى ب يوتكن من آيات الل ه ياا واذكرن ما ي ت ركم ت كمة أهل الب يت وي يفاا خبياا وا إن الل ه كان ل

"Na bakieni majumbani mwenu na wala msionyeshe mapambo uonyeshaji mapambo wa zama za ujahili. Na simamisheni swalah, na toeni zakaah na mtiini Allaah na Mtume Wake. Hakika Allaah Anataka Akuondosheeni uchafu enyi watu wa nyumba na Akutakaseni mtakaso barabara. Na dhukuruni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Ayaat za Allaah na Hikmah, hakika Allaah daima ni Mjuzi, Mwenye khabari." (33:33-34)

Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema katika Tafsiyr yake:

"Aayah hii ni dalili juu ya kwamba wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa

sallam) wanaingia katika familia yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa

sababu wao ndio sababu ya kuteremka kwa Aayah. Sababu ya kuteremka kwa

Aayah na kwamba inaingia ndani yake ni jambo lisilokuwa na tofauti juu

yake. Ima inaingia na kutumika hiyo tu, jambo ambalo ni maoni moja, au hiyo

na nyenginezo, jambo ambalo ndio maoni sahihi zaidi."

al-Bukhaariy amepokea kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh)

kuhusu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumuoa kwake Zaynab bint Jahsh

na humo kumetajwa ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia

ndani kwenye chumba cha ´Aaishah na kusema:

"Ah-ul-Bayt [watu wa nyumba yangu]! Swalah na salaam iwe juu yao!"

Ndipo akasema: "Swalah na salaam iwe juu yako!"

Yaliyotajwa vilevile kuhusiana na fadhila zao, ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

م بالمؤمي من أنفس ج أو م ال ات وأزواجه أم

"Nabii ana haki zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao na wake zake ni mama zao." (33:06)

Inahusiana na uzito, heshima, maadhimisho, utukufu na wema wa mama wa waumini. Hata hivyo haijuzu kuwa pamoja nao faragha. Ni jambo lenye

Page 68: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

68

www.firqatunnajia.com

maafikiano juu ya kwamba nafasi hii haihusiani na wasichana wao na dada zao.

Page 69: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

69

www.firqatunnajia.com

10. ´Aqiydah sahihi juu ya karama za mawalii

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaamini karama za mawalii ambazo Allaah

(Ta´ala) ametaka wafanye, jambo ambalo limetajwa katika Maandiko mengi.

Kwa mujibu wao walii ni yule mwenye kutekeleza maamrisho ya Kishari´ah

na akajiepusha na yale ambayo yamekatazwa kwa mujibu wa Shari´ah.

Amesema (Ta´ala) kuhusu mawalii:

م زنون الذين آموا وكانوا ي ت قون أ إن أولياء الل ه خوف علي و هم

"Tanabahi! Hakika vipenzi wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa wanamcha Allaah." (10:62-63)

Ili mtu awe sampuli hii ya mtu kunahitajika imani na uchaji Allaah.

Karama ni kitu chenye kwenda kinyume na mazowea ambacho Allaah

(Ta´ala) huwafanya wachaji Allaah na waja waumini wakifanye. Mambo hayo

yanawasaidia kufanya mambo ya kidini au ya kidunia. Lakini hata hivyo

karama za mawalii hazifikii ile daraja ya miujiza ya Manabii na Mitume.

Miongoni mwa karama za mawalii wa Allaah ni kile kisa cha watu wa

Pangoni, kisa cha Maryam (Radhiya Allaahu ´anhaa) pindi uchungu

ulipompeleka katika shina la mtende ambapo akaamrishwa na Allaah kutikisa

mashina yake na matunda yakawa yameanguka pembezoni mwake, kule

Allaah kumruzuku kwa njia ya kwamba alikuwa akipata matunda ya majira

ya baridi wakati wa joto na matunda ya majira ya joto wakati wa baridi, kisa

cha ´Aaswif, ambaye alikuwa ni mwandishi wa Sulaymaan, kisa cha mtu

ambaye Allaah alimfisha miaka mia moja halafu baada ya hapo akamuhuisha,

kisa cha Jurayj, kisa ch watu watatu katika wana wa Israaiyl ambao

walichukua hifadhi kwenye pango na jiwe likawa limeziba maingilio yao na

mfano wa visa kama hivyo ambavyo ni vyenye kujulikana kwa wanachuoni

na vimethibiti katika Qur-aan, Sunnah iliyothibiti au yaliypokelewa kutoka

kwa Salaf au waliokuja baada yao.

Page 70: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

70

www.firqatunnajia.com

Karama itaendelea kuwepo katika Ummah huu hadi Qiyaamah kisimame,

kwa kuwa sababu yake ni imani na uchaji Allaah na hivyo vitu viwili

vitaendelea kuwepo mpaka siku ya Qiyaamah.

Lakini ikiwa jambo lenye kwenda kinyume na mazowea linatoka kwa mtu,

hiyo haina maana kuwa ni dalili yenye kuonesha wema, imani na uchaji

Allaah wake. Katika hali hii ni lazima matendo yake kwanza yalinganishwe

na Qur-aan na Sunnah ili kuangalia kama yanaafikiana navyo na kama

anavifuata kidhahiri na kindani.

Page 71: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

71

www.firqatunnajia.com

11. ´Aqiydah sahihi juu ya watawala wa waislamu

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaitakidi kuwa Allaah (Ta´ala)

amewawajibishia waumini kuwatii watawala wao katika yote yasiyokuwa

maasi.

Wanaamini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)

iliyotajwa katika Hadiyth ya ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu

´anh):

"Sikiliza na utii katika kipindi chako kizito na chepesi, katika

unayoyapenda na unayoyachukia hata kama watatawalia juu yako mambo

ya kidunia pasi na kukupatia haki yako, hata kama watachukua mali yako

na kupiga mgongo wako, midhali haihusiani na maasi."

Wanaonelea kuwa ni haramu kuwafanyia uasi watawala, hata kama

watakuwa wakandamizaji na wenye kudhulumu, midhali hawajaona kufuru

ya wazi ambayo kwayo wana dalili kutoka kwa Allaah. Hayo ni kutokana na

yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

"Wabora wa viongozi wenu ni wale mnaowapenda na wao wanakupendeni

na wale mnaowaombea du´aa na wao wanakuombeeni du´aa. Waovu wa

viongozi wenu ni wale mnaowachukia na wao wanakuchukieni na

mnawalaani na wao wanakulaanini." Kukasemwa: "Ee Mtume wa Allaah!

Je, tusipambane nao kwa panga?" Akasema: "Hapana, maadamu

wanasimamisha swalah. Mtapoona kitu kutoka kwa watawala wenu

mnachokichukia, basi chukieni kitendo chake na wala msinyanyue mkono

kutoka katika utiifu."

Katika matamshi mengine imekuja:

"Yule aliye na mtawala juu yake na akaona anafanya kitu katika kumuasi

Allaah, basi na achukie kitendo kinachomuasi Allaah na wala asinyanyue

mkono kutoka katika utiifu." Ameipokea Muslim kutoka kwa ´Awf bin

Maalik (Radhiya Allaahu ´anh).

Page 72: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

72

www.firqatunnajia.com

Yule mwenye kutoka katika Mkusanyiko, basi Shari´ah itamuadhibu adhabu

kali duniani na Aakhirah kutegemea na ukubwa wa dhambi yake. Mwenye

kufa baada ya kutoka katika utiifu na akafarikiana na Mkusanyiko, basi

amekufa kifo cha kipindi cha kikafiri. Mtu asiulizie juu ya mtu mwenye

kufarikiana na Mkusanyiko kutokana na ukubwa wa dhambi yake. Mwenye

kufarikiana na Mkusanyiko basi hana hoja yoyote mbele ya Allaah (Ta´ala)

siku ya Qiyaamah. Yule mwenye kufarikiana na Mkusanyiko shaytwaan yuko

pamoja naye bega kwa bega. Mwenye kufarikiana na Mkusanyiko basi damu

yake ni halali.

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaonelea kuwa ni jambo zuri na lenye

kusifika kumuombea mtawala kwa Allaah juu ya mafanikio na usalama. Nayo

ni alama yenye kuonesha kuwa mtu ni katika Ahl-us-Sunnah, kama

alivyosema Imaam al-Barbahaariy katika kitabu "Sharh-us-Sunnah":

"Ukimuona mtu anaomba dhidi ya mtawala, basi tambue kuwa ni katika watu

wenye kufuata matamanio. Na ukimuona mtu anamuombea du´aa mtawala

juu ya mafanikio, basi tambua kuwa ni katika watu wa Sunnah - Allaah

akitaka."

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

"Lau mimi ningelikuwa na du´aa [yenye kuitikiwa] basi nisingelimuombea

mwengine asiyekuwa mfalme. Tumeamrishwa kuwaombea utengemavu na

hatukuamrishwa kuomba dhidi yao hata kama watakuwa ni wakandamizaji

na wenye kudhulumu. Ule ukandamizaji na dhuluma zao ni jambo

linawapata wao wenyewe na waislamu pia na kutengemaa kwao ni jambo

linawapata wao wenyewe na waislamu pia."

Imaam as-Swaabuuniy amesema katika "´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-

Hadiyth":

"Wanaonelea kuwaombea utengemavu, mafanikio na uongofu."

Page 73: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

73

www.firqatunnajia.com

Wanaona wale wakubwa wa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla

Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa ni wenye kuafikiana juu ya kwamba ni

haramu kuwatukana. Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

"Wakubwa wetu wa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) wametukataza [kwa kusema]: "Msiwatukane watawala

wenu, msiwafanyie ghushi na wala msiwachukie. Mcheni Allaah na kuweni

na subira, hakika mambo yako karibu."" Ameipokea Ibn Abiy ´Aaswim katika

"as-Sunnah" na wengineo.

Page 74: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

74

www.firqatunnajia.com

12. Msimamo sahihi juu ya mijadala katika dini

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ahh wanakataza mijadala na mizozo katika dini,

kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza hilo.

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu

´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

"Isomeni Qur-aan maadamu nyoyo zenu zimezunguka kwayo.

Mtapotofautiana, basi simameni kutoka kwayo."

Katika "al-Musnad" na "as-Sunan" ya Ibn Maajah - asli matamshi yake

yanapatikana katika "as-Swahiyh" ya Muslim kutoka kwa ´Abdullaah bin

´Amr - kumesimuliwa:

"Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka na wao wakijadiliana

juu ya Qadar. Uso wake ukageuka mwekundu kabisa kama mkomamanga.

Akasema: "Haya ndio mliyoamrishwa au mliumbwa kwa ajili ya haya?

Mnaigonganisha sehemu ya Qur-aan na nyingine. Haya ndio yaliwafanya

kuangamia nyumati zilizokuwa kabla yetu.""

Imepokelewa vilevile kuwa mijadala ni njia moja wapo ya adhabu ya Allaah

kwa Ummah. Katika "as-Sunan" ya at-Tirmidhiy na Ibn Maajah

kumepokelewa kutoka kwa Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ya

kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Hakuna watu waliopotea baada ya uongofu waliokuwemo isipokuwa

baada ya kuanza kujadili." Kisha akasoma:

ما ضربو لك إ جدا

"Hawakukupigia mfano huo isipokuwa tu kutaka kubisha." (43:58)

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

"Misingi ya Sunnah kwetu ni kushikamana yale waliyokuwemo Maswahabah

wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwaiga, kuacha Bid´ah na

Page 75: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

75

www.firqatunnajia.com

kila Bid´ah ni upotevu, kuacha magomvi na kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´ pamoja

na kuacha mizozo, mijadala na magomvi katika dini."

Yote haya yanazingatiwa kuwa ni mijadala ya batili, mijadala ya haki baada

ya kuwa haki imeshabainika, mijadala ambayo hoja zake hazitambuliki na

yule anayejadiliwa, mijadala juu ya zile Aayah zisizokuwa wazi au mijadala

pasi na kuwa na nia nzuri na mfano wa hayo.

Hata hivyo endapo mijadala itakuwa ni yenye kuhusiana na kuidhihirisha na

kuibainisha haki na ikawa ni yenye kubainishwa na mwanachuoni aliye na nia

nzuri na amelazimiana na adabu, basi inazingatiwa kuwa ni yenye kusifiwa.

Allaah (Ta´ala) amesema:

كمة والموعظة ا سبيل ربك با سن سة ادع إ هي أ م بال ن ضل عن سبيله وجاد وهو أعلم إن ربك هو أعلم تدين بالم

"Waite watu katika njia ya Mola wako kwa hikmah na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa njia bora zaidi. Hakika Mola wako Yeye Anamjua zaidi aliyepotea njia Yake Naye Anawajua zaidi walioongoka." (16:125)

سن هي أ ادلوا أهل الكتاب إ بال و

"Na wala msibishane na Ahl-ul-Kitaab isipokuwa kwa yale ambayo ni bora zaidi." (29:46)

ت من قالوا يا نوح ا تعدنا إن ك الصادقي قد جادلت ا فأك رت جدالا فأتا

"Wakasema: “Ee Nuuh! Kwa yakini umejadiliana nasi na umekithirisha majadiliano nasi, basi tuletee adhabu unayotutishia nayo ukiwa ni miongoni mwa wakweli."" (11:32)

Kadhalika Amesimulia (Ta´ala) juu ya mjadala wa Ibraahiym (´alayhis-

Swalaatu was-Salaam) na watu wake na Muusa (´alayhis-Swalaatu was-

Salaam) na Fir´awn. Katika Sunnah kumetajwa mjadala wa Muusa na Aadam

(´alayhimaas-Swalaatu was-Salaam) kama ambavyo vilevile kumetajwa

mijadala mingi kutoka kwa Salaf. Yote hii ni mijadala yenye kusifiwa midhali

Page 76: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

76

www.firqatunnajia.com

ndani yake ina elimu, nia nzuri, yenye kuafikiana na Shari´ah na adabu katika

kujadiliana.

Page 77: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

77

www.firqatunnajia.com

13. Matahadharisho ya kukaa na Ahl-ul-Ahwaa´

Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanatahadharisha vikali kabisa kukaa na Ahl-

ul-Ahwaa´ wal-Bid´ah, kwa sababu kukaa nao ni kwenda kinyume na

maamrisho ya Allaah. Isitoshe ni alama ya kuwapenda. Vilevile kunachelea

kwa yule mwenye kukaa nao akajisalimisha na upotevu wao na akawafuata

katika batili yao. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)

amesema:

"Bid´ah ambayo mtu anazingatiwa kwayo ni katika Ahl-ul-Ahwaa´ ni zile

zenye kujulikana kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah zinazoenda kinyume na

Qur-aan na Sunnah. Mfano wa Bid´ah hizo ni kama Bid´ah ya Khawaarij,

Raafidhwah, Qadariyyah na Murjia-ah."

Allaah (Ta´ala) amesema:

ديث غي وضوا م وضون آياتا فأعرض ع ت قع وإذا رأيت الذين سي ك الشيان ف د ب عد الذكرى مع القوم وإما ي الظالمي

"Na unapowaona wale wanaoziingilia Aayaat Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu." (06:68)

Ibn ´Abbaas amesema:

"Kila mwenye kuzua katika dini ameingia katika Aayah hii na kila mzushi

mpaka siku ya Qiyaamah."

Haya yamenukuliwa kutoka kwa al-Baghawiy katika Tafsiyr yake. Ibn Jariyr

at-Twabariy amesema:

"Katika Aayah hii kuna dalili ya wazi kabisa juu ya makatazo ya kukaa na

watu wa batili kwa sampuli zote za wazushi na watenda madhambi pindi

wanapoingilia batili yao."

Ibn ´Abbaas amesema:

Page 78: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

78

www.firqatunnajia.com

"Usiikae na Ahl-ul-Ahwaa´, kwa kuwa kukaa nao kunazigonjwesha nyoyo."

Page 79: al-Barjas

al-Mu´taqad as-Swahiyh

Shaykh ´Abdus-Salaam Barjas

79

www.firqatunnajia.com

14. Hitimisho ya kitabu

Mpaka hapa kwa himdi na mafanikio ya Allaah ndio mwisho wa kitabu "al-

Mu´taqad as-Swahiyh al-Waajib ´alaa kulli Muslim I´tiqaaduh". Ninamuomba

Allaah (Ta´ala) akijaalie kiwe kimefanywa kwa ajili ya Uso Wake Mtukufu,

chenye kuafikiana na Sunnah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi

wa sallam) na awanufaishe nacho waislamu wote kwa jumla.

Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, watu wa nyumbani

kwake watwaharifu, Maswahabah zake bora na wale watakaowafuata kwa

wema hadi siku ya Malipo.