1. 2. - parliament.go.tz · ulinzi na usalama kuanzia machi, 2018 hadi januari, 2020. katika...
TRANSCRIPT
1
HOTUBA YA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHESHIMIWA DKT.
HUSSEIN ALI MWINYI (MB.), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA
KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21
UTANGULIZI
1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba
Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na
Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2020/21.
2. Mheshimiwa Spika, kwanza napenda nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu,
mwingi wa rehema na fadhila kwa kuendelea kutujalia uzima na afya njema na kutuwezesha
kukutana kwa mara nyingine tena leo hapa Bungeni kwa shughuli hii muhimu. Vile vile, kwa
heshima na unyenyekevu mkubwa namshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuniteua na kuendelea
kuniamini kushika wadhifa huu katika kipindi cha Awamu ya Tano. Nawashukuru pia Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, na Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kwa uongozi wao makini na
maelekezo wanayonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara yangu.
3. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewe, Spika wa Bunge hili Mhe. Job Yustino
Ndugai (Mb.), Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.), pamoja na Waheshimiwa
Wenyeviti wa Bunge kwa kuliongoza Bunge la kumi na moja (11) kwa mafanikio makubwa.
Namuomba Mwenyezi Mungu azidi kuwapa maarifa, busara, hekima na nguvu ili muweze
kuendelea kuliongoza Bunge letu katika kutekeleza majukumu yake mazito.
4. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee kabisa napenda kumshukuru Mhe. Mussa
Azzan Zungu (Mb.), aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama kuanzia Machi, 2018 hadi Januari, 2020. Katika kipindi chote cha uongozi
wake aliiongoza Kamati kwa umakini na weledi.
5. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ambayo kwa sasa inaongozwa na Mhe. Salum
2
Mwinyi Rehani (Mb.), kwa kuchambua na kushauri juu ya kuboresha mapendekezo ya Makadirio
ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 ninayowasilisha leo hapa
bungeni. Wakati wote Kamati hii imekuwa mstari wa mbele katika kuishauri Serikali juu ya
umuhimu wa kuimarisha utendaji wa Vyombo vya Ulinzi vya nchi yetu. Serikali na Wizara kwa
ujumla imezingatia ushauri huo. Nawashukuru sana.
6. Mheshimiwa Spika, napenda nitumie fursa hii kumshukuru aliyekuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ninayoisimamia Dkt. Florens Martin Turuka ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa
Mujibu wa Sheria. Kwa niaba ya Wizara tunamshukuru sana kwa kuitumikia Wizara kwa ufanisi
na mafanikio makubwa. Ni imani yetu kuwa ataendeleza ushirikiano huo huko aliko kwa maslahi
ya Taifa. Pia, nampongeza Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, namtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu
yake mapya.
7. Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi kwa Mhe. George Boniface Simbachawene
(Mb.), kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mhe. Mussa Azzan
Zungu (Mb.), kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na
Mazingira. Sambamba na pongezi hizi, nawatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yao
muhimu ya kuwatumikia wananchi na Taifa kwa ujumla.
8. Mheshimiwa Spika, vile vile, naomba kumpongeza Kanali Joseph Peter Bakari kwa
kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Kijeshi Duniani ndani ya Baraza la Michezo
ya Majeshi Duniani (International Military Sports Council - CISM). Namtakia kila la kheri katika
utekelezaji wa majukumu ya Baraza hilo.
9. Mheshimiwa Spika, naungana na wenzangu waliotangulia kutoa salamu za pole kwako
Mhe. Spika, Waheshimwa Wabunge, familia na wananchi wote kwa kuondokewa na wapendwa
wetu waliokuwa Wabunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika nyakati tofauti. Mnamo
tarehe 15 Januari, 2020, Bunge lako Tukufu liliondokewa na Mhe. Rashid Ajali Akbar aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, tarehe 20 Aprili, 2020 Bunge liliondokewa na Mhe. Mch. Dkt.
Getrude Pangalile Rwakatare, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum na tarehe 29 Aprili, 2020
liliondokewa pia na Mhe. Richard Mganga Ndassa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumve. Vile
vile, kwa namna ya pekee natoa pole kwa Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu na kwako Mhe. Spika,
Wabunge na wananchi kwa kuondokewa na Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Kuteuliwa
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga, aliyefariki tarehe 01 Mei, 2020.
3
10. Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa natoa pole kwa Mhe. Rais na Amiri Jeshi
Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Maafisa, Askari, Watumishi wa Umma, Familia za Wanajeshi, kufuatia
vifo vya Kuruta 10 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania vilivyotokea tarehe 03 Februari,
2020 wakati wakiwa katika mafunzo ya Kijeshi huko Msata, Mkoani Pwani. Sambamba na hili,
natoa pole kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali Simon Sirro na kwa familia za Askari
watatu wa Jeshi la Polisi waliofariki tarehe 03 Februari, 2020 kwa ajali ya gari Mkoani Njombe.
Naomba Mwenyezi Mungu azilaze kwa amani roho za marehemu. Vile vile, natoa pole kwa
wananchi waliopata majanga na kuondokewa na ndugu, jamaa na marafiki kutokana na matukio
mbalimbali yaliyosababishwa na madhara ya mvua kubwa, ajali na magonjwa.
11. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi kwa mara nyingine sasa ninayo
heshima kubwa kusimama mbele ya Bunge lako tukufu kwa lengo la kuwasilisha Mpango na
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa
Fedha 2020/21. Kabla sijafanya hivyo, naomba nielezee kwa kifupi Dira, Dhima na Malengo ya
Wizara.
DIRA, DHIMA NA MALENGO YA WIZARA
12. Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ya Ulinzi na JKT ni kuendelea kuwa Taasisi iliyotukuka
ya kulinda na kudumisha amani na usalama wa Taifa letu. Vile vile, Dhima ya Wizara ni
kuendelea kulinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya adui wa aina yoyote kutoka ndani
na nje ya nchi kwa kuhakikisha kuwa mamlaka na maslahi mapana ya nchi yetu yanakuwa
salama.
13. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha Dira na Dhima, Malengo ya Wizara yameendelea
kuwa yafuatayo:
(a) Kuwa na Jeshi dogo lenye wataalam, zana na vifaa vya kisasa;
(b) Kuendelea kuwajengea vijana wa kitanzania ukakamavu, maadili mema, utaifa, moyo
wa uzalendo, na uwezo wa kujitegemea;
(c) Kujenga uwezo katika tafiti mbalimbali za uhawilishaji wa teknolojia kwa matumizi ya
kijeshi na kiraia;
(d) Kuimarisha Jeshi la Akiba;
4
(e) Kusaidia Mamlaka za Kiraia katika kukabiliana na athari za majanga na matukio
yanayoweza kuhatarisha maisha, amani na utulivu nchini; na
(f) Kudumisha amani na usalama kwa kushirikiana na nchi nyingine duniani.
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BUNGE NA USHAURI WA KAMATI YA KUDUMU YA
BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA
14. Mheshimiwa Spika, wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama ilipokaa na kujadili Makadirio ya Mapato, Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 ilitoa maoni, ushauri na maelekezo kwa Wizara
yaliyolenga kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumu yake. Napenda kuliarifu Bunge lako
Tukufu kuwa maoni, ushauri na maelekezo yaliyotolewa yamefanyiwa kazi na hoja mbalimbali
zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa mjadala huo pia zimezingatiwa wakati wa
kuandaa na kukamilisha Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21 ninayowasilisha leo hapa
Bungeni.
UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 2015-2020 NA
MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MIAKA MITANO (2016/17 – 2020/21)
15. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020, sambamba na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) na majukumu mengine ya Wizara. Maelekezo ya Ilani
kwa Wizara yameainishwa bayana kwenye Ibara ya 146 katika vifungu vifuatavyo, naomba
ninukuu:
(i). “Kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea raslimali watu na
raslimali fedha kwa kadri uchumi utakavyoruhusu;
(ii). Kuendelea kuboresha maslahi ya watendaji katika vyombo vya Ulinzi na Usalama;
(iii). Kuendelea kuweka mazingira mazuri yanayoliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa
kuimarisha mafunzo kwa vijana wanaojiunga kwa hiari na wale wanaojiunga kwa
Mujibu wa Sheria;
(iv). Kuendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU) katika
shughuli za Ulinzi wa Amani kwenye nchi mbalimbali duniani ili majeshi yetu
yaendelee kupata uzoefu na mbinu za kisasa za ulinzi wa amani;
5
(v). Kuendeleza na kuimarisha mpango wa ulinzi shirikishi na kuwashirikisha wadau
mbalimbali nchini kutoa elimu kwa umma dhidi ya imani potofu zinazosababisha
mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Aidha, hatua kali na
za haraka za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kujihusisha na uhalifu
wa aina hii, ujambazi na vitendo vyenye mwelekeo wa ugaidi; na
(vi). Kuendelea kushirikiana na Mataifa mengine na Asasi za Kimataifa katika
kupambana na makosa yanayovuka mipaka (cross border crimes) hasa ugaidi,
uharamia, utakatishaji wa fedha (Money Laundering), biashara haramu ya madawa
ya kulevya na usafirishaji wa binadamu”.
16. Mheshimiwa Spika, napenda kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Wizara imeendelea
kutekeleza maelekezo ya Ilani kwa ufanisi kama ilivyoonyeshwa katika Kiambatisho Na. 1
HALI YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA YA NCHI
17. Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina mipaka ya nchi kavu na kwenye maji. Kwa upande wa
nchi kavu inapakana na nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Zambia, Malawi, Msumbiji na upande wa kwenye maji hususan bahari ya Hindi inapakana
na nchi za Comoro na Shelisheli.
18. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, hali ya Ulinzi na Usalama wa
mipaka yetu kwa ujumla imeendelea kuwa shwari na hapakuwa na matukio ya uhasama
yaliyoripotiwa baina ya nchi yetu na nchi tunazopakana nazo. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), limeendelea kujizatiti ipasavyo kudhibiti ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi
yetu. Hata hivyo, zipo changamoto chache kwenye baadhi ya maeneo ya mipaka ya nchi
zinazohitaji kutatuliwa ili udhibiti wa mipaka yetu uzidi kuimarika na kuimarisha usalama wa nchi
yetu.
19. Mheshimiwa Spika, miongoni mwa changamoto hizo ni uharibifu wa alama za mipaka kwa
baadhi ya maeneo ya mipaka. Aidha, kuendelea kuwepo kwa migogoro na viashiria vya
machafuko ya ndani katika baadhi ya nchi tunazopakana nazo imekuwa sababu mojawapo
inayochangia wakimbizi na wahalifu kuingia nchini. Hata hivyo, juhudi zinaendelea kufanyika
kuhakikisha alama za kudumu za mipaka zinawekwa katika maeneo ya Taifa letu.
20. Mheshimiwa Spika, changamoto nyingine ni wafugaji kutoka baadhi ya nchi tunazopakana
nazo kuendelea kuingiza mifugo yao ndani ya nchi yetu. Mfano, katika Ranchi ya Taifa ya Misenyi
6
iliyopo Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera ambapo wafugaji kutoka Rwanda na Uganda huingiza
mifugo kutafuta malisho na maji. Vile vile, nchi yetu imeendelea kukumbwa na tatizo la wahamiaji
haramu kutoka nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda na
usafirishaji haramu wa binadamu kutoka nchi za Ethiopia, Eritrea na Somalia. Baadhi ya
wahamiaji haramu wamekuwa wakijihusisha na uhalifu wa aina mbalimbali. Hata hivyo, Serikali
imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa mujibu wa sheria ili kudhibiti hali hiyo. Mheshimiwa
Spika naomba kutoa rai kwa Waheshimiwa Wabunge na viongozi waendelee kuwaelimisha
wananchi hususan maeneo ya mipakani kutoa taarifa kuhusu wahamiaji haramu watakao onekana
katika maeneo yao.
21. Mheshimiwa Spika, sambamba na hayo, kama ilivyo hapa nchini na duniani kote kwa
ujumla na nchi jirani tunazopakana nazo pia zimekumbwa na janga la ugonjwa wa homa kali ya
mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Hata hivyo, Serikali kupitia vyombo
vyake vya Ulinzi na Usalama inaendelea kuchukua hatua madhubuti kuimarisha ulinzi wa mipaka.
Mpaka wa Mashariki
22. Mheshimiwa Spika, mpaka wa Mashariki una urefu wa kilomita 1,424 ambapo Tanzania
inapakana na nchi za Kenya, Visiwa vya Shelisheli, Comoro na Msumbiji. Hali ya Ulinzi na
Usalama katika mpaka huu ni shwari. Changamoto zilizopo ni pamoja na; uvuvi haramu katika
Bahari ya Hindi, biashara za magendo na kutumika kama mapitio ya wahamiaji haramu,
usafirishaji wa madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu. JWTZ kwa kushirikiana na
Vyombo vingine vya Usalama linaendelea kuimarisha Ulinzi na Usalama ili kukabiliana na
changamoto hizo kwa kufanya doria za mara kwa mara. Kutokana na hatua hizo matukio
hayo yameendelea kupungua.
Mpaka wa Kaskazini
23. Mheshimiwa Spika, mpaka huu una urefu wa kilomita 1,281.2 ambapo Tanzania
inapakana na nchi za Kenya na Uganda. Hali ya usalama katika mpaka huu kwa ujumla ni shwari.
Hata hivyo, ipo changamoto ya baadhi ya wavuvi wa Tanzania kukamatwa na Vyombo vya Ulinzi
na Usalama vya nchi jirani. Mfano, tarehe 17 Machi, 2020 wavuvi 73 wakiwa na boti 5
walikamatwa katika Kisiwa cha Rasi Jimbo eneo la Bazo katika Bahari ya Hindi kwa tuhuma za
kufanya uvuvi kwenye eneo la Kenya. Kufuatia juhudi za Kidiplomasia kati ya Serikali ya
Tanzania na Kenya wavuvi hao waliachiwa huru tarehe 18 Machi, 2020 baada ya kulipa faini.
7
24. Mheshimiwa Spika, aidha, katika mpaka huu eneo la nchi kavu lina vipenyo vingi
vinavyoshawishi uwepo wa biashara za magendo, uhamiaji haramu na uhalifu. Vile vile,
mwingiliano wa wakazi pamoja na raia wa kigeni wa maeneo ya vijiji vya Mkwaja Kipumbwi
(Pangani) na vijiji vya Moa na Jasini (Mkinga) mkoani Tanga unahatarisha usalama wa nchi.
JWTZ limeendelea kuimarisha Ulinzi na Usalama katika maeneo hayo kwa kufanya doria na
kuanzisha Viteule vya ulinzi.
25. Mheshimiwa Spika, katika mpaka wa Tanzania na Uganda kuna matatizo ya kuharibiwa
alama za mipaka (Boundary Pillars - BP) na ujenzi holela unaofanywa na baadhi ya watu waishio
maeneo ya mipakani kwa lengo la kujipatia ardhi kwa ajili ya kilimo, malisho na makazi. Aidha,
matatizo ya mpaka kati ya Tanzania na Uganda yanaendelea kutafutiwa ufumbuzi.
Mpaka wa Magharibi
26. Mheshimiwa Spika, mpaka huu una urefu wa kilomita 1,220 ambapo Tanzania inapakana
na nchi za Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hali ya Ulinzi na Usalama
katika mpaka huu ni shwari. Hata hivyo, yamekuwepo matukio ya uhalifu yakiwemo mauaji
yaliyofanywa na makundi ya waasi ya Allied Democratic Forces (ADF), Democratic Forces for
Liberation of Rwanda (FDLR), The Republican Forces of Burundi (FOREBU), National Liberation
Forces na MAIMAI. Pia, kumekuwepo na matukio ya ujenzi wa makazi na kilimo ndani ya eneo la
mkuza, ambalo linapaswa kuwa wazi kulingana na makubaliano kati ya nchi na nchi. Pamoja na
kuwepo hali hiyo JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama limeendelea kufuatilia
kwa karibu hali ya usalama katika nchi hizo.
Mpaka wa Kusini
27. Mheshimiwa Spika, mpaka huu una urefu wa kilomita 1,536 ambapo Tanzania inapakana
na nchi za Msumbiji, Malawi na Zambia. Hali ya Ulinzi na Usalama katika mpaka huu kwa ujumla
ni shwari. Hata hivyo, usalama wa mpaka huu unatishiwa na kundi la kigaidi la “Ansar Al Sunnah
Wa Jamaah (AASWJ)” katika mpaka wa Msumbiji ambalo linaendelea kufanya uhalifu nchini
Msumbiji katika Jimbo la Cabo Delgado. Eneo lenye mgogoro lipo jirani na mpaka wa nchi yetu
(Mkoa wa Mtwara). Katika hatua ya kuimarisha ulinzi wa mpaka huu, mwezi Machi, 2020, Serikali
ilipeleka vikundi vya ulinzi katika maeneo ya Msimbati na Sindano, Mkoa wa Mtwara na Chiwindi
katika Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
28. Mheshimiwa Spika, hali ya usalama wa mpaka wa Tanzania na Malawi imeendelea kuwa
shwari kwani hakuna tishio la wazi dhidi ya nchi yetu. Changamoto ya mpaka katika Ziwa Nyasa
8
inaendelea kufanyiwa kazi. Serikali yetu kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki inaendelea kutumia njia za kidiplomasia ili kulipatia suala hili ufumbuzi wa kudumu,
ambapo imekubalika kuwa pande husika zisijishughulishe na utafiti wa kiuchumi katika eneo
lenye mgogoro.
MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2019/20
Ukusanyaji wa Maduhuli
29. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara ilikadiria kukusanya mapato
ya jumla ya Shilingi 81,104,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu kama ifuatavyo:Fungu 38
– NGOME Shilingi 20,001,000.00, Fungu 39 - JKT Shilingi 59,903,000.00 na Fungu 57 - Wizara
Shilingi 1,200,000.00.
30. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2020 Wizara ilifanikiwa kukusanya
maduhuli ya jumla ya Shilingi 67,153,000.00 sawa na asilimia 82.80 ya makadirio. Kwa upande
wa Fungu 38 – NGOME lilikusanya Shilingi 11,500,000.00 ambazo zimetokana na mauzo ya
nyaraka za zabuni na kamisheni zinazotokana na JWTZ kuwa wakala wa ukusanyaji wa makato
ya bima zinazokatwa kwa Wanajeshi kutoka makampuni mbalimbali ya bima. Fungu 39 – JKT
lilikusanya Shilingi 55,653,000.00 zilizotokana na mauzo ya nyaraka za zabuni na mauzo ya
mazao ya kilimo ikiwemo mboga mboga na matunda na Fungu 57 – Wizara, halikuweza
kukusanya maduhuli kwa kipindi husika kwa kuwa mapato iliyoyategemea kutokana na pango la
kantini kutopatikana kufuatia kufungwa kwa kantini iliyokuwepo Dar es Salaam baada ya
watumishi kuhamishiwa Dodoma. Mchanganuo wa maduhuli kwa kila Fungu umeoneshwa
kwenye Jedwali Namba. 1
Jedwali Na 1: Makadirio ya Mapato na Makusanyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/20
Fungu Makadirio ya Mapato 2019/20
Makusanyo Julai 2019 hadi Machi, 2020
Makusanyo (%)
38 – NGOME 20,001,000.00 11,500,000.00 57.00
39 – JKT 59,903,000.00 55,653,000.00 92.90
57 – Wizara 1,200,000.00 0 -
Jumla 81,104,000.00 67,153,000.00 82.80
Matumizi ya Kawaida
31. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara ya Ulinzi na Jeshi
la Kujenga Taifa iliidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,854,037,343,000.00 kwa ajili ya matumizi ya
9
kawaida na maendeleo katika mafungu yake matatu. Kati ya fedha hizo,
Shilingi 1,726,037,343,000.00 zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, na
Shilingi 128,000,000,000.00 zilitengwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Mchanganuo wa
bajeti kwa kila fungu umeoneshwa katika Jedwali Na. 2.
Jedwali Na. 2 Mchanganuo wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2019/20 kwa Fungu
Fungu Matumizi ya Kawaida (TZS)
Matumizi ya Maendeleo (TZS)
Jumla (TZS)
38-NGOME 1,406,726,908,000.00 6,000,000,000.00 1,412,726,908,000.00
39-JKT 300,035,425,000.00 2,000,000,000.00 302,035,425,000.00
57-Wizara 19,275,010,000.00 120,000,000,000.00 139,275,010,000.00
Jumla 1,726,037,343,000.00 128,000,000,000.00 1,854,037,343,000.00
32. Mheshimiwa Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, hadi kufikia mwezi Machi,
2020 Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 1,487,607,866,819.10 sawa na asilimia 80.24 ya
bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,381,414,181,653.84 ni kwa ajili ya matumizi ya
kawaida na Shilingi 106,193,685,165.26 ni kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo.
Mchanganuo wa fedha zilizopokelewa kwa mafungu yote matatu umeoneshwa katika
Kiambatisho Na. 2.
33. Mheshimiwa Spika, fedha za matumizi ya kawaida kiasi cha
Shilingi 1,381,414,181,653.84 zimetumika kulipa mishahara na posho mbalimbali kwa Maafisa,
Askari, Watumishi wa Umma, Vijana wa Mujibu wa Sheria na wa Kujitolea. Aidha, fedha hizo
zimetumika pia kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi, shughuli za kijeshi na kiulinzi ikiwemo mazoezi,
mafunzo na operesheni. Vile vile, sehemu ya fedha hizo zimetumika kugharamia huduma ya afya
kwa Wanajeshi, kuwasafirisha Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma waliostaafu kuanzia
mwezi Juni, 2018. Pia, fedha hizo zilitumika kugharamia Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa
Tanzania Bara, kulipa madeni ya huduma ya simu ya TTCL, wazabuni, Maafisa, Askari na
Watumishi wa Umma.
34. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa fedha za maendeleo, hadi kufikia mwezi Machi, 2020
Wizara imepokea jumla ya Shilingi 106,193,685,165.26 sawa na asilimia 83.00 ya fedha
zilizoidhinishwa. Fedha hizo zimetumika katika kuliimarisha Jeshi kwa ununuzi wa zana na vifaa,
kujenga miundombinu muhimu ya Jeshi, ukarabati wa zana na miundombinu ya Jeshi,
kugharamia ukamilishwaji wa uundaji wa magari mawili ya zimamoto na kugharamia uwekaji wa
umeme kwenye Minara ya Mawasiliano Salama Jeshini kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati
10
Vijijini (Rural Energy Agency – REA). Vile vile, Wizara imefanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya
maendeleo inayotekelezwa na Wizara na Taasisi zake.
35. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, upimaji na uhakiki wa maeneo
yaliyotwaliwa na Jeshi ambayo yanatakiwa kulipwa fidia umeendelea kufanyika. Aidha, usuluhishi
wa migogoro unaendelea kufanyika katika maeneo ya Chita - Morogoro, Nachingwea - Lindi,
Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) - Arusha, Kunduchi (KTC) na Kimbiji– Dar es
Salaam. Vile vile, Wizara imefanikiwa kupata Hati Miliki za maeneo mawili ya Jeshi ambayo ni
Msasani Beach Club (Dar es Salaam) na Tarime Mjini (Mara). Pia, uthamini umefanyika katika
maeneo ya Kigongo Feri na Ilemela - Mwanza, Nyamisangura - Mara na Kaboya – Kagera.
Maelezo ya Matumizi ya Fedha za Kawaida
36. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara imefanikiwa kutekeleza
shughuli mbalimbali kwa kutumia fedha za matumzi ya kawaida kama ifuatavyo:-
(a) Mafunzo na Mazoezi ya Kijeshi
37. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya kozi
za kijeshi katika shule na vyuo vya kijeshi ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwapatia Wanajeshi
mafunzo ya awali na kuwaendeleza katika taaluma mbalimbali na uongozi.
38. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika suala la kuwajengea weledi Maafisa na Askari
wetu limeendelea kupewa uzito mkubwa ambapo yamefanyika pia mazoezi mbalimbali ya kitaifa
na ya kimataifa yafuatayo: SHARED ACCORD; Zoezi hili lilifanyika nchini Rwanda Agosti, 2019,
USHIRIKIANO IMARA 2019; Zoezi hili la kituo cha uamrishaji (Command Post Exercise)
lilifanyika nchini Uganda Novemba, 2019; na maandalizi ya zoezi la BEACH LANDING
OPERATION yaliyofanyika Bagamoyo, Mapinga kuanzia tarehe 22 Desemba, 2019 hadi 16
Januari, 2020.
(b) Mafunzo ya Jeshi la Akiba
39. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania limetoa mafunzo kwa Jeshi la Akiba kwa wananchi katika ngazi ya awali. Mafunzo hayo
yalijumuisha wananchi kutoka katika mikoa yote ya Tanzania.
(c) Huduma za Afya na Tiba
40. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutoa huduma za matibabu kwa Maafisa, Askari,
Vijana wa JKT, Watumishi wa Umma, familia zao na wananchi kwa ujumla. Aidha, imeendelea
11
kuboresha huduma za afya na tiba kwa kununua dawa na vifaa tiba ili kukidhi mahitaji ya Hospitali
Kuu ya Jeshi Lugalo, Hospitali za Kanda na Vituo vya Tiba Vikosini, ununuzi wa mashine za
kusafishia figo na utoaji wa huduma ya usafishaji wa figo. Vile vile, JWTZ limejipanga kusaidia
Mamlaka za Kiraia katika kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na
virusi vya Corona (COVID-19).
(d) Ushirikiano wa Kiulinzi na Kijeshi na Nchi Nyingine
41. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeendelea kushirikiana na
nchi mbalimbali katika masuala ya kiulinzi na kiusalama katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya
maeneo hayo ni mafunzo, misaada ya kitaalam, vifaa, zana na mitambo. Mpaka sasa JWTZ
linashirikiana na nchi za Jumuiya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) katika mafunzo na ubadilishanaji wa wataalam. Aidha, JWTZ linapata
msaada wa mafunzo kwa Maafisa na Askari kutoka nchi zifuatazo: China, Misri, Marekani,
Ujerumani, India, Urusi, Uingereza, Bangladesh, Morocco, Canada, Uholanzi, Indonesia na
Jamaica.
42. Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali ya Jamhuri ya
Watu wa China kupitia Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) ilitoa msaada wa magari idadi
arobaini kwa ajili ya Makamanda wa JWTZ pamoja na ujenzi wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi awamu
ya pili. Aidha, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali ya Ujerumani kupitia kikundi cha
Germany Armed Forces Technical Adivisory Group (GAFTAG) imetoa msaada wa ujenzi wa
karakana ya matengenezo ya magari, ujenzi wa Hospitali Kuu ya Kanda Arusha, Ujenzi wa
mahanga ya Maafisa na Askari katika Chuo cha Ulinzi wa Amani Kunduchi Dar es Salaam na
italijengea Jeshi Hospitali Kuu ya Rufaa ( Level Four Hospital) Jijini Dodoma.
43. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) inaendesha mafunzo
ambapo mpaka sasa inashirikiana na nchi zifuatazo katika mpango wa ubadilishanaji wa washiriki
wa kozi hiyo kwa lengo la kubadilishana uzoefu. Baadhi ya nchi hizo ni China, Zimbabwe, Afrika
Kusini, Kenya, Misri, Nigeria, Rwanda, Malawi, Zambia, Namibia, Botswana, Burundi na
Bangladesh.
(e) Ushiriki wa JWTZ katika shughuli za Ulinzi wa Amani
44. Mheshimiwa Spika, JWTZ limeendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa, Umoja wa
Afrika na Jumuiya za Kikanda katika operesheni za ulinzi wa amani katika nchi mbalimbali zenye
12
migogoro kwa kupeleka vikosi, Waangalizi wa Kijeshi, Wanadhimu na Makamanda. Mpaka sasa
JWTZ lina Vikosi vya ulinzi wa Amani katika nchi zifuatazo: Lebanon (UNIFIL), Sudan (UNAMID),
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO Force Intervention Brigade – FIB) na Jamhuri
ya Afrika ya Kati (MINUSCA) . Aidha, Jeshi lina Maafisa Wanadhimu, Waangalizi wa Kijeshi, na
Makamanda kwenye operesheni za ulinzi wa amani nchini Lebanon, Sudan, Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
(f) Ushirikiano na Mamlaka za Kiraia Katika Shughuli Mbalimbali za Kitaifa
45. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania limeendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika shughuli mbalimbali za
maendeleo na huduma za kijamii. Maeneo mbalimbali ambayo JWTZ limeshirikiana na Mamlaka
za Kiraia ni: utoaji wa huduma za afya na tiba kwa wananchi ambapo takwimu zilizopo
zinaonyesha kwamba asilimia 70 ya wanaopata huduma katika Hospitali za Jeshi ni raia;
usafirishaji wa korosho kutoka kwenye maghala kupeleka bandarini kwa ajili ya kusafirisha nje ya
nchi; usafirishaji wa vitabu vya kiada na ziada kwenda mikoa mbalimbali nchini; ushiriki katika
kuboresha huduma katika Taasisi za Serikali; kuhamisha mizigo ya wizara mbalimbali kuja Makao
Makuu ya Serikali Dodoma, kusaidia ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu na majengo
mbalimbali ya Serikali, na kuondoa miti katika eneo la mradi wa Bwawa la Umeme Rufiji (Julius
Nyerere Hydro Power Project).
46. Mheshimiwa Spika, kupitia Shirika la Mzinga, Wizara imeendelea kusimamia zana na
silaha zinazomilikiwa na mashirika mbalimbali yanayoingiza meli katika bandari zetu ili kuzuia
matumizi mabaya ya silaha hizo. Jukumu hilo limekuwa likienda sambamba na utunzaji wa silaha
zinazomilikiwa na meli kutoka nje ya nchi mara tu zinapotia nanga kwenye bandari za nchi yetu.
(g) Maeneo mengine ya utekelezaji
47. Mheshimiwa Spika, pamoja na majukumu ya msingi, Wizara imeweza kutekeleza agizo la
Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu la Wizara kuhamia rasmi Dodoma ambapo Makao Makuu
ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) yalihamia tarehe 08 Novemba, 2019.
48. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JWTZ imewezesha Timu za Jeshi kushiriki Michezo ya
Majeshi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) 2019, ambapo mashindano yalifanyika
13
mwezi Agosti, 2019 nchini Kenya na Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (International Military
Sports Council - CISM) 2019 ambapo mashindano yalifanyika mwezi Oktoba, 2019 nchini China.
(h) Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Vijana
49. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara kupitia Jeshi la
Kujenga Taifa imeendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, stadi za kazi,
kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2019 hadi Machi, 2020
jumla ya vijana 20,413 wa Mujibu wa Sheria “Operesheni Makao Makuu Dodoma” walipatiwa
mafunzo kwenye Kambi mbalimbali za Jeshi la Kujenga Taifa. Kati ya vijana hao 15,712 ni wa
kiume na 4,701 ni wa kike. Kadhalika, vijana wapya wa kujitolea “Operesheni Makao Makuu
Dodoma” wapatao 11,099 wamejiunga na mafunzo ya JKT, ambapo kati yao wa kiume ni 7,761
na wa kike ni 3,338. Vile vile, Ujenzi na Ukarabati wa Kambi za JKT umewezesha kuongezeka
kwa vijana wanaoandikishwa kujiunga na mafunzo ya Mujibu wa Sheria na wa kujitolea.
(i) Mkakati wa JKT Kujitosheleza kwa Chakula
50. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia JKT imeandaa mkakati wa kujitosheleza kwa chakula ili
kuipunguzia Serikali gharama za kulisha vijana wanaohudhuria mafunzo ya JKT. Katika mwaka
2019/20 Jeshi la Kujenga Taifa limeanza kutekeleza mkakati huo kwa kuzalisha mazao ya
kimkakati ambayo ni mahindi, mpunga, maharage, ufuta na alizeti. Uzalishaji wa mazao hayo
unafanywa kupitia mashamba ambayo yako chini ya usimamizi wa Makamanda Vikosi. Jumla ya
ekari 8,417 zimelimwa msimu huu katika kambi mbalimbali za JKT. Kati ya ekari hizo, ekari 2,200
ni za kimkakati ambapo, mahindi ni ekari 1000, mpunga ni ekari 1000 na maharage ni ekari 200.
Ekari hizo zimelimwa katika vikosi vya Chita-Morogoro na Milundikwa-Rukwa. Matarajio ya
mavuno katika ekari hizo ni kupata tani 1,800 za mpunga na mahindi, na tani 120 za maharage.
(j) Mapambano Dhidi ya Magonjwa Ambukizi na Yasiyoambukiza
51. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza na kusimamia mikakati ya kupambana
na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa kama
vile kisukari, shinikizo la damu, n.k. Aidha, elimu imekuwa ikitolewa katika vituo na hospitali zenye
huduma ya mama na mtoto (Reproductive and Child Health) kwa lengo la kutokomeza
maambukizi ya mama kwa mtoto, kushiriki mafunzo kwa wataalamu mbalimbali wa tiba na kutoa
ushauri nasaha kwa walioambukizwa na kutoa elimu ya kujikinga ili kuzuia maambukizi mapya.
Vile vile, Wizara inaendelea kutoa elimu kwa Watumishi kuhusu ugonjwa wa homa kali ya mapafu
unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) na namna ya kujikinga.
14
52. Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, kwa wale wenye Virusi vya UKIMWI wamekuwa
wakipatiwa dawa za kupunguza makali ya Virusi (ARV’s) bure katika vituo vya huduma na
matibabu (Care and Treatment Centres) vilivyo katika Hospitali Kuu za Kanda. Kwa upande wa
magonjwa yasiyoambukizwa jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika ikiwemo kutoa elimu ya afya
ili kupunguza magonjwa hayo, kupima afya mara kwa mara, kushauri Maafisa, Askari na
Watumishi wa Umma kuacha uvutaji wa sigara, unywaji pombe uliopitiliza na kufanya mazoezi ya
mwili na michezo.
(k) Utawala Bora
53. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza dhana ya Utawala Bora katika maeneo
ya kazi kwa kushirikisha watumishi wake kupitia vikao mbalimbali kama vile Baraza la
Wafanyakazi, Kamati ya Ukaguzi, Kamati ya Maadili, Bodi ya Manunuzi na Kamati ya Ajira.
Wizara pia imeendelea kuimarisha jitihada za kupambana na rushwa. Kwa upande wa
mapambano dhidi ya rushwa, taarifa za kila robo mwaka zimekuwa zikiandaliwa na kuwasilishwa
kwenye mamlaka husika. Aidha, Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wameendelea
kuhimizwa kuzingatia sheria, kanuni na maadili ya utendaji kazi bila kusahau uzalendo na weledi
katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
(l) Utunzaji wa Mazingira
54. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa shughuli za utunzaji wa mazingira katika Mwaka wa
Fedha 2019/20, baadhi ya vikosi, shule na vyuo vya kijeshi vimeanza kutumia nishati ya gesi
badala ya kutumia kuni na mkaa. Aidha, Jeshi limefanya tathmini ya usambazaji wa mabomba ya
gesi ya asili ili kuviwezesha vikosi vyote vinavyopitiwa na bomba la gesi kutumia nishati hiyo.
55. Mheshimiwa Spika, Wizara inamiliki maeneo mengi na makubwa yenye miti ya asili
ambayo hutunzwa kwa kufanya doria mbalimbali, hivyo kufanya maeneo hayo yasivamiwe kwa
shughuli za kijamii, mfano eneo la Pongwe Msungura lililopo Msata, Mkoa wa Pwani na
Ngerengere lililopo Morogoro. Kwa ujumla maeneo yote ya Jeshi yana zuio la ukataji miti na
kuchoma mkaa.
56. Mheshimiwa Spika, Mashirika yaliyo chini ya Wizara, Tanzania Automotive Technology
Centre (TATC) - NYUMBU na MZINGA yanafanya uzalishaji kwa kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu za uhifadhi wa mazingira. Uzalishaji huo hutumia njia za kisasa za kutibu maji yenye
15
kemikali (water treatment) yanayotoka viwandani. Vile vile, viwanda vina utaratibu wa kuwapa
wafanyakazi wake vifaa kinga na vina mfumo wa kudhibiti sauti ili kuzuia kelele.
57. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara kupitia Shirika la TATC -
NYUMBU imefanikiwa kufanya utafiti na kubuni mashine kwa ajili ya uzalishaji wa nishati mbadala.
Mashine hizo ni za Agrowaste briquette na Coal briquette ambazo zinatumia mabaki ya
mashambani, vyakula, vumbi la makaa ya mawe na udongo mfinyanzi kutengeneza mkaa.
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo
58. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara imefanikiwa kutekeleza
shughuli mbalimbali kwa kutumia fedha za maendeleo kama ifuatavyo:-
i. Ununuzi wa zana na vifaa, ujenzi na ukarabati wa miundombinu
59. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20 Wizara imeendelea kununua zana
na vifaa mbalimbali vya kijeshi pamoja na kugharamia matengenezo na utunzaji wake kwa ajili ya
kuliimarisha Jeshi letu. Aidha, Wizara imeendelea na ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa,
ukamilishaji wa Makao Makuu ya JKT, ujenzi wa kambi ya JKT Kibiti (Pwani) na ukamilishwaji wa
ujenzi na ukarabati wa Kambi za JKT zifuatazo: Makuyuni (Arusha); Mpwapwa na Makutupora
(Dodoma); Itaka (Songwe); Milundikwa na Luwa (Rukwa); Bulombora (Kigoma); Mbweni (Dar es
Salaam); Nachingwea (Lindi); Mafinga (Iringa) na Maramba (Tanga).
ii. Mawasiliano Salama Jeshini
60. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza Mradi wa Mawasiliano Salama Jeshini,
pamoja na kukamilisha shughuli za kuunganisha mtandao wa mawasiliano ambapo hadi sasa
yanapatikana katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya
Nishati kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imeingia mkataba na M/S Electrical Transmission
and Distribution Construction and Maintenance Company Limited (ETDCO) ambayo ni Kampuni
Tanzu ya TANESCO kuipatia umeme minara 74. Kampuni hiyo imekwishaanza kusambaza nguzo
za umeme kuanzia mkoa wa Dodoma kuelekea mikoa ya Kanda ya Magharibi. Upatikanaji wa
Nishati hiyo utawezesha Mawasiliano kupatikana katika vikosi vilivyopo Mikoa tisa iliyobaki
kwenye Kanda ya Kusini, Magharibi, Ziwa na Kaskazini.
16
iii. Upimaji, Uthamini na Ulipaji Fidia
61. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kufanya upimaji na uthamini wa maeneo
yaliyotwaliwa kwa matumizi ya Jeshi ambayo yanatakiwa kulipwa fidia. Katika Mwaka wa Fedha
2019/20, Wizara imefanya uthamini katika maeneo ya Kigongo Feri na Ilemela - Mwanza,
Nyamisungura –Mara na Kaboya – Kagera pamoja na ufufuaji wa mipaka na upimaji upya
(Boundary Restoration and Resurvey) eneo la Kimbiji – Kigamboni. Vile vile, Wizara imefanikiwa
kupata Hati Miliki za maeneo mawili ya Jeshi ambayo ni Msasani Beach Club (Dar es Salaam) na
Tarime mjini (Mara). Katika kudhibiti uvamizi wa maeneo ya Jeshi, Wizara imeendelea
kurekebisha mipaka ya maeneo hususan maeneo ya Jeshi yaliyoko mijini, mfano Kambi ya
Kunduchi KTC – Dar es Salaam.
62. Mheshimiwa Spika, naomba nitoe rai kwa Waheshimiwa Wabunge na viongozi kuendelea
kuwaelimisha wananchi kuacha kuvamia maeneo ya Jeshi.
iv. Ufuatiliaji na Tathmini
63. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Wizara ilifanya ufuatiliaji na tathmini
katika miradi iliyopatiwa fedha kwa ajili ya kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi hiyo. Utekelezaji
wa miradi hiyo kwa ujumla unaendelea vizuri. Hata hivyo, kwa baadhi ya miradi kuna changamoto
zilizojitokeza na hatua za utatuzi wake ziliainishwa kwa ajili ya kufanikisha ukamilishaji wake.
SHUGHULI ZILIZOTEKELEZWA NA MASHIRIKA YANAYOSIMAMIWA NA WIZARA
64. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia mashirika yake ya TATC - NYUMBU, MZINGA na
SUMAJKT imeendelea kufanya tafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa na
huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia.
Shirika la TATC - NYUMBU
65. Mheshimiwa Spika, Shirika limeendelea na shughuli za utafiti na uhawilishaji wa teknolojia
mbalimbali kwa matumizi ya kijeshi na kiraia. Katika Mwaka wa Fedha 2019/20 Shirika
limeendelea kutoa mchango wa kupunguza matumizi ya Serikali kwa kukarabati vifaa na zana za
kijeshi kwa ajili ya vikosi vya ulinzi wa amani, magari ya kivita na vifaa mbalimbali kwa ajili ya
matumizi ya Jeshi. Vile vile, Shirika limeweza kuunganisha magari mawili ya zimamoto ambapo
gari moja limekamilika na lingine limefikia asilimia 70. Shirika pia limeendelea kutengeneza vipuri
vya mitambo mbalimbali kwa ajili ya matumizi katika sekta za ulinzi, kilimo, usafirishaji, madini na
maji. Pia, Shirika limefanikiwa kutengeneza terminal traillers tano kwa ajili ya matumizi ya
17
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Brake blocks kwa ajili ya matumizi ya Shirika la Reli
Tanzania.
Shirika la MZINGA
66. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20, Shirika limeendelea na shughuli za
uzalishaji wa zao la msingi kwa ajili ya matumizi ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama. Shirika pia
limeendelea kuagiza na kusambaza baruti zinazotumika katika ujenzi na uchimbaji wa madini.
Aidha, Shirika linaendelea na utafiti wa uzalishaji wa malighafi na vipuri vinavyotumika katika zao
la msingi. Vile vile, Shirika limefanya ukarabati wa silaha mbovu kutoka kwa washitiri mbalimbali
na kutengeneza mabomu ya kufukuzia wanyama (thunderflash) ambayo hutumiwa zaidi na
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa - TANAPA.
67. Mheshimiwa Spika, Shirika kupitia kampuni yake Tanzu ya ujenzi (Mzinga Holding
Company Limited), limeendelea na shughuli mbalimbali zikiwemo ujenzi wa majengo ya Taasisi za
Umma na Watu Binafsi. Baadhi ya shughuli zinazoendelea katika kipindi hiki ni za ujenzi wa:
Hospitali ya Nyamagana (Mwanza); Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi (Singida); Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu (Manyara); Ofisi ya Halmashauri ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busekelo (Mbeya); majengo ya Hosteli ya
Watawa Kashozi (Bukoba); kiwanda cha sukari Kagera; na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Sambamba na shughuli hizo Shirika linafanya ukarabati wa
Shule ya Sekondari Kahororo na Shule ya Sekondari Bukoba.
Shirika la Uzalishaji Mali la JKT (SUMAJKT)
68. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2019/20 SUMAJKT limeendelea kutekeleza
shughuli zake katika misingi ya kibiashara kupitia Kampuni Tanzu na Idara zake ambazo ni
Kampuni ya Ujenzi (SUMAJKT Construction Company Ltd), Kampuni ya Ulinzi (SUMAJKT Guard
Ltd), Idara ya Viwanda na Mradi wa Matrekta. Katika kipindi husika Shirika limetekeleza
shughuli zifuatazo:
69. Mheshimiwa Spika, SUMAJKT kupitia Kampuni yake tanzu ya SUMAJKT Construction
Company Limited (SCCL) limetekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo; Ujenzi wa Vituo vya
Madini katika Mikoa ya Tanga (Handeni), Ruvuma (Songea), Katavi (Mpanda), Mbeya (Chunya),
Simiyu (Bariadi), Mara (Musoma) na Kagera (Bukoba); ujenzi wa Majengo ya Halmashauri za
Wilaya za Kibaha, Kibiti, Mpimbwe, Chamwino, Kondoa, Simanjiro, Kalambo, Mafinga, Mpanda,
18
Nsimbo na Newala. Vile vile, Kampuni hiyo ya ujenzi imetekeleza ujenzi wa majengo katika
Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Maabara ya Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine (SUA), ujenzi wa Hosteli na Madarasa Chuo Kikuu cha Mzumbe, ujenzi wa sakafu ngumu
(Paving) ya Bandari Kavu (Dry Port) Kwala na ukarabati wa Hosteli ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
70. Mheshimiwa Spika, SUMAJKT kupitia SUMAJKT Construction Company Limited (SCCL)
limefanikiwa kutekeleza na kusimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi kupitia Kanda
saba (7) ikiwemo ujenzi wa: madarasa ya Shule ya Sekondari Lindi, Chuo cha Ustawi wa Jamii,
Zahanati, Jiko na Karakana Ikulu, One Stop Centre – Mirerani, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kyerwa,
Jengo la Utawala DUCE, Hospitali ya Rufaa Katavi, Chuo cha Ualimu Kabanga, hoteli ya kitalii
Chato, Hospitali ya Rufaa Bariadi, na Jijini Dodoma ujenzi wa jengo Makao Makuu ya Uhamiaji,
Hospitali ya Uhuru, Ofisi ya Idara ya Uhamiaji na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
71. Mheshimiwa Spika, SUMAJKT Guard Ltd, hutoa huduma ya ulinzi katika Ofisi za Serikali,
Mashirika ya Umma na Sekta Binafsi. Mpaka sasa Kampuni imeajiri jumla ya walinzi 10,633
ikilinganishwa na walinzi 8,574 waliokuwepo Juni, 2019. Taasisi zinazopata huduma
zimeongezeka kutoka 270 na kufikia 369 hadi kufikia mwezi Machi, 2020.
72. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuwa nchi ya uchumi wa
viwanda, SUMAJKT limeendelea kuimarisha viwanda vyake vikiwemo: Kiwanda cha Ushonaji-
Mgulani (National Service Garments Factory) ambacho kinaendelea kushona sare za Wanajeshi ili
kupunguza gharama za kuagiza sare hizo nje ya nchi; Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi (SUMAJKT
Leather Products) – Mlalakuwa JKT, ambacho huuza bidhaa zake kwa Maafisa na Askari wa
JWTZ, Walinzi wa SUMAJKT Guard Ltd, Mgambo na Kampuni Binafsi za Ulinzi. Kiwanda cha Maji
ya Kunywa Mgulani Dar es Salaam, Kiwanda cha kuchakata nafaka za Mahindi - Mlale (Songea)
na Kiwanda cha Samani - Chang’ombe - Dar es Salaam ambacho hutengeneza samani za aina
mbalimbali za Maofisini na Majumbani.
73. Mheshimiwa Spika, Shirika kupitia Mradi wake wa Matrekta limeendelea kuagiza na
kuuza matrekta, vipuri na zana zake kwa bei nafuu ili kumfanya mkulima kuweza kumudu
kununua. Aidha, mradi umefanikiwa kuuza matrekta 67 kati ya matrekta 100 yaliyoagizwa mwaka
2018/19 na mradi unatarajia kuagiza matrekta mengine 100 kabla ya Juni, 2020. Mradi huu bado
unaendelea kuifanyia kazi changamoto ya urejeshwaji wa madeni kwa wakati kutoka kwa wateja
waliokopeshwa matrekta na zana zake ambapo hadi kufikia Machi, 2020 mradi ulikuwa unadai
19
wateja wake kiasi cha Shilingi 34,975,526,768.32 kutoka deni la Shilingi 35,395,604,512.83
mwezi Julai, 2019. Jitihada za kukusanya madeni kutoka kwa wateja wanaodaiwa wakiwemo
Viongozi wa Serikali, Wabunge, Watumishi wa Umma na watu binafsi zinaendelea kufanyika.
74. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka wa Fedha 2019/20 SUMAJKT kupitia shughuli zake
mbalimbali limeweza kupata mapato ya Shilingi 64,924,594,208.73. Aidha, Shirika linaendelea
kutekeleza shughuli mbalimbali ili kuipunguzia Serikali gharama za uendeshji wa mafunzo ya
vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa.
CHANGAMOTO ZA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KATIKA MWAKA WA FEDHA
2019/20
75. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/20
changamoto mbalimbali zimejitokeza zikiwemo upungufu wa rasilimali fedha na watu pamoja na
Washitiri kutokulipa madeni. Kwa upande wa rasilimali fedha kiasi cha fedha za maendeleo na
matumizi mengineyo kilichoidhinishwa ni pungufu ukilinganisha na kiasi kinachohitajika kutekeleza
majukumu ya msingi ya Wizara.
76. Mheshimiwa Spika, upungufu huo umesababisha Wizara kutofikia malengo ya
utekelezaji kwa baadhi ya maeneo hususan utafiti na uzalishaji wa mazao ya msingi katika
viwanda vya Kijeshi, upimaji, uthamini na kulipa fidia kwa maeneo yaliyotwaliwa kwa matumizi
ya Jeshi, kuboresha makazi, kambi na ofisi, kuboresha Mawasiliano Salama Jeshini, kugharamia
matengenezo na matunzo ya zana na vifaa, kugharamia likizo na uhamisho kwa Wanajeshi na
Watumishi wa Umma, kutoa viwango vya fedha za chakula kulingana na mahitaji halisi na kulipa
madeni ya wazabuni na wakandarasi waliotoa huduma mbalimbali.
77. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa rasilimali watu, Mashirika ya MZINGA na TATC -
NYUMBU yanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa rasilimali watu iliyosababishwa na
watumishi kustaafu. Aidha, SUMAJKT linakabiliwa na changamoto ya washitiri kutolipia huduma
kwa wakati na kuzalisha madeni kwa Shirika ambayo yanakwamisha utekelezaji wa miradi
mbalimbali na malengo ya Shirika.
HATUA ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
78. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kukabiliana na changamoto ya
upungufu wa rasilimali fedha, kwa kuendelea kutumia vizuri fedha inayotolewa
20
kutekeleza majukumu yake. Pia, Wizara imeendelea kukutana na wazabuni pamoja na
Wizara ya Fedha na Mipango kwa lengo la kupitia na kukubaliana utaratibu wa kulipa
madeni husika. Aidha, majadiliano yanaendelea kati ya Wizara na Wizara ya Fedha na
Mipango kuona uwezekano wa kuongeza wigo wa bajeti kulingana na majukumu na
vipaumbele vya Wizara.
79. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuwasiliana na Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kupata vibali vya ajira kuziba nafasi
zilizo wazi ili kukabiliana na upungufu wa rasilimali watu katika Mashirika ya MZINGA na
TATC - NYUMBU. Aidha, Mashirika yameandaa mipango ya maendeleo ya muda wa kati na
muda mrefu. Shirika la TATC - NYUMBU limeandaa Mpango wa Miaka Kumi (2019/20 – 2028/29)
wa kuliimarisha ambao upo katika hatua za majadiliano ngazi ya Kamati ya Makatibu
Wakuu, ili hatimaye uwasilishwe kwenye Baraza la Mawaziri kupata ridhaa na kuweza
kutekelezwa. Shirika la Mzinga limeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa Miaka
Mitano (2017/18 – 2021/22). Vile vile, Wizara kupitia SUMAJKT imeendelea na juhudi mbalimbali
za kukusanya madeni kwa kutumia kampuni ya ukusanyaji madeni na mnada ya SUMAJKT
(SUMAJKT Auction Mart).
MPANGO NA MWELEKEO WA BAJETI MWAKA WA FEDHA 2020/21
80. Mheshimiwa Spika, Mpango na Mwelekeo wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
katika Mwaka wa Fedha 2020/21 ni kutekeleza majukumu yake kwa weledi kulingana na Dira na
Dhima yake. Mwelekeo wa kazi zinazokusudiwa kufanyika katika Mwaka wa Fedha 2020/21
utazingatia maeneo ya kipaumbele yafuatayo:
(a) Kuliimarisha Jeshi kwa zana na vifaa vya kisasa, mawasiliano pamoja na
rasilimali watu;
(b) Kuendelea kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi kwa Wanajeshi
ikiwemo mafunzo, matunzo ya zana na miundombinu, maslahi, huduma bora
za afya, ofisi na makazi;
(c) Kuendelea kujenga uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa kuboresha
miundombinu ili liweze kuchukua vijana wengi zaidi na kutoa mafunzo ya
uzalendo, ukakamavu, umoja wa kitaifa na stadi za kazi kwa vijana wa
Kitanzania;
21
(d) Kuendeleza tafiti na uhawilishaji wa teknolojia kwa ajili ya kuzalisha bidhaa
na huduma kwa matumizi ya kijeshi na kiraia;
(e) Kuendelea kuimarisha na kuratibu Jeshi la Akiba;
(f) Kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU),
Jumuiya za Kikanda na nchi nyingine katika nyanja za kijeshi na kiulinzi;
(g) Kuendelea kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kukabiliana na majanga
na dharura inapohitajika; na
(h) Kuendelea kupima, kuthamini na kulipa fidia ya ardhi iliyotwaliwa kutoka kwa
wananchi kwa matumizi ya Jeshi.
SHUKRANI
81. Mheshimiwa Spika, kabla sijahitimisha Hotuba yangu napenda kutumia fursa hii
kuwashukuru wafuatao kwa michango yao katika maandalizi ya Hotuba hii ya Makadirio ya
Mapato na Matumizi ya Wizara yangu: Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo, Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali
Yacoub Hassan Mohamed, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Charles
Mang’era Mbuge, Wakuu wa Kamandi na Wakuu wa Mashirika.
82. Mheshimiwa Spika, pia napenda kuwashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo (Makao Makuu
ya Wizara), Wakuu wa Matawi (NGOME), Wakuu wa Idara (Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga
Taifa), Maafisa, Askari na Watumishi wa Umma wa Wizara kwa kuendelea kunipa ushirikiano
katika kufanikisha majukumu ya Wizara. Aidha, naishukuru Kamati ya Wizara iliyoandaa hotuba
hii.
83. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mnyimi wa fadhila endapo sitawashukuru Wahisani
mbalimbali waliotoa michango yao kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha maendeleo ya
Jeshi. Wahisani hao ni pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Ujerumani, India, Marekani
Canada, Ufaransa, na Uturuki. Aidha, tunazishukuru nchi rafiki kwa ushirikiano wao katika
shughuli zetu za kiulinzi. Nchi hizo ni pamoja na Bangladesh, Falme za Kiarabu, Ghana,
Indonesia, Jamaica, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Misri, Morocco, Nigeria, Uingereza,
Urusi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Nchi za Maendeleo
Kusini mwa Afrika.
22
84. Mheshimiwa Spika, naomba pia kuwashukuru wananchi wote kwa ushirikiano wanaoutoa
kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika ulinzi wa nchi yetu. Kwa namna ya pekee
naomba kuwashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Kwahani kwa ushirikiano walionipa katika
kipindi chote cha miaka mitano tangu wanichague kuwawakilisha hapa Bungeni. Ni matumaini
yangu kuwa tutaendelea kushirikiana zaidi kwa manufaa ya Jimbo letu na Taifa kwa ujumla.
85. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Spika, mwisho napenda kukushukuru wewe binafsi,
Mawaziri wenzangu, na Wabunge wote kwa ushirikiano walionipa ndani na nje ya Bunge wakati
wote nikiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Aidha, nawatakia kila la kheri na fanaka
kwenye Uchaguzi Mkuu ujao na ni matumaini yangu kuwa tutakutana tena hapa Bungeni katika
kipindi kijacho.
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21
Makadirio ya Mapato
86. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2020/21, Wizara inatarajia kukusanya
maduhuli ya jumla ya Shilingi 85,103,000.00 kutoka katika mafungu yake matatu kwa
mchanganuo ufuatao:
Jedwali Na 3: Makadirio ya Kukusanya Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2020/21
Fungu Makadirio ya Maduhuli 2019/20 38 – NGOME 22,000,000.00
39 – JKT 61,903,000.00 57 – Wizara 1,200,000.00 Jumla 85,103,000.00
Matumizi ya Kawaida na Maendeleo
87. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2020/21, inaomba kuidhinishiwa jumla
ya Shilingi 2,141,034,489,000.00 kwa mafungu yote matatu ambapo kati yake,
Shilingi 1,977,034,489,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na
Shilingi 164,000,000,000.00 ni kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Mchanganuo kwa
kila Fungu ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na 4: Mchanganuo wa Bajeti kwa Fungu kwa Mwaka wa Fedha 2020/21
Fungu Matumizi ya Kawaida
(TZS)
Matumizi ya
Maendeleo (TZS)
Jumla (TZS)
38-NGOME 1,607,164,984,000.00 10,000,000,000.00 1,617,164,984,000.00
23
39-JKT 350,234,958,000.00 4,000,000,000.00 354,234,958,000.00
57-Wizara 19,634,547,000.00 150,000,000,000.00 169,634,547,000.00
Jumla 1,977,034,489,000.00 164,000,000,000.00 2,141,034,489,000.00
MWISHO
88. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Hoja.
KIAMBATISHO NA.1
UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 2015-2020 KATIKA
MWAKA WA FEDHA 2019/20
Serikali kupitia Wizara imeendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
ya mwaka 2015-2020 pamoja na majukumu mengine ya Wizara. Katika Mwaka wa Fedha 2019/20
Wizara imetekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 – 2020 kama ifuatavyo:
Ibara 146 (i) Kuviwezesha vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuviongezea raslimali watu na
raslimali fedha kwa kadri uchumi utakavyoruhusu.
Utekelezaji: Katika kipindi husika Serikali imetoa kibali cha ajira kilichowezesha kuandikisha
Maafisa na Askari. Aidha, Wizara ilipatiwa Watumishi wa Umma katika kada ya Afya. Katika
kutekeleza majukumu yake Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu amekuwa akitunuku Kamisheni kwa
Maafisa wanaohitimu mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) na nje ya nchi.
24
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Amiri Jeshi Mkuu akikagua gwaride la Maafisa wapya kundi la 67/19 kabla ya kuwatunuku
Kamisheni katika viwanja vya Ikulu Dar es Salaam tarehe 08 Februari, 2020.
Ili kuwajengea uwezo Maafisa na Askari wake kiutendaji katika ngazi mbalimbali, Serikali kwa
kupitia Wizara imeendelea kuliimarisha Jeshi kwa kuwapatia mafunzo ya weledi Wanajeshi katika
Shule na Vyuo vya Kijeshi ndani na nje ya nchi. Aidha, Serikali imekuwa ikiongeza bajeti ya
Wizara kila mwaka wa fedha kulingana na hali ya uchumi wa nchi yetu.
Ibara 146 (ii) Kuendelea kuboresha maslahi ya watendaji katika vyombo vya Ulinzi na Usalama
Utekelezaji: Serikali imeendelea kuboresha maslahi ya Wanajeshi na Watumishi wa Umma kwa
kuwapatia mishahara na posho mbalimbali kwa wakati. Aidha, Wizara imeendelea kuboresha
huduma za afya na tiba kwa Wanajeshi ikiwemo ununuzi wa dawa na vifaa tiba kukidhi mahitaji ya
Hospitali za Jeshi ikiwa ni pamoja na utoaji huduma ya usafishaji wa figo baada ya kupata
mashine za dialysis.
Ibara 146 (iii) Kuendelea kuweka mazingira mazuri yanayoliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa
kuimarisha mafunzo kwa vijana wanaojiunga kwa hiari na wale wanaojiunga kwa Mujibu wa
Sheria.
Utekelezaji: Katika utekelezaji wa Ilani ya CCM, Jeshi la Kujenga Taifa limeendelea kujenga
uwezo kwa kuongeza kambi mpya. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2018/19 Jeshi la Kujenga
Taifa limejenga kambi mpya ya Kikosi cha Jeshi 830 katika eneo la Mkupuka Wilaya ya Kibiti
ambayo kwa sasa imeanza kuchukua vijana kwa Mujibu wa Sheria na wa kujitolea. Hata hivyo,
Jeshi la Kujenga Taifa limeendelea kujenga uwezo kwa Wakufunzi kupitia Chuo cha Uongozi cha
Jeshi la Kujenga Taifa kilichopo Kimbiji na hivyo kuendelea kuweka mazingira mazuri ya mafunzo
kwa vijana wanaojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.
25
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilipotembelea Mradi wa ujenzi wa bwalo kwenye Kikosi kipya cha Jeshi 830 – Kibiti, Mkoa wa Pwani tarehe 15 Machi, 2020.
Ibara 146 (iv) Kuendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU) katika
shughuli za Ulinzi wa Amani kwenye nchi mbalimbali Duniani ili majeshi yetu yaendelee kupata
uzoefu na mbinu za kisasa za ulinzi wa amani.
Utekelezaji: Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeendelea kushirikiana na
Jumuiya za Kikanda na za Kimataifa, katika Operesheni za Ulinzi wa Amani chini ya Umoja wa
Mataifa na Umoja wa Afrika ili kuleta amani na usalama kwenye nchi zenye migogoro na
machafuko. Kwa kuzingatia hayo, JWTZ limeendelea kupeleka Maafisa na Askari katika
Operesheni za Ulinzi wa Amani katika nchi za Lebanon, Sudan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo – DRC, na Jamhuri ya Afrika ya Kati – CAR.
Aidha, Jeshi linao Maafisa Wanadhimu, Waangalizi wa Kijeshi, na Makamanda kwenye
operesheni za ulinzi wa amani nchini Sudan, Sudan Kusini, Lebanon, Jamhuri ya Afrika ya Kati na
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Vile vile, Jeshi limekuwa likishiriki katika vikao mbalimbali vya kikanda ikiwemo mikutano ya
Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) na Nchi za Eneo la Maziwa Makuu.
Katika kuimarisha ushirikiano kwa Jumuiya za Kikanda na nchi rafiki, Jeshi limeshiriki mazoezi
mbalimbali yafuatayo na nchi za kanda ya SADC, EAC na nchi nyingine ikiwemo:
a. Shared Accord: Zoezi hili lilifanyika nchini Rwanda mwezi Agosti, 2019;
26
b. Ushirikiano Imara 2019: Zoezi hili la Kituo cha Uamrishaji lilifanyika nchini Uganda
Novemba, 2019; na
c. Maandalizi ya zoezi la Beach Landing Operation: yaliyofanyika Mapinga - Bagamoyo,
kuanzia tarehe 22 Desemba, 2019 hadi 16 Januari, 2020.
Jeshi pia lilishirikiana na nchi rafiki katika masuala mbalimbali ya kiulinzi mfano katika Mwaka wa
Fedha 2019/20 JWTZ lilipata msaada kutoka Serikali ya Ujerumani wa ujenzi wa Karakana ya
matengenezo ya magari.
Ibara 146 (vi) Kuendelea kushirikiana na Mataifa mengine na Asasi za Kimataifa katika
kupambana na makosa yanayovuka mipaka (Cross Border Crimes) hasa ugaidi, uharamia,
utakatishaji wa fedha haramu (money laundering), biashara haramu ya madawa ya kulevya na
usafirishaji wa binadamu.
Utekelezaji: Wizara kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imeendelea kushirikiana na
Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama nchini na Mataifa mengine katika kupambana na matishio
ya kiusalama yakiwemo ugaidi, uvuvi haramu, uharamia, biashara haramu ya madawa ya kulevya
na usafirishaji haramu wa binadamu. Ushirikiano huu ambao umefanywa kupitia mafunzo na
Operesheni mbalimbali umeliwezesha JWTZ kupata uzoefu na kujifunza mbinu mpya za
kupambana na wahalifu wa makosa hayo.
27
KIAMBATISHO NA.2
Mchanganuo wa Fedha Zilizopokelewa Kuanzia Julai 2019 Hadi Machi, 2020
Fungu Matumizi Yaliyoidhinishwa
Bajeti ya Mwaka ya Fedha 2019/20
Kiasi Kilichopokelewa hadi Machi, 2020
Asilimia
38 - NGOME
Mishahara 1,102,392,157,000.00 847,622,973,405.20 76.89
Fedha za Chakula 210,751,950,000.00 156,609,341,000.00 74.31
Matumizi Mengineyo
31,503,201,000.00 66,954,844,374.68 212.53
Posho ya Msamaha wa Kodi
62,079,600,000.00 46,599,700,000.00 75.06
Maendeleo 6,000,000,000.00 2,515,468,293.00 41.92
Jumla ya Fungu 1,412,726,908,000.00 1,120,302,327,072.90 79.30
39 - JKT
Mishahara 189,923,371,000.00 153,604,697,996.00 80.00
Fedha za Chakula 52,200,000,000.00 51,084,743,500.00 97.8
Matumizi Mengineyo
30,419,054,000.00 21,535,071,497.16 63.0
Mafunzo ya Vijana kwa Mujibu wa Sheria
16,000,000,000.00 16,000,000,000.00 100.0
Posho ya Msamaha wa kodi
11,493,000,000.00 8,619,750,000.00 75.0
Maendeleo 2,000,000,000.00 0 0.00
Jumla ya Fungu 302,035,425,000.00 250,844,262,993.16 83.00
57 - WIZARA
Mishahara (Wizara na Mashirika)
10,170,965,000.00 6,743,468,500.00 66.3
Ruzuku (Mashirika na Majenerali)
6,874,634,814.00 3,619,750,839.80 52.65
Matumizi Mengineyo
2,229,410,186.00 2,419,840,541.00 108.54
Maendeleo 120,000,000,000.00 103,678,216,872.26 86.40
Jumla ya Fungu 139,275,010,000.00 116,461,276,753.06 83.62
JUMLA KUU 1,854,037,343,000.00 1,487,607,866,819.12 80.24