annuur 1224

20
ISSN 0856 - 3861 Na. 1224 RAJAB 1437, IJUMAA , APRILI 8 - 14, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/= Sauti ya Waislamu www.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST Bila CCM, CUF kukaa mezani… Zanzibar inaelekea kuzimu… Huyu Dr. Banna vipi? Heri ya Vuai Ali Apewa Darsa na mwanasheria Awadh Ugaidi Ubeligiji… Padiri afichua kitendawili kuchomwa kanisa Yombo Bendera ya IS Dar, Paris hadi Brussels Nani anamchukia nani? Katika hili Maalim amefaulu! Majeshi, Vikosi warudi kambini kwao Wakasake majambazi, wabwia unga Soma Uk. 18 KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Soma Uk. 10 Soma Uk. 4 Mtume(saw) amesema, “Mwenye kuja kunizuru baada ya mauti yangu ni kama aliyenitembelea wakati wa uhai wangu”. Neema iliyoje kumzuru Mtume(saw)! Uko wapi ushahidi wa mapenzi yako kama hujamzuru Mtume wako? Gharama zote kwa Hijja 2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/ 0688895777; 0765462022; 0712735363. Zanzibar: 0777468018; 0777458075; 0777845010; 0777497300. (4) JEE, UMESHAMZURU MTUME WAKO? ANNUUR NEW.indd 1 4/6/2016 9:33:22 AM

Upload: anonymous-x8qgwff

Post on 13-Jul-2016

688 views

Category:

Documents


0 download

TRANSCRIPT

Page 1: ANNUUR 1224

ISSN 0856 - 3861 Na. 1224 RAJAB 1437, IJUMAA , APRILI 8 - 14, 2016 BEI TShs 800/=, Kshs 50/=

Sauti ya Waislamuwww.annuurpapers.co.tz au facebook:[email protected] AHLU SUNNA WAL JAMAA HAJJ AND UMRA TRUST

Bila CCM, CUF kukaa mezani…

Zanzibar inaelekea kuzimu…Huyu Dr. Banna vipi? Heri ya Vuai AliApewa Darsa na mwanasheria Awadh

Ugaidi Ubeligiji…

Padiri afichua kitendawili kuchomwa kanisa Yombo

Bendera ya IS Dar, Paris hadi Brussels

Nani anamchukia nani?Katika hili Maalim amefaulu!

Majeshi, Vikosi warudi kambini kwaoWakasake majambazi, wabwia unga

Soma Uk. 18

KATIBU Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Soma Uk. 10

Soma Uk. 4

Mtume(saw) amesema, “Mwenye kuja kunizuru baada ya mauti yangu ni kama aliyenitembelea wakati wa uhai wangu”. Neema iliyoje kumzuru Mtume(saw)! Uko wapi ushahidi wa mapenzi yako kama hujamzuru Mtume wako? Gharama zote kwa Hijja 2016/1437 ni Dola 4,600. Umra ya Ramadhani ni Dola 2,700. Karibuni Ahlu Sunna wal Jamaa kwa huduma nzuri na uongozi bora. Wasiliana nasi: Tanzania Bara: 0679895770/ 0688895777; 0765462022; 0712735363. Zanzibar: 0777468018; 0777458075; 0777845010; 0777497300.

(4) JEE, UMESHAMZURU MTUME WAKO?

ANNUUR NEW.indd 1 4/6/2016 9:33:22 AM

Page 2: ANNUUR 1224

2 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Mafundisho ya Qur'an/Uwanja wa Maarifa

Fethullah-Gulen

Jee Unajua?

MASUALA1. Sura gani na aya ya ngapi? ‘Na kupishana usiku na mchana, na riziki

anayo iteremsha Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni, na kwayo akaifufua ardhi baada ya kufa kwake, na mabadiliko ya upepo, ni Ishara kwa watu wenye akili.’ Jawabu : 45 :5 (Surat Al Jaathiya)

2. Sura gani na aya ya ngapi? ’Walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.’ Jawabu : 47 :1 (Surat Muhammad)

3. Sura gani na aya ya ngapi?’’Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka” Jawabu : 49 :7 (Surat Al Hujuaraat)

4. Sura gani na aya ya ngapi? ‘’Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!” Jawabu : 77 :19 (Al Mursalaat)

5. Sura gani na aya ya ngapi? ‘’Na bila ya shaka tulimtuma Nuhu na Ibrahim, na tukaweka katika dhuriya zao Unabii na Kitabu. Basi wapo miongoni mwao walio ongoka, na wengi katika wao ni wapotovu. ‘’ Jawabu : 57 :26 (Suratul Al H’adiid)

6. Kuna aya ngapi za Sajda katika Qur’an? Jawabu : 147. Jamaa yupi wa Mtume aliotajwa katika Qur’an? Jawabu : Abu Lahab8. Sura za Makka ni ngapi? Jawabu : 869. Sura za Madina ni ngapi? Jawabu : 2810. Siku ya Qiyama hali ya watu itakuwaje? Jawabu : Mfadhahiko

JAWABU CHEMSHA BONGO NAMBA: 45

CHEMSHA BONGO: 46Weka duara kwenye jawabu ilio sawa. Jawabu kamili wiki ijayo.

MASUALA 1. 1. Sura ya ngapi na aya ya ngapi isemayo ‘Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa’2. Sura ya ngapi na aya ya ngapi isemayo ‘Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia’ 3. Sura ya ngapi na aya ya ngapi isemayo ‘Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.’4. Sura ya ngapi na aya ya ngapi isemayo ‘ Hakika pamoja na uzito upo wepesi.’5. Sura ya ngapi na ni aya ya ngapi isemayo ‘Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.’6. Wakati gani Sayyidna Khalid bin Walid alisilimu?7. Ilikuwa wakati gani Mtume Muhammad (SAW) aliwasili Madina ikiwa ni Hijjra?8.. Mtu yupi ambaye aliuliwa na Mtume (SAW) kwenye vita?9. Wakati wa kiongozi yupi ndipo Waislamu walitengeneza pesa zao za kutumia?10. Sahaba yupi ndio aliokuwa wa mwanzo kuzikwa katika Makaburi ya Baqii?

MWENYEZI Mungu ndiye mjuzi zaidi wa mahali atakapouweka ujumbe wake”. [Al –An-Aam 124]

Wiki iliyopita, tulitoa sehemu ya mwanzo ya ufafanuzi wa aya hii kama ilivyoandikwa na mfasiri. Leo tunaangalia sehemu ya pili.

Umedhihirika umoja wa Manabii watukufu, maana nikwamba Mtume (s.a.w.), ulikuwa ujumbe wake wa ulimwengu mzima, wenye kuenea, wenye kukusanya fikra za Manabii wote watukufu kwa wanadamu na ujumbe wao. Kwa sababu hiyo, yeye anahesabiwa kwa upande wa kuanzisha masuala yote ya imani yaliyolazimu – anahesabiwa kuwa ni muasisi, na anahesabiwa kwa upande wa kusahihisha upotoshaji. Kuwa ni msahihishaji na anahesabiwa ni mfanyaji upya wa mambo, katika yale mambo ambayo yanahitajia kufanywa upya na kukamilishwa. Kwa sababu hiyo, hapana mjumbe wala Nabii baada yake. Kwa sababu masuala ya itikadi yamefikia kwenye umoja wenye kukamilika. Kama akija mwingine atakuwa hana la kufanya, pengine atabakia tu kuuchana chana umoja huu, uliyokamilika. Kwa msingi huo, yeye ni Mtume na Nabii wa mwisho, maana yeye ni mwisho wa Manabii na Mitume. Kwa sababu binadamu wamefikilia kupitia kwa Mtume huyu katika fikra na katika dini na itikadi na katika kuongoza na mwenendo na njia kwenye funguo zote za mambo yaliyofungwa katika

itikadi na fikra na maisha kwa sifa ya kuwa hakuna haja tena ya ujumbe mpya. Kwa sababu hii, ni juu ya binadamu wote kupanga masuala yote ya maisha juu ya mwangaza wa ujumbe wa mwisho, na juu ya uongofu wake.

Na upande mwingine wa maudhui haya ni kwamba Utume wa Muhammad (s.a.w.) na ujumbe wake ulikuwa kabla ya Manabii na Mitume wote. Kwa hakika imekuja katika moja ya hadithi “Kitu cha kwanza alichokiumba Mwenyezi Mungu ni nuru yangu. Na katika hadithi nyingine “Nilikuwa Nabii na hali ya kuwa Adamu ameanguka katika udongo wake maana kwa hakika, mpango wa kupelekwa kwake hali ya kuwa Mtume ulikuwa kabla ya Mitume wote na kwa hakika watu wa Taswawwuf, wamelishughulikia jambo hili chini ya anuani hii “Hakika ya Ahmad” wamesimama hapo sana. Na hali yakuwa wao wanaona kwamba hakika ya Ahad hakika hiyo wakati huo huo ni hakika hiyo wakati huo huo ni hakika ya ulimwengu mzima na wamekusudia kwa maneno hayo kuonyesha utukufu wa Mtume (s.a.w) na kwamba yeye alikuwa ni muonekano wa utukufu wa ujumbe wake.

Ni jambo lenye faida hapo tusimame kitambo kidogo mbele ya jambo hili lifuatalo: Hakika Mtume (s.a.w.) alifikia kwenye daraja ambalo hajafikia kwenye daraja hilo mtu yeyote pindi tutakapochukua kwa mtazamo wa mazingatio, nuru ambayo ameieneza kwa upande wa kiasi na kwa upande wa namna vile vile na hawezi mtu yeyote kufikia kwenye nuru hiyo. Na hili kwa upande wa kisayansi ni kielelezo kikubwa sana na ushahidi mno juu ya ukubwa na utukufu wa ujumbe ambao ameuchukua na akaubeba.

1. Hilo ni kwa sababu ya kwamba

mamia ya dini mbalimbali kama vile dini ya Budha Barham na Tawtan na zisizokuwa hizo na hata dini za mbinguni, kama Ukristo na Uyahudi zimepatwa na upotoshaji na ubadilishwaji kwa kiwango fulani. Ukubwa wa Uislamu huenda ukawa Ukristo hivi leo umeenea sana kuliko Uislamu isipokuwa ni jambo gumu sana lau kuukuta Ukristo wa hakika kama vile alivyokuja nao Bwana Masiah (a.s.). Ni vigumu leo kuufahamu Ukristo ambao umezama katika mkondo wa maelezo na tafsiri ambazo zimefungwa. Na lau tusingeona katika Qur’an tukufu kueleza kwa uhakika juu ya Maseeh (a.s.) kusingewezakana kujua kuwa umetolewa katika kitabu kitakatifu, katika mlolongo wa kupingana kwingi ambako kunapatikana kutoka kitabu hicho kuhusiana na Bwana Maseeh kwa sababu Issa (a.s.) ambaye anaonekana mbele yetu katika Injili ya Yohana na katika Injili ya Mathayo na Luka hatofautiani katika kitu chochote na Mwenyezi Mungu mtukufu “Kutakata ni kwa Mwenyezi Mungu” kwani yeye yuko juu ya kiti cha enzi ubavuni mwa Mwenyezi Mungu anagawana naye Ubwana na hawaepukani wanaadamu na dhambi ya urithi – kufuatana na madai yao na hawawezi kuingia peponi pepo ambayo waliipoteza isipokuwa kwa fadhila yake. Ndiyo, kwa hakika ya Maseeh (a.s.) imefungwa inayumba, na iko mbali na kusadikiwa mpaka kiwango hiki katika misemo iliyopo hivi sasa ya kitabu kitakatifu. Na ni mfano wa mambo yote mengine ambayo yamethibiti hatukujuwa hakika ya Maseeh (a.s.) isipokuwa kwa fadhila ya ujumbe wa Mtume wetu (s.a.w.). (Itaendelea)

Suratul An-aam 124

1. Mauaji ya Kimbari ni mauaji ya kutisha ambayo mwandamu anawaangamiza wanadamu wenzake kwa maalfu, Utawala wa watu wa Ulaya kunyakua ardhi ya Marekani, inakisiwa wakaazi wa asili wa Marekani waliuliwa kutoka idadi baina ya watu 2,000,000-100,000,000 : http://www.rantpolitical.com/2014/12/06/15-worst-genocides-in-history/2. Mauaji ya Kimbari yaliofanywa na viongozi na ya kutisha, Mao Dze Tung kwa China 34,300,000-63,784,000, Stalin kwa nchi ya Urusi vifo 23,000,000-60,000,000, Hitler wa Ujerumani vifo 6,000,000, Waziri Mkuu wa Japan Hideki Tojo alisababisha vifo 5,000,000 : http://justontop.blogspot.com/2011/11/top-5-worst-genocides-in-history.html3. Kuweka ndevu zama hizi zimeonekana kuwa ni Waislamu wenye siasa kali wakati Mtume Muhammad (SAW) katupendezesha kuweka ndevu kuliko Sharubu, juu ya hayo sasa tafiti zinaonyesha wale wenye ndevu huepukana na madhara ya miale na kuhujumiwa na Baktiria na mtindo wa kuweka ndevu umerudi na hata wachezaji wa soka katika EPL wengi siku hizi wanaweka ndevu. Kuna wanasayansi wengi wakiweka ndevu na walikuwa mahiri na sio Waislamu kati ya hao ni Sir, Charles Darwin, Lord Kelvin, Augus Kekule, James Clark Maxwell, Wiliam Crookes, Dimitriv Mendeleer na wengineo : http://www.famousscientists.org/top-10-scientists-beards/4. Sio wajuzi wote hushuhudia uvumbuzi wao kukubalika ingali wapo hai, kuna kama wavumbuzi 7 waliokuja na uvumbuzi mkubwa lakini wakiwa bado hao uvumbuzi wao ulikataliwa kati ya hao ni Alferd Wegner 1880-1930 alieleza kuwa dunia na mabara yanakwenda kidogo kidogo, mwengine ni Ignaz Semmelweis 1818-1865 alielezea namna ya kuzaliwa kwa mtoto na wengineo : http://www.famousscientists.org/7-scientists-whose-ideas-were-rejected-during-their-lifetimes/5. Inasemekana kuna magwiji wavumbuzi wa Sayansi kama 77 waliishi kufikisha umri wa miaka 90 akiwemo Alferd Russel Wallace, Antonie Van Leewenhook, Mary Somerville, Chen Ning Yag na wengineo : http://www.famousscientists.org/scientists-into-their-nineties

A O A B C D E F G A 77 :19 M A S

B P K A Q M C Y H B W F S I

C Q L S W N E R T U X A X R

D R M D E B A KJ G L 57 :26 D C T

E S B F R V S H B A 14 H V Y

F T D H T C D H N H 86 A T F

G U C G Y X A J M A Y H B T

H V V H U Z S K S B Z I F Y

I W F J I A D K S R Q K R V

J X B K O Q D J D Y A O T B

K Y D L G W S H F U 49 :7 D Y G

L Z F M F ER B G G I 28 D U Y

M V G N D F C B K O 47 :1 F N R

N V H V T V V N O P 45 :5 G M S

V M T N T U J I T 86 :6 12 U U

I A A O H B R B A 5 :6 R M T

T A I O I I E N R 2 :115 A A H

A M F U Y bin U H I 45 B R M

V U B R A K S A K 94 :6 I A A

Y N A J B H A S B 16 :5 U B N

A Y S A B A L H I 56 :9 A U Ibn

U A R D A L E A N 90 :20 W B M

H T A I T F M M Z 236 A A A

U T H D O I K K I 67 :8 L K Z

D H L N U F A A Y 21 :25 A A O

J R M U N R S D A 5 :12 L R O

N B N B L F W I D 89 :14 I I N

ANNUUR NEW.indd 2 4/6/2016 9:33:30 AM

Page 3: ANNUUR 1224

3 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

Habari

Zanzibar inaelekea kuzimu…Bila CCM, CUF kukaa mezani…

ZANZIBAR inakoelekea sio kuzuri, kama hazitafanyika juhudi za makusudi kuviweka mezani vyama vikuu vya siasa visiwani humo, CUF na CCM.

Hayo yamebainishwa katika mjadala uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia Sauti ya Ujerumani (DW).

Mjadala huo uliowahusisha Naibu Katimu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai, mwanasheria Awadh Ali Said na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Benson Banna, ulikuwa ukijadili hatma ya Zanzibar baada ya uchaguzi wa marudio na Dr. Ali Mohammed Shein kutangazwa mshindi.

Hoja ya msingi ilikuwa kwamba, Zanzibar kulikuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, lakini sasa kwa hali ilivyo, itakuwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa na Baraza la Wawakilishi lililo la chama kimoja, CCM.

Pamoja na hoja mbalimbali zilizotolewa, jambo moja la msingi wanalokubaliana wataalamu hao ni kuwa, itakuwa ni jambo la kujidanganya iwapo itadhaniwa kwamba Zanzibar itakuwa na mustakbali mzuri, yenye amani na utulivu na ustawi, iwapo hakutakuwa na juhudi za kuvikutanisha vyama vikuu pinzani na kufanya mazungumzo na maridhiano.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliosikiliza mazungumzo hayo, wamehoji yale yaliyosemwa na Dr. Banna baada ya kutoa hoja tatanishi na kuchemka kama mwanasiasa aliyeko katika jukwaa la kampeni.

Awali msomi huyo wa Chuo Kikuu kikongwe nchini alipopewa fursa ya mwanzo kufungua mjadala alisema kwamba, jambo lililotokea la kufuta uchaguzi wa Oktoba 25, lilikuwa la kuhuzunisha, kusononesha, kukatisha tamaa, linaloturudisha nyuma na lenye kufanya watu wajiulize, Zanzibar inaelekea wapi.

Hata hivyo baada ya kuyasema hayo, akageuka na kuanza kulaumu na

Na Mwandishi Wetu

kukishambulia Chama Cha Wananchi, CUF, akidai kwamba kimekosa uzalendo kwa kususia uchaguzi wa marudio.

Na kwamba, kama waliona kuwa Jecha alikuwa kakosea kufuta uchaguzi, kwa nini hawakwenda mahakamani.

Mwanasheria Awadh Ali Saidi alipopata fursa ya kuchangia, ilibidi ampe darsa profesa huyo wa sayansi ya siasa akimkumbusha kuwa alikuwa katika timu ya waangalizi wa uchaguzi mkuu uliofutwa na taarifa ya timu yake ilisema wazi ikisifu uchaguzi kuwa ulikwenda vizuri, wa haki, na huru uliokidhi vigezo vyote vya uchaguzi huru wa kidemokrasia, na kwamba wakati uchaguzi unafutwa, tayari washindi takribani wote wa Uwakilishi na Udiwani, walishakabidhiwa vyeti vyao vya ushindi.

Kwa hiyo jambo la mwanzo la kuhoji na kujadili, lilikuwa uhalali wa kufuta uchaguzi, sio kulaumu waliokataa kushiriki uchaguzi wa marudio.

Kama ni mjadala, na kama ni lawama ianze kwa kuhoji, kwa sheria gani na kwa vigezo gani vya demokrasia, vilimpa mamlaka mwenyekiti wa Tume kufuta uchaguzi na kuitia nchi katika mtafaruku.

Hata lilipokuja sula la kisheria na katiba, Dr. Banna

alionekana kujikwaa pia mpaka pale mwanasheria Awadh alipomtajia vifungu vya katiba ambavyo ninazuiya shuguli za Tume ya Uchaguzi kuhojiwa mahakani.

Hoja ya Dr. Banna ilikuwa kwamba inachokataza sheria ni kuhoji matokeo ya urais yakishatangazwa na Tume ya Uchaguzi. Lakini kingine chochote kinaweza kuhojiwa mahakamani.

Hata hivyo, mwanasheria Awadh akamrerejesha katika Katiba ya Zanzibar kifungu cha 119 (13) na pia ya Tanzania kifungu cha 74 ambavyo vinazuiya mahakama yoyote kuchunguza jambo lililofanywa na Tume ya Uchaguzi.

Baadhi ya wakati Dr. Banna alionekana kupandwa na jazba na kuongea kama mwanasiasa aliyeko katika jukwaa la siasa kwa kukariri misemo ya wanasiasa majukwaani.

Kauli kama ‘hatukubali’ kuchezewa muungano wetu, umoja wetu, amani yetu’ kwa sababu ya watu fulani kutaka madaraka.

Ambapo katika muktadha wa mjadala ulivyokuwa ukiendelea, ilikuwa ni kana kwamba anasema kuwa yaliyofanyika ni sawasawa kwa sababu ilishaonekana kuwa kuna watu wanataka kuvunja umoja wetu na muungano wetu.

Hali hiyo, ilimtatiza hata mwendesha mjadala Mohammed Khelef na kutaka ufafanuzi kwa kumuuliza Dr. Banna iwapo waliona (yeye Banna kama msomi au CCM?) kwamba kikikamata chama kingine, kitahatarisha muungano ndio hawakubali? (Wanachukua hatua kama aliyochukua Jecha?)

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai, alikiri kwamba kutokushiriki CUF katika uchaguzi wa marudio, ni dosari kubwa na kwamba japo wanafurahi kushinda, lakini furaha yao imeingia doa kubwa.

Kwa upande mwingine, Vuai alisema kuwa ile dhamira ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ilishaingia dosari kwa sababu palikwisha anza kutokea vitendo vya kupigwa watu na kuchomwa moto nyumba, vitu ambavyo vinaonyesha kuwa bado kuna dalili za chuki na uhasama uliokusudiwa uondoshwe na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Hata hivyo, mwanasheria Awadh alipokuja kutoa hoja akasema kuwa, tatizo kubwa lililopo ni kuwa matukio yaliyokuwa yakifanyika, yakidaiwa kufanywa na ‘mazombi’, yalichukuliwa kisiasa badala ya kuwa ni jinai kama jinai nyingine.

Yalifanywa ya kisiasa kwa sababu wahusika hawakamatwi na kufikishwa mahakamani.

Inabaki ni suala la kutolewa kauli tu katika majukwaa ya kisiasa hali inayoonesha kuwa hata vyombo vya dola na kisheria ni kana kwamba vilishikwa mikono visishughulikie hujuma hizo kama jinai nyingine.

Jambo ambalo linaleta hoja nyingine kwamba huenda ni mambo ya kupangwa ili kuleta kisingizio kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa, imeshindwa kuondoa chuki na hivyo haina maana iondoke.

Hata hivyo, pamoja na kukinzana huko kwa hoja, washiriki wote walikubaliana kuwa bila ya kuwa na mazungumzo baina ya CUF na CCM na kuleta maridhiano, mbeleni ni kiza kitupu Zanzibar.

DKT. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Maalim Seif Sharif Hamad.

ANNUUR NEW.indd 3 4/6/2016 9:33:32 AM

Page 4: ANNUUR 1224

4 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

Tahariri/Tangazo

AN-NUUR S.L.P. 55105, Simu: +022 2400786

Cel: 0784 370 208, 0713 110 148, 0755 260 087 , DSM. www.annuurpapers.co.tz E-mail: [email protected]

Ofisi zetu zipo: Manzese Tip TopUsangi House, barabara ya Morogoro, D'Salaam

MAMA mmoja wa Kiislamu jijini Brussels Ubeligiji, amenusurika kufa mapema wiki hii, baada ya kugongwa na gari kwa makusudi na mtu aliyedhamiria kumkanyaga na kulipitisha gari lake juu yake. Mama huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja, hivi sasa anauguza majeraha akiwa hospitali.

Akipita kando ya barabara, akiwa kavaa hijabu, ghafla aligongwa na gari, lakini kwa bahati akarushwa pembeni, kwa hiyo, jitihada za aliyemgonga kumrejea na kupita juu yake zikashindikana. Hata polisi walipokuja, mtu huyo aliyemgonga, wala hakukimbia bali akifurahia ‘mchezo wake’.

Taarifa ya polisi inasema kuwa waliotaka kumuuwa mama huyo wa Kiislamu, ni vijana wa Kikristo wenye chuki na Waislamu ambao wala hawakuona kuwa wamefanya kosa, bali walikuwa wakifurahi na wakijipiga picha walipozingirwa na polisi baada ya tukio hilo.

Inaelezwa kuwa matukio kama hilo dhidi ya Waislamu, yamekuwa ni ya kawaida katika miji mbalimbali ya Ulaya baada ya matukio ya kigaidi ya Paris na Brussels yanayonasibishwa na Waislamu. Itakumbukwa kwamba, masaa machache baada ya lile tukuio la Paris, mwaka jana, mtu mmoja kule Marekani, ambaye ni afisa mstaafu wa jeshi (retired Marine), Ted A. Hakey Jr., kwa hasira, akiamini kuwa waliofanya shambulio lile ni Waislamu, alichukua bunduki yake na kuanza kuumiminia risasi msikiti ulikokuwa jirani na nyumba yake. Hiyo ilikuwa Novemba 13, 2015.

Hii ni kuonyesha kuwa kama lengo la waliofanya mashambulizi yaliyodaiwa kuwa ya kigaidi, lilikuwa kupandikiza chuki baina ya Waislamu na Wakristo,

Nani anamchukia nani na kwa nini?Manazi wa ugaidi wazingatie hili

basi wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

Hiyo ni Ulaya na Marekani ambako idadi ya Waislamu, ni ndogo sana. Ni katika mazingira, unayoweza kusema kuwa Waislamu wapo katika bahari ya Ukristo na Wakristo. Hebu njoo hapa nyumbani ujiulize hali itakuwaje tukifikia mahali pa kujijengea mazingira kama hayo ya Brussels ya vijana wa Kikristo kuendesha Audi A1 zao na kuwagonga kwa makusudi akina mama wa Kiislamu waliovaa hijabu!

Nimetumia neno ‘kujijengea mazingira’, kwa sababu nyuma kidogo hapa kulikuwa na mchezo wa kutumia vyombo vya habari kushabikia habari za ugaidi bandia unaochochea chuki na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo.

“Why Do Europe’s Muslims Hate The West?“ Kwa nini Waislamu wa Ulaya wanaichukia Ulaya?

Hilo ni swali likiwa ni kichwa cha Makala/maoni yaliyochapishwa katika moja ya vyombo vya habari. Ni maoni yaliyoandikwa kufuatia shambulio la Brussels ambapo ilidaiwa kuwa magaidi wa IS walifanya shambulio la kujitoa muhanga wakauwa watu 34.

Shambulio hilo la Brussels, lile la Paris, Boston, London na mengine kama hayo, ndiyo yanayochukuliwa kama ushahidi kwamba Waislamu wanawachukia binadamu wenzao wa Ulaya. Swali linajaaliya kuwa ni kweli matukio hayo yamejiri na kwamba waliohusika ni Waislamu na wanafanya hivyo kwa lengo la kuuwa Wakristo wa Ulaya kwa chuki tu za kijahili.

Yanatolewa maelezo marefu kuonesha kuwa Waislamu ni watu wa ajabu sana, wasio na shukurani hata kidogo. Shukurani ya punda mateke. Inaelezwa kuwa huko katika nchi zao, Somalia, Iraq, Syria, Libya, Yemen, hakuna

la maana ila kuuwana wenyewe kwa wenyewe. Mambo yakizidi, wanakimbilia Ulaya ambapo wanawakuta Wakristo walio na moyo wa ubinadamu, wanawapokea, wanawafungulia milango ya nyumba zao na kutokana na kodi zao wanapewa huduma za makazi, chakula na afya. Lakini Waislamu hao hao badala ya kuonyesha shukrani, wanageuka wanafanya mashambulizi ya kigaidi kama lile la Brussels. Watu gani hawa?

Maelezo ni mengi, lakini inaelezwa kuwa pamoja na wema wanaofanyiwa kwa kukaribishwa Ulaya, bado Imani yao ya kidini inawaambia kuwa ni halali/na amri kuendesha harakati za kuuwa watu wa Ulaya, ikiwemo njia ya kujitoa muhanga. Na inadaiwa kuwa huo ni utafiti uliofanywa na wataalamu mbalimbali wa Ulaya.

Mwisho linatolewa hitimisho kwamba hakuna namna ya kuwafanya Waislamu kuipenda Ulaya/ulimwengu wa Kikristo. Kwa hiyo serikali zichague moja kati ya mambo mawili: ziwafukuze na kuwafungia milango Waislamu kuingia Ulaya au zisahau kabisa kuwa

na ustaarabu, amani na usalama zikiendelea kuwakirimu watu ambao hawana shukurani.

Kwa nini Waislamu wa Ulaya wanaichukia Ulaya? Kwa nini Waislamu wanawachukia Wakristo? Unajibu nini ukiulizwa swali kama hili! Ni swali ambalo lishakupachika uhalifu, kwa hiyo unachoulizwa ni kama kusema kwa nini wewe muhalifu? Kwa nini wewe ni mtu mbaya? Muuwaji! Katili! Kwanini?

Somalia, Libya, Iraq, Yemen, Syria, Afghanistan, zote zilikuwa nchi za amani na utulivu kabla ya kuvamiwa na kuharibiwa na wanaojiita ‘wastaarabu’ wa Magharibi. Zimevurugwa sasa watu wanauwana ovyo. Aliyezivuruga na anayeendelea kuzivuruga ndiye huyo huyo anawageuzia kibao watu wa nchi hizo na kuwashutumu kuwa kazi yao ni kuuwana.

Ndani ya Ulaya, inafanyika michezo na usanii wa ugaidi (false flag terror attacks) mithili ya zile zama za Operation Gladio (Italian: Operazione Gladio) na Operation Northwoods, kisha inapigwa propaganda kuwa ni magaidi Waislamu wanalenga Wakristo. Hata ndani ya nchi za

Kiislamu zinafanyika ‘Sting Operations’ kama lile shambulio la Lahore. Watu wanauliwa, inadaiwa ni Waislamu wanalenga Wakristo. Usisahau na wale wanaodai kuwa Waislamu Tanzania wanachoma makanisa!

“What did ‘we’ do to ‘them’? We opened up our cities, our houses, our wallets. And in our secular temples of progress — our metro stations and airports and theaters — their sons are killing themselves and taking our sons and daughters with them.”

Anauliza mwandishi wa Kidachi Leon de Winter, akiandika juu ya kile alichokiita “Occidentophobia”-Chuki dhidi ya Ulaya. Kwamba pamoja na ukarimu wote wanaofanyiwa Waislamu, lakini hugeuka kuwa magaidi wa kujilipua wakiuwa watoto, wasichana kwa wavulana wa Kikristo wa Ulaya.

Katika mazingira hayo sasa unaulizwa-“Kwa nini Waislamu wanachukia Wakristo?” Unajibu nini?

Labda tuache hiyo iwe changamoto kwa kila Muislamu kutafakari na kushughulisha kichwa chake.

AFRICA MUSLIMS AGENCY TANZANIA OFFICE The Africa Muslims Agency is a humanitarian, development

and Dawah organization based in Kuwait with offices across Africa. The agency has 11 schools across Tanzania both secondary and primary.The Agency has 6 positions for the post of accountant in its 6 secondary schools in the regions mentioned below;

Job Title: AccountantJob Station: Tanga,Moshi,Morogoro, Mtwara and Dar es Salaam

Roles and ResponsibilitiesDocuments financial transactions by entering account information.Substantiates financial transactions by auditing documents.Maintains accounting controls by preparing and recommending policies and procedures.Reconciles financial discrepancies by collecting and analyzing account information.Secures financial information by completing data base backups.Maintains financial security by following internal controls.Prepares payments by verifying documentation, and requesting disbursements.Complies with state and local financial legal requirements by studying existing and new 

legislation, enforcing adherence to requirements, and advising management on needed actions.Prepares special financial reports by collecting, analyzing, and summarizing account information 

and trends.Maintains customer confidence and protects operations by keeping financial information 

confidentialContributes to team effort by accomplishing related results as needed.QualificationsA holder of diploma in Accounting or equivalentHas at least 2 years in similar position with good track recordMust be willing and available to work in the named stations.Strong leadership, communication, interpersonal, and organizational skills Computer application skills.Experience in working with donor funded projects.Excellent written and oral communication skills in English and Kiswahili, including report writing.Excellent networking and organizational skillsSelf motivated personArabic Language will be added advantageMode of ApplicationSend your Application, CV and copies of certificates to:The Director Africa Muslims AgencyP o Box 9211Dar es Salaam        [You can drop the application in our office Tabata Muslim]Or Email: [email protected] Deadline: Two weeks after first advertisement.

ANNUUR NEW.indd 4 4/6/2016 9:33:35 AM

Page 5: ANNUUR 1224

5 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016HABARI ZA KIMATAIFA

IMAM wa Msikiti wa al-Islam mjini Washington, Sheikh Abdul-alim Musa, amesema serikali ya nchi hiyo na Wazayuni wana muelekeo wa pamoja na wanashrikiana katika kuwakandamiza Waislamu wa nchi hiyo.

Sheikh Musa alisema serikali za Democrats na Republicans kwa kushirikiana na Wazayuni wenye ushawishi, wameukandamiza sana Uislamu na Waislamu nchini Marekani na kwamba, mwenendo huo bado unaendelea.

Imam huyo alieleza kuwa Waislamu wamekuwa wakikabiliwa na mashambulio ya moja wa moja ya Wazayuni wa Kimarekani wenye hadhi na ushawishi.

Kwa mujibu wa Sheikh Abdul-alim Musa, kaulimbiu za kampeni zinazotolewa na wagombea wa uteuzi wa kuwania urais wa Marekani zimekuwa zikiilenga jamii ya Waislamu nchini humo.

Aidha aliongeza kuwa makundi makubwa ya kutetea haki za kiraia nchini Marekani yamenyamaza kimya na wala hayatetei haki za Waislamu.

Donald Trump, ambaye anaongoza miongoni mwa wanaowania kuteuliwa kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican, wiki iliyopita alirudia tena kauli yake ya kutaka Waislamu wasiruhusiwe kuingia nchini humo.

Seneta Ted Cruz na wagombea wengine wa uteuzi wa kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican, nao pia wametaka hatua kali za usalama zichukuliwe katika maeneo wanayoishi Waislamu nchini humo.

Wakati Imam Musa akitoa kauli yake hiyo kushutumu serikali za Democrats na Republicans kwa kushirikiana na Wazayuni wenye ushawishi, kukandamiza Uislamu na Waislamu nchini Marekani, Rais Barack Obama amekiri kwamba Waislamu wamekuwa ni waathirika wa ugaidi.

Hata hivyo Rais Obama ambaye alikuwa kihutubia katika shughuli za kidini mjini Washington, alisema

Waislamu ni wahanga wa ugaidiWazayuni wachangia kuwanyanyasa

kuwa wanaoathirika ni wote Wakristo na Waislamu.

Alisema wote wamekuwa waathirika wa ugaidi na kwamba, lengo la magaidi ni kudhoofisha imani za watu na kueneza chuki na mtazamo mbaya kuhusu dini na imani tofauti.

Rais Obama aliongeza kuwa mashambulizi ya kigaidi yanawashawishi Wamarekani wawafukuze watu wanaotafuta hifadhi.

Pamoja na Rais Barack Obama kudai kwamba Waislamu na Wakristo wote ni waathirika wa ugaidi, lakini Marekani na washirika wake ndio wamekuwa wakiyaunga mkono na kuyafadhili kwa misaada ya kifedha na kijeshi makundi ya kigaidi kama Daesh, ambayo yanafanya jinai za kutisha katika nchi kama Iraq na Syria.

Hata hivyo, pamoja na kuonekana kuwa waathirika wa vitendo vya kigaidi ni watu wa imani zote za Kikristo na Kiislamu, lakini linapotokea tukio lolote la kigaidi, msako wa kamatakamata, uchunguzi, mahojiano na utesaji vimekuwa vikiwalenga zaidi wale wote wenye kunasibishwa na Uislamu.

Rais Barack Obama.

WAZIRI wa Haki za Wanawake wa Ufaransa, Laurence Rossignol, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa matamshi ya kuwavunjia heshima wanawake wa Kiislamu na vazi lao la stara la hijabu.

Bi. Laurence Rossignol, alilazimika kuwaomba radhi wanawake hao wa Kiislamu nchini humo kwa kuwafananisha na watu weusi waliokubali kufanywa watumwa nchini Marekani.

Katika mahojiano na televisheni ya BMF na idhaa ya RMC nchini Ufaransa wiki iliyopita, Waziri huyo aliyakejeli matamasha yanayowaruhusu wana-mitindo waliovalia mavazi ya stara kama burqa na kufunika mikono na miguu yao na kusema kuwa hatua hiyo ni ya kipumbavu.

Muda mfupi baada ya kutoa kauli zake hizo za kibaguzi na dharau, maelfu ya wanaotumia mitandao ya kijamii walimjia juu na kumtaka aombe radhi kwa matamshi yake hayo.

Kwa masaa machache tu, sahihi zaidi ya elfu 10 zilikuwa zimekusanywa katika ukurasa mmoja wa mitandao ya kijamii, kumshinikiza Waziri huyo ajiuzulu kutokana na kauli yake ya kibaguzi.

Baadaye Rossignol alilazimika kuomba radhi na kusema kuwa 'ulimi uliteleza'.

Chuki dhidi ya Waislamu na Uislamu barani Ulaya zimeongezeka kwa asilimia 275, baada ya shambulizi la Paris lililofanywa na watu wanaodaiwa kuwa ni kundi la kigaidi la Daesh na kusababisha watu zaidi ya 130 kuuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa mwishoni mwa mwaka 2015 na kufuatiwa na shambulio katika uwanja wa ndege jijini Brussels.

Mbali na Ulaya, baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Marekani kama vile Donald Trump, wamekuwa wakitoa kauli za chuki dhidi ya Waislamu katika kampeni zao.

Waziri aomba radhi kwa kukejeli hijabu

PADRI mmoja wa Kanisa Katoliki mjini Milan nchini Italia, amesimamishwa kazi baada ya kubainika kuwa amekuwa akimhonga kijana mmoja barobaro ili afanye naye liwati.

Askofu Mkuu wa Kanisa hilo katika eneo la Muggiano mjini Milan, Kadinali Angelo Scola, alisema kuwa amemsimamisha kazi Padri Alberto Paolo Lesmo kwa tuhuma za kumhadaa kijana aliyekuwa muathirika wa mihadarati kati ya mwaka 2009 na 2011 na kisha kufanya naye tendo la liwati.

Padri atimuliwa kwa kuwalawiti vijana Italia“Ni majuzi tu tumegundua kuwa

Padri Lesmo, alikuwa anafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kuhusu uozo huo tangu mwaka 2013, hata hivyo tumeanzisha uchunguzi wetu juu ya tuhuma hizo lakini kwa sasa tumemvua Upadri na kumsimamisha kazi.” Alisema Kadinali huyo.

Madai ya liwati na visa vya kushiriki ngono na watoto wadogo sio mapya kwa Kanisa Katoliki. Katika miaka ya hivi karibuni waathiriwa wa vitendo hivyo vichafu, wamekuwa wakijitokeza hadharani na kufichua kashfa hizo.

Licha ya Kiongozi wa Kanisa

Katoliki duniani Papa Francis, kutoa tamko la kutaka kuchukuliwa hatua za kinidhamu Maaskofu wanaoficha kashfa za kulawitiwa watoto wadogo na Mapadri wa Kanisa hilo, lakini visa hivyo vimekuwa vikiripotiwa kila uchao.

Miongoni mwa nchi ambazo zimerekodi idadi kubwa ya wakuu wa Kanisa Katoliki kugunduliwa kuwa wanawalawiti wavulana wadogo ni Marekani, Ireland, Uholanzi, Australia, Ufaransa, Ujerumani, Austria, Ubelgiji, Canada, Mexico na Poland. parstoday.com

SHIRIKA la ndege la United Airlines la Kimarekani limeitoa familia moja ya Kiislamu ndani ya ndege ya shirika hilo kutokana na muonekano wao wa Uislamu waliokuwa nao.

Gazeti la Independent la Uingereza limeandika kuwa kapteni wa ndege ya shirika hilo aliitaka familia ya hiyo ya Kiislamu kutoka ndani ya ndege kwa sababu ya kuvaa hijabu na kudhihirisha hali ya Uislamu wao, huku kapteni huyo akidai kuwa kuwatoa kwake nje ni kwa ajili ya masuala ya usalama.

Aiman Saadi Shalbiy, mke wake na watoto wake watatu walikuwa wakisubiri ndege kuruka kutoka uwanja wa ndege Chicago O’Hare kwenda Washington, alifuatwa na mhudumu na kapten wa ndege hiyo na kumtaka yeye na familia yake washuke katika ndege hiyo.

Aiman aliwajibu kuwa kitendo chao hicho ni cha udhalili na kibaguzi, Kapten alimjibu kuwa hatua hiyo ni kwa ajili ya usalama wa ndege hiyo.

Baada ya taarifa hizo za udhalilishaji na kibaguzi kulifikia Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani, lilichukua hatua ya kukemea na kulishambulia shirika hilo kutokana na tabia ya kapten wake.

Baadae United Airlines waliamua kuiomba radhi familia hiyo.

Familia ya Kiislamu yatolewa ndani ya ndege Marekani

GAZETI la Washington Post la Marekani limeripoti kuwa polisi nchini humo wameeua karibu raia 1,250 wa nchi hiyo tangu mwaka jana hadi sasa.

Washington Post limeandika kuwa, katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu wa 2016, Polisi wa Marekani imeua raia 256 na mwaka jana iliua raia 990 kwa kuwapiga risasi.

Ripoti hiyo inasema ukatili wa Polisi wa Marekani dhidi ya raia unaongezeka huku jamii ya nchi hiyo ikiendelea kulalamika dhidi ya mwenendo huo wa kikatili wa polisi wanaotumia silaha za moto dhidi ya raia.

Maafisa wa Polisi Marekani wamedai kuwa, idadi kubwa ya raia waliouawa mwaka jana kwa kupigwa risasi na Polisi walikuwa na silaha au walikuwa tishio kwa Polisi na raia.

Hata hivyo maafisa hao wa polisi wamekataa kuweka wazi majina ya waathirika 210 waliouawa mwaka jana kwa kupigwa risasi na Polisi wa nchi hiyo.

Maelfu ya Wamarekani wameuawa na polisi

ANNUUR NEW.indd 5 4/6/2016 9:33:36 AM

Page 6: ANNUUR 1224

6 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Hoja ya Juma Kilaghai

BAADHI ya viungo nyeti vya mwili vinaweza vikabadilishwa na mtu ukaendelea kuishi, na tena ukabaki kuwa mtu yule yule. Maendeleo ya tekinolojia ya kitabibu yamewezesha wagonjwa kuwekewa viungo bandia, au vya watu wengine kama moyo, ini, figo, macho nakadhalika kwa mafanikio. Neno mafanikio linamaanisha kuwa siyo tu kwamba wameendelea kuishi, lakini pia wameendelea kuishi wakiwa na haiba zao zilezile walizokuwa nazo hapo awali.

Kesi ya ubongo ni tofauti kidogo. Kiufundi inawezekana kumwekea mtu ubongo wa mtu mwingine na akaendelea kuishi. Tatizo ni kwamba aliyewekewa ubongo hataendelea kuwa mtu yuleyule. Kihaiba atabadilika na kuwa kama yule mtu aliyekuwa anamiliki huo ubongo hapo awali! Mathalani kama aliyewekewa ubongo alikuwa ni shaikh au padiri, na mtoa ubongo alikuwa jambazi, basi usishangae shaikh au padiri huyo akitoka hospitali akabadilika na kuanza harakati za ujambazi!

Ubongo ni moja ya viungo vya lazima katika mwili. Bila ubongo uhai hauwezekani kwani utendaji kazi wa viungo vyote vya mwili na shughuli zinazofanywa na viungo hivyo hutegemea maelekezo kutoka katika ubongo. Inakisiwa kuwa kwa wastani ubongo wa mwanadamu una kati ya seli bilioni 160 na bilioni 180. Kutokana na umuhimu wa ubongo, kuna haja ya kuchukua hatua za makusudi kuulinda na kuuimarisha.

Kunywa kiasi cha kutosha cha maji safi na salama kila siku ni moja ya mbinu muhimu za kulinda ubongo wako. Kiasi cha kutosha mahitaji ni lita moja ya maji kwa kila kilo 25 za uzito wa mwili wako. Unapokuwa na upungufu wa maji, ubongo wako husinyaa na hivyo basi ufanisi katika utendaji kazi wake hupungua.

Mbinu nyingine muhimu ni kunywa kiasi cha vijiko 3 hadi 4 vya chakula vya mafuta ya nazi (ya kula) kila siku. Hii ni kwa sababu kadri umri wako unavyoongezeka, ndivyo ubongo wako unavyoshindwa kutumia glukosi kama chanzo cha nishati. Hii ni kutokana na seli za ubongo kujenga ubutu dhidi ya homoni ya insulin. Pamoja na kwamba uzito wa ubongo wako ni 2% tu ya uzito wote wa mwili wako, ubongo huo hutumia 20% ya nishati yote inayozalishwa mwilini. Mafuta ya nazi ni mbadala mzuri

Hakuna ubongo bandia au mbadala, chukua hatua kuutunza huo ulionao!

UBONGO.sana wa glukosi kwa sababu hayahitaji insulin kutumiwa na seli za mwili ili kuzalisha nishati. Aidha mafuta ya nazi yamebainika kutoa kinga dhidi ya protini inayojulikana kama amyloid beta. Kuwepo kwa protini hii husababisha uharibifu wa seli za ubongo zinazoitwa neurons ambazo zina jukumu maalum la kusafirisha taarifa kati ya ubongo na maeneo mengine ya mwili. Uharibifu wa neurons pamoja na mambo mengine, husababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaoitwa alzheimer.

Kama ilivyo kwa mafuta ya nazi, tafiti zimebainisha kuwa kutumia kiasi cha kijiko cha chai cha manjano (turmeric) kila siku pia kunatoa kinga mujarabu dhidi ya protini ya amyloid beta.

Kutumia kiasi cha gramu 3 za mafuta ya omega 3 kila siku ni mbinu nyingine mujarabu ya kuupa ubongo wako siha inayohitajika. Omega 3 ni mafuta yanayopatikana zaidi kwenye mafuta ya samaki na mafuta ya viumbe wengine wa majini. Mbegu za mmea aina ya flax pia hutoa kiasi kikubwa cha mafuta ya omega 3. Mafuta ya omega 3 yana faida nyingi sana mwilini ikiwa ni pamoja na kuimarisha ujazo wa ubongo. Tafiti zimebainisha kuwa matumizi ya omega 3 yanatoa kinga dhidi ya ugonjwa wa mfadhaiko (depression) na pia yanasababisha ongezeko la ujazo wa eneo la ubongo lenye tishu za rangi ya kijivu (gray matter), hasa kwenye maeneo yenye seli zinazohusishwa na kujisikia furaha.

Kuulinda ubongo wako unahitaji pia kuacha mambo fulani fulani. Moja ya vitu unavyotakiwa kuachana navyo

ni matumizi ya dawa, vinywaji au vyakula vyenye kiambata cha aluminium. Tafiti zimebainisha kuwa aluminium ni madini yanayosababisha uharibifu wa seli za ubongo.

Ni vema pia kuachana na matumizi ya viuavijasumu (antibiotics) vya kundi la fluoroquinolones. Pamoja na kwamba hivi ni viuavijasumu vyenye nguvu sana, na vinaweza kukukinga dhidi ya maambukizi ya bakteria hatari, hasa ikiwa umefanyiwa upasuaji, lakini viuavijasumu hivi vinahusishwa na uharibifu mkubwa wa seli za akili, mishipa ya fahamu na maeneo mengine ya mwili ikiwa ni pamoja na tumbo, moyo, mifupa, macho, masikio, kano (tendon), nakadhalika. Baadhi ya fluoroquinolones maarufu ni pamoja na: ofloxacin (Floxin®), levofloxacin (Levaquin®, Tavanic®), ciprofloxacin (Cipro®,Baycip®, Cetraxal®, Ciflox®, Cifran®, Ciplox®, Cyprobay®, Quintor®), norfloxacin (Noroxin®, Amicrobin®, Anquin®, Baccidal®, Barazan®, Biofloxin®, Floxenor®, Fulgram®, Janacin®, Lexinor®, Norofin®, Norxacin®, Orixacin®, Oroflox®, Urinox®, Zoroxin®), enoxacin (Penetrex®), lomefloxacin (Maxaquin®), grepafloxacin(Raxar®), trovafloxacin (Trovan®), sparfloxacin (Zagam®), temafloxacin (Omniflox®), moxifloxacin (Avelox®), gatifloxacin (Tequin®), gemifloxacin

Inashauriwa pia kuachana na matumizi ya dawa za kupunguza lehemu (cholesterol) mwilini za kundi la statins. Dawa hizi zimebainika kusababisha madhara kwa mwili

ikiwa ni pamoja na kusababisha uharibifu katika seli za ubongo zinazohusika na kumbukumbu, kusababisha kisukari cha ukubwani na kusababisha uharibifu wa misuli. Dawa hizi ni pamoja na: Altoprev (lovastatin), Crestor (rosuvastatin), Lescol (fluvastatin), Lipitor (atorvastatin), Livalo (pitavastatin), Mevacor (lovastatin), Pravachol (pravastatin), Zocor (simvastatin), Advicor (lovastatin / niacin), Simcor (simvastatin), na Vytorin (ezetimibe).

Aidha, inashauriwa pia kuachana na matumizi ya dawa za mswaki zenye fluoride. Hii ni kwa sababu fluoride ni madini yanayojulikana kuwa yanasababisha uharibifu wa seli za ubongo na mishipa ya fahamu.

Kama uwezekano upo tumia maji yaliyochujwa kwa filter zinazotumia tekinolojia ya reverese-osmosis. Filter hizi zina uwezo wa kuondoa taka mbalimbali kwenye maji ya kunywa ikiwa ni pamoja na mabaki ya dawa za kusafishia na kutakasia (disinfect) maji. Madawa mengi ya kusafishia maji yana kiambata cha aluminium ndani yake na yale ya kutakasia maji yanaweza kuwa na kiambata cha fluoride.

Mwisho funga kula mara kwa mara. Tafiti zinaonyesha kuwa ukarabati katika seli za ubongo hufanyika tu pale inapokuwepo homoni ya ghrelin. Aidha tafiti zinaonyesha kuwa homoni ya ghrelin huzalishwa na mwili pale tu tunapokuwa na njaa. Hii ina maana kuwa unapokuwa umeshiba muda wote, mwili wako hauzalishi ghrelin, na kama mwili wako hauzalishi ghrelin, basi ukarabati wa seli za ubongo haufanyiki.

(Juma Killaghai ni mtaalam wa lishe, ni mtaalam wa stadi za tiba na ni Mkemia Mtafiti wa bidhaa zinazotokana na viumbe hai (Organic Natural Products Research Chemist). Kwa mawasiliano piga: 0754281131/0655281131.

Juma Killaghai ana kibali cha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa ajili ya kutoa elimu inayohusu masuala ya siha; na pia ana leseni ya Baraza la Tiba Mbadala na Tiba Asilia kwa ajili ya kutoa tiba asilia.)

ANNUUR NEW.indd 6 4/6/2016 9:33:39 AM

Page 7: ANNUUR 1224

7 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Kalamu ya Ghassani

RIWAYA ya ‘Babu Alipofufuka’ imeandikwa na mwandishi maarufu wa kazi za fasihi na mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, Profesa Said Ahmed Mohammed, na kuchapishwa na Jomo Kenyatta Foundation mwaka 2001. Katika gamba lake la mbele, pameandikwa: “pengine ni riwaya ya ujasiri mno kupita zote Said A. Mohammed alizowaji kuandika.” Na hivyo hasa ndivyo ilivyo – hii ni riwaya ya kijasiri, ya kimapinduzi.

Hii ni riwaya iliyoandikwa kwa mtindo wa kejeli, lakini yenye mchomo mkali kwa wale wanaoelekezewa kejeli hiyo – yaani watawala waovu – na pia inayoibua hisia nzito kwa wale wanaoathirika na uovu wa watawala – yaani raia wa kawaida.

Uovu wenyewe unadhihirishwa katika riwaya hii kwa namna ya tashnina na inda, lakini katika hali inayowiana sana na ukweli halisi uliomo katika maisha ya kila siku kwenye mataifa yetu ya dunia inayoambiwa inaendelea. Hadithi nzima inasimuliwa kupitia mazingira yasiyo ya kawaida. Huyo Babu mwenyewe Aliyefufuka anatujia kwa umbo la ajabuajabu kupitia kichwani mwa mjukuu wake, K, ambaye ndiye muhusika mkuu. K mwenyewe ni sehemu ya hao watawala ambao kwao kijembe cha riwaya nzima kinaelekezwa. Kwa ustadi wa hali ya juu, mwandishi anampa Babu nguvu za kuziunganisha dunia zetu mbili – baina ya ile tuionayo kwa macho ya nje na ile ionekanayo kwa jicho la ndani tu.

Baina ya dunia hizi mbili, ndipo msomaji anapopewa taswira halisi ya tafauti za waziwazi na za kificho walizonazo wanaoishi ndani yao. Upande mmoja ni maisha ya starehe na anasa za watawala, kule kujilabu na kujitapa kwao, ule uroho na tamaa zao zisizokwisha. Upande wa pili ni maisha magumu ya watawaliwa, kule kutumai na kutamauka kwako, kule kuinuka na kuanguka kwao, na kule kupambana na kujipapatuwa kwao kutoka makucha ya “wenye dunia yao”.

Katika ukurasa wa 14 hadi 15, kwa mfano, tunakutaka na maelezo kuhusu K ambayo yanawasilisha hisia zake za kuutaka na kuupenda ufakhari kama ilivyo kawaida ya watawala wa aina yake:

“Mbali na gari, kulikuwa pia na kasri la kuonewa fahari. Na fahari ndiyo madhumuni yenyewe. Na kasri lake K linamstahiki kwa kila hali, kwa kile cheo cha kiungo. Kama chumvi na chakula alikuwa. Bila ya yeye, mengi ya wakubwa na wadogo hayachapuki… Mjengo wa kasri lake ni wa aina ya zile husuni za tasnifa tunazoziona kwenye sinema za filamu za sayansi ya kubuni.”

Wakati akina K wakiishi maisha hayo ya ukwasi na kujitanua,

‘Babu alipofufuka’.

Na Mohammed Ghassani

akina Kali ndio muhanga wa anasa hizo za watawala. Kwao maisha ni msegemnege na hali zao ni ngumu kupindukia. Huko ndiko kwenye ‘maitikwenenda’ kama wanavyoitwa na mwandishi na walivyowahi kuitwa na Sembene Ousmane kwenye God’s Bits of Wood au Ayi Kwei Armah kwenye The Beautiful Ones Are Not Yet Born.

Katika ukurasa wa 115 hadi 116, kwa mfano, tunasimuliwa maisha ya watu kula togonya na mboga ya kikwayakwaya sio kwa kupenda, bali kwa kuwa hawana namna nyengine. Huku ndiko ambako mtu anakwenda hospitalini kusaka matibabu, lakini anaondoka akiwa ameongezwa maradhi mengine zaidi kwa kuwa serikali imezitelekeza zahanati zake:

“Walipofika zahanati, mlango ulikuwa wazi, lakini mwuguzi aliyekuwa zamuni hayupo. Ilichukuwa saa nzima mpaka alipopatikana. Alikuwa kenda kumpiga mtu sindano kwa pesa. Alipofika alimkagua Kali, alisema anahitajia wembe wa kumnyoa nywele. Kisha uzi wa kushonea anao lakini anahitajia sindano au shazia ambayo hanayo. Alisema japo ya kushonea nguo inafaa. Zaidi ya hayo hana vidonge vya kuondolea maumivu. Plasta pia hakuna… Kali akanyolewa bila maji, akashonwa bila ya sindano ya ganzi, akatiwa plasta na kupewa vidonge viwili vya asprini kubwia…. alipoondoka, juso na jichwa lake zima lilikuwa limemvimba.” (Uk. 121-22)

Huko kunaitwa Kataa na K anaamini kisa cha kuitwa hivyo ni kwa kuwa watu wa huko ni wakaidi na hawakubaliani hata kidogo na watawala wao. Ndiko hasa alikotokea K, lakini ambako mwenyewe amekutupa na kukusahau kwa miaka yote hiyo. Kwa ujumla, hali ya maisha ya watu wa huko ni duni sana, nyumba zao ni dhaifu na hawana pesa za kununulia hata mahitaji ya lazima:

“Mbele zaidi waliposonga wakipasua kiini cha miti na mimea iliyokuwa mali kubwa hapo zamani, maisha na uhali yalianza kujiliza. Vibanda viwili vilivyolalia yombo. Kitambo… vibanda vyengine vitano vikirukuu. Hatua… vibanda vyengine vikisujudu…. ghafla walitokeza mahala ambapo ungeweza kupapagaza jina la sokoni. Watu walionekana… wamesogelea chanja zilizowekwa biashara… wote wametumbua macho, bila ya kuweza kununua chochote. Wengine wanavitumbulia macho vidaka vya nazi. Wengine vichungwa, vilimau, viembe na vipapai… kwenye soko la samaki, mafungu ya dangaauronga na dagaaupapa yakishindana kutumbuliana macho na watu…” (Uk. 95)

Kwa hivyo, riwaya ya Babu Alipofufuka ni kielelezo cha usimulizi unaoakisi uhalisia wa dunia mbili zinazoishi ndani ya jamii moja kwenye mataifa yetu. Mwandishi anampa Babu nguvu za kumfanya mjukuu wake, muhusika mkuu K, azidurusu dunia hizo ambazo kwa kila hali zimekuwa sehemu yake – moja aliyotokea na akaikimbia na kuitelekeza na nyengine aliyokimbilia, kuipenda na kuitukuza. Babu yake alipofufuka na kumjia kwenye maisha yake ya ndani, ndipo anatoa wasaa kwa msomaji kuyaona yaliyomo kwenye nafsi za madhalimu na madhulumu na zinavyosawirika dunia zao.

Baada ya kuziona dunia hizo, mwandishi anamfanya msomaji wake ahitimishe kwa mambo

matatu haya:Kwanza, watu wa aina ya K,

ambao wameendeleza dhuluma kubwa kwa kutumia vyeo na majina yao, huwa wanaishi na khofu ya milele ya kuporomoka. Matokeo yake, kila siku hutamani na kupigania kwenda juu na juu zaidi kusudi wasifikwe na walio chini, ambao wanadhani kuwa endapo mikono yao itawafikia tu, basi watawashika miguu na shingo zao na kuwaporomosha chini kwa kishindo kikubwa. Kwa hivyo, ishara yoyote ya kuporomoshwa huwatia jaka moyo kubwa na kuwatetemesha hadi machango. Katika ukurasa wa 92, mathalan, mwandishi anatuonesha namna K anavyogwaya akiliogopa anguko lake:

“Ghafla alijihisi anachukuliwa na lepe jengine lililomdidimiza katika singizi zito la ajabu. Alitumbukia kwenye singizi huku akienda. Lilikuja tu kwa hakika hilo singizi ama upepo wa ghafla. Lilikuja kumvaa na kumdidimiza kwenye maweko ya chini ya kiini cha dunia. Alihisi anazama kwenye dimbwi refu lisilo ukomo… di, di, di… alididimia mpaka akajihisi ameibuka pahala penye mwangaza wa maisha. Akajihisi kama katupwa hapo. Katupwa kama gunia. Moyo ukaanza kupiga beni alipogundua hivyo. Aa, kubwagwa kila siku yeye alikuwa akikuogopa. Kuanguka alikuchelea. Akihofu kutupwa, hasa namna hiyo.”

Pili, msomaji anahitimisha kuwa watawala wa aina ya K wanakuwa wanajijuwa hasa kwamba wamewakosea raia. Kwa hivyo, kila wanapokaa huwa wanajitia wasiwasi kuwa wanaandamwa au wanafuatwafuatwa na watu hao wenye hasira na wakati wowote wanaweza kulipiziwa kisasi kwa maovu yao. Hayo ndiyo matokeo ya kuishi kwa dhuluma. Siku zote huwa unakhofu kuwa madhulumu wako watakurudi kwa yale uliyowatenda. Huwa huko huru. Angalia vile wanavyopita barabarani kwenye magari yaliyofungwa vioo vyote, tena vyeusi visivyopenya risasi na bado mbele yao ving’ora mita kadhaa ili wapishwe njia peke yao na bado maaskari kibao na bunduki. Hawa hawafanyi yale kwa kupenda, bali kutokana na khofu waliyonayo kwa umma walioukosea (Uk.24-7). Wakati Babu anamzukia K kwa mara ya kwanza kwenye ndoto-macho zake, alijitambulisha kwa namna hii:

“Nikwambie tena, mimi ni babu yako; kisha niongeze kuwa mimi ni dhahiri kwa kisia kikubwa kuliko hata wewe, kwa sababu sina farakano na watu. Wala sina makiwa na utawa kama ulionao wewe. Sina hofu wala siogopi kama uogopavyo wewe. Nakwenda nipendapo. Nakutana na nimpendaye. Ufunguo wa kasi yangu ninao mwenyewe. Hakuna niliyemdhulumu.” (Uk. 21-2)

Tatu, msomaji anahitimisha kuwa khofu hizi za watawala zina uhalali wake na ni za kweli. Ni kweli kuwa wananchi walioonewa na kudhulumiwa kwa miaka mingi hufika pahala pa kusema “hapana” kwa watawala wao. Miongoni mwao huwa wanasema hivyo kwa maneno, wengine kwa vitendo, wengine wakiwa na akili zao na wengine tayari wameshachanganyikiwa kwa

mateso ya muda mrefu. La muhimu ni kuwa wananchi hufika mahala wakasema “liwalo na liwe” lakini hawatakubali tena dhuluma nyengine dhidi yao. Katika ukurasa wa 92, K alimkuta Mussa katika eneo la Kataa akijisemea peke yake njiani:

“La, hatutaki, hata ikiwaje hatutaki tena…. La, hatutaki, hata iwaje hatutaki tena…. La, hatutaki, hata ikawaje, hatutaki tena..”

Lakini madhulumu wengine huamua kwenda mbali zaidi ya kupita mitaani wakijisemea peke yao tu. Wao huamua kuwarudi madhalimu wao kwa namna yoyote ile wanayoiona inawafalia na wanaimudu. Mno yachosha eti! Na ni hiki ndicho ambacho kinadhihirika mwishoni, pale umma uliokwishachoshwa na udhalimu wa watawala wao, unapoingia barabarani na kuukabili mkono wa utawala.

“Nje aliwakuta wale mahasimu zake wamejipanga upande huu na huu wa njia. Sasa walikuwa mamia kwa mamia… Kuna waliochukuwa marungu na wengine mabango yaliyoandikwa maneno mengi…M’MEZIFISIDI NAFSI ZETU…. MMEVUNJA HESHIMA ZETU…. VIJANA WETU WANAPOTEA… VIFO NA NJAA NA MARADHI SABABU SI SISI… HATUNA NAFASI PANAPOSTAHIKI NAFASI ZETU… ARDHI INACHUKULIWA HIVI HIVI TUNAONA…. KESHO YETU IMO KATIKA GIZA…TUNAANGAMIA…TUMESHAKWENDA KAPA…na zaidi na zaidi…Mlio ule wa bunduki K aliusikia ndani apokuwa tayari ameshakua kitini ofisini mwake. Alitetemeka kwa muda. Lakini alipojishika, aligunduwa kwamba hata ofisini mambo yalikuwa yamegeuka pia.” (Uk. 154-56)

Riwaya inamalizika kwa kumuonesha K akipoteza kila kitu – ulwa, nyumba, gari na, zaidi kuliko yote, hata ile heshima aliyojidhani alikuwa nayo. Na mwisho anakufa kifo cha kidhalilifu kama alivyosababisha maelfu ya wengine kufa katika udhalilifu kwenye zama za madaraka yake.

“Alfajiri ya siku ya pili, watu wa kijiji kile waliamshwa na sauti ya jibwa kubwa, Biye aliloliita Doggy. Ilikuwa si kawaida jibwa kubwa kama lile kubweka kwa muda mrefu namna ile hapo kijijini. Walipoufuata mbweko wa jibwa, walimkuta K ananing’inia kwenye kigogo cha mti uliokuwa umeota katikati ya kaburi la Babu. Alikuwa mkavu keshang’ang’anaa.” (Uk.165)

Naam, hapa ndipo hasira ya umma ilipomfikisha K. Hapa, kwa hakika, ndipo kiuhalisia wafikishwapo watawala madhalimu wa aina yake. Hivyo ndivyo umma unavyomuhukumu mkosaji wake. Umma ukikosewa kiasi kikubwa kama hiki, ni wenyewe ndio ambao hushitaki, na wenyewe ukahukumu. Na hivi ndivyo Babu Alipofufuka na kumtahadharisha mjukuu wake, K:

“…Pia unashitakiwa na wakati ulioutumia vibaya…Unashitakiwa vile vile na matendo yako mwenyewe…matendo ya upotofu…Maovu yako mwenyewe….Hakuna uchaguzi. Huna njia. Wakati ukifika, utakwenda tu; utakwenda tu…” (Uk. 137)

ANNUUR NEW.indd 7 4/6/2016 9:33:41 AM

Page 8: ANNUUR 1224

8 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

DENIS Galava alikuwa mhariri katika gazeti la Nation linalochapishwa kila siku jijini Nairobi. Hili ni gazeti linalomilikiwa na kampuni ya Nation Media Group (NMG), pamoja na mengine yaliyoko Uganda na Tanzania. Mmiliki wake mkuu ni Aga Khan. Moja ya majukumu ya Galava ilikuwa ni kuandika tahariri. Na ndipo mwishoni mwa 2015 ikaamuliwa kuwa aandike tahariri maalum kuukaribisha mwaka mpya wa 2016. Alitumia muda wa saa sita akifanya utafiti katika maktaba, akisoma habari kuhusu mwaka 2015. Akakuta habari kuhusu skandali, migomo ya wafanyakazi, mashambulizi ya kigaidi, kutetereka kwa uchumi na kadhalika. Mwishowe akaamua huo ulikuwa mwaka wa maumivu na mateso kwa wananchi wa Kenya.

Akaanza kuandika tahariri ikiwa katika mfumo wa barua kwa rais Uhuru Kenyatta, ikisema: “Mheshimiwa Rais, jirekebishe katika mwaka huu wa 2016.” Akamkumbusha rais kuwa anasahau ahadi alizotoa kabla ya kushika madaraka mnamo 2013. Akaendelea:

“Mheshimiwa Rais, mwaka 2015 ulikuwa ni mbaya kwa Wakenya. Misingi ya taifa letu imetikisika na kuingia nyufa. Familia chache za matajiri zimekuwa zikizoa mabilioni kupitia zabuni za ajabu kwa ushirikiano wa wanasiasa. Mwananchi anaachwa nyuma, mamilioni wanakosa ajira na idadi yao inaongezeka.”

Galava akabuni neno la kimombo tenderpreneurs kwa maana ya ‘wajasiriatenda’ badala ya ‘wajasiriamali ili kuelezea tabaka la mafisadi wanaochota mabilioni kwa kupitia tenda/zabuni bandia za serikali. Alimradi Galava hakumung’unya maneno. Alisema yale aliyokusudia.

Tarehe 2 Januari 2016 tahariri hiyo ikachapishwa katika

Na Nizar Visram

Uhuru wa Habari mashakani nchini Kenya gazeti la ‘Nation.’ Mara moja mtandao wa jamii ukafurahia na kumpongeza Galava kwa kusema ukweli. Lakini si wote waliofurahi. Siku iliyofuata mhariri mtendaji wa NMG (wikiendi), Bw Eric Obino alimuita na kumwambia kuwa tahariri hiyo ilikuwa na maneno makali ingawa ni ya ukweli. Baadaye ofisa mwandamizi kutoka ikulu ya Nairobi aliipigia simu ofisi ya NMG na kusema kuwa mheshimiwa Kenyatta alikuwa amekasirishwa na anakusudia kumueleza Aga Khan ambaye ni mmiliki wa NMG. Mhariri mkuu wa NMG, Bw Tom Mshindi akawa na wakati mgumu. Bila shaka mengi yalizungumzwa kati yake na bodi ya kampuni. Kwani siku tano baada ya tahariri kuchapishwa Galava akaitwa na bosi wake Tom Mshindi. Akamtaarifu kuwa anasimamishwa kazi. Tarehe 20 Januari akaambiwa anafukuzwa kazi. i”

Galava aliambiwa kosa lake ni kutofuata utaratibu wa kushauriana na wakuu wake kabla ya kuchapisha tahariri. Yeye akajibu kuwa amewahi kuandika tahariri zaidi ya 100 na hajawahi kuelezwa kuhusu huo ‘utaratibu’. “Huo utaratibu haukuwepo, ulibuniwa wakati nikisimamishwa na kufukuzwa,” akaongeza.

Galava anasema ukweli ni kuwa mabosi wake wamekuwa wakimkanya asiendelee kufichua kashfa za NYS, Eurobond na kahawa. Walimuambia kuwa kashfa hizo zinahusishwa na muungano wa vyama (Jubilee) unaoongozwa na rais Kenyatta. Hicho ni chanzo cha kufukuzwa kwake na wala si kutofuata taratibu.

Inakisiwa kuwa nchini Kenya asilimia 40 hadi 50 ya mapato ya vyombo vya habari yanatokana na matangazo ya serikali na mashirika yake. Hii inatumika kama njia ya kuwadhibiti wahariri. Hata makampuni makubwa nayo yanatumia mbinu hiyo hiyo. Mwanaharakati mmoja wa chama cha wahariri nchini Kenya amesema, kwa mfano, ni vigumu sana kuandika habari ikizikosoa kampuni za mawasiliano na mabenki. Akaongeza kuwa wakati huohuo vyombo vya habari vinazidi kuhodhiwa na matajiri wachache.

Hivyo, kampuni mbili za habari nchini zinamiliki magazeti 13, vituo vya redio vitatu, na vituo vya TV vitatu. Mara nyingi wanasiasa na watawala wanakuwa na hisa katika makampuni haya. Kwa maneno mengine, wamiliki wa magazeti na TV wakiwa wafanyabishara na wawekezaji, basi ni muhali kwa vyombo

hivyo vikahatarisha maslahi yao ya kibiashara na kisiasa. Katika hali kama hiyo ni vigumu kuzungumzia uhuru wa habari.

Galava sasa amewasilisha kesi mahakamani, akiishitaki NMG kwa kumfukuza kazi kinyume cha sheria. Anadai fidia ya shilingi za Kenya milioni 400. Katika mashtaka yake anasema: “Naamini kuwa mhariri mkuu amekwepa weledi na wajibu wake kwa kunisimamisha kisha kuniachisha kazi ili kujikomba kwa vigogo wa kibiashara na kisiasa”

Hata hivyo utawala wa NMG umekanusha kwa kusema kuwa Galava alikuwa amekiuka taratibu na kanuni za kuchapisha tahariri. Galava anasema huo utaratibi haukuwepo na ulibuniwa baada ya yeye kusimamishwa.

Katika kesi yake anadai kuwa Tom Mshindi aliwahi kumuonya kuwa aache kuandika habari za skandali, hasa zile zinazohusu chama tawala cha Jubilee na rais Kenyatta. Anasema alikataa agizo hilo kwani litawavunja moyo waandishi wanaofanya kazi chini yake.

Galava anasema siku chache kabla ya Aga Khan kuwasili Kenya kama mgeni rasmi katika sherehe ya Jamhuri mnamo Disemba 2015, Tom Mshindi alimuita na kumwambia makala za kashfa zisimamishwe. “Akaniambia kuwa serikali inaweza kukasirishwa na hivyo kuikosesha NMG mapato,” akaongeza.

Magazeti ya NMG yamekuwa yakisifika sana nchini kwa msimamo wake wa kutetea haki na ukweli. Msimamo huu ulianza katika awamu ya Rais Daniel arap Moi ambaye alitawala kimabavu kwa muda wa miaka 24 chini ya chama chake cha KANU. Nation ilithubutu kusema ukweli na hata kumkosoa Moi. Gazeti likajenga umaarufu na likawa linaongoza katika sekta ya habari.

Moi alidai kuwa utawala wake ni “demokrasia ya chama kimoja”. Wakati huo alikosolewa na watu wengi, pamoja na viongozi wa dini waliofichua udikteta wake. Mwishowe wafadhili wakasimamisha misaada yao ya dola milioni 350. Ndipo Moi akatii amri zao na kuanzisha uchaguzi wa vyama vingi. Hiyo ikawa ni fursa ya kumtimua madarakani, licha ya jitihada zake za kuwagawa wananchi katika misingi ya kikabila na dini. Pia alifanya jitihada za kuchakachua matokeo ya uchaguzi lakini akashindwa.

Baada ya Moi akaja Mwai Kibaki kuanzia 2002 hadi 2013. Inasemekana chini ya utawala wake vyombo vya habari vilipewa nafasi ya kupumua. Lakini Kenyatta alipoingia Ikulu mwaka 2013 mambo yakaanza kuharibika na wengi sasa

waamini kuwa Kenya inarudia mfumo wa zamani.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 inahakikisha uhuru wa habari. Hata hivyo tangu muungano wa vyama vya Jubilee (sawa na Ukawa ya hapa petu) kuchaguliwa mwaka 2013, Rais Kenyatta amepitisha sheria zinazominya uhuru huo.

Kwa mfano iwapo mwandishi anaandika habari ambayo inakisiwa kuwa inadhoofisha jitihada za kupambana na ugaidi, basi anaweza kuwekwa gerezani miaka mitatu na kutozwa faini ya shilingi za Kenya milioni tano. Hata hivyo asasi za wanahabari zikapinga sheria hizo mahakamani na kesi ingali inaendelea. Wakati huohuo wanaharakati wanasema waandishi wanaendelea kudhalilishwa. Asasi ya Freedom House (kituo cha uhuru) imeripoti mnamo 2014 kuwa waandishi wasiopungua 19 walishambuliwa. Mmoja kati yao ni John Kituyi ambaye alipigwa hadi kufa mjini Eldoret, mnamo Aprili mwaka jana. Wauaji wakaondoka na simu yake wakaacha fedha na saa ya mkononi.

Leo hii Kenya inashika nafasi ya 100 kati ya nchi 180 katika uhuru wa habari. Mwaka 2002 ilikuwa ya 75, yaani kiwango chake kimeporomoka. Pia mnamo 2013 wanahabari takriban 300 walihojiwa kote nchini. Zaidi ya asilimia 90 walisema kuwa wamewahi kutishwa kutokana na kazi zao. Wengi wao walisema kutokana na mazingira hayo waaandishi wameamua kujizuia kuandika habari za kashfa.

Tukiachia kufukuzwa kwa Galava, mwengine aliyeachishwa kazi hapo Nation ni mchoraji maarufu wa vibonzo anayejulikana kama Gado. Huyu ni Mtanzania aitwae Godfrey Mwampembwa ambaye amekuwa na NMG tangu 1992. Mwishoni mwa mwaka jana aliitwa na Tom Mshindi na kuambiwa kuwa mkataba wake umemalizika. Alipouliza sababu aliambiwa “wao wameamua”. Alipouliza ni nani hao hakupata jibu.

Mara kadha Gado amewahi kuchora vibonzo vilivyowakwaza watawala wa nchi za Afrika Mashariki – kuanzia Kenyatta na Museveni hadi Kikwete. Kufukuzwa kwa Gado kumelaaniwa na asasi ya kimataifa ya kutetea haki za wanahabari (PEN) pamoja na matawi yake nchini Kenya na Afrika Kusini. Mchoraji maarufu wa vibonzo nchini Afrika Kusini aitwae Zapiro naye amelaani kufukuzwa kwa Gado.

(0713 562181) [email protected]

ANNUUR NEW.indd 8 4/6/2016 9:33:43 AM

Page 9: ANNUUR 1224

9 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

UBUNGO ISLAMIC HIGH SCHOOL KIRINJIKO ISLAMIC HIGH SCHOOL NYASAKA ISLAMIC HIGH SCHOOL

Waislamu kote nchini mnatangaziwa nafasi za Kidato cha Tano kwa shule zifuatazo:Ubungo Islamic High School - Dar es Salaam : 0687 820895/0657 350172Kirinjiko Islamic High School - Same, Kilimanjaro: 0784 296424/0756 676441Nyasaka Isamic High School - Mwanza: 0786 417685/0713 749020Shule hizi ni za Kiislamu zenye lengo la kuwapa wanafunzi taaluma ya hali ya juu na malezi bora ya Kiislamu. Shule hizi ni za BWENI za mchanganyiko wa wavulana na wasichana.Zipo Combinations zote za SAYANSI, ARTS na BIASHARA.Muombaji awe na ufaulu wa masomo matatu (3) kwa kiwango cha ‘Credit’ (yaani A, B na C) Daraja la III (Division three) au zaidi na Grade D kwenye masomo ya Combination.

Mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 02/05/2016. Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 10,000= katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

NAFASI ZA KIDATO CHA TANO - 2016/2017

WAHI KURUDISHA FOMU ILI UJIHAKIKISHIE NAFASI

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu Bondeni : 0783 438676/0715 438676.KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:0767345367/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0713 115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. Ugweno – Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa: 0784 655614TANGA: Twalut Islamic Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop - Lushoto: 0782257533. Handeni –Mafiga -0782 105735/0657093983MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770/0714097362.BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484

KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531 MOROGORO: Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu: 0659 158958GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056DODOMA: Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel – karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039. MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid Rahma: 0784491196KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727. Kibondo – Islamic Nursery School: 0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802/0763 298440LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783

488444/0653 705627.MTWARA: Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic High School :0654 876317MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini – 0785425319. Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319. Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786 313830TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754 576922/0784576922.IRINGA: Madrastun – Najah: 0714 522 122.PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.UNGUJA: Madrasatul – Fallah: 0777125074. PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa LumumbaMAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.

FORM V TANGAZO.indd 1 3/21/2016 3:58:37 AM

Tangazo

ANNUUR NEW.indd 9 4/6/2016 9:33:45 AM

Page 10: ANNUUR 1224

10 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

Na Omar Msangi

NI kiasi wiki mbili sasa toka litokee shambulio lililoitwa la kigaidi katika uwanja wa ndege wa Zaventem, Brussels, Ubelgiji. Kiasi watu 34 wanadaiwa kuuliwa huku ikidaiwa kuwa ‘magaidi wa Islamic State (IS)’, wamedai kuhusika. Taarifa ya polisi ilidai kuwa ilikutwa bendera ya IS katika eneo la tukio pamoja na milipuko (mabomu ya misumari). Imekuwa ni ada hivi sasa, kila yakitokea matukio kama haya, iwe ni Dar, Nairobi, Ulaya au Marekani, basi polisi hawatakosa kuwa na kitambaa cheusi chenye maandishi ya Kiarabu na kudai kuwa ni bendera iliyokutwa eneo la tukio, ikiwa ni alama kuwa wahusika ni magaidi wa IS, Al Shabaab au Boko Haram.

Maadhali vumbi lishatulia na ile karamu ya habari kwa vyombo vyetu vya habari, inamalizika, sasa ni wakati muafaka kwa wenye akili zao timamu kukaa na kuchambua kujua ukweli. Nini kilitokea, nani alihusika kwa lipi na kwa sababu gani, nini agenda.

Ipo aya ndani ya Qur’an ambayo inasema kuwa wengi katika majini na wanadamu wataingia motoni (Jahannamu) kwa sababu nyoyo wanazo lakini hawataki kufahamu kwazo, na macho wanayo lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Aya inamalizia kwa kusema kuwa hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotofu zaidi. Na hao ndio walioghafilika. (Al-A’raf: 179)

Ukiisoma aya hii, unaweza kujiona kuwa wewe huhusiki kwa vile unavyojiona kuwa ni mjanja, unayaelewa mambo. Lakini tuchukulie mfano mdogo wa tukio hili la Brussels. Waandishi na watangazaji wa Televisheni zetu na magazeti yetu, yakinukuu habari za CNN, BBC, Sky News, CBS, ABC na wengine, wametuambia kuwa magaidi wa IS walifanya shambulio la kujitoa muhanga katika jiji la Brussels na kuuwa watu kadhaa huku wengi wakijeruhiwa. Hapana shaka tumeziamini habari hizo.

Baada ya vumbi kutulia, baadhi ya wachambuzi wamechukua habari zile zile zilizoitwa za ‘Breaking News’ kama zilivyorushwa na CNN, Fox News na BBC na kuanza kuzichambua.

Katika jumla ya habari na picha zilizoonyeshwa katika televisheni kuelezea tukio hilo, ni watu walioonekana kuwa ni wasafiri, wakiwa na mabegi yao wakiwa barabarani, Wazungu na watu Weusi. Kijana mmoja Muafrika anahojiwa anasema:

“Kuna majeruhi wengi sana.

Ugaidi Ubeligiji…

Padiri afichua kitendawili kuchomwa kanisa Yombo

Bendera ya IS Dar, Paris hadi Brussels

uchambuzi wake.)Katika tukio hili, mtoa habari

mkuu ambaye inadaiwa alikuwa katika eneo la tukio akisafiri kwenda Geneva, ni mwandishi Ketevan Kardava (36) wa Shirika la Utangazaji la Georgia (Georgian Public Broadcaster). Katika CNN na CBS News, Keteban Kardava anaonekana akihojiwa akisema yupo katika eneo la tukio. Anasema kuwa mlipuko umetokea, watu wanakimbia ovyo, wengi wamejeruhiwa, wametapakaa damu usoni na mwilini, maiti zimezagaa chini, huku wengine wakiwa wamekatika viungo. Akisema hivyo, zinaletwa picha kuonyesha hali ilivyo uwanja wa ndege. Hapo unachoona ni watu wanaendelea na shuguli zao, wapo wanaochati na simu, wengine ni wapenzi wamekumbatiana, wengine wanatembea ama wakitoka nje ya uwanja au wakiingia. Ila utaona watu watatu, mmoja mwanamume kalala chini anaonekana kama ana damu mguuni suruali imechanika, akionekana kama anaomba msaada. Kwa mbali anaonekana mwingine kalala chini akionekana naye kama anaomba msaada. Sasa mchambuzi kwa kutumia picha hizo hizo za CNN anauliza, watu waliotapakaa damu usoni wapo wapi? Watu waliokatika viungo wapo wapi? Maiti zilizozagaa zipo wapi? Inakuwaje lilipuke bomu, baadhi ya watu wafe na wengine waumie, wamelala chini, lakini abiria wengine hawana habari wanapita na kuendelea kuchati na simu zao?

Mchambuzi anakupeleka ndani ya uwanja na kukuonyesha picha za CCTV, abiria wanaowasili na wanaosubiri kuondoka hali ni shwari kabisa. Ila baaade anakuja askari mmoja wa kike, mrefu ameshika tochi mkononi, anawafukuza. “Tokeni nje. Ondokeni hapa kuna tukio sio la kawaida”. Abiria wanabaki wakimtizama askari huyo huku wengine wakiburuta mabegi yao ya safari. Hawaelewi kwanini wanaambiwa tokeni nje.

“You have to go out”. Nasema tokeni nje, anafoka polisi. “Okay, okay, okay, I go”, anaonekana abiria mmoja akimjibu polisi huyo na kuanza kuburura begi lake kutoka nje. Anapofika nje, anabaki kushangaa, hali ni shwari, ila kunaonekana kuwa na askari na magari kama ya ambulesi yamesimama kwa mbali na kuna mtu amelala chini akionekana kama amejeruhiwa.

Katika televisheni, France24, kichwa cha habari cha ‘Breaking News’ juu ya shambulio hilo, kilikuwa “Frenzy and Chaos inside and outside airport”. Sasa mchambuzi anakupitisha katika

Inaendelea Uk. 11

Lakini bahati nzuri watu wa uokozi, zima moto na magari ya kubebea wagonjwa (ambulances) walifika mapema sana.”

Mwandishi anamuuliza: “Uliona bomu lilikotokea? Anajibu: “Bomu lilipuka katika eneo abiria wanaoondoka wanaposubiria (departure level). Nilikuwa nimewasindikiza watu wa familia yangu walikuwa wakisafiri.”

Mwandishi anawageukia watu wengine wakiwa na mabegi. Huyu ni Mzee wa Kizungu akiwa kavaa jaketi, Mama wa Kizungu akiwa na jaketi jeupe na kijana mmoja wa Kiafrika.

Mzee wa Kizungu anasema: “Nilikuwa katika eneo la kuondokea abiria nikiwa na familia yangu. Nikaondoka kidogo tu, kiasi dakika tano, bomu likalipuka. Mabomu mawili yakalipuka. Familia yangu bado wapo pale (sijui kama wazima au wamekufa.)”.

“So what is it like there now-hali ikoje sasa baada ya mabomu hayo? Anauliza mwandishi.

“Nothing is left. There is nothing left.” Anajibu. Na wakati anajieleza mzee huyo wa Kizungu, anaonekana akipita yule kijana wa Kiafrika akichechemea kama ameumia

mguu.Ukitizama taarifa hizo kama

zilivyokuwa zikirushwa katika TV, utadhani ni kweli kabisa, ni tukio halisi. Sasa nakuomba msomaji fungua: “Brussels Joins the Terrible Crisis Actor’s Guild.”

Watu wametafiti, wameibuka na mkanda wa igizo hilo lilipofanyika. Ilikuwa ni katika barabara moja na pia katika uwanja. Unaona kabisa watu wanavyopangwa na kuigiza. Wasanii wacheza filamu, ukiwaambia toka au ingia katika ‘shot’, wanajua nini maana yake. Yule kijana wa Kiafrika anaonekana amesimama kando wakati babu Mzungu akihojiwa, halafu anapewa ishara ya kuingia katika ‘shot’. Anakuja taratibu anatembea, hachechemei, anapofika mahali pa kuingia katika ‘shot’ kwa maana kwamba sasa kamera inamsoma, anaanza kuchechemea. Kama nilivyosema, tazama: Brussels Joins the Terrible Crisis Actor’s Guild. (If this doesn't sway you into believing that the Brussels Bombing was nothing but a TOTAL GOVERNMENT SPONSORED PSYOP...NOTHING WILL.-Ndivyo anavyosema mchambuzi wa mkanda huo anapomaliza

MWANDISHI Ketevan Kardava.

ANNUUR NEW.indd 10 4/6/2016 9:33:48 AM

Page 11: ANNUUR 1224

11 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 201611 AN-NUUR

Inatoka Uk. 10

Makala

Padiri afichua kitendawili kuchomwa kanisa Yombo

picha hizo hizo za televisheni, anakuuliza hiyo taharuki ipo wapi? Maana watu wapo wanaendelea na shuguli zao, ukiacha wale, unaoweza kusema kuwa ni ‘wasanii’ walioandaliwa kwa ‘igizo’ hilo.

Katika taarifa moja ya NBC News na BBC walionyesha mtu mmoja amebeba mtoto mchanga na kudai kuwa ni mmoja wa watoto waliokolewa katika shambulio hilo. Lakini hebu tizama video hii inayopatikana katika Youtube - Brussels attack hoax, A closer look part 4. Kilichodaiwa kuwa ni mtoto, ilikuwa mdoli. Na aliyedaiwa msamaria mwema, ni ‘msanii’ akiigiza kama muokoaji wa majeruhi. Kabla ya hapo alionyeshwa mama mmoja akiigiza kulia, akadai kuwa alikuwa na watoto wawili, mmoja hamuoni. Tazama pia: The Journalist and the Basketball Player (Brussels Bombing Hoax). A look at a couple of the main characters from the Brussels Bombing Story.

Katika tukio hili, mchezaji huyo wa basketball wa zamani wa Canada, Sébastien Bellin anaonekana kalala chini ikidaiwa kuwa kavunjika miguu. Suruali ya jinzi aliyovaa inaonekana kuchanika upande wa chini, lakini uso unamuumbua hauonyeshi kuonyesha maumivu. Baadae anaonyeshwa akiwa hospitali anakuja Ketevan Kardava wanakumbatiana na kuangua kicheko. Hiki kinaonekana wazi kuwa kicheko cha kupongezana kufanikisha ‘igizo’. Mchambuzi mmoja anavuta kwa karibu picha ya mchezaji huyo akiwa kalala chini alipodaiwa kuanguka alipoumia, picha inaonyesha wazi kuwa suruali inayoonekana kuchanika imefanya kufungwa juu ya nguo yake aliyovaa. Imefungiwa juu kidogo ya paja.

Lakini kitu kingine kinachotatiza juu ya taarifa ya mwandishi Ketevan Kardava wakati akihojiwa na CNN ni kuwa anadai kuwa alikuwa karibu kabisa na begi jeusi ambalo inadhaniwa ndio lilikuwa na bomu. Ghafla likalipuka. Akaona watu wamekatika viungo, na wengine damu kutapakaa usoni huku maiti nazo zikizagaa. Lakini huyu Ketevan Kardava yeye haonyeshi kuwa na hata chembe ya jeraha wala damu. Tujaaliye kuwa ulitokea muujiza yeye hakujeruhiwa. Bomu zito limelipuka, sekunde chache baadae linalipuka la pili, watu wanakimbia ovyo, ujasiri gani atakuwa nao mwana mama huyu, badala ya kukimbia kusalimisha maisha yake, yeye anatoa kamera na kuanza kupiga picha?

Taarifa ya USA TODAY

ikimnukuu Kardava inasema: "Everyone was covered in blood. They lost their legs. All of them. I was not able to help them. I kept looking to see my legs. With my hands, I wanted to feel them."

Kwamba baada ya mlipuko mwandishi Kardava aliona watu wakiwa wametapakaa damu, wakiwa wamevunjika miguu. Na hakuweza kuwasaidia kwa sababu naye alikuwa ameumia akipigwa na mshtuko akidhani kuwa naye kapoteza miguu yake.

Katika CNN wakati anaeleza hayo, picha katika uwanja wa ndege linapodaiwa kutokea tukio, hakuna hata mtu mmoja anayeonekana kukatika mguu. Na yeye Kardava hakuweza kuonyesha hata picha moja ya anachokisema. Anaulizwa na mtangazaji wa CNN, ulikuwa umbali gani kutoka ulipotokea mlipuko? Anajibu “very very near”, inaweza kuwa kiasi cha mita tano, sita hivi. Sasa kama alikuwa “very, very near”, mbona hana hata mchubuko wakati watu wengine anadai kuwa wamekatika miguu? Lakini kitu kingine cha kushangaza ni kauli yake kwamba alijua yeye ni mwandishi pekee aliyeko katika tukio hilo. Anasema:

“I new I was the only one (journalist) at this spot. It was my duty to take these photos and show the world what was going on.” (CNN 22. 3. 2016)

Swali ni je, huyu mwandishi alijuaje kuwa ni yeye pekee aliyekuwepo katika eneo la tukio na ulimwengu mzima unategemea picha zake? Yeye anasema alikuwa msafiri kama wasafiri wengine. Alijuaje kuwa hapakuwa na msafiri mwingine aliyekuwa pia mwandishi wa habari?

Kwa kifupi ukitizama picha hizo za CNN na wenzake, kama hupo katika lile kundi la watu waliotajwa katika Al-A’raf: 179, utakuwa na maswali mengi ya kujiuliza badala ya kumeza tu taarifa kama zinavyotolewa na vyombo vya habari.

Mapadiri kutoka MarekaniKipo kile kitendawili cha

mapadiri kutoka Marekani ambao nao walidaiwa kujeruhiwa katika shambulio

Inaendelea Uk. 16

HUU ni mfano wa kidonda cha 3rd degree burn.

PICHA kulia vijana wawili watumishi wa Kanisa la The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (Mormons) waliodai kuunguzwa na mabomu uso na mikono katika tukio la kigaidi Brussels. Juu kabisa kabla ya tukio na chini wakiwa Hospitalini.Linganisha mikono yao na uso wao unaodaiwa kuungua kwa 3rd degree burn na kidonda halisi hapo chini. Mason Wells alikuwa pia katika shambulio la Boston na Paris.

ANNUUR NEW.indd 11 4/6/2016 9:33:50 AM

Page 12: ANNUUR 1224

12 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 201612 Tangazo

ISLAMIC PROPAGATION CENTRE

Muda wa Kozi ni miaka miwili

SIFA ZA MUOMBAJI:(a) Awe Muislamu.(b) Awe amefaulu masomo matatu (3) au zaidi kwa kiwango cha D au zaidi katika Mtihani wa Kidato cha 4.(c) Atakayekuwa na ufaulu wa kiwango cha D au zaidi katika masomo ya Lugha ya Kiarabu, Kiingereza, Kiswahili na Elimu ya Dini ya Kiislamu atapewa kipaumbele zaidi.Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 15 JULAI, 2016.Fomu za maombi zinapatikana kwa gharama ya Shilingi 5,000/= (elfu tano) katika Tovuti:www.ipcorg.tz na katika vituo vifuatavyo:

KOZI YA UALIMU WA LUGHA YA KIARABU, KIINGEREZA, KISWAHILI NA ELIMU YA DINI YA KIISLAMU NGAZI YA CHETI 2016/2017

USIKOSE NAFASI HII ADHIMU - WAHI KUCHUKUA FOMU SASA!

Bismillahir Rahmaanir Rahiim

KIRINJIKO ISLAMIC TEACHERS’ COLLEGE - SAME, KILIMANJARO

Kwa maelezo zaidi piga simu: 0787 188964, 0784 267762 na 0654 613080

ARUSHA: Ofisi ya Islamic Education Panel, Jambo Plastic, Ghorofa ya 2 mkabala na Msikiti Mkuu Bondeni : 0783 438676/0715 438676.KILIMANJARO: Moshi: Msikiti wa Riadha:0767345367/0686938077. Same Juhudi Studio mkabala na Benki ya NMB Same: 0757 013344. Same: Kirinjiko Islamic Secondry School: 0784 296424/0713 115041. Usangi- Falhum Kibakaya : 0787 142054. Ugweno – Simbomu centre Mwl. Hidaya A. Mussa: 0784 655614TANGA: Twalut Islamic Centre – Mabovu Darajani : 0715 894111/0713 014469. Uongofu Bookshop: 0784 982525. Korogwe: SHEMEA SHOP : 0754 690007/071569008. Mandia Shop - Lushoto: 0782257533. Handeni –Mafiga -0782 105735/0657093983MWANZA: Nyasaka Islamic Secondary School : 0717 417685/0786 417685. Ofisi ya Islamic Education Panel – Mtaa wa Rufiji mkabala na Msikiti Al-Amin 0785 086 770/0714097362.BUKOBA: Ofisi ya Kutaiba Saccos: 0765 748056MUSOMA: Ofisi ya Islamic Ed Panel -Mtaa wa Karume,Nyumba Na. 05 : 0765024623/0787868611SHINYANGA: Msikiti wa Majengo karibu na Manispaa

ya Shinyanga Mjini :0655608139/0768895484KAHAMA: Ofisi ya Kamati ipo karibu na zahanati ya Doctor Dalali: 0754 994738/0782 994738Dar es Salaam: Ubungo Islamic High School : 0756584625/0657350172/0712 033556. Ofisi ya Islamic Ed. Panel –Temeke -Msikiti wa Nurul Yakin : 0655144474/0787119531 MOROGORO: Wasiliana na Ramadhani Chale : 0715704380. Ifakara wasiliana na Mwl. Sharifu: 0659 158958GEITA: Ofisi ya Kamati karibu na mashine ya kukobolea mpunga shilabera: 0765 748056DODOMA: Hijra Islamic Primary School : 0716 544757/0718661992SINGIDA: Ofisi ya Islamic Education. Panel – karibu na Nuru snack Hotel : 0786 425838/0784 928039. MANYARA: Ofisi ya Islamic Ed. Panel – Masjid Rahma: 0784491196KIGOMA: Msikiti wa Mwandiga: 0714717727. Kibondo – Islamic Nursery School: 0766406669. Kasulu: Murubona Isl.SS: 0714710802/0763

298440LINDI: Wapemba Store: 0784 974041/0783 488444/0653 705627.MTWARA: Amana Islamic S.S: 0715 465158/0787 231007.SONGEA: Kwa Kawanga Karibu na Msikiti wa NURU : 0713249264. Mkuzo Islamic High School :0654 876317MBEYA: Ofisi za Islamic Education Panel Uhindini – 0785425319. Rexona Video mkabala na Mbeya RETICO: 0713 200209/0785425319. Rukwa: Sumbawanga:Jengo la Haji Said –Shule ya Msingi Kizwike: 0757090228/0786 313830TABORA: Kituo cha Kiislamu Isevya: 0784 944566/0718 556355. Nzega - Dk. Mbaga-0754 576922/0784576922.IRINGA: Madrastun – Najah: 0714 522 122.PEMBA: Wete: Wete Islamic School : 0777 432331/0712772326.UNGUJA: Madrasatul – Fallah: 0777125074. PANDU BOOKSHOP 0777462056 karibu na uwanja wa LumumbaMAFIA: Ofisi ya Ust. Yusufu Ally jirani na msikiti mkuu : 0773580703.

ARABIC CHETI.indd 1 3/21/2016 3:59:12 AM

ANNUUR NEW.indd 12 4/6/2016 9:33:54 AM

Page 13: ANNUUR 1224

13 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

Sheikh wetu kasema kweliIla kawafaidisha wabaya wetuKatimiza walilotaka awafanyie

SIKU moja baada ya shambulio la kigaidi Lahore, Pakistan, nilikuwa katika gari na jamaa zangu tukisikiliza taarifa ya habari ya BBC huku tukiendelea na safari.

“Yote aliyosema Sheikh wangu, akichambua historia ya Pakistan, kasaidia jambo moja tu ambalo ndio BBC walikuwa wakilitaka. Kathibitisha kuwa walioshambulia kwa kujitoa muhanga ni Waislamu na walikuwa wamewalenga Wakristo.” Alisema jamaa yangu baada ya mtangazaji kumaliza mahojiano na Sheikh Mohammed Issa.

“Afadhali na wewe umeliona hivyo, sijui kama Sheikh wangu aliona mtego wa mwandishi ulipo!” Alijibu jamaa yangu mwingine ambaye tulikuwa pamoja katika gari.

Shambulio linalozungumziwa hapa ni lile lililotokea Jumapili, siku ya Pasaka Machi 27 likidaiwa kufanywa na Muislamu aliyejitoa muhanga (suicide bomber). Taarifa za vyombo vya habari ziliarifu kuwa mtu huyo ni Taliban na kwamba alijilipua na kuuwa watu 67 na kujeruhi wengine 300 waliokuwa wakisherehekea Sikukuu ya Pasaka katika bustan iitwayo Gulshan Iqbal Park. Kama kawaida yanapotokea matukio kama hayo, tukaarifiwa kuwa kundi moja la Taliban ya Pakistan likijulikana kwa jina la Jamat-ul-Ahrar, limedai kuhusika.

“Ni sisi tuliwashambuilia na kuwauwa Wakristo wakisherehekea Pasaka, na mashambulio kama hili hayatakoma. Tutaendelea kuwapiga Wakristo.” Anadaiwa kusema msemaji mmoja wa Taliban, Ehansullah Ehsan, kama ilivyoripotiwa na BBC na vyombo vingine.

Katika jumla ya maswali waliyouliza BBC kumuuliza Sheikh wangu Mohammed Issa, ni kutaka kujua kwa nini shabaha ya ‘magaidi’ inakuwa Wakristo/jamii ndogo wasio kuwa Waislamu. Moja ya maelezo ya Sheikh, ambayo ni sahihi kabisa, ni kuwa Pakistan iliundwa kuwa taifa na nchi rasmi ya Waislamu. Sasa wengine wanatizamwa kana kwamba sio kwao.

Kitu cha kuzingatia hapa ni kuwa, kwanza swali limejaaliya kuwa ni kweli waliofanya shambulio lile ni Waislamu, Taliban. Na pili, walilenga kuuwa Wakristo. Sasa kama hukuzingatia, hilo ukitoa tu maelezo (ambayo ni kweli kama alivyosema Sheikh Mohammed Issa), unachofanya ni kuthibitisha na kusaidia kutangaza kuwa Waislamu (Taliban) wamefanya

Na Mwandishi Wetu

shambulio la kigaidi kuuwa Wakristo. Matokeo yake, unazidi kuchochea na kuhalalisha inayoitwa ‘Crusade’ dhidi ya Waislamu kwa sababu ni magaidi. Lakini pili, unasaidia kuchochea chuki baina ya Waislamu na Wakristo.

Katika hali kama hii, jambo la awali ni kushughulika na maswali ya msingi. Kujua ukweli. Je, shambulio limetokea? Nani kahusika? Je, ni kweli Taliban wanahusika?

Bila shaka tunakumbuka kisa cha Malala Yousafzai, ambaye amepewa Tuzo ya Nobel Prize, ambaye naye tunaambiwa kuwa kalani mauwaji hayo ya Lahore akisema:

“I am devastated by the senseless killing of innocent people today in Lahore. Pakistan and the world must unite. Every life is precious and must be respected and protected.”

Tuliambiwa kuwa binti huyo alipigwa risasi ya kichwa na Taliban kwa vile anapigania haki ya wanawake kusoma. Wengi tukaamini. Lakini hebu soma taarifa ya mwandishi Scott Creighton- “The Staged Malala Yousafzai Story: UK Medical Report Does Not Conform to Photos or Previously Reported Treatment of Malala.”

Taliban ni kundi la Kiislamu ambalo walipambana kuiondoa serikali ya kisekula ya Afghanistan ambayo iliundwa baada ya Mujahidina kutumiwa na Marekani kumng’oa Mrusi aliyeivamia nchi hiyo. Swali ni je, Taliban ambao kwa ustaarabu na wema wao walimfanya mwandishi wa Kiingereza, Mzungu, Yvonne Ridley, aamue kuisoma Qur’an

na kisha kusilimu, wanaweza kumpiga risasi ya kichwa bint mdogo Malala eti kwa sababu anapigania wanawake kwenda shule? Je, wanaweza kujifunga mabomu wakajilipua kuuwa watoto na wanawake wa Kikristo? Hili ndio swali la kujiuliza kwanza kabla ya kuparamia kujibu maswali ya BBC/DW yanayolenga kusaidia kukoleza propaganda kuwa Waislamu ni magaidi.

Kawaida yanapotokea matukio kama hilo la Lahore, zile siku za awali zinakuwa ni za karamu ya habari za tukio hilo kwa vyombo vya habari. Baada muda kiasi wiki moja hivi, ndio watu makini hukaa na kuchambua kujua ukweli ni upi na kwa nini. Lakini kwa bahati baya mara nyingi inakuwa uchambuzi wao haupewi nafasi katika zinazoitwa ‘main stream media’ na kwa maana hiyo, ni wachache wanaojua ukweli. Wengi hubaki na taarifa zile zile za karamu ya mwanzo wa habari.

“Zionist Controlled Espionage Agencies Behind the Lahore Easter Attack Massacre”, ni moja ya uchambuzi ambao hivi sasa unapatikana katika mtandao. Kubwa kinachoelezwa hapo ni kuwa tukio kama lile haliwezi kufanywa na Taliban, bali ni kazi ya maadui wa Uislamu ambao, wanalenga kuupaka matope Uislamu lakini pia kuchochea chuki na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo.

“This clearly is an act by Zionist Jewry through their well-established espionage systems. The attack is meant to polarize Christians against Muslims and to, once again,

create global demonization against Islaam. People were randomly slaughtered in this act. It is attributed to a suicide bomber. Yet, no one has proven, yet, the source of the bombing and or the parties responsible for the detonation.”

Inasema sehemu ya uchambuzi huo huku ikieleza kuwa mtu anayedaiwa kusema kuwa Taliban wanahusika, ni kachero anayetumiwa na Mossad. Taarifa zaidi zinasema kuwa hata ile kusema kwamba waliolengwa ni Wakristo, ni jambo la kuzua tu kwa sababu wengi wa waliokufa ni Waislamu, kama taarifa ya polisi inavyosema na kama alivyoripoti mwandfishi wa shirika la AFP kwamba:

“Christians were not the specific target of this attack because the majority of the dead are Muslims. Everybody goes to this park.”

Utafiti zaidi unaonyesha kuwa hawa wanaojiita Taliban wa Pakistan- Jamaat-ul-Ahrar, ni jina na watu wanaotumiwa na makachero linapofanywa shambulio la kigaidi lakini na wenyewe sio wanaofanya.

Yapo madai na maelezo kuwa wanaofanya vitendo vya kigaidi na kisha kusingizia kuwa ni Taliban, Al Qaida na makundi mengine kama hayo, ni askari wa kukodiwa wa Blackwater kutoka Marekani. Taliban wenyewe washasema na kulalamika mara kadhaa kwamba, Xe Services (the security contractor formerly known as Blackwater) wanafanya vitendo vya kigaidi kisha hurusha na kusambaza habari kuwa waliofanya mauwaji ni Taliban. (Soma: Taliban: Blackwater to blame for Pakistan attacks-By Daniel Tencer. Tazama pia: Leaked Video Shows US Contractors Randomly Killing Civilians)

“Tehreek-e-Taliban hawahusiki na ulipuaji mabomu na kuuwa watu kigaidi. Wa kulaumiwa ni Blackwater na idara ya usalama ya Pakistan (inayotumiwa na mabeberu, maadui wa Uislamu)” Anasema msemaji wa Taliban, Azam Tariq, wakati akihojiwa na Al Jazeerah.

Gazeti la Christian Science Monitor nalo lilipata kuripoti kuwa, kinyume na inavyodaiwa kuwa mashambulizi ya kigaidi hufanywa na Taliban, inavyoonekana ni Blackwater, wanaofanya kazi hiyo. Na kwa maana hiyo, katika tukio kama hilo la Lahore, hutegwa bomu likalipuka na kuuwa watu, halafu taarifa hutolewa kuwa ni mtu wa kujitoa muhanga. Na tunaambiwa kuwa Blackwater wanahusika pia na mashambulizi ya kigaidi Somalia, Afghanistan, Sinkiang region of China, Iran na Iraq. Zipo habari kuwa hivi sasa Blackwater washafungua kambi

Inaendelea Uk. 16

Malala Yousafzai (kulia).

ANNUUR NEW.indd 13 4/6/2016 9:33:58 AM

Page 14: ANNUUR 1224

14 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

MAKALA/MASHAIRI

NI TAASISI YA KIDINI ILIYOANZISHWA NA KUSAJILIWA KISHERIA MWAKA 2014 MKOANI MOROGORO KWA LENGO LA KUIHAMASISHA JAMII YA WAISLAMU KUIKUMBUKA NA KUITEKELEZA NGUZO YA TATU YA ZAKKA.

PAMOJA NA HAYO TAUZAMO KUPITIA UTOAJI ZAKKA INALENGA KUIUNGANISHA JAMII KUWA KITU KIMOJA, KUFUFUA UCHUMI WA KIISLAMU ULIOKUFA NA KUIFANYA QUR’AN NDIYO MUONGOZO SAHIHI KWA UMMA.

TAYARI TAUZAMO IMEFANIKIWA KUWA NA BAYTUL MALL ILIYOKO MTAA WA SIMU KATIKA KATA YA MJI MPYA MANISPAA YA MOROGORO PAMOJA NA KUFUNGUA AKAUNTI KATIKA BANK YA KCB TAWI LA MOROGORO NAMBA 3301064116.

ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO HAYO NA MENGINE, TAASISI INAHITAJI UUNGAJI MKONO KWA HALI NA MALI KUTOKA KWENYE TAASISI NA VIKUNDI MBALIMBALI.

UNAWEZA KUFIKA OFISINI MAKAO MAKUU MTAA WA SIMU KATA YA MJI MPYA MANISPAA YA MOROGORO AU WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBARI 0686240494 AU 0717337919

TANGAZO HILI NI KWA HISANI YA MWENYEKITI WA TAUZAMO SHEIKH SALEH HUSSEIN SANGA (BWAWANI).

TAASISI YA UKUMBUSHO WA ZAKKA MOROGORO (TAUZAMO)

Nikabu nawasilisha, Bara nako Visiwani, Kilio chenye kutisha, mijini na vijijini, Kinoathiri maisha, yangu jama tambueni, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Wengi mwanidhalilisha, mwenzi wenu hadharani, Akali kuwakumbusha, sina budi shairini, HADHI yangu mwaishusha, nijulisheni kwanini?, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Shoga yangu Mwanaisha, swahiba wangu mwandani, Vyema nikakujulisha, yalo mwangu mtimani, Kuhusu yangu maisha, kuwa nawe sitamani, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

'Mefanya yangu maisha, kuwa duni mitaani, Kuliko kunaibisha, nivue nache nyumbani, Kunivaa wajitwisha, zigo la dhambi jamani, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Si haki kunambatisha, na za kubana mwilini, Libasi zinoonyesha, za ndani yote ramani, Mbona wanidhalilisha, pasi na soni usoni? Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Baani kuniketisha, dhamirayo hasa nini? Eti soda waninywesha, dukani 'sende kwanini? Mbona wanifedhehesha, na kunishusha thamani? Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Kwa HUDUDI kunivusha, ya ALLAH u hatiani, Dhamira si kukutisha, bali haki kubaini, Kwani wanisababisha, nipuuzwe mitaani, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Machozi kuporomosha, mimi 'we u furahani! Ruwaza yako sitisha, ulinde yangu thamani, Mbona waniadhirisha, kunyamaza natamani, Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Kulia kumenichosha, naomba mniauni, Machozi yangu yatosha, kuwa SHAHIDI jamani, Maneno sitazidisha, ebu ninyamazisheni! Mimi NIKABU jamani, mbona HADHI mwanishusha!

Ashara beti zatosha, RISALA zingatieni, Lengo langu kukumbusha, NIKABU kuithamini, Wala si zogo kuzusha, kalamu naweka chini, Acheni basi jamani, HADHI yangu kuishusha. ABUU NYAMKOMOGI

KILIO CHA NIKABU!!!

INASEMEKANA kuwa mtu mmoja alipigwa na kiharusi baada ya kuleta kejeli akidhihaki Surat ‘Al-Fyl’.

Inaelezwa kuwa mtu huyo, jina lake tunalihifadhi, alipatwa na masaibu hayo na kulazwa hospitali Chake kwa zaidi ya wiki moja.

“Viko wapi hivyo ‘vi-alamtara’ vyenu na dua zenu. Uchaguzi umefanyika na Dr. Shein Rais.”

Inasemeka mtu huyo alisema hayo kwa njia ya kejeli akiwazomea wale ambao hawakwenda kupiga kura.

Habari zinasema kuwa baada ya kuyasema hayo, alishikwa na kiharusi (stroke) na kukimbizwa hospitali akiwa taabani.

Alamtara, ni neno la mwanzo katika sura Al-Fyl, sura ya105 iliyo katika Juzuu Amma, Juzuu ya 30.

Hii ni sura inayozungumzia tukuio la kuangamizwa jeshi la tembo la Liwali Abraha wa Yemen ambaye alikusudia kwenda kuiangamiza Al Qa’ba katika mwaka aliozaliwa Mtume (s.a.w) na ndio maana inasemwa kuwa Mtume kazaliwa mwaka wa tembo.

Askari wa Abraha walikuwa wameingia Makkah wakiwa wamepanda tembo, kama mtu anavyopanda farasi au ngamia.

Vibweka vya CCM, CUF, yadaiwa…Kejeli ya ‘viji-Alamtara’ yamlaza sipitali Pemba

Ni baada ya ushindi wa Dr. SheinNa Mwandishi Wetu Sura inaanza kwa

swali: “Je! Huoni jinsi Mola wako alivyowafanya watu wenye ndovu? Je, hakujaaliya vitimbi vyao kuharibika? Na akawapelekea ndege makundi kwa makundi. Wakawapiga kwa mawe ya udongo wa kuchoma. Akawafanya kama majani yaliyoliwa (yakatapikwa.?)”

‘Hadisi’ ni kuwa walikuwepo watu ambao walikuwa wakiomba Dua wakisoma sura hiyo kumuomba Mwenyezi Mungu ajaaliye vitimbi vya waliofuta uchaguzi wa Oktoba 25, viharibike kama alivyoharibikiwa Liwali wa Yaman Abraha.

Sasa maadhali uchaguzi umefanyika upya, ndio inadaiwa kuwa Ustaz mmoja ambaye inaelezwa kuwa ni mwalimu wa skuli ya Istiqama, Chake, akaja na kejeli hiyo kwamba ‘vijialamtara’ havijaweza kuzuiya uchaguzi na kuapishwa Dr. Shein kuwa Rais.

Japo ndugu na jamaa wa mtu huyo hawasemi moja kwa moja kuhusika na kejeli anayodaiwa kusema, na maradhi yaliyomsibu, lakini habari zilizoenea Pemba ni juu ya tukio hilo.

“Kwa anavyojulikana, hashindwi kusema hayo”, alisema mzee mmoja ambaye alihojiwa kutaka kuthibitisha tukio hilo.

Wakati huo

huo, mtu mmoja aliyefariki eneo la Mjananga, Uwandani siku ya uchaguzi Machi 20, naye ameacha gumzo ikidaiwa kuwa kifo chake ni jibu kwa maneno yake ya kufru.

Mtu huyo anadaiwa kusema maneno ya kufru baada ya kurejea kupiga kura huku akiwatabiria wenzake kifo, kama ‘walivyouliwa’ kwa kuporwa ushindi na kupewa CCM.

Hata hivyo, wengine wamesema kuwa kifo cha mtu huyo kimetokea kama jambo la kawaida tu, lakini sasa kwa vile kuna maneno yalishatangulia, na kuna watu wana uchungu na yaliyojiri hiyo Machi 20, lazima watafute namna ya kujifariji kwa kuzua kwamba walioshiriki wanaadhibiwa na Mungu.

“Yote haya yanakuja kutokana na mtizamo potofu ambapo, wapo baadhi wanaona kuwa mtu kuwa katika CCM ni ukafiri, lakini kuwa mfuasi wa Maalim, ndio katika kupata Radhi za Allah (SW). Kumbe wote, CUF na CCM wapo katika boti moja tu, wanapigania kuongoza nchi kwa misingi ileile ya kisekula isiyozingatia mamlaka ya Mwenyezi Mungu na Mwongozo wake. Sasa mshindi hapo ni yule mbabe zaidi katika midani za siasa na kutumia mabavu.” Alisema Sheikh mmoja wa Wete akihojiwa na mwandishi juu ya tukio hili.

ANNUUR NEW.indd 14 4/6/2016 9:34:00 AM

Page 15: ANNUUR 1224

15 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

SHUKRANI zote zinamstahikia Allah (sw) na sala na salamu zimfiie Mtume Muhammad (saw), mtukufu wa daraja, Masahaba wake na wote wanaofuata mwenendo wake mpaka siku ya malipo.

Somo la tatu katika mfululizo huu, lilikuwa ni kukufurishana, na tuliona itikadi sahihi ni kutokumkufurisha Muislamu. Lakini pia ni kuamini kuwa dhambi inapunguza imani na ibada zinaongeza imani, na tulionesha ubaya wa kuwaita Waislamu makafiri.

Katika somo hili tutatoa ufafanuzi wa aya na hadithi ambazo hutumiwa na baadhi ya makundi, kama ni hoja ya kuwakufurisha Waislamu. Allah (sw ) anasema katika suratul Maida sura ya 5 aya ya 44 “......na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Allah (sw), basi hao ni makafiri”. Maelezo ya aya hii kutoka kwa Masahaba waliotafsiri Qurani, nao wamepokea kutoka kwa Mtume (saw) ni kama ifuatavyo:

Amesimulia Ali Ibn Abi Talha kutoka kwa Ibn Abbas (ra) kuhusu aya hii amesema “Anayekanusha aliyoteremsha Allah (sw) huyo amekufuru, na anayezikubali zile sheria na hazihukumii huyo ni dhalimu fasiki (amepokea Tabary).

Amesimulia Tawus amesema aliulizwa Ibn Abbas (ra) kuhusu tamko la Allah (sw) “wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Alla (sw), basi hao ni makafiri”, akasema hii ni kufru lakini si kama kumkufuru Allah (sw) na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake. Amesimulia Thawry kutoka kwa Attai kuwa ni kufru si kufru ( kamili), ni dhulma si dhulma na ni ufasiki si ufaski (kamili). (Amepokea Tabary).

Tawhiid -5

Imepokewa kutoka kwa Tawus kuwa ukafiri katika aya hii si ukafiri wa kumtoa mtu katika mila ya Kiislamu. (Tabary). Maelezo haya yanapatikana katika Tafsyr Tabary, Ibn Kathyr na Tafyr Tabary, chini ya aya hii.

Ni dhahiri kwamba si kila anayehukumu kwa sheria za kijahili ni kafiri, hutegemea na imani yake kuhusu zile sheria ikiwa anaamini kuwa sheria za kitwaghuti ndizo bora zaidi na sheria za Kiislamu hazina maana na zimepitwa na wakati, basi huyu ametoka katika Uislamu. Na huo ndiyo msimamo wa Uislamu katika aya hii, msimamo ambao umetokana na Masahaba kutoka kwa Mtume (saw). Na Mtume (saw) amezitaja karne tatu za mwanzo kuwa ni karne bora zaidi kwa maana hii, hawezi kutokea mtu leo, au kikundi cha watu wakaanza kuitafsiri Qurani kwa kuilazimisha ifuate hoja yao, hayo yatakuwa ni makosa makubwa katika aqida, kwa maana lazima tuwe na itiqadi kuwa, Quani na sunaa lazima vitafsiriwe na kufahamika kwa

mujibu wa ufahamu wa Masahaba, ikiwa Abdillahi Ibn Abbas (ra) na wenzake waliokaa na Mtume mwenyewe, wameona kuwa viongozi wanaohukumu kinyume na sheria za Kiislamu si makafiri moja kwa moja, basi hiyo ndiyo hoja iliyosawa, na fikra nyengine yeyote ile kinyume na hiyo ni uzushi na upotofu.

Baadhi ya itikadi za makundi ni kinyume na uwelewa sahihi wa Uislamu , na vijana kwa kukosa itikadi sahihi huwa wahanga, huhama majumbani mwao wakahamia msituni na kuanza kuwahujumu Waislamu wenzao kwa kuwavamia na kuwapiga mabomu na kujiripua, wakidhani kuwa wanapigana jihadi. Ifahamike pia kuwa jihadi pia ina sharti zake na kuna fiqhi maalumu inaitwa fiqhi l jihad, ambayo mtu akitaka kuanza ibada hii lazima aisome na aielewe vizuri. Jihadi hutangazwa na Amiri wa Dola ya Kiislamu, na kama hayupo basi Maulamaa waliofikia kiwango cha Utoaji fatwa kwa pamoja hukaa na kuamua jihadi. Tena baada ya kupatikana sababu za kisheria za kupigana, kama kuvamiwa na maadui, si kupigana tu ukimkuta mtu umuuwe. Mtume(saw) aliishi vizuri na makafiri huko Madina, na alipigana pale tu ilipolazimu kufanya hivyo, yaani pale makafiri waliposhika silaha kumpiga. Aidha kwa kuvamiwa na maadui, au kujihami. Si kikundi tu cha watu walio na pupa ya kusimamisha Dola ya kiislamu kukamata silaha na kuua maelfu ya watu wasio na hatia , au kukamata silaha dhidi ya kiongozi aliyekuwepo madarakani na kutaka kumpindua eti kwa

sababu hasimamishi sheria. Hilo ni kosa kwenye Uislamu na ni msimamo wa makundi yaliyokosa aqida sahihi. Vita vinavyopiganwa Syria Iraq na Libya ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya Waislamu, na kusababisha maelfu kuhama nchi zao, wanawake wa Kiislamu kudhalilishwa, huo ni uovu wa wazi na Dola ya Kiislamu haisimamishwi hivyo. Dola ya Kiislamu husimamishwa kwa kufanya mapinduzi makubwa ya fikra na itikadi za watu, kwa kulingania watu kwa wema na lugha nzuri, ili watu wamjue Mola wao, na kuanza mtu kuibadilisha familia yake, na familia zikiwa nyingi huzaa jamii ya Kiislamu na kidogo kidogo jamii hugeuka kimaadili na ikawa jamii ya Kiislamu, nayo jamii hiyo baada ya muda mrefu hubadilisha mila na desturi na silka pia na sheria , na haya ni mambo yanategemea juhudi, umoja na mshikamano wa walinganiaji, na kutokuwa na pupa kwani mambo mazuri hayataki haraka.

Hadithi mbali mbali za Mtume (saw) ambazo zinataja ukafiri pia zinatafsiriwa kuwa ni ukafiri wa kivitendo katika hadithi zifuatazo.

Amesimulia Abdillahi Ibn Masuud (ra), amesema Mtume (saw) “kumtukana Muislamu ni ufasiki na kupigana naye ni ukafiri”( SM64 SB48). Amesema Imamu Nawawy katika sherhe ya hadithi hii “Kumtukana Muislamu bila ya haki ni kosa kwa makubaliano ya Maulamaa na mfanyaji wa kosa hilo ni fasiki, ama kumuua bila ya haki hakumfanyi kuwa kafiri mbele ya watu wa haki katika ukafiri unaomtoa katika mila ila atakapohalalisha kumuua. Na makusudio ya ukafiri hapa ni kukanusha ihsani na udugu wa Muislamu si ukafiri kamili.”

Na Mussa Ame

Makhatibu wanapaswa kubadilikaInatoka Uk. 20 utekelezaji wa jambo lolote. Ni

ukweli ambao si rahisi kuruka patupu kwamba kuna tofauti kubwa ya kiathari na kimatokeo kati ya shughuli au kazi inayofanywa kwa kutanguliwa na maandalizi na ile inayofanywa pasi na kutanguliwa na maandalizi. Kwa msingi huo huo, ni dhahiri kuwa hata katika utoaji wa khutba za Ijumaa kuna tofauti kubwa sana katika kufikia ufanisi wa suala hilo kati ya khatibu mwenye kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya kuwasilisha khutba yake na yule asiyefanya maandalizi.

Kuhusiana na utofauti unaoweza kudhihiri pamoja na athari inayoweza kujitokeza katika mioyo ya hadhira kutokana na kipengele cha maandalizi, baina ya khatibu mwenye maandalizi ya kutosha na asiyekuwa na maandalizi ya kutosha Sheikh Saffar anapambanua hali hiyo katika ukurasa wa tisini na tisa (99) wa kitabu chake kwa kuwatanabahisha makhatibu kwamba ''Uzoefu umetufundisha kwamba hotuba ambayo tunaiwasilisha baada ya kujiandaa na kujitayarisha vizuri kwa

namna nzuri inakuwa ni hotuba inayofaa, na inakuwa na uwezo mkubwa wa kuathiri katika nafsi za wasikilizaji, wakati ambapo hotuba ya kushitukiza isiyo na maandalizi haileti matokeo hayo. Hakika mimi ninahisi kabla ya mwingine udhaifu wa hotuba hii na ufinyu wa kuathiri kwake, na hili ni jambo la kawaida''.

Aidha, mhariri wa gazeti hili katika tahariri yake ile alibainisha, pamoja na mambo mengine, ukweli kuhusiana na athari hasi zinazoweza kujitokeza kwa khutba ya khatibu asiye na maandalizi ya kutosha kwa kutanabahisha kwamba ''Tuweke tu wazi kwamba katika misikiti mingi, hutba za Ijumaa zimekuwa zinafanywa mithili ya zima moto. Yaani zinatolewa kwa ajili ya kutimiza tu wajibu Swala ya Ijumaa ipite. Hakuna maandalizi ya kutosha, somo linakinahi mapema, haliwavutii wasikilizaji, wala halitoi ujumbe wa wiki kwa waumini''. Pamoja na ukweli huu, Jambo linalosikitisha ni kutoweka kwake (ukweli huu) katika akili za baadhi ya makhatibu wetu wa Ijumaa na kutawala akilini mwao mazingira ya

kimaada na mawazo ya kimaslahi kwao kiasi kwamba kutoa khutba imekuwa ni kazi na ajira na hivyo kufanywa ni sababu kati ya sababu za kujipatia riziki na chumo na si vinginevyo. Hivyo basi, kwa muktadha huu, unamkuta khatibu mwenye mtazamo huu anafanya kazi hii kwa ajili ya kupata malipo au kwa kuwa anapatiwa mshahara kila mwezi na mengine yasiyokuwa hayo miongoni mwa manufaa mengine ya kidunia.

Kwa mantiki hii, nihitimishe kwa kuwakumbusha na kuwahiza makhatibu wetu kwamba ni juu yao kuhudhurisha ukweli huu katika akili na fikra zao wakati wanapopanda mimbari na kuwahutubia au kuwapa watu waadhi ama kuwaelimisha kuhusu mambo mbali mbali kupitia khutba zao. Na hilo linawezekana biidhinillaahi kwa kuwa na au kujenga yakini kwamba wanatekeleza wajibu huo kwa msingi wa kutekeleza amri ya Allah (s.w.) na wajibu wake wa kuwalingania na kuwaelimisha waja wake pamoja na viumbe wake, na hii ndio hatua ya kwanza ambayo inatengeneza kanuni ya msingi katika kazi ya khatibu.

kuathiri, jambo ambalo huifanya hotuba yake iwe na faida nyingi na iwe na uwezo wa kukinaisha na kuathiri''.

Ukiidurusu kwa makini na utulivu tahariri katika toleo namba 1223 la gazeti hili pamoja na nukuu zilizobainishwa katika aya zilizotangulia, utabaini kwamba, pamoja na mambo mengine, yaliyozungumziwa katika pande zote mbili (tahariri na nukuu), ambayo makhatibu wetu wanapaswa kuyazingatia ili kuleta ufanisi katika khutba zao, suala la maandalizi limeshadidiwa sana kutokana na umuhimu wake. Kwa leo tuanze uchambuzi na upembuzi wetu na suala hili, masuala mengine ya msingi ya kimazingira yanayopaswa kuzingatiwa na makhatibu wetu ili kuleta ufanisi katika khutba zao kama yalivyodokezwa katika nukuu na tahariri, yataendelea kujadiliwa katika mwendelezo wa makala haya katika siku za usoni inshaallaah.

Maandalizi ni jambo la msingi katika kuleta ufanisi katika

ANNUUR NEW.indd 15 4/6/2016 9:34:05 AM

Page 16: ANNUUR 1224

16 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

Sheikh wetu kasema kweliInatoka Uk. 13Somalia na Abudhabi. Na kwamba ni marufuku Muislamu kuingizwa katika kikosi hicho cha mamluki wauwaji kwa sababu si jambo la kawaida Muislamu kutumwa kwenda kumuuwa Muislamu mwenzake na akaifanya kazi hiyo. (Tazama: Blackwater/Xe In Somalia. Blackwater Founder Moves to Abu Dhabi Blackwater/Xe Terrorist Cells Conducting False Flag Terrorist Attacks in Pakistan.)

TAZAMA PIA-“ORDER OUT OF CHAOS: CIA, BLACKWATER RESPONSIBLE FOR BOMBINGS, ASSASSINATIONS IN PAKISTAN”-BY Kurt Nimmo. Na “CIA Hired Private Military Firm Blackwater for Secret Assassination Program 2 of 2”-By Jeremy Scahill.

Pengine nimalizie kwa kusisitiza jambo moja hapa. Ukisikia kuna shambulio la kigaidi katika miji ya Waislamu, na watu kadhaa wamekufa, iwe Nigeria, Pakistan, Afghanistan, basi ujue ni kweli kuna watu wameuliwa. Ambalo litakuwa ni la kuhangaika kujua ukweli, ni nani kahusika. Wao watakuambia kuwa ni Boko Haram, Al Qaida, Taliban au Al Shabaab. Lakini ni wao wenyewe viranja wa ‘crusade’ wanatuma watu wao kulipua. Ila

ukisikia kuna shambulio Paris, au Brussels na watu kadhaa wamekufa, uwezekano mkubwa ni kuwa hakuna mtu aliyekufa. Ni mchezo wa kuigiza. Lakini baada ya hapo itapigwa propaganda wakisingiziwa Waislamu, watasakwa na hata kuuliwa baadhi ya Waislamu au kuwekwa korokoroni. Ni mshumaa unaunguzwa pande zote. Katika miji yao, wanauliwa kisha hudaiwa kuwa ni magaidi wamewauwa. Halafu unafuatia msako na wanakamatwa na hata kuuliwa Waislamu. Hapa nakumbuka lile wimbi la kuchomwa makanisa hapa nchini. Nakumbuka katika kisa kimoja ilidaiwa kuwa kuna makanisa kadhaa yamechomwa Yombo, na wachungaji wamekuja juu wanataka hatua zichukuliwe. Tulifika hadi eneo la tukio, hapakuwa hata na kanisa moja lililochomwa moto! Nakumbuka serikali ya mtaa ya eneo hilo nayo ilitoa taarifa kwamba habari zilizodai kuchomwa makanisa katika eneo hilo ulikuwa uwongo mtupu.

Ni hivyo hivyo, ukija katika miji ya Ulaya, unatungwa uwongo halafu, wanauliwa na kusakwa Waislamu. Na hili ndio tunaloliona juu ya lililodaiwa kuwa shambulio la Brussels na Lahore.

Padiri afichua kitendawili kuchomwa kanisa Yombo

Inatoka Uk. 11hilo. Wachungaji hao ni Richard Norby, Joseph Empey, na Mason Wells wa kanisa la The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints (Mormons). Kwa mujibu wa taarifa za uchuguzi zilizotolewa na mwandishi Josh Feldman na zile za NBC News, wachungaji hawa wa Mormons, walikuwa pia katika matukio ya kigaidi ya Boston na Paris. Baba yake Mason Wells akizungumzia suala hilo juu ya kijana wake anasema:

“This is his third terrorist attack. We live in a dangerous world and not everyone is kind and loving.”

Swali hapa ni je, imekuwa jambo la bahati nasibu tu kwamba wachungaji hawa wanakuwepo katika matukio haya ya kigaidi au ni jambo la kupangwa? Je, ni kweli Mason aliumia?

Fox News, magazeti na televisheni mbalimbali zikiripoti juu ya kuumizwa Mason na magaidi waliodaiwa kuwa ni Waislamu, ziliripoti kuwa “Mason Wells had 3rd Degree burns on his face and hands.” Vyombo vingine vikasema 2nd degree burns. Na yeye mwenyewe akihojiwa akasema, “There was fire around my face

and my feet…and I was covered in blood.” Kwamba uso wake na miguu ilizingwa na moto na kutapakaa damu kutokana na majeraha ya moto.

Waulize madakitari, nini hali ya mtu aliyeungua moto katika kiwango cha 3rd degree burn!

Sasa ingia katika mtandao tafuta picha za Mason akiwa hospitali au tazama: The Brussels Bombing: Media Lies and Mason Wells The Cat With 9 Lives. Hakuna mahali popote picha zinaonyesha Mason akiwa kaungua mikono wala uso. Akiongea ananyanyua mikono, na hakuna jeraha hata moja. Lakini pia utaona kuwa japo uso umeviringishwa kitambaa cheupe, lakini ni kisafi kabisa cheupee, kuonyesha kuwa hakuna jeraha lolote usoni. Lakini pia anaonekana akitabasamu, hana tatizo kabisa.

Kutokana na utata wa hali hii, kati ya yanayosemwa na

vyombo vya habari na hali halisi, watafiti na wachambuzi wa mambo wamezama na kuibuka na taarifa kwamba wachungaji hao ni Freemasons. Na kwamba katika matukio kama hili la Brussels, hutumiwa na ‘Mazayuni’ kuandaa matukio ya kuupaka matope Uislamu na Waislamu na kuchochea chuki na uhasama baina ya Waislamu na Wakristo. Na kanisa lao- The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints, lilianza mwaka 1840 kama Masonic Lodge (Nauvoo lodge) iliyokuwa Illinois, waanzilishi wakiwa ni ‘Latter Day Saints’ Joseph Smith na kaka yake Hyrum Smith ambao walikuwa Freemasons. Na tunaambiwa kuwa “Mormonism na Freemasonry ni wamoja”. Juu ya u-masons wa familia hii ya Smith tunaambiwa kuwa:

“[The Joseph Smith family] was a Masonic family which lived by and practiced the estimable and admirable tenets of Freemasonry. The father, Joseph Smith, Sr., was a documented member in upstate New York. He was raised to the degree of Master Mason on May 7, 1818 in Ontario Lodge No. 23 of Canandaigua, New York. An older son, Hyrum Smith, was a member of Mount Moriah Lodge No. 112, Palmyra New York. (Tazama: The Mormon Church and Freemasonry (2001) By Terry Chateau.)

Ufupi wa maneno ni kuwa hawa wanaodaiwa kuwa wachungaji kutoka Marekani, walikuwa ni katika waigizaji-paid actors katika tukio hili la ugaidi Ubeligiji. (Tazama: Mormonism, or The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints and Freemasonry. Tazama pia-Paid Actors From Paris to Brussels. Na Belgium Terror Attack Hoax Prt 2-Reusable Actors, Training Drills Explained, Bad acting busted.)

Ukitizama rejea hizi utakuta kuwa picha za waliodaiwa kuwa ni majeruhi, hazina tofauti na zile katika ‘igizo la usanii’ (mazoezi) lililofanyika siku moja kabla ya tukio lililodaiwa kuwa la kigaidi. Katika zoezi na igizo hilo, watu wanaonekana wakiongozwa na ‘mwongoza filamu’, wakijifanya wameumia na wengine wakitoa msaada. Na picha kama hizo ndio zinaonekana katika tukio linalodaiwa la ugaidi katika

uwanja wa ndege. Na ndio maana kunakuwa na utata, kwamba watu wachache wamelala chini wameumia, lakini wengine wanachati na simu zao wala hawana habari.

Kwa upande mwingine, yapo madai kuwa picha iliyotumika kuonyesha kuwa bomu limevunja paa na jumba la airport, ilipigwa toka mwaka 2011 na haikuwa Brussels, bali ilikuwa tukio katika uwanja wa ndege wa Domodedovo (Domodedovo Airport) Urusi mwaka 2011. (Tazama: BUSTED! Brussels attacks: Video purporting to show Zaventem Airport explosion was shot 2011.)

Nimalizie kwa kusema kuwa ushiriki wa wachugaji hawa wa Mormon Missionary, unatukumbusha, ‘hamkani si shwari tena’ iliyokuwa imezushwa na baadhi ya wachungaji nchini wakidai kuwa kuna Waislamu wanachoma makanisa na kushambulia wachungaji na mapadiri. Baadhi ya wanasiasa wetu nao walidaka madai hayo na kuijia juu serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo. Serikali ikashutumiwa kuwa imekuwa legelege, inalea udini mpaka sasa viongozi wa dini wanauliwa na makanisa kuchomwa moto. Nakumbuka kauli za James Mbatia na wanasiasa wengine, wakiwemo Mawaziri na wabunge wa CCM juu ya jambo hili. Kilichokuwa kinatakiwa na wachungaji wale na wanasiasa hao, ni kuwa serikali ichukue hatua kama ilivyofanyika wakati wa kadhia ya ‘Mauwaji ya Mwembechai’. Kwamba Paroko anakuja na madai kuwa Waislamu wanamtukana Yesu, serikali inachukua hatua bila kuchunguza iwapo madai ni ya kweli au la. Sasa ilipoonekana serikali haifanyi hivyo, ndio baadhi ya wanasiasa wakaja juu ikafikia hatua baadhi ya wachungaji kuwataka watu wao wamebebe silaha kujihami kwa sababu eti serikali imeshindwa kuwalinda Wakristo!

Almuhimu kilichokuwa kikifanyika, ni kama haya wanayofanya akina Norby, Joseph Empey, na Mason Wells wa kanisa la The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints. Kuupaka Uislamu matope, kuwatangazia ubaya Waislamu na kuita hasira za walimwengu wote, ziwaangukie. Katika mazingira kama haya ya ‘ugaidi feki’, hebu jaaliya unapigiwa simu kuhojiwa na BBC, CNN, DW au Aljazeera, unaulizwa:

“Kwa nini Waislamu wanawachukia Wakristo?” Ushahidi ukiwa ni shambulio la Brussels na Lahore. Utajibu nini? Tazama tahariri yetu.

ANNUUR NEW.indd 16 4/6/2016 9:34:06 AM

Page 17: ANNUUR 1224

17 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

MAKALA

KUMEKUWA na msamiyati wa neno ‘gaidi’, na ugaidi;linalo vuma kwa kasi sana duniani kwa wakati huu, kuliko wakati mwingine wo wote uliopita. Kwa bahati mbaya mfumo unaoendesha dunia hii umekusudia kuwafanya wanadamu kuwa sawa na maroboti; wa kujazwa ujinga na kuuamini bila kutumia akili zao. Kwa lugha inayolazimishwa kuzoeleka ni kuwa, ugaidi ni uharibifu kwa maana halisi ya uharibifu, uliopindukia unyama. Yaani, uuwaji wa watu wasiokuwa na makosa, utekaji watu na ulipuaji wa maeneo ya watu kwa ajili ya kuwaua na kuharibu kila kilichokuwemo.

Na gaidi kwa mtazamo huo, ni yule au wale wanaofanya vitendo hivyo.

Lakini kwa wale waliobuni msamiati huo, wana maana iliyofichwa, ambayo hawataki walimwengu wasiokuwa wao waijue. Nayo ni kuwa, kila anayetokea kukataa kukokotwa na sheria zao na amri zao, huyo ni gaidi. Lakini nao hao wana makundi matatu wanayoyatazama kwa mitazamo mitatu tofauti. Lakwanza, ni lile linaloitwa “waasi”. Hilo linajumuisha, waasi, lakini ni waimani moja ya dini na wakuu wa nchi za Magharibi na Marekani.

Mfano wa hao ni waasi wa Aireland, ambao mwaka 2016 wamesherehekea miaka mia moja (100) ya uasi wao na mauaji; lakini hawaitwi magaidi. Waasi wa nchi ya Kongo, D.R.C. Tangu mwaka wa 1960 alipouawa Waziri Mkuu wa kwanza Patrice Lumumba, mpaka sasa vikundi vyote vya mauaji vinaitwa vya waasi, sio magaidi. Joseph Konyi wa Uganda, mpaka leo ni muasi sio gaidi. Jonas Savimbi wa Angola, kaacha jina la muasi sio gaidi. John Garan, Sudani Kusini, kaacha sifa ya muasi sio gaidi. Kundi la Seleka, Afrika ya Kati, hao ni waasi hawatajwi kuwa ni magaidi n.k.

Kundi la pili ni lile linalotumwa na nchi za Magharibi na Marekani kwenda katika nchi fulani kufanya mapinuzi; hayo ni kama yale yaliyo ingia Afghanstan, Iraqi, Libiya, Siriya n.k. Hayo yanaitwa kuwa ni ya waasi sio magaidi. Hata yakiuwa watu wote wa nchi husika hayalaumiwi, maana yana kibali cha mababa wa uuwaji.

Kundi la tatu ni lile linalotetea maslahi ya nchi yao na kudai haki, au uhuru wa nchi yao; hawa huitwa magaidi na watawala, na kuteswa kwa miaka; lakini ikiwa wataungwa mkono na wananchi wengi, baada ya kupata Uhuru, jina linabadilika linakuwa, Rais wa nchi husika, badala ya kiongozi wa magaidi; na Chama chao kilichoitwa kundi la kigaidi, kinabadilika jina na kuitwa Chama cha Siasa (cha ukombozi) mfano wao ni kama kina:-

Mzee Jomo Kenyatta, Mzee Nelson Mandela, Samora Marshel, Patrice Lumumba n.k.

Kama ugaidi na magaidi ni kwa kufanya matendo ya Ufisadi kwa maana halisi ya Ufisadi katika ardhi; ni nani atakayewapa majina waharibifu hawa lisilokuwa la kigaidi au magaidi? Kina mfalme wa Ureno aliyewatuma kina Pedro

Ugaidi ni nini, nani gaidi?Na Khatibu J. Mziray

Cabral, Christopher Columbus, Vasco da Gama, D’Almeida; na walioanzisha vita vikuu vya kwanza na vya pili, na waliopiga mabomu ya atomic kule Hiroshima na Ngasaki, Japani! Waliowauwa wenyeji wa asili wa Marekani (Wahindi Wekundu), walioanzisha vita na kuuwa watu kule Vietnam, Laos, Cambodia, na Korea. Waliowauwa Waislamu elfu name (8,000) kwa mpigo kule Bosnia, waliowauwa Waislamu kule Iraq, Libiya, na sasa Siriya n.k. Hawa tuwape jina gani zuri linalolingana na sifa yao hiyo zaidi ya kuwa ni mababa wa ugaidi na mababa magaidi?

Mataifa haya yaliyokaa kule Ujerumani mwaka wa 1884/5 wakaigawa Afrika na kuivamia kijeshi na kuitawala na kutuachia virusi vinavyotuhangaisha mpaka sasa, ni nani anayewapa jina zuri zaidi kinyume na magaidi?

Jina ugaidi kwa sasa limepandishwa daraja kwa lengo maalumu, ambalo ni muhimu kwa Waislamu wakalijua kwa undani. Kulingana na muasisi wa kupandisha chati neno ugaidi na gaidi, Rais George W. Bush, alibeba mambo mawili makuu, yanayobebana kimfumo wa nchi za Ulaya na Marekani. Kwanza ni kutumia ugaidi kwa kuupiga vita Uislamu na Waislamu; kwa kuwauwa na kupora mali zao na kuvuruga nchi za Kiislamu ili zisielewane na ziwe masikini ili zifanye kusaidiwa na nchi za Ulaya na Marekani (za Kikristo) ili ionekane kuwa Ukristo ndio unaojali watu na kuwahurumia kwa kuwasaidia wakati wa shida.

Lakini ili nchi za Kanisa zivutike zaidi kuwa Rais George Bush anachofanya ni agizo kutoka kwa Mungu alisoma maandiko kutoka katika Biblia 18:17, kabla ya kuamuru kushambuliwa nchi ya Iraq.

Si maana yangu kulumbana na viongozi wa Kanisa na waandishi wa vyombo vya utangazaji vya Kanisa, la, bali kuonesha jinsiwanavyoliaibisha Kanisa

na Ukristo kwa jumla, kutokana na yale wanayoyashabikia, hata kama yanaonekana wazi kuwa yanaongozwa na shetani:-

“BWANA akasema, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo…” mw 18:17.

Haikuelezwa na yeyote kuwa ni nini alichokusudia Rais Bush kusoma andiko hilo kisha kunyanyuka kwenye kiti na kutangaza vita.

Huyo ni Mcbungaji Teghua aliyeandika makala yake katika gazeti la Kanisa la Nyakati l Machi 23-29.2003, toleo Na. 95. Makala aliyoipa kichwa cha habari cha:

Biblia yasema Iraq ina pepo shujaa wa vita… Walipigana na Malaika wa Mungu angani siku 21… Ilibidi Malaika mkuu Mikaeli ashuke kuingilia kati… Rais Bush asoma Biblia kabla ya kutangaza vita.

Kwa maelezo yake hayo, Mchungaji anaiambia dunia kuwa, Sadam Husseni na Wananchi wa Iraq ni mapepo (Mashetani) na anamshabikia Rais Bush kuwa aende Iraq akawaue mapepo (mashetani) yaani Waislamu. Ndiyo maana Mchungaji Teghua akasherehesha:-

“Kama vile alivyosema Bwana Yesu kuwa siku za mwisho zitakuwa kama ilivyokuwa Sodoma na Gomora, ujumbe huo aliousoma Rais Bush, ni muhimu sana hasa kwa vile ndio uliokuwa ujumbe wa utangulizi kabla ya Mungu kuziangamiza Sodoma na Gomora, hivyo bila shaka ni ishara nyingine ya Mungu kuangamiza tena kizazi hiki kiovu na uovu wake.”

Huyo ni kiongozi wa dini, anayemsifu mlokole Rais Bush na kumfananisha na wale Malaika waliotumwa na Mungu kwa Nabii Ibrahimu wakati wa kuangamiza Sodoma na Gomora; kuwa naye Bush ametumwa kuwaangamiza wa Iraq, na ananukuu maneno ya Yesu.

Kama ulokole wenyewe na Uchungaji ni wa matendo hayo ya Mchungaji Teghua na Rais Bush, tulioshuhudia maangamizi ya watu wa Iraq n.k. Kwanini usiwe ni aibu

na janga kwa Ukristo dunian? Jambo la pili, ni kuwapunguza

Waislamu kwa kuwauwa kwa kuwachonganisha kivita, na kupata watumwa kwa kuwavuna kwa kuwafanya wakimbizi. Wale wanaokimbilia Ulaya watakuwa wanawachagua wale wanaowahitaji, na wale wasiowahitaji wanaitwa wahamiaji haramu;

usishangae wakirudishwa makwao, na hata kutoswa baharini na watosaji wakalipwa fidia; kwani hata hao waliokwisha kuzama baharini hatujasikia wasafirishaji walioshitakiwa na kuhukumiwa. Ikumbukwe kuwa wakati watumwa walipokuwa wakisafirishwa kwenda Marekani wasafirishaji walikuwa wanawatosa baharini na kudai fidia:-

“Mwezi Mei mwaka 1783 Jaji wa Mahakama Kuu huko Uingereza, Lord Justice Manfield alisikiliza kesi iliyozua utata mkubwa wa kisheria.

Utata huo ulihusu kama Mzungu anaweza kufunguliwa mashitaka akimwua mtumwa wake kwa makusudi. Tukio lenyewe lilitokea mwaka 1781. Nahodha wa meli ya Uingereza iliyoitwa Zong, Bwana Luke Collingwood, kwa kushirikiana na mabaharia wenzake waliamua kuwauwa kwa makusudi watumwa 131 kwa kuwatosa baharini ili kampuni yao ya meli iweze kunufaika na malipo ya bima. Watumwa hao walikamatwa Afrika Magharibi na walikuwa wakipelekwa Jamaika.

Jitihada za kuwafungulia mashitaka ya mauaji mabaharia hao ziligonga mwamba kwa sababu mahakama iliambiwa nayo ikaafiki kuwa ‘kufungua mashitaka kama hayo ni wendawazimu kwa sababu watu Weusi ni mali na bidhaa.

Hii ni kesi ya mtu kutupa mali yake’ (Walvin, 1992:19). (Mkutano wa hali ya siasa Tanzania 16-17/9/2003 uk.1).

Walikuweko watu walioandaliwa kuwakamata watu na kuwakusanya na kuwauza kwa Wazungu; ndio hao waliokuwa wakisema kuwa ni bidhaa zao, kisha kuwatosa baharini ili kulipwa na makampuni yao ya bima. Hao ni wa Afrika ya Magharibi; hatuambiwi kuwa waliokuwa waliwakamata watu hao ni kinanani. Lakini wale waliokamatwa Afrika ya Mashariki na ya Kati wanatajwa kuwa ni Waarabu. Historia haiwataji Wazungu kuwa ni wahusika wakuu.

Sasa mtindo umebadilika; mataifa haya ya Ulaya na Marekani huandaa vikundi ya watu, na kuwapa majina yenye kushabihiana na Uislamu, au waasi na kuwapa nyenzo za kuanzishia uasi katika nchi za Waislamu, kisha kuzivuruga kiuchumi na vita; na kuporamali asili, kisha kuwafanya raiya wa nchi husika kuwa wakimbizi.

Lakini kwa kuwa nchi za Afrika, Arabuni na Asia zimeenezwa uhasama na vita, nchi hizo za Ulaya na Marekani hupiga poropoganda kuwa, Ulaya kuna maisha mazuri na haki za binadamu, kiasi cha kuwafanya wakimbizi kuamua kukimbilia huko. Lakini inaonekana kama kuna makampuni yaliyoandaa watu wa kuwavusha bahari kwa kuwapakia katika mataboti yasiyo kidhi viwango, ndiyo maana watu wengi wamezama baharini; au kwa bahati mbaya au kwa mpango kama huo hapo juu wa wale watumwa waliozamishwa baharini wakidaiwa kuwa ni bidhaa.

Hivi watu wa Libiya, kabla ya kuondolewa Gaddafi, ni lini walilalamika kuwa maisha ya nchi yao ni magumu, ili tuseme kuwa walikuwa wakitamani waende Ulaya? (Itaendelea)

RAIS wa zamani wa Marekani, George W. Bush (kulia) na Rais wa zamani wa Ufaransa Chirac.

ANNUUR NEW.indd 17 4/6/2016 9:34:08 AM

Page 18: ANNUUR 1224

18 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016Makala

SIKU ya Jumamosi, tarehe 2 Aprili, 2016, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama Cha Wananchi – CUF, lilifanya kikao chake cha kawaida cha siku mbili katika hoteli ya Mazsons, iliyopo Shangani, mjini Unguja, chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama hicho, Twaha Taslima. Pamoja na mambo mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, limetoa taarifa (MAAZIMIO) ya mwelekeo wa Chama Cha Wananchi – CUF kuhusu hali ya kisiasa nchini na hususan visiwani Zanzibar mara baada ya kukamilika kile kilichoitwa “Uchaguzi Mkuu wa Marudio” uliofanyika Machi 20, mwaka huu ambao ulisusiwa na vyama zaidi ya tisa (9) kikiwemo chama cha CUF kati ya vyama kumi na nne (14) vilivyoshiriki katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 na matokeo yake kufutwa Oktoba 28, 2015, na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha.

Jumatatu, Aprili 4, 2016, Baraza Kuu la Uongozi la CUF, Taifa, walifanya mkutano na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya Chama hicho, iliyopo maeneo ya Vuga, mjini Unguja. Lengo la mkutano huo na waandishi wa habari ilikuwa kutoa taarifa (MAAZIMIO) ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi ambacho kilikutana kwa muda wa siku mbili. Taarifa hiyo ilikuwa na MAAZIMIO kumi na tatu (13), pamoja na mambo mengine yaliyotolewa katika MAAZIMIO hayo, hoja kubwa zilikuwa ni tatu.

1. Kuendelea kuwataka wananchi waendelee kuitunza amani.

2. Kusisitiza kutoutambua utawala wa SMZ uliopo madarakani kwa sasa.

3. Kuendelea kuitafuta haki ya wanachi kwa njia ya demokrasia.

Kwa msingi wa kusimamia hoja yangu niliyoikusudia hapa, naomba nilinukuu AZIMIO la kumi na mbili (12).

“…..inaendelea kuwataka Wazanzibari, kuwa watulivu na kulinda amani iliyopo na linawahakikishia kwamba, CUF inaendelea na juhudi zake za kutafuta haki yao na kusimamia maamuzi

Katika hili Maalim amefaulu!Majeshi, Vikosi warudi kambini kwaoWakasake majambazi, wabwia unga

Na Ally Mohammed

yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015, kwa njia za amani na za kidemokrasia”.

“Njia hizo za amani zimefanikiwa na kuungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa, ambayo imeanza kuchukua hatua dhidi ya ubakwaji wa demokrasia uliofanyika”. Mwisho wa nukuu.

Ni maneno yenye mantiki na busara ya hali ya juu kwa anayetambua nafasi ya kiongozi anayetakiwa kuwa na busara. Busara inahitajika wakati ambao kauli yeyote kwa wakati huo atakayoitoa kiongozi inaweza kubadili hali ya mambo aidha kuwa hasi au chanya na kwa hili la CUF ni wazi limekuja na taswira chanya.

Nimesukumwa kuandika makala hii baada ya kuona baadhi ya watu wakikosoa vikali tena kwa dharau kubwa eti hakuna jipya, ni yale yale, wamefeli, imebaki stori na kauli nyengine za aina hiyo zenye kejeli, dharau na ni wazi zinatoka kwa aidha, watu waliokata tamaa au wasiojua siasa na kupigania haki kwa misingi ya demokrasia za kistaarabu na za kisomi. Nasema ni watu waliokata tamaa au wasiojua siasa za kistaarabu kwa sababu, nimefundishwa ukitaka kupinga kitu chochote ni lazima uwe na hoja madhubuti ambayo itakuwa na uzito na utaweza kuitetea. Lakini huwezi kupinga na kudharau kitu bila kushauri njia mbadala ambazo wewe unaziona ni nzuri na zingefaa kutumika kwa wakati huo

kwa kile unachokiona.Kuna watu walidhani

pengine CUF wangekuja na MATAMKO mazito, yenye kuhamasisha vurugu, chuki, fitna na uhasama kwa jamii. Huu ni uwendawazimu na upetevu wa kiwango cha kidhalimu usiopaswa kuwazwa na binaadamu mwenye akili timamu hata dakika moja. Kwamba CUF watoe MAAZIMIO ya kuhamasisha watu wake waingie barabarani na kufanya vurugu, kweli? Katika kipindi hichi ambacho Vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo ‘moto’ na vimejiandaa vya kutosha kukabiliana na hata sisimizi atayeleta ‘fyokofyoko’! Nitakuwa mtu wa mwisho kuunga mkono CUF kuhamasisha vurugu katika kipindi kibaya zaidi cha tahadhari tunachokipita kwa wakati huu. Ningewashangaa CUF (Uongozi), na kuwatoa thamani viongozi wote wa chama hicho kama wangekuja na MATAMKO ya kuchochea vurugu kwa wanachama na wafuasi wake.

Sifa kubwa ya kiongozi ni kutawaliwa na busara katika kipindi ambacho kauli au uamuzi wake wowote utaleta matokeo hasi, katika hili CUF wamefaulu kwa asilimia zote.

Ni wazi, kuna wafuasi wa Chama hicho (CUF) wanaonekana kukata tamaa na kuona matamko ya Chama chao hayana athari yeyote kwa sasa na pengine mawazo yao wanaona hayana hata haja ya kutolewa, wao wanataka kusikia kauli ya

kuhamasishwa kuingia barabarani na kufanya vurugu. Hiki ni kiwango kibaya zaidi cha kufikiria kwa binaadamu mwenye uelewa, mwenye kuzitambua siasa za Tanzania na hasa Zanzibar, mwenye kutumia ‘jicho la tatu’ kuangalia mambo kwa uhalisia wake na matokeo yake ya baadae. Ni kipindi ambacho busara inahitajika zaidi kuliko kibri, ni kipindi ambacho wenye elimu na busara wanalazimika kufikiria zaidi ya upeo wao ili kufanya maamuzi ya busara. Tusisahau ya 2001!

Unapokuja na kauli za dharau, kejeli, kashfa, kukata tamaa kwa kisingizo eti, MAAZIMIO ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF hayana jipya wala hayawezi kubadilisha kitu, hivi tulitaka CUF waje na kauli gani nyengine? Kwamba CUF iseme “tumechoka na sasa tunawataka wananchi wote waingie barabarani kudai haki yao kwa nguvu” Tulitaka CUF waseme hivyo? Tunazishirikisha akili zetu katika kufikiri au ni mihemko tu?

Uongozi sio kiburi na hasira, kwa wenye familia tuangalie hata mfano tu wa familia zetu zinapokuwa kinzani, tunatumia njia gani kutafuta suluhisho? Na Matokeo ya njia hizo ni nini? Watu waache kuongozwa na ‘sauti za shetani’ kila wakati, kuwa kwa kuwa wameminywa sauti yao, basi njia nyengine iliyobaki ni kuitafuta haki yao kwa njia za vurugu. Ni nani aliyetarajia kuwa tungepita katika kipindi hichi kwa utulivu mkubwa? Je, tumesahau kuwa tulijiandaa kwa kununua vyakula na mahitaji yote muhimu tukiamini kutatokea vurugu kubwa wakati wa uchaguzi? Ni nani anajitoa fahamu na kutokuiona nguvu kubwa ya Chama Cha Wananchi – CUF katika kuhamasisha amani na utulivu na wafuasi wao wakatii hilo? Tuwe na desturi ya kuchanganua mambo kwa kuangalia leo, kesho na mtondogoo. Hasara na faida na matarajio yetu ni yapi badala ya kuwa na akili ya kuipinga busara bila kuwa na suluhisho lenye matokeo chanya. Kulalamika kusikokuwa na mpango mkakati wa baadae, hakuna msaada zaidi ya kupoteza muda na kupunguza uwezo wa kufikiri.

(Ally Mohammed anapatikana kwa barua-pepe ya [email protected])

MAALIM Seif Sharif Hamad.

ANNUUR NEW.indd 18 4/6/2016 9:34:11 AM

Page 19: ANNUUR 1224

19 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

M

Ukurasa wa Watoto

Somo la Kwanza: Tawhiid -6

WIKI iliyopita tulimalizia darasa letu kwa kuuliza swali: Nani aliyemuumba ng’ombe wa kwanza? Bila shaka watoto wote watakuwa washapata jibu.Katika darasa la leo tunatafiti ili kujua, sisi binadamu tumetoka wapi?Abdul Azizi ni mtoto wa darasa la kwanza.Anasoma Madrasatul-Aqswaa.Siku moja Abdul Azizi aliulizwa na Ustadh:Ustadh: Abdul Azizi umezaliwa na nani?Abdul Azizi: Nimezaliwa na mama yangu.Ustadh: Mama yako

amezaliwa na nani?Abdul Azizi: Mama amezaliwa na bibi yangu.Ustadh: Bibi yako amezaliwa na nani?Abdul Azizi: Bibi yangu amezaliwa na mama yake.Ustadh: Mama yake bibi yako amezaliwa na nani?Abdul Azizi: Mama yake bibi yangu amezaliwa na mama yake.Maswali haya na majibu hayana mwisho.Labda Ustadh angeuliza: Binadamu wa kwanza ametoka wapi?Nani aliyemuumba binadamu wa kwanza?Turudie na yale maswali ya somo lililopita.

MWANAFUNZI wa Madrasat Firdaus,Yusra Yahabu, akisoma Qur an, katika hafla ya mashindano ya kuhifadhi Qur an yaliyoandaliwa na Madrasa Firdaus, Tabata,Kisiwani, Jijini Dar es Salaam. (Picha kutoka Maktaba yetu)

Mama MAMA yake mama (Bibi)

Mama yake Bibi

1. Nani aliyemuumba kuku wa kwanza?2. Nani aliyemuumba ng’ombe wa kwanza?

3. Nani aliyemuumba mtu wa kwanza?

Watoto wote watafute najibu ya maswali haya.

ANNUUR NEW.indd 19 4/6/2016 9:34:20 AM

Page 20: ANNUUR 1224

20 AN-NUURRAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 201620 MAKALA AN-NUUR

20

Soma gazeti la AN-NUUR

KWA TSH 800/=kila Ijumaa

Gazeti hili hutolewa na Islamic Propagation Centre S.L.P. 55105 na kupigwa chapa na Business Printers Ltd, Dar es Salaam.

RAJAB 1437, IJUMAA APRILI 8 - 14, 2016

HAIIBA TIMAMU TEA CHAI YA AJABU KWA AJILI YA KUKABILIANA NA

SHINIKIZO LA DAMU (HYPERTENSION/HIGH BLOOD PRESSURE)

UGONJWA WA MOYO KIHARUSI JONGO (GOUT) MAUMIVU YA VIUNGO (RHEUMATISM) MAUMIVU SUGU YA KICHWA BAWASIR (PILES/HEMORRHOIDS) MAGONJWA YA INI SARATANI MBALIMBALI UOTO/UVIMBE MBALIMBALI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI VYA MWANAMKE (FIBROIDS, POLYPS NA CYSTS)

KUSHINDWA KUZUIA MKOJO (URINARY INCONTINENCE)

ATHARI ZA KISUKARI CHA UKUBWANI PUMU UPUNGUFU WA KINGA ZA MWILI KASI YA KUZEEKA MATATIZO YA MFUMO WA MZUNGUKO WA DAMU

MKAKAMO WA NGOZI; UDHAIFU WA MACHO KUPOTEZA KUMBUKUMBU KASI NDOGO YA KUPONA MAJERAHA MAKOVU KWENYE MAPAFU UGONJWA WA NGOZI KUCHUJA RANGI, YAANI, VITILIGO

HAIIBA TIMAMU TEA INAPATIKANA

HERBAL IMPACT

MOSQUE STREET, NO. 1574/144 (MKABALA NA MSIKITI WA SUNNI), KITUMBINI, DAR ES

SALAAM

TUTEMBELEE AU TUPIGIE SIMU NAMBA:

0754281131/0655281131/0686281131/0779281131

TATIZO LANGU LA PUMU LIMEPUNGUA SANA BAADA YA KUTUMIA HAIIBA TIMAMU TEA

Na. Mwalimu Said Mwanzoni mwa mwaka jana (2015) nilipata ugonjwa wa kichwa wa kutisha. Muda wote bila kujali kuwa ni mchana au ni usiku kichwa kiliniuma bila kikomo. Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio kazini nikapewa likizo ya ugonjwa. Ilinitisha sana kwa sababu sikujua mwisho wa huu ugonjwa ingekuwa nini.Kwa bahati siku moja rafiki yangu mmoja alinishauri nitumie chai fulani inayoitwa HAIIBA TIMAM TEA. Ilikuwa ni muda wa usiku lakini baada ya kuwasiliana na wahusika nikabaini kuwa nyumbani kwangu na kwao hakukuwa mbali sana. Usiku huo huo nilifanya jitihada nikapata pakiti moja ya hiyo chai. Mambo ya ajabu sana! Baada ya kuchemsha usiku ule na kutumia asubuhi niliamka bila maumivu yoyote! Hadi hivi leo miezi kadhaa imeshapita na yale maumivu hayajarudi tena. https://www.facebook.com/Herbal-Impact-157972014402705/

MAUDHUI ya tahariri ya toleo la gazeti hili la juma lililopita yaliyosanifiwa chini ya anwani kubwa iliyosomeka 'Maalim Bassaleh awe kigezo' pamoja na vijianwani vidogo viwili vilivyosomeka 'Waislamu, Wakristo wamkosa Idrisa' na 'Mimbari zitumike vyema kutoa ujumbe'; yamenikumbusha maudhui yenye mwelekeo kama huo niliyowahi kuyasoma katika tafsiri ya kitabu 'ALQIYAADAATUD DIINIYYATIL KHITWAABI WAL-AADAAIL-IJTIMAAIYYI' kilichoandikwa na Sheikh Hassan Mussa Saffar na kufasiliwa kwa lugha ya Kiswahili na Bw. Abdulkariim Juma Nkusui kama 'UONGOZI WA KIDINI-MAELEKEZO NA UTEKELEZAJI WA KIJAMII'.

Katika sura ya pili ukurasa wa arobaini na tisa (49) wa toleo la kwanza la tafsiri ya lugha ya Kiswahili ya kitabu hicho, mwandishi anamnukuu Dr. Khalis Jalabiy kupitia makala yake yenye anwani 'MATATIZO YA HOTUBA ZA IJUMAA'. Pamoja na anwani hiyo ya makala ya Dr. Jalabiy, ni vyema ieleweke wazi kwamba kimsingi khutba kama khutba

Makhatibu wanapaswa kubadilikaNa Abuu Nyamkomogi hazina tatizo kwa kuwa hazijiandai

zenyewe, bali huandaliwa na hazina uwezo wala utashi wa kufanya uamuzi wa kukiuka utaratibu wa mwandaaji wake. Na kwa kawaida waandaaji wa khutba za Ijumaa ni makhatibu. Kwa hiyo unapozungumziwa udhaifu au uimara wa khutba fulani ya Ijumaa, kinadharia na kwa mtazamo wa harakaharaka, udhaifu au uimara huo, unaweza kudhaniwa kuwa ni wa khutba yenyewe, lakini kiutendaji, viwili hivyo (udhaifu na uimara) hutokana na khatibu.

Baada ya kunukuu, ndani ya kitabu chake nilichokitaja katika aya ya kwanza ya makala haya, ushahidi na mifano kadhaa iliyotolewa na Dr. Jalabiy kuhusiana na hali ya mwenendo wa makhatibu wetu kwa upande mmoja na khutba zao kwa upande wa mwingine; mwandishi wa kitabu hicho, Sheikh Hassan Mussa Saffar naye akatoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na hali na mwenendo wa baadhi ya makhatibu wa zama zetu kama anavyobainisha kupitia sherehe yake katika ukurasa wa hamsini hadi wa hamsini na moja (50-51) wa kitabu chake kwamba ''Kama makhatibu hawa (waliotolewa mfano na Dr. Jalabiy) wanakabiliwa na udhuru wa kutokuwa na na maarifa kamili

na uelewa sahihi kuhusu zama zao, na kutokujua ujumbe wao, basi hakika sehemu nyingine ya makhatibu wanafanya uzembe, wao hawatumii juhudi za kutosha katika kuandaa hotuba zao.

Nitafafanua zaidi baadhi ya nukta kutoka katika nukuu hiyo, wakati wa kujadili kipengele cha namna khatibu anayetambua jukumu lake na mazingira yake pamoja na ulimwengu wa sasa unavyokwenda anavyopaswa kujiandaa, kadri fursa na wasaa vitakaporuhusu huko mbele katika mwendelezo wa makala haya inshaallaah.

Mwandishi anazidi kutanabahisha kwamba ''Na katika jamii yetu ya leo kuna idadi kubwa ya wabobezi na wenye ubobezi ambao unawezekana kuwaomba ushauri na kunufaika na maoni yao katika kutatua mambo yanayohusiana na ubobezi wao. Hakika udhaifu wa maandalizi ya khatibu katika kuandaa hotuba unafanya uchambuzi wa khatibu uwe ni wa juu juu na mwepesi, kama ambavyo uhandisi wa maudhui na mfumo wa kuwasilisha unavyokuwa na mkanganyo na usio na umakini wala ufanisi. Wakati ambapo khatibu mwenye juhudi katika kuandaa hotuba, huwa ni mwenye

kudhibiti maudhui ya utafiti wake, mwenye mtiririko mzuri wa nukta (pointi) zake, na hukinaisha fikra zake kwa hoja na ushahidi wenye

'Maalim Ally Bassaleh

Inaendelea Uk. 15

ANNUUR NEW.indd 20 4/6/2016 9:34:22 AM