zanzibar daima online. toleo namba 6

Upload: hassan-mussa-khamis

Post on 04-Jun-2018

775 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    1/21

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    Zanzibar DaimaOnline

    Ni

    Toleo06

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    2/21

    PAGE

    2

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    3

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    2

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    MHARIRI MKUUAhmed Rajab

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSAIDIZIMohammed Ghassani

    Email: [email protected]

    MHARIRI MSANIFUHassan M Khamis

    Email: [email protected]

    COMMUNICATION MANAGERHassan M Khamis

    WAANDISHIJabir Idrissa

    Email: [email protected]

    Othman MirajiEmail: [email protected]

    Hamza RijalEmail: [email protected]

    Salim Said SalimEmail: [email protected]

    Ally SalehEmail: a [email protected]

    WASAMBAZAJImzalendo.net

    zanzibardaima.netzanzibardaima/facebook

    MATANGAZOHassan M Khamis

    Simu: +44 7588550153Email: [email protected]

    WASIALIANA [email protected]

    JARIDA HILI HUCHAPISHWA NAZanzibar Daima Collective

    233 Convent WaySouthallUB2 5UH

    Nonnstr. 2553119 Bonn

    Germany

    www.zanzibardaima.net

    Zanzibar DaimaOnline

    Timu Yetu

    Zanzibar Daima Online Toleo 05 03

    Mhariri Mkuu Ahmed Rajab

    PenyeNia pana njia

    Safari hii Jabir Idrissaametuletea makalayenye kuthibitisha ule

    usemi kwamba panapo niapana njia. Haukwenda ari-

    jojo ule msimamo wa Wa-zanzibari, wakisaidiwa navyama vikuu vya Upinzanivya Tanzania, wa kushikiliakwamba hawakushirikishwakatika kujadili Mapendekezoya Marekebisho ya Sheria yaMabadiliko ya Katiba.

    Rais Jakaya Kikwete naserikali yake wamebidi wajematao ya chini na wakirikwamba kwa hilo kweli Wa-zanzibari hawakutendewahaki. Na sasa serikali ya Jam-

    huri ya Muungano imeridhiakufanya marekebisho mapyakatika hiyo Sheria ya Mab-adiliko ya Katiba, licha yakuwa Kikwete amekwisha-tia saini yake katika warakahuo.

    Hilo si fanikio dogo. Walahalikupatikana kwa urahisi.Ni wazi kwamba serikali hai-kutaka matokeo ya kadhiahiyo yawe kama yalivyoku-wa. Lakini Wazanzibari nawapinzani walipata ushindi

    kwa sababu mbili.

    Kwanza walishikamana nakuwa na msimamo mmojana pili, walisimama imarakuutetea huo msimamowao. Hawakugawika walahawakuyumbayumba.

    Hivyo ndivyo upinzani, ka-tika mfumo wa kidemokra-sia, utakiwavyo uwe. Kila

    pale seri-kali inapoja-ribu kukatamaamuzikibabe vyama

    vya upinzanivinawajibikakuzitupiliambali ari zaona kuunganaviwe na msi-mamo mmojadhidi ya seri-kali.

    Vikifanya hivyo, serikalihuwa haiwezi kufua dafu nakujifanyia itakavyo ikiyapuu-za matakwa ya wananchi.

    Fanikio hilo la vyama vya up-inzani ni funzo pia kwambalau vyama hivyo vitauen-deleza umoja wao basi vi-taweza kuleta miujiza yaharaka katika siasa za Tan-zania, miujiza ya kushindwakwa Chama cha Mapinduzi(CCM) katika uchaguzi ujaowa 2015.

    Tokea hapo chama hichokinaregarega Bara naVisiwani na kuna is-hara nyingi zenye kuashiria

    kwamba kitapata taabu kuu-nyakua ushindi kama ilivyokawaida yake. Sasa vyamavya upinzani vikiweza ku-shikamana na kuwa na mka-kati wa pamoja wa kukibo-moa chama hicho katika kila

    jimbo la uchaguzi ni rahisikukiona chama hicho kikon-gwe kikiporomoka katikamajimbo mengi ya uchaguzikatika sehemu zote mbili za

    Muungano.

    Swali ni kuwa je, vyama vyaupinzani vitaweza kwelikuvumiliana, kuaminianana kuwa na msimamo wapamoja wenye lengo lakukingoa kwenye madarakachama cha CCM.

    Na kama hivyo vyama vyaupinzani vitaweza kusahautafauti zao na vikawa naumoja kutazuka maswalimengine: je, CCM nacho kita-

    jiachia kilale kikijua kwambamshikamano wa vyama vyaupinzani utakiua? Au kita-fanya hila zake za kuviingiliavyama hivyo, kuvifitinisha

    na kuvifanya vikinzane vy-enyewe kwa vyenyewe ilivipwae visiweze kuwa nanguvu za kutosha kukikabiliCCM?

    Tunamaliza kwa kuyarejeayaleyale kwamba vyama vyaupinzani vinaweza kukian-gusha CCM endapo vitakuwana nia ya dhati ya kufanyahivyo

    Mazungumzo Baadaya Habari

    Mkeka wa Mwanawa Mwana

    Tufungue Kitabu

    Waraka kutokaBonn

    Kalamu ya Bin Rajab

    Uk. 18.Farrel J FoumKikwete akithubu ataweza

    Uk. 20. Riziki OmarZanzibar iuzwapo kwakikombe cha chai

    Uk. 24. Ridder SamsomSitiari za Mzee wa Kimbunga

    Uk. 22. Othman MirajiSerikali ni sisi sote

    Uk. 28. Ahmed RajabHofu na chuki hazina tenanafasi Zanzibar

    Kauli ya MwinyiMkuu

    Uk. 32. Jabir IdrissaTangu lini Stendi ya gariikawekwa barabarani

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    3/21

    PAGE

    4

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    5

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    4

    AADA y

    a Zanzibar kupaisha kilio kizito cha kutoshirikishwa katika kujadili mapendekezoya marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, sasa ime-sikilizwa. Si hivyo tu lakini tayari serikali imeridhia kupeleka marekebisho mapya katika

    sheria hiyo, Zanzibar Daima Online limefahamishwa.

    Na Jabir Idrissa Habari Kuu

    Hata hivyo, pamoja na wakuuwa Serikali ya Muungano chiniya Rais Jakaya Kikwete kuan-daa mapendekezo mapya yakuirekebisha sheria iliyotungwamwaka 2011 na Bunge, mjiniDodoma, kuna ripoti zinazose-ma kuwa vyama vya upinzanivimezuia mapendekezo hayokuwasilishwa bungeni mpakakwanza vijiridhishe kama ndiyoyaliyokubaliwa.

    Taarifa kutoka ndani ya serikalizote mbili, Ofisi ya Bunge, na

    vyama vya siasa vilivyoundaumoja wa kupigania haki yakusikilizwa wakati serikali ilip-owasilisha mswada wa sheriaambao hatimaye ulipitishwakinyemela na wabunge waChama Cha Mapinduzi (CCM) naMwenyekiti wa Tanzania Labour(TLP) Augustine Mrema pekee,zinasema mapendekezo hayomapya yatasubiri mwafaka.

    Kwa mujibu wa taarifa hizo,viongozi wa Chama cha Wanan-chi (CUF), Chama cha Demokra-

    sia na Maendeleo (Chadema) naNCCR-Mageuzi, waliounda timuya wataalamu wa kuchambua mapende-kezo yanayopaswa kuzingatiwa katikakurekebisha sheria hiyo iliyopitishwa naBunge Septemba 6, wameona ni muhimukujiridhisha na mapendekezo ya serikali.

    Wameona ni muhimu kwao kuyapitiamapendekezo yenyewe ya marekebishokama yalivyoandaliwa na Serikali ili kujiri-dhisha kwa sababu wanadhani ipo haja ya

    kuhakikisha kila kitu kimekwenda kulinganana makubaliano yao. Hatua hii ni ya lazimakwa kuwa uzoefu unaonesha kuwaachiawatendaji wa serikali waamue peke yaokunaweza kuleta matatizo mengine, chan-zo cha habari hizi kimemnukuu mmoja wawajumbe wa timu ya wataalamu ya vyamahivyo.

    Mpashaji habari huyo amemnukuu mjumbewa timu ya wataalamu ya vyama akisemakwamba mapendekezo ya kurekebishasheria ya katiba yamezingatia vilio vya kilaupande likiwemo suala la kupatikana kwausawa wa wajumbe wa Bunge Maalum

    la Katiba kati ya Zanzibar na Tanganyika,kinyume na ilivyowekwa katika sheria hiyoambayo kupitishwa kwake kulizua mtafa-ruku hasa pale Zanzibar ilipolalamika kwakutoshirikishwa katika kujadili mapende-kezo yaliyowasilishwa bungeni na Waziri waSheria na Katiba wa Serikali ya Muunganoya kurekebisha sheria ya 2011.

    Kwa sababu ya hatua hiyo ya vyama kuzuiamapendekezo hayo mpaka kwanza kujirid-hisha, huenda sasa Mswada wa marekebi-sho ya sheria ile ukawasilishwa kwa njia yadharura, badala ya utaratibu wa kawaidawa kuzingatia muda wa kuusoma mara

    mbili kabla ya kuwasilishwa rasmi bungeni.

    Taarifa za karibuni kutoka Ofisi ya Bungezimesema kuwa kama ni mapema kulikoilivyokusudiwa hapo kabla, basi mswadahuo unaweza kuwasilishwa bungeni katikasiku mbili za mwisho za mkutano wa bungeunaoendelea mjini Dodoma kwa sasa, am-bao ulianza Jumanne ya wiki iliyopita.

    Jarida hili limefanikiwa kuyaona mapende-kezo yaliyoandaliwa awali na timu ya wata-

    Zanzibar yashika mpini kisu cha Katiba Mpya

    HABARI KUU

    Waziri wa Sheria na Katiba wa

    Zanzibar Abubakar Khamis Bakari

    [katikati], akizungumza na Waziri

    Mkuu Mizengo Pinda [kulia]

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    4/21

    PAGE

    6

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    7

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    6

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    alamu ya vyama vilivyoungana, mara baadaya kukutana na Rais Kikwete, Ikulu jijini Dares Salaam, katika mkutano ulioitishwa kamanjia ya kupata mwafaka na vyama hivyovitatu vilivyopinga Sheria ya Marekebishoya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuwailipitishwa kinyemela.

    Suala la Zanzibar kuingiza wajumbe kwaidadi sawa katika Bunge Maalum la Katibapamoja na wale watakaotoka Tanganyika,limezingatiwa na mwafaka umefikiwa kuwawajumbe wa bunge hilo litakalojadili nahatimaye kupitisha Rasimu ya pili ya Katiba,watakuwa sawa.Mapendekezo hayo yanaonesha kuwa bungelitakuwa na wajumbe 908 wakiwemo zaidiya wajumbe 200 watakaotokana na uwakili-shi wa asasi za kiraia ambazo sasa zinatajwarasmi ndani ya sheria, kinyume na ilivyoku-wa awali wajumbe hao kuwa 166 na ambaowangeteuliwa na Rais baada ya kupende-

    kezwa na taasisi zilizobainishwa.Sheria iliyopitishwa na wabunge wa CCM naMrema pekee haikutaja orodha ya taasisina iliachia mamlaka ya uteuzi kwa Rais kwautaratibu wa kupelekewa majina ya wa-

    jumbe tisa kila taasisi, naye kuteua angalauwatatu kati yao.

    Sheria hiyo ilipingwa tangu pale kambirasmi ya upinzani bungeni iliposema kuwautaratibu huo utampa nafasi Rais kuon-geza wajumbe wenye mtizamo anaoutakayeye, huku tayari kiongozi huyo anayetokaCCM akiwa na sauti kubwa inayotokana nawabunge wa sasa pamoja na wajumbe wa

    Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

    Ni malalamiko ya kambi ya upinzani bun-geni kuwa katika mazingira ambayo BungeMaalum la Katiba litakuwa na wabunge wasasa; wajumbe wa Baraza la Wawakilishi,CCM itakuwa na sauti kubwa na itakuwa

    kubwa zaidi iwapo Rais atabaki na mam-laka ya kuteua wale wajumbe 166 kutokamakundi ya taasisi za kiraia.

    Hili Rais Kikwete alilielewa vizuri. Lakinialitaka viongozi wa vyama pamoja na chakecha CCM wakakae na kujadiliana namna

    watakavyoliwekea utaratibu wa kuteu-liwa wajumbe nje ya utaratibu wa sasa.Makubaliano yalifikiwa hapa na hata walipo-kutana baada ya hapo, walielewana haja yataasisi zenyewe kuteua wajumbe wenyewekwa kuwa wanaelewana, alisema ofisamwandamizi ndani ya Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali, Dar es Salaam.

    Pendekezo jingine lililoridhiwa kuwa nalolijumuishwe katika marekebisho yatakayo-pelekwa bungeni, ni lile la kuwekwa kiwangocha kura za upitishaji rasimu ya katiba chazaidi ya nusu ya kura za kila upande kati yaZanzibar na Tanganyika. Hii ni kura ya maoni

    itakayopigwa kwa ajili ya kupitisha katibampya baada ya Bunge Maalum la Katiba kui-pitisha rasimu ya mwisho.

    Taarifa zinasema kuwa utaratibu wa awaliwa sheria iliyopitishwa na bunge Septembamwaka huu, kwamba katiba itatamkwakuwa tayari imeidhinishwa rasmi na wanan-chi iwapo kura ya maoni iliyopigwa mara yapili itakuwa na matokeo yaleyale ya kutopa-tikana kwa theluthi mbili za kura kwa kilaupande wa washirika wa Muungano.

    Suala hili la kiwango cha upitishaji Katibalimekuwa nyeti hasa kwa kuwa serikali ili-

    taka theluthi mbili isipopatikana pale am-bapo kura ya maoni ilipigwa kwa mara ya pili,baada ya mara ya kwanza kutofikiwa, basiKatiba iwe ndiyo imepitishwa.

    Vyama vya upinzani ndani ya bunge vili-pinga utaratibu huo kwa kusema si wa

    kidemokrasia na hautakuwa umezingatiauhalali wa kila upande wa Muungano kutoakauli thabiti ya kama umeiridhia Katiba auumeikataa. Walitaka kiwango cha kura kiweasilimia zaidi ya 50 ya uamuzi.

    Utaratibu huo ulipingwa na taasisi za kiraia

    za pande zote mbili: Zanzibar na TanzaniaBara.Wiki iliyopita, Muungano wa Asasi za Kiraianchini Tanzania (AZAKI) uliokutana jijini Dares Salaam, ulitaka sheria itamke wazi ninikitafanyika ikitokea upande mmoja umei-kataa Katiba katika kura ya maoni.

    Akizungumza katika mkutano huo, Mwe-nyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), ambaye pia ni kiongozi wa AZAKI,Usu Mallya, alisema Katiba inayohangai-kiwa ni ya Watanzania. Upo ulazima wakila upande wa Muungano kutoa sauti yakendipo itakuwa yapo makubaliano na marid-

    hiano katika kupitisha Katiba mpya ya ta-aifa.

    Mvutano mkubwa ulitokea wakati mswadawa sheria ulipowasilishwa bungeni Septem-ba 4 na Waziri wa Katiba na Sheria wa Seri-kali ya Muungano, Mathias Chikawe. Kambirasmi ya upinzani ilitaka mabadiliko lakinikutokana na mazingira magumu yaliyotu-mika kuongoza mkutano, wabunge wa up-inzani waliona wamekandamizwa na NaibuSpika wa Bunge, Job Ndugai na waliamuakutoka nje.

    Kutoka kwao kulilazimisha wakutane nje

    ya ukumbi wa Bunge, halafu wakaafikianakuendeleza umoja wa kupinga sheria iliyopi-tishwa huku wakieleza bayana malalamikoyao pamoja na kasoro za mswada ambaowakati huo ulikuwa ukisubiri kusainiwa naRais ili uwe sheria rasmi.

    Kutoshirikishwa kwa Zanzibar katika ku-

    jadiliwa kwa mapendekezo ya mswada huo,kuliibuliwa na Mbunge wa Mkanyageni,Mkoa wa Kusini Pemba, Mohamed HabibMnyaa (CUF), aliyetoa hoja hiyo aliposi-mama na kuomba mwongozo wa Spikakuhusu kutoshirikishwa kwa Zanzibar ka-tika jambo hilo. Naibu Spika Ndugai aliahidi

    kutoa majibu ya mwongozo huo, pamoja namingine miwili yaliyoombwa baadaye, kati-ka wakati mwafaka. Hakutoa ufafanuzi wakauli hiyo na wapinzani wakaichukulia kuwani kauli ya kuwapuuza.

    Waliposhikilia kutaka majibu ya miongozoyao, ukiwemo na ule uliotolewa na Mbungewa Ubungo, John Mnyika (Chadema),waligoma kupitia kiongozi wa Upinzani Bun-geni, Freeman Mbowe (Chadema), ambayehatimaye aliamriwa na Ndugai atoke nje.Alipogoma, na wabunge wa vyama vinginekumkingia kifua asitoke, ndipo naibu spikahuyo alipoamuru askari wa usalama waingie

    ukumbini na wamtoe kwa nguvu.Wabunge waliamua kutoka naye na hati-maye mjadala wa mswada ukaendelea kwawabunge wa CCM pekee kushiriki, pamojana Mrema, mpaka kuupitisha mswada.

    Nje ya Bunge, Zanzibar ilishikilia kuwa hai-kushirikishwa hasa pale Waziri wake waKatiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakary,aliposema baadaye kuwa yale yaliyowasil-ishwa bungeni siyo hasa yaliyofikishwa seri-kalini na kujadiliwa na kutolewa maoni.

    Waziri Abubakar alisema kwamba wakati

    mswada ulioletwa serikalini ulikuwa navifungu vinne, ule uliowasilishwa bungeni,ulikuwa na vifungu 12, vikiwemo vile am-bavyo vina matatizo makubwa kwa maslahiya Zanzibar iwapo vitabaki hivyo

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    5/21

    PAGE

    8

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    9

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    8

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 05 - 2013

    Wiki hii zilizuka habarikuwa kumeanza

    juhudi za kupun-

    guza na pengine baadayekuondoa kabisa vitendo vyakikundi kinachojiita UbayaUbaya ambacho kimekuwamaarufu kwa vitendo viovuinavyovifanya bila ya kuwana hofu yoyote ya kuchuku-liwa hatua.

    Kikundi hicho ni kikuu mion-goni mwa vikundi vyenginevidogo vidogo ambavyo

    vimekuwa vikidaiwa ku-fanya vitendo vya uharibifu,unyanganyi na uchomaji wa

    maeneo mbali mbali hasamara tu hali inapoelekeakuchafuka.

    Lakini kwa wakaazi wamaeneo mengine ya njeya mji wa Zanzibar, UbayaUbaya ni kikundi wanachoi-shi nacho kila siku. Kime-kuwa kama vile vikundi vyakijambazi vya Ulaya vyenyekutawala maeneo kihalifu.

    Hivi sasa kuna maeneo am-bayo ni shida kukalika. Kwamfano, mtu hawezi kutoka

    nje ifikapo saa fulani, kamamwanamke anataka kutokanje huku akivaa dhahabubasi lazima azivae dhahabuzake kwa kificho. Chako kiki-takiwa basi ni lazima ukitoe.Katika maeneo hayo AskariJamii na hata Askari Polisihawana ubavu wowote ule.

    Kuna maelezo ya kwa ninikikundi hiki au vyengine

    Barza ya Jumba Maro

    kama hiki vimezuka. Namengi ya maelezo hayoyanaelekeza katika rubaa

    za kisiasa kwamba ndiowalioviunda au kusababishakuundwa vikundi hivyo.

    Ndipo wengi walipoanzakujenga imani kuwa, kwamfano, matukio makubwaya fujo za mwaka jana am-bazo zilipelekea kuzukakizaazaa cha wiki moja nahatimaye kukamatwa vion-gozi wa Uamsho, vilihimiz-

    wa na kukuzwa na makundiya Ubaya Ubaya na yanay-ofanana nayo.

    Imani ya watu ni kuwakwa vile vikundi hivi havi-

    jachukuliwa hatua yoyoteile na Polisi na wala havi-

    jalalamikiwa na upandemmoja wa siasa za Zanzibarbasi tabaan viunaungwamkono na Chama cha Map-induzi (CCM) kwa sababuvina manufaa na upandehuo wa siasa za Zanzibar.

    Si rahisi kuamini kuwachama hicho kinahusikarasmi na vikundi hivyo. Laki-

    ni maelezo yanasema kuwavikundi hivyo vimetokana navijana ambao wameshind-wa kutimiziwa ahadi naCCM baada ya kushirikikatika harakati mbali mbalihasa za kiuchaguzi.

    Kadri ninavyojua CCM hai-jawahi kutoa kauli kujibushutuma hizo. Kwa upandemwingine, Chama cha Wa-

    Hata Ubaya Ubaya watuondoshee Wazungu?

    Na Ally Saleh

    Vijana wa CCM Zanzibar katika moja ya mikutano yao ya hadhara

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    6/21

    PAGE

    10

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    11

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    10

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    Vichwa maji wangalipo, tunao tele kibaoPande zote wao wapo, zi tele alama zaoKisikiza wasemapo, utajuwa hawa ndioChuki ndiyo lugha yao!

    Hawaoni japo yapo, na wanayo macho yaoKamwe hawasikiipo, wangawa na masikioHata nyoyo zidundapo, haziji fikira zao

    Hasira sauti yao!

    Walipo ndipo walipo, kwenda mbele mwiko kwaoKazi yao ni viapo, kushindana ndiko kwaoNa katu hawashindwipo, sababu ujinga waoHikima si hadhi yao!

    Basi wapo tele wapo, waoneni muonaoWapapo kila tulipo, na ni kubwa namba yaoNchi haitakuwapo, kifatwa wayatakayoVichwa vyao ni vimeo!

    Mohammed Ghassani - Bonn - Ujerumani

    Vichwamaji Tungenao

    Siri ya mtungi, kata ndie mjuajiNasema wala sivungi, maneno yaso dibajiVimenisakama vingi, vyengine sikutarajiMungu ndie mlipajiMwanzo sikuweza sema, nilibaki kulalamaMoto umesharindima, wanishinda kuuzimaSi wima si uchutama, naitafuta khatima

    Hata juu ya vilima

    Kiza hutanda kwa ndani, nje kuna mwanga wakeSiri siri mtungini, ikitoka ni mashukeKata wanyamaza nini, yaseme usisumbukeAu waogopa teke

    Mtungi hukaa sana, hadi mwisho huvunjikaMaji yalotulizana, mwisho nje humwagikaNa hayazoleki tena, maji yakishamwagikaCha ndani kishaoneka

    Ally Hilal, Wete, Pemba

    Siri Mtungini

    nanchi (CUF) kupitia KatibuMkuu wake Maalim SeifShariff Hamad kimetoa la-wama za wazi juu ya viten-do vyao na kujiuburi Polisikuchukua hatua.

    Hakuna taarifa yoyote kuwaPolisi imechukua hatua ma-

    kini kukivunja kikundi hicho,wala kuomba msaada waShirika la Uchunguzi wa Jinaila Marekani (FBI) ili kujipe-nyeza katika kikundi hichona kukisambaratisha kwasababu ni tishio kwa watuwengi na mustakabali wakiusalama wa Zanzibar.

    Taarifa zilizoenea wiki hiini kuwa sasa Wazunguwameamua kulipania sualala Ubaya Ubaya ili kulijuaundani wake na tabaan ku-

    chukua mbinu za kukivunjakikundi hicho, jambo ambalo

    Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar, japo haijashindwalakini ilikuwa haina nia yakisiasa kulichukulia hatua.

    Kwa mujibu wa taarifa tulizonazo ni kuwa Ubalozi waMarekani na shirika mojala Norway ndio walioamua

    kuifanya kazi hiyo am-bayo kihalali kabisa ilikuwatuifanye sisi wenyewe amakwa kutumia nguvu za Polisiau kwa rai za Serikali.

    Wazungu ndio Wazun-gu bwana. Nina hakikawatakaa na vijana hao, am-bao kwa hakika wana madaiyanayoweza kujadilika ili piawawaonyeshe juu ya ubayana hasara za matendo yaona ubaya na hasara hizozinavyoweza kuwarudia

    wenyewe.

    Naamini Wazungu haowatatizama suala hilo ki-saikolojia na kijamii lakinipia watalitizama katika sia-sa na siasa za ushindani nakuibuka na jawabu za kwanini hali imefikia kama ilivyona wakati huo huo kutoamapendekezo ya kulimaliza.

    Ingawa Serikali yetuimeshindwa lakini Wazunguhao watagundua kuwavijana hao wametumiwavibaya, wamejazwa jazba naukatili, wamejengwa imanimbaya kuwa wasiokuwa wachama chao au wasiofanananao kifikra ni maadui na wa-nafaa kufanyiwa ubaya nalabda ndio pakazuka UbayaUbaya.

    Wazungu watawaeleza wa-

    jibu wa kiraia, watawafundi-sha kuwa wazalendo, wa-

    tawaelekeza juu ya wajibuwao katika jamii na jinsi yakuwa raia wema na kwam-ba hiyo ndio nguzo muhimuya kujenga nchi yao ambayohaipaswi kurudi ilikotokahasa baada ya kuundwaSerikali ya Umoja wa Kitaifa(SUK).

    Na Wazungu hao wa-taendelea kuwaambia Uba-ya Ubaya au wengine kamahao kuwa wasikubali ku-tumiwa na wanasiasa kwasababu mwisho wake nikuachwa wao wakamatwena mkono wa sheria, mbaliya kuhasimiana na ndugu na

    jamaa na kujijengea tabia yauovu bila ya sababu.

    Hawa Wazungu watagun-dua jambo ambalo Serikali

    ya Zanzibar imeshindwa

    kugundua. Nalo ni kuwavitendo kama hivyo ndivyovinavyotumika kuwa mbo-lea ya kuzalisha makundi yakigaidi na kuwa njia moja yakuwazuia Al Shabaab na AlQaida kuingia nchini ni ku-wapa uwezo wa kujiamuliahatma yao vijana wetu.

    Mwisho kabisa Wazunguhao watashauri kuwa tatizokubwa ni ajira. Ukiwapatiaajira vijana hao na kuwaon-dosha vibarazani, ukiwapasenti mfukoni na kutowa-fanya kufikiri wala kutokub-ali kutumiwa na mtu yoyote,hasa wanasiasa wetu, basiutaweza kulipatia dawatatizo hili.

    Sasa Wazungu wakishali-maliza hili tatizo la Ubaya

    Ubaya uso wa Serikali yetu

    utakuwa wapi? Tupewemisaada ya kifedha sawa,basi pia misaada ya kukabilimatatizo kama ya makundikama haya ambayo tuna-

    jua hakika yana hasara nayanaweza kuwa na mad-hara ya kuenea na kuletamadhara, mpaka pia wajeWazungu watusaidie?

    Hivi muda wote wa maten-do ya Ubaya Ubaya namakundi kama hayo, Seri-kali yetu ilikuwa ikiwazanini? Natamani ningeingiandani ya ubongo wa Serikalikujua nini kilichokuwakikiendelea. Kwamba UbayaUbaya itayeyuka yenyewena kusambaratika? Kamadhana ilikuwa hiyo basi ndiomaana tukasubiri mpakaWazungu waje hata hili

    watumalizie?

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    7/21

    PAGE

    12

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    13

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    12

    Makala Maalum

    Katikati ya mwezi Oktoba, vyama vita-tu vya upinzani Chama cha Wananchi(CUF), Chama cha Demokrasia na Maen-deleo (Chadema) na NCCR-Mageu-zi vilimuandikia Rais Jakaya Kikwetemapendekezo yao juu ya namna ya ku-patikana kwa Katiba Mpya ya Jamhuri yaMuungano wa Tanzania kufuatia mgogorouliojitokeza Bungeni, Dodoma, wakati wakupitishwa Sheria ya Mabadiliko ya She-ria ya Kura ya Maoni mnamo mwezi wa

    Septemba 2013. Kwa mnasaba wa mja-dala mpana wa kitaifa na kwa kuwa RaisKikwete aliagiza kurejeshwa tena Bungenikwa sheria hiyo hata baada ya kuiwekasaini, tunachapisha Nukta ya 3 na ya 5 yawaraka huo wa vyama vya upinzani kwaRais, ambazo zinazungumzia nafasi naushiriki wa Zanzibar Mhariri.

    TANBIHI

    Bila ya kuwashirikisha Wazanzibari, hatutakuwa na Katiba Mpya

    K

    una ubishanimkubwa kuhusu

    kushirikishwa kwaSerikali ya Mapinduzi Zan-zibar katika mchakato wakupitishwa kwa Muswadahuu. Wakati Serikali ya Jam-huri ya Muungano imetan-gaza hadharani kwambaSerikali ya Mapinduzi Zanzi-bar ilishirikishwa kikamilifukatika hatua zote za kupit-ishwa kwa Muswada, Seri-kali ya Mapinduzi Zanzibaryenyewe imetoa kauli zenyeutata mkubwa kuhusu sualahili.

    Kwa mfano, wakati Makamuwa Pili wa Rais wa Zanzibaramedai hadharani kwambaSerikali ya Mapinduzi Zanzi-bar ilishirikishwa kikamilifu,Waziri wa Katiba na She-ria Zanzibar MheshimiwaAbubakar Khamis Bakariamesema hadharani kwam-ba ushirikishwaji wa Serikaliya Mapinduzi Zanzibar uli-

    husu vifungu vinne tu vyaMuswada huu.

    Vifungu vingine vyote vyaMuswada vilivyopitishwa naBunge havikupelekwa Zan-zibar na kwa hiyo Serikaliya Mapinduzi Zanzibar hai-kushirikishwa kwenye ku-vitolea maoni na msimamo.Aidha, kwa barua yake yenyekumbu kumbu Na. OMPR/WKS/TS.7/1/62 ya tarehe13 Septemba, 2013, Maka-mu wa Pili wa Rais wa Zan-zibar amemwandikia WaziriMkuu akimweleza kwamba

    Serikali ya Mapinduzi Zan-zibar haikushirikishwa kika-milifu katika kupitishwa kwaMuswada huu.

    Hii ni licha ya Makamu waPili wa Rais huyo kutangazahadharani kabla kwambaSerikali ya Mapinduzi Zan-zibar ilishirikishwa. Kwa vy-ovyote vile, suala hili linaubishani mkubwa ambao

    utatuzi wake unahitaji Mus-wada kurudishwa Bungeni

    kwa ajili ya kujadiliwa upya.Endapo hili halitafanyikakama tunavyopendekeza,kuna uwezekano mkubwakwa Baraza la Wawakili-shi Zanzibar kukataa kurid-hia Muswada huu na hivyokufanya utekelezaji wakekushindikana na mchakatowote wa Katiba Mpya kuk-wamishwa.

    Jamhuri ya Muungano waTanzania ilizaliwa kwa kuun-ganisha nchi mbili zilizoku-

    wa huru na zenye hadhi nahaki sawa, licha ya tofautizao za ukubwa wa eneo auidadi ya watu wake. KatibaMpya ambayo mchakatowake umeleta mgogoro wasasa inatakiwa kuakisi hakina hadhi sawa kati ya nchihizi mbili.

    Kama ambavyo mtaalamummoja wa masuala ya she-

    ria na Katiba na mjumbewa Tume ya Mabadiliko ya

    Katiba ambavyo amesemakuhusu mchakato wetu waKatiba Mpya, katika kuan-dika katiba mpya, wabia waMuungano wanarudi kwausawa.

    Hata hivyo, MheshimiwaRais, dhana hii ya haki na ha-dhi sawa kati ya Washirikawa Muungano haijazingati-wa wakati wa kupitishwakwa Muswada huu. Kwamujibu wa kifungu cha 22(2)cha Sheria, idadi ya wajumbe

    wa Zanzibar katika BungeMaalum watakaotokana nawajumbe 166 walioainishwakatika kifungu cha 22(1)(c) ...haitapungua theluthi mojaya wajumbe hao.

    Hii ina maana kwamba,kwa uchache kabisa, wa-

    jumbe hao wa Zanzibar ha-watapungua 55. Kwa sasaWabunge wanaotoka Zanzi-bar katika Bunge la Jamhuriya Muungano ni 83, wakatiBaraza la Wawakilishi Zan-

    zibar lina wajumbe 76.

    Kwa ujumla, kwa hiyo, ilikutekeleza matakwa ya ki-fungu cha 22(1) na (2) chaSheria, Zanzibar itakuwana wajumbe 214 katikaBunge Maalum, ambayo nisawa na takriban 35% yawajumbe wote. Dhana yahaki na hadhi sawa ilikuba-

    lika na kutekelezwa wakatiwa kuundwa kwa Tume ya

    Mabadiliko ya Katiba. Dhanahii inapaswa pia kukuba-lika na kutekelezwa wakatiwa kuundwa kwa BungeMaalum la Katiba.

    Sisi tunaamini kwamba hojaya usawa wa idadi ya wa-

    jumbe wa Bunge Maalumla Katiba ina nguvu zaidikuhusu Bunge Maalum ku-liko ilivyokuwa kwa Tume.Hii ni kwa sababu, ni BungeMaalum ndilo litakalokuwana mamlaka ya kuijadili na

    kuipitisha Katiba Mpya kablaya kupelekwa kwenye kuraya maoni ya wananchi.

    Upande wenye wajumbewengi utakuwa na nafasi ny-ingi zaidi za kuzungumza ku-liko upande wenye wajumbewachache. Hii ina maanakwamba hoja za upande huondio zitakazosikika zaidi ku-liko hoja za upande mwing-ine.Vinginevyo labda kuwe namasharti ya sheria yatakay-

    olazimu kila upande waJamhuri ya Muungano uwena fursa sawa za kuchangiakatika mijadala ya BungeMaalum. Na kama itakuwahivyo, kutakuwa na hojahalali kwamba wajumbeambao hawatapata nafa-si ya kuchangia wanaendakufanya nini katika BungeMaalum!

    Kwa sababu hizi, tu-napendekeza kwamba ha-

    dhi na haki sawa baina yaWashirika wa Muungano ili-yotumika wakati wa kuundaTume itumike vile vile katikakuunda Bunge Maalum laKatiba. Kwa maana hiyo tu-napendekeza kwamba idadiya wawakilishi wa Zanzibarkatika Bunge Maalum ion-gezwe hadi kufikia nusu yawajumbe wote wa BungeMaalum. Hili linawezekanakwa namna mbili.Kwanza, kwa kuongeza

    idadi ya wajumbe waliota-jwa katika kifungu cha 22(1)(c) kama tulivyopendekeza.Na pili, kwa kurekebisha ki-fungu cha 22(2) ili kisomekekwamba idadi ya wajumbekutoka Zanzibar haitapun-gua asilimia sitini na nne yawajumbe hao.Kama pendekezo hili lita-kubaliwa, wajumbe waBunge Maalum kutoka Zan-zibar wataongezeka kutoka214 kwa mujibu wa Sheriailivyo sasa, hadi 438, wakati

    idadi ya wajumbe wa kutokaTanganyika nao watakuwa438. Muhimu zaidi, BungeMaalum litakuwa limetimizamatakwa ya usawa wa hakina hadhi kati ya Washirikahawa wa Muungano.

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    8/21

    PAGE

    14

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    15

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    14

    i m e r u d iziara yawiki tatuya nyum-bani Zan-

    zibar na nina habari njema,kwamba kote nilikopita Pemba na Unguja kunadalili za kusonga mbelekama jamii, kama taifa.

    Kwa mfano, kisiwani Pembanimekuta barabara inayoi-unganisha miji midogo yaMzambarauni Takao, Wing-wi Mapofu, Finya na Mzam-barauni kwa Kyarimu na ileinayoziunganisha Likoni naKangagani zikiwa zimemal-izika. Barabara ya Konde-

    Wete imetekelekezwa kamaambavyo siku ya kujengwaya Wete-Chake isivyofaha-mika.

    Lakini kando ya barabarazote hizo, mumeota vijumbavizuri vya kudumu vya mat-ufali. Baadhi yake vilizoelekakushuhudiwa tu kwenye mi-taa ya Msasani, Dar es Sa-laam au Mazizini, Unguja.

    Nimeambiwa kasi hii yaujenzi imechochewa na fidiaya wale waliovunjiwa nyum-ba zao kupisha ujenzi wabarabara, kupanda kwa beiya karafuu na pia Wapembawanaoishi nje ya nchi ambao

    sasa wameamua kuelekezanguvu zao nyumbani. Ma-hala palipoangushwa mba-vu za mbwa, pameinuliwanyumba ya tufali la kuchon-ga.

    Kisiwani Unguja halikad-halika. Maeneo ya mijiniyanazidi kushuhudia ujenziwa majengo mapya, makub-wa na ya kudumu. Mitaaya Michenzani na Darajanikumewekwa taa zinazotu-mia nishati ya jua. Angalauusiku unakuwa na mwan-gaza wa kuonana kama sikuoneana.

    Kumbuka kuwa nazung-

    Na Mohammed Ghassani Ngurumo la Mkama Ndume

    umzia miaka mitatu ya ku-tokuwapo kwenye ardhi yakwetu. Ni kipindi kifupi mnokurudi nikakuta majengokama yale ya Mamlaka yaMapato ya Zanzibar na ujen-zi unaoendelea kwa kasikwenye eneo la Shangani.Maduka ya kisasa Mji Mkon-gwe na hata jengo jipya laBandari ya Malindi.

    Mote pia Pemba na Ungu-ja nimekutana na wavujajasho wakisaka tonge zaokwa juhudi kubwa. Vijana,watu wazima, wake kwawaume, wanaendelea ku-faya kazi za kukimu maishayao. Hili la kuendelea ku-

    fanya kazi nalisisitiza kup-ingana na dhana potofu ili-yojengeka kwamba watu wapwani, Wazanzibari tukiwa-mo, ni wavivu na mamwinyiwasiojiweza, wasiojishika.

    Hapana. Nimeikuta mikonodada yangu mwenye umriwa miaka 45 ikiwa imezidikusinyaa na kuwa migumukwa kazi za sulubu. Hatanilipoondoka akanifungiapepeta kutokana na mpun-ga alioulima, akauvuna naakautwanga kwa mikonoyake mwenyewe. Nimepiki-wa ndizi mbivu ya Mkono waTembo iliyolimwa na mamayetu mwenye umri wa kari-

    buni miaka 70 sasa.

    Ninalotaka kusema hapa nikwamba watu wangu, Wa-zanzibari, si wavivu na ha-wajasita kufanya kazi. Ha-wajaacha kujituma.

    Ikiwa miundombinu yabarabara na majengo na ku-vuja jasho ni dalili ya kuson-ga mbele kimaendeleo, basitukubaliane kwamba Zan-zibar inaelekea kwenye njiasahihi ya maendeleo. Lakinikuna walakini.

    Miaka mitatu ya kuishi kan-do ya jamii yangu imeni-wezesha kuyaona yale am-

    Meli ya MV Maendeleo ikipakia k arafuu kwenye bandari ya Mkoanikisiwani Pemba.

    Tukipima maendeleo kwa kutoendelea,hatutaendelea

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    9/21

    PAGE

    16

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    17

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    16

    bayo kama ningelikuwamondani yake nisingeliyaona.Mojawapo ni huku jamii yan-gu inavyojipima maendeleoyake kwa kutokuendeleakwake. Na hapa nitapiga mi-fano miwili mitatu.

    Kule dikoni kwa samakiNungwi, kaskazini Unguja,nilikutana na mnada. Wavuvihuwatoa samaki wao mojakwa moja madauni na kujakuwabwaga chini ya Mkun-gu. Dalali wa serikali anawa-tia bei na baadaye mnunuzimwenye fedha nzuri anaka-bidhiwa. Samaki hawa wa-nagaragara mchangani,wanangongwa na nzi na ku-pigwa na jua.

    Kando kidogo, serikali ili-jenga soko dogo lakini zuri,ambapo shughuli hizozingefanyika. Lakini hazi-fanyiki. Bado watu wanguwanaona kuuza samaki so-koni kutawagharimu zaidi,pengine kwa kulipia kodi ya

    jengo. Hivyo, wanabakia nauholela wa kibiashara.

    Mfano huu wa samaki waNungwi unazaa mwenginendani yake. Bei ya samakiimepanda sana. Mtungowa samaki ambao sasa un-agharimu shilingi 20,000,miaka mitatu nyuma un-geuzwa kwa 7,000, ingawamtu aliyeweza kununua sa-maki hao kwa bei hiyo ya

    mwaka 2010 ndiye yule yule

    anayeweza kuwanunua leokwa bei hii ya 20,000.

    Hili linasema kwamba kipatokimeongezeka, lakini halise-mi kwamba maisha ya mtuhuyo yameimarika. Sijauliziawala sijataka kujua kuhusukima cha pato apatalo mlajiwetu wa samaki wa shilingi20,000. Nasikia Serikali yaUmoja wa Kitaifa imeongezamshahara, lakini hauwezikuwa umeongezeka maratatu kama alivyoongezekaTasi wa Nungwi.

    Hata hivyo, wakati naon-doka nikawasikia baadhi yaviongozi wa serikali waki-

    jisifia kwamba hilo la ku-

    ongezwa kwa mishahara ni

    hatua kubwa ya maendeleoambayo haikuwahi kupig-wa kwa miaka kadhaa hukonyuma. Huko ni kuyapimamaendeleo kwa kutokuen-delea kwetu. Kwa hali hiyohatutaendelea sana na autukuwa tunapiga hatua ndo-go ndogo kama ngoma yambwa kachoka, huku tuki-

    jisifu kwamba tunasongambele.

    Kama nilivyotangulia kuse-ma, nimewakuta watuwakiumuka jua-mvua ku-saka tonge yao. Zao la kara-fuu limeendelea kuzaliwakwa wingi kisiwani Pemba.Mchana nimewakuta watuwakiwa mitini wameitawa

    mikarafuu, mapakacha na

    vingowe vyao juu na mapoloyao chini, watoto wao wa-naokota vitawi na au wana-chuma zilizo matawi ya chini.Jioni nikawakuta wakizin-yambua, asubuhi wenginewakizianika, na wenginewakiwa wamezipakia kwe-nye magari ya ngombe kuz-ipeleka vituo vya Shirika laBiashara la Zanzibar (ZSTC)kwenda kuziuza.

    Katika mtiririko huo sijaonalililobadilika ingawa naambi-wa bei ya karafuu imekuwaya juu sana. Miaka takribani200 ya kuwa na mkara-fuu visiwani Zanzibar, badomkulima anapaswa kutu-mia mbinu zile zile za Sul-

    tan Barghash bin Said katika

    kuzivuna, kuzitayarisha nakuziuza.

    Licha ya kuwa kwake zaolinaloiingizia nchi fedha ny-ingi za kigeni, bado hakunamaendeleo kwenye sayansiya ukulima wake. Hatuwezikupima maendeleo ya kilimocha karafuu kwa kuangaliabei yake tu, ambayo kwa vy-ovyote inategemeana sanana soko la dunia na amba-lo linaathiriwa pia na ainaya mazao tunayoyapelekahuko.

    Tubadilike na tuibadili nchi.Na haya yamo ndani yauwezo wa akili zetu kamayalivyo kwenye mikono yetu.

    KWA MAPUMZIKO

    PEMBAKwa mapumziko ya rahana furaha ukiwa kisiwani

    Pemba, fikia kwenye Hoteliyenye huduma za uhakika,

    vyumba vyenye nafasi yakutosha

    Huduma mbali mbali pia zinapatikana kupitiakwenye Hoteli yetu kama, ukodishaji wa Pikipiki,boti, na kupelekwa kuzamia huko Misali.

    www.zanzibaroceanpanorama.com

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    10/21

    PAGE

    18

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    19

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    18

    Moja ya urathi waMheshimiwa NelsonMandela barani Afrika

    ni utawala wake uliongozanchi ya Afrika ya Kusini kwamisingi ya usawa, haki nauadilifu wa hali ya juu. Mpakaleo hii barani Afrika ni wach-ache walioweza kufikia roboya vigezo vya utawala wakijasiri wa Mandela na kuon-dosha ile dhana ya kwambaAfrika haijaweza kutoa kion-gozi na uongozi wa uadilifuwa hali ya juu.

    Tanzania nafasi hii inayohasa kwa sasa chini yautawala uliobakia wa Dkt.Jakaya Kikwete ikiwa niaya kweli ipo ya kuutazamautawala kama nyenzo yamabadiliko makubwa kwa

    faida ya wananchi na nchiyenyewe.Kilichonivuta kuandikamakala haya ni tukio la kari-buni lililomfanya Kikwetekuwaita wapinzani Ikulukuzungumzia Rasimu yaKatiba kwa misingi ya umojana kuwahakikishia wanan-chi kwamba katika sualahili la Katiba hakuwa tayarikuyumba kwa sababu tu yawachache wanaohisi kuwandio wenye hati miliki ya nchihii.

    Kauli za mawaziri wake nakebehi walizozionyesha nda-ni ya bunge ziliashiria ubabewa kufuta imani za wap-inzani katika upatikanaji waKatiba ya nchi kwa wananchiwote. Kuwaita na kuzung-

    umza nao katika mazingiraya upendo, heshima na fu-raha imerejesha imani kwetusisi wananchi wa kawaidakwamba katika uongoziKikwete bado ni mwokozina pengine muumini pekeewa kweli wa mabadiliko yaKatiba yatayowajumuishawananchi wote.

    Ninaamini kwamba kwakuridhia uundwaji wa Serikaliya Umoja wa Kitaifa Zanzi-bar na kutoingilia mchakatowa mabadiliko ya Katiba yaZanzibar ya mwaka 2010,na kuachia kauli ya waliowengi katika kura ya maoniya kuidhinisha mabadilikohayo alionyesha upevu wakewa kisiasa na imani yake juuya demokrasia. Wazanzi-

    Kikwete akithubutu,ataweza

    Na Farrel Jnr Foum Mazungumzo baada ya Habari

    bari tutaendelea kumshukurukwa kuikubali kauli yetu juuya mabadiliko ya kiutawalaVisiwani ambayo pia ilikuwachanzo cha msukumo wa

    haya mabadiliko ya Katiba yaJamhuri ya Muungano.

    Kinachostaajabisha ni hawawabunge wa Zanzibar waliod-harau usimamizi wa nchi yaokwa kuruhusu mabadilikoambayo yangelivua ngao yaZanzibar iliowekwa maalumkujilinda na wachache ambaowangeliweza kutumia mwan-ya wa wingi wa wabungebadala ya mfumo wa thuluthimbili kuleta mabadiliko am-bayo yangeweza kuwa na

    athari kubwa hata juu ya kue-ndelea kuwepo kwa Zanzibarkama nchi kamili inayojiende-sha na kujitegemea.Kama Kikwete bado ana niaya kuweka urathi mfano waMandela, kipindi cha miaka hiimiwili na nusu iliobakia akiwaRais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanganyika na Zanzibarbasi lazima awe tayari kuwak-abili wakereketwa wenzakewanaofikiri wana haki zaidi yamaamuzi ya nchi na uendesh-waji kuliko wananchi wengine.

    Ningelimshauri Kikweteahakikishe kuanzia sasa kuwaanarejesha heshima yote yautawala kwa wananchi kwakusimamia ipasavyo haki nauadilifu kama kanuni za uon-gozi nchini. Akiwa mwenyekitiwa CCM na Rais wa Jamhurianazo nguvu za kutosha zakurejesha heshima ya chamachake kama taasisi ilio safi nainayoendeshwa kwa uwazina pia serikali ilio tayari kusi-

    mamia haki, sheria na uadilifu.Hakuna nchi ilioweza kupigahatua bila ya nguzo imara zademokrasia ilio wazi na yenyekufuatwa na kuthaminiwa

    hasa na watawala. Huwezikuwa mfuasi wa demokrasiabila ya kuwa na upinzani uliona kila nyenzo ya kujiende-sha bila ya vitisho vya ainayeyote. Upinzani sio uaduibali ni chachu ya maende-leo ya nchi kwa kila sekta.Kuwathamini, kuwalinda nakuwaheshimu waliothubutukuwa na mawazo tafauti ndiolengo la demokrasia makini nandicho hasa kitachomtafauti-sha Kikwete na utawala wakena wale waliotangulia.

    Kabla ya kumaliza muda waketungelitegemea kuwa mbaliya kwamba kisiasa marekebi-sho ya Katiba yatatoa fursakubwa ya kupatikana ma-geuzi, kwa mfano pendekezola kuundwa Tume ya uchaguziiliojengeka kiuwazi na ki-uadilifu, bado kuna mambo yakiutawala yanayohitaji kuta-zamwa upya.

    Ikiwa Kikwete anayo damuinayomchemka ya kuachaurathi atakaokumbukwa

    nao basi lazima mahakama,vyombo vya sheria na vikosivya usalama vifanyiwe ma-geuzi mapya yanayoendanana wakati tulionao. Nina aminikwamba matatizo tuliyo nayosasa yamesababishwa na jinsitulivyozivamia siasa za ush-indani wa vyama vingi bila yakufanya mageuzi katika taa-sisi za serikali hususan katikasekta inayosimamia sheria zanchi. Jeshi la polisi, kwa mfa-

    no, limekuwa likitumika zaidikisiasa badala ya kuimarishausalama wa nchi.Mwisho ni maendeleo ya nchina wananchi wenyewe. Bila

    ya sera zilizojengwa kwa arimpya ya kuhakikisha unafuukwa wananchi na maendeleokwa nchi bado hataweza kui-weka nafasi yake katika safuya mashujaa waliothubutuna kuweza barani Afrika. Kwakipindi hichi cha miaka miwilina nusu iliobakia, Rais an-gelijaribu kuhakikisha serikaliyake inaviweka wazi vipaum-bele kuanzia ujenzi wa makazinafuu ya wananchi, uimarish-waji wa elimu, usimamizi borawa sera za afya, upatikanaji

    wa maji safi na umeme wakudumu. Kwa kipindi kilicho-bakia haya yakiwa yatatazam-wa kwa uangalifu zaidi tut-aweza kupiga hatua kubwa nakujenga msingi wa maende-leo kwa anayemfuatia. Nimal-izie kwa kumkumbusha yotehaya yanawezekana ikiwa niathabiti ipo, timu imara ipo nasera safi zipo. Kama alivyo-likingia kifua suala la mabadi-liko ya Katiba ya Muungano nakuhakikisha linakwenda kwanguvu za wananchi basi na

    haya manne tulioyaorodheshayanawezekana. Ikiwa suala laKatiba litapita bila ya shenge-sha za wafurukutwa na hayamaeneo ya maendeleo tu-lioyaorodhesha yatafanyiwakazi ipasavyo basi historiaitamkumbuka Rais Kikwetekuwa miongoni mwa walio-thubutu kuleta maendeleo yakweli kwa wananchi na nchina akaweza.

    Rais Jakaya Kikwete [kulia] akimkaribisha Mbunge Tundu Lissu Ikulu

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    11/21

    PAGE

    20UKURASA

    21

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    20

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    Katika agizo lake kwenyeSemina Elekezi kwa Wa-tendaji wa Serikali kule

    Ngurdoto, Arusha, mwanzonimwa muhula wa uraisi wake,Rais Jakaya Kikwete alisemakile alichoona yeye kwenyeMuungano si kwamba kuli-kuwa na tatizo la msingi, balikukosekana tu kwa mazun-gumzo baina ya pande mbilizinazounda Muungano we-nyewe, Bara na Zanzibar.

    Kwa hivyo, akaitisha harakaharaka utaratibu wa pandehizo mbili kukutana ili anga-lau watu wakutane kwa ku-nywa chai na kahawa pamoja.

    La kukutana kunywa chai nahuku mnazungumzia mamboyanayohusu hatima ya taifa ni

    jambo zuri sana, lakini mwe-nendo wa mambo katika ku-kutana huko daima ulikuwana umeendelea kuwa na wa-lakini.

    Unakumbusha kile kisa ki-nachozungumziwa kwenyekitabu cha Mohammed Saidcha Historia ya AbdulwahidSykes. Kwenye kitabu hicho,mwandishi anazungumzia tu-kio la tarehe 10 Agosti 1957,wakati chama cha kupiganiauhuru cha Tanganyika, Tan-ganyika African Union (TANU),kilipokuwa kinafungua tawilake katika mtaa wa Mvita,nyumba namba 10, Dar es Sa-

    laam.

    Katika sherehe hiyo muhi-mu, TANU iliwaalika wajumbewa Baraza la Kutunga Sheria,wengi wao wakiwa machi-fu kama vile Chifu KidahaMakwaia, Humbi Ziota, Msa-bila Lugusha, Mwami TheresaNtare na wengineo na ikawa-kirimu waalikwa wao vitafu-nio, vinywaji baridi na chai.

    Katika kutoa shukrani za TANUkwa wanachama wa TANU,Mwalimu Julius Nyerere alika-mata kikombe cha chai na ku-kionyesha juu kwa wasikilizajiwake. Akawaambia wasidhanikwamba kitendo cha kumpamtu chai ni kitu kidogo, maanakuna watu wameiuza nchi hiikwa kupewa kikombe cha chaina wakoloni.

    Upande wa Zanzibar kwenyeMuungano huu unaheshimusana njia ya mazungumzokama suluhisho la pekee kati-

    ka kufikia utatuzi wa matatizoyanayolikabili taifa. Lakinimazungumzo yenye uwezowa kutoa suluhisho ni yaleyanayozingatia nini kinazun-gumzwa, nani wanazungu-mza, vipi na kwa nini yana-zungumzwa.

    Kila moja kati ya maswali hayalina maana kubwa kwa hiti-misho na suluhisho litokana-lo na mazungumzo yenyewe.

    Mazungumzo haya yaliyo-kuwa yanafanyika baina yaSerikali ya Jamhuri ya Muun-gano kupitia Ofisi ya WaziriMkuu na Serikali ya Mapin-duzi ya Zanzibar (SMZ) kupitiakwanza Ofisi ya Waziri Kion-gozi na baadaye ya Makamuwa Pili wa Rais ni mazungu-mzo kwa manufaa ya mazun-gumzo tu na sio mazungumzokwa manufaa ya suluhisho.

    Msimamo huu si wa kibu-busa. Una mifano hai ndaniya historia ya karibuni kabi-sa ya mazungumzo yenyewe.Mmojawapo ni ule wa Ripo-ti ya Baraza la Mapinduzi laZanzibar ya 2003.

    Tarehe 29 Mei 2003, Ikulu yaZanzibar ilichapisha Ripoti yaBaraza la Mapinduzi juu yaMatatizo na Kero za Muunga-no na Taratibu za Kuziondoa,ambapo katika sura yake yatatu, ripoti hiyo ilitoa orod-ha ya mambo yanayopaswa

    kuondolewa katika Muunga-no. Mambo hayo ni:

    i. Mafuta na Gesi Asiliaii. Elimu ya Juuiii. Postaiv. Simu (Mawasiliano)v. Biashara ya Njevi. Kodi ya Mapatovii. Ushuru wa Bidhaaviii. Usafiri wa Angaix. Takwimux. Utafiti

    Na Riziki Omar Mkeka wa Mwana wa Mwana

    xi. Ushirikiano wa Kima-taifa

    xii. Leseni za Viwandaxiii. Polisixiv. Usalama

    Katika kuhakikisha kuwa hayayanatekelezeka, SMZ ilitakakuwepo kwa misingi mitano yakuzingatiwa, ambayo ni:

    a. Masuala ya Muunganoyalindwe kwa misingi yaKatiba na Sheria badalaya siasa na maelewano

    b. Muungano uwe na mae-neo machache yanayo-weza kusimamiwa nakutekelezwa kwa urahisi

    c. Muungano uainishewashirika wake wakuu,mipaka na haki zao

    d. Muungano utowe fur-sa sawa za kiuchumikwa pande zote mbili zaMuungano

    e. Lazima pawe na Muun-gano unaoweza kuhimilimabadiliko ya kisiasa nakiuchumi

    Hivi ndivyo SMZ ilivyosematangu mwaka 2003; na kwahakika kama mwakilishi wawananchi wa Zanzibar seri-kali hiyo ilikuwa imesema vileambavyo Wazanzibari wame-kuwa wakisema tangu siku zamwanzo za Muungano huu.Ni wazi kuwa ripoti hii ya SMZimewahi kuweko mezani kwaOfisi zote mbili, ya Waziri Mkuuna Waziri Kiongozi (na baadayeMakamu wa Pili wa Rais).

    Lakini kinachotokezea kilabaada ya kikao cha watendaji

    wakuu wa serikali hizo mbili, nitaarifa ya kuhuzunisha pana-pohusika kile hasa kinachohi-tajika kutatuliwa.

    Kwa mfano, taarifa ya kikaocha mwisho cha mwezi Mei2009 iliyotolewa na Ofisi yaMakamu Rais, Idara ya Muun-gano, ilisema kwamba kerotatu za Muungano zilikuwa zi-meshafutwa na kuanzia hapohazikuwa kero tena.

    Kero hizo ni Tume ya Haki zaBinadamu, Uvuvi wa Ukan-da wa Bahari na Shughuli zaBiashara ya Meli. Katika mawi-li ya mwanzo, kufutwa kwakekutoka orodha ya kero ni kwamambo hayo kukubalika ras-mi kuwa ya Muungano, am-bapo sasa upande wa Zanzibaruliridhia. La mwisho kufutwakwake ni kwamba Zanzibar ili-ruhusiwa kuendesha shughuliza biashara ya meli kwa kushi-rikiana na Tanzania Bara.

    Hii maana yake ni nini? Nikwamba, kumbe hakuna pen-dekezo lolote la kupunguzaidadi ya mambo ya Muunga-no, kama yalivyo matakwaya Zanzibar, lililoweza kuwalinajadiliwa na vikao hivi vyapande mbili; maana chini yaChama cha Mapinduzi (CCM)wahusika wa vikao hivi wa-lishaamua kuwa kupunguzaorodha ya Mambo ya Muun-gano hakuwezi kuimarishaMuungano, bali kinyume chakendicho sawa!

    Yaani, kuimarisha Muunganokuna maana moja tu, nayo ni

    ama kukichukua kila cha Zanzi-bar na kukifanya cha Muun-gano na, au, kukifanya kila ki-lichoko Tanzania Bara kivukemaji na kiwe cha Zanzibar.

    CCM na Serikali zake zimeufa-nya Muungano huu ushabi-hiane sana na kile kisa chaMfalme Jeta aliyemo kwenyeriwaya ya Kusadikika ya Mare-hemu Sheikh Shaaban Robert.

    Mfalme huyu alikutwa namjumbe wa Kusadikika akiwaamekaa katika eneo ambapomto uliokuwa unakokozoa kilakitu mawe, magogo, majen-go, n.k. unatiririkia kinywanina kuishia tumboni mwake, la-kini kila mara alisikikana akilia:Njaa! Njaa! Kiu! Kiu!

    Hivyo ndivyo Muungano wetuulivyofanywa, kwamba uweunakula na kunywa kila kitu nabado kila siku uwe unalalamikakufa njaa na kiu. Na ili kuufa-nya usife, wakubwa wanaa-mua kuulisha kila cha Zanzibarna kila cha Tanzania Bara.

    Swali ni ikiwa je, katika kum-lisha Mfalme Jeta huyu, Zanzi-bar ilitenzwa nguvu? Jibu mo-

    jawapo ni kwamba hapana,viongozi wa Zanzibar wana-ohudhuria vikao hivyo wame-kuwa wakienda kunywa chaitu, huku wakimruhusu Mfal-me Jeta ameze kila kile kilichocha Zanzibar, halafu wakarudiKisiwandui kusema yasiyoe-leweka.

    Zanzibar iuzwapo kwa kikombe cha chai

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    12/21

    PAGE

    22UKURASA

    23

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    22

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    Mtaani kwetu,Mwembe-tanga, Unguja

    mjini, kulikuwekomzee akiitwa AliMrandazi, mpole,hapitwi na sala ya

    jamaa msikitini. Ali-kuwa mtu wa watu,akisomesha burewatoto msikitini, nandiye pekee tuliom-tegemea mtaani ku-

    kosha maiti. Hajako-sekana katika misibana harusi za watu naalitumika kwa moyosafi katika shughulihizo.

    Kila asubuhi alfajiri,na hata kama ina-nyesha mvua, BwanaAli ataelekea Hos-

    pitali ya Mnazi

    Mmoja huku akishiki-lia kikapu mkononikilichojaa machung-wa, maembe, ndizimbivu na matufaa,ikitegemea ni msimugani wa mazao hayo.Huenda kuwatembe-lea wagonjwa katikavyumba vyote vyahospitali, na anapofi-ka katika kitanda chamgonjwa husimama

    na pamoja naye hu-soma Suratul Faatihana kumwachia tundakitandani. Hiyo iliku-wa katika miaka yahamsini na sitini.

    Karibuni nilipofi-ka matembeziniMwembetanga ni-likutana na watuambao bado wanam-

    kumba Mzee AliMrandazi. Waliniarifukwamba tangu ali-pokufa mzee huyomiaka mingi iliopitahajachomoza mtumwingine kuchuku-wa nafasi ya kuten-da mambo ya kherialiyokuwa akiyafanyamtaani. Hapa Ujeru-mani ninakoishi maranyingi kazi za kujito-

    lea kama alizokuwaakizifanya marehe-mu hufanywa namakanisa au jumuiyaza kutoa misaada yakiutu ambazo nyingi-ne zina wafanya kaziwanaolipwa.

    Mtaa wangu waRondorf ninakoishikwa miaka 37 sasa

    unanikumbusha ulewa utotoni mwanguwa Mwembetan-ga. Katika mtaa huuwa sasa kuna watuwachache walio nasifa karibu sawana za Ali Mrandazi,wako tayari wakatiwowote kuwasaidiawenziwao waliokokatika shida. Kunawale wanaotenga

    masaa fulani katikawiki kwenda mahos-pitali kuwapumbazawagonjwa kwa ku-wasomea vitabu vyahadithi, magazeti aukucheza nao karata.Kuna wale wanao-safisha magugu yamtaani yasiokuwakaribu na nyumbazao, ambalo ni juku-

    Na Othman MirajiWaraka kutoka Bonn

    Serikali si mama walababa yetu, ni sisi sote

    mu la baraza la mji.Hapa Ujerumanikuna milolongo yaharakati za watuwenyewe kushirikikatika mambo yaliokwa maslaha yao yapamoja. Raia wana-

    fika hadi ya kujiundiajumuiya ndogondogo(Burgerinitiatives),bila ya urasimu,zenye kupiganiamaslahi yao ya pa-moja, wanaelekezafikra na ubunifu waokujituma na kujaribukuyatanzua matatizoyao madogomadogobila ya kuitegemeaserikali. Jumuiya hizohuwa mbioni kufa-nya mashauriano namaafisa wa serikalina kuwabinya kwahoja ili zitafutwe njiaza haraka na muja-rabu ili wajirahisishiemaisha yao.

    Ninapokuweko Zan-zibar mjini ninajiulizakwa nini raia wana-bakia tu wanalalamaikiwa kwa masikumagari ya kuzoleataka hayajatokeakwenda kuchukuwataka majaani? Kwanini wanaendeleakuziangalia tu takazile zikirundikanambele ya macho yao,huku nzi na mapa-nya yakisheheni nakuhatarisha afya zawakaazi? Kwa nini

    wenyewe raia hawa-chukui masepeto nakujiondoshea udhiahuo?

    Fleti za Kilimani, Kik-wajuni na Michenza-ni zimejengwa na se-

    rikali zaidi ya miaka45 iliopita na kupewawananchi, na hivisasa ziko hoi, zina-hitaji matengenezoau angalau kutiwarangi nje. Lakini yao-nesha wakaazi mita-ani wanaingojea seri-kali iwafanyie kazihiyo kama mwanzoilivowajengea. Nahisiraia wenyewe ina-bidi wabuni fikra zakujiondoa katika halihiyo. Kwa masikitikotumejenga utama-duni wa kuichukuliaserikali kama mamana baba, tunain-gojea itufanyie kilakitu, itulishe chakulamdomoni.

    Fleti hizo zilijengwawakati wa utawalawa rais wa kwanza,Sheikh Abeid Kar-ume. Yeye alitakakutimiza malengo yaMapinduzi ya mwa-ka 1964 kuwapatiawananchi nyum-ba bora za kuishikama binadamu.Nikikumbuka nyingiya nyumba hizo nakwa sehemu kub-wa zilijengwa kwa

    nguvu za kujitolea zawananchi wenyewe.Ziko baadhi zilijeng-wa kwa msaada wakiufundi wa Wajer-umani. Wakati waMzee Karume sikuya jumamosi wafa-

    nya kazi wa serikali,akiwemo mwenye-we rais na mawaziriwake, watoto washule na watu wamitaani walijitoleakwa saa chache kilammoja katika kaziya pamoja, pia ku-safisha mitaa, kwamanufaa ya jamiinzima. Kiongozi huyoalijenga mwamko wawatu wajitegemeewenyewe kutokangazi za chini, hivyokuipunguzia serikalimzigo.

    Miradi kadhaa yamaendeleo ya jamiiambayo minginebado ingali hai hadileo ilianzishwa naKarume kutokana namoyo wa kujitoleawenyewe wananchi.Na alifanikiwa zai-di kwa vile rushwana wizi wa mali zaumma ni mamboambayo yalikuwahayana nafasi kabisa,mwiko, katika uta-wala wake.

    Tunapozungumziahaja ya utawala borabasi tuanzie mitaani,

    wenyewe raia tujiuli-ze nini cha kujifanyiasisi wenyewe, kwaakili na nguvu zetuwenyewe, kabla yakuwauliza wenginenini watufanyie. Seri-kali ni wewe na mimi

    pia, na ili kuhakikishahilo ni juu yetu sotekuthibitisha kwambatunachangia kiviten-do katika maslahaya jamii, kuanziamtaani. Kukaa viji-weni tu, kulalamana kupiga maso-ga ambayo wakatimwingine hayanamaana, tukitegemeamambo yatabadilikana maisha yetu yakesho yatakuwa borakuliko ya leo, huko nikujidanganya.

    Serikali inakuwa nadhamana na ina-andamwa na raiaitimize wajibu wakepale raia wenyewenao wanapooneshadhamana ya kwendambio kwa upandewao na kuazimia kik-weli kufanya maishayao yawe bora, bilaya kutegemea watuwengine wawahi-mize. Hamna njia yamkato kufikia maen-deleo. Ali Mrandazihakuwa walii, ali-kuwa binadamu wakawaida tu, kamawewe na mimi.

    Jumba Namba 4 Mtemani Wete Pemba, moja ya alama za mafanikiona pia kurudi nyuma kwa Zanzibar.

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    13/21

    PAGE

    24

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    25

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    24

    TANBIHI

    Hii ni sehemu ya tatu namwisho ya makala hayaambayo kwa mara yamwanzo yalichapishwakwa jina la Tungo zaBwana Kimbunga: Haji

    Gora Haji. Yamean-dikwa na mtaalamuwa lugha ya Kiswahilimzaliwa wa Uholanzi,PROFESA RIDDER H.SAMSOM, kuelezea kaziza kifasihi za gwiji wasanaa ya ushairi kati-ka zama hizi visiwaniZanzibar, Haji Gora Haji.Tunayachapisha tenahapa yakiwa yameha-ririwa kidogo kuakisiwakati wa sasa.

    Sifa ya tungo zaHaji Gora siyokatika umbo

    tu la upinzani,yaani kujibizanana kuhitilafiana,pia maudhui yake

    yameelezwakwa taswirazinazohalifiana.Mwenyeweamesema kuwamtindo huu simbinu wala

    hekima, lakini nisiri ndani ya siri.

    Kwani ndichoKimbunga ganikinachoangamizakila chenye nguvu

    na kukiachilia kila chenye udhaifu?

    Kimbunga mji wa Siyu, kilichowahi kufika

    Si kwa yule wala huyu, ilikuwa patashika

    Kimeingowa mibuyu, minazi kunusurika

    Nyoyo zilifadhaika

    Yalizuka majabali, yakibirukabiruka

    Zikadidimia meli, ngarawa zikaokoka

    Kimbunga hicho kikali, mavumbi hayakuruka

    Nyoyo zilifadhaika

    Nyumba kubwa za ghorofa, siku hiyo zimeruka

    Zikenenda kwa masafa, kufikia kwa kufikaVibanda vyao malofa, vyote vikasalimika

    Nyoyo zilifadhaika

    Chura kakausha mto, maji yakamalizika

    Pwani kulikuwa moto, mawimbi yaliyowaka

    Usufi nusu kipeto, rikwama limevunjika

    Nyoyo zilifadhaika

    Kuna kikongwe ajuza, viumbe kimewateka

    Hicho kina miujiza, kila rangi hugeuka

    Watakaokiendekeza, hilaki zitawafika

    Nyoyo zikafadhaika

    Vipi meli zikadidimia na ngarawa kuokoka, nyumba za ghorofa zikaruka na vibanda kusalimika?Sitiari yake ya Kimbunga ina utata mkubwa, ni fumbo hasa. Je, hicho Kimbunga ni sitiariinayotoa picha ya mtu wa tabia fulani, au kinawakilisha mabadiliko ya ghafla katika jamiiambayo watu wenyewe walikuwa wameathirika kwa namna mbalimbali?

    Lakini kilikusudia si kwa yule wala huyu mji wa Siyu, kilichowahi kufika, mji ambao hadi sikuhizi una jina kwa sababu ya ushujaa wake katika ukinzani wake, pamoja na Waoromo na Waso-mali, dhidi ya utawala wa kigeni, yaani wa Kireno na hasa wa Kiomani.

    Je, Kimbunga ni hayo mabadiliko ya ghafla ya mwaka 1964 ambayo watu wameyaita map-induzi. Na nini hasa kimepinduliwa? Na ikiwa ni hivyo, huu upepo wa malaleji katika shairi laShuwari alilotunga Haji Gora baadaye unawakilisha mabadiliko gani?

    Shuwari ya malaleji, imeshangaza wahengaKimya wake uvumaji, tafauti na kimbungaLakini popotoaji, sitambuwi zake kungalporomosha milima, kugeuza tambarare

    Ilizuka aridhini, kuzagaa kwenye angaUshabihi wa tofimi, kila kimoja kugonga

    Sitiari za Mzee waKimbunga: Haji Gora(Sehemu ya Tatu)

    Mzee Haji Gora

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    14/21

    PAGE

    26

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    27

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    26

    Sinini wala sinini, hakuna kisichotingalporomosha milima, kugeuza tambarare

    Haipulizi vuvuvu, jakusi na mwanashangaBali chake kinyamavu, sio mzaha narongaKimeleta uokovu, nakupeperusha jangalpomomosha milima, kugeuza tambarare

    Kwa kote ilifirimba, pwani na kwenye viungalkavugika myamba, na mawe yakawa ungaUtahisi kama kwamba, kilobomowa mizingalporomosha milima, kugeuza tambarare

    Malaleji (au maleleji) ni upepo unaobadilikabadilika, hasa katika miezi ya Aprili na Novemba,lakini kamusi ya kibaharia ya Prins inaeleza kuwa huko Tumbatau unavuma mwezi wa Juni pia.Ni majira ya upepo shwari ambao hujui unatoka sehemu gani. Hata hivyo iporomosha milima,kugeuza tambarare inawezekana ni mtu mkimya mwenye nguvu nyingi za kuweza kuwashawi-shi watu wengi.

    Lakini ikiwa kimbunga ni sitiari ya mabadaliko ya kijamii, kwa nini maleleji isiwe hayo. Mabadilikotangu mwaka 1985 huko Zanzibar, wakati wa vyama vingi na kulegezwa kwa masharti ya kiu-chumi, kulipa soko uhuru fulani, mabadiliko hayo yote yalikuwa yakienda shwari na upepo huuhaukuvuma vuvuvu.

    Fikra kuu ya Mzee Haji, dhana anayoshikilia na kusisitiza kila mara ni kupinda na kupindua,

    kuweka sambamba vitu viwili vinavyogongana na kushindana, kuweka juu chini na chini juu,kuonesha matukio yatukiayo kinyume na matarajio.

    Alivyosema, ni siri ndani ya siri, yaani kimbunga kinavunja yaliyo makubwa, lakini yaliyo madogohayavunjwi nacho, kumbe malaleji ambayo ni kinyume cha kimbunga, imefika kote na kubomoakila kitu, hata hivyo imeleta usalama

    Baada ya Kimbunga na Shuwari ilikuja Mkasa Namba Mbili:

    Kuna kinyozi ambae, kunyowa kiendeleyaKilofanya nishangae, anyolewae aliyaHata na kinyozi nae, hajimudu kwa kuliyaWote wanacholiliya, wala hakijulikani

    Hawataki kueleza, kilichowafikiliya

    Kama utawauliza, kama kwamba wachocheyaSauti zao hupaza, huzuni kuashiriyaBali wanacholiliya, wala hakijulikani

    Pengine yaweza kuwa, kwa ninavyofikiriyaAmbae ananyolewa, labuda anaumiyaKinyozi anaenyowa, kwa nini mbona aliyaBali wanacholiliya, wala hakijulikani

    Hiki ni kitandawili, kinachowategemeyaWateguzi mbali mbali, jawabu kukipatiya

    Nimeifunga kufuli, wafunguzi nangojeyaKipi kinachowaliza, haraka nitajiyeni

    Ajabu kubwa tena mtu mmoja anaumia akinyolewa, lakini anayemnyoa anaumia vivyo hivyo Baliwanacholiliya, wala halijulikani.

    Hatumo tena katika historia, tumefika kwenye siku za Ieo hii hii. Mtu wa tatu anapowakuta watuwawili wakilia katika hali kama hiyo, bila sababu kujulikana, atajaribu kuwapatanisha. Basi inavy-osemekana na kutangazwa Maridhiano ya Wazanzibari yamefikiwa karibuni tu.

    Tungo nyingi za Haji Gora Haji zinaeleza hali ilivyo: hali ya jamii, ya watu, ya historia, kwa kutumia

    sitiara zinazogongana, kuhalifiana na kuhitilafiana. Ndilo jambo na kinyume chakeTaswira anazotumia zinamfanya msomaji amtambue kuwa ni mtu anayejijua nafsi yake. Kwaurahisi anatambulika kama mtu wa pwani, Mtumbatu, Mswahili. Huenda msimamo wake umefi-chika, hutokea msimamo wake u wazi kabisa kama ulivyo katika mfano huo wa mwisho.

    Waswahili husema: kutoa ni moyo. Kinyume chake ni kunyang anya au kupokonya Muyaka binHaji el-Ghassany ameshughulikia suala hilo katika shairi la Kupewa:

    Semani nawapulika, siyo sambe kwamba siviSiwi cha mfunda koka, muawa na wavuviUnipile sikupoka, sikunyanganya kwa wiviNawauliza wakorofi, mnashika nta gani

    Nyanganya hukunyanganya na kuiba hukuiba

    Daima watu hufanya kupana vitu kwa hubaHilo mimi sikukanya na yangakwisha mahabaKupawa ndiyo taliba, kilicho changu mudani

    Naye Haji Gora Haji ameendeleza fikra hiyo na kuonesha imani yake katika shairi lake Mpewahapokonyeki, ambalo limeimbwa na kikundi cha Culture Musical Club na kunaswa sauti kwenyeCD yao ya Kidumbaki:

    Aliyepewa kapewa, naapa hapokonyekiKwa alichojaaliwa, Wallahi hapunguzukiUkimlilia ngowa, unajipatisha dhikiMpewa hapokonyeki, aliyepewa kapewaWewe ukifanya chuki, bure unajisumbuwa

    Mola ndiye atowae, akawapa mahuluki

    Humpa amtakae ambaye humbarikiNa kila amnyimae, kupata hatodiriki

    Wa tisa humpa tisa, wa moja haongezekiAlomnyima kabisa, hata akitaharukiAtabaki na kunasa, atakwama hanasuki

    Mola hutowa hidaya, tafauti na rizikiKwa anomtunukiya, huwa ndiyo yake hakiNa asiye mtakiya, huwa si yake laiki

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    15/21

    PAGE

    28

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    29

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    28

    Ninailinda na nitaendelea kuilinda haki ya Mzanzibari yeyote yule ya kutoamaoni yake kama anavyoruhusiwa na Katiba ya nchi kwani huu ndio msingi wademokrasia. Na wala siwafik kumpunguzia Mzanzibari yeyote uhuru wake wa

    kusema, wa kutoa maoni na wa kukusanyika katika vikundi. Hizo ni haki za kimsingimiongoni mwa haki za binadamu.

    Hofu na chuki hazina tena nafasi Zanzibar

    Lazima kila mmoja wetu awe imara naasimame kidete kuzilinda na kuziteteahaki hizo. Uhuru wa kusema na wa ku-toa maoni ni adhimu. Ni wajibu wetusote tuyavumilie maoni ya Wazanzibariwenzetu hata kama tunayaona maonihayo kuwa ni machungu au kuwa yanap-ingana na fikra zetu. Lazima tuulee natuustawishe utamaduni wa kukubalianakuhitilafiana.

    Lakini utamaduni huo hautoweza kustawiwala kudumu endapo pataibuka kikundicha wakereketwa wa imani yoyote au wachama chochote wanaojipa kazi ya kutu-kana, kuhubiri siasa za chuki na kusemauongo.

    Kwa bahati mbaya kikundi kama hichokipo na mara baada ya mara huibuka nahuanza kueneza siasa za chuki, kutoamaelezo ya uongo kuhusu historia ya ki-siasa ya Visiwa hivi.

    Akhasi zaidi ni kwamba badala ya kutu-mia hoja katika mijadala na midahalo yakekikundi hicho hutumia matusi na vitishodhidi ya mahasimu wake wa kisiasa. Ki-kundi hicho kina jumla ya watu wasiozidikumi hapa Zanzibar.

    Watu hao, wasio na lao jambo, hawamwakili-shi mtu yeyote yule bali kazi yao ni kuropokwakwenye majukwaa ya mikutano ya hadharabila ya kujali athari za kauli zao kwa waathirikawanaowatukana kila uchao.

    Hivi majuzi tulimsikia mkereketwa mmoja waCCM, Baraka Shamte, akiipotosha historia yakisiasa ya Hassan Nassor Moyo na pia akimka-shif kwa matusi Maalim Seif Sharif Hamadi.Mkereketwa mwengine alithubutu kutumiaukabila kuwatisha Wazanzibari wenye asili yaKihindi wenye kuupinga Muungano. Ni wazi

    kwamba alikuwa akiwalenga kina Ismail JussaLadhu wa CUF, ambaye ni Mwakilishi wa MjiMkongwe, na Mohamedraza Dharamsi waCCM, ambaye ni Mwakilishi wa Uzini.

    Tunawaambia wakereketwa hao na wenzaowachache kwamba Wazanzibari tumechoka namatusi yao na hatutaki kurudishwa nyuma.

    Siku za hofu, migawanyiko na machafukozimepita. Hazitarudi na wala hazitaweza ku-rudishwa. Siasa za chuki na za matusi hazinatena nafasi hapa Zanzibar kwani sote tunatakautulivu, amani na maendeleo.

    Mohammedraza Dharamsi, Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Zanzibar

    Na Ahmed Rajab Kalamu ya Bin Rajab

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    16/21

    PAGE

    30

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    31

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    30

    Tunayataka yote hayo kwasababu tumekwishaonahasara ya migawanyiko nachuki mambo ambayo ya-meipotezea nchi yetu hadhina mandeleo yake.

    Tunawaomba wananchi wen-zetu walio kwenye chama

    cha wakorofi hao wawakataeviongozi aina hiyo wenye ku-palilia chuki ya aina yoyote ile.

    Kwanza hatujui wakereketwahao wanamsemea nani.Hatujui wanamsemea Mzan-zibari gani.

    Tunachokijua ni kwambamatamshi yao yanakwenda

    kinyume na moyo wa Marid-hiano yaliyoleta faraja kubwaZanzibar pamoja na Umojawa Kitaifa. Kwa sababu yaMaridhiano hivi sasa hakunamtu anayejihisi kuwa yuko njeya serikali au anayefikiriwana serikali kuwa ni adui kwavile yeye ni mpinzani na hasaikiwa mtu huyo anaupinga

    Muungano.

    Serikali haiwezi tena kusemakuwa kuna wasaliti, mahainiau wapinga Mapinduzi Zan-zibar. Na inaelewa vyemakwamba hakuna mwenyekutamani kuurejesha mfumowa utawala wa kifalme.

    Wenye kupalilia chuki wana

    ajenda yao inayojikita ka-tika ubinafsi. Kwa hivyo nimuhimu kwamba vyombovya habari visiwape umuhimuwatu aina hiyo kwani kufanyahivyo kunaweza kuleta hasarakatika jamii kwa kuuvurugausalama wake.

    Jambo moja lenye kushan-

    gaza ni kuliona jeshi la Polisilinamkataza Maalim Seifkwenda Donge na chamachake kuhutubia mkutano wasiasa. Wakati huohuo jeshihilohilo linawaachia baadhiya watu, wote wakereketwawa CCM, waropokwe bila yakujali athari za kauli zao kwawaathirika wanaowatukanakila siku.

    Historia ya kisiasa ya Zan-zibar ya zaidi ya miaka 50iliyopita inadhihirisha kwam-ba Zanzibar ilipata hasarakubwa kutokana na chuki naukhasama wa viongozi nawafuasi wao kwanza kati yaASP na ZNP, na tangu 1992hadi 2010 kati ya CUF na

    CCM.

    Miongoni mwa hasara hizoni pamoja na kupotea kwaroho za watu wasio na hatia,kuteswa watu na kudhulu-miwa mali baadhi ya Wazan-zibari.

    Kwa jumla, ni wazi tukipendatusipende, kuwa Zanzibar ya

    kale ilikuwa na maisha yalio-kuwa mema. Na wakati huokulikuwako neema, amani nautulivu.Wakati huo pia, Zanzibar iki-ongoza katika kila fani katikakanda hii ya Afrika, ukiitoaAfrika ya Kusini. Hii leo halihalisi ya Zanzibar ni dhikizisizokwisha zinazowakabili

    wakazi wa Unguja na Pembakatika kuendesha maishayao.

    Kwa bahati mbaya wakazihao wa Zanzibar hawanatamaa ya kuepukana naumaskini na ukosefu wa fed-ha mifukoni mwao kwa saba-bu serikali inakataa ushauri.Hali hii haitobadilika mpaka

    serikali itapougeuza mfumowa uchumi na sera zake zotekatika sekta hiyo na kurudi-sha Zanzibar mambo yote yauchumi, pamoja na ya ustawiwa kijamii, kutoka Muunganona kuyatumia mambo hayokwa lengo la kuifanya Zanzi-bar iwe na uchumi wa mfumowa bandari huru kama vile

    Singapore na Mauritius.

    Siasa za chuki na matusi navitisho hazitotufikisha popotepale bali zitaturudisha nyumatulikotoka. Lakini umoja wetuukiambatana na hali ya amanina utulivu katika nchi yetu naupanuzi wa demokrasia ndiosuluhisho letu la kuleta ma-geuzi

    Zanzibar Daima Online

    Inawatakieni kheri za Mwaka

    Mpya wa Kiislamu 1435 AH

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    17/21

    PAGE

    32

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    33

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    32

    Tangu linistendi ya gari

    ikawekwabarabarani?

    ivi pembeni mwa tawi la Benki ya Barclays, maarufu kama Donge huko nyuma paliwahi kutumika kama sehemu ya kupata chipsikuku na juice, pakiitwa Donge ndio mahali mwafaka kwa kuege-

    sha gari hizi?

    Kwamba pale tuweke kituo cha gari za Fuoni, Chuo Kikuu (Kibele), Kwara-ra, Uwanja wa Ndege (Kiembesamaki) na Mwanakwerekwe?

    Hivi ni kweli hasa serikali inajitapa haijakosea kutaka watu wanaokwendaHospitali Kuu ya Mnazimmoja, watokao njia kuu ya Mkoa wa KaskaziniUnguja, washukie Kinazini au watu wanapopaita Pinda Mgongo, Saateni?Hapa hapajawahi kuandaliwa kufaa kukusanyika maelfu ya wananchi.

    Hakuna vyoo wala benki.Kwa hivyo anayetoka Nungwi,Kidoti, Mkokotoni, Mkwajuni,Chaani, Matemwe, Pwanim-changani, Kiwengwa, Kinyasi-ni, Donge, Mahonda, Bumbwi-ni, Mfenesini, Kama, Mbuzinina Bububu, washuke Kinazini?Eneo la Mikunguni, pale

    palipowahi kuwa soko la

    muda baada ya kuhamishwakwa soko la nyuma ya mtaamdogo unaoendea machinjioya kuku Darajani, napo pana-pangwa kuwa stendi ya gariza njia kuu ya Amani, Ma-gogoni, Kinuni, Mwera, Koani,Machui, kweli?

    Watu wa njia Maungani,Chukwani, Fumba waungane

    na watu wanaokwenda To-mondo kukutanika uwanja waKwa Binti Amrani, Mpendae.Hapa ndio imewekwa stendiya gari hizi, kweli?

    Haiingii akilini kwamba vion-gozi, tena wakiwemo wenyeuzoefu katika utumishi waumma, wanapanga na kua-mua kuweka stendi ya gari

    Na Jabir IdrissaKauli ya Mwinyi Mkuu

    nyingi kwenye maeneo ya ovyokama haya. Yaani pale KwaKhamis Machungwa leo nikituo cha daladala; aibu iliyoje

    jamani?

    Mshangao mkubwa zaidi

    unakuja pale ninapoelezwakuwa viongozi wa serikaliwakiwemo hawa wa Baraza laManispaa la Mji wa Zanzibar,wanajitapa kuwa hawakukuru-puka katika kufikia maamuzi yakuhamisha stendi Darajani na

    kuipeleka katika maeneo hayotofauti.

    Hivi kama hawakukurupukawanafaa kuitwa nani kwauamuzi wao wa kukutanishamaelfu ya wananchi kila siku

    Pirika za Maisha ya kila siku Darajani Zanzibar.

    ZANZIBAR

    ZANZIBAR

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    18/21

    PAGE

    34

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    35

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    34

    kwenye barabara pale mlan-goni mwa Afisi Kuu ya ChamaCha Mapinduzi (CCM) Kisi-wandui?

    Waitwe nani viongozi hawa iliionekane hasa wametendewahaki? Inashangaza sana.

    Kama Darajani hapafai kwaajili ya stendi ya gari za us-afiri wa umma, kwa sababuhapana nafasi, kama wase-mavyo wakubwa, wanarid-hika kuwa kwenye maeneohaya ya Saateni/Kinazini kwagari za upande wa Kaskazini;Mikunguni kwa gari za njia yakati; na Mpendae kwa gari zanjia Namba 7, kuna nafasi yakutosha kwa ajili hiyo? Hawaitakuwa ufahamu wao ufinyu.

    Niliposikia taarifa za jambohili, harakaharaka nilivutafikra zangu nyuma. Nikaji-uliza hivi haya ndiyo matokeoya mpango wa kuwafunzautumishi mzuri watendaji waserikali?

    Serikali ilikubaliana na Chinamwaka 2011, kupeleka wa-tendaji wake nchini China ku-pata mafunzo ya njia nzuri yakufanya kazi za serikali. Kweli,makumi kwa makumi yawatendaji maofisa wadogo,wa kati na waandamizi wakatengenezewa safari.

    Wacha watendaji, hatamawaziri wameshakwendaChina kujifunza masualambalimbali ya uongozi wakileo.

    China ni taifa lililopiga hatuakubwa ya maendeleo kwasasa. Maendeleo ya nchi hiiyenye watu wengi zaidi du-niani, yameyashtua mataifamakubwa yaliyoendelea tan-gu zamani. Ukuaji wa uchumiwake unasumbua sana akiliza wachumi wa Marekanina Ulaya, hasa Uingereza,Ujerumani na Ufaransa.China imejenga majengo yakisasa. Miji ya kisasa ya vi-wango tafauti. Miji mikubwana midogo iliyojaa viwanda

    vidogo, vya kati na vikubwa.Miji ya viwanda imekuwaikichangia mapato kwe-nye uchumi, kwa kuwa inaza-lisha bidhaa zinazosafirish-wa na kuingiza mabilioni kwamabilioni ya dola.

    Viongozi wengi wa Zanzibarwamekutwa wakizungukakwenye miji hii yenye ma-

    jengo na miundombinu yakisasa. Hapana shaka wanap-ita wakiangalia kwa machomawilimawili maendeleo yaWachina.

    Sasa najiuliza, hivi walichok-wenda kujifunza watendajiwa SMZ, tena wakiwemowale wapya walioingia kwe-nye nafasi za juu za uongozindani ya Serikali ya Umoja waKitaifa, ndio mabadiliko hayaya uhamishaji stendi za gariza usafiri wa umma?

    Kwamba kule China wame-kuta kuna maeneo yabarabara kuu au za mitaaWachina wameweka vituo

    vya daladala? Au tusemeWachina wameweka vituovya daladala maeneo yasiyona huduma za chakula, choo,maduka ya vyakula na vi-faa vya ujenzi na nyumbani,pamoja na benki? Siamini.Watendaji wa SMZ wame-kwenda kutembea China siyokujifunza. Ningeona mabadi-liko ya maana katika utendajiwao wa kazi, ningesema sa-wasawa, zile safari zilikuwana maana kwa maendeleo yaWazanzibari. Sijaona.Mpaka sasa na hasa baadaya kushuhudia uamuzimbaya ulivyoathiri mipangoya wananchi, nataka kua-mini serikali haijafanikiwakubadilisha mitizamo au fikraza watendaji wake ili ziwezinazoelekeza jamii katikakupenda maendeleo.

    Watendaji hawa wangekuwawamekwenda China kujifun-za ili wakirudi nyumbani ma-funzo yale yawasaidie katikakuleta ufanisi wa kazi zao, nakwa hivyo kusaidia kuijenga

    nchi yao, basi wasingebakina fikra za kale na zilizojaahisia za ubinafsi zaidi kulikokufikiria jamii.

    Walipoanza kwenda Chinakwa ziara za kujifunza,Bustani ya Jamhuri ilikuwaimeruhusiwa kutumikaupande mmoja kwa ajili yakujenga pembea za kuchezawatoto. Leo tayari upandemwingine wa bustani hii yaenzi na enzi kumejengwanako.

    Kwanza hii bustani haikuku-sudiwa mahali pa kujengachochote. Hii ni kwa ajili yamapito ya wananchi. Ndiomaana kuliwekwa njia mbilitu. Hakujakuwa na jengohata dogo kwa miaka yote.

    Lakini Serikali ya Awamuya Sita (SAS) kwa sababuya ulafi tu wa madaraka natamaa ya mapato haramu,ikaidhinisha kujengwa pem-bea kwa ajili ya michezo yawatoto. Na haya yakaitwa

    matumizi bora ya ardhi.Ni fedheha kubwa kugeuzamatumizi ya bustani hii.Fedheha zaidi kuruhusu eneodogo kutumika kukalishawatoto wengi kama ina-vyoonekana. Wazazi wanahi-taji eneo la kupeleka watotowao kucheza, lakini eneo le-nyewe liwe la viwango, siyomahali finyu kama Bustaniya Jamhuri. Tunakaribishamajanga.

    Sitaki kufikiria hatari itakayo-tokea siku pakitokea hitilafuya umeme eneo hili. Si-taki kufikiria kamwe watotowengi wanaoingia wataka-vyotoka. Watatokaje walivyowengi mahali ambapo mlan-go wake ni mdogo sana?

    Sasa kama mafunzo ya Chinakwa watendaji wetu ndiyoyameleta matokeo hayayote, nathubutu kusema kuleChina wakubwa walikwendakufanya shopping siyo ku-soma ili kuendeleza kwao.

    ZANZIBAR

    ZANZIBAR

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    19/21

    PAGE

    36

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    37

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    36

    Matukio ya hivi karibu-ni kuhusu Mswada waSheria wa Marekebi-

    sho ya Mabadiliko ya Ka-tiba yameainisha ni kina naniwanaoitakia mema Zanzibarna Tanzania kwa jumla nanani wasiokuwa na nia hiyona ambao wanathamini zaidimasilahi yao binafsi badala yamustakbali wa taifa.

    Labda nianzie na matukioya bungeni ya tarehe 5 Sep-temba ambapo kwa maraya kwanza katika historia yaTanzania wabunge wa chamakinachotawala Chama chaMapinduzi (CCM) na wa Up-inzani waliingiana mwilini .

    Mzizi wa fitna ulikuwa ni

    Mswada uliowasilishwa naserikali kuhusu Rasimu yaKatiba mpya ambao upinzaniulidai umefanyiwa marekebi-sho kwa lengo la kukidhimatakwa ya CCM na kupingausijadiliwe. Naibu Spika JobNdugai akataka upigiwe kurakama ujadiliwe au la, akijuwafika kwamba chama tawalakinalihodhi bunge kwa wingiwake mkubwa. Msimamo

    wake ulionyesha mapungufualiyonayo katika kuliongozabunge, kiasi ya kumtaka hataMkuu wa upinzani FreemanMbowe atoke bungeni nakuzua kasheshe. Wabunge wavyama vya upinzani CHADE-MA, CUF na NCCR-Mageuziwakatoka nje. Ubabe ukatumi-ka kwa kura kupigwa bila yawao kuweko na Mswada huokupitishwa.

    Hatua hiyo ililiweka taifa njiapanda. Wapinzani wakaamuakwamba watalivalia njuga nakuuzuia Mswada huo usisaini-we na Rais Jakaya Kikwete nawakatishia kufanya maanda-mano nchi nzima.

    Kadhalika walifanya miku-

    tano kadhaa ya hadhara ikiwapamoja na ule uliofanywaZanzibar na kuwajumuisha vi-ongozi wakuu wa vyama hivyoFreeman Mbowe,IbrahimLipumba James Mbatia pamojana Mwenyekiti wa chama chaUPDP Fahmi Dovutwa .

    Ninavyokumbuka ni kwambamara ya mwisho kwa viongoziwa vyama vya siasa kutoka

    Bara kuhutubia Zanzibar ili-kuwa wakati wa kampeni yauchaguzi mkuu 2000.

    Tangu uchaguzi wa 2005 up-inzani sio tu ulionekana ku-kosa umoja bungeni bali hatamshikamano wao uliyumba .

    Ni suala la jamii nzima :Suala la Katiba sasa limewale-ta pamoja wapinzani.Lakini bado kuna mamboyanayohitajika kuimarishavuguvugu hilo ili ilipatikaneKatiba maridhawa. Miongonimwayo ni :-1. Ushiriki wa vyama visivyona uwakilishi bungeni au ka-tika Baraza la Wawakilishi2. Asasi za kijamii

    3. Asasi zisizokuwa za kiseri-kali

    Makundi yote hayo ni sehemuya jamii na ni wadau muhimukwa kuzingatia kwamba mus-takbali wao mwema unatat-egemea ushirikishwaji wao namaamuzi watakayotoa. Jiraniyetu Kenya ilifanikiwa kujipatiaKatiba mpya kwa kuwashiriki-sha wadau wote katika jamii.

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mwenyekiti wa

    Chadema, Freeman Mbowe, Ikulu Dar es Salaam.

    Tunaweza kujifunza kutokakwa wenzetu hawa hasa tuki-wa tunakabiliwa na mambomawili makubwa tunayoyasu-biri mbele ya safari: Bunge laKatiba na Kura ya maoni.Kikwete ametumia busara:Nikirejea nyuma katika mvu-tano uliozuka kuhusu Mswadawa Marekebisho ya Mabadi-

    liko ya Katiba, inastaajabishakuona kuwa wapo wenyekumbeza Rais Jakaya Kikwetekwa kukutana na viongozi wavyama vya upinzani vyenyeuwakilishi bungeni ,wakiwemowawakilishi wa TLP na UDP.

    Kiroja cha mambo ni kuwahata baadhi ya mawa-ziri waliowakejeli wapinzani

    wakati wa mjadala wa Mswa-da huo walikuwemo katikaujumbe wa CCM kwenye ma-zungumzo hayo Ikulu.

    Kikwete na pandezilizolalamika, wakakubalianakwamba mapendekezoyao ya marekebishoyawasilishwe bungeni nakutokana na makubaliano

    Na Mohamed Abdulrahman Nionavyo

    La Katiba Mpya si la vyama

    pekee

    ZANZIBAR

    ZANZIBAR

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    20/21

    PAGE

    38

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    39

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaima.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    UKURASA

    38

    hayo, wapinzani wakaridhiautiwe saini Mswada huo,uliorejeshwa bungeni ku-

    jadiliwa zaidi. Pamoja nahayo wakakubaliana kuundaKamati ya demokrasia.

    Bado kuna viongozi nawanasiasa wa CCM ambaohawakupendezewa na mku-tano huo wa kiungwana Ikulu. Miongoni mwao ni mbungewa Kikwajuni Hamad Ma-sauni Yussuf, aliyejitokeza etikutahadharisha.

    Msimamo wake si wa kusta-

    ajabisha. Masauni anasahaumapema kwamba alilaz-imika kujiuzulu Uenyekitiwa Umoja wa Vijana waCCM, baada ya kugunduliwaalighushi tarehe ya kuzaliwa.

    Hadi leo kuna hata wana-chama wa chama chakewanaojiuliza ilikwendakwendaje mwongozo wachama kuhusu uongozi uli-wekwa kando na akapit-ishwa kuwa mgombea waubunge wa jimbo la Kikwa-

    juni ?Watu wa aina hii wanapoku-

    wa tayari kukiuka taratibuza kutafuta uongozi ni shidakuheshimu maamuzi yoyoteya kiadilifu, kiungwana naya mustakbali mwema kwataifa. Wana kila haki ya kum-kosoa hata Mwenyekiti wao,kwani hiyo ndiyo demokrasialakini kwa hili, ukosoaji huonitauita usaliti.

    Ninakumbuka mwezi Meimwaka huu wakati akichan-gia katika mjadala kuhusuuhuru wa vyombo vyahabari katika nchi za Af-rika, Masauni ambaye pia ni

    mbunge wa Tanzania katikabunge la Afrika, alinukuliwaakisema serikali lazima iwewazi na ikubali kukosolewana watu binafsi, viongozi wadini na wanataaluma, wa-nasiasa na wadau wenginena changamoto hizo wazi-fanyie kazi ili kurekebishakasoro zilizojitokeza kwawakati na kujenga hali borakwa raia wa nchi zetu. Hayoni maneno ya hikima, lakinibahati mbaya hotuba zakeVisiwani zinaashiria menginekabisa.

    Ni dhahiri kwamba jinsialivyolishughulikia sualahilo, Kikwete ameanza vi-zuri, amecheza na shingokutoa akiwapa fundisho hatawana CCM wanaotaka kuutiamunda mchakato wa kupataKatiba mpya kwamba hilo nisuala la mustakbali wa taifana si la chama fulani. Uamuziwa kukipa jukumu Kituo chaDemokrasia Tanzania (TCD)kuratibu jambo hilo kwakushirikiana na wadau wen-gine ni wa busara.

    Muhimu ni Katiba ita-

    kayokuwa mhimili wamatakwa ya Wazanzibarina Watanganyika, matakwaambayo ninaamini yata-heshimiwa.

    Bado Kikwete ana wajibu wakuhakikisha mchakato huuhauyumbishwi kiitikadi nachama au kikundi cha watufulani. Kwa wahafidhina Visi-wani wanaoendelea na fitnana hujuma, Waswahili tunamsemo, Nyimbo mbayahailei mtoto kwani ma-tokeo ya maisha yake huwamabaya.

    KWA MARIDHIANO

    HONGERENI WAZANZIBARI

    Na Ismail Jussa Kutoka

    Leo ni Siku ya Maridhiano. Ni tarehe5 Novemba ambapo tunaadhimishamiaka minne (4) ya tukio la kihistoria

    Zanzibar pale viongozi wawili jasiri,shupavu na wazalendo wa Zanzibar, RaisMstaafu, Dr. Amani Karume na KatibuMkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamadsiku kama ya leo tarehe 5 Novemba 2009walikutana na kumaliza hasama za kisiasavisiwani mwetu. Waliweka upande maslahiyao binafsi na ya vyama vyao na wakaweka

    mbele maslahi ya Zanzibar. Walizikamifarakano na wakaleta Maridhiano.

    Hatimaye, maamuzi ya viongozi hawawawili yaliyojaa ushupavu wa uongoziyakapewa baraka na Baraza la Wawakilishina kisha kuridhiwa na wananchi waZanzibar kupitia kura ya maoni iliyofanyika

    tarehe 31 Julai 2010 ambapo asilimia 66.4walipiga kura za NDIYO kuunga mkonohatua hiyo.

    Ni maridhiano hayo ndiyo yaliyopelekeaZanzibar kwa mara ya kwanza kushuhudiauchaguzi mkuu wa 2010 kumalizika kwasalama na amani.

    Hivi sasa wapo vitimbakwiri wanaofanyanjama, hila na vitimbi kutaka kuwarudisha

    Wazanzibari kule kwenye siasa za hasama,vurugu, mifarakano na ubaguzi. Lakiniwanaona wenyewe jinsi Wazanzibari nahasa vijana wa kizazi kipya wanavyokataanjama, hila na vitimbi hivyo vichafu.Zanzibar imeshasonga mbele na hairudi

    tena kule ilikotoka.

    MaridhianoRais Mstaafu wa Zanzibar Amani

    Karume, akipena mkono na Katibu

    Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff

    Hamad, Ikulu Zanzibar tarehe 5

    Nov 2009, ishara ya mwan-

    zo ya Maridhiano

    Ni maridhiano ndiyoyametuunganisha Wazanzibarikusimama pamoja kutakaMamlaka Kamili ya nchi

    yetu. Hatuwezi katu kukubalikuipoteza fursa hii adhimu.

    Tunapoadhimisha siku hiitunawapa hongera Wazanzibari

    wote wanaoamini katikaMARIDHIANO na tunawakatishatamaa wahafidhina wotewanaotamani kurudisha

    MFARAKANO.Zanzibar Kwanza, ShengeshaBaadae!

    Y O U R JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    ZANZIBAR

  • 8/14/2019 Zanzibar Daima Online. Toleo Namba 6

    21/21

    Y O U R

    L O G OH E R E

    UKURASA

    41

    JARIDA LA KILA MZANZIBARI

    www.zanzibardaim a.net Toleo 06 - 2013

    ZANZIBAR

    D A I M A

    O N L I N E

    Magazetini

    iliovuma

    Suala la tofauti ya ushuru wa forodha katika bidhaazinazoingizwa kutoka nje, kati ya Zanzibar na TanzaniaBara, limechukua sura mpya baada ya Serikali kukiri

    kuwa linaumiza wafanyabiashara.

    Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alisema kuwatofauti hizo zitaondolewa baada ya sehemu hizo mbilikuanza kutumia mfumo mmoja wa utozaji kodi na ushuru.

    Alisema kuwa utaratibu wa kutumia mfumo mmoja wakulipa kodi unatarajiwa kuanza baada ya makubalino,utapunguza malalamiko ya wafanyabiashara ambaowanadhani hawatendewi haki.

    Saada alisema kuwa baadhi ya wafanyabiasharawamekuwa wakilalamikia kulipa kodi mara mbili,wanapokwenda Zanzibar kununua bidhaa ambapo piahulazimika kuzilipia tena wanapofika Bandari ya Dar esSalaam.

    Wakati naibu waziri huyo akieleza hayo, wafanyabiasharawengi wa jijini Dar es Salaam wanalalamika kwamba watuwanaoingiza bidhaa kupitia Bandari ya Zanzibar wanatozwakiasi kidogo ikiliganishwa na wale wanaoingiza kupitiaTanzania Bara..

    Walidai kuwa kontena moja la futi 40 hutozwa kodi Sh2.5milioni Zanzibar wakati kontena kama hilo hutozwa kati yaSh25 milioni na Sh30 milioni Tanzania Bara.

    Shimbe Kinena ambaye ni mfanyabiashara wa nguo jijiniDar es Salaam alisema kuwa bidhaa zinazoingizwa nchinikupitia Bandari ya Zanzibar hutozwa

    ushuru mdogo na baadaye kuingizwa jijini kinyemela kwanjia za panya ikiwamo bandari bubu.

    Alisema kuwa hali hiyo inawafanya wanaoingiza bidhaakutoka nje kupitia bandari na njia za barabara Tanzania

    Bara kushindwa kuuza bidhaa, zao kwa vile zile zinazoingiakupitia Zanzibar huuzwa kwa bei ya chee.

    Waziri Saada akizungumzia madai ya kontena moja lafuti 40 kutozwa kodi ya ndogo Zanzibar, ukilinganisha nabara alisema: Siwezi kuthibitisha kama gharama ndiyozipo hivyo, ninachojua kwa upande wa Zanzibar malipoyanaweza kuwa hata nusu ya yale ya Bara.

    Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi waMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayomboalisema kuwa mfumo mmoja wa ulipaji kodi utaondoa

    tofauti za viwango vya kulipa kodi vilivyopo sasa.

    Hata hivyo, alikanusha kuwa gharama za kulipia kontenamoja kwa Zanzibar ni ndogo ikilinganishwa na zile zaTanzania Bara.

    Siyo sahihi kwamba gharama za kulipia kontenaZanzibar ni ndogo sana kuliko Tanzania Bara kwasababu kinachoangaliwa kwenye kontena ni thamani yamzigo uliopo ndani na siyo kwamba kuna bei maalumuiliyowekwa,alisema.

    Alisema kwamba kuna viwango maalumu vya kisheria

    vilivyowekwa kwa pande zote mbili vinavyofuatwa nakwamba vitabadilishwa utaratibu mpya utakapoanza.

    Alibainisha kuwa mpango huo unaoratibiwa na Serikaliutaanza kutekelezwa baada ya kukamilika kwa sera husika.

    Hilo ndiyo lengo letu, ni jambo la kisera, ambalo sisitunaletewa na kutekeleza tuubishi uliopo sasa kuhusutofauti za kodi hautakuwepo, alisema Kayombo

    Makala ya Goodluck Eliona, Gazeti la Mwananchi tarehe 3 Novemba 2013

    Waziri: Tofauti ya mfumo wa ushuru wa forodha unaumiza wafanyabiashara

    Na Goodluck Eliona Iliovuma Magazetini