kampuni ya reli tanzania.docx
TRANSCRIPT
KAMPUNI YA RELI TANZANIATAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI YA KUAHIRISHA SAFARI YA
TRENI KWENDA BARA LEO IJUMAA SEPTEMBA 11, 2015, HADI KESHO JUMAMOSI SEPTEMBA 12, 2015 SAA 11 JIONI!
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unasikitika kuwataarifu
abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na ajali ya treni
ya mizigo iliyotokea kati ya Ngerengere na Kinonko jana mkoa wa
Morogoro , safari ya treni ya abiria kwenda Bara iliopangwa
kuondoka leo saa 11 jioni imeahirishwa hadi kesho Jumamosi
Septemba 12, 2015 saa 11 jioni.
Mafundi wa TRL wako katika eneo la ajali tokea jana wakifanya kazi
kwa lengo la kuhakikisha njia inafunguliwa kwa wakati ili huduma
ya treni za kampuni zirejeea kama kawaida mapema hapo kesho.
Uongozi wa TRL unawaomba radhi wale wote watakaopatwa na
usumbufu wowote utakaojitokeza.
Atakaye soma taarifa hii amwarifu na mwenziwe!
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji Mhandisi Elias Mshana
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Septemba 11, 2015