abdallah ibn sabaa

159
i ABDULLAH IBN SABA` NA NGANO NYINGINEZO Kimetungwa na: ALLAMAH SAYYID MURTADHA AL- ASKARI Kimetarjumiwa na: Al-Akhi Ramadhani Kanju Shemahimbo P.O. Box 107 DAR ES SALAAM TANZANIA.

Upload: alitrah-foundation

Post on 25-Mar-2016

1.037 views

Category:

Documents


1 download

DESCRIPTION

Kitabu hiki kinahusu ngano ya Ibn Saba mtu ambaye hajawahi kuishi katika ulimwengu huu. Lakini mtu huyu ambaye amepachikwa jina la Abdullah Ibn Saba, amesukwa kwa maneno katika vitabu vya historia mpaka watu wakaamini kwamba kweli alikuwepo mtu kama huyu, na baya zaidi, watu wakapotoshwa kwamba huyu ndiye aliyeanzisha Ushia.

TRANSCRIPT

i

ABDULLAHIBN SABA`

NA

NGANO NYINGINEZO

Kimetungwa na:ALLAMAH SAYYID MURTADHA AL- ASKARI

Kimetarjumiwa na:Al-Akhi Ramadhani Kanju Shemahimbo

P.O. Box 107DAR ES SALAAM

TANZANIA.

ii

©Haki ya kunakili imehifadhiwa na:AL - ITRAH FOUNDATION

ISBN # 9987 - 665 - 30 - 6

Kimeandikwa na:

Sayyid Murtadha Al - Askari

Kimetarjumiwa na:

Al-Akhi Ramadhani Kanju Shemahimbo

S. L. P. 1017

Email: [email protected]

Website: www.alitrah.org

Kupangwa katika kompyuta na:

Ukhti Pili Rajabu.

Toleo la kwanza: Oktoba 2004

Nakala:1000

Kimetolewa na kuchapishwa na:Al-Itrah Foundation

P. O. Box 1017Dar-es-Salaam, TanzaniaSimu: +255 22 2110640Fax: +255 22 2113107Email: [email protected]

Website: www.alitrah.org

iii

NENO LA MCHAPISHAJI

Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza, kwa jinala"Ibn Saba and other myths" (Ibn Saba na ngano nyingine) kilichoandikwa naSayyid Murtadha Al - Askari

Kitabu hiki kimeandikwa na Mwanachuoni mkubwa, mwanahistoria na mtafiti.Kitabu hiki kinahusu ngano ya Ibn Saba mtu ambaye hajawahi kuishi katikaulimwengu huu. Lakini mtu huyu ambaye amepachikwa jina la Abdullah Ibn Saba,amesukwa kwa maneno katika vitabu vya historia mpaka watu wakaamini kwam-ba kweli alikuwepo mtu kama huyu, na baya zaidi, watu wakapotoshwa kwambahuyu ndiye aliyeanzisha Ushia.

Ili kuwatoa watu katika dhana hii potofu Mwanachuoni huyu mahiri amefanya utafi-ti wa kina na kuthibitisha pasina shaka yoyote kwamba hajakuwepo mtu kamahuyu duniani. [Itabidi wale wanaoshikilia dhana hii, kama hawataki ukweli, wamta-fute Ibn Saba mwingine lakini sio huyu tena].

Kutokana na ukweli huu tumeona tukitoe kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili ilikizidishe mwanga wa elimu kwa Waislamu wazungumzaji wa Kiswahili ili kuon-dokana na dhana hii potofu. Na hili ndilo lengo kubwa la Taasisi yetu ya 'Al-ItrahFoundation' katika kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru Ndugu yetu al-Akhy Ramadhani Kanju Shemahimbo kwa kukubalijukumu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vile vile tunawashukuru wale wotewalioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabuhiki.

Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni mwanga kwa wasomaji wetu nakuzidisha upeo wao wa elimu katika dini.

Mchapishaji:

Al-Itrah FoundationS. L. P. 1017Dar-es-Salaam.

iv

YALIYOMO.

i. Dibaji ya Mchapishaji………………………………....................... ixii. Maelezo ya Mtunzi……………………………….............................xiii. Wasifu wa Mwandishi……………………………. ..........................1

Hatua zilizochukuliwa……………………………............................1Mtu wa Elimu na Vitendo………………………..............................2Taasisi na Mashirika ya Kiislam………………….. ........................5

.iv. Maoni ya Dr. Hamid Hafni Dawood: (Profesa wa lugha ya Kiarabu

katika chuo Kikuu cha Cairo)…………….. .................................10Ukweli nyuma ya uwongo…………………………........................10

v. Maoni ya: Sheikh Mahmood Abu Riyya………............................13vi. Maoni ya: Al-Sheikh Jawad Mughniah (Mwanazuoni wa

Kishiah)…………………………………….....................................15vii. Maoni ya:Profesa James Robinson D.L.H.D.D Glasgow,

U.K…………………………………………………………...............17Mpendwa Sayyed Murtadha Al-Askari………………...................17

1. UTANGULIZI…………………………………………….............................20Ngano ya 'Abdullah Ibn Saba'……………………………........................ 20

2. ASILI YA NGANO HII YENYEWE……………………….......................... 20Seif ni nani (Wasifu Mfupi)………………………………........................... 21Jeshi la Usama………………………………………………....................... 22Saqifa, ukumbi wa Bani Saidah……………………………....................... 22 Kuhusu ukumbi wa Saqifa Banu Saidah kwa Mujibu wa vyanzo sahihi……………………………………………….................... 23

3. DIBAJI…………………………………………………………..................... 24Vipi na kwa nini kitabu hiki kimekuja………………………...................... 24 Ngano ya Abdullah Ibn Saba'…………………………………...................25Mukhtasari wa kile kinachojulikana kutoka kwa Wanahistoria….............

4. ASILI YA NGANO YENYEWE NA YA WASIMULIAJI WA NGANO HII…….....................................................................................................28Muhammad Rashid Ridha…………………………………….................... 28Abdul Fida ( Kafa 732H.L. 1331 AD)………………………….................. 28Ibn Athir (Kafa 630H.L - 1229 A.D)………………………........................ 28

v

Ibn Kathir ( Kafa 774 H.L - 1289.A.D)………………………......................29Ibn Khaldun……………………………………………………..................... 29 Muhammad Farid Wajdi…………………………………….........................29Al-Bustani……………………………………………………….................... 29Ahmed Amin…………………………………………………….................... 30Hasan Ibrahim…………………………………………………................... 32Van Flotten (volten) (Johannes 1818-1883)……………………............. .33Nicholson, Reynold alleyne (1868-1945)……………………….................33Ensaiklopidia ya Kiislamu………………………………………...................33Donaldson, M. Dewight…………………………………………. ................ 34Well Housen Juliua (184-1918)………………………………….................35Mirkhand katika kitabu chake Rawzatus Safa…………………................35Ghiathud din (Kafa 940H.L. - 1455A.D)...………………………................35Tabari na chanzo chake………………………………………….. ...............36Ibn Asakir (Kafa 571H.L- 1086A.D)…………………………… ..................36Ibn Bardan (Kafa 1346 H.L. 1851A.D)………………………….................36Ibn Abibakr (Kafa 741H.L- 1256A.D…………………………….................37Sa'd Afghani…………………………………………………….....................37Dhahabi (Kafa 784H.L-1263 A.D)…………………………….....................37

5. SEIF IBN UMAR AT-TAMIMI (Kafa baada ya 170A.H)………………...39

6. UCHUNGUZI KUHUSU SEIF NA SIMULIZI ZAKE……………………… 40Seif ni nani………………………………………………………....................40Vitabu vya Seif……………………………………………….........................40Tathmini ya maandishi ya Seif…………………………………...................41

7. JESHI LA USAMA…………………………………………………………....44Ngano ya Seif…………………………………………………......................44Masimulizi ya wengine mbali na Seif………………………………............44Ulinganisho…………………………………………………..........................45Baadhi ya Masahaba watambulishwa………………………….................46Busara za Muhammad katika kitanda chake cha mauti…………............47

8. SEIF NA SAQIFAH………………………………………….........................49Uchunguzi juu ya ukweli wa Ngano kuhusu Saqifa kama zilivyandikwa na Seif………...........................................................................................51

vi

Msimuliaji wa Ngano……………………………………………...................51Tukio la Saqifa na wanahistoria wangine mbali na Seif…………………...51Saqifa na Abubakr………………………………………………...................51Je Mtume alieleza nia yake kwa maandishi?……………………..............52Kifo cha Mtume s.a.w.w…………………………………………..................55Hawa wagombea kabla ya mazishi ya Mtume s.a.w.w………….............57Mgombea wa pili wa urithi wa Mtume s.a.w.w…………………................58Mgombea aliyefaulu…………………………………………….. .................59Kiapo cha hadhara………………………………………………..................62Baada ya kiapo cha utii…………………………………………...................63Mazishi ya Mtukufu Mtume s.a.w.w……………………….........................63Hifadhi katika nyumba ya Fatimah……………………………...................64Mwisho wa matukio pale kwenye kiapo………………………...................68

9. MAONI YALIYOTOLEWA NA WATU MBALI MBALI KUHUSU HICHO KIAPO CHA UTII …………………………………………........... ..70Fadhl Ibn Abbas………………………………………………......................70Abdullah Ibn Abbas………………………………………….........................70Salman Farsi……………………………………………………...................71

Umma Mistah……………………………………………………...................71Abu Dhar…………………………………………………………..................71Miqdad……………………………………………………………................. 71Bibi mmoja kutoka Bani Najjar …………………………………................ 72Abu Sufian………………………………………………………...................72Wito wa Abu Sufian- Enyi wana wa Abd Manafi………………................72Mu'awiyah………………………………………………………....................75Khalid Ibn Said………………………………………………….....................75Sa'd Ibn Ubaidah………………………………………………….................76Umar………………………………………………………….........................78Tathmin ya simulizi ya Seif…………………………………….. .................78

10. RIDDAH (Uasi)…………………………………………………………….....84Uasi katika Uislamu……………………………………………. ..................84 Waasi wakati wa Mtume s.a.w.w………………………………. ............ .. 84

vii

Uasi wakati wa Abubakr………………………………………................ .. 85

11. MALIK IBN NUWAIRA…………………………………………………........90Ngano ya Maliki kwa Mujibu wa Seif…………………….......................... 93

Kiini cha ngano za Seif………………………………………...................... 95Ni nani hawa Sa’b,Atyya na Uthman………………………........................95Kwa nini Ngano za Seif ni za uwongo……………………........................95Maandishi ya Ngano za Seif……………………………………..................96Ulinganisho……………………………………………………….................. 96

12 NGANO YA ALA IBN HAZRAMI………………………………………… ...99 Seif anatueleza kuhusu Ala Ibn Hazrami…………………….....................99Asili ya ngano ya Seif…………………………………………....................101Ngano ya Ala kutoka kwa wengine mbali na Seif……………….............101Vita dhidi ya waasi (ulinganishaji na Hitimisho)………………................101

13. HAUW-AB NCHI YA MIJIBWA…………………………………………….104Chanzo cha ngano ya Seif……………………………………...................104Ni nani alibwakiwa na Mbwa hapo Hauwab?……………………............104

14. KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIA YA ZIAD……….109Kiini cha ngano ya Seif……………………………………….....................110Ilivyoelezwa na wengine mbali na Seif…………….................................110

15 NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA…………………………………... 111Wanahistoria wengine………………………………………….................. 113Asili ya ngano ya Seif…………………………………………....................116

16. KIFUNGO CHA ABU MAHJAN…………………………………………...118Simulizi ya Seif………………………………………………….................. 120Asili ya ngano ya Seif………………………………………….................. 120

17. SIKU ZA SEIF…………………………………………………………….....123Siku ya Ng'ombe…………………………………………..........................123Vyanzo vya ngano za Seif……………………………………....................123Siku za Armath, Aqwas na Emas………………………………................124Chanzo cha ngano ya Seif……………………………………...................124

viii

Siku ya Jarathim…………………………………………….......................124

18. MASHAURIANO NA KIAPO CHA UTII KWA UTHMAN………………..128

Ngano ya mashauriano kutoka kwa wengine mbali na Seif…. ...........128Ushauri na Umar………………………………………………...................129

19. QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZAN KWA MUJIBU WA SEIF…136

Ngano kama ilivyoelezwa na wengine mbali na Seif…………...............136

20. MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF……………………………………………...139

Doluth……………………………………………………...........................139

Tawous…………………………………………………………....................140

Je'rana na Na'man……………………………………………....................140

Qorduda……………………………………………………….....................140

Mto Utt…………………………………………………………....................140

Irmathi Aghwath na Amas ……………………………………................ 141

Altheni, Thanya Talkerab, Al-Qodais Al-maqr, Wayakhord

Walaja na Alhawafi….............................................................................141

21. SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZO……………………………...........143

22. HITIMISHO …………………………………………………………….........145

ix

Dibaji ya mchapishaji(Chapa ya Kiingereza)

Islamic Thought Foundation (Taasisi ya Fikra za Kiislam) ni taasisi ya msaadainayojihusisha na uchapishaji wa vitabu na majarida ya Kiislam katika lugha tofau-ti. Taasisi hii imechapisha karibu vitabu 50 kwa Kiarabu, Kiingereza, Kijerumani,Kifaransa, Kihindu, Kijapani, Kiurdu, Kituruki, na Kiswahili.Kitabu hiki "Abdullah ibn Saba" ambacho kipo mikononi mwako sasa ni utunzi wamwanazuoni mashuhuri Bw.Sayyid Murtadha Al-Askari. Ni (utunzi) wa kipekee nawenye mwanga wa namna yake wenye kuweza kuondoa shaka miongoni mwamadhehebu tofauti za Kiislamu na kuzileta karibu zaidi pamoja. Kitabu hiki kime-pokelewa vizuri na kusifiwa na wanazuoni wote Sunni na Shi'ah na mustashirki waMagharibi vilevile, kama inavyoweza kuonekana kwenye mapokezi yao yaliyomokwenye kurasa za utangulizi za chapa hii.

Taasisi ya Fikra za Kiislam imeamua kuchapisha nakala mpya ya "Abdullah ibnSaba" kwa sababu mbili. Kwanza, kitabu kinadhihirisha ukweli juu ya matukio yaawali ya kihistoria ya Uislam ambayo kwa mara ya kwanza yanatoa mwanga juuya mabadiliko yaliyofanywa wakati wa matukio haya. Pili, kitabu cha namna hii nihatua muhimu, ya kawaida na ya msingi katika kuleta umoja miongoni mwa mad-hehebu za Kiislam. Taasisi inatumaini kwamba wasomaji wanaopenda kujua nawatafutaji wa ukweli watayaona haya yaliyomo humu ni yenye faida.

x

Bismi llahi r- Rahmani r- RahiymKwa jina la Allah Mwingi wa Rehma Mwenye Kurehemu.

Shukurani zimwendee Muumba wa Ulimwengu, na salamu na amani kwa mitumeWake na kwa Mtume Muhammad (rehma na amani juu yake na kizazi chake) nawateule wa nyumba yake.

Hii, ikiwa ni chapa ya tatu ya kitabu hiki kwa lugha ya Kiingereza (ya kwanza kwaKiswahili) imetolewa kwa wale wanaotafuta ukweli kuhusu historia ya Uislamu,hususan wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.).Tunamuomba Allahatusaidie na kutuongoza tufanikiwe na kufanya vitendo vinavyompendeza Yeye.

Mwandishi.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

1

WASIFU WA MWANDISHI

Sayyid Murtadha Al - Askari alizaliwa katika mji mtukufu wa Samarrah (Iraq),mwezi 8 Jamadu Thani, 1332 (A.H). Alisoma katika Hauza (Kituo cha Theolojia yaKiislam), na katika Muharram ya 1350 (A.H) alihamia kwenye mji mtukufu wa Qumhuko Iran na akaishi hapo mpaka 1353 (A.H).

Huko Qum, yeye na marafiki zake wawili, Ayatullah Sheikh Murtadha Haeri naSayyid Ahmad Sajjadi walijifunza sheria ya dini na kanuni zake kutoka kwa walimumashuhuri na viongozi wa kidini, kama vile: Ayatullah Sayyid Shehabul-DinMarashi Najafi (R.A) na Ayatullah Sheikh Muhammad Husein Shari'at-Madar…..Allamah Sayyid Murtadha Al-Askari pia alijifunza masomo mbalimbali ya itikadipamoja na Imam Khomeini (R.A.), masomo ya tafsiri pamoja na Sheikh MirzaKhalil Kamrei na maadili pamoja na Ayatullah Sheikh Mahdi Shahidi (msimamiziwa Shule ya Razawi). Inafahamika wazi kwamba Ayatullah Sheikh Mahdi Shahidialikuwa katika Shule ya Razawi kwa miaka miwili, kisha akaenda Hauza Feyziyeh.Kwa kweli , alichukua jukumu muhimu katika utengenezaji wa hadhi ya AllamahAskari na alikuwa ndiye mshauri wake hasa.

Hatua zilizochukuliwa kuimarisha mfumo wa elimu wa Hauza.

Allamah Askari, wakati wa masomo yake katika Hauza hii, alifikia uamuzi kwambamarekebisho fulani ni lazima yafanywe kuhusu mfumo wa kielimu wa Kituo hiki.Kwa sababu hii, yeye pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Hauza hii wenye moyowalifanya jitihada kuunda upya mfumo wa elimu wa Haudha hii. Walijaribu kuan-daa upya programu za kielimu kwa namna ambayo kwamba Hauza iweze kufanyajukumu la uhakika kwa uwezo wake wote na kutimiza wajibu wake kwa ummah waKiislamu.

Baadhi ya masomo yaliyojadiliwa katika mpango wao au mfumo wa elimu uliopen-dekezwa ni: Somo la tafsiri, somo la ngano, na somo la uchambuzi linganifu wamaoni ya Kiislamu sambamba na somo la sheria ya kidini (fiqh) na kanuni na tarat-ibu zake. Mfumo huu wa elimu ulioshauriwa pia ulihusu: Jinsi ya kutoa hutuba; jinsiya kuandika na kuhariri sawasawa; na jinsi ya kufundisha kazi za kijamii kwawanafunzi wa theolojia pamoja na mkazo juu ya kujifunza na kufanya tafiti mbal-imbali kuhusu hali ya Waislamu katika jamii tofauti na kuwaonyesha namna yakukielimisha na kukifunza kizazi cha baadae chenye kukubali ushauri na kili-chotaalamika cha Waislamu halisi ili kupata Ummah bora wa Kiislamu.

Uamuzi huu ulifanywa wakati wa kipindi cha mamlaka ya Ayatullah Uzma SheikhAbdul-Karim Haeri, mwasisi wa kituo maarufu cha Theolojia ya Kiislamu chaHauza Ilmiyyah, Qum.

Baadaye, Allamah Askari alirudi nyumbani kwake kwenye asili yake nchini Iraq,

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

2

kwenye mji mtukufu wa Samarrah ili kuendelea na masomo yake ya kidini mpaka1366 A.H. hadi kufikia kiwango cha 'Al-Kifayeh' pamoja na Sheikh HabibullahEshtehardi. Masomo haya yaliendelea mpaka mwanzoni mwa Vita Kuu ya Pili.

Mtu wa Elimu na Vitendo

Tangu alipokuwa na umri wa miaka 15, Allamah Al-Askari alionyesha shaukukubwa katika historia, na safari za wavumbuzi wa dunia. Kwa matokeo ya juhudizake alilimbikiza habari katika nyanja hii ambayo ilikuwa ni zaidi ya kiwango chakawaida cha elimu miongoni mwa wenzie wa darasani.

Baada ya kuyasoma maandishi ya wanafunzi wa Ayatullah Shirazi juu ya Sheriaya Tumbaku na kile walichokiandika watu wa Magharibi kuhusu nchi za Kiislamkatika vitabu vyao vya kumbukumbu za kila siku, alichambua tarehe ya uvamizi wawakoloni kwenye nchi za Kiislam. Kwa ujuzi na akili yake, aliyatambua malengo yauovu ya wakoloni ya kusambaza milki yao ya kielimu na kiutamaduni katikaulimwengu wote wa Kiislam na kuufichua utambulisho wao sahihi.Uvamizi wa kiso-mi haujamalizika bado hata pamoja na mwisho wa milki ya moja kwa moja yawakoloni juu ya nchi za Kiislam na bado unaendelea kwa kificho. Aligundua pia jiti-hada za hatari za kuhusisha kwa makusudi fikra sahihi na maoni ya Kiislam nafikra za kisasa za Kimagharibi na matokeo yake katika kubadili sura halisi yaUislamu katika mawazo ya vizazi vya baadae.

Allamah Askari alikuwa miongoni mwa wasomi wa Kiislamu wa awali wa Iraq wali-ogundua sababu halisi ya programu za kielimu zilizoandaliwa na washauri wakigeni katika shule za serikali kwa vijana wa nchi za Kiislam. Baada ya uchunguzimakini, alielezea tofauti kubwa kati ya programu za kielimu za nchi kamaUjerumani, Ufaransa, Japani, n.k., na programu za zile nchi zilizomilikiwa na muk-tadha wa vitabu vyao vya kiada.

Kutokana na tofauti hizi, aligundua kwamba moja ya sababu kubwa za kuwanyuma kwa nchi za Kiislam ni hii mipango ya kielimu na mafunzo. Ndiyo maanaakaziita shule zetu 'kiwanda cha kuandaa waajiriwa wa baadae,' kwa sababu shulewakati ule zilianzisha waajiriwa wa kazi zisizo na sulubu 'white-collar employees'ambao wangefanya chochote kutekeleza amri za mamlaka kuu na programu kati-ka jamii bila hoja wala majibizano.

Allamah Askari pia aliuona ukosefu wa uhusiano kati ya Hauza hiyo na vyuo vikuuvya kisasa, hizi nguzo kuu mbili muhimu za jamii ya Kiislamu. Hauza ilitengwa nakujihusisha na kuwafunza wanafunzi kuwa mabingwa wa ujuzi na walimu wabaadae wa Hauza na si kingine chochote; na vyuo vikuu pia vilikuwa na mwelekeo

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

3

wa Kimagharibi na walikuwa wageni kwenye jamii yao ya Kiislam.

Kwa hiyo, kulikuwa na haja ya harakati (chama) za kuondoa mkwamo huu na kufu-ta utengano na unyonge huu. Allamah Askari alianzisha harakati hii wakati ule VitaKuu ya Pili ilipoihatarisha Iraq na watu wake. Harakati yake ya kwanza ya kita-maduni ilikuwa ni kuandaa mikutano ili kuwajulisha watu na kuwaelimisha.

Wakati huo huo, alianzisha shule ya kuwasomesha vijana na alipanga namna yamasomo yeye mwenyewe, kisha akaifanya shule hii kama sehemu ya mpangowake mkubwa. Katika shule hii, baadhi ya wanazuoni, kama vile Sheikh MirzaNajmu-Din Sharif Askari, Sheikh Hassan Kumeil, Sayyid Jafar Shahrestani naSheikh Mahdi Hakim walifundisha.

Wakati akianzisha na kupanga, Allamah Askari kama mwana mageuzi mwingineyeyote yule katika karne zilizopita, alipambana na upinzani wa kijinga na wa kiza-mani. Hivyo aliona ni bora kuandika kitabu kuhusu utamaduni wa Kimagharibi nauvamizi wa kisomi katika nchi za Kiislamu na akasanifu mipango mbalimbalikupambana na uvamizi huu. Baadhi ya mipango hiyo ilikuwa ni:

a) Kuasisi shule za kisasa za kuelimisha kizazi kichanga na kuwatambulishakwenye utamaduni na elimu ya Kiislam.

b) Kuasisi shule nyingine zenye wahitimu waliobobea katika dini ya Kiislamuambao wanaweza kuhamishia elimu yao kwa jamii.

c) Kuchapisha vitabu na majarida ya Kiislamu.

Kitabu chake hiki kilipokwisha, alikiita; 'Maradhi ya Jamii na Matibabu Yake'.

Baada ya muda, alirudi Iraq na kuishi katika mji mtukufu wa Kazimayn ili kupatamazingira bora ya kutibu baadhi ya maradhi ya jamii yaliyokuwepo kwa utamaduniwa Kiislamu. Hapa alimtembelea Profesa Ahmad Amin (Mwandishi wa kitabu-'Mageuzi katika Uislam') na kwa kubadilishana alimpa kitabu chake. Katika kuku-tana huku kulikotokea mwaka 1363 A.H. wanazuoni wakubwa wawili hawa wali-fikia makubaliano ya kuanzisha shule ya maandalizi. Marhum Ahmad Aminalikubali jukumu la kubuni muundo wa shule kwa msaada wa Allamah Askari nakumtia moyo kwake. Mwishowe shule hii ilianzishwa hapo Kazimayn na waliiita'Muntada Al-Nashr'.

Mara tu baadae, shule hii ilijiunga na jamii ya 'Muntada Al- Nashr' au 'Kituo chauchapishaji' cha Najaf ili kupata kibali cha kazi kutoka serikalini harakaiwezekanavyo. Kwa kuhakikishiwa uanzishwaji wa shule hii, Allamah Askari aliru-di Samarrah. Lakini kwa vile Ahmad Amin alikabiliana na matatizo kadhaa,alimkaribisha tena kuishi Kazimayn, kuwa mkuu wa shule na kuweka taratibu

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

4

mbalimbali kueneza utamaduni wa Kiislamu. Baada ya kukamilika kwa sehemu yakwanza ya mpango huo ambao ulikuwa mafanikio ya muundo wa shule, AllamahAskari aliamua kutekeleza sehemu ya pili ya mpango wake, yaani, kupata kibalicha ujenzi wa taasisi, kama ile shule ya theolojia iliyokuja kuanzishwa baadaehuko Baghdad, ili kuifundisha dini ya Kiislamu na kufunza watu wenye akili.

Kwa kukamilika kwa sehemu ya pili ya mpango wake, Allamah Askari alianzaawamu mpya katika maisha yake ya kidini. Alirudi Samarrah na kutumia miakamiwili kupata fiqhi iliyochanganuliwa kutoka kwa Profesa wake AyatullahEshtehardi.Wakati huohuo, aliandika na kuhariri vitabu mbalimbali juu ya historiaya fikra za Kiislamu. Aligawanya matokeo yake katika sehemu nyingi zitokanazona sura tofauti za uundwaji wa fikra za Kiislamu tokea mwanzo kabisa wa kuji-tokeza kwa Uislamu mpaka mwisho wa ugavana wa Bani Abbas.

Baadhi ya vikwazo vigumu kwenye maendeleo ya utafiti wake vilikuwa: nganombalimbali zilizokubaliwa na Waislamu walio wengi zilipoteza kuaminika kwakebaada ya uchunguzi wa kina, kwa mfano, zile ngano kutoka kwa Ummul-Mu'minin(Ayisha), Abu Huraira, Ibn Abbas, Aun Ibn Malik na kadhalika. Matokeo ya utafitihuu na uchunguzi yalikuwa safi sana kwa vile Allamah Askari aliona udhaifu wangano hizi kwa uthibitisho usiopingika. Nyingi ya ngano hizi zilikuwa hazina msin-gi, hasa ngano ya 'Abdullah Ibn Saba' na 'Masahaba Mia na Hamsini wa Uongo'.Kwa matokeo ya ugunduzi wa utafiti huu muhimu, baadhi ya mambo yanayofa-hamika yaliyokubalika kwa watu kwa karne, yalipoteza kusadikika kwake, na msin-gi wa maandishi na ngano za Tabari au wana-historia mashuhuri wengine haziku-ungwa mkono. Vitabu vya kwanza vya Allamah Askari vilivyochapishwa kuhusumatokeo haya ya utafiti mwaka 1375 A.H. vilikuwa 'Abdullah Ibn Saba' na 'Pamojana Dr. Alwardi'.

Ingawa Allamah Askari alitumia muda wake mwingi kwa kujifunza na kuandika,hakuacha harakati zake za kidini na kijamii. Punde baadae, aliamua kuendelezashughuli zake kwa dhahiri kabisa na akaanzisha shule na Haudha mbalimbali zadini za kipekee. Hakuguswa hata kidogo na vikwazo na matatizo yaliyokuwepo.Kwa hiyo, alihamia Iran na akamtembelea mmoja wa wenye mamlaka (ya kidini)wa wakati wake Ayatullah Sayyid Agha Husein Burujerdi (R.A.). Katika mkutanohuu walikuja kukubaliana kuanzisha Hauza maalum ya kidini huko Qum naAllamah Askari akiwa ndiye mkuu wake.

Lakini utata wa hali ya kisiasa huko Iran kwa wakati ule na nguvu ya migonganokati ya Ayatullah Kashani na wafuasi wake kwa upande mmoja, na Dr. Mussadiqna wafuasi wake kwa upande mwingine, vilimlazimisha arudi Iraq na kuishi hukoKazimayn. Alianza kutengeneza Hauza ya kidini katika mji huo lakini hakuwezakukamilisha kazi hiyo kwa sababu ya vikundi mbalimbali vya upinzani. Hivyo alian-za kujenga shule nyingine, Shule ya Imam Kadhim (A.S.) ambayo ilikuwa imarahadi wakati wa mapinduzi ya tarehe 14,Julai,1968.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

5

Taasisi na Mashirika ya Kiislamu

Baada ya kuona ueneaji wa shughuli za vyama vya kidunia kama vile: vyama vyaKikomunisti na cha Baathi, na ongezeko la mashambulizi ya mpangilio ya kipro-paganda za wamisionari (wa Kikristo) katika kiwango chake cha juu yakidhihirikatika shule na taasisi zao, kama Taasisi ya Watawa wa Chalde (RahebatAlkaldan) na Taasisi ya Watawa wa Bikra Maria (Rahebat Maryam Al-Uzra),Allamah Askari alikusanya nguvu zake zote na pamoja na ndugu zake katika dinina marafiki kutoka Najaf na Baghdad na chini ya usimamizi wa moja kwa moja waMarhum Ayatullah Sayyid Muhsin Hakim, akaanzisha makabiliano makali kabisaya kisiasa na kisomi na vyama hivyo na wamisionari. Sasa, mbali na wajibu wakewa kidini, ilibidi akubali majukumu ya shughuli za kisiasa pia. Kwa sababu hii,Allamah Askari alikwenda kwenye jimbo la Al-Bayyaha la Baghdad kama mwakil-ishi wa wenye mamlaka na kutoka hapo na kuendelea alikwenda kwenye jimbo laKarradeh Mashariki (huko Baghdad). Yeye na wafuasi wake walidhamiria kulitumiajimbo hili kama kituo chao kikuu cha kuanzishia harakati na kufanya mabadilikokwenye mji wote wa Baghdad.

Mwanzo wa harakati za Kiislamu ulikuwa kutoka ndani ya 'Hussainiya' ( sehemuambazo kifo cha kishahidi cha Imam Hussein kinaombolezewa). Katika wakati waAllamah Askari, kikundi cha wanafunzi wa kidini (kwa namna ya waombolezaji waImam Hussein (a.s.) waliandamana wakati Marhum Dr. Dawud Al-Attar aliyekuwakiongozi wao,alikiongoza kikundi hicho kutoka "Shule ya Imam Kadhim" kwendaKazimayn na kwenye Kuba la Imam Kadhim (a.s.). Harakati hii ilichukua kasi kati-ka miaka michache iliyofuata.

Ni jambo linalothibitika kwamba Allamah Askari alikuwa na majukumu makubwakatika harakati ya Kiislamu. Harakati hii ilikusanya Iraqi, Makuba matukufu yaBaghdad, Karbala na Najaf, na ardhi ya Mtume na Maimamu.

Imani ya Allamah Askari ilikuwa ndiyo dhamana ya maendeleo ya juhudi naharakati. Harakati za Kiislamu inakuwa na nguvu tu kama imeundwa katika shiri-ka au taasisi ya Kiislamu siyo na mtu asiyejua. Pili, harakati hiyo isiingiliwe namaoni binafsi. Matokeo yake, Sayyid Hebatul-Din Shahrestani aliasisi 'Kituo chaKiislamu cha Utoaji Sadaka na Allamah Askari alikuwa ndiye mtu wa kwanzabaada ya Hebatul-Din Shahrestani aliyekuja kuwa mkuu wa kituo hiki. Kabla yakuanzishwa kwa kituo hiki, Allamah Askari alikuwa tayari amekwisha anzisha kituokingine kwa jina la "Jumuiya ya Mwongozo wa Kiislam", lakini aliondoka kwenyejumuiya hiyo kwa sababu ya baadhi ya migogoro kati ya uongozi.

Na Allamah Askari akiwa mkuu wa "Kituo cha Kiislamu cha Utoaji Sadaka", kituohiki kilianzisha miradi mbalimbali. Baadhi ya huduma muhimu sana za kituo hikikatika uwanja wa utamaduni zilikuwa kule kuanzishwa kwa vituo vya elimu yaKiislamu. Kutokana na vituo hivi kilijitokeza kizazi kilichovutika kidini waliokubali

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

6

baadhi ya majukumu mazito ya jamii ya Kiislamu, na wakashiriki katika harakatitukufu ya Iraqi, n.k. Majina ya baadhi ya vituo hivi vya kielimu ya Kiislam ni:

Shule za Imam Jawad huko jimbo la Karradeh Mashariki, Baghdad. Shule zote

hizi ziliongozwa na Dr. Dawud Al-Attar.

Shule za Baghdad -Baghdad, ziliongozwa na Abdul-Rahim Shawki.

Rawdhat al-Zahra - Chekechea ya watoto.

Al-Zahra Shule ya Wanawake huko Kazimayn. - Shule hizi ziliongozwa na

Shahid Bint-al-Huda Sadr, marehemu dada yake Ayatullah Shahid Sayyid

Muhammad Baqir Sadr.

Shule za Imam Sadiq - huko jimbo la Basra. Zikiongozwa na viongozi wa kidini

wa Basra na mkuu wake alikuwa ni Sayyid Muhammad Abdul-Hakim.

Sekondari ya juu ya Imam Baqir huko Hellah. Ikiongozwa na Sheikh Ali

Samakeh.

Sekondari ya juu ya Imam Hasan huko Diwaniyah. Ilianzishwa na Sheikh

Muhammad Mahdi Shams Al-Din na ikaongozwa na 'Kituo cha Kiislamu cha

Utoaji Sadaka'.

Kituo cha Elimu kwa Wanawake huko Numaniyyah - katika jimbo la Kute.

Kilianzishwa na Sayyed Qassim Shobba na kuongozwa na 'Kituo cha Kiislamu

cha Utoaji wa Sadaka'.

Kwa kutaja baadhi ya michango yake ya kijamii, mtu anaweza kuangalia uanzish-waji wa kituo cha kliniki cha "Mostosef Al-Ri'ayeh Al-Islamiyyah" (kituo cha afyacha Kiislam) katika jimbo la Karradeh Mashariki ya Baghdad mwaka 1382 A.H., nakituo kingine cha afya kwa jina hilohilo katika jimbo la Kazimayn ili kuuguza nakutibu wanafunzi wa kidini wa Kiislamu, wenye kuzuru kwenye makuba matukufuna masikini. Alidhamiria pia kutengeneza hospitali kubwa iitwayo "Hospitali yaImam Hussein".

Lakini mpango mkubwa na muhimu sana wa Allamah Askari ulikuwa ni kuanzishashule ya theolojia huko Baghdad mwaka 1384 A.H. ili kuanzisha chuo kikuu kikub-wa zaidi cha Kiislam chenye masomo yote ya taaluma.

Baada ya kutokeza kwa chama cha Baath, ambao ni makafir (wasioamini) nautawala wake juu ya mambo ya Iraqi, Allamah Askari chini ya uongozi wa AyatullahHakim (R.A) na wafuasi wengine walionyesha upinzani wao kwa huo utawala wa

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

7

Baath. Matokeo yake, chama cha Baath kilitoa amri ya kukamatwa kwa AllamahAskari na ilimbidi aondoke Iraqi mwaka 1389 A.H. na kwenda Lebanon. Hii nchi yabaadae, pamoja na viongozi wengine wa kidini kama Sayyed Musa Sadr, mkuu waBunge Kuu la Kiislamu la Shi'ah, Muhammad Hussein Fazlullah na SheikhMuhammad Mahdi Shams Al-Din waliendeleza upinzani wao dhidi ya utawala waIraqi. Lakini alipogundua kwamba nia ya utawala wa Iraqi ilikuwa ni kumkamata aukumteka nyara huko Lebanon, aliondoka nchini humo na akarudi Iran.

Siku hizi, Allamah Askari, bila ya kujali umri wake wa uzee, anajitolea muda wakemwingi kushughulika na upeo mpana wa uandishi wake. Mengi ya maandishi yakehayajachapishwa bado na yeye (kama inavyotegemewa) bado anakerwa namatukio ya sasa hivi na anaweka juhudi zake zote bila unyimi kutetea dini yaUislamu na kupeperusha bendera tukufu ya Uislamu kwenye nchi zote zaKiislamu.

Huko Iran, Allamah Askari alitumia muda wake mwingi kusoma, kuendesha uchun-guzi na kuchapisha vitabu. Pia, alifanikisha huduma mbalimbali za kijamii na kiu-tamaduni zikiwemo:

a) Kuanzishwa kwa Baraza la Kisayansi la Kiislamu mwaka 1398 A.H.b) Kuchapishwa kwa vitabu vya kiada vitakavyo fundishwa katika Hauza za kidi-

ni. Miongoni mwa vitabu hivi mtu anaweza kurejea:

i. Ta'alim Al-Lugha til arabiyyah (jinsi ya kufundisha lugha ya Kiarabu).ii. Al-Amthila wa Sarf Mir.iii. Al-Tassrif.iv. Al-Hidayah Fi Al-Nahaw.v. Qhawa'id Al-Imlah.vi. Tahdhib Al-Balaghah.vii. Al-Mantiq wa Manahij - Al-Bahth Al-Ilmi.viii.Tahdhib Sharh Ibn Aqil (cha kuchapishwa).ix. Tahdhib Al-Mughni.x. Muntakhab Hiliat Al-Mutaqin.xi. Al-Manhad Al-Muqtarrah Lisanawat Al-Arba

(Mpango uliokusudiwa wa masomo ya kufundishwa kwa miaka minne)

Majina ya vitabu vilivyochapishwa na Allamah Askari. Uchapishaji wake ni kamahivi hapa chini.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

8

* Utafiti juu ya Qur'ani Tukufu - katika juzuu 3.

1) Qur'ani Tukufu wakati wa utume wa Mtukufu Mtume Muhammad

(s.a.w.) na baada ya utume wake.

2) Qur'ani Tukufu na ngano za kidini ( chategemea kuchapishwa)

3) Qur'ani Tukufu na simulizi za Ahlu'l-Bayt [kizazi kitukufu cha Mtukufu

Mtume (s.a.w.)] - chategemea kuchapishwa.

*Utafiti katika theolojia ya Kiislam (kufundisha Uislamu).

1. Kufundisha Uislamu (kimechapishwa).2. Maadili na kanuni za Kiislamu (kimechapishwa).3. Muntakhab Al-Adiyah (dua zilizoteuliwa) - kimechapishwa.4. Sheria katika Uislamu (cha subiri kuchapishwa).5. Siasa katika Uislamu juu ya amri za kiserikali (cha subiri

kuchapishwa).6. Maoni ya Uislamu ndani ya Qur'ani Tukufu, juzuu tatu.

i) Maoni ya Kiislamu toka siku ya kwanza ya kuumbwa hadi Qiyamah(kimechapishwa).

ii) Tabia na mwenendo wa Mitume na Maimamu (cha subiri kuchapish-wa)

iii) Sheria za mwisho za kidini ( za kuchapishwa).

*Ma'alim al-Madrassatayn (kigezo cha madhehebu mbili) katika juzuu nne.

1) Utafiti na uchunguzi wa madhehebu mbili (makatib) juu ya masahabawa Mtume na Maimam (a.s.)

2) Utafiti na uchunguzi wa madhehebu mbili juu ya Rasilimali ya Sheriaza Dini ya Kiislam (kimechapishwa).

3) Athari za kusimama kwa Imam Hussein katika kuhuisha sunnah zaMtukufu Mtume (kimechapishwa)

4) Maendeleo ya fikra za madhehebu mbili na makabiliano yao na maka-

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

9

bila ya Mongoli na shutuma zao kwa kizazi kitukufu cha Mtume tokakarne ya 2 A.H. mpaka karne ya 12 A.H. (kitachapishwa)

*Ensaiklopidia ya uchunguzi ili kutakasa sunnah ya Mtume kutokana nangano potovu zilizohusishwa kwake:

i) Ngano (simulizi) za Ummul-Mu'minin (Ayisha) - sehemu za maishayake, juzuu ya1 (kimechapishwa).

ii) Ngano za Ummul-Mu'minin (Ayisha) - uchunguzi wa simulizi zake,juzuu ya 2 (cha tegemewa kuchapishwa).

iii) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 1(kimechapishwa).iv) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 2(kimechapishwa).v) Abdullah Ibn Saba na ngano nyinginezo, juz. 3( kuchapishwa).vi) Masahaba mia na hamsini wa uwongo kama Ghamim,

juz.1(kimechapishwa).

viii) Masahaba mia na hamsini wa uwongo pamoja na wa makabila

mwengine, juz. 3(cha kuchapishwa). ix) Wasimuliaji wasio Sahihi (cha kuchapishwa). x) Aina mbalimbali za uwongo na waongo (cha kuchapishwa).xi) Ngano za Wayahudi na ngano za wakana-mungu na wapiga chuku

(cha kuchapishwa).xii) Baadhi ya sifa na tabia za Mtume (s.a.w.) na kizazi chake kitukufu.xiii) Wasifu wa wale masahaba ambao walimuona Mtume (s.a.w.) na

kupokea toka kwake (cha kuchapishwa)xiv) Wasifu wa wale masahaba waliomuona Mtume(s.a.w.) lakini

hawakupokea toka kwake (cha kuchapishwa)xv) Wasifu wa wale masahaba ambao hawakumuona Mtume(s.a.w.) na

hawakupokea toka kwake (kuchapisha).

*Mfululizo wa vitabu vilivyoandikwa kwa Kifursi kuhusu dhima ya Maimam(A.S.) katika kuhifadhi mafundisho ya Uislam:

1. Istilahi za Kiislam (kimetafsiriwa kwa Kiarabu)2-7 Ni kuhusu mambo muhimu kabla na baada ya Uislam.8. Mtazamo mfupi kuhusu tabia na mwenendo wa Mtukufu Mtume

(s.a.w.w.) katika jamii za Waarabu kabla ya Uislam

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

10

9. Sunnah baada ya Mtume(s.a.w.).10) Madhehebu za Kiislam.11) Uimam (uongozi) kwa mtazamo wa madhehebu mbili: amri za Mtume

(s.a.w.), watekelezaji na viongozi na walinzi wa Uislam.12) Imani katika Tawhid (upweke wa Allah) kwa mtazamo wa madhehe-

bu mbili.13) Maelezo ya kanuni mbalimbali za Kiislam.14) Wajibu wa Imam katika kuhuisha Sunnah.

MAONI YA DR. HAMID HAFNI DAWOOD,PROFESA WA LUGHA YA KIARABU KATIKA CHUO KIKUU CHA CAIRO.

UKWELI NYUMA YA UWONGO

Kumbukumbu ya kuzaliwa Uislam ya 1300 imekwisha sherehekewa. Katika wakatihuu baadhi ya waandishi wetu wasomi wamewashutumu Mashi'ah eti kwakutokuwa na maoni ya Kiislam. Waandishi hao walivutia maoni ya watu dhidi yaShi'ah na wakasababisha hitilafu kubwa miongoni mwa Waislam. Badala yabusara na elimu, maadui wa Shi'ah walifuata imani na upendeleo wao wenyewewaliouchagua, kuufunika ukweli, na kuwashutumu Mashi'ah eti kuwa ni wenyeitikadi za kidhana n.k. Hivyo Elimu ya Kiislam ilipata taabu sana, kwa kuwa maoniya Shi'ah yalikandamizwa sana.

Kwa matokeo ya shutuma hizi, kupotea kwa Elimu ya Kiislam kulikuwa kukubwakuliko hasara waliyoipata Mashi'ah wenyewe kwa sababu chanzo cha maarifahaya ya sheria, ingawa ni kitajiri na chenye manufaa, kilitelekezwa, ikaishiakwenye kuwa na elimu finyu.

Lakini! Huko nyuma watu wetu waliosoma walidhuriwa, vinginevyo tungewezakunufaika kutokana na maoni mengi ya Ki-Shia. Yeyote anayetaka kufanya utafitikatika maarifa ya sheria ya Kiislam lazima aangalie rejea za Ki-Shia na zile zaSunni vilevile.

Hakua Imam wa Ki-Shia Jafar al-Sadiq (aliyefariki mwaka 148 H.L), mwalimu waMaimam wawili wa Ki-Sunni? yaani Abu Hanifah al-Nu'man Ibn al-Thabit (aliyek-ufa mwaka 150 H.L.) na Abu 'Abdullah Malik Ibn Anas (aliyekufa mwaka 179 H.L.).

Abu Hanifah alisema, "Bila ya ile miaka miwili Nu'man angeangamia," akiashiria ilemiaka miwili aliyonufaika kutokana na elimu ya al-Imam Jafar as-Sadiq.

Malik pia alikiri wazi wazi kabisa, kwamba hajakutana na mtu yeyote aliyebobea

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

11

sana katika maarifa ya sheria ya Kiislam zaidi ya al-Imam Jafar as-Sadiq.

Bado watu wasomi kama hao, kwa bahati mbaya walizidharau taratibu za utafitikwa kunufaisha malengo yao. Hivyo elimu haikufunuliwa kwao kikamilifu, na wal-isababisha tofauti kubwa kati ya Waislam. Ahmed Amin alikuwa mmoja wa walewalionyimwa mwanga wa elimu, wakabakia katika giza, ingawa hata hivyo mshu-maa wa Ushia ulikuwa ukiwaka daima na hakukuwa na mwanga mwingineo.

Historia imelinakili doa hili katika joho la Ahmad Amin na marafiki zake, ambao wal-ifuata kwa upofu madhehebu moja maalum. Katika makosa mengi yaliyofanywa nayeye, kubwa kabisa linaelezwa katika ngano ya 'Abdullah Ibn Saba'. Hii ni moja yasimulizi zinazosimuliwa ili kuwashutumu Mashia kwa uasi (wa kidini) na matukioyaliyopita.

Mtafiti mashuhuri wa kisasa, mstahiki Sayid Murtadha al-Askari, katika kitabuchake amethibitisha kwa ushahidi thabiti, kwamba 'Abdullah Ibn Saba' alikuwa niwa kubuni, na kwa hiyo ni uongo mkubwa kusema yeye alikuwa ndiye mwanzilishiwa Ushia.

Sayyid Murtadha al-Askari ameshughulika sana katika historia na amethibitishakutokana na rejea za Kisunni kwamba maadui wa Mashia ni wa uongo.

Tangu siku za mwanzoni za Uislam hadi sasa, ngano kama zile za kuhusu'Abdullah Ibn Saba' zilizoelezwa na Seif Ibn Umar, ziliaminika kama zilitokakwenye vyanzo vya uhakika, lakini katika kitabu hiki, utafiti mkubwa sana ume-fanywa kuhusu ngano hizi, ili kuwezesha kupatikana kwa ukweli juu yao.

Mwenyezi Mungu ameagiza kwamba watu waliosoma waufichue ukweli bila yakujali lawama wanazoweza kupata. Mtangulizi katika nyanja hii ni mstahiki mtunziwa kitabu hiki,ambaye amewafanya wasomi watafiti wa Kisunni kukipitia kitabucha historia cha Tabari,(Historia ya Mataifa na Wafalme) na kuchekecha zile nganosahihi kutoka zile za uongo. Ngano ambazo zilibakia bila kubadilishwa nakugeuzwa kwa karne kama Maneno ya Mwenyezi Mungu.

Mwandishi mstahiki huyu, kwa ushahidi mwingi, ameuondoa utando au utata kuto-ka kwenye matukio yale ya kihistoria, na kwa njia bora kabisa akaufichua ukweli,kwa kiasi ambacho baadhi ya mambo yanaonekana yakushitusha. Bila shaka,baadhi yao yanaonekana kushangaza, kwani yanapingana na imani ya kipindi chauhai wa mtu, na urithi wetu wa kidini - kwa umri wa karne nyingi. Lakini tunapaswakuutii ukweli hata kwa kuonekana ugumu kiasi gani. "Haki ni bora ifuatwe"

Ili kujua yote inahusu nini, mtu inambidi kusoma kitabu hiki na kuchunguza kwamakini matukio ambayo kwamba kuna maoni tofauti; kama vile:

"Jeshi la Usama.""Kifo cha Mtukufu Mtume""Ngano ya Saqifah"

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

12

Yote ambayo yamechunguzwa na mwandishi.

Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokaribia kufa, baadhi ya watu waliondokakwenye Jeshi la Usama bila ruksa, na wakarudi Madina kwa matumaini ya kupatakazi za nyadhifa. Mwandishi anawatambulisha watu hawa kwetu. Akiwa kwenyekitanda cha mauti yake, Mtume alitaka kufanya wosia lakini watu wengine waka-puuza haja hii, na wakaiita "kuweweseka kwa mtu anayekufa". Penginewalikuwa wanahofia uwezekano wa kumtambulisha kwake al-Imam Ali kama mshi-ka makamu wake.

Mwandishi anaufichua ukweli kuhusu matukio haya. Ni nini Umar alikuwa nachokichwani mwake kukataa kifo cha Mtukufu Mtume? Kwa nini alikuwa anawatishiakuwaua wale waliokuwa wakieneza habari za kifo cha Mtume?

Wakati al-Imam Ali, binamu yake Mtume, ami yake Abbas na watu wazimawanaosha mwili wa Mtukufu Mtume, Umar na Abu Ubeydah kwa haraka sanawakaja Saqifah (chumba chenye baraza yenye paa) na kuwataka watu watoekiapo chao kwa Abu Bakr. Ambapo kama wangengojea mpaka mazishi ya Mtumeyakaisha, Ali ndiye mtarajiwa pekee wa ushika makamu wa Mtume, na BaniHashim hawakumjua mtu mwingine.

Mtunzi, chini ya vichwa vya habari vitatu hivi vilivyotajwa kabla, ameuchuja ukwelikutokana na uongo, wema kutokana na ubaya, mpaka ameufikia ukweli uliodhahiri; na kwa sababu ya utafiti wake, milango ya ulaghai na udanganyifu ime-fungwa daima kwa wala njama.

Masomo mengine katika kitabu hiki yanaonyesha ukweli kwa uwazi kabisa, kwam-ba hivi karibuni, mabadiliko makubwa katika historia ya Uislam yatatokea.

Ningependa kuweka maswali matatu kwa wasomaji kabla sijamalizia makalayangu:

1. Je hivi sahaba wa karibu wa Mtume anaweza kufanya kosa?2. Je tunaweza kukosoa kazi yake?3. Je, tunaweza kusema kwamba sahaba mtukufu wa Mtume ni mnafiki au

asiyeamini (kafir)?

Majibu kwa maswali mawili ya kwanza ni dhahiri, lakini jibu kwa la tatu liko kinyume- siyo kwa sababu nina chuki na ninasema kitu kilicho kinyume na mantiki - -lahasha, ninayo sababu ya msingi na ya kimantiki, kwani kutoamini na unafiki kuna-toka moyoni, na hakuna yeyote ila Allah (swt) anayejua yaliyomo kwenye mioyoyetu na siri za wanadamu. Ninafurahi kutoa heshima kubwa kwa kitabu hiki namtunzi wake mstahika, mtafiti aliyebobea Sayyid Murtadha Askari. Nimeridhishwapia na Bw. Murtadha Rizvi Kashmir (mchapishaji) ambaye amekitoa kitabu hikikatika sura ya kupendeza, ametimiza wajibu wake, huduma kwa Uislam. Jukumuhili litabeba uzito zaidi katika kuhuisha historia halali ya Kiislam.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

13

Dr. Hamid Hafni Dawood12thOctober,1961Cairo - Misri.

Makala hiyo hapo juu imeandikwa na mwanachuoni wa Kisunni, ambaye ameuka-ta mzizi wa ushabiki na kugombana kwa nia tu ya kuzozana.

MAONI YASHEIKH MAHMOOD ABU RIYYA

Profesa Sheikh Murtadha Al - Askari, Najaf, Iraq

Utukufu na amani ya Allah uwe juu yako

Hivi karibuni kulikuwa na mjadala miongoni mwa kikundi cha wanazuoni waKiislam juu ya mada tofauti, yakiwemo maandishi yenye maana ya wanasayansina watunzi ambayo ni yenye faida kwa Waislam. Mmoja wa washiriki alikitajakitabu chenye thamani "Abdullah Ibn Saba" ulichoandika wewe na ambacho ndaniyake umezungumzia bayana kwa mara ya kwanza kuhusu baadhi ya mambomapya na ambayo ndiyo maana nimeshawishika sana kujifunza zaidi kuhusukitabu hicho na nikategemea kupata nakala moja kwa moja kutoka kwako. Bilashaka nitakuwa na deni kwako, ikiwa utaweza kunitumia nakala. Naomba nitan-gulize shukurani zangu za dhati Amani na Utukufu wa Allah uwe juu yako.

Mahmood Abu RiyyaMisri, Jimbo la Al-KhabirahRajab 20, 1380 HijiriaJune 11, 1960.

Mmoja wa Ulamaa wa Misri Bwana Abu-Riyya ametuma barua ifuatayo kwaAllamah Sayyed Murtadha Al-Askari na kuomba nakala ya ya kitabu chaAbdullah Ibn Saba.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

14

Mpendwa Profesa Murtadha Al-Askari

Amani na Utukufu wa Allah na Rehma Zake ziwe juu yako.

Ningependa kuchukua nafasi hii kusema maneno kidogo juu ya kitabu chako"Abdullah Ibn Saba." Nimekisoma mara moja na ninakusudia kukisoma tena hivikaribuni. Ngoja niseme kwamba umetumia mtazamo mpya na wa kitaalam juu ya suala hilikatika utafiti na mijadala yako, ambao haujatumiwa na mtu mwingine yeyote kabla.Nakupongeza kwa uaminifu na kwa dhati kweli kweli, kwani Allah amekujaaliawasaa wa kufuatilia mjadala huu na amekuongoza kufichua mambo ambayo haku-na mwingine aliyeyazungumzia katika karne 14 zilizopita.

Matokeo ya utafiti wako yanathibitisha ubishi wa mwanasayansi wa Kizungu,Wales, aliyesema, "Historia moja kwa moja ni mwandamano wa uongo." Kwabahati mbaya inaoana na historia ya Uislam iliyoandikwa kwa shauku ya chuki naubaguzi kwa nyakati tofauti. Hii ni kweli kwa kiwango fulani kwamba inaletaumuhimu sasa wa kuanza uchunguzi wa historia wa makusudi na wa kina.

Hasa, kitabu chako "Abdullah Ibn Saba" ndiyo chanzo juhudi kama hiyo ya utafiti.Tumshukuru Allah (swt) kwamba uliipata fursa hii na namuomba Allah (swt) akupenguvu na moyo wa kuendelea katika njia hii bila woga, kufichua mambo bila kusi-ta, na akuongoze katika kutumia kipaji na fasaha yako katika mijadala yako nakuomba kwamba wasomaji wako nao wafanye vivyo hivyo katika kulifahamu hilojambo, hasa kuhusu Abu Bakr na Umar kwa vile hatuwezi siku zote kustahimiliukweli wa wazi.

Kwa kufunga, naomba nizitume salamu zangu za kweli kwako. Utukufu na Neemaza Allah (swt) ziwe juu yako.

Wako wa kweli,

Mahmood Abu RiyyahMisri, Jimbo la Al-KhabirahRajab 20, 1380 Hijiria - 1961.

Baada ya kupokea na kukisoma kitabu alituma barua ifuatayo kwa Ayatullah Al-Askari na Kuthibitisha yale yaliyokuwemo ndani ya kitabu hicho.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

15

MAONI YA AL - SHEIKH JAWAD MUGHNIYYAH(MWANACHUONI WA KISHIAH)

"Kila kitu katika dunia hii kinabadilika isipokuwa maandishi dhidi ya Shiah. Kwa kilamwanzo una mwisho, isipokuwa shutuma dhidi ya Mashiah. Kila hukumu inaung-wa na ushahidi, isipokuwa hukumu dhidi ya Shiah. Kwa nini? Kwani Mashiah niwakorofi au wachochezi wenye vurugu ambao wanapenda tu kuwavuruga watu?"Jibu hili hapa.

Katika Karne ya Pili ya Enzi ya Uislam (H.L.), aliishi mtu aliyeitwa Seif Ibn Umarat-Tamimi. Aliandika vitabu viwili:

1. al-Fatuh wal Reddah.2. al-Jamal wal Masiiri Ayishah wa Ali.

Alifanyia kazi malengo mawili katika vitabu vyake viwili:

1. Kubuni ngano bila msingi.2. Kunukuu matukio katika njia ambayo kwamba ukweli ulionekana kama

uongo, na uongo ukaonekana kama ukweli.

Alibuni Masahaba kwa ajili ya Mtume kama vile Suiir, Hazhaaz, Ott,Humaiza n.k. Alinukuu ngano zake kwa namna ambayo zilionekanakama zimesimuliwa na watu ambao walikutana na masahaba hawa.

Miongoni mwa mashujaa wake wa kubuni ni 'Abdullah Ibn Saba', ambaye anad-haniwa kuwahi kusimulia hadithi kuhusu Mashia; ngano zote dhidi ya Mashia zili-zoandikwa na wana historia zimetokana na Seif. Baada ya Seif, wana historiawalivikubali vitabu vyake kama vya kweli tupu.

Tabari alikuwa mwanahistoria wa kwanza aliyetegemea vitabu vya Seif.

Wanahistoria wengine, Ibn Athir na Ibn Asakir, miongoni mwao, walimfuata Tabarikiupofu. Seif alibuni ngano na akachanganya matukio sahihi lakini chanzo pekeecha ngano zake zote ni vitabu vyake mwenyewe 'al-Fatuh' na 'al-Jamal

Hiki kitabu 'Abdullah Ibn Saba' kinathibitisha kwamba maelezo hayo hapo juu ni yakweli na kazi ya mtunzi wake mwenye elimu, ni kuonyesha ukweli kamaulivyokuwa, bila ya kuuharibu kwa kuupamba sana. Hakuna hata mtu mmojamwenye elimu anayeweza kukataa, au kushuku chochote kile ambacho SayyidMurtadha al-Askari ameandika kwa sababu kitabu chenyewe kinatokana naushahidi wa kimantiki na hakuna anayeweza kukataa mantiki na usemi wa dhahiri.

Nimekijadili 'Abdullah Ibn Saba' na watu wengi, lakini nimewajibu kama wasomiwaliopita walivyofanya, isipokuwa kwamba nimefanya rahisi kwao kuelewa, kwam-ba, niliamini kuwepo kwa 'Abdullah Ibn Saba'. Sasa, msomi mzuri sana Sayyid

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

16

Murtadha al-Askari, ameibadili kabisa ngano hiyo, na akathibitisha kwamba'Abdullah Ibn Saba' ni wa kubuni. Ninaweza kusema kwamba hiki ni kitabu chakwanza cha Kiarabu kilichochunguza historia kisayansi.

Mtunzi amefanya huduma kubwa siyo tu kwa ajili ya dini, elimu na Ushia, bali kwaUislam. Ameufunga mlango kwa wale ambao walitaka kuuvuruga umoja waWaislam, na kwa wale Sunni wanaopata ujasiri kutokana na ngano zao za uongo.Leo ushahidi wao wa kwanza na wa pekee, ngano za Ibn Saba na Ibn Sauda zili-zobuniwa na Seif zimethibitishwa kuwa ni za uongo.

Mohammed Jawad MughniyyahLebanon.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

17

MAONI YA PROFESA JAMES ROBINSOND. Ltt., D. D. Glasgow, U. K.

Mpendwa Sayyid Murtadha al-Askari,

Ilikuwa ni katikati ya mwezi wa Agosti iliyopita nilipopokea kutoka kwako nakala zavitabu vyako viwili, 'Abdullah Ibn Saba' wa Asatir Ukhra, na Khamsun wa-mi'aSahabi Mukhtalq, al-Qasim al-Awwal. Wakati nilipokuandikia napenda nisemekwamba sasa ni mzee na siko mwenye afya njema, kwa hiyo, nitahitaji muda wakuvipitia vitabu hivi. Imenichukua mudu mrefu kuliko nilivyotegemea; lakini nimevi-soma vitabu hivi mara mbili kwa shauku kubwa, na ingawa ningependa kuandikakwa kirefu kiasi, nahisi ni lazima niandike kuelezea kufurahishwa kwangu na njiailiyochukuliwa na utaalam makini ulioonyeshwa katika vitabu viwili hivi. Kwa umriwangu siwezi kutazamia kwa kujiamini kuwa na uwezo wa kuandika na hivyonaona nisichelewe zaidi nisijejikuta sina uwezo tena wa kuandika.

Katika kitabu cha kwanza nimependa yale maelezo ya kina ya ngano ya jadi ya'Abdullah Ibn Saba' na Sabaiyyah (wafuasi wa Ibn Saba), ikifuatiwa na mjadalamzito wa waandishi (wa zamani na wa sasa) huko Mashariki na Magharibi namielekeo ambayo waliitegemea. Ile jedwali iliyoko ukurasa wa 43 ni yenye msaa-da sana katika kuonyesha vyanzo vikuu vya habari kuhusu Seif na ngano zake najinsi waandishi wa baadae walivyotegemea juu ya moja au nyingine kati ya hizi.

Kisha inakuja orodha ya baadhi ya waandishi waliotoa maoni yao juu ya tathminiya ngano za Seif, kutoka kwa Abu Dawud (kafa 275 - maandishi yanasema 316kimakosa) kwa Ibn Hajar (kafa. 852 ). Kama wote wanavyozungumza kwakukosoa, kwa kutumia maneno kama "dhaifu", "ngano zake zimeachwa," "Hainathamani", "Muongo", "Anashukiwa kuwa Zandiki" n.k. Wanakubaliana katikakuthibitisha huko kutokuaminika, au hata uongo wa ngano hizo. Hii ni hoja nzitokabisa. Katika kuchunguza maoni ya waandishi juu ya wasimuliaji mbali mbali,nimegundua kwamba wote hawakubaliani. Lakini hapa hakuna kutokukubalianaambako kunamfanya mtu ashangae kwa ninni waandishi wa baadae wamekuwatayari hivyo kukubali taarifa za Seif.

Lakini ningependa kutoa maoni juu ya Tabari ambaye hana wasiwasi katika kum-nukuu Seif. Historia yake (kitabu chake), siyo kitabu cha historia kwa namna yauandishi wa kisasa, kwani lengo lake kuu linaonekana lilikuwa ni kuandika habarizote alizokuwa nazo bila kulazimika kutoa maoni juu ya tathmini yake. Mtu, kwahiyo, yuko tayari kuona kwamba baadhi ya taarifa zake siyo za kuaminika kulikonyingine. Hivyo, pengine tunaweza kumsamehe kwa kutumia njia ambayohaikubaliki siku hizi. Ametoa angalau lundo la habari. Inabakia kwa wanazuoniwatambuzi kama wewe mwenyewe kupambanua kati ya kweli na batili. Katikakujadili idadi fulani ya mambo yaliyotajwa na Seif, hoja hiyo inaendeshwa katikanamna inayofaa, kwanza kutoa maelezo ya Seif na kisha kuyalinganisha na

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

18

maelezo yaliyotolewa na wengine. Ulinganishaji huu makini unashughulika navyote, habari zenyewe na sanadi, na inaonyeshwa kwamba Seif mara nyingiananukuu watu wasiojulikana. Hii inaleta swali kwamba kwa nini hata mmoja waoasinukuliwe na wasimuliaji wengine, na inamuongoza zaidi mtu kufikiria kwambaSeif amewabuni. Shutuma hii kali ni dhana ya maana kwa kumlinganisha Seif nawengine.

Imeonyeshwa kwamba Seif anazo ngano zenye kutokea kwa maajabu ambazo nivigumu kuziamini, kama vile mchanga wa jangwani kuwa maji kwa ajili ya majeshiya Waislam, bahari zigeuke kuwa mchanga, ng'ombe wanazungumza na kuwajul-isha Waislam walipokuwa wamefichwa, n.k. Katika wakati wa Seif ilikuwainawezekana kwake kufanikiwa kutengeneza ngano na historia kama hizo, lakiniwakati huu mwanafunzi makini kwa kawaida huziona ngano kama hizo hazi-wezekani kabisa. Hoja zenye nguvu pia hutumika kuonyesha jinsi habari za Seifkuhusu Ibn Saba na hao Sabaiyya siyo za kuaminika kabisa.

Mwandishi anadokeza kwamba baadhi ya mutashirki wameegemeza uchunguziwao juu ya taarifa za Seif, mambo kama ile idadi kubwa ya watu waliouawakwenye vita vya awali vya Waislam, wazo la kwamba Myahudi asiyejulikana,Abdullah Ibn Saba, yangeweza kuwa kishawishi cha kuwapotosha Masahaba waMtume kutoka kwenye imani yao, na kimekuwa kishawishi kikuu katikakuwaamsha watu kuasi dhidi ya Uthman na kusababisha kifo chake, nakuchochea mapigano yaliyofanywa na Ali pamoja na Talha na Zubayr. Hii inawezakuwa kweli kwa baadhi, lakini haikuwa kweli kwa wote. Hili ni dhahiri kutokana namakala kuhusu Abdallah Ibn Saba katika chapa ya kwanza na ya pili zaEnsaiklopidia ya Uislam. Seif alitumia muda mwingi kutengeneza mashujaa kuto-ka Tamim, kabila ambalo Seif alifuatilizia nasaba yake, lakini Sir William Muirzamani sana alieleza jinsi Tamim walivyokuwa wasalimu amri kwa majeshi yaUkhalifa wa awali katika wakati wa kile kinachoitwa kuritadi. Sir Thomas Arnoldanaweza kuonekana akivuta nadhari kwenye ukweli kwamba ule ushindi wamanzo haukuwa hazikuwa hasa kwa madhumuni ya kueneza imani, kwa ajili yakupanua eneo la utawala wa Waislam.

Katika kitabu cha pili inavutwa nadhari kwenye ukweli kwamba Seif ambaye aliishikatika robo ya kwanza ya karne ya pili ni wa Tamim, moja ya makabila ya Mudarambao waliishi Kufa (Iraq). Hii inamsaidia mtu kuchunguza mwelekeo wake naathari zinazopelekea kwenye hekaya hii. Kuna mjadala wa Dini ya zamani yawaajemi. Moyo na ushabiki wa chama unasemekana kuendelea kutoka wakati waMtume, mpaka ule wa Bani Abbas. Seif alitetea makabila ya kaskazini, akibunimashujaa, washairi wanaosifu hao mashujaa wa makabila, masahaba wa Mtumekutoka kabila la Tamim, vita na mapigano yasiyo na ukweli, mamilioni waliouawana idadi kubwa ya mateka kwa nia ya kuwatukuza hao mashujaa aliowabuni.Mashairi yaliyohusishwa na kwa mashujaa wa kubuni yalikuwa ya kuwatukuzamakabila ya Mudar, kisha Tamim, kisha Ibn 'Amr, kabila dogo Seif alilofuatilizia asili

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

19

yake. Seif aliwataja watu wa Mudar kama viongozi wa vita ambavyo viliongozwana watu wa makabila mengine, viongozi wake wa uongo wakati mwingine wakiwawatu wa kweli, wakati mwingine majina yalitokana na ubunifu wake. Inasemekanakwamba udanganyifu wa habari zake ulikuwa kwa sehemu fulani wa kugeuzaimani ya wengi na sehemu fulani kuwapa wasiokuwa Waislam dhana potofu.Alikuwa fundi sana katika udanganyifu wake kiasi kwamba ulionekana kama his-toria halali.

Huu ni mukhtasari mfupi wa uongo ambao kwamba Seif alikuwa na hatia. Sehemukuu ya kitabu inaelezea kwa kirefu kuhusu watu ishirini na watatu, wakitoa mifanoya maandishi ya Seif na kuonyesha jinsi alivyotofautiana na waandishi halali siyotu katika habari bali pia katika sanadi kwa kutumia majina ya watu ambao hawapo.Kazi hiyo imefanywa kwa maelezo makubwa ikitoa hoja nyingi mno dhidi ya tege-meo la Seif mbali na waandishi mashuhuri wanaoweka habari katika maandishiyao. Vitabu viwili vya Seif vinachunguzwa kuonyesha kwamba siyo vya kutege-mewa kama maandishi mengine ambayo watunzi wa baadae wamenukuu kutokakwake.

Huu ni uchunguzi unopenyeza sana uliofanywa kwa utambuzi makini na ukosoajiwa hali ya juu sana. Ninashukuru sana kwa kuweza kupata fursa ya kutumia mudamwingi wa kutosha kuchunguza hoja ambazo zinanivutia kama zenye kuridhishasana, na nina hakika kwamba wote wanaochunguza vitabu hivi kwa uwazi wa fikrawatakuwa tayari kuthamini nguvu ya hoja hizo.

Pamoja na shukrani nyingi sana kwa kunitumia vitabu hivi, na ninaomba samahanikwa, kutokana na umri wangu pamoja na udhaifu mwingine kwa sababu ya uzee,kuchukua muda mrefu katika kukujibu.

Wako mwaminifu,

James Robinson.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

20

UTANGULIZINGANO YA 'ABDULLAH IBN SABA'

Wanahistoria wanasema kwamba Myahudi anayeitwa 'Abdullah Ibn Saba' alibadil-ishwa kuwa Mwislamu katika wakati wa Khalifa Uthman, ili kutimiza malengo yakekwa amani kwa kufanya maadui ndani ya Ummah wa Kiislam.

Huyu 'Abdullah Ibn Saba alieneza mawazo yafuatayo miongoni mwa Waislam.

a) Kufufuka kwa Mtume.b) Mitume wote walikuwa na warithi - mrithi wa Mtume Muhammad ni Ali,

binamu yake na mkwewe. Amenyan'ganywa cheo chake kitukufu nakhalifa Uthman, na kwa hiyo ni muhimu kuasi dhidi ya Uthman kwafadhila ya Ali.

Abdullah Ibn Saba aliunda kundi lililoitwa Sabaia (wafuasi wake Ibn Saba), nakundi hili liliasi na kumuua Uthman, khalifa wa tatu. Pia walifanya fitna kati yamajeshi ya Ali na Talha, adui yake, wakati makubaliano ya amani yalikuwayakitegemewa katika Vita vya Jamal karibu na Basra. Hawa Sabaia ambaowalikuwa wameandikishwa kwenye majeshi yote, walianza kurusha mishalemapema asubuhi moja bila kungojea amri yoyote kutoka kwa amirijeshi, na hivyowaliianzisha vita. Kwa hiyo, Myahudi huyu alikuwa ndiyo chanzo hasa cha fitinahizi na vita miongoni mwa Waislam, na ndiye mtu aliyeeneza wazo la kufufuka kwaMtume Muhammad, na wazo la Ali kuwa mrithi wa Mtume miongoni mwa Waislam.

ASILI YA NGANO YENYEWE

Kisa cha 'Abdullah Ibn Saba' kina zaidi ya karne kumi na mbili sasa. Wana-histo-ria na waandishi, mmoja baada ya mwingine wakakiandika, na kuongeza zaidi nazaidi juu yake.

Wanahistoria wote wanakubali kwamba ngano hii ilisimuliwa kwanza kabisa naSeif. Wana-historia wafuatao waliinukuu moja kwa moja kutoka kwa Seif:

1) Tabari.2) Dhahabi - aliisimulia pia kutoka kwa Tabari.3) Ibn Abi Bakr - amenukuu pia kutoka kwa Ibn Athir 15, ambaye

amenukuu kutoka kwa Tabari.4) Ibn Asakir.

Wafuatao wamenukuu katika mzunguuko (siyo moja kwa moja toka kwa Seif):

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

21

5) Nicholson kutoka kwa Tabari 2.

6) Ensaiklopidia ya Uislam kutoka kwa Tabari 2.

7) Van Floton kutoka kwa Tabari 2.

8) Wellhauzen kutoka kwa Tabari 2.

9) Mirkhand kutoka kwa Tabari 2.

10) Ahmad Amin kutoka kwa Tabari, na kutoka kwa Wellhauzen.

11) Farid Wajdi kutoka kwa Tabari 2.

12) Hassan Ibrahim kutoka kwa Tabari 2.

13) Saeed Afghani kutoka kwa Tabari 2, na kutoka kwa Abi Bakir 3, Ibn

Asakir 4, na Ibn Badran 21.

14) Ibn Khaldoun kutoka kwa Tabari 2.

15) Ibn Athir kutoka kwa Tabari 2.

16) Ibn Kathir kutoka kwa Tabari 2.

17) Donaldson kutoka kwa Nicholson 5, na Ensaklopidia 6.

18) Ghiathud Din kutoka kwa Mirkhand 9.

19) Abulfada kutoka kwa Ibn Athir 15.

20) Rashid Redha kutoka kwa Ibn Athir 15.

21) Ibn Badran kutoka kwa Ibn Asakir 4.

22) Bostan kutoka kwa Ibn Kathir 16.

Orodha hiyo hapo juu inatoa ushahidi kwenye ukweli kwamba ngano ya 'AbdullahIbn Saba' imeanzishwa na Seif na kusimuliwa kwa mara ya pili kutoka kwa Tabari.Kwa hiyo, tabia na historia ya Seif ichunguzwe na kuchambuliwa kwa uangalifumkubwa.

SEIF NI NANI? (WASIFU MFUPI)

Seif Ibn Umar Tamimi aliishi katika karne ya pili ya zama za Uislam (karne ya 8A.D.) na akafa baada ya mwaka 170 A.H. (750A.D.). Aliandika vitabu viwili.

1) al-Futuuh wal Ridhah - ambacho ni historia ya kipindi kabla ya kifo chaMtukufu Mtume mpaka Khalifa wa tatu Uthman alipochukua madaraka kamamtawala wa ulimwengu wa Kiislam.

2) al-Jamal wal Masiiri Ayishah wa Ali - ambacho ni historia toka kuuawa kwaUthman mpaka vita vya Jamal.

Vitabu hivi viwili vimejaa msisimko mwingi kuliko ukweli; baadhi ya ngano za

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

22

kubuni, na baadhi ya matukio ya kweli ambayo, kwa makusudi, yameandikwa kwanamna ya dhihaka.

Kwa vile Seif alizungumza juu ya baadhi ya masahaba wa Mtume, na pia akabunibaadhi, ngano zake zimeathiri historia ya Uislam wa awali. Baadhi ya waandikawasifu kama vile watunzi wa Usudulghabah, Istiab na Isabah na wana-jogorafiakama vile watunzi wa Mujami-ul Buldan na Al-ruwzumi'tar wameandika maisha yabaadhi ya masahaba wa Mtume, na wakataja majina ya sehemu ambazo zimo tukwenye vitabu vilivyoandikwa na Seif. Kwa sababu hii, maisha na tabia ya Seif laz-ima yachunguzwe kwa makini na kwa uangalifu.

Matokeo ya uchunguzi wa maisha ya Seif yanaonyesha kwamba Seif alikuwamkana habari za Mungu na msimuliaji ngano asiyeaminika. Ngano zilizosimuliwana yeye ni zenye mashaka na zote au sehemu zake ni za kubuni. Zifuatazo nibaadhi ya ngano alizosimulia yeye:

1. JESHI LA USAMA:

Mtume aliandaa jeshi la kwenda Syria. Kiongozi wa jeshi hili alikuwa ni Usama.Kabla ya safu ya mwisho haijaondoka mpakani mwa mji wa Madina, MtukufuMtume akafa. Usama akamtuma Umar kupata idhini kutoka kwa Abu Bakr mrithiwa Mtume. Umar pia alibeba ujumbe kutoka kwa baadhi ya Ansari wakishaurikwamba jemedari Usama abadilishwe. Abu Bakr aliusikia ujumbe huo, akaruka, naakamkamata Umar kwenye ndevu zake, akamfedhehesha kwa kusema, "Mtumealimfanya Usama kuwa jemedari, mimi sitambadilisha." Akaamuru kuondoka hara-ka kwa jeshi la Usama na kumlaani Umar akisema, "Msiba uwe juu yako."

Wanahistoria wa wakati huo wameliandika tukio hilo kwa tofauti kabisa.

2. SAQIFA, UKUMBI WA BANI SAIDAH:

Siku ile ile aliyokufa Mtume (s.a.w.), Seif anasema, Muhajirina wote walimuungamkono Abu Bakr kama mrithi wa Mtume, isipokuwa wale walioukataa Uislam.Habari za kuchaguliwa Abu Bakr zilimsisimua sana Ali kiasi kwamba alitoka, akiwaamevaa shati lake tu. Akapeana mikono na Abu Bakr kirafiki na baadae nguo zakezilipoletwa akazivaa, akakaa chini kando ya Abu Bakr. Seif anaendelea, akisemakwamba Abu Bakr alidai kuwa na shetani katika moyo wake na kwamba Waislamlazima wamuangalie, na wamzuie kutenda dhulma kwake.

Seif alisimulia ngano saba za kuhusu Saqifah. Walikuwepo mashujaa watatu kati-ka ngano hizi, wakiwemo miongoni mwao Masahaba wa Mtume. Majina yaohayakutajwa mahali popote isipokuwa kwenye ngano za Seif. Upekee huu unam-fanya mtu kufikiri, na kutilia shaka ukweli wa ngano zenyewe. Wakati vitabu vyakuaminika, vinavyokubaliwa na viongozi wa Sunni vikitazamwa, mkengeuko waSeif toka kwenye ukweli, katika kuandika matukio ya Saqifah, unaweza kuwatayari kugundulika.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

23

KUHUSU UKUMBI WA SAQIFA BANU SAIDAH KWA MUJIBU WA VYANZOSAHIHI

Katika kitanda chake cha umauti, Mtume Muhammad alitaka kuandika wosia.Umar akampinga, na baadae alitoa vitisho dhidi ya watu kama watathubutukueneza habari za kifo cha Mtume mpaka Abu Bakr alipofika. Kisha ghafla Umarakanyamaza. Wakati familia ya Mtume wakihangaika na ibada za mazishi, Kundila Ansari lilikusanyika ndani ya ukumbi kumchagua Sa'd Ibn Ubada kama mrithi waMtume. Umar, Abu Bakr na marafiki zao walikimbilia kwenye ukumbi huo kujiungana mkutano huo. Mwishowe, uchaguzi ulikamilika kwa kuchaguliwa Abu Bakr.Kundi hilo kisha ndipo likaenda Msikitini kutoa kiapo cha utii cha Waislamu wotekwa Abu Bakr. Wakati wote huu mwili wa Mtukufu Mtume ulilazwa ndani ya nyum-ba yake na familia ya Mtume tu na mtu mmoja wa Ansari ndiyo waliokuwepo.

Baada ya kiapo cha utii kwa Abu Bakr katika ukumbi na Msikitini kilipokwisha, watuwalikwenda kwenye nyumba ya Mtume na wakajiunga na sala za mazishi. Mwiliwa Mtume ulilala kwenye kitanda chake cha mauti toka Jumatatu mchana hadiJumanne usiku mazishi yalipofanyika.

Familia ya Mtume tu ndiyo iliyohudhuria mazishi. Al-Imam Ali na Bani Hashim(binamu zake Muhammad), hawakutoa ridhaa ya kuchaguliwa Abu Bakr kamamrithi wa Mtume, na walichukua hifadhi kwenye nyumba ya Fatima, binti yaMtume. Umar alikwenda nyumbani hapo kuwachukua kuwapeleka Msikitini kutoakiapo cha utii kwa Abu Bakr. Lakini walikataa kumuunga mkono Abu Bakr kwakipindi chote cha uhai wa Bibi Fatima. Baada ya miezi sita Ali na Bani Hashim hati-mae wakatoa ridhaa yao na kiapo baada ya kufariki Fatima.

Matukio yote hayo hapo juu, uamuzi juu yao kutoka kwa Ibn Abbas, Abu Dhar,Miqdad, Abu Sufyan, Mu'awiyyah na Umar Ibn Khatab, mukhtasari juu ya maishaya Sa'd Ibn Ubadah katika umri wake wa uzeeni, na ulinganisho baina ya maan-dishi ya Seif na yale ya kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika, yamekusanywakatika kitabu hiki cha sasa. Kinaonyesha jinsi Seif alivyoandika wasifu za masa-haba wa Mtume kuiridhisha serikali ya wakati huo na kufaa maoni ya watu wakawaida. Seif alighushi ili kuunga mkono ushahidi wake na kulinda maoni yake, ilikuidhihaki historia ya Kiislam. Kwa karne nyingi ngano za Seif zilikuwazikionekana kama ndiyo historia ya Uislam. Ni wakati wa kufichua vyanzo vya hizingano za uongo za Seif na watu wa aina yake, ili kuuonyesha Uislam kama ulivyohasa, kwa kujifunza ngano za kweli kuhusu Muhammad, familia yake na masaha-ba. Tusimtetee Seif na simulizi zake, au kuzilinda kwa jina la ngano za Kiislam.Vinginevyo, tutaudhuru Uislam kwa kupinga uenezaji wa ukweli wa Uislam.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

24

DIBAJI

VIPI NA KWA NINI KITABU HIKI KIMEKUJA

Mnamo mwaka 1949(1369H.L.), nilikuta ngano za Uislam zenye mashaka ndaniya vitabu vya historia ya Kiislam. Hizi nilizikusanya kutoka kwenye vyanzo tofauti.Baada ya uchunguzi makini niliridhika kwamba baadhi yao zimezushwa kwamalengo maalum. Kisha nilihisi wajibu wa kutekeleza kuzitangaza. Nilipangamaelezo yangu ili kutengeneza kitabu cha kuitwa ngano za Seif. Msomi mkubwa,mashuhuri ndugu Sheikh Radhi Aali Yasin, mwandishi wa kitabu 'Sulhul Hasan'alinihimiza kuendelea na kazi hiyo, na akanishauri kitabu hicho nikipe jina la'Abdullah Ibn Saba' , na mimi nikakubali kwa furaha sana. Maandishi ya maelezohayo yaliwekwa kwa miaka saba mbali na ndugu zangu wasomi wachache, haku-na aliyeyajua. Nilikuwa na wasiwasi kwamba ningeamsha hisia za watu waMashariki, kwani yalikuwa kuhusu matukio katika wakati wa Mtume mpaka mwaka36H.L. Vitabu vya historia vya miaka hiyo vilikubaliwa kama kweli tupu na bilashaka watu walikuwa na imani juu yao, na walijifunza kutoka humo juu ya wahen-ga wetu wa kale wa Uislam. Mjadala huu unavunja misingi ya kihistoria juu yakeambayo wanahistoria wameegemeza vitabu vyao. Unaonyesha jinsi ganizisivyoaminika baadhi ya ngano za Kiislam, na kukanusha usahihi wa baadhi yavyanzo. Msomaji ataona kwamba mjadala huu haukukomea kwenye ngano za'Abdullah Ibn Saba' tu, bali katika mazungumzo haya, itaonekana kwamba vikovyanzo vingine vingi visivyoaminika.

Kwa sababu hii, nilihofia mpaka nilipogundua kwamba waandishi wengine wawiliwalikwisha jadili (kwa maandishi) baadhi ya sehemu zake. Ndipo nikaanzakuchapisha kitabu changu. Nimetaja tu vile vitabu vilivyokuwa vimeandikwa kablaya mwaka wa 500 H.L.

Murtadha al-AskariBaghdad, 1955 A.D.15 Ramadhan,1375.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

25

NGANO YA ABDULLAH IBN SABA

Kwa miaka elfu moja wana-historia wamekuwa wakiandika ngano za kushangazakuhusu 'Abdullah Ibn Saba' na wafuasi wake - Sabaia

a) Abdullah alikuwa ni nani, na nani walikuwa Sabaia - wafuasi wake?b) 'Abdullah alisema nini, na ni nini alichokifanya?

MUKHTASARI WA KILE KINACHOJULIKANA KUTOKA KWA WANAHISTORIA

Myahudi kutoka Sana'a (Yemen) alijifanya kama aliyesilimu na kuwa Mwislamukatika wakati wa Uthman, Khalifa wa tatu na akapanga njama dhidi ya Uislam naWaislam. Alisafiri nje kwenye miji mikubwa kama: Kufa, Basra, Damascus, naCairo, akihuburi imani ya Kufufuka kwa Mtukufu Mtume Muhammad, kuwa kamakurudi kwa Isa (Yesu) duniani hapa, kabla ya Siku ya Qiyammah. Alihubiri pia wazola unabii, na akadai kwamba al-Imam Ali alikuwa ndiye mrithi wa haki wa MtumeMuhammad akimshutumu Uthman kwa kupora kwa dhulma nafasi ya al-Imam Ali.Aliwasisitiza watu kwa bidii sana kumuua Khalifa Uthman, ambaye baadae ali-uawa.

Wanahistoria walimuita Myahudi huyu, 'Abdullah Ibn Saba' , kama shujaa wangano hizo. Alijulikana kama Ibn Amatus-Sawda, ikiwa na maana ya mtoto wamtumwa wa ki-Negro. 'Abdullah alituma ujumbe wake kwenye miji mingi akijifanyakuhubiri imani ya kweli ya Kiislam kuhimiza mema, na kukataza mabaya, aki-wahimiza watu kuasi dhidi ya magavana wao na hata kuwauwa. Katika orodha yawafuasi wa 'Abdullah Ibn Saba wamo baadhi ya masahaba wema wa MtukufuMtume, kwa mfano, Abu Dhar pia na baadhi ya Tabi'in, kama Malik Ashtar.

Katika wakati wa Imam Ali, watu wawili Talha na Zubair, waliasi dhidi ya Imam Aliwakidai kuadhibiwa kwa wauaji wa Uthman. Kwa sababu ya hili, Vita vya Jamalvikapangwa. Imam Ali na wapinzani wake wawili wakakubaliana kwenye sulhu,lakini baadhi ya Sabaia, yaani wale waliokuwa na hatia ya kumuua Uthman,hawakutaka ugomvi huo usuluhishwe kwa sababu majina yao yalikuwayamefichuliwa. Hivyo, wale Sabaia kwa siri wakajiandikisha kwenye majeshi yote;jeshi la Imam Ali na lile jeshi lililoasi. Wakati wa usiku ambapo kila mtu alikuwaanaota kuhusu ule mkataba wa amani utakaofanyiwa makubaliano siku inayofua-ta, wala njama hawa wakaanza kurusha mishale pande zote. Kama matokeo yahili, Vita vya Jamal vikaanza bila ya ruksa wala kujua kwa ma-amirijeshi wa pandezote mbili.

Kabla ya kujadili ngano ya Abdullah Ibn Saba kwa kirefu, inafaa kuwachunguzawale watu ambao majina yao yamo kwenye orodha ya wa-Sabaia:

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

26

1) Abu Dhar.2) Ammar Ibn Yasir.3) Muhammad Ibn Hudhaifa.4) Abdur-Rahman Adis.5) Muhammad Ibn Abubakr, - mwana wa Khalifa wa kwanza.6) Sa'sa'a Ibn Suhan Abdi.7) Malik Ashtar.

1) Abu Dhar (Jundub Ibn Junadih) Ghifari: Yeye ni mtu wa tatu katika orodha yawatangulizi wanne waliokuwa wa kwanza kuukubali Uislam. Alikuwa Muuminiwa Mungu mmoja hata kabla ya kusilimu kwake. Alitangaza imani yake juu yaUislam huko Makkah katika Msikiti Mtukufu Baitul Haram. Maquraishi wal-imtesa karibu ya kufa lakini aliokoka akaishi, na kwa maagizo ya MtumeMuhammad, alirudi kwenye kabila lake. Baada ya vita vya Badr na Uhud, aliru-di Madina na akaishi hapo mpaka alipokufa Mtume. Kisha Abu Dhar alipelek-wa Sham (Damascus) ambako hakuweza kukubaliana na Mu'awiyah. Baadae,Mu'awiyah alilalamika kuhusu Abu Dhar kwa Uthman, Khalifa wa tatu, nayealimpeleka uhamishoni Abu Dhar kwenda Rabaza ambako baadae alikufa.

Simulizi nyingi zimeandikwa kuhusu Abu Dhar kutoka kwa Mtukufu Mtume. Wakatimmoja alisema: "Chini ya mbingu ya rangi ya samawati, na juu ya ardhi, hakunaaliye mnyoofu na mkweli kuliko Abu Dhar."

2) Ammar Ibn Yasir: Alikuwa akijulikana kama Abuyaqzan. Alikuwa mmoja kati yakabila la Bani Tha'laba na alihusiana na Bani Makhzum. Jina la mama yakelilikuwa Sumayya. Yeye na wazazi wake walikuwa watangulizi katika kuukubaliUislam, na alikuwa wa saba katika kutamka imani yake. Wazazi wake wali-uawa baada ya kuteswa na kabila la Quraishi kwa sababu ya kuingia katikaUislam. Zipo ngano sahihi zilizosimuliwa na Mtukufu Mtume kuhusu Ammar,kama vile, "Ammar amejawa na imani". Alipigana katika upande wa Imam Alikatika vita vya Jamal na Siffin, na aliuawa katika medani ya vita akiwa na umriwa miaka 93.

3) Muhammad Ibn Hudhaifa (akiitwa Abul Qasim): Baba yake alikuwa Utba IbnRabi'a al-Abshami na mama yake alikuwa Sahlah, binti ya Suhail Ibn AmrAmeryyah. Alizaliwa huko Ethiopia katika wakati wa Mtume. Baba yake ali-uawa shahidi huko Yamama, hivyo, Uthman alimchukua kama mtoto wakupanga. Uthman, wakati wa utawala wake, alimpa ruksa ya kwenda Misriambako aliasi dhidi ya Uqba Ibn Ameir, yule msaidizi wa Madina, Abdullah IbnAbi Sarh (mtu wa 10 kuwa Gavana wa Misri) aliyekuwa amekwenda Madina,na alikuwa haruhusiwi kuingia tena Misri. Muhammad Ibn Hudhaifa alifaulu naakawa ndiye Gavana mpya, kisha alihamasisha askari mia sita chini ya Abdur-

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

27

Rahman Ibn Adis, kupigana na Uthman huko Madina. Baada ya Imam Ali kuwaKhalifa, alimruhusu Muhammad kubakia kama Gavana wa Misri. WakatiMu'awiyah akiwa njiani kuelekea Siffin alikwenda Misri, Muhammad alimzuiakuingia Fostat. Lakini Mu'awiyah alifunga mkataba na Muhammad. Chini yamkataba huu Muhammad Ibn Hudhaifa na Abdur-Rahman Ibn Adis, pamoja nawatu 29 waliondoka Cairo ili kuwa salama kutokana na Mu'awiyah, lakinibaadae Mu'awiyah aliwakamata na kuwafunga. Muhammad aliuawa akiwajela huko Damascus na mtumwa wake mwenyewe Mu'awiyah aitwayeRushdain. Muhammad alikutana Mtume.

4) Abdur-Rahman Ibn Adis Balavi: Alikuwa mmojawapo wa watu waliohudhuriakwenye mkataba wa Shajara. Alishiriki katika vita vya Misri, na baadhi ya ardhiya Misri ilikuwa chini ya ulinzi wake. Alikuwa ndiye kamanda wa jeshi lililo-tumwa kutoka Misri kwenda kupigana na Uthman. Alitekwa na Mu'awiyah naakafungwa huko Palestina. Baada ya kufanikiwa kutoroka alikamatwa tena naakauawa. Alipata fursa ya kukutana na Mtume.

5) Muhammad Ibn Abubakr: Mama yake alikuwa Asma binti UmaisKhathamyiah, mke wa Jafar Ibn Abi Talib. Baada ya Jafar kuuawa shahidi,Asma aliolewa na Abubakr na akamzaa Muhammad. Imam Ali alimchukuakama mtoto wa kupanga baada ya kufa Abubakr. Muhammad alikuwa kaman-da wa jeshi la askari wa miguu katika vita vya Jamal. Alikuwepo vilevile katikavita vya Siffin. Imam Ali alimteuwa kama Gavana wa Misri, na aliichukua kaziyake tarehe 15/9/37 H.L. Mu'awiyah alituma jeshi chini ya uongozi wa Amr IbnAl-Aas kwenda Misri mwaka wa 38, waliopigana na kumteka Muhammad nakisha wakamuua. Mwili wake ulitiwa kwenye tumbo la punda aliyekufa nakuchomwa moto.

6) Sa'sa'a Ibn Souhan Abdi: Bwana huyu alikuwa mzungumzaji mzuri na alisilimuwakati wa Mtume. Alipigana katika vita vya Siffin wakati Mu'awiyah alipoika-mata Kufa. Mu'awiyah alimhamisha Sa'sa'a kwenda Bahrain ambako ndikoalikofia.

7) Malik Ashtar al-Nakhai: Alikutana na Mtume na alikuwa mmoja wa Tabi'inwaaminifu. Alikuwa ndiye mkuu wa kabila lake, na baada ya kupata jerahakwenye moja ya macho yake katika vita vya Yarmuuk, alikuja kujulikana kamaAshtar. Katika vita vya Jamal na Siffin, alikuwa pamoja na Imam Ali na walipa-ta ushindi mkubwa. Katika umri wa miaka 38, aliteuliwa kuwa Gavana wa Misri,lakini akiwa njiani kuelekea huko, karibu na Bahari Nyekundu (Red Sea), alik-ufa baada ya kula asali iliyochanganywa na sumu iliyopangwa na Mu'awiyah.

Hizo hapo juu ni wasifu fupi za baadhi ya Waislam mashuhuri. Inasikitisha kwam-ba baadhi ya wana-historia walidai kwamba walifuata Myahudi asiyejulikana.Baada ya kulijua hili, tujaribu sasa kuchanganua dhamira za ngano za AbdullahIbn Saba.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

28

ASILI YA NGANO YENYEWE NA YAWASIMULIAJI WA NGANO

Ni karne kumi na mbili zimepita tangu wanahistoria walipoanza kuandika kuhusuAbdullah Ibn Saba. Mtu anaweza kwa shida sana kuona mwandishiasiyezungumza kuhusu yeye ikiwa anaandika kuhusu masahaba, Waislam ambaowalikutana na Mtume. Tofauti kati ya maandishi ya wanahistoria wa zamani na wasasa wa Uislam wanapozungumzia kuhusu ngano za Abdullah Ibn Saba - nikwamba hawa wa sasa wamechagua njia ya kisasa ya mchanganuo wa uandishi,ambapo wale wa zamani walikisimulia kisa hicho kwa lugha ya Hadith (nukuu yasemi za Mtume). Kuisoma na kuichunguza ngano hii kwa ufasaha, hebu natuwatafute wasimuliaji walioongea na, au walioandika juu yake.

1) MUHAMMAD RASHID RIDHA

Miongoni mwa waandishi wa kisasa ni Muhammad Rashid Ridha, ambaye katikaKitabu chake al-Sunna wal Shiah (uk. 4-6), anasema: "Ushiah ulibuniwa naAbdullah Ibn Saba. Alidai kwamba ameikana imani yake ya Kiyahudi na amesilimuna kuwa Mwislamu. Alitia chumvi sana kuhusu Ali, mrithi wa nne wa MtumeMuhammad, na akabuni Ushia kwa jina la Ali. Kubuni Ushia kulikuwa mwanzo wavurugu katika mambo ya kidini na ya kidunia ya umma wa Muhammad, kwa kuzuatofauti kati ya Waislam." Kisha Ridha akaipindisha ngano kumfaa yeye binafsi, nakama mtu anataka kujua mwanzo wa ngano hii, Muhammad Rashid Ridha anakiriakisema, "Yeyote anayetazama ngano zinazohusu vita vya Jamal katika kitabu chahistoria cha Ibn Athir kwa mfano, atagundua kiwango cha athari za uovu waSabaia katika majeshi ya pande zote, wakati sulhu ilikuwa inatarajiwa (rejea juz.ya3, uk. 96, 103)." Hivyo chanzo cha habari cha Sayid Rashid kilikuwa kitabu cha his-toria cha Ibn Athir.

2) ABDUL FIDA (KAFA 732 H.L. - 1331A.D.)

Abdul Fida katika kitabu chake al-Mukhtasar, anasema: "Nimefanya mukhtasarikatika kitabu changu yale ambayo Sheikh Izzid-Din Ali, anayejulikana kama IbnAthir Jazari, aliyoandika katika kitabu chake kamili." Hivyo vyanzo vya waandishihao wawili hapo juu vilikuwa ni Ibn Athir.

3) IBN ATHIR (KAFA 630 H.L. - 1229 A.D.)

Ibn Athir ameitaja ngano hii miongoni mwa matukio yaliyotokea katika miaka ya 30-36 H.L. Haelezei chanzo cha ngano hizi isipokuwa kwenye utangulizi wa kitabuchake Tarikh al-Kamil (kilichochapishwa Misri, 1348 H.L.), akisema: "Nimezionangano hizi katika kitabu cha Abu Jafar al-Tabari," Hicho kitabu kamili cha historiacha Tabari (17) ndiyo Msahafu wa Waislam wa historia, kitabu pekee cha kutege-mewa miongoni mwa Waislam wanaokirejea wakati jambo lolote lenye mashaka

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

29

likitaka kuchunguzwa. Tabari ameandika ngano nyingi katika sehemu tofauti zakitabu chake, kuhusu tukio moja; lakini nimezipanga upya ngano hizi chini ya kich-wa cha habari makhsusi na nimechagua ngano iliyokamilika zaidi kwa kila tukio.Kuhusu Masahaba nimenukuu ngano zao vilevile hasa kama Tabari (17) alivy-oziandika kwenye kitabu chake, na isipokuwa maelezo ya ufafanuzi yasiy-oingiliana na nukuu hizo.

Huyu ni Ibn Athir (3) ambaye kutoka kwake Muhammad Rashid (1) na Abul Fida(2) wameazima ngano zao.Huyu Ibn Athir (3) ameandika hasa kile at-Tabari (17)alichoandika.

4) IBN KATHIR (KAFA 774 H.L. - 1289 A.D.)

Ibn Kathir katika kitabu chake Al-Bidaia wal Nihaya juz. 7, akimnukuu Tabarianasema: "Seif Ibn Umar amesema kwamba chanzo cha uasi dhidi ya Uthmankilikuwa ni Abdullah Ibn Saba aliyejifanya ni Mwislamu na akaenda Misri kuenezangano za uongo."

Kisha Ibn Kathir anaiandika ngano kamili ya Abdullah Ibn Saba, ikiwemo vita vyaJamal. Anasema katika ukurasa wa 246: "Huu ni mukhtasari wa kile ambacho AbuJafar Ibn Jarir Tabari (17) (Mola Amrehemu) alichokiandika."

5) IBN KHALDUN

Mwana-falsafa wa wana-historia katika kitabu chake al-Mubtada wal Khabar ame-wataja Sabaia katika Matukio ya Nyumba (kifo cha kishujaa cha Uthuman) naJamal. Kisha katika juz. 2, uk. 425 wa kitabu chake, anasema: "Huu ni mukhtasariwa matukio ya Jamal kutoka kwenye kitabu cha Abu Jafar Tabari (17) kwa sababuanategemewa sana na kuaminiwa sana kuliko wanahistoria wengine pamoja naIbn Qutaybah." Pia, katika uk.457, anasema: "Hili ni neno la mwisho kuhusuumakamu wa Kiislam, na watekaji wa ki-maasi na vita. Baada ya hili yatakuwamakubaliano na Mkutano (al-Jamaat) miongoni mwa Waislam. Nimechukua don-doo hizi kutoka kwenye kitabu cha Muhammad Ibn Jarir at-Tabari (17) kama kilivyocha kutegemewa sana, na hakiwakosoi Masahaba na Tabi'in."

6) MUHAMMAD FARID WAJDI

Muhammad Farid Wajdi katika kitabu chake Ensaiklopidia chini ya neno: Atham nachini ya Vita vya Jamal, pia katika wasifu wa Ali Ibn Abi Talib, ameitaja ngano yaAbdullah Ibn Saba na katika uk. 160, 168 na 169, anatueleza kwamba chanzochake cha habari ni kutoka kwa Tabari (17).

7) AL-BUSTANI

Katika Ensaiklopidia yake chini ya jina Abdullah Ibn Saba, anasema: "Abdullah IbnSaba anasema Ibn Kathir………."

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

30

8) AHMAD AMIN

Mmoja wa wanahistoria wa leo ambaye ametumia mbinu ya uchambuzi ya kuandi-ka ngano hizo ni Ahmed Amin. Katika kitabu chake Fajrul Islam kuhusu Waajemi1na athari zao katika Uislam, anaandika: "Tofauti kuu kati ya dini ya Mazdak na dininyinginezo ilikuwa ni ile dhana yao ya kisoshalisti (kijamaa). Dini ya Mazdak iliami-ni usawa wa mwanadamu kwa kuzaliwa na kueleza kwamba ni lazima kwa hiyo,wawe na fursa sawa katika namna yao ya maisha. Aliyaona mambo ya muhimusana katika usawa wa mwanadamu kuwa ni mali na wanawake, haya yakiwa ndiyochanzo cha migogoro. Hivyo alisema wanawake na mali vilikuwa ni sawa kwawote. Wanaume wa hali ya chini walichukua fursa ya mafunzo ya Mazdak nawakasababisha matatizo mengi. Wafuasi wake walivamia kwenye nyumba, waki-gawana miongoni mwao wenyewe, wanawake na vitu. Hii iliendelea kwa mudamrefu kiasi kwamba watoto hawakujua baba zao ni nani, na akina babahawakuweza kutambua watoto wao." Ahmed Amin anaendelea akisema, "Namnahii ya maisha ilitwaliwa na Kerman (Uajemi ya Kusini) ambako dini hii ilikuwa badoikitumika katika enzi za ufalme wa Amawy." "Kutokana na hili" anasema AhmedAmin, "tunaona kufanana kwa dhana ya Abu Dhar na Mazdak kutokana namgawano wa mali unavyohusika." "Abu Dhar", anasema Tabari, "alisimama hukoDamascus (Sham) akisema, "Enyi watu matajiri, gawaneni fedha zenu na maski-ni", na akasoma Aya hii ya Qur'ani: "Wabashirie adhabu iliyo chungu wale wanao-hodhi dhahabu na fedha na wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu.Siku zitakapochomwa katika moto wa Jahannam na kwazo vikachomwa vipaji vyanyuso zao na mbavu zao na migongo yao." (Qur'ani 9:34).

Abu Dhar alirudia nukuu hii mara kwa mara kiasi kwamba watu masikiniwakachukulia kwamba ni wajibu kwa watu matajiri kugawa fedha zao, nawakawakera sana matajiri mpaka wakamlalamikia Abu Dhar kwa Mu'awiyah,Gavana wa Syria, naye akamuamuru Abu Dhar kwenda Madina kumuona KhalifaUthman.

"Ewe raia wa Damascus, kwa nini ulimi wako unalalamika sana?" AkaulizaUthman. "Watu matajiri hawapaswi kuweka fedha zao kwa ajili yao peke yao tu",akasema Abu Dhar.

1Kabla ya Ahmad Amin, Rashid Ridha ameandika ngano hii katika kitabu chake, as-Sunna wa Shia.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

31

"Tunaona kutokana na hayo hapo juu", anasema Ahmad Amin, "kwamba dhana yaAbu Dhar ilikuwa karibu sana na ile ya Mazdak kuhusu mali." Lakini Abu Dharamepata wapi wazo hili? Tabari anajibu: "Ibn al-Souda alikutana na Abu Dhar naakashauri dhana hii ya kijamaa, katika mkutano na Abu Darda2 na Ubada IbnSamit, lakini hawa wa baadae hawakudanganyika na walimchukua Ibn al-Soudampaka kwa Mu'awiyah na kumwambia huyu ndiye mtu aliyemshawishi Abu Dharkukuchosha.3

Ahmed Amin anaendelea: "Tunajua pia kwamba Ibn al-Souda alijulikana kamaAbdullah Ibn Saba aliyekuwa Myahudi kutoka Sana'a (Yemen). Alijifanya kuwaMwislamu katika wakati wa Uthman, na akajaribu kuibomoa dini ya Waislam kwakueneza dhana zenye madhara." Hili tutalijadili baadae.

"Abdullah Ibn Saba", anaendelea Ahmed Amin, "alisafiri kwenda kwenye miji mingikatika Bara Arabu kama vile: Basra, Kufa, Damascus na Cairo. Anaweza kuwaameipata dhana hii ya kijamaa kutoka kwa wafuasi wa Mazdak huko Iraq auYemen. Hivyo, Abu Dhar alijifunza hiyo kutoka kwake."

Ahmed Amin aliandika pambizoni mwa kitabu chake hivi: "Rejea Tabari Juz. 5, uk.66 na kuendelea." Katika ukurasa wa112 Ahmed anamalizia kwamba: "Mashiawaliwaona Ali na wanae kama ni watakatifu, kama walivyofanya wahenga wao waKiajemi na Wapagani kuhusu Wafalme wao wa utawala wa Sasanid."

Ahmed Amin alikuwa mwaminifu wa ahadi yake aliposema, "tutazijadili dhana zaAbdullah Ibn Saba zenye madhara baadae."

Ahmed Amin katika ukurasa wa 254, akizungumzia juu ya madhehebu tofautianasema: "Mwishoni mwa uongozi wa Uthman, baadhi ya vikundi vya siri, vilivy-otawanyika kila mahali, viliasi dhidi ya Uthman, vikijaribu kumnyan'ganya madara-ka na kumpa mtu mwingine. Miongoni mwa vikundi hivi vingine vilikuwa vikiombakuungwa mkono kwa ajili ya Ali, nguvu kuu nyuma ya kitendo hiki katika Basra,Kufa na Damascus ilikuwa ni Abdullah Ibn Saba. Alisema: " Kila Mtume ana mrithina Ali ndiye mrithi wa Mtume Muhammad. Ni nani dhalimu zaidi kuliko yule mtuambaye amepora nafasi ya Ali kwa dhulma?"

Alilisisitiza hili mpaka Uthman akauawa.

"Hatuna budi", anasema Ahmed Amin, "kuijadili ngano hii kwani madhehebumatatu yalizuka kama matokeo yake, nayo ni Shia, n.k."

2 Walijulikana kama Wafuasi wa Mtume (Masahaba).

3 Ngano hii ni ya uongo na ilitungwa na Abdullah Ibn Saba, Abu Dhar kamwe hakuhubiri dhidi ya watumatajiri, mazungumzo yake yalimlenga Mu'awiyah na ufalme wake, ambao walitwaa mali za watu kwanguvu na Abdullah Ibn Saba akajaribu kulifunika jambo hilo kwa kutunga ngano hizi.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

32

Katika mlango unaohusu Shia katika ukurasa wa 266-278, anasema kwamba iledhana ya kuja kwa mara ya pili kwa Nabii Eliyah ni ya Wayahudi. Abdullah IbnSaba alijifunza hili kutoka kwa Wayahudi. Shia waliitwaa kutoka kwa Abdullah IbnSaba kukubaliana na dhana zao kuhusu Mahdi aliyetarajiwa kuja na kuujaza hakiulimwengu . Ushia ni kimbilio la kuhifadhi wale wanaotaka kuubomoa Uislam kwakificho cha mapenzi kwa watu wa nyumba ya Mtume. Myahudi yeyote au Mkristoanaweza kuelezea maoni yake kuhusu Uislam kupitia kwenye Ushiah, kama iledhana ya Kiyahudi kuhusu kuja kwa mara ya pili kwa Eliyah.4 Katika ukurasa wa277, anasema: "Kwa mujibu wa Wellhouzen, Ushia unatokana zaidi na imani zaKiyahudi kuliko za Kifursi, kwa sababu Abdullah Ibn Saba alikuwa Myahudi." Kwamaneno mengine, Ahmed Amin anasema kwamba Mashia walipata imani zao juuya umakamu wa Ali, na kuja kwa mara ya pili kwa Watakatifu na Mahdi, kutoka kwaIbn Saba, yaani, toka kwa Myahudi.

Abu Dhar alipata fikra zake za kikomunisti kutoka kwa Ibn Saba. Ibn Saba alijifun-za ukomunisti kutoka kwa watu wa Mazdaki ambao waliishi katika wakati wautawala wa Amawiy. Mazdak alikuwa Mfursi, na Wafursi waliwatukuza wafalmewao. Vivyo hivyo Mashia wanawatukuza Maimamu wao. Ushiah ni kificho kwawale wanaotaka kuuvunja Uislam kwa chuki na wivu. Ni hifadhi pia kwa mtu yey-ote anayetaka kuanzisha dini ya Kiyahudi, Ukristo au imani ya Kizoroasta katikaUislam, Tunaona kwamba fikra zote hizi zinatoka kwa Abdullah Ibn Saba, ambazoAhmed Amin amezichukua kutoka kwa Tabari na Wellhouzen. Tutaona kwambaWellhouzen pia, ameziandika kutoka kwa Tabari (17).

9) HASAN IBRAHIM

Mwanahistoria mwingine wa siku hizi ambaye amechukua njia ya uchambuzi kati-ka kitabu chake Islamic Political History (Historia ya Siasa za Kiislam), ni Dr.Hasan Ibrahim. Baada ya kutazama hali ya Uislam mwishoni mwa Ukhalifa waUthaman anasema: "Mazingira yalikuwa tayari kuvikubali vitendo vya Sabaia.Mmoja wa Masahaba wa Mtume anayejulikana sana kwa uchamungu wake nauadilifu, alikuwa mmoja wa viongozi wa wasimulizi, akiitwa Abu Dhar Ghafari.Alikuwa ni bwana huyu aliyesababisha matatizo, kama alivyoathiriwa na propa-ganda zenye uchochezi za Abdullah Ibn Saba, na akampinga Uthman na Gavanawake huko Syria, Mu'awiyah. Abdullah Ibn Saba alikuwa Myahudi aliyejifanyakuwa Mwislamu na alisafiri kwenda Hijaz, Kufa, Syria na Misri.

Dr. Hassan Ibrahim amechukua ngano hii kutoka juz.1,uk.2859 ya Tabari (17). kati-ka ukurasa 349 anasema, "Abdullah Ibn Saba alikuwa mtu wa kwanza kuwaon-goza watu dhidi ya Uthman, na kusababisha yeye kupinduliwa."

4 Inasikitisha kwamba kitabu cha Ahmed Amin, Fajrul Islam na Historia ya Siasa za Kiislam cha HassanE. Hassan ndiyo vitabu pekee kuhusu fikra za Kishia kwenye vyuo vikuu vya Magharibi.

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

33

Katika pambizo ya kitabu chake alimrejea Tabari mara nne kuhusu ngano yaAbdullah Ibn Saba. Pia anarejea kwa Tabari mara kumi na mbili kuhusu ngano hiikatika kitabu chake. Bado amejiepusha kunukuu kile Tabari alichoandika katikakitabu chake kuhusu Sabaia, ingawa hata hivyo shujaa katika ngano zote ni huyohuyo - Abdullah Ibn Saba.

Mpaka sasa tumeona jinsi wanahistoria wa Kiislam walivyonukuu kutoka kwenyekitabu cha historia cha Tabari (17) kuhusu Sabaia

10) VAN FLOTTEN (VOLTEN) (JOHANNES 1818-1883)

Katika kitabu chake Arabian Rule and Shiah and Israilyat in Amawid Time, (Sheriaya Kiarabu na Shiah na Uyahudi katika Wakati wa Bani umayyah), kilicho tafsiriwana Dr. Hassan Ibrahim na Muhammad Zaki Ibrahim (chapa ya 1 Misri, uk. 79)anasema kuhusu Shiah: "Hawa Sabaia, wafuasi wa Abdullah Ibn Saba walimuonaAli kama mtu mwenye haki ya urithi wa Mtume katika wakati wa Uthman." Kishaanarejea kwa Tabari(17) kwenye pambizo ya uk. 80 katika kitabu chake.

11) NICHOLSON, REYNOLD ALLEYNE (1868-1945)

Katika kitabu chake The History of Arabian Literature (Historia ya fasihi ya Kiarabu)Cambridge, uk. 215, anasema, "Abdullah Ibn Saba aliasisi jamii ya Sabaia.Alitokea Sana'a huko Yemen. Inasemekana kwamba alikuwa Myahudi ambaye,katika wakati wa Uthman, aliingia Uislam. Alikuwa kwa kweli ni msafiri, mmisionarifisadi, aliyejaribu kuwapotosha Waislam. Alianzia Hijazi, na akaenda Basra, Kufana Syria. Hatimae aliishi Misri. Aliamini katika kuja kwa mara ya pili kwa Mtume."Akasema, "Watu waliamini kuja kwa mara ya pili kwa Yesu, lakini wakapinga kujakwa mara ya pili kwa Mtume Muhammad, ingawa hii imetajwa katika Qur'ani.Aidha, Mwenyezi Mungu ametuma mitume zaidi ya elfu moja, na kila mmoja waoalikuwa na msaidizi na mrithi. Ali ndiye mrithi wa Mtume Muhammad wa mwishowao." Kisha katika pambizo ya kitabu chake anamrejea Tabari (17), na kuuonye-sha ukurasa wenyewe.

12) ENSAIKLOPIDIA YA KIISLAM

Katika Ensaiklopidia hii, iliyoandikwa na baadhi ya mutashirki, ngano hiyo ime-andikwa kama ifuatavyo:

"Kama tunataka kuangalia tu kile Tabari na Maghrizi walichoandika, tunasemakwamba moja ya mambo Ibn Saba aliyokuwa akiyahubiri ilikuwa ni kuja kwa maraya pili kwa Muhammad. Hii ilikuwa ndiyo nadharia -- kwamba kwa kila Mtume yupomrithi, na Ali ndiye mrithi wa Muhammad. Hivyo, kila Mwislamu, kwa hiyo, lazimaamsaidie Ali kwa maneno na vitendo." Inasemekana kwamba Abdullah Ibn Sabaalituma wamisionari nchi nzima kuhubiri nadharia yake hiyo. Yeye mwenyewebinafsi alikuwa miongoni mwa wale walioondoka toka Misri kuelekea Madina kati-ka mwezi wa Shawwal 35 H.L., April, 656 A.D. Ensaiklopidia hii inarejea kwa Tabari

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

34

na Maghrizi, Tabari aliishi miaka 300 baada ya ngano yenyewe, na Maghrizi miaka800. Tabari anataja majina ya wale aliowanukuu, lakini Maghrizi hataji. Kwa hiyomaandishi ya Maghrizi hayafikiriwi kama ni ya kuaminika kama yale ya Tabari,aliyeishi miaka 500 kabla ya Maghrizi. Tutaandika kuhusu Maghrizi baadae.

13) DONALDSON, M. DEWIGHT.

Katika kitabu chake The Shiah Articles of Faith, (Shuruti za imani za Kishia) tafsiriya Kiarabu katika uk. 85 anasema: "Kumbukumbu za awali zinatuonyesha kwam-ba yale madai ya wafuasi wa Ali, kuhusu urithi wake hayakuwa ya kisiasa tu, baliwaliamini kwamba urithi wa Ali ulikuwa wa majaaliwa ya kimungu. Bado mtu waajabu anaweza kufikiriwa kuhusika sana na imani hiyo. Katika wakati wa utawalawa Uthman, Abdullah Ibn Saba alianzisha harakati za kuubomoa Uislam, kamainavyosemwa na Tabari."

Donaldson hakunukuu moja kwa moja kutoka kwa Tabari, lakini kwa mujibu wapambizo ya uk. 59 katika kitabu chake, amenukuu kutoka kwenye Ensaiklopidia yaKiislam iliyotajwa hivi punde na kutoka kwenye kitabu History of Arabian Literature.Tumeeleza mapema kwamba wao wenyewe wamenukuu kutoka kwa Tabari (17)

14) WELLHOUSEN JULIUS (1844 - 1918)

Katika uk.56-57 katika kitabu chake Sabaian and the Spirit of Prophethood, anase-ma: "Kikundi kiliundwa huko Kufa, kinachoitwa Sabaian, na kikundi hiki kilifanyamabadiliko makubwa katika Uislam. Mbali na mafundisho ya Qur'ani, walihubiriutakatifu wa Mtume Muhammad. Sabaians waliamini kwamba Muhammad alikufakimwili lakini siyo kiroho, kwamba roho yake ni tukufu, na iko hai daima milele."

Kama katika nadharia ya kupata mwili - incarnation, wanasema kwamba roho yaMungu imepandikizwa kwenye Mitume yake na kupita kwa manabii wote, mmojakwenda kwa mwingine, na kwamba baada ya Muhammad, ilipitishwa kwa Ali nakisha kwa kizazi chake. Hawakuona kwamba Ali alikuwa sawa na Makhalifawaliomtangulia na walikuwa warithi wa Muhammad, bali waliwaona Makhalifa waleni batili. Walimtangaza Ali kama mrithi pekee, mtakatifu, na wa haki wa MtumeMuhammad, na utii kwake ulikuwa uonekane kama utii kwa Mwenyezi Mungu.

Wellhousen pia amesema kwamba inafahamika kwamba hawa Sabaian wanapa-ta jina lao kutoka kwa Ibn Saba, Myahudi wa Yemen, na chini ya kichwa 'wak-ereketwa wa Sabaia na Wanaoamini juu ya Uhamisho wa roho' - kutoka kiumbekwenda kiumbe. Anasema,: "Hawa wakereketwa wanayo majina tofauti yasiyofaakutajwa, lakini majina hayo yote yalithibitisha kwamba wamekwenda kombo -wamepotoka." Seif Ibn Umar Tamimi anasema: "Sabaian tokea mwanzoniwalikuwa wakorofi, kwa kumuua Uthman, na kuanzisha vita vya wenyewe kwawenyewe…….. Wengi wao walikuwa watumwa wasiokuwa Waarabu. Waliaminijuu ya kupita kwa roho kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, hasa rohoya Muhammad kuhamia kwa Ali, kisha kizazi cha Ali, kwa Fatima, binti ya Mtume,

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

35

waliwakataa hawa Sabaia, hivyo walimfuata Muhammad al-Hanafiyah, mtoto waAli lakini siyo kwa Fatima. Hawa Sabaia walimfuata Aba Hashim mtoto waMuhammad al-Hanafiyah, mtu asiyestahili kama baba yake. Aba Hashim alim-teuwa mwanae Muhammad Ibn Ali Abbasy. Hivyo urithi wa Ali ulitoka kwake kwen-da kwenye ufalme wa Bani Abbas. Bani Abbas, kama Sabaia, ni wa asili ya Kufa.Makundi yote yaliasi dhidi ya Waislam Waarabu na wafuasi wao walikuwa niwatumwa wa ki-Iran."

Wellhousen anamrejea Seif mara mbili katika ngano hii katika pambizo ya kitabuchake. Hivyo ni wazi kwetu kwamba ameichukua ngano hii kutoka kwa Tabari (17)mwanahistoria wa kwanza kumtaja Seif.

Hivyo, tumeandika juu ya wanahistoria waliomtaja Tabari, moja kwa moja auvinginevyo, wakati wa kuandika hii ngano ya Ibn Saba. Wapo waandishi wengineambao hawakumtaja mwandishi wa asili wa ngano hii ya Ibn Saba. Lakini katikasehemu nyingine katika vitabu vyao wamemtaja Tabari au vitabu vilivyonukuukutoka kwa Tabari kama vile:

15) MIRKHAND KATIKA KITABU CHAKE - RAWZATUS-SAFA.

16) GHIATHUD DIN (KAFA 940H.L. - 1455 A.D.)

Mtoto wa Mirhand, katika kitabu chake Habibus Siyar, amenukuu kutoka kwa babayake kama inavyotajwa kwenye utangulizi wa kitabu chake. Wanahistoria wotehapo juu wamenakili kutoka kwa Tabari (17).

17) TABARI NA CHANZO CHAKE

Abu Jafar Muhammad Ibn Jarir Tabari Amuli (kafa 310 H.L. - 825 A.D.). Katikakitabu chake Tarikhul Umam wal Muluuk (Historia ya Mataifa na Wafalme), Tabariamenakili ngano ya Sabaia pekee kutoka kwa Seif Ibn Umar Tamimi. Anarejea tukwenye baadhi ya matukio ya mwaka wa 30H.L. kama ifuatavyo:

"Katika mwaka huo huo (i.e. mwaka wa 30 H.L) tukio la kumhusu Abu Dhar lili-tokea. Mu'awiyah alimtoa Abu Dhar kutoka Sham (Damascus) kwenda Madina.Mambo mengi yanasemwa kuhusu tukio hilo, lakini sipendi niyaandike. Sari ame-niandikia juu ya wale wanaotafuta visingizio juu ya Mu'awiyah, kutokana namatukio yanayomhusu Abu Dhar. Shuaibhas alimweleza Sari kwamba Seif alise-ma, "Wakati Ibn Sawda alipofika Shaam (Damascus) alikutana na Abu Dhar naakamweleza kitu ambacho Mu'awiyah alikuwa anakifanya.' Na Tabari anaisimuliangano ya Sabaia kama ilivyosemwa na Seif, na anamalizia ngano ya Abu Dharkwa maneno yafuatayo, 'Wengine wamesema mengi kuhusu hii ngano(yakufukuziwa uhamishoni kwa Abu Dhar), lakini ninasita kuwataja.'Juu ya matukio ya miaka hiyo (30 - 36 H.L.), Tabari anaandika hii ngano ya Ibn

36

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Saba na wale Sabaia, mauaji ya Uthman (Khalifa wa tatu) na Vita vya Jamal kuto-ka kwa Said Seif akiwa ndiye mmoja tu aliyeweza kunakili toka kwake. Tabarianasimulia ngano yake kutoka kwa Seif kupitia watu wawili, 1. Ubaidullah Ibn Sa'idZuhri kutoka kwa ami yake Ya'qub Ibn Ibrahim na kisha toka kwa Seif. Kutokakwenye sanadi hii ngano zikaanza "nimesimuliwa" au "tumesimuliwa". 2. Sari IbnYahya kutoka kwa Shuaib Ibn Ibrahim toka kwa Seif. Tabari akinakili kutokakwenye vitabu viwili, al-Futuuh na al-Jamal kutoka kwa Seif, ameanza na"Aliniandikia", "Alinisimulia", na "Katika barua aliyoniandikia". Mpaka hapotumeshughulika na chanzo cha Tabari.

18) IBN ASAKIR (KAFA 571 H.L. - 1086 A.D)

Ibn Asakir anaandika kutoka kwenye chanzo kingine. Ndani ya kitabu chake TheHistory of Damascus (historia ya Damascus) wakati akiandika wasifu wa Talha naAbdullah Ibn Saba, ameandika sehemu za ngano ya Sabaian, kupitia kwa AbulQasim Samarqandi kutoka kwa Abul Hussein Naquur kutoka kwa Abu TahirMukhallas toka kwa Abubakr Ibn Seif toka kwa Sari toka kwa Shuaib Ibn Ibrahimkutoka kwa Seif.

Kwa hiyo, wa mwanzo ni Sari, mmoja kati ya sanadi ambazo Tabari amenakili tokakwao.

19) IBN BARDAN (KAFA 1346 H.L. - 1851 A.D.)

Ibn Bardan ameandika ngano katika kitabu chake Tahdhib bila kutaja majina yawatu ambao amenakili kutoka kwao.Ameandika baadhi ya ngano ya Ibn Saba kati-ka kitabu chake bila ya kuwataja waanzilishi wake. Lakini katika wasifu wa Ziad IbnAbih amemtaja Tabari kuhusiana na ngano za Seif (juz.5, uk.406).

20) IBN ABIBAKR (KAFA 741 H.L. - 1256 A.D.)

Ibn Abibakr anacho kitabu kinachoitwa at-Tamhid, ambacho baadhi ya waandishiwamenakili kutoka humo. Kitabu hicho kinahusu mauaji ya Khalifa Uthman na kati-ka utangulizi wake hili jina la al-Futuuh, la kitabu cha Seif limetajwa, vilevile na jinala Ibn Athir. Ibn Athir amenakili kutoka kwa Tabari na Tabari kutoka kwa Seif.Mpaka hapa ngano za Seif zina vyanzo vikuu vitatu:

1) Tabari (kafa 310H.L. - 825 A.D.);2) Ibn Asakir (kafa 571 H.L. - 1086 A.D.);3) Ibn Abibakr (kafa 741H.L. - 1256 A.D.).

Baadhi ya waandishi wamenakili kutoka kwenye rejea moja, wengine kutoka viwili,

37

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

na wengine kutoka kwenye vyote vitatu.

21) SA'ID AFGHANI

Katika kitabu chake Aisha and Politics (Aisha na Siasa), Sa'id Afghani ameandikabaadhi ya ngano za Sabaian chini ya vichwa vifuatavyo:

"Mtume dhidi ya Uthman na Matokeo yake.""Ibn Saba Shujaa wa Siri wa Kuogopesha""Uchunguzi wa Maafikiano" na "Njama."

Anawataja pia hawa Sabaia katika mlango mwingine wa kitabu chake. Rejea yakekuu ni Tabari, akifuatiwa na Ibn Asakir, kisha Tamhid ya Ibn Abibakr. Anamtegemeazaidi Tabari kuliko mwingine yeyote, akitoa kama sababu yake kule kumuaminikwake Tabari alikonako, akisema kwamba Tabari anategemewa zaidi, na kwambawanahistoria wote waliopita walimuamini. Kisha anasema, "Kwa kiasi nilivyoweza,nimenukuu kutoka kwenye kitabu cha Tabari vile hasa kilivyokuwa."

22) DHAHABI (KAFA 784 H.L. - 1263 A.D.)

Kuna sanadi nyingine ya ngano ya Ibn Saba inayoitwa maandishi ya Dhahabi.

Ameandika baadhi ya sehemu za ngano hii katika kitabu chake The History ofIslam (Historia ya Uislam) juz.2, uk.122 - 128, ambamo ameonyesha kuuawa kwaUthman miongoni mwa matukio ya mwaka wa 35H.L. Anaanza kama ifuatavyo:

"Na Seif Ibn Umar amesema kwamba Atyya amesema, kwamba Yazid al-Faq-asialisema wakati Ibn Sawda alipokwenda Misri……" Dhahabi ameandika pia nganonyingine iliyosimuliwa na Seif kwa maelezo zaidi kuliko Tabari. Baadae, ameandi-ka mukhtasari wa kile Tabari alichokiandika. Asili ya ngano hizo zilizoandikwa naDhahabi kuhusu Sabaia na nyinginezo, inaweza kupatikana kwenye utangulizi wakitabu chake.

1) Vitabu kama vile al-Futuuh cha Seif, ambacho kutoka humo Dhahabi amepa-ta habari muhimu kwa ajili ya kitabu chake.

2) Vitabu ambavyo kutokana navyo amepata kile alichokiandika kamamukhtasari.

3) Vitabu anavyorejea mara kwa mara, kama vile Tabari.

Kwa vile Dhahabi amekitaja kitabu cha al-Futuuh cha Seif na aliishi katika karneya 8 ya zama za Uislam basi hiki kitabu cha al-Futuuh lazima kiwe kilikuwa kinap-atikana mpaka kufikia wakati huo.

Kwa mukhtasari tunaweza kusema kwamba wanahistoria wote hawa waliotajwa,

38

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

wamechukua ngano zao na kisa cha Abdullah Ibn Saba kutoka kwa Seif. Wannewa wanahistoria hawa: Tabari, Ibn Asakir, Ibn Abibakr na Dhahabi wamechukuangano zao moja kwa moja toka kwa Seif.

Hiyo chati kwenye ukurasa ufuatao inaonyesha sanadi ambazo kwazo kisa chaSabaia kimeandikwa kutoka kwa msimuliaji wa asili - Seif.

39

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

SEIF IBN UMAR AT-TAMIMI(KAFA BAADA YA 170 A.H)

ADH-DHAHABI AT-TABARI IBN ABI BAKR IBN ASAKIR

(748 A.H) (310 A.H) (741A.H) (571 A.H)

R.A ENCYCLOPAEDIA VAN J.WELL MIR KHUND IBN KATHIR IBN IBN AL-

NICHOLSON OF ISLAM FLATON HAUSEN (903 A.H.) (747 A.H) KHALDUN ATHIR

(808 A.H) (630A.H)

GHIYATH AD-DIN

(940 A.H) ABU`L FIDA

(732 A.H.)

AHMAD AMIN

D.M. DONALDSON

RASHID RIDA IBN BADRAN

(135 A.H) (1346 A.H)

FARIDWAJDI HASAN IBRAHIM SA’ID AL AFGHANI

UCHUNGUZI KUHUSU SEIF

NA SIMULIZI ZAKE

SEIF NI NANI?

Kwa mujibu wa Tabari, juz.1,uk.1749, na Europe and Lubabul Ansab, juz.1,uk.49,jina kamili la Seif lilikuwa ni Seif Ibn Umar al-Tamimi al-Usayyadi. Kwa mujibu waJamharatul Ansab, uk. 199, na al-Ishtiqaq cha Ibn Duraid, uk. 201 - 206, jina laUsayyad lilikuwa ni Amr Ibn Tamimi. Kwa sababu Seif alikuwa ni kizazi cha Amramechangia zaidi sana kuhusu matendo ya kishujaa ya Bani Amr kuliko wengine.

Imeandikwa "Usady" katika kitabu cha Nadim, Fihrist, badala ya Osayyad.

Imesimuliwa ndani ya Tahdhibul Tahdhib, al-Burjumi wal Sa'ady au al-Zaby.

Kama hii ingekuwa kweli inadhihirisha tu kwamba hili kabila la Burjum na Usayyadwalikuwa na namna ya makubaliano (mkataba wa amani n.k.) kati yao kwa vileBurjun na Usayyad hawakuwa ndugu wa karibu hata kama tutaamini kwambamakabila yote haya yalikuwa kizazi cha Bani Tamimi.

Imeandikwa katika Tahdhibut Tahdhib, Khulasatut Tahdhib na Hidayatul Arifinkwamba Seif alitokea Kufa na akaishi Baghdad.

Kwa mujibu wa KhulasatutTahdhib, Seif alikufa mwaka wa 170H.L. Imeandikwandani ya al-Tahdhib, "Nimeuona mwandiko wa Dhahabi akisema kwamba Seif alik-ufa wakati wa utawala wa Harun al-Rashid."

Ismail Pasha katika kitabu chake al-Hidaia, anasema, "Yeye (Seif) alikufa Baghdadwakati wa utawala wa Harun al-Rashid katika mwaka wa 200 na al-Rashid alikufamwaka wa 193." Hakuna mwingine yeyote aliyesema hivyo, wala Ismail Pashahakuonyesha rejea ya taarifa yake.

VITABU VYA SEIF

Kwa mujibu wa al-Fihris na al-Hidaia, Seif aliandika vitabu viwili:

1) al-Futuuh al-Kabir wal Ridhah.2) al-Jamal wa Masiri Aishah wa Ali.

Na kwa mujibu wa al-Lubab, Tahdhib na Kashful-Zunuun, Seif aliandika kitabukimoja tu "al-Futuuh".Tabari katika kitabu chake ameandika kutoka kwenye vitabu viwili vya Seif, al-Futuuh na al-Jamal katika mpango wa majina ya watu wanaohusika kwenye hilo

40

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

41

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

tukio, lakini hakufanya marejeo kwenye vitabu vya Seif.

Dhahabi katika historia yake ya al-Kabir; na Ibn Asakir katika al-Tamhid wame-andika kutoka kwa Seif kwa mujibu wa majina ya watu wanaohusika katika hilotukio na wamefanya marejeo kwenye vitabu vya Seif.

Wanahistoria maarufu kabisa ambao wameandika kuhusu masahaba wa Mtume niIbn Abdul Birr, Ibn Athir, Ibn Hajar na Dhahabi. Wanahistoria hawa wameandikamajina ya mashujaa waliobuniwa na Seif pamoja na majina ya Masahaba wa kweliwa Mtume.

Wanajogorafia kama al-Hamawi, katika Mujam yake; na al-Him'iari katika al-Ruuzwametaja majina ya sehemu zisizopo zilizobuniwa na Seif. Abdul Mumin ame-andika sehemu za Seif kutoka kwa al-Hamawi.

Mtu wa mwisho, tuliyempata, aliyesema kwamba alikuwa anacho kitabu cha Seifmkononi mwake ni Ibn Hajar (kafa 852H.L.). Yule mwandishi wa al-Isabah.

TATHMINI YA MAANDISHI YA SEIF.

1. Yahya Ibn Maiin (k. 233H.L.), amesema kuhusu Seifi “mapokezi yake ni dhaifuna hazifai."2. Nasai (k.303H.L.) katika sahih amesema, "mapokezi yake ni dhaifu,

zisithaminiwe kwa sababu hakuwa wa kutegemewa na hakuwa mwaminifu."3. Abu Dawuud (k.316H.L.), "Hana thamani, ni muongo."4. Ibn Abi Hatam (k.327H.L.), "Wamezitelekeza mapokezi yake."5. Ibn al-Sakan (k.353H.L.), "Ni dhaifu."6. Ibn Udai (k.365H.L.), "Ni dhaifu, baadhi ya mapokezi yake ni maarufu bado

nyingi ya ngano zake zinatweza na hazifuatwi."7 Ibn Hibban (k.354H.L.), "Katika mapokezi yake, ametaja majina ya watu

waaminifu, lakini wanasema alishutumiwa kwa uasi na ngano za kuzua."8. Hakim (k.405H.L.), "mapokezi yake zimetelekezwa, alishutumiwa kwa uasi."9. Katib al- Baghdad…10. Abin Abd al-Bir (k.463H.L.) alisimulia kutoka kwa Abi Hayan kwamba

"mapokezi yake Seif zilitelekezwa, tulikuwa tukizitaja kwa ajili ya elimu tu."11) Safiud Din (k.923H.L.) "Alionekana dhaifu."12) Firuuzabadi (k.817H.L.) katika Tuwalif ametaja, "Seif pamoja na hao

wengine akisema ni dhaifu."13) Ibn Hij'r (k.852H.L.), baada ya mapokezi yake mamoja kutajwa, "kwamba

imesimuliwa na wasimuliaji dhaifu, dhaifu zaidi yao wote, ni Seif."

42

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Haya ndiyo maoni ya waandishi wa wasifu juu ya Seif na ngano zake. Sasa hebutuziangalie ngano zenyewe. Na kwa kufanya hivyo itabidi turejee kwenye kitabucha historia cha Tabari miongoni mwa vingine kwa sababu kina tarehe za mwan-zo kuliko vinginevyo na kilichorejewa zaidi katika vitabu vya historia. At-Tabariamesimulia nyingi ya ngano za Seif akinakili kutoka kwenye vitabu vyake viwili, al-Futuuh wal Radah na al-Jamal. Pia amesimulia kutoka kwenye mapokezi yakekuhusu Saqifa na kifo cha Uthman. Hivyo kuzifany mapokezi yake ni rejeamashuhuri, zinazotajwa kwenye historia zote za Kiislam hadi leo hii.

Tutaiangalia historia ya Tabari kwanza na kisha wasimuliaji wengine waliomtege-mea Seif katika simulizi zao na tutalinganisha na kutofautisha ngano zake nanyinginezo ili kujua ni mbinu gani alizotumia katika kuzighushi na tathmini yangano zake.

43

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

1. TUKIO LA JESHI LA USAMA

KAMA LILIVYOSIMULIWA NA SEIF

NA WENGINEO MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

44

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

JESHI LA USAMA

Tabari (juz.3.uk.212, juz.1,uk.1849-50 EUR), na Ibn Asakir (juz.1,uk.427), kuhusumatukio ya mwaka 11 wa Hijiria, historia iliyoandikwa ya Jeshi la Usamailiyosimuliwa na Seif ni kama ifuatavyo:

NGANO YA SEIF

"Mtume wa Mwenyezi Mungu, kabla ya kifo chake, alikusanya pamoja jeshi chiniya uongozi wa Usama. Umar Ibn Khatab alikuwemo ndani ya jeshi hilo. Kabla yajeshi hilo halijatoka hata nje ya mipaka ya mji wa Madina, Mtume wa MwenyeziMungu akafariki. Usama akamtuma Umar kwenda kwa mrithi wa Mtume (Khalifa)kuchukua ruksa ya jeshi hilo kurudi Madina. Masahaba wa Mtume, waliokuwemokwenye jeshi hilo, walimwambia Umar amuombe Abubakr amuondoe Usama naachague kiongozi mwingine." Abubakr akaruka mbele na kumkamata Umarkwenye ndevu zake akisema, "Ewe Ibn Khatab, mama yako akalie kwenye kitan-da chako cha mauti. Alikuwa ni Mtume mwenyewe aliyemchagua Usama kuwakiongozi wa jeshi, bado unanitaka mimi nimuondoe na nichague mtu mwinginebadala yake."

Abubakr kisha akaliamuru jeshi kuondoka na akawaangalia wakiondoka, akiwaa-ga akisema, "Nendeni, Mwenyezi Mungu akuangamizeni kwa mauaji na tauni."

Hii iliyopita imesimuliwa na Seif kuhusu jeshi la Usama. Lakini wengine wamese-ma ngano yenyewe ni kama ifuatavyo:

MASIMULIZI YA WENGINE MBALI NA SEIF.

Katika mwaka wa 11 wa Hijiria, siku ya Jumatatu, kukiwa kumebakia siku nne zamwezi wa Safar, Mtume aliwaamuru watu wajiandae kwa vita na Warumi. Siku iliy-ofuata alimuamuru Usama kuongoza jeshi hilo akimwambia, "Nenda sehemuambayo baba yako aliuawa shahidi, na uwashambulie." Siku ya Jumatano Mtumemwili ukawa na joto kali na maumivu ya kichwa. Siku iliyofuatia, Alhamisi, Mtumemwenyewe akatengeneza bendera ya vita na akamkabidhi Usama. Usama ali-ichukua bendera na akaondoka Madina, akipachagua Jurf kama sehemu yakambi.

Wakubwa wa makundi ya Muhajir na Ansari, Abubakr, Umar Ibn Khatab, AbuUbaydah Jarrah, Sa'd Waqqas Said Ibn Azid na wengineo waliamriwa kuundajeshi chini ya uongozi wa Usama. Kwa vile Usama alikuwa kijana mdogo sana,kulikuwa na vipingamizi kuhusu kufanywa kwake kiongozi wa jeshi kwa kupen-delewa kuliko wale watu wazima wa Waislamu Muhajir.

45

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Mtume wa Mwenyezi Mungu akavisikia vipingamizi hivi na akatoka nje ya nyumbayake, kichwa chake kikiwa kimefunikwa na kitambaa, na taulo mabegani mwake,kwa vile alivyokuwa mgonjwa. Alivyopanda juu ya mimbari akawaambia watuakisema, "Ni habari gani hizi nilizosikia kuhusu Usama, ambaye amechaguliwakuwa kamanda. Mlifanya upinzani kwa baba yake sasa mnampinga yeye. WallahiUsama ana uwezo wa kushika nafasi hii, kama alivyokuwa baba yake." Mtumekisha akashuka kutoka kwenye mimbari, na Waislam waliokuwa wanakwendakambini huko Jurf wakasema kwa heri.

Afya ya Mtukufu Mtume ilizidi kuzorota, na Usama alimtembelea wakati Mtumealipokuwa hana uwezo wa kuongea aliweza tu kumbusu Usama busu la kwa heri.Jumatatu iliyofuata, Mtume alipata nafuu, na alimpokea Usama, akisema, "Nenda,kila la kheri juu yako." Usama alirudi kambini na kuamuru msafara kuondoka.Alipokuwa anataka tu kupanda farasi wake, ujumbe ukaja kutoka kwa mama yakeukisema Mtume ni mgonjwa sana.

Usama, Umar na Abu Ubaydah walirudi Madina, na siku ile ile Mtume akafariki.Baada ya kifo cha Mtume, wakati Abubakr alipokuwa Khalifa, alimuamuru Usamakuchukua kazi ile ile kama alivyoamrishwa na Mtume, (Ibn Asakir, juz.1, uk.433).

Katika ukurasa wa 438 Ibn Asakir pia anasema, "Abubakr alimwambia Usamakwamba Mtume alikwishatoa maagizo yote muhimu, na haongezi chochote juuyake." Abubakr hakuwasikiliza wale waliomshauri msafara ule uakhirishwe.

ULINGANISHO

Ulinganisho kati ya njia hizo mbili hapo juu za uandishi. Kuna baadhi ya mamboyanayofaa kutajwa juu ya uandishi wa Seif. Anasema:

1) “Jeshi hilo lilikuwa likivuka mpaka wa Madina wakati Mtume anafariki.” Seif ali-uongeza msitari huu katika kitabu chake kuficha ukweli kwamba kulikuwa naucheleweshaji uliozuia jeshi hilo kuondoka; na hapakuwa na vurugu kutokakwa hao wakorofi waliosababisha kukawia huko.Bado katika wakati akiwa nafahamu kamili Muhammad alikasirika kwamba jeshi limekawizwa, na akarudiaamri yake ya awali, "Jeshi la Usama lazima liondoke."

2) Seif anasema, "Wakati Usama aliposikia kwamba Mtume amekufa alimtumaUmar kwa mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu kupata ruksa ya kurudi kwajeshi hilo Madina." Maelekezo mengine yanasema, "Usama alisikia kwambahali ya Mtume ilikuwa mbaya sana, hivyo akaenda Madina na Umar, Abubakrna Abu Ubaydah. (Wengine wanasema Abu Ubaydah hakuwa pamoja nao.)Baada ya kifo cha Mtume, na baada ya kuchaguliwa kwa Abubakr huko Saqifa,na uchaguzi wake wa mwisho hapo Msikitini, ndipo akashughulika na jeshi laUsama."

Hapa tena Seif anarudisha nyuma urithi wa Abubakr, kuufanya uonekane

46

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kwamba alichaguliwa kuwa mrithi (Khalifa) kabla ya kifo cha Mtume.3) Seif anasema, "Ansar walimuomba Abubakr kumuondoa Usama na kuchagua

kamanda mwingine wa jeshi hilo." Ibn Asakir (juz.1,uk.438) na wanahistoriawengine wanasema, "Muhajirina wa mwanzo walimuomba Mtume ambadil-ishe Usama." Hapa tena Seif amebadilisha jina la wapendekezaji kutokaMuhajir kwenda Ansar kuridhisha Serikali ya wakati huo ambayo ilikuwa yakundi la Muhajirina.

Seif anasema: "Abubakr alimpa Usama maelekezo kumi." Wanahistoriawengine wanasema:Abubakr alisema kwamba Mtume alitoa maagizo muhimuna hakuwa na haja ya kuongeza chochote juu yake." Seif anasema: "Abubakralimshika Umar kwenye ndevu zake kwa sababu alileta ujumbe wa Ansar,"ingawa mjumbe hawezi kulaumiwa. Seif anasema, "Abubakr alililaani hilo jeshina akategemea wataangamizwa kwa tauni." Seif akiwa ni muasi alitakakufanya dhihaka ya Uislam kama dini, na vile vile kumfurahisha Khalifa wawakati wake. Ngano zilizozushwa na Seif hazina msingi, na mashujaa walio-tajwa ndani yake hawakuwapo kamwe kwani walikuwa ni utungo tu wa fikirazake. Tutaelezea kwa ufasaha zaidi baadae.

BAADHI YA MASAHABA WATAMBULISHWA

Wakati umefika sasa kwetu kuwatambulisha kwa ufupi Masahaba tuliowatajampaka hapa wa 1 na wa 2. Hakuna haja, kwa kweli, ya kusema chochote kuhusuAbubakr na Umar, Makhalifa wa kwanza na wa pili wanaofahamika sana.

3) Abu Ubaydah Jarrah Amer, mwana wa Abdullah Ibn Jarrah na Umaymah, bintiya Ghunm Ibn Jabir. Abu Ubaydah alikuwa mmoja wa waliosilimu mwanzonikabisa kuingia Uislam kutoka kabila la Quraish, na alihama mara mbili kuto-ka Makkah. Abubakr alimfanya kamanda wa jeshi lililotumwa kwenda Syria.Alikufa kwa tauni na akazikwa huko Jordan.

4) Sa'd Waqqas, Abu Ishaq, mtoto wa Malik, kutoka kwenye familia ya Zuhra yakabila la Quraish. Alikuwa mtu wa saba kuingia Uislam. Alishiriki katika Vitavya Badri na vita vingine vyote vilivyofanywa na Mtume. Alikuwa Mwislam wakwanza kutupa mshale kwa maadui, kamanda mkuu wa majeshi yaliyotekaIraq. Umar alimchagua kuwa Gavana wa Kufa. Sa'd alikuwa mmoja wawajumbe sita wa kamati iliyoteuliwa kumchagua Khalifa baada ya Umar.(Alikuwa ni Umar aliyeamuru kamati hiyo ianzishwe mara moja baada yakuchomwa vibaya na Abu Lulu). Sa'd alirudi kwenye makazi yake Aqiq karibuna Madina, baada ya Uthman kuuawa. Alikufa wakati wa utawala waMu'awiyah na alizikwa Baqi kwenye makaburi ya Madina.

5) Said Ibn Zaid. Anatoka kwenye ukoo wa Adi wa kabila la Quraishi, na ni bina-mu yake Umar Ibn Khatab. Umar alimuoa Atikah, dada yake Said, naye Saidakamuoa Fatimah, dada yake Umar. Said na Fatimah waliingia Uislam kabla

47

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

ya Umar. Wakati Umar aliposikia kwamba dada yake amekuwa Mwislamu,alikwenda nyumbani kwake, na akampiga makofi kwa nguvu sana uso wakempaka ukaanza kutoka damu. Umar alisikitika sana kwa kitendo chake chapupa, na papo hapo yeye mwenyewe akaukubali Uislam. Said alikufa mwakawa 50 au 51 H.L. na alizikwa Madina.

6) Usama. Baba yake Usama alikuwa ni Harithah, mtumwa aliyeachwa huru naMtume Muhammad. Mama yake alikuwa Ummu Ayman, mtumwa waMuhammad aliyemuacha huru. Usama alizaliwa mwanzoni mwa Uislam, naalikufa wakati wa utawala wa Mu'awiyah.

BUSARA ZA MUHAMMAD KATIKA KITANDA CHAKE CHA MAUTI

Katika dakika zake za mwisho za maisha yake Mtume alifanya maajabu, aliwaon-doa watu wazima wote na kumuacha Ali pekee Madina. Alisisitiza kuwapelekaViongozi wa vikundi wote kwenda Syria, mbali na moyo wa Uislam, na akamuwe-ka mtu ambaye wazazi wake ni watumwa, kuwa kiongozi wa watu wazima hao.(Hili litaelezwa baada ya kuyachunguza matukio yaliyotukia baada ya Mtume waMwenyezi Mungu kufariki.)

48

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

2. SEIF NA TUKIO LA SAQIFAH

KAMA ILIVYOELEZWA NA SEIF

NA WENGINEO MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

49

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

SEIF NA TUKIO LA SAQIFAH

Ngano ya mjadala na mabishano ya mwanzoni huko Saqifah yanayohusu urithi waAbubakr kama Khalifa wa Mtume ni moja kati ya ngano za kuvutia zilizosimuliwana Seif ambayo inahitaji uchunguzi makini. Seif anasema:

2.1) Isabah (juz.2,uk. 230). "Wanasema kwamba Qa'qa Ibn Umar amesema,'Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokuwa anakufa, nilikuwepo. Mtummoja alikuja Msikitini wakati wa sala ya mchana, na akawaambia baadhi yawatu kwamba Ma-Ansari wanakwenda kumchagua Sa'd Ibn Ubaydah kwakauli moja, kama Khalifa, na kupuuza mkataba wa Mtume wa MwenyeziMungu. Muhajirina waliguswa sana na hili.'"

2.2) Tabari (juz.3,uk.201). Matukio ya mwaka wa 11. Msimuliaji alimuuliza Amr IbnHuraith, 'Ulikuwepo wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipofariki?' Jibulilikuwa ndiyo. Swali la pili lilikuwa, 'Ni siku gani Abubakr alichaguliwa?', najibu likawa, 'Siku hiyohiyo alipokufa Mtume, kwa sababu watu hawakutakakuchangukana ingawa kwa nusu siku.' Kisha akauliza, 'Kulikuwa na upinzaniwowote?' 'Hapana, ulitoka kwa waasi tu au wale waliokaribia kuwa waasi,''Kuna jamaa yeyote wa Muhajiriin aliyempinga?' aliulizwa tena, na jibu likawa,'Hapana, wote walitoa kiapo cha utii kwa Abubakr kwa hiari kabisa, mmojabaada ya mwingine.'"

2.3) Tabari, kuhusu Ansar kumuunga mkono Sa'd Ibn Ubaydah, na kumkataa:kwao Abubakr, anasema: "Zahhak Ibn Khalifah amesema kwamba Hubab IbnMunzir alisimama na upanga mkononi mwake, akisema, "Mimi ni gongo lakuegemewa juu yake, mimi ndiyo jiti ambalo ngamia wanajikunia pale mahaliwanapolala. Mimi ndiyo mti mkubwa ambao chini yake wanatafuta kivuli nahifadhi. Siogopi madhara kutoka kwenye upepo wowote. Mimi ndiye baba wawatoto wa simba ndani ya zizi lao."

Umar akaruka haraka mbele na kuugonga upanga huo kutoka mkononi mwaHubab. Umar akauokota huo upanga na kumshambulia nao Sa'd Ibn Hubab, nawatu wengine waliokuwa wakimpinga Sa'd, walimuunga mkono Abubakr, kum-saidia kushinda uchaguzi huo.

Uungaji mkono wa Ansari kwa Sa'd ulikuwa ni kosa kama lile la wakati wa ujahiliawa kabla ya Uislam. Bahati nzuri, Abubakr alimpinga Sa'd kwa nguvu naakayumbisha uungaji mkono wa watu kuja kwake. Wakati watu walipomshambu-lia Sa'd, mtu mmoja alipiga kelele kwamba ameuawa. Umar akasema, 'MwenyeziMungu amuue, ni mnafiki.' Kisha Umar akauchukua upanga huo na kuuvunjakwenye jiwe."

50

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

2.4) Tabari (baada ya ngano hiyo hapo juu): Mubashshir amesema kwamba Jabiramesimulia kwamba "Sa'd alimwambia Abubakr, 'Enyi Muhajir mlikuwa nawivu juu ya nafasi yangu kama mkuu wa nchi, na kwa wewe Abubakr, ulini-lazimisha nikutii, kwa msaada wa kabila lako mwenyewe.' Muhajirina waka-jibu, 'Kama tulikulazimisha kuondoka kwenye mkusanyiko ulikuwa na haki yakutupinga, lakini tunakulazimisha kubaki ndani ya mkusanyiko. Sasa kamautapinga chombo cha jumla ya Waislam, utakatwa kichwa.'"

2.5) Tabari. "Ali alikuwa nyumbani kwake wakati habari zilipomfikia kwamba watuwametoa kiapo cha utii kwa Abubakr. Akiwa bado kwenye nguo yake yausiku, alikurupuka kutoka nje, kwenda mara moja kwa Abubakr, na waka-peana mkono naye. Baadae, aliletewa nguo zake na akazivaa."

2.6) Tabari: "Abubakr alitoa hotuba mbili ndefu siku iliyofuatia kifo cha Mtume waMwenyezi Mungu. Alizungumzia zaidi juu ya mashaka ya dunia, maangamioya mwanadamu, na Siku ya Qiyammah. Alisisitizia sana shetani aliyekuwanaye akisema, 'Kuna shetani wa maovu aliyeko ndani yangu. Niepukeniwakati nguvu hii ya uovu inaponizidi, ikiwa nitakuwa sipori tu mali zenu, balihata nafsi zenu.'"

2.7) Tabari: Mubashshir Ibn Fuzail alisimulia kwamba Jubair (mlinzi wa Mtume)alisema kwamba baba yake alisema: "Khalid Ibn Saiid Ibn Aas alikuja Madinakutoka Yemen, mwezi mmoja baada ya Mtume wa Uislam kufariki. Alikuwaamevaa koti la hariri alipokutana na Umar na Ali. Umar akakemea, "Chanenikoti la Khalid vipande vipande kwani amevaa hariri wakati wa amani.' Khalidakageuka na akaongea na Ali, akisema, 'Ewe Abul Hasan, Enyi wana wa AbdManafi mmeachia urithi wa Mtume, hivyo mmeshindwa. Enyi wana wa AbdManafi ni ninyi tu mnaostahili kuwa warithi wa Mtume.' Umar akasema, 'EweKhalid, Mungu aukate ulimi wako; waongo daima watatumia maneno yakodhidi ya Uislam, na hii hatimae itakuwa dhidi yao wao wenyewe.' Umarbaadae akamweleza Abubakr kuhusu kukutana kwake na Khalid. Muda mrefubaadae, Umar alimzuia Abubakr kumuweka Khalid kuwa kamanda wa jeshilinalopigana dhidi ya waasi. Umar alimwambia Abubakr kwamba Khalidalikuwa mbaya, ambaye alisema uongo ambao umesababisha mnon'gonodaima na kwa hiyo msaada wake usihitajike. Abubakr alimpeleka Khalid Syriakama msaidizi wa Kamanda wa Jeshi huko Tima; kwani Abubakr alimsikilizaUmar nusunusu."

51

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

UCHUNGUZI JUU YA UKWELI WA NGANO KUHUSU SAQIFA KAMAZILIVYOANDIKWA NA SEIF.

1) Msimamo na tabia ya wasimuliaji.2) Yaliyomo kwenye ngano za Seif.

a) Seif amenakili ngano yake ya kwanza kutoka kwa Qa'qa Ibn Amr at-Tamimi.

Lakini Qa'qa ni mtu wa bandia aliyebuniwa na Seif, na ni katika kitabu cha Seif tundimo anamotokea. Hakuna dalili ya Qa'qa mahali pengine popote ila katika vitabuvile ambavyo waandishi wake wananakili kutoka kwa Seif. Baada ya Seif, kwabahati mbaya, wanahistoria wengine na waandishi wametaja sehemu, viwanja vyavita, mashairi na shughuli za kijamii za kumhusu Qa'qa, na wamemtaja kamammoja wa masahaba wa Mtume (tazama masahaba wa bandia).

Seif ameandika ngano yake ya nne kutoka kwa Mubashshir, ambaye jina lake hali-wezi kupatikana popote, ila ndani ya ngano za Seif.

Sakhr ni mtu mwingine wa bandia aliyebuniwa na Seif, na alitokea katika ngano zamwisho za Seif. Seif alimtambulisha kama mlinzi wa Mtume, na bado jina lakehalionekani popote katika habari za watu mashuhuri iitwayo "Nani ni nani".

b) Yaliyomo kwenye ngano za Seif. Seif alikuwa mahiri katika kutoa ngano zauzushi kama za kweli na katika kupotosha ngano za kweli kukidhi haja yake.Mfano mmoja ni anaposema, "Siku ile ambayo Mtume alikufa, mtu mmoja alikujaMsikitini na kusema, "Watu wanakwenda kumchagua Sa'd kama mrithi wa Mtumena kuvunja mkataba wa Mtume.' Katika kuisoma hii, mtu anapata picha kwambaMtume alichagua mrithi kabla hajafa, na kwamba lile kundi la Ansari lilikuwa linam-saliti Mtume." Seif vilevile anasema kwamba Usama alimtuma Umar kwa Abubakrbaada ya kusikia habari za kifo cha Mtume. Kwa kusema hivi anataka kujulishakwamba Abubakr alikwisha chaguliwa tayari kama Khalifa kabla Mtume hajafa.

MSIMULIAJI WA NGANO

Ule mkutano muhimu huko Saqifa, uliopelekea kuchaguliwa kwa Abubakr kamaKhalifa, ulikuwa ni jiwe la pembeni la madaraka kwa ajili ya Khalifa na Mu'awiyah.Seif, msimuliaji wa ngano, alipindisha matokeo ya mkutano huu kukidhi maoniyake binafsi. Tutayatazama matukio ya mkutano huo, yaliyoandikwa na wanahis-toria wasomi wa Sunni kabla ya kuchunguza maandishi ya Seif juu yake.

TUKIO LA SAQIFAH NA WANAHISTORIA WENGINE MBALI NA SEIF SAQIFAH NA ABUBAKR

Maandalizi kwa ajili ya mkutano wa Saqifa yalianza kabla ya kifo cha MtukufuMtume. Akiwa kwenye kitanda chake cha mauti, Mtume alijaribu kuwaondoa

52

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kwenye Makao Makuu ya Umma wa Kiislam wale Wakuu wa Vikundi, na aka-muweka Ali peke yake hapo Madina. Aliwaamuru kwa kurudiarudia viongozi haowaondoke Madina na kujiunga na vikosi viendavyo kwenye Uwanja wa Vita hukoSyria (Sham). Walipuuza amri ya Mtume na kwa makusudi kabisa wakakawizauondokaji wa jeshi hilo mpaka Mtume akafariki. Katika muda huu wa uchelewe-shaji, lilitokea tukio la ajabu lililobadilisha mwelekeo wa historia.

JE? MTUME ALIELEZA NIA YAKE KWA MAANDISHI?

Dakika za mwisho za Mtume zilikuwa zinakaribia. Madina ilikuwa katika hali yahofu. Kila mmoja alihisi kwamba yule kiongozi wa mwanadamu, alikuwa anaiagadunia milele. Mtukufu Mtume alikuwa na mpango kwa ajili ya muda huu kwawakati; ilikuwa akilini mwa Mtume awaweke mbali na Madina wale Wakuu wavikundi, lakini walikataa kuondoka. Wao pia walikuwa na mpango, na walikuwawakiyaangalia matukio kwa karibu sana. Walimzuia Mtume kuacha hati kwaWaislam kwa ajili ya uongozi wa mwanadamu.

Kwa mujibu wa Tabaqat cha Ibn Sa'd juz.2,uk.243-244, Umar Ibn Khatabmwenyewe anasema, "Tulikuwa kando ya Mtume na wanawake walikuwawamekaa nyuma ya pazia, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, 'Nioshenina maji mifuko saba ya ngozi iliyojaa, na nileteeni wino na karatasi kusudi niwezekuwaandikia ujumbe utakaokuzuieni msipotee.' Wale wanawake wakasema,'Mleteeni Mtume wa Mungu hicho anachokitaka.'" Maghrizi anasema kwambahaya yalisemwa na Zainab binti ya Jahash, mke wa Mtume, na wanawakealiokuwa nao. Umar akasema, 'Niliwaambia wanawake hao wanyamaze kimya,kwamba walikuwa ndiyo wanawake waliofumba macho yao na kujidai kulia wakatiMtume alipokuwa mgonjwa, lakini waliomkalia kooni alipokuwa mzima." Wakatihuo, Mtume akawaambia wale wanaume, 'Wanawake ni bora kuliko ninyi."

Katika Tabaqat, juz.2,uk.242, Ibn Sa'd ameandika kwamba Jabir alisema, "Mtume,katika kitanda chake cha mauti, alitaka karatasi na kalamu ili aweze kuandikaujumbe kwa watu wake, akiwapa maagizo nini cha kufanya, kusudi kwamba wasi-weze kupotea au kupotoshwa. Lakini watu walikusanyika hapo na kufanya ghasiampaka Mtume akaliacha wazo lake hilo."

Katika Musnad Hanbal, juz.1,uk.293, (sherehe ya Ahmad Shakir, Ngano 2676), IbnAbbas alisema, kifo cha Mtume kilipokaribia alisema, "Nileteeni fupa la bega lakondoo, na nitawaandikia ujumbe. Kisha baada ya kifo changu, hakuna watu waw-ili watakaotofautiana baina yao." Wale waliokuwepo walipiga makelele mengi namwanamke mmoja akauliza, "Hamuoni kwamba Mtume ataandika wosia?"

Ibn Abbas mahali pengine alisema kwamba Mtume katika maradhi yake yamwisho, alisema, "Nileteeni karatasi na wino niwaandikie ujumbe, ili kwamba ham-tapotea baada ya kifo changu." Umar Ibn Khatab akasema kwamba kulikuwa bado

53

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kuna miji, kama vile mji fulani na fulani, ya kuteka, na kwamba Mtume hatakufampaka awe ameichukua yote. Kama anakufa watasubiri kurudi kwake kama BaniIsrail walivyomngojea Musa. Zainab, mke wa Mtume kwa muda huu, akasema,"Hamuwezi kuona kwamba Mtume atatengeneza wosia?" Kisha pakawepo nakelele kubwa na ghasia na Mtume akasema, "Tokeni, nyote," kisha mara mojaakafariki.

Kutoka kwenye matukio tuliyotaja, na yale ambayo tutayaandikia, inakuwa wazikwamba licha ya udhaifu (wa afya) wa Mtume kabla ya kifo chake, aliitisha winona karatasi, lakini wale waliokuwepo wakasababisha ghasia kubwa kiasi kwambaMtume akaliacha ombi lake. Maelezo yetu yanayofuata yanaonyesha kwambakwa sababu ya mabishano ya makusudi na yasiyo na maana, Mtume hakuwa nanjia nyingine ila kuliacha wazo lake hilo.

Katika kitabu cha Sahih Bukhari, Ibn Abbas alisema, "Oh Alhamisi! Siku gani hii."Alikuwa na huzuni kiasi kwamba machozi yaliyotoka machoni mwake yalitiririkakwenye mchanga uliokuwa chini yake. Pale ugonjwa wa Mtume wa MwenyeziMungu ulipozidi, Mtume akasema, "Nileteeni karatasi na wino ili niwaandikieujumbe, utakaokuokoeni na kupotea nitakapokuwa nimeondoka." Kisha pakawana mabishano mengi na majadiliano miongoni mwa wale waliokuwepo pale,ingawa kusingekuwa na mabishano mbele ya Mtume. Wengine wakasema kwam-ba Mtume alikuwa anaongea kwa kuweweseka. Kisha Mtume akasema,"Niondokeeni, nitahitaji faragha kwa muda huu."

Katika sehemu nyingine Ibn Abbas amemtambulisha yule mtu aliyetamka kaulihiyo. Anatuambia katika kitabu cha Sahih Bukhari kwamba Mtume katika kitandachake cha mauti alisema, "Msipoteze muda. Ngojeni niwaandikie jambo lakuwaokoeni msipotee." Umar ambaye alikuwa miongoni mwa mkusanyiko huoakasema, "Maradhi yameizonga akili ya mtu huyu, Qur'ani, Kitabu cha Allah, kipopamoja nasi, na kinatosha." Kisha likaanza zogo na mabishano. Mtume alikasirikana akasema, "Tokeni nje, msibishane na kupingana mbele yangu."

Katika vitabu: Musnad Hanbal na Tabaqat, imeelezwa kama ifuatavyo:

"Waliongea upuuzi mwingi mpaka ukamfanya Mtume ahuzunike." Baadae IbnAbbas alikuwa akisema, "Ulikuwa ni muda mfupi wa msiba mkubwa kwambawalipozungumza upumbavu walimzuia Mtume kuandika ujumbe huo."

Katika ngano zote za hapo juu, hakuna yeyote ila Umar aliyetajwa kama ndiyealiyemzuia Mtume kuandika ujumbe huo. Umar ndiye aliyewaambia wanawake,"Nyie ni wake za mtu." Alikuwa ni Umar aliyewakemea kwa ukali wake za Mtume,akizungumza nao kwa namna isiyo ya adabu. Umar alitoa kauli hii ya kifedhuli kwawanawake hawa pale waliposema, "Leteni karatasi na wino, Mtume anatakakuandika." Umar ndiye aliyesema, "Kama Mtume atakufa nani ataiteka miji yaWarumi?" Umar ndiye mtu, ambaye baada ya kuona wengi wanapendelea kukid-hi ombi la Mtume na kumletea karatasi na wino, akasema, "Maradhi yamemzidi

54

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

mtu huyu. Anaweweseka. Qur'ani, Kitabu cha Allah kipo pamoja nasi - kinatosha."Alikuwa ni Umar aliyesema kwamba Mtume anaweweseka.Kwa maongezi kama hayo alifanikisha lengo lake kwa sababu hata kama wenginewaseme, kwa nini Mtume hakusisitiza kuchagua mtu kwa maandishi? Tutambuehata hivyo kwamba hata hati ya maandishi isingekuwa na thamani sana, kwasababu kwa shutuma za Umar wangesema maandishi hayo yamefanywa wakatianaweweseka na akiwa hajui anachokifanya. Hili limesimuliwa pia na Ibn Abbas.

Kwa mujibu wa mapokezi kutoka kwa Ibn Abbas, mtu mmoja alimfuata Mtume naakamuuliza kama alikuwa bado anahitaji hiyo karatasi na wino. Mtume akajibu,"Baada ya hili kisha kuna nini?" Ikimaanisha kwamba baada ya mtu kusemakwamba anaweweseka itachukuliwa kwamba kitu chochote alichoandika kitakuwahakina thamani, kwa sababu kiliandikwa wakati wa weweseko. Inaweza kuonekanikwamba Umar aliufanya mpango wake wa kifitna kwa werevu sana kwa kutoakauli ile; na kwamba alimzuia Mtume kuandika ujumbe wa kuwaokoa Waislamkutokana na kupotea baada ya kifo chake.

Baada ya maelezo hayo hapo juu pengine Umar angeulizwa swali lifuatalo, "Ulithubutu kumshutumu Mtume kuzungumza akiweweseka, kwa nini basi hukupin-ga wosia wa Abu Bakr alioutolea imla wakati wa kuweweseka?"

Katika Tabaqat, juz.4,uk.52, Abubakr akiwa kwenye kitanda chake cha mauti,alimpokea Uthman peke yake. Alimwambia aandike, "Kwa Jina la Mwingi waRehma, huu ni wosia wangu. Pendekezo kwa Waislam kutoka kwangu mimiAbubakr Ibn Quhafa." Mara kufika hapa alipotelewa na fahamu, hivyo Uthmanakaendelea kuuandika wosia, kwa majisifu hayo hayo, kama ifuatavyo,"Nimeamua kumfanya Umar kuwa mrithi wangu, Khalifa wangu. Nimewafanyienivizuri." Kufikia hapa Abubakr akazinduka na kusema, "Nisomee tena kile uli-choandika." Uthman akafanya hivyo, na Abubakr kisha akasema, "Allah Akbar.Uliogopa kwamba ningekufa bila ya kupata fahamu, Waislam wangekuwa hawanaKhalifa, na wangepotea." Uthman akaitika, na Abubakr akasema, "MwenyeziMungu akulipe vema kwa msaada ulioutoa kwa Waislam na Uislam."

Umar angeulizwa, jibu lako ni lipi kwa wosia wa Abubakr?" Umar alikuwa nyum-bani kwake, akiwa amezunguukwa na marafiki zake, akiwa amevalia na kusubirikutokea kwa mtumwa wa Abubakr akileta huo wosia, ambao yaliyomo ndani yakeyangefanywa rasmi. Umar aliipokea barua hiyo, na kisha akaihutubia hadhara hiyohivi, "Sikilizeni enyi watu! Tiini kile ambacho Khalifa wa Mungu amesema. Khalifaanasema amewafanyieni vizuri." Umar huyu huyu, aliyemzuia Mtume kuandikawosia wakati wa maradhi yake ya mwisho na akasema, "Mtu huyu anaweweseka- kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu," sasa anaikubali barua ya Abubakr,iliyoandikwa katika kitanda chake cha mauti kwenye hali ya kuweweseka. IbnAbbas kwa kweli alikuwa na haki ya kulia mpaka mchanga uliokuwa ardhini ukaloakwa machozi.

55

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

KIFO CHA MTUME (S.A.W.W.)

Wakati wa mchana siku ya Jumatatu, Mtukufu Mtume alifariki chumbani kwakehuko Madina. Umar alikuwepo, na Abubakr alikuwa kwenye makazi yake, Sanh,ambako ni maili moja kutoka Madina. Umar na Mughirah walipewa ruksa ya kuin-gia kwenye chumba ambamo mwili wa Mtume ulikuwa umelala. Umar akafunuanguo iliyokuwa imefunika uso wa Mtume, akisema, " Mtume amezimia." Mughirahakamwambia Umar wakati wanatoka chumbani humo, "Lakini unajua kwambaMtume wa Allah alikuwa amekufa." Umar akamwambia, "Unadanganya, Mtumehakufa. Wewe ni mkorofi. Mtume wa Allah kamwe hatakufa mpaka awaangamizewanafiki wote." Umar aliwatisha wale wote waliosema Mtume amekufa, kwa vifovyao wenyewe. Akatangaza, "Baadhi ya wanafiki wanadhani Mtume wa Allahamekufa, hakufa. Amekwenda kwa Mola kama vile Musa alivyofanya kwa sikuarobaini. Watu walifikiri Musa alikufa lakini alirudi na hivyo Mtume wa Allah ataru-di,na atakata mikono na miguu ya wale ambao walifikiri amekufa." Umar akasema,"Nitamkata kichwa yeyote anayesema kwamba Mtume wa Allah amekufa, Mtumeamepaa Mbinguni." Ibn Makhtum Amr Ibn Qais ndipo akasoma kifungu cha Qur'anikinachosema, "Muhammad ni Mtume kama wale waliokufa kabla yake. Mtageukiakwenye njia zenu za zamani kwa sababu amekufa? Yeyote mwenye kugeukanyuma hamdhuru chochote Mwenyezi Mungu, lakini Mwenyezi Mungu atawalipawaumini." Abbas, ami yake Mtume akasema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu kwahakika amekufa, nimeuona uso wake na umefanana na nyuso za watoto wa AbdulMuttalib waliokufa."

Kisha akawauliza watu, "Hivi Mtume alisema chochote kile kwenu kuhusu kifochake? Kama ndivyo, tafadhali tujulisheni." Watu wakajibu kwamba hawajui cho-chote. Kisha akamuuliza Umar, "Unajua chochote?" Lakini Umar akajibu kwambahakujua chochote.

Ndipo Abbas akawahutubia watu akisema, "Shuhudieni, kwamba hakuna hatammoja anayejua chochote ambacho Mtume amekisema kuhusu kifo chake. Naapakwa Mola, ambaye ni mmoja tu na hakuna anayefanana kama Yeye, kwambaMtume wa Allah amekufa." Umar bado alikuwa anarindima kwa hasira na kufanyavitisho, lakini Abbas aliendelea akisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu, kama mtumwingine yeyote anapaswa kufa na kupata maradhi; na amekufa. Mzikeni bilakukawia. Hivi Mungu anatuua sisi mara moja, na amuue Mtume wake mara mbili?Kama unayosema ni kweli, Allah anaweza kumfufua toka kaburini. Mtume wa Allahamemuonyesha mwanadamu njia sahihi ya kwenye ustawi na uongofu katika uhaiwake." Umar aliendelea kukemea, na sasa alikuwa anatokwa na povu mdomonikwa ukali wake. Salim Ibn Ubaid ndipo akaenda kwa Abubakr na kumueleza kina-cho tokea. Alikuja Madina na akamuona Umar amesimama pale na kutishia watu,akisema, "Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko hai. Hakufa. Atatoka chumbani kwakena kuwakata mikono wale wanaoeneza uongo juu yake, atawakata vichwa,atawanyonga." Pale Umar alipomuona Abubakr, alitulia; Abubakr akamtukuza

56

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Mungu akisema, "Kwa wale wanaomuabudu Mungu, Mungu yuko hai, lakini kwawale wanaomuabudu Muhammad, Muhammad amekufa."

Kisha akasoma kutoka kwenye Qur'ani, "Muhammad alikuwa ni Mtume. Kablayake wamepita mitume wengi." Umar akauliza kama hicho kilikuwa ni kifungu kuto-ka kwenye Qur'ani na Abubakr akathibitisha kwamba ndivyo. Lakini hotuba yaMughira, kule kusoma toka kwenye Qur'ani kwa Amr Ibn Qais na Abbas, ami yakekufafanua, vilishindwa kumshawishi Umar kwamba Mtume alikuwa amekufa, laki-ni akamsikiliza Abubakr kwa ukimya.

Hebu na tusikie simulizi kutoka kwa Umar mwenyewe. "Ninaapa kwa Allah,nilipomsikia Abubakr akisoma ile Aya magoti yangu yalilegea hivyo kwamba nil-ianguka chini, nisiweze kuamka, na nilitambua kwamba Mtume wa MwenyeziMungu amekufa." Hivi alikuwa Umar siku hiyo, amechanganyikiwa kwa kumpotezaMtume wa Mungu, kwamba mpaka akashindwa kujimiliki mwenyewe; na ni kwelikwamba alikuwa mwenda wazimu siku hiyo kama baadhi ya wanahistoriawalivyoandika? Hatuyaamini mambo haya, kwani tunaijua sababu nyuma yakuubadili ukweli.

Ibn Abil Hadid anasema, "Wakati Umar alipokijua kifo cha Mtume, akawa na wasi-wasi kama kutakuwa na mabishano kuhusu mrithi wa Mtume. Aliogopa kwambakundi la Ansari au wengineo wangepata madaraka, hivyo akazusha mashaka naakaonyesha ukaidi wa kukubali kifo cha Mtume, kama ulinzi wa Imani mpaka kufi-ka kwa Abubakr."

Ibn Abil Hadid alikuwa sawa, kwa sababu Umar aliogopa kwamba Ali angewezakushinda uchaguzi huo. Kulikuwa na wagombea watatu tu wa urithi huo, na Umaralimuunga mkono mgombea wa tatu, ambaye ni Abubakr. Wagombea watatu haowalikuwa ni:

1) Ali Ibn Abi Talib, aliyekuwa akiungwa mkono na wafuatao:

a. Bani Hashim, ule ukoo wa Mtume.b. Abu Sufian, kiongozi wa upinzani kabla ya kubadilika kuwa

Mwislamuc. Khalid Ibn Saeed Amawi, Bara Ibn Azib Ansari, Salman, Abu Dhar,

Miqdad na masahaba mashuhuri wengine wa Mtume wa MwenyeziMungu.

2.) Sa'd Ibn Ubaidah Ansari: ambaye alikuwa mgombea wa kabilala Khazraj (kundi la Ansari).

3) Abubakr ambaye waungaji mkono wake walikuwa Umar, Mughira Ibn Shu'ba,na Abdur-Rahman Ibn Auf. Ali na Abubakr walikuwa na nafasi nzuri ya kushin-da uchaguzi huo, kwa vile mgombea wa pili alitoka kundi la Ansari na hakuwana uungwaji mkono kutoka kwa Muhajirina. Kama Ali angekuwepo kwenye

57

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

uchaguzi huo baada ya mazishi ya Mtume, angeweza kupata kura nyingi zaidiya Abubakr, kwa sababu Muhajirina, Ansari na kabila lote la Abd Manafiwalikuwa upande wake. Kwa hiyo yote yale aliyofanya Umar (Abu Hafsa),kabla na baada ya kifo cha Mtume, yalisababishwa na woga wake kwamba Aliangewekwa madarakani.

Ukweli ni huu: Kama kifo cha Mtume kimemchanganya sana Umar, angebakia nakusaidia kwenye maandalizi ya mazishi, badala ya kusema kwamba Mtume haku-fa, na kukimbilia Saqifah kuchagua mrithi wa Mtume.

Ibn Hisham anasema, "Wakati Umar na Abubakr (masheikh wawili hawa) walipo-jua kifo cha Mtume, Umar alimwambia Abubakr, "Twende tukaone Maansariwanafanya nini?" Mwili wa Mtukufu Mtume ulikuwa umelala chumbani mwake nakwa mujibu wa Tabari, Umar na Abubakr walimwacha Ali kando ya kitanda chaMtume, akimtayarisha kwa mazishi, na wakaenda Saqifah. Wakiwa wamo njiani,walikutana na Ubaidah Jarrah na akaenda nao Saqifah.

Ma-Ansari walikuwa Saqifah na wakaungwa na Muhajirina, hakuna yeyote, ilaukoo wake, waliomsaidia katika matayarisho ya mazishi ya Mtume.

Abi Zuwaib Huzali anasema, "Nilifika Madina na kuwakuta watu wanalia na kuto-ka machozi kama vile mwanzoni mwa hija. Nikauliza sababu, wakaniambia kwam-ba Mtume alikuwa amekufa. Niliharakisha kwenda Msikitini lakini sikukuta mtupale. Mlango wa chumba cha Mtume ulikuwa umefungwa, na nikaambiwa kwam-ba alikuwa yupo chumbani mwake na familia yake ikiwa imemzunguuka. Nikaulizawatu wote walikuwa wamekwenda wapi, na nikaambiwa kwamba wamekwendaSaqifa kujiunga na Ansari. Watu pekee waliobaki nyumbani kwa Mtume kumta-yarisha kwa mazishi walikuwa, ami yake Abbas, Ali Ibn Abi Talib, Fadhil Ibn Abbas,Qathm Ibn Abbas, Usama Ibn Haritha na mtumwa wake Saleh. Ali akiwa amevaashati tu, alimbeba Mtume kifuani kwake. Abbas, Fadhl na Qathm walimsaidia Alikumgeuza Mtume. Usama na Saleh walimmwagia maji, na Ali alimuosha Mtume.Uas Ibn Khawali Ansari alisimama karibu, akiangalia."

HAWA WAGOMBEA KABLA YA MAZISHI YA MTUME (S.A.W.W)

Kampeni ya nyumba hadi nyumba kwa ajili ya mrithi wa Mtume ilianza kabla yamazishi yake. Ali alikuwa mmoja wa wagombea hao. Ibn Sa'd ameandika katikaTabaqat yake kwamba Abbas alimwambia Ali, "Nitapeana mikono na wewe had-harani kama ishara ya kiapo cha utii, na kuwahimiza wengine kufanya vivyo hivyo."

Masoud anasema kwamba Abbas alimwambia Ali, "Ngoja nikupe mkono wa kiapoewe mwana wa ndugu yangu, ili kwamba pasiwe na mgogoro kuhusu wewe kuwamrithi wa Mtume." Dhahabi na wengine wanasema kwamba Abbas alisema,"Ngoja nikupe mkono wa kiapo, ili kwamba watu waseme kwamba ami yake na

58

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

familia yake wameushika mkono wa mpwawe; na mara uchaguzi utakapo kwishahauwezi kufutwa."Jawhari anasema kwamba Abbas alimlaumu Ali baadae, akimwambia, "WakatiMtume alipokufa, Abu Sufiani na mimi tulikujia, tukikutaka umuache mkuu wa ukoona mimi mwenyewe tupeane mkono na wewe. Kabila la Bani Hashim wangefanyavivyo. Pindi makabila ya Abd Manafi na Bani Hashim yangekuwa upande wako,urithi wako ungesimama imara. Lakini ulituambia tuakhirishe jambo hili mpakabaada ya mazishi ya Mtume."

Tabari anasema kwamba Abbas alimwambia Ali kwamba asipoteze muda, lakini Alialikataa kumsikiliza. Ali hakuwa na upungufu wa wanaomuunga mkono, lakinikwake yeye mazishi ya Mtukufu Mtume yalikuwa yenye umuhimu zaidi kwa wakatiule kuliko haja ya kushika mamlaka. Alikuwa akisita sana kushiriki katika harakatiza kabla ya uchaguzi wa mrithi wa Mtume huku Mtume akiwa amelala maiti nahajashughulikiwa. Kusita kwa Ali kunyakua mamlaka kulimfanya Abbas amlaumukwa kukawia kwake. Lakini kwa kweli ushauri huo na shutuma havikuwa na maanakwa sababu:

a) Mtukufu Mtume tayari alikuwa amemteua Ali kama mrithi wake kamabaadhi ya Waislam wanavyoamini; na kama Waislam wangetakakukubali kile ambacho Mtume amekisema, wasingesema alikuwaanaweweseka.

b) Kama mambo ya Waislam yangeachwa mikononi mwao wenyewena Mtume, uingiliaji wa Abbas ungewanyan'ganya Waislam haki yaoya kumchagua yeyote kama kiongozi.

MGOMBEA WA PILI WA URITHI WA MTUME

Mgombea wa pili alikuwa ni Sa'd Ibn Ubaidah ambaye, mbali na kuumwa kwake,aliletwa mpaka Saqifa. Alipewa kura ya kuwa na imani na Ansari. Alianza hotubayake kwa kumtukuza Allah, na kuwakumbusha watu jinsi gani Ansari walivyokuwawema na wenye msaada kwa Uislam na kwa Mtume, pia kwamba waliitunza hes-hima ya Mtume kiasi kwamba alikuwa na imani juu yao mpaka ile siku ya kifochake. Kisha akawaambia Maansari, "Ninyi lazima mlishughulikie hili jambo laurithi." Alishinda kura ya makubaliano ya kundi la Maansari, lakini baadhi ya watuwalishangaa kwamba uamuzi utakuwa vipi endapo watapingwa na kundi laMuhajirina, kwa sababu walikuja kutoka Makka na Mtume, na walikuwa nduguzake. Baadhi yao walijibu kwamba kiongozi mmoja angechaguliwa na Maansari,na mmoja na Muhajiriina, viongozi hao wawili wangefanya kazi pamoja. Sa'dalililalamikia hili akisema, halitawezekana.

59

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

MGOMBEA ALIYEFAULU

Katika kusikia kwamba watu wamekusanyika huko Saqifah, Abubakr na Umarwakaenda huko. Waliungwa humo njiani na baadhi ya marafiki zao ambao ni:Usaid Ibn Hudhair, Uwaim Ibn Saideh, Asim Ibn Adi ambaye alitoka kabila la al-Ajlan katika Ansari, Mughira Ibn Shu'bah na Abdur-Rahman Ibn Aufi. (WakatiAbubakr na Umar waliposhika madaraka, watu hawa walipendelewa sana.).

Abubakr alimpenda sana Usaid Ibn Hudhair zaidi kuliko Maansari wengine naUmar akimwita ndugu yake. Abubakr alionyesha mapenzi yake kwake baada yakufa kwake.

Pale Uwaim alipokufa, Umar alikaa juu ya kaburi lake na akasema, "Hakuna mtuyeyote duniani hapa anayeweza kusema ni mbora kuliko huyu mtu aliyelala katikakaburi hili." Abu Ubaidah aliteuliwa kama mkuu wa jeshi lililotumwa kupigana naFalme ya Warumi. Wakati Umar alipotaka kujichagulia mrithi, alijuta kwamba AbuUbaidah hakuwa hai, kumtaja kama Khalifa wa Waislam anayefuata.

Na kwa Mughira Ibn Shu'bah, Umar alitupilia mbali adhabu ya uzinifu kuhusu yeyena siku zote alikuwa miogoni mwa wakubwa wakati Umar alipokuwa Khalifa. Umarpia alimsaidia sana Abdur-Rahman Ibn Aufi, na akamchagua kama mtu maalumkatika kuchagua Khalifa wa tatu. Watu hawa ndiyo wale waliouacha mwili waMtume na hawakushiriki katika mazishi yake, badala yake walikimbilia Saqifahkuchagua Khalifa wa kwanza, na wakapambana na Ansari katika kutawalaWaislam.

Baada ya kumtuliza Umar pale Saqifah, Abubakr alimshukuru Allah na akasema,"Uislam ulianzishwa na Muhajiriina, na ndiyo watu wa kwanza duniani kumwabuduMwenyezi Mungu na kumuamini Mtume. Walikuwa marafiki na ndugu wa Mtume,kwa hiyo wana haki ya kumrithi. Hapana isipokuwa mtu dhalimu atakayebishananao." Kisha Abubakr akawasifu Maansari, akisema, "Hakuna yeyote isipokuwawale Muhajir wa mwanzoni walio karibu nasi kuliko ninyi. Wao watakuwa viongozina ninyi mtakuwa mawaziri."

Hubab Ibn Mundhar alisema, "Enyi Maansari, kuweni imara na muungane ilikwamba wengine watawatumikieni, na hakuna atakayethubutu kukupingeni.Vinginevyo watu hawa (Muhajirina) watafanya kwa mujibu wa mpango wa Abubakrambao mmeusikia hivi punde, tujichagulie wenyewe mtawala wetu na tuwaachewao wachague mmoja kwa ajili yao."

Umar akasema, "Wallah, watawala wawili hawawezi kutawala kwa wakati mmoja,mahali pamoja. Waarabu hawatakutiini ninyi (Maansari) kwa sababu Mtumealikuwa Muhajirina na kwa hili tunao ushahidi wa wazi. Ni wale tu ambaowameuacha waislamu watahoji kuhusu urithi kwenye urawala wa Muhammad."

60

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Hubab Ibn Mundhir akasimama tena na akazungumza na ile hadhara akisema,"Enyi Maansari, msiwasikilize watu hawa, Umar na marafiki zake. Watakuporenihaki zenu na kukunyimeni uhuru wenu wa kuchagua. Kama hawakubaliani nanyiwarudisheni nyumbani kwao, na muunde Serikali mnayotaka kuwa nayo. Wallah,mnastahili kuwa watawala kuliko mtu mwingine yeyote. Watu hawa (Muhajirin)ndiyo watu walewale ambao hawakumuamini Mtume kabla; na kama isingekuwakwa ajili ya woga walionao juu ya panga zenu, wasingejisalimisha kamwe kwenyeUislam." Kisha akaendelea kuonyesha uungaji mkono wake kwa Maansari kamawangeuhitaji kama lile gogo la mti ambalo juu yake ngamia wanajikunia, au kamajiti kubwa ambalo chini yake watu wanapata hifadhi wakati wa mvua. Kisha akase-ma, "Tutafanya vita kama ni lazima, na kulazimisha matakwa yetu juu ya walewanaotupinga."

Umar akasema: "Mwenyezi Mungu na akuue wewe," akimuangusha chini, akimpi-ga mateke, na kushindilia udongo kinywani kwake.

Abu Ubaidah ndipo akasema: "Enyi kundi la Ansari, mlikuwa wasaidizi wa kwanzawa Uislam, msiwe wasaliti wa kwanza."

Kisha Bashir Ibn Sa'd wa kabila la Khazraj na wa kundi la Ansari akazungumzaupande wa Kundi la Muhajirina katika kumpinga Sa'd Ibn Ubaidah. Viongozi hawawawili wa kundi la Ansari walikuwa washindani kabla hawajaingia Uislam. BashirIbn Sa'd akasema: "Enyi watu wa kundi la Ansari, sisi Maansari tuliwapiga wapa-gani, na tukausaidia Uislam, siyo kwa ajili ya heshima ya kidunia bali kwa kumrid-hisha Allah tu. Tusiutafute ukubwa. Muhammad alitokana na Ma-Quraish, hawaMuhajirina, na mmoja wa ndugu zake anastahili kuwa mrithi wake zaidi kuliko sisi.Naapa kwa Allah, kwamba sitabishana naye (Ali). Ninatumaini hamtabishanavilevile."

Abubakr kisha akasema: "Umar na Abu Ubaidah wapo kwa ajili yenu, thibitisheniyeyote kati yao kama kiongozi wenu." Lakini Umar na Abu Ubaidah wakajibukwamba madhali Abubakr alikuwepo, hawangeweza kuukubali uteuzi huu.

Abdur-Rahaman Ibn Aufi akasema: "Enyi Ansari, inakubalika kwamba ninyi ni wab-ora, lakini hakuna miongoni mwenu kama alivyo Abubakr, Umar au Ali."

Mundhar Ibn Arqam akasema: "Hatuukatai ubora wa hao uliowataja, hususanmmoja ambaye hakuna mtu awezaye kumkataa." Alikuwa akimzungumzia Ali.

Hapa, Maansari na baadhi ya watu wengine walikemea, "Hatumtaki yeyote ila Ali."

Kwa mujibu wa Tabari na Ibn Athir, pale Maansari walipotambua kwamba Abubakralikuwa karibu ashinde uchaguzi huo kwa msaada wa uungwaji mkono na Umar,wakasema kwamba Ali ndiye pekee waliyemtaka.

Zubair Ibn Bakkar akasema kwamba baada ya Maansari kushindwa katika uch-aguzi huo waliungana pamoja na kufanya mkarara (kuimba kwa kurudiarudia),

61

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

"Tunamtaka Ali tu."

Imeandikwa kwamba baadae Umar alisema: "Palikuwa na kelele nyingi na ghasiampaka nikaogopa pangetokea ugomvi, hivyo nikaushika mkono wa Abubakr kamaKhalifa."

Imeandikwa pia kwamba baadae Umar pia alisema, "Niliogopa kwamba kamawatu wangetawanyika bila kuchagua mrithi, basi baadae wangechagua mtuambaye tusingekubaliana naye hivyo kusababisha ugomvi, au kwamba wange-muunga mkono mtu huyo bila kuwa na hiari." Umar na Abu Ubaidah walitembeakuelekea kwa Abubakr, lakini Bashir Ibn Sa'd wa kabila la Khazraj, alikwenda hara-ka zaidi, akimpa Abubakr mkono wa kwanza, hivyo kumtambua yeye kama ndiyemrithi wa Mtume.

Hubab Ibn Mundhar alimkemea Bashir akisema: "Oh Bashir Ibn Sa'd, ewemwenye balaa, hata wazazi wako walikuchukia wewe. Umepuuza makualiano yafamilia, hukuweza kuvumilia kumuona binamu yako (Sa'd) akiwa Mtawala." Bashirakasema, "Hapana, umekosea, sikutaka kutokubaliana na chaguo la watu. Munguamewapa haki hiyo."

Kabila la Aus liliona kwamba lile kabila la Khazraj lilikuwa madhubuti sana katikakumpendelea chifu wao mgombea, Sa'd. Kwa hiyo waliamua kumuunga mkonoAbubakr, wakidhani kwamba kama Sa'd angechaguliwa, kabila la Aus lisingekuwana sauti katika mambo ya baadae. Pale binamu yake Sa'd, Bashir, alimuungamkono Abubakr waziwazi kwa kupuuza uamuzi wa watu wa kabila lake, ndipokabila la Aus walitiwa moyo zaidi kumuunga mkono Abubakr na Usaid Ibn Hudhair,mmoja wa machifu wa kabila la Aus, haraka sana akaushika mkono wa Abubakr.

Watu walipoona kwamba kabila la Khazraj lina wapinzani wengi sana, walisimamana kumuunga mkono Abubakr, na kwa mujibu wa Yaqoubi, walimpa mkono.Ilikuwa ni wakati huu ambapo Sa'd Ibn Ubaidah alikuwa karibu apondwe chini yawatu walipokuwa wanaruka zulia alilokuwa amekalia. Walinzi wa Sa'd walikuwawanapiga ukelele "Ondokeni, mpeni Sa'd nafasi ya kupumulia." Ndiyo wakati huoUmar alipokemea, "Muueni Sa'd, Mungu na amuue huyo." Kisha akamfuata Sa'dakisema: "Nataka kukuponda chini ya miguu yangu."

Kwa hili, Qais Ibn Sa'd alimwambia Umar, "Kama utadhuru japo unywele mmojawa kichwa cha Sa'd, utakugharimu meno yako yote."

Abubakr akakemea, "Umar, nyamaza. Katika nyakati hizi dhaifu tunahitaji utulivujuu ya yote." Umar akaondoka alipo Sa'd, lakini Sa'd akakemea nyuma yake,"Kama ningekuwa na uwezo wa kusimama, ningesababisha fujo hiyo katikaMadina, kiasi kwamba wewe na rafiki zako mngejificha kwa woga. Kisha ningeku-rudisha kwa watu kama mtumishi wao, na siyo kama mtawala wao." Kisha aki-wageukia watu wake, akasema: "Niondoeni mahali hapa." Wakafanya hivyo.Jauhari ameandika kwamba siku hiyo , Umar ambaye alikuwa amevaa rasmi kwa

62

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

tukio hili, alikimbia mbele ya Abubakr na akakemea, "Sikilizeni, watu wametoamkono kwa Abubakr wa kiapo cha utii, ninyi pia mfanye vivyo hivyo."

Kisha Abubakr akapelekwa Msikitini na watu, ili wengine waweze kumpa mkono.Kwa wakati huu Ali na Abbas walikuwa bado wanashughulika kuuosha mwili waMtume, waliposikia mwito "Allahu Akbar" kutoka Msikitini. Ali akauliza ni nini kina-chotokea, Abbas akasema ni maajabu, lakini alilitarajia hilo.

ONYO:

Bara' Ibn Azib alikwenda kwenye nyumba ya ukoo wa Bani Hashim akisema kwasauti kubwa, "Oh Bani Hashim, watu wengi wamempa mkono wa kiapo Abubakr."Ukoo wa Bani Hashim wakaambiana wenyewe kwa wenyewe, "Kabla ya hapaWaislam hawajafanya namna hii bila kwanza kutuona sisi, ndugu wa karibu waMuhammad." Abbas akajibu, "Kwa Mungu wa Ka'aba, yote yamekwisha." Kwamujibu wa Bara' Ibn Azib, kama ilivyoandikwa na Yaqoubi, Abbas kisha akawaam-bia ukoo wa Bani Hashim: "Mmepoteza mamlaka yenu milele. Nilikushaurinikuchukua tahadhari, lakini mkapuuza onyo langu."

Tabari ameandika kwamba kabila la Aslam lilikuja Madina, wakijazana kwenyevichochoro, wakimpa mkono wa kiapo cha utii Abubakr. Baadae Umar alizoeakusema, "Wallah, baada ya kuwaona kabila la Aslam wakimuunga mkonoAbubakr, nilipata imani kwamba tumeshinda."

Sheikh Mufid, katika kitabu chake al-Jamal, anasema kwamba ilikuwa ni bahati tukwamba lile kabila la Aslam siku hiyo lilikuwa Madina, kama walivyokuja kununuamahitaji. Waliambiwa kwamba ni lazima wamuunge mkono mrithi wa Mtume kablahawajauziwa mahitaji yao, wakafanya hivyo. Wafuasi wa Abubakr waliwachukuakuwapeleka Msikitini ambako Abubakr alikaa kwenye mimbar mpaka jioni,akipeana mkono na yeyote aliyetokea mbele yake.

KIAPO CHA HADHARA

Siku iliyofuatia matukio ya Saqifah, Abubakr alikaa kwenye ngazi za mimbari ndaniya Msikiti. Umar akasimama, akamshukuru Mungu, kisha akasema, "Manenoniliyosema jana hayakutoka kwenye Qur'ani wala hayakuwa maneno ya Mtume.Nilidhani kwamba Mtume atayashughulikia mambo yote yaliyowahusu watu, nakwamba atakuwa mtu wa mwisho kufa. Ameiacha Qur'ani kati yenu, na kama mta-fuata maelekezo yake, itakuongozeni kama ilivyomuongoza Mtume. Sasa uongoziwenu uko mikononi mwa mtu bora miongoni mwenu, Sahaba wa Mtume,aliyekuwa naye pangoni. Simameni na mshike mkono wake." Bukhari anasemakwamba wengine walikubaliana na urithi wa Abubakr pale Saqifah, lakini onyesho

63

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kubwa la hadhara la kiapo lilifanyika pale Msikitini.

Imesemwa na Anas Ibn Malik kwamba, ilibidi Abubakr ashawishiwe na Umar,kwenda kukaa kwenye ngazi za mimbari ambapo watu walikwenda kumpa mkono.Baada ya kumshukuru Mungu, Abubakr alisema, "Enyi watu, utii wenu sasa ukokwenye dhamana yangu. Mimi siyo mbora zaidi miongoni mwenu, lakini kama nikosawa basi nifuateni. Kama ninakosea basi niongozeni. Kama ninamtii MwenyeziMungu na Mtume wake, basi nitiini. Kama simtii Mungu na Mtume wake, msinitiimimi. Sasa simameni kwa ajili ya Sala. Mwenyezi Mungu na akusameheni."

BAADA YA KIAPO CHA UTII

Siku ya Jumatatu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - Rehema na amani ziwe juu yakena juu ya kizazi chake, alifariki dunia, badala ya kuhudhuria mazishi, watu wal-ishiriki katika matukio matatu yaliyofikisha mchana wa siku iliyofuata, Jumanne.

1) Maandamano.2) Onyesho la kwanza la kiapo cha utii huko Saqifah.3) Tangazo la mwisho la kiapo cha hadhara hapo Msikitini lililoishia

na hotuba ya Umar na Abubakr kuongoza sala ya kundi zima.

Baada ya mlolongo wa mambo ya tukio la tatu yalipokwisha hiyo siku yaJumanne, watu tena ndipo walipokwenda nyumbani kwa Mtume kutekeleza salaya maiti. Mmoja mmoja, kundi kwa kundi.

MAZISHI YA MTUKUFU MTUME (S.A.W.W.)

Masahaba wa Mtume walimwacha mikononi mwa ukoo wake. Toleo moja linaelezakwamba Abbas, Ali, Fadhl na Saleh (mtumwa wa Mtume), walitayarisha mwiliwake kwa ajili ya mazishi na wakamzika. Habari nyingine zinaeleza kwamba Ali,Fadhl, Qasam, watoto wawili wa Abbas na Shoqran (mtumwa wa Mtume), wali-husika na mazishi ya Mtume.

Baada ya tukio wakati hadhara ilipotoa kiapo cha utii, Jauhari katika kitabu chake'Saqifah', anasema kwamba Abubakr aliwataka Umar, Abu Ubaidah na Mughirahkutoa maoni yao kuhusu tukio hili. Kwa pamoja walimshauri kupata ridhaa yaAbbas kwa kumgawia zawadi. Kisha baada ya Abbas kutoa radhi zake, Alihataweza kufanya chochote kuwapinga. Watu wanne hawa wakamwendea Abbasusiku, na Abubakr, baada ya kumshukuru Mungu akasema, "Allah ametuma Wahyiwake kupitia kwa Muhammad kutuongoza sisi, na Muhammad alitimiza ujumbewake mpaka Mungu akamchukua Kwake na akampa malipo yake. Muhammad ali-waachia watu kujichagulia njia yao wenyewe, na watu wamenichagua mimi kama

64

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kiongozi wao. Sina woga. Mafanikio yangu yanakubaliwa na Mungu, ninamwami-ni Yeye, na nitarejea Kwake. Sasa habari zimekuja kwamba baadhi ya watuwamechukua fursa ya nafasi yako, na wananishutumu mimi mbali na kuungwamkono na umma. Tumekuja kukuomba uungane nasi kama wengine walivyofanya,au kuutaka upinzani kusimamisha harakati zao. Na kwa malipo yako, sisi tutakuza-wadia. Watu wanaijua nafasi yako, na ile ya rafiki yako, lakini wamekuwekeni pem-beni. Enyi Bani Hashim tulieni, Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa wetu kamavile alivyokuwa wenu" Umar akaongezea, "Kuja kwetu kwako hakuna maanakwamba tunakuhitaji.Tunakutaka tu ujiunge na wengine kwa usalama wako,vinginevyo utakutana na matokeo mabaya, hivyo lifikirie jambo hilo."

Abbas naye, baada ya kumshukuru Mungu, akasema, " Allah alimchaguaMuhammad kama Mtume wake, na msaidizi kwa marafiki zake, masahaba nawafuasi waaminifu. Allah aliwapendelea Waislam kwa kumtuma MtumeMuhammad. Sasa Allah amemchukua Kwake, na kuwaacha Waislam wamuduwenyewe mambo yao, kuchagua kiongozi sahihi kuwazuia wasipotee. Sasa,Abubakr, kama umeikalia nafasi hii kwa sababu ya uhusiano wako kwa Mtume, sisituko karibu sana naye kuliko wewe, na kama umechukua kiti hiki kwa idhini yawafuasi wake, sisi pia ni wafuasi wake ambao kamwe hamkututaka ushauri. Kamaumekichukua kama wajibu kwa niaba ya Waislam hatujaitoa kamwe haki hiikwako. Unajipinga mwenyewe kwa kusema watu wamekuchagua, na wakati huohuo kusema kwamba watu hawatoi ridhaa ya kurithi kwako. Kwa upande mmoja,unasema kwamba wewe ndiye mrithi wa Mtume. Kwa upande mwingine, unase-ma kwamba watu wamekuchagua. Kama hicho unachonipa, kile ambacho ni maliya waumini, huna haki ya kukitumia; na kama ni chetu kwa haki tunakitaka kamilisiyo kwa sehemu sehemu. Sisi ni tawi la mti wa Mtume, wewe ni wale tu wanaopa-ta hifadhi katika majani yake. Hivyo nyamaza kimya." Abubakr na rafiki zakewakamwacha Abbas bila kufanikiwa malengo yao.

HIFADHI KATIKA NYUMBA YA FATIMAH

Umar anasema, "Baada ya kifo cha Mtume tuligundua kwamba baadhi ya watuwamekusanyika katika nyumba ya Fatimah ili kutupinga sisi." Hawa walikuwa niAli, Zubair, Abbas, Ammar Ibn Yasir, Utbah Ibn Abi Lahab, Salman Farsi, Abu Dhar,Miqdad Ibn Aswad, Bara' Ibn Azib, Ubai Ibn Ka'b, Sa'd Ibn Waqqas na Talha IbnUbaidullah. Wengine kutoka makundi ya Muhajir na Ansari walitajwa. Kwa vileWaislam walisita kutoa tofauti zao, waliandika tu kwamba baadhi ya watu walijiku-sanya pamoja kwenye nyumba ya Fatimah kwa upinzani. Kwa bahati mistarimichache kuhusu upinzani huo imeandikwa katika kitabu cha historia chaBaladhuri. Baladhuri anasema kwamba Abubakr, baada ya kupingwa na Ali,alimuamuru Umar kumleta Ali mbele yake. Umar alikutana na Ali akajadili swalahilo naye. Ali akamwambia Umar, "Mnakamua ng'ombe wa urithi, nusu kwa ajili ya

65

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Abubakr na nusu nyingine kwa ajili yako mwenyewe. Hivyo anakufanya wewendiye mrithi wake." Pia (Baladhuri) anasema kwamba Abubakr katika kitandachake cha mauti aliitoa kauli hii. "Kuna mambo matatu tu ambayo nayajutia - nata-mani nisingepekua nyumba ya Fatima, ingawa walikuwa wanajiandaa kutupigasisi………."

Yaquubi anaandika katika juz.2,uk.115 wa kitabu chake kwamba Abubakr alisema,"Natamani nisingepekua nyumba ya Fatimah, na nisingetuma watu kwenda kum-nyanyasa; hata kama nyumba yake ilikuwa ikitumika kama hifadhi ambayoingesababisha vita."

Wanahistoria wamewataja wafuatao kama wale waliokwenda kwenye nyumba yaFatima kuwatawanya watu waliokuwa wamejihifadhi hapo:

1) Umar Ibn Al- Khatab2) Khalid Ibn Al-Walid3) Abdur Rahman Ibn Aufi4) Thabit Ibn Shammas5) Zaid Ibn Labid6) Muhammad Ibn Muslamah7) Salamah Ibn Salem Ibn Waqash8) Salamah Ibn Aslam9) Usaid Ibn Hudhair10) Zaid Ibn Thabit

Ali, Zubair na baadhi ya Muhajirina waliopinga urithi wa Abubakr, walikusanyikakatika nyumba ya Fatimah, na baadhi ya silaha. Habari ilimfikia Abubakr kwambaupinzani umekusanyika kutoa mkono wa kiapo kwa Ali, hivyo akamtuma Umar nawatu wengine kwenda kuwatawanya kwa nguvu au vinginevyo. Umar alichukuamienge ya moto unaowaka kwenda kwenye nyumba ya Fatima, na katika kuzionandimi za moto, Fatima alimuuliza Umar kama alidhamiria kuichoma nyumba yake,Umar akasema, "Ndiyo, kama hamtawafuata Waislam wengine na kutoa kiapokwa Abubakr."

Iliandikwa katika kitabu cha 'al-Imamah wa al-Siyasah' kwamba Umar aliwaamr-isha watu watoke nje ya nyumba hiyo, lakini walimpuuza. Umar akaagiza kuni naakawaambia wale walioko ndani ya nyumba, "Kama hamtoki nje, nitaichomanyumba hii. Naapa kwa Allah Ambaye anayo roho yangu mikononi Mwake." Mtummoja akamwambia Umar kwamba Fatimah alikuwemo ndani ya nyumba hiyonaye akasema, "Halina umuhimu kwangu nani yumo ndani ya nyumba hii."

Katika kitabu cha al-Ansabul Ashraf, juz.1, uk.586, imeandikwa kwamba Abubakralimtaka Ali amuunge mkono, lakini Ali alikataa, kisha Umar akaelekea nyumbanikwa Ali na mwenge wa moto unaowaka. Mlangoni akamkuta Fatima ambayealimwambia, "Unakusudia kuchoma mlango wa nyumba yangu?" Umar akasema,

66

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

"Ndiyo, kwa sababu hii inaimarisha imani iliyoletwa kwetu na baba yako."

Jauhari katika kitabu chake anasema, "Umar na baadhi ya Waislam walikwendanyumbani kwa Fatima kuichoma na pia kuwachoma wale waliokuwa katika upin-zani."

Ibn Shahna anasema, "Kuchoma nyumba na wakazi wake." Imeandikwa ndani yaKanzul Ummal, juz.3,uk.140, kwamba Umar alimwambia Fatimah, "Najua kwam-ba Mtume wa Mwenyezi Mungu hakumpenda yeyote kuliko wewe, lakini hili hali-tanizuia kutekeleza uamuzi wangu, kama watu hawa watakaa ndani ya nyumbayako, nitauchoma mlango huu mbele yako."

Wakati Abdullah Ibn Zubair alipokuwa anagombea madaraka, Bani Hashim wal-imtoroka kwenye njia ya mlimani. Abdullah alitoa amri ziletwe kuni awachomemoto. Urwah, ndugu yake Abdullah, alitoa kisingizio cha kitendo cha kikatili chandugu yake akisema, "Ndugu yangu aliwatishia, kama walivyokuwa wametishiwakatika tukio lililopita walipokuwa hawatoi kiapo cha utii." Alimaanisha pale BaniHashim walipokataa mamlaka ya Abubakr.

Hafidh Ibrahim (mshairi wa ki-Misri) ametunga shairi lifuatalo kuhusu ngano hii:

Umar yule mashuhuri alimwambia Ali mtukufu,Nitaichoma nyumba yako hatimaye,Kama hutautambua urithi wa AbubakrKwenye kiti cha Mtume na ujumbe wake,Pamoja na Fatima kuwemo ndani, Umar ndiye mmoja pekeeAliyeweza kumwambia hivyo Ali, huyu shujaa wa Adnani.(Abubakr katika kitanda chake cha umauti aliubainisha uvamizi,kwenye nyumba ya Fatimah aliamuru ufanyike.)

Yaqubi anasema: "Walikuja katika kundi na wakaishambulia nyumba ya Ali……..na yeye (Umar) akauvunja upanga wake (Ali) kisha (lile kundi) likaingia ndani yanyumba."

Tabari anasema, "Umar Ibn Khatab alikwenda nyumbani kwa Ali wakati Talha naZubair na baadhi ya Muhajir walikuwemo ndani. Zubair alitoka nje na akamsham-bulia Umar, lakini aliteleza na upanga ukamtoka mkononi mwake. Wafuasi waUmar wakamkamata na pia wakamkamata Ali wakati alipokuwa anasema, 'Mimi nimtumishi wa Mwenyezi Mungu na ndugu yake Mtume.'" Walimleta kwa Abubakr nakumwambia ashike mkono wa Abubakr. Ali akasema, "Mimi ninastahili zaidi nafasihii kuliko yeye. Mngepeana mkono wa kiapo na mimi. Hoja yenu na Ansari juu yauhusiano wenu na Mtume, naweza kutumia hoja hiyo hiyo kwani niko karibu zaidina Mtume kuliko nyinyi. Ansari walikubali maelezo yenu, nyie lazima pia mkubaliyangu, ama sivyo ninyi ni wahalifu."

Umar akasema, "Hatukuachii wewe mpaka ukubaliane nasi." Ali akajibu, "Kamueni

67

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

ng'ombe huyu na ugawane nusu kwa nusu na Abubakr. Mfanyie kazi yake leo, nakesho atakufanya wewe mrithi wake. Ninaapa kwa Allah kwamba sitakusikilizawewe Umar, na sitaushika mkono wa Abubakr."

Abubakr akamwambia Ali, "Sitakulazimisha kukubaliana na mimi." Abu Ubaidahakamwambia Ali, "Wewe ni kijana sasa hivi, Ewe Abul Hasan, hawa ndiyo watuwazima na wanajua jinsi ya kuuendesha urithi huu; wafuate sasa, na kamautabakia utawarithi, kwa sababu ya fursa zako na kwa sababu uko karibu sana naMtume; na mtangulizi wa Uislam ambao kwao umepigania vita vitukufu (jihad)." Aliakajibu, "Enyi kundi la Muhajirina, muogopeni Mungu, msimnyang'anyeMuhammad na kizazi chake mamlaka yao. Msihamishie kitovu cha Uislam kwenyenyumba yenu, kutoka kwenye sehemu yake halisi ya asili. Wallah, madhali kunawatu wajuzi katika Qur'ani, Sheria za Ki-Islam, na ngano za Mtume, miongonimwetu familia ya Mtume, tunastahili zaidi kumrithi Mtume kuliko mtu mwingineyeyote. Wallah nyumba yetu inacho kile mnachokitaka. Msifuate matamanio yenu,vinginevyo mtazidi kupotea."

Bashir Ibn Sa'd akasema, " Ee Ali, kama Maansari wangekusikia ulichosema hivipunde, hakuna hata mmoja ambaye angebishana na wewe, lakini yote yamek-wisha, tumeushika mkono wa Abubakr." Bila ya kushikana mkono na Abubakr, Aliakarudi nyumbani.

Ibn Abil Hadid amenakili kutoka kwa Jauhari kwamba pale Fatimah alipoona jinsigani Ali na Zubair wanavyotendewa vibaya, alikuja mpaka mlangoni na akasema," Abubakr, ni mapema kiasi gani umeighilibu familia ya Mtume wa MwenyeziMungu! Sitaongea tena na Umar kamwe pindi ningali niko hai."

Simulizi nyingine anasema kwamba Fatimah huku akiwa analia, alitoka nje nakuwafukuza watu. Yaqubi anasema kwamba Fatimah alitoka nje na kusema,"Tokeni nyumbani kwangu, ama sivyo Wallah, nitafunua kichwa changu, nanitaomboleza kwa Allah na nywele zilizotulia." Hivyo watu walitawanyika kutokanyumbani kwake hata wale waliokuwa wamejihifadhi pale.

Nidhaam pia anasema, "Siku hii Umar alimpiga Fatimah tumboni nakumsababishia mimba yake kutoka, wakati akikemea na kuchoma nyumba (wakatiwengine wameondoka na ni Ali na wanawe Hasan na Husein waliokuwa ndani)."

Masud anasema kwamba baada ya kiapo siku ya Jumatatu na Jumanne, Ali alik-wenda ja kwa Abubakr na kumwambia, "Umeharibu nafasi yetu, kwa vile hukutu-fikiria sisi." Abubakr akajibu, "Hiyo ni kweli, lakini nilihofia kungetokea uasi na gha-sia."

Yaqubi pia anasema kwamba baadhi ya watu walikwenda kwa Ali kumpa mkonowa kiapo, lakini Ali akawaambia waje siku inayofuata, na vichwa vilivyonyolewa,lakini ni watatu wao tu waliorudi.

68

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Baada ya matukio hayo ya kiapo, Ali alikuwa akienda na Fatima, wakiwawamepanda punda, nyumba hadi nyumba kuomba kura. Lakini watu walimwambiaFatima, "Ewe binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, binamu yako angetutakakumuunga mkono kwetu, tusingemchagua mtu mwingine yeyote ila yeye, lakinitayari tumekwisha kupeana mkono na Abubakr."

Jibu la Ali lilikuwa ni hili, "Aibu hii, mlinitegemea mimi kuuacha mwili wa Mtume, nakujihusisha katika kugombea mamlaka?" Fatima alikuwa akisema kwamba Aliamefanya kile ambacho angepaswa kufanya, nao wamefanya mambo ambayoAllah angewauliza juu yake.

Mu'awiyah katika barua yake kwa Ali, aliitaja simulizi hiyo hapo juu akisema,"Inaelekea kama ni jana tu pale ulipompakia mkeo kwenye yule punda, ambayeungemuweka ndani ya nyumba yako, akiwa ameshika mikono ya wanao, Hasanna Husein,ukigonga milango ya nyumba za wale watu waliokuwepo kwenye Vitavya Badri, na kuwaambia wasimuunge mkono Abubakr, yule rafiki yake Mtume, ilawakuunge wewe mkono. Hata hivyo, ni watu wanne au watano tu waliokubali.Naapa kwa nafsi yangu mwenyewe, kwamba kama ungekuwa kwenye hakiwangekuunga mkono wewe. Ulidai kile ambacho siyo chako. Ulisema mamboambayo hayajasikika kabla. Naweza kuwa na kumbukumbu mbaya, lakini kamwesitasahau maneno uliyomwambia Abu Sufyan, 'Ningekuwa na watu arobaininingekwenda kuchukua haki yangu kutoka kwa watu hawa kwa nguvu.'"

Katika vita vya Siffin, Amr Ibn Aas alimkumbusha Mu'awiyah kwamba Ali alisema,"Kama ningekuwa na watu arobaini ….." n.k. Amr Ibn Aas alikuwa na maanakwamba Ali aliyasema haya ile siku walipoivamia nyumba ya Fatimah.

MWISHO WA MATUKIO PALE KWENYE KIAPO

Usudu'l-Ghabah , juz.3,uk.222 kimeandika: "Wapinzani waliafikiana kumkubaliAbubakr miezi sita baada ya onyesho la hadhara la kiapo kwake." Yaqubijuz.2,uk.105, "Ali alipeana mkono na Abubakr miezi sita baada ya onyesho la had-hara la kiapo." Istiab juz.2uk.244 na al-Tanbih al-Ashraf, uk.250, "Ali hakupeanamkono na Abubakr mpaka baada ya Fatima kufariki." Katika al-Imamah waSiyasah imeandikwa kwamba Ali alitoa kiapo chake kwa Abubakr baada ya Fatimakufariki, ambapo ilikuwa siku 75 baada ya kifo cha Mtume.

Kwa mujibu wa Zubair, Fatimah, baada ya mabishano aliyofanya na Abubakrkuhusu urithi wa Mtume, hakuongea tena naye kamwe.

Dhuhari pia anasema kwamba Ali hakumpa mkono Abubakr mpaka miezi sitabaada ya kiapo cha hadhara na Banu Hashim wakamfuatia.

Katika Taysiir al-Wusuul, juz.2,uk.46, Dhuhari anasema, "Wallah, Ali

69

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

hakukubaliana na Abubakr mpaka ilipopita miezi sita na Bani Hashim wakamfua-ta. Wakati Ali alipoona kwamba watu wanamtelekeza, akajifungamanisha naAbubakr."

Baladhuri katika Ansabul Ashraf, juz.1,uk.587, anasema, "Wakati Waarabuwalipoukataa Uislam na wakabadilika kwenye uasi, Uthman alikwenda kwa Ali nakumshawishi amuunge mkono Abubakr, ili kuwapa moyo Waislam kuwapiga vitawaasi chini ya Abubakr. Ali akapeana mkono wa kiapo na Abubakr, na mchafukokati ya Waislam ukatulizwa. Kisha vikosi vya Waislam vikatayarishwa ili kuwapigawaasi."

Baada ya kifo cha Fatimah, na kupoteza shauku kwa watu, Waislam waka-gawanyika, cheo cha Abubakr kilikuwa imara, hivyo Ali akapatanishwa naye. Hatahivyo, Ali kamwe hakuyasahau matukio haya, hata pale aliposhika nafasi ya mrithiwa Mtume. Katika hotuba yake iitwayo Shaq-shaqiah, anasema, "Ilinibidi niwemwenye subira kwa ajili ya maarifa ya kawaida, nilingojea kwa uvumilivu ingawailikuwa ni ngumu kama kuwa na mwiba kwenye macho yangu, na mfupa uliokwa-ma kooni mwangu. Niliiona haki yangu ya urithi kwa Mtume ikichukuliwa kinyumetoka kwangu, wakati siku za yule wa kwanza (Abubakr) zilipokwisha, na nuru yamaisha yake kuzimishwa; aliipitisha tunzo ya urithi wa Mtume mikononi mwa IbnKhatab. Oh tofauti iliyoje kati ya kupanda ngamia, (kukabiliana na matatizo pekeyako) na kukaa kwenye kiti kwa Hayan, akiishi maisha ya raha bila ya kujali kati-ka kasri ya ndugu yake Jabir. Inashangaza kwamba Abubakr alikuwa akiwaombawatu wafute kiapo chao kwake kama mrithi wa Mtume, lakini kabla ya kifo chake,Abubakr kwa imara alimuweka Umar kuwa mrithi. Waporaji wawili wale waliugawaurithi kati yao wenyewe, kama kugawana matiti mawili ya ngamia yaliyojaa mazi-wa.

70

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

MAONI YALIYOTOLEWA NA WATU MBALIMBALIKUHUSU HICHO KIAPO CHA UTII

A. FADHIL IBN ABBAS

Kwa mujibu wa Yaqubi, pale ukoo wa Bani Hashim walipozipata habari kuhusukuchaguliwa kwa Abubakr kama mrithi wa Mtume, Fadhil Ibn Abbas aliliambiakabila la Quraish, "Kamwe hamtamrithi Mtume kwa udanganyifu, tunastahili sisinafasi hiyo siyo ninyi, sisi ndiyo tulio na haki, hususan rafiki yetu Ali." Ndipo UtbaIbn Abi Lahab akasoma shairi lifuatalo:

Mimi sikudhani kamwe watu watawaangusha Bani HashimWala kwamba watamwacha Abul Hassan peke yake,Alikuwa mtu wa kwanza kumfuata Muhammad,Na wa mwisho kuuacha mwili wake - kwa huzuni sana.Kumsaidia na kumliwaza Ali, Malaika walishuka,Kutoka mbinguni kuja kwenye kitanda cha umauti cha Mtume.

Utba kisha akapokea ujumbe kutoka kwa Ali ukimtaka aache hayo, kwa sababuyalikuwa ni matakwa ya Ali kwamba Waislam wote wawe kwenye ushawishimmoja.

B. ABDULLAH IBN ABBAS

Amesimulia mazungumzo haya na Umar:

Umar: "Hivi unajua, Ibn Abbas, kwa nini watu hawakuuunga mkono ukoo wenu,ndugu wa Muhammad, kuwafanya warithi wake?"

Abdullah: "Kama sijui, basi Kiongozi wa Waumini atanifahamisha."

Umar: "Bani Hashim walitaka Mtume, na warithi wake wote wawe wanatokakwenye ukoo wao, lakini sisi, Maquraish, kwa mafanikio kabisa tumech-agua mrithi wake."

Abdullah: "Naweza kuruhusiwa kusema kitu?"

Umar: "Kama ikibidi, ewe Ibn Abbas."

Abdullah: "Ingekuwa bora kwa Maquraish, kama wangeridhika na kile ambachowalichokipewa na Allah; basi kusingekuwa na wivu. Umesema kwam-ba hii haikuwa hivyo, kwamba Maquraish hawakutaka kile ambachoMungu amewafadhilishia juu yao. Watu kama hawa wanazungumziwandani ya Qur'ani, 'Kwa sababu hawakuupenda wahyi wa Allah, amrizake, kazi zao hazikuwa chochote.'"

71

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Umar: "Sikutaka niamini kile nilichosikia kuhusu wewe, kwa sababu kingeni-fanya nipoteze heshima yangu juu yako milele."

Abdullah: "Kama kila kitu nilichokisema ni cha kweli, sitaogopa kuvunjiwa heshima, na kama nilichosema ni uongo, basi mtu kama mimi lazima ajisahi-hishe mwenyewe."

Umar: "Nimesikia kwamba umesema kwamba tumetwaa madaraka kwa kuwadhulumu watu ambao tunawaonea wivu?"

Abdullah: "Kila mtu anajua jinsi mlivyotumia dhulma, na vilevile juu ya wivu wenu,Shetani alimwonea wivu Adam na sisi ni watoto wa Adam ambayealikuwa mkandamizwaji na wivu."

C . SALMAN FARSI

Jauhari amesimulia kwamba Salman, Zubair na Ansari walitaka kutoa mkono wakiapo kwa Ali, na pale Abubakr alipokuwa Khalifa, Salman akasema, "Mumeipatadhahabu ndogo lakini mumeikosa dhahabu mama. Mumemchagua huyo mzee namkasahau nyumba ya Mtume. Mngewaachia wamrithi Mtume, mungenufaikazaidi, na kusingekuwa na kutoelewana kati ya Waislam."

D. UMMA MISTAH

"Kutofautiana kati ya Ali na Abubakr kuliwakera Waislam." Umma Mistah binti yaUthathah, alikwenda kwenye kaburi la Mtume na akasoma shairi lifuatalo:

Tofauti kati ya Waislam zilianza,Mpendwa Mtume, mara tu baada ya ulipoondoka,Bila ya wewe, tulipoteza mwelekeo wetu tena,Kama maua na nyasi bila ya mvua.

E . ABU DHAR

Hakuwepo Madina wakati Mtukufu Mtume alipofariki, lakini aliposikia Abubakramemrithi Mtume alisema, "Umepokea zawadi ndogo kwa ajili ya juhudi zako.Ungeunga mkono madai ya jamaa za Mtume kushika nafasi hiyo, ungelinufaikasana, na kusingekuwa na kutofautiana kati ya Waislam."

F. MIQDAD

Yaqubi amesimulia katika kitabu chake kutoka kwa msimuliaji ambaye amemuonamtu katika Msikiti wa Madina akiwa katika huzuni kubwa kana kwambaamenyang'anywa utajiri wake mkubwa. Mtu huyo alikuwa akisema, "Ni ajabu sanakwamba nafasi hiyo imeondolewa kwenye mikono ya watu wenye kustahiki."

72

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

G. BIBI MMOJA KUTOKA BANI NAJJAR

Baada ya Abubakr kuchukua kiti cha Ukhalifa, alituma pesa kwa kila mwanamkewa Muhajirina na Ansari, Zaid Ibn Thabit alibeba fungu la bibi mmoja kutoka BaniNajjar kumpelekea, lakini alikataa kuzipokea akisema, "Abubakr anataka kuinunuadini yetu kwa kutoa rushwa."

H . ABU SUFIAN

Alikuwa ni Sakhr mwana wa Harb, mwana wa Umayya, mwana wa Abd Shams,mwana wa Abd Manafi. Alipigana na Mtume hadi ule wakati Mtume alipoitekaMakka na kupewa msamaha. Wakati wa kifo cha Mtume, hakuwapo Madina.Akiwa njiani kurudi hapo, Abu Sufian alipata habari juu ya kifo cha Mtume na zaAbubakr kuwa mrithi.

Aliuliza, "Walilichukulia vipi hili Abbas na Ali, wawili hawa waliodhulumiwa?"Alijulishwa kwamba walikuwa kimya majumbani kwao. Abu Sufian akaapa akise-ma, "Kama nitabakia nitawasaidia wao kujaza nafasi yao ya halali. Ninaona wingula vumbi hewani linalohitaji damu kulisafisha." Alipoingia Madina alianza kusomashairi hili lifuatalo:

Oh Bani Hashim, msimpe mtu yeyote fursaYa kuwa na wivu, hasa hawa Taim na Adi.5Mamlaka ya ki-Islam yalianzishwa nanyi,Mwacheni Abul Hasan (Ali) aongoze, kama mnataka kuendelea.

Kwa mujibu wa Tabari, Abu Sufian alisema, "Kuna vumbi katika hewa, Wallah, nimvua ya damu tu inayoweza kulisafisha. Enyi wana wa Abd Manafi, kwa niniAbubakr aliruhusiwa kuwa ndiye mrithi wa Mtume? Wako wapi Ali na Abbas ambaowalidhulumiwa?" Kisha alitaka kupeana mkono wa kiapo na Ali, lakini Ali alikataa.Abu Sufian ndipo tena akasoma shairi lifuatalo:

Punda na siyo mtu muungwana, anaonyesha unyenyekevu,Kuna alama mbili tu za udhalili,Mambo ya hema chini ya nyundo nzito, naNgamia wa mhamahamaji na mzigo wake.

WITO WA ABU SUFIAN: "ENYI WANA WA ABD MANAFI."

Hili lingeweza kubadili mwelekeo wa historia ya ki-Islam kama Ali angekuwa fid-huli, na angeshawishiwa na Abu Sufian kuasi dhidi ya Khalifa. Inashangaza kuonakwamba Abu Sufian, yule adui halisi wa Uislam, aliyepigana na Mtume mpakaalipoona ni vigumu kwake kuendelea kupigana, amejitolea msaada wake kwa Ali.Je, alikuwa na maana ya kusaidia kweli? Au kuchochea ugomvi?

5 Makabila ya Abubakr na Umar.

73

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Cha kushangaza zaidi ni kukataa kwa Ali kukubali msaada toka kwa Abu Sufian naAbbas, wakuu wa makabila mawili yenye nguvu, wakati alikuwa akitafuta msaadakutoka sehemu yoyote inayowezekana. Baada ya kuyachunguza madhumuni yaAbu Sufian na Ali, hatukubakia na mashaka yoyote juu ya asili ya mipango yao.

Mababu wa Mtume na Abu Sufian walikuwa mabinamu waliokuwa na migogoroya ki-ukoo. Mapigano kati ya koo mbili hizi yaliishia na ukoo wa Mtume kushindanafasi ya kuwa kama mkuu wa Kabila. Abu Sufian alikuwa ni mpinzani wa Mtumekwa nafasi ya utemi (uchifu), na msimamo wake juu ya Mtume kama kiongozi wakidini ulikuwa ni ule wa kutojali. Kwa sababu hii, pale Mtume alipoiteka Makka, AbuSufian alimwambia Abbas, "Mpwa wako ameanzisha ufalme mkubwa sana."Abbas akasema, "Huu ni utume siyo ufalme." Abu Sufian akaikubali kauli hii bilahoja. Ingawa Abu Sufian alishindwa na ndugu zake, hakutaka wageni kuwa namamlaka, na kuliacha kabila lake mikono mitupu.

Mtume alijaribu kuzuia mahusiano ya kiukoo kuingilia njia ya haki lakini haku-fanikiwa sana. Tunaona, pale tunapoyaangalia matukio yaliyotokea kati ya koowakati wa uhai wa Mtume, kwamba lile tukio la jinsi Abbas, ami yake Mtume, alivy-omtetea Abu Sufian, ni mfano mzuri wa nguvu za fungamano la ukoo.

Ibn Hisham aliandika kwamba ule usiku kabla ya kutekwa Makkah, kambi zaWaislam ziliuzunguka mji huo. Abbas, ami yake Mtume, alipanda juu ya farasi waMtume, alikuwa akizurura akitaraji kuona baadhi ya maadui. Alitaka kuwajulishajuu ya shambulio linalokuja la Waislam, kumpa adui yoyote fursa ya kuombamsamaha. Alimkuta Abu Sufian aliyekuwa akiwapeleleza Waislam, Abbasakamwambia, "Shukuru Mungu nimekuona Abu Sufian, panda farasi, na nitaku-peleka kwa Mtume, ili uweze kuomba hifadhi, au vinginevyo kesho kama utatek-wa, unaweza ukakatwa kichwa."

Abbas akapanda farasi huyo na Abu Sufian nyuma yake. Walipita makundi mengiya Waislam ambao walikuwa wamewasha mioto mingi kuwatisha maadui, na ilikuangalia hatari yoyote inayowezekana kutokea. Waislam wale wakasema,"Tazama, ami yake Mtume juu ya farasi wake." Umar, kwa bahati, akamuona AbuSufian na akakemea, "Yule adui wa Mwenyezi Mungu. Shukuru Mungu ukomikononi mwetu na huna ahadi ya mtu yoyote ya kukulinda wewe." Kisha Umarakakimbia kwa Mtume kuomba ruksa ya kumuua Abu Sufian. Lakini Abbas, juu yafarasi yule, alimpita Umar na kumkuta Mtume kwanza. Umar ndipo akafika nakusema, "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunaye Abu Sufian pamoja nasi,akiwa hana dhamana yoyote ya usalama. Nipe ruksa nimkate kichwa." LakiniAbbas akasema, "Tulia ewe Umar, kama Abu Sufian angetoka kwenye kabila lakola Adi, usingesisitiza juu ya kumuua yeye. Lakini kwa vile anatoka Abd Manafiunasema maneno ya kikatili." Ngano hii inathibitisha kwamba mafungamano yaukoo yalikuwa na nguvu wakati ule. Inaonyesha pia kwamba matilaba ya Abbas ili-chomoza kutoka kwenye mapenzi ya kabila lake. Sababu ya dhihirisho la AbuSufian dhidi ya Abubakr ilikuwa pia ni matokeo ya umuhimu wa ukabila.

74

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Yale mamlaka ya juu kabisa ya ukoo wa Abd Manafi, ambao hawa Bani Hashim(familia ya Muhammad) na hawa Bani Umayya (familia ya Abu Sufiani) wame-tokana nao, ulikuwa unajulikana kwa kila mtu. Hivyo pale baba yake Abubakralipoarifiwa kwamba mwanae amekuwa Khalifa, akasema, "Bani Hashim na BaniUmayyah wamekubaliana?" Alipojibiwa kwa kukubaliwa, akasema, "Kile Munguanachokitaka, hakuna anayeweza kukizuia."

Upole wa Abu Sufian kwa familia ya Muhammad, baada ya kifo chake, ulitokanana hisia za umoja wa kikabila. Kwani Abu Sufian alipigana na Mtume kila wakatialipopata fursa. Kusema kwake, "Kama nitabakia hai nitamsaidia Ali na Abbaskuikamata tena nafasi yao," hakukuwa na sababu ila upendo wa ki-kabila; kamailivyo desturi ya Waarabu kusaidia ndugu wa karibu dhidi ya wageni wa mbali.

Abu Sufiani, Abbas na Ali wana asili moja ya kikabila, Kabila la Qussai ambalolilikuwa kubwa na maarufu sana. Hii ndiyo sababu Abu Sufiani alisema, "Yeyotealiye na Qussai kama mfuasi wake, kwa vyovyote atashinda." Abubakr na Umarwalitoka kwenye makabila madogo ambayo hayakuweza kamwe kushindana naQussai. (Qussai, asili ya kabila la Quraish lilikuwa ndiyo mzizi mkuu wa kabila laAbd Manafi, kabila la Bani Hashim na Abu Sufiani.)

Ilikuwa ni desturi katika siku zile kwa kabila kupendelewa maslahi ya mmoja wawatu wake lenyewe. Ali, kwa kuungwa mkono na Abu Sufiani na Abbas, angewezabila wasiwasi kumshinda Abubakr. Lakini Ali, yule shujaa, mwana wa Abi Talib,alikataa msaada wa kabila lake maarufu, kwa sababu desturi hii ilikuwa kinyumena mafundisho ya Ki-Islam. Kwa hiyo alishindwa na Abubakr. Kwa kweli, baada yakifo cha Mtume, matukio yote yalishawishiwa na chuki ya makabila mengine kwakabila lake au familia yake. Ansari walipendekeza kwamba Sa'd angekuwa ndiyemrithi wa Mtume kwa sababu tu ya upinzani kwa Muhajirina. Walijua kwambabaadhi ya Muhajiriina ni waumini wakubwa katika Uislam na kwa hiyo ni wenyekustahiki zaidi kutambuliwa. Lile kabila la Aus lilimuunga mkono Abu Bakr ilikumpinga Sa'd, mgombea wa kabila la Khazraj. Ile hotuba ya Umar pale Saqifahilikuwa ni ushahidi wa kweli wa upendeleo wa ki-kabila. Uungaji mkono wa AbuSufiani kwa Ali pia ulitokana na chuki ya ki-kabila. Ni Ali tu, ambaye alilelewamapajani mwa Mtume tangu utoto wake, aliyetaka kushikilia Uislam, hivyo alitakauungaji mkono wa wale Waislam ambao hawasukumwi na chuki za kikabila, naambao hawakuwa na muungo wa kifamilia, watu kama Abu Dhar, Miqdad naSalman, ambao dhamira yao tu ni kuamini kwao imani ya Uislam.

Hitimisho la simulizi hizo hapo juu, kuhusiana na Abu Sufiani kumuunga mkono Ali,lilikuwa kwamba, ingawa dhamiri ya Abu Sufiani haikuwa ya kidini, bali kwasababu aliamini sana mamlaka ya kabila lake ambalo Ali ni mmojawapo - kwasababu hii yeye peke yake alimuunga mkono Ali dhidi ya Abubakr. Abu Sufianialikuwa mkweli kwa Ali katika upinzani kwa Abubakr kwa sababu ya chuki zakiukoo, lakini kama inavyotokea mara kwa mara mambo yasiyo sahihi yames-imuliwa, na Abu Sufiani na wote wale waliompinga Abubakr, walishutumiwa kwa

75

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

uasi na waliitwa wakorofi. Matukio yaliyopita kuhusu Abu Sufiani yanaifanya nganoifuatayo kuwa rahisi kuiamini. Imesimuliwa kwamba Abu Sufiani alimuuliza Ali,"Kwa nini ulimkubalia Abubakr kumrithi Mtume? Kama ukitaka, nitaijaza mitaa yoteya Madina na askari wa farasi na wa miguu." Ngano inaendelea kama Ali anavyo-jibu, "Abu Sufiani, umekuwa kwa muda mrefu wa kutosha adui wa Uislam. Huwezikusababisha madhara yoyote zaidi sasa. Lazima nikubali kwamba Abubakr anas-tahiki nafasi hiyo." Ngano hii haielekei kuwa sahihi kwa sababu msimuliajihakuishi wakati wa tukio lenyewe. Pia baadhi ya ngano hizi za uongo zimesimuli-wa na Awanah, aliyejulikana kuwa si wa kuaminika. Maelezo haya hayaendi sawakwa sababu kama Ali angesema, "Nakubali Abubakr anastahiki nafasi hiyo," basiAbu Sufiani angemuuliza, "Kwa nini hupeani mkono wa kiapo naye?" Ambacho Alikwa kweli alichokisema kilikuwa ni, "Kama ningekuwa na waumini arobaini wenyemoyo wa sawasawa, ningepigana naye."

Ali katika barua yake kwa Mu'awiyah anaandika, "Baba yako (Abu Sufiani) aliiele-wa haki yangu zaidi kuliko ufanyavyo wewe. Ungenijua mimi kama baba yakoalivyonijua, ungekuwa na busara zaidi."

Hiyo serikali ilikuwa inamuogopa Abu Sufiani, Umar alimwambia Abubakr, "Mpatiepesa kidogo ili kumnyamazisha." Abu Sufiani, akiwa hakuridhishwa na Ali, ali-ikubali posho hiyo. Tabari anasimulia kwamba Abu Sufiani hakuacha kutingishampaka mjukuu wake Yazid akateuliwa kama Kamanda wa Jeshi lililopelekwaSyria.

I . MU'AWIYAH

Mu'awiyah alimwandikia Muhammad, mtoto wa Abubakr, "Baba yako alijua, nasitunajua kwamba Ali alistahiki kuwa mrithi wa Mtume. Tulimheshimu Ali sana sana.Pale Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani juu yake, alipokamilishaujumbe wake na roho yake ikaenda kwa Mungu, baba yako (Abubakr) na mkonowake wa kulia Umar, ndiyo watu wawili walioingilia haki ya Ali. Walipanga pamojana wakamtaka Ali ashirikiane nao. Ali akakataa, nao wakala njama dhidi yakempaka Ali akakubali.

Hawakumruhusu kamwe Ali kushiriki katika siri yao mpaka Mungu alipozichukuaroho zao. Sasa tuko kwenye njia ambayo baba yako aliitengeneza. Kama alikuwakwenye njia ya sawa, tutamfuata yeye. Kama alikuwa kwenye njia potofu, mlaumubaba yako - siyo sisi kwa kumpinga na kutouachia Ukhalifa kwake. Amani iwe juuya wale wanaotubu."

J. KHALID IBN SAID

Khalid, mwana wa Saeed, mwana wa Aas, alikuwa mmoja wa watu wa kwanzakuuingia Uislam. Ibn Qutaibah ndani ya Maarif, uk.128, anaandika, "Khalid alikuwaMwislamu kabla ya Abubakr." Khalid alihama kwenda Ethiopia na pale Uislamulipokua na kuwa na nguvu alirudi kutoka huko. Yeye na ndugu zake wawili, Amr

76

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

na Aban, wakawa, kwa amri ya Mtume, Wakusanya Kodi ambao walikusanya tokakabila la Madhaj. Kisha wakahamishiwa Sana'a huko Yemen. Wakati Mtume alipo-fariki, walirudi Madina, Abubakr akawauliza ni kwa nini wameviacha vituo vyao,nao wakajibu, "Tulichaguliwa na Mtume kwenye nafasi hii, na hatutamfanyia kazimtu mwingine yeyote sasa kwa vile amekufa." Walitoa visingizio vingine, nahawakumpa Abubakr mkono wa kiapo, mpaka miezi miwili ikapita. Khalid ali-waambia Bani Hashim, "Ninyi ndiyo mti mtukufu, wenye matunda na nitawafuateninyie." Alikwenda kwa Ali na Uthman siku moja na kuwaambia, "Nyie, kizazi chaAbd Manafi, hamkuichukulia nafasi yenu kwa makini mpaka wenginewamekupiteni." Alimchunuku Ali, na akamuomba ampe mkono wake, lakini ilikuwaimechelewa kwani Abubakr tayari alikwisha kuwa Khalifa. Hivyo Khalid alimkubalikama walivyofanya Bani Hashim.Abubakr hakujali tabia ya Khalid ya vurugu zaupole, lakini Umar aliichukulia nongwa ya dhati. Baadae Abubakr alimteua Khalidkuwa mkuu wa kikosi cha jeshi lililopelekwa mpakani na Syria. Umar akabishanana Abubakr na kusisitiza kwamba amuondoe Khalid kwenye nafasi hiyo. Abubakrndipo akamuondoa Khalid na kumteua Yazid mtoto wa Abu Sufiani kushika mahalipake. Khalid hakujali kama alikuwa askari ama kamanda, na alipigana kama askarikatika mpaka wa Syria mpaka alipouawa shahidi katika mwaka wa 13 wa Hijiria,mausiku mawili kabla ya mwisho wa mwezi wa Mfungo nane.

K . SA'D IBN UBAIDAH

Sa'd Ibn Ubaidah alikuwa ndiyo mkuu wa kabila la Khazraj. Alikuwepo hukoAqabah (kama mmoja wa wakilishi waliokuja kutoka Madina kuelezea kuridhiakwao kumsaidia Mtume kama angetaka kuhama toka Makkah kwenda Madina).Sa'd alishiriki katika vita vyote Mtume alivyopigana,isipokuwa labda vile Vita vyaBadr. Katika siku ya kutekwa Makka, alionyesha mwelekeo wa kivita akisema, "Hiini siku ya kupigana, siku ambapo wanawake watachukuliwa mateka." HivyoMtume akaitoa bendera kwa mwanae Sa'd, aitwae Qais, na kupunguza hadhi yaSa'd kuwa haji wa kawaida. Sa'd, akiwa ameshindwa katika juhudi zake za kum-rithi Mtume, aliachwa kabisa wakati wa kutoa kiapo, lakini siku chache baada yaAbubakr kuwa Khalifa, Sa'd alitakiwa kumpa mkono, kama sehemu ya kabila lakeilivyofanya, lakini Sa'd alikataa na kusema, "Wallah, mradi ninayo mishale kwenyezaka langu ya kuweza kuwapigeni nyie, mkuki wa kuchovya kwenye damu yenu,na upanga, na nguvu katika mkono wangu, nitapigana nanyi kwa msaada wa walewa kabila langu ambao bado wananitii. Sitapeana mkono wa kiapo na wewe, hatakama watu na majini watatangaza vita dhidi yangu katika kukusaidia wewe, mpakaninakufa na kuipeleka kesi yangu kwenye mahakama ya mbinguni." Umar alim-sisitiza Abubakr amlazimishe Sa'd kukubali, lakini Bashir Ibn Sa'd akasema alijuakwamba Sa'd ni mkaidi na hatakubali. Pia, alikuwa na sauti bado miongoni mwawatu wake na hangeweza kuuawa mpaka watu wengi wa kabila lake, na nduguzake pia wawe wameuawa. Sa'd kwa hiyo hakuguswa kwa ushauri wa Bashir.

(Bashir, mtu wa kwanza kumpa mkono Abubakr alikuwa ni adui wa Sa'd.) Sa'd

77

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

hakuhudhuria kamwe ibada za jamaa zilizoendeshwa na watu wa utawala, na ali-hiji tofauti na makundi yaliyoongozwa na serikali. Kwa mtindo huu alizipitisha sikuzake mpaka Abubakr alipofariki. Pale Umar alipomrithi Abubakr, alikutana na Sa'dna wakapeana kauli za maudhi. Sa'd akasema, "Abubakr alikuwa mhisani zaidikuliko wewe, sipendi kuwa pamoja nawe." Umar akasema, "Kama mtu hapendikuwa karibu na mtu mwingine, atakaa mbali."

Ndipo Sa'd akaondoka Madina kwenda Damascus. Umar alituma mtu kwendakuchukua mkataba na Sa'd au kumuua kama hatakubali. Mjumbe huyo alikutanana Sa'd kwenye shamba la miti ya matunda na akamtaka akubaliane na Umar.Sa'd akakataa na yule mtu akamtisha bila mafanikio. Kisha akamuua.

Masudi amesimulia kwamba Sa'd hakutoa mkono wa kiapo, na alihamia Syriaambako aliuawa. Ibn Abd Rabbih amesimulia kwamba Sa'd aliuawa na mshambu-liaji asiyejulikana, na kwamba majini walimuombolezea kama inavyoelezwa katikaubeti ufuatao:

Tulimuua Sa'd, mkuu wa kabila la Khazraj, leo,Mapigo yetu mawili moyoni kwake hayakwenda kombo."

Ndani ya Tabari, imeandikwa kwamba Sa'd alikuwa anakwenda haja pale mtualipomshambulia na kumuua. Wakati mwili wake ulipogunduliwa baadae, ngoziyake ilikuwa imegeuka rangi ya kijani.

Katika Usudu'l-ghabah, imeandikwa kwamba Sa'd hakumkubali Abubakr, walaUmar. Alihamia Syria ambako aliuawa. Kisha sauti ikaja toka shimoni na kuwajul-isha watu juu ya mauwaji ya Sa'd. Mwili wake ulionekana karibu na nyumba yakehuko Huuran ndani ya Damascus, na ulikuwa umegeuka rangi ya kijani.

Abdulfattah ndani ya kitabu chake, al-Imam Ali Ibn Abi Talib, amesimulia kwambawatu wa kawaida wanasema kwamba Sa'd aliuawa na majini, lakini kwa kweliKhalid Ibn Walid na mmoja wa marafiki zake walimuua Sa'd, na kumtupa kwenyeshimo. Ile sauti iliyosema kwamba Sa'd ameuawa ni ile ya rafiki yake Khalid, siyoya majini.

Baladhuri amesimulia kwamba Umar alimuamuru Khalid na Muhammad IbnMuslima kumuua Sa'd na wakafanya hivyo.

Mtu mmoja wa Kundi la Ansari alitunga ubeti ufuatao kuhusu kifo cha Sa'd:

Sa'd aliuawa na majini wanasema,Ustadi ulioje; huo sio wa kawaida kabisa, njia………Sa'd hakutenda dhambi ile iliyo ndogo kabisa katika nchi,Lakini vilevile hakuushika mkono wa Abubakr.

Wanahistoria hawakupenda kuandika sababu ya kifo cha Sa'd. Baadhi yaowamelipuuza kabisa tukio hili, na wengine wamewashutumu majini. Kama wale

78

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

waliosema majini wamemuua Sa'd wangesema, "Majini waaminifu hawakupendaSa'd ampinge Abubakr, hivyo wakamuua." Basi ngano hii ingewezekana kuamini-ka kirahisi.

L . UMAR

Tumetaja mishughuliko yake kwa upande wa Abubakr wakati wa kiapo. Umaralisema, "Wengine wanabashiri kifo changu, na wanamkisia mrithi wangu. Ngojaniwafafanulieni hili; kile kiapo na Abubakr lilikuwa ni kosa, lakini Mungu alituokoana matokeo yake."

TATHMINI YA SIMULIZI YA SEIF

Tumeandika hapo kabla matukio ya kiapo cha utii kwa Seif na wengineo. Sasatunafanya ulinganisho kati ya simulizi zao. Seif amesimulia kwamba:

a) Hakuna aliyekataa kula kiapo na Abubakr isipokuwa waasi au waliokaribiauasi; na kwamba kundi lote la Muhajiriin lilipeana mkono na Abubakr kwahiari.

b) Ali alitoka mbio nje ya nyumba yake katika nguo ya usiku kuokoa muda,baada ya kuwa amesikia kwamba watu wamepeana mkono wa kiapo naAbubakr, na kwamba alipeana mkono naye pia. Walimletea nguo zakebaadae, na akazivaa.

c) Qa'qa alisema, "Nilikuweko Msikitini kwa ajili ya sala ya mchana, wakati mtummoja alipoleta habari za kifo cha Mtume; na za kukusanyika kwa Kundi laAnsari pale Saqifah, kumfanya Sa'd kuwa mrithi wake kinyume na amri yaMtume. Habari hii iliwafanya kundi la Muhajir kuwa na wasiwasi mkubwa."

d) Hubab Ibn Mundhar alikuwa karibu amshambulie Abubakr kwa upanga wake,lakini Umar aliupiga upanga huo kutoka mkononi mwake. Kisha Maansariwakasongamana kumpa mkono Abubakr, wakiruka juu ya kichwa cha Sa'd,ambaye alikuwa mgonjwa na amekaa njiani mwao. Kosa hili la Maansarililikuwa sawa na lile kosa lililotokea wakati wa ujahilia, lakini Abubakr alizuiamatokeo yaleyale kwa nguvu zote.

e) Sa'd alimwambia Abubakr, "Wewe na kabila langu, mmenilazimishanikubaliane nawe." Walikuwa wamemwambia, "Tungekulazimisha kuuachaumma ungeweza kuwa na sababu. Lakini tumekufanya ujiunge na kila mtumwingineo. Kama utakwenda kinyume na jamii, au kusababisha ufa,tutakukata kichwa chako."

f) Hotuba mbili ndefu zilitolewa na Abubakr.

g) Khalid Said Amawi alivaa koti la hariri wakati wa amani, na Umar akamwamu-ru kulichana. Kwa sababu hii Khalid akamwambia Ali, "Ewe mjukuu wa Abd

79

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Manafi, umelipoteza suala lako?" Ali akamwambia Khalid, "Unalichukulia hilikama mchezo?" Ndipo Umar akamwambia Khalid, "Mwenyezi Mungu akuk-wamishe mdomo wazi. Umesema kitu ambacho kitakamatwa na waongo(kutengeneza ngano za uzushi)."

Tunapolinganisha namna Seif alivyosimulia matukio haya, na vile ambavyowengine walivyosimulia, tunaona kwamba Seif ametengeneza kwa uhodari sanamatukio ya kukidhi malengo yake, kwa mfano:

A) Anasema kwamba Ali na Sa'd walipeana mkono wa kiapo na Abubakr siku ileile ya kwanza aliyomrithi Mtume. Bado wanahistoria wengine wametueleza juuya kuakhirishwa kwa makubaliano ya Ali na Sa'd kwa Abubakr. Licha ya yaleSeif anayosema, "Ali, kwa uwazi kabisa, aliidai nafasi hiyo, na Muhajirina naBani Hashim, kwa makubaliano na Ali, walikataa kiapo na Abubakr. Watu wotehawa walitaka kupeana mkono wa kiapo na Ali, na alimradi kwa muda huobinti yake Mtume alikuwa hai, hawakumkubali Abubakr." Kama yale Seifanayosema ni kweli, na Ali alikwenda kwa Abubakr siku ile ya kwanza hasa,basi ni nani alikuwa anashughulika na maandalizi ya mazishi ya Mtume?

B) Sa'd hakukubaliana na Abubakr. Aliishi Damascus na majini wakamuua kwamapigo mawili, kwa sababu hakuushika mkono wa Abubakr.

C) Kwa kusema kwamba Maansari walitaka kuvunja mkataba wa Mtume, nakufanya kiapo na Sa'd, Seif anataka kusema kwamba Mtume alimchaguaAbubakr.

D) Seif alitaka kuthibitisha kuchaguliwa kwa Abubakr na Mtume, pale aliposema,"Usama alimtuma Umar kwa Khalifa Abubakr alipopata habari za kifo chaMtume." Seif anaonyesha kwamba Abubakr alichaguliwa na Mtume.

E) Seif alibuni maneno ya Qa'qa kama ifuatavyo: "Watu, mmoja baada yamwingine kwa hiari zao walipeana mkono na Abubakr." Bado Qa'qa hakuishikamwe. Amekuwepo tu katika ngano za Seif.

F) Kuthibitisha kwamba baadhi ya Maansari wanampinga Abubakr, anasemakwamba Hubab - mmoja kundi la Maansari, alishambulia kwa upanga wake.Kusema kweli alikuwa ni Zubair, binamu wa pili wa Mtume, aliyekuwa mmojawa Muhajir - (Kundi la Ali) aliyeshambulia kwa upanga wake.

G) Umar alitoa kauli kwamba ule uchaguzi wa Abubakr ulikuwa ni makosa. Seifpia aliuita upinzani wa Ansari ni makosa kumlinda Umar na kuthibitisha ilekauli aliyoitoa Umar, kwamba ilikuwa dhidi ya Maansari.

H) Seif anasema kwamba hotuba mbili ndefu za uzinduzi zilitolewa na Abubakrbaada ya kiapo cha hadhara. Muundo na maneno ya hotuba zile mbilizinaonyesha kwamba ni za kughushi; na ile hotuba ya kweli ya uzinduzi yaAbubakr ni tofauti kabisa. Ule muundo wa zile hotuba za kughushi siyo sawa

80

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

na ule wa hotuba za Makhalifa watatu mara baada ya Mtume. Piahazikuandikwa vizuri kama kazi nyingine za Seif - inaelekea kwamba Seifhakuwa stadi katika kutunga hotuba za kidini. Tena, hotuba ndefu hazikuwakawaida katika wakati wa Mtume na wa Abubakr. Hizi hotuba ndefu zilianzawakati wa Ukhalifa wa Umar, na zilifikia kilele wakati wa enzi ya Ali. Hotubaya kwanza ya kiongozi yoyote kwa kawaida huwa ni fupi - ikionyesha ulempango mpya.

I) Ule usemi uliotumiwa na Abubakr kwamba shetani alikuwa akikaa ndani yake,ulikuwa kiasi unachekesha na kushusha hadhi. Seif alitaka kueleza wazo lakwamba baada ya Mtume, watu hawakutaka tena kujihusisha na uchamunguna utakatifu. Maneno haya kutoka kwa Khalifa wa kwanza, Abubakr, yali-fanana na dua yake baada ya jeshi la Usama liliposababisha Uislam kupatasifa mbaya.

J) Kitu cha kipekee kuhusu hotuba ya Abubakr inayodaiwa, kilikuwa kwamba,ilianzisha katika dini ya Kiislam mtazamo wa masikhara, kiasi kwamba watuwanaweza kuchukulia, kutoka kwenye hotuba ya kiongozi wa Waislam, kwam-ba Uislam haukuwa ni dini ya kweli, au baya zaidi kwamba hakukuwa namungu.Sababu ya tafsiri hii potovu ya Uislam ya Seif, ni kwa sababu ime-andikwa kwamba Seif alikuwa ni mkana mungu (asiyemuamini Mungu).

K) Seif anasema kuhusu Khalid Ibn Sa'd Amawi kwamba Khalid alivaa nguo yahariri, na Umar akaamuru kwamba ile nguo ichanwe. Kwa matokeo ya hili,hisia za Khalid kwa Abubakr na Umar zilikuwa ni za kisasi. Khalid akamwambiaAli, "Kabila lako (Abd Manafi) limeshindwa na kabila la Abubakr (Taim)." Aliakajibu, "Nafasi ya urithi wa Mtume, haihusiki chochote na umaarufu wa kika-bila. Ni nafasi ya ki-ungu." Khalid akamwambia tena Ali, "Kabila lako linastahi-ki sana kwenye nafasi hii." Ndipo Umar akamwambia Khalid, "MwenyeziMungu akunyamazishe, umesema kitu ambacho kitawafanya waongo kuzuangano." Hapa tena Seif anataka kusema kwamba ni Khalid tu aliyeamini kwam-ba umaarufu wa kikabila ulikuwa ndiyo dhamira ya watu kuwaunga mkonowagombea, vinginevyo, Muhajir na Ansari walikuwa hawana hatia kabisakuchanganya siasa ya makundi na dini. Hivyo Ali na Umar wote walimdharauKhalid. Seif hapa tena anajaribu kuthibitisha kwamba hakukuwa na upinzanikwa Abubakr kuwa Khalifa.

L) Seif anatuambia kwamba hakukuwa na hitilafu kati ya Ali na Umar, na kamahitilafu yoyote itaonekana baadae, watu watadhani chanzo chake ni Khalid.Kwa hiyo Umar akamwambia Khalid, "Baadae waongo watatunga ngano zakile ulichokisema." Hii ni nukta muhimu na yenye kufaa kuangaliwa.

M) Kwa kumalizia, tusisahau kwamba Seif aliisimulia ngano hiyo hapo juu kutokakwa Sakhr aliyekuwa mlinzi wa Mtume; lakini Mtume hakuwa na mlinzi mwenyejina hilo.

81

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

N) Shambulizi la nguvu la Seif juu ya upinzani huo liko kwenye kusema kwake,"Hakuna yeyote aliyempinga Abubakr isipokuwa yule aliyekuwa muasi, aualiyekusudia kuuacha Uislam." Madai ya Seif yametoa sababu ya kuwafanyawasomaji waamini kwamba Waislam kwa pamoja walimkubali Abubakr kamaKhalifa, mbali na wale waliougeuka Uislam. Hapa tutawatambulisha walewaliompinga Abubakr na kumuunga mkono Ali kwa moyo wote; hakuna yey-ote anayeweza kumshuku yoyote kati yao kuhusika na shutuma za Seif za'Uasi'.

1. Zubair Ibn Al- Awam, binamu ya Mtume.2. Abbas, ami yake Mtume.3. Sa'd Ibn Waqqas, aliyeiteka Iraqi.4. Talha Ibn Ubaidullah.5. Miqdad Ibn Al- Aswad.

Wafuatao walikusanyika katika nyumba ya Fatima katika upinzani juu ya Abubakr.6. Abu Dhar Al- Ghifari.7. Salman Al- Farsi.8. Ammar Yassir.9. Bara Ibn Azib Al- Ansari.10. Ubbay Ibn Ka'b Al- Ansari.11. Fadhl Ibn Abbas, binamu ya Mtume.12. Abu Sufian Harb Al- Amawi.13. Khalid Ibn Said Al- Amawi.14. Aban Ibn Said Al- Amawi.

Kwa nyongeza ya hao kumi na wane hapo juu, hakuna katika Bani Hashim aliye-peana mkono wa kiapo na Abubakr mpaka binti ya Mtume alipofariki. Upinzaniwao ulikuwa tu kwa sababu ya kumuunga mkono kwao Ali. Mbali na watu hawa,Sa'd Ibn Ubaidullah alimpinga Abubakr, kwa vile yeye mwenyewe alikuwamgombea…….Anaweza mtu yoyote kuamini kwamba yeyote kati ya hao hapo juualigeuka kutoka kwenye imani ya Uislam? Au kwamba walikuwa waasi? Hawawalikuwa ndiyo wapinzani hapo Madina. Sasa tunawaelekea wale waliokuwa njeya Madina. Baadhi yao waliuawa kwa sababu waliipinga hiyo serikali kama vileMalik Ibn Nuwayrah, ambaye Seif alimtaja kama muasi. Yale mapambano dhidiyao yaliitwa na Seif Vita Tukufu dhidi ya waasi.

82

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

HITIMISHO

Seif ameichezea kwa ufundi sana historia ya Uislam katika ngano zake zauongo,kiasi kwamba wana historia, mutashirki, na hata ulimwengu wa Kiislamumewakubali wale mashujaa wa kubuni wa kitabu cha Seif kama masahaba wakweli wa Mtume, na mashuhuri wa Kiislam. Tunaamini wakati umefika wa kuu-fichua, kwa utafiti na mjadala, ukweli kuhusu historia ya Uislam; na kumtambulishaMtukufu Mtume wa Uislam na kizazi chake kitukufu, kwa walimwengu katika sifazao bainifu, kuliko kuzihami ngano za Seif kwa jina la Uislam.

83

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

3. RIDDAH { UASI}MAANA YA KIARABUMAANA YA QUR'ANI

KATIKA WAKATI WA MTUMEKATIKA WAKATI WA ABUBAKR

NA SEIF

ULINGANISHO

84

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

RIDDAH (UASI)Wapinzani wa Abubakr, nje ya makao makuu waliitwa 'Waasi', na vita vilivyopi-ganwa dhidi yao vilifunikwa kwa udanganyifu kama Vitakatifu.

UASI KATIKA UISLAM

Uasi ni 'Irtidad' (kuritadi) kwa Kiarabu ikimaanisha 'geuka'. Qur'ani inasema, "Basialipofika yule mwenye habari njema na akaiweka kanzu ya Yusufu usoni kwaYaqub kuona kwake kulimrejea (Irtadda)."

Neno 'Raddah' pia limetumika katika Qur'ani kumaanisha 'geuka kutoka kwenyedini' kama katika aya ifuatayo: "Enyi mlioamini, kama mtasikiliza kikundi cha walewaliopewa kitabu huko nyuma, watakurudisheni ( Yarudduukum) kwenye ukafirimbali na imani yenu:"

Tena katika aya hii: "Enyi mlioamini!Kama mtageuka (Yartadid) kutoka kwenye diniyenu, Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine anaowapenda na wanaompendaYeye. Ni wapole kwa waumini na n iwakali kwa makafiri.

Tunasoma pia ndani ya Qur'ani: "Wanapigana na ninyi ili wakuondoeni(Yarudduukum) kutoka kwenye dini yenu, na kama mkiiacha imani yenu, na kishamkafa, amali zenui zitakuwa bure."Lakini hili neno 'Irtaddah' limehusishwa marakwa mara na uasi, kwamba si chochote ila uasi ndiyo unaokuja akilini pale linapo-tumika.

WAASI WAKATI WA MTUME

Baadhi ya Waislam waligeuka (waliritadi) kutoka kwenye Uislam wakati waMuhammad kama wafuatao: Abdullah Ibn Abi Sarh.

Abdullah alikuwa mmoja wa waandishi wa wahyi wa Qur'ani aliyekimbia kurudiMakkah toka Madina. Alikuwa akiwaambia Maquraishi, kwamba aliandika manenotofauti na yale Muhammad aliyokuwa akimsomea. Kwa mfano, pale Muhammadaliposema, "Allah ni Mjuzi na Mwenye Hekima." Abdullah aliuliza kama anawezakuandika "Allah ni Mwenye Nguvu zote na Hekima." Muhammad atasema, "Hiyoni sawasawa kama inavyotumika."

Ile siku alipoiteka Makka, Muhammad alisema, "Damu ya Abdullah haina thamani,na hata kama atatafuta kimbilio katika Ka'ba, ni lazima auawe." Uthman akam-ficha, na baadae akampeleka kwa Mtume akiomba msamaha, ambao alipatiwa.

Muasi mwingine alikuwa ni Ubaidullah Ibn Jahesh, mume wa Umma Habiba,ambaye alihamia Ethiopia. Aliingizwa kwenye Ukristo, na akafa huko kamaMkristo.Abdullah Ibn Khatal alikuwa ni muasi mwingine aliyeuawa akiwa ameshika funiko

85

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

ya kuba Tukufu ya Ka'ba akitafuta kimbilio.

UASI WAKATI WA ABUBAKR

Habari zinazochoma moyo za kifo cha Mtume, zilienea kwa haraka kwenye rasi yaArabia yote. Yale makabila ambayo, mpaka hapo, hayajaingia kwenye Uislam, yal-ishangilia, na yakaendeleza juhudi zao dhidi ya Uislam. Makabila ya kiislam piayalishikwa na wasiwasi kwa sababu yalikwisha sikia kwamba baadhi ya masaha-ba wa Mtume, kwa sababu ya siasa ya makundi, walikuwa wakipigana wenyewekwa wenyewe kwa ajili ya cheo cha ukhalifa. Kule kutoridhia kwa ndugu waMtume, Bani Hashim, na upinzani wa Sa'd, mkuu wa kabila la Khazraj, kwaAbubakr kama Khalifa, kulisababisha baadhi ya makabila ya Kiislam kukitilia shakacheo cha Ukhalifa. Hawakukanusha imani yao, wala kukataa kusali au kupingakulipa kodi, walikataa tu kulipa kodi inayostahili kwa serikali ya Abubakr. Wapinzanihawa waliitwa 'waasi' na walikuwa waondoshwe kwa vita vilivyobatizwa kama nivya jihad. Baada ya kuwaangamiza wapinzani wao wa kiislam, serikali hiyoikayapiga makabila ya kipagani na mitume wa uongo na washirika wao. Hatimae,vikosi vilitumwa nje ya Arabia. Vita vyote vile vilivyopiganwa wakati wa Abubakr,viliitwa Riddah, (vita dhidi ya waasi). Hivyo wale wapinzani wa Kiislam wa Abubakrnje ya Madina waliitwa 'Murtadiina' - Waasi.

Dr, Hassan Ibrahim aliliunga mkono wazo hili katika kitabu chake: 'Historia yaSiasa za Kiislam'. Uk.251 : "Baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kufariki na kifochake kikathibitishwa, baadhi ya Waislam walisita juu ya ukweli wa Uislam, nawengine waliogopa kwamba Maquraish, au kwa kweli kabila lolote, linaweza kuin-gia madarakani na kuanzisha taifa la kidikteta. Walikuwa wakitambua kwamba niMtume wa Allah tu aliyekuwa mtakatifu (asiyefanya dhambi wala kosa), na mtumwingine yeyote atakayemrithi yeye, hatakuwa na sifa hiyo, ambayo ilimuweze-sha kuwaona watu wote, kama meno ya kitana, kuwa wako sawa. Kwa hiyo,walikuwa na mashaka kwamba kama mrithi wa Mtume atapendelea ukoo na kabi-la lake mwenyewe, na akayashusha makabila mengine, ingevuruga haki ya jamiiya Kiislam. Tunakisia hivi kwa sababu tunaona kwamba, baada ya Mtume, kilaMwarabu kiupendeleo aliunga mkono ukoo na kabila lake, na mwenendo wakiarabu wa kizamani, ukarudi. Huko Madina, Maansari walikuwa na hofu kwambaMuhajiriin na Maquraishi wataingia madarakani. Makundi mawili haya yalikuwayakitiliana shaka. Maansari walitaka serikali ya mseto. Muhajirina walitaka kiongoziatoke kwenye kabila lao, na msaidizi wake awe Ansari. Wale Aws na Khazraj,sehemu za Ansari, zilisalitiana zenyewe wakati wa uchaguzi wa Khalifa.

Makka hakukuwa salama zaidi ya Madina kwani huo uchaguzi ulisababishamgogoro wa kikabila huko vilevile. Bani Hashim hawakukubaliana na Abubakrkama Khalifa, Ali alikataa kumuunga mkono Abubakr na Abu Sufiani alijaribukumshawishi Ali kuandaa mapinduzi ya serikali (coup d'etat).

"Mwishowe Muhajirina, Maansari na Maquraish waliokuwa watangulizi katika

86

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Uislam na wafuasi wa Uislam, na jamaa za Mtume, hawakuweza kuungana kuun-da serikali kwa amani. Hili liliyafanya makabila mengine ya kiarabu kuishiwa naimani, na hatimae wakakata tamaa ya kuwa na sauti, au nafasi katika serikali hiyo.Kwa hiyo, wengi wao walimpinga Abubakr kama Khalifa na wakakataa kumlipazaka iliyostahili. Baadhi ya wanazuoni wa kigeni wanalichukulia hili kama uasi, nakama ushahidi wa kuendelea kwa Uislam kwa upanga huko Arabia. Hilo siyo kwelihata hivyo, kwa sababu wale watu ambao Abubakr amewapiga kama waasi, wal-ibakia waaminifu kwa Uislam." Walikuwa wa makundi mawili.

1) Lile kundi lililoamini kwamba Zaka ilikuwa ni kodi ya Mtume, na baada ya kifochake hakuna aliyestahili kuidai; hivyo walikataa kuilipa kwa Abubakr na kwaajili hii akapigana nao. Umar alitoa maelezo kwa niaba ya watu hao akisema,"Mtume alikuwa akisema, 'Napigana na watu mpaka waamini Mungu Mmoja,na yeyote anayemuamini Mungu, damu yake na mali zake vitalindwa.'"

2) Lile kundi ambalo hawakuamini hiyo dini. "Kwa kweli hawakuwa Waislam.Uongozi wa Kiislam katika wakati wa Abubakr ulijali tu juu ya kutekelezahukumu za kifo, na haukuzingatia juu ya waasi wanaorejea kwenye Uislam."

Bado, kwa mujibu wa Uislam, kama ilivyoelezwa na Dr. Hassan Ibrahim, "Muasiyeyote lazima apate siku tatu za kujadili maoni yake na viongozi wa kidini. Hivyo'wacha shutuma zithibitishwe kabla hajaangamia, na yule anaebakia salamaanakuwa hivyo kwa uthibitisho.'"

Kuliweka sawa jambo hili, tunarejea kwenye baadhi ya maoni ya viongozi waSunni. Imam Abu Hanifah anasema: "Muda mfupi kabisa unaoruhusiwa kwa mtukurekebisha mawazo yake ni siku tatu. Kama Murtadi anaomba muda wanyongeza, mpatie siku tatu za kujadili hoja zake."

Imam Malik anasema: "Murtadi , awe mtumwa au muungwana, mwanamume aumwanamke, mpatie siku tatu tangu siku aliyothibitika kuwa ni Murtadi . Anawezakupewa chakula na asiteswe."

Imam Shafii anasema: "Murtadi, mwanamme au mwanamke, lazima aheshimiwekwa sababu yeye alikuwa Mwislam wakati fulani. Wengine wanasema mpenyongeza ya siku tatu."

Imam Hanbal anasema: "Murtadi, mwanamme au mwanamke, kama siyo majinunilazima aitwe kwenye Uislam kwa siku tatu."

"Pamoja na maoni hayo hapo juu, siyo haki kusema kwamba Mwislamamekanusha imani yake kwa kukisia tu, labda kila Mwislam aseme kuwa ni muasi.Baadhi ya wanazuoni wa Kiislam wamesema kwamba kama mtu ni Mwislamu asil-imia moja, siyo haki kumchukulia mtu huyo kama ni Murtadi mpaka iwe imethibiti-ka kwamba kweli yuko hivyo."

87

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Huu ndio mwisho wa maelezo ya Dr. Hassan Ibrahim ndani ya kitabu Historia yaSiasa za Kiislam.

Ibn Kathir katika kitabu chake cha Albidaya Wannihaya, juz.6,uk.311, anasema:"Wapokezi wote, isipokuwa Ibn Majah, wameandika kwamba kwa mujibu wa AbuHurairah, Umar alimkatalia Abubakr kupigana na watu, akisema kwamba Mtumealilinda roho na mali za yeyote aliyekiri Upweke wa Allah na Unabii waMuhammad, labda walipopatikana na hatia. Abubakr akajibu, 'Wallah, nitawapigawale ambao hawanilipi Zaka ile ambayo ilikuwa ikilipwa kwa Mtume wa MwenyeziMungu. Na iwe ngamia au kamba ya kufungia ngamia. Wallah, nitampiga yeyoteanayetofautisha kati ya kulipa Zaka na kusali. Nitawapiga mpaka wanipe ile zakawaliompa Mtume.' Umar akasema, 'Pale nilipoiona dhamira ya Abubakr ya kupi-gana, nikaelewa kwamba alikuwa na haki.'"

Kwa mujibu wa Tabari (juz.2,uk.474), waasi walimwendea Abubakr kwa vikundi,wakikubali Swala, lakini wakipinga kulipa Zaka. Abubakr hakukubali maoni yao naaliwafukuza. Ibn Kathir ndani ya Albidaya Wannihayah (juz.6,uk.311), anasemakwamba makundi ya Waarabu yalikuwa yanakuja Madina waliokubali sala lakiniwakakataa Zaka. Walikuwepo baadhi waliokuwa hawataki kutoa Zaka kwaAbubakr, baadhi yao walikuwa wakisoma ubeti huu:

Pale Mtume alipokuwa miongoni mwetu, tulikuwa watiifu,Lakini kipindi cha Abubakr ni tukio la kipekee,Ambalo limetuvunja migongo yetu, tutaasi,Bado, anaweza akamfanya mwanae Khalifa hapo atakapokufa.

Katika Tabari (juz.2,uk.48), Seif ameandika kutoka kwa Abu Makhnaf kwambawapanda farasi wa kabila la Tay walitoa maneno juu ya wapanda farasi wa maka-bila ya Asad na Fazareh, wakati walipopishana. Lakini hapakuwa na mapambanokati yao. Watu wa Asad na Fazareh walipenda kusema, "Hatutakubaliana na Abul-Fasil" (lakabu ya Abubakr, ikiwa na maana ya baba wa mtoto wa ngamia). Walewapanda farasi wa kabila la Tay hujibu, "Tuna uhakika mtakubaliana na Abul-Fahl-Akber." (yenye maana ya baba wa ngamia mkubwa, mtu mkubwa).

Kutokana na ngano hiyo hapo juu inaeleweka kwamba ule uasi katika wakati waAbubakr ulikuwa siyo wa kukana imani, bali ni katika kukwepa kulipa Zaka kwaAbubakr.

Kwa vile makundi yaliyoshindwa ni ya Mabedui na Wahamaji, hayakuwa na nafasiya kutawala, lakini wapinzani wao, watawala wa wakati huo, walikuwa na mamla-ka mikononi mwao kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kile ambacho ndani yakehistoria ya wakati huu iliandikwa. Pia historia ya yale matukio ambayo imetufikiasisi yameandikwa kwa rejea zao. Ni juu yetu kuchunguza ukweli wa ngano zile zili-zo andikwa juu ya watu walioshindwa.

88

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Tabari katika kitabu chake (juz.6,uk.461), ameandika kutoka kwa Seif kwambaWaarabu waliikana imani yao baada ya Abubakr kuwa Khalifa. Uasi ulikuwa ndiyomtindo wa kawaida wa wakati huo, lakini yalikuwepo makabila ambamo ni sehe-mu tu iliyokuwa ya kiuasi. Ni makabila ya ki-Quraish na Thaqif tu yaliyobakia kuwawaumini.

Seif amempita Antara Ibn Shaddad na waandishi wengine wa uongo katika kubuni.Mashujaa wa ngano za Seif wanatembea kwenye maji bila kulowesha nyayo zao.Wanaongea na wanyama wa porini - malaika wanawasiliana nao - wanatoa chem-chemi kutoka kwenye mawe huko jangwani. Zaidi ya hayo, Seif amesimulia nganozake katika namna ya kuwapendeza watawala wa wakati huo, na kuuficha ukwelikwamba walikuwa wasiopendwa na watu.

Ili kuonyesha ni katika mtindo gani Seif ameziandika ngano zake, tutazitoa baad-hi yake kutoka kwenye kitabu chake, al-Futuuh Wal-Riddah zilizoandikwa katikakitabu cha Tabari.

89

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

4. MALIK IBN NUWAIRA

KAMA ILIVYOANDIKWA

NA SEIF

NA WENGINEO MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

90

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

MALIK IBN NUWAIRABwana huyu alikuwa ni wa kabila la Yarbu na wa ukoo wa Tamim. Alikuwa akiju-likana kama Abu Handhalah na lakabu yake ilikuwa Jafoul.

Marzubani ameandika kwamba Malik Ibn Nuwaira alikuwa mshairi, msomi, nampanda farasi mashuhuri katika kabila lake. Baada ya kuingia katika Uislam,Mtume alimteua kuwa mkusanya Zaka kwenye kundi la familia yake. Mtume alipo-fariki, Malik hakutoa makusanyo yake serikalini, bali aliyagawanya miongoni mwafamilia yake akisema:

Fedha mliyonipa nitairudisha,Matatizo ya kesho hayatuhusu sisi,Kama mtu, siku moja, atajaribu kuurudisha Uislam,Tutakuwa watiifu kwa Serikali hiyo.

Tabari katika juz.2,uk.503, ameandika kile kisa kutoka kwa

Abdul-Rahman Ibn Abubakr, kama ifuatavyo:

"Wakati jeshi la Khalid lilipofika Butah, alituma kikundi cha askari wake, chini yauongozi wa Zirar Ibn Azwar, kushambulia kabila la Malik usiku kucha. Abu Qatada,mmoja wa jeshi lile alisema baadae, 'Tulipolishtukizia kabila la Malik usiku kuchatuliwatishia. Walivaa mavazi yao ya kivita yenye deraya haraka haraka, nawakatangaza kwamba wao walikuwa ni Waislam. Kamanda wetu akawauliza nikwa nini wana silaha, na wao wakamuuliza swali hilo hilo. Tuliwaambia wawekesilaha zao chini, kama walikuwa ni Waislam, na wakafanya hivyo. Kisha tulisalisala zetu, na wao wakafanya vivyo hivyo.'"

Ibn Abil-Hadid katika kitabu chake anasema, "Walipoacha silaha zao, wale askariwakawafunga pingu, na wakawapeleka kwa Khalid."

Katika Kanzul Ummal, juz.3,uk.132, na ndani ya Yaqubi, juz.2,uk.110, ngano hiyohapo juu imeandikwa kama ifuatavyo: "Malik Ibn Nuwaira pamoja na mkewewalikuja kwa Khalid. Khalid katika kumuona yule bibi alimpenda, na akamwambiamumewe, 'Hutarudi nyumbani kamwe, Wallah, nitakuua."

Katika Kanzul Ummal, juz.3,uk.132, imeandikwa kwamba Khalid alimshutumuMalik kwa uasi, ambapo Malik alikataa na wote Abdullah Ibn Umar na Abu Qatadawaliingilia kati kwa niaba yake. Lakini Khalid akamuamuru Zirar Ibn Azwar kumka-ta kichwa. Kisha Khalid akamchukua mke wake Umma Tamim na akalala naye.

Katika Abdulfada uk.158 na ndani ya Alwafaiat, imeandikwa Abdullah Ibn Umaralizungumza bila mafanikio na Khalid kuhusu Malik, na Malik akaomba apelekwekwa Abubakr kwa ajili ya uamuzi wake. Khalid akasema, "Mwenyezi Mungu

91

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

hatakusamehe kama mimi nitakusamehe," na akamuamuru Zirar kumkata kichwa.Malik alimuangalia mkewe akisema, "Wewe ndiyo sababu ya kuuawa kwangu."Khalid akasema, "Mungu amesababisha kifo chako kwa sababu ya uasi wako."Malik akasema, "Wallah mimi ni Mwislam na dini yangu ni Islam." Lakini Khalidakamuamuru Zirar kumkata kichwa chake.

Imeandikwa ndani ya al-Isaba, juz.3,uk.337 kwamba Thabit Ibn Qasim ameandikandani ya al-Dalail kwamba Khalid alimpenda mke wa Malik katika kumuona kwamara ya kwanza, kwa vile alikuwa mzuri sana.

Malik alimwambia mkewe, "Wewe umeniua."

Imeandikwa pia katika al-Isaba kwamba Zubair Ibn Bakkar ameandika kutoka kwaIbn Shahab kwamba Khalid aliamuru kichwa cha Malik kitumike kama nishati yamoto wa kupikia. Lakini kabla ya moto kuifikia ngozi ya kichwa cha Malik, chakulakikawa kimeiva, Malik alikuwa na nywele nyingi. Khalid, usiku uleule akamuoa mkewa Malik aliyeuawa.

Abu Namir Sa'di ametunga shairi lifuatalo:

Hivi wale wapanda farasi waliotushambulia wakati wa usiku,Wanajua kwamba kamwe hatutauona mwanga wa asubuhi?Khalid alikuwa amuondoe Malik kwa kweli, Kumchukua yule mwanamke aliyempenda hapo kabla,Khalid hakuwa na utashi wa kuepukana na matamanio yake,Na kuiambaa ile dhambi, hakuwa na uchamungu unaohitajika,Asubuhi ya usiku ule maskini yule mume akatoweka,Mke wake mikononi mwa Khalid.

Imeandikwa katika al-Isaba kwamba Minhal aliuona ule mwili wa Malik usio nakichwa na akaufunika.

Hiyo ilikuwa ni simulizi ya Malik. Na tuone sasa ni hatua gani zilichukuliwa naserikali kwa Jenerali wake.

Yaqoubi ameandika kwamba Abu Qatada alilieleza tukio hili kwa Khalifa Abubakrna kusema, "Wallah sitakwenda popote chini ya uongozi wa Khalid. AmemuuaMalik, japokuwa alikuwa Mwislam."

Tabari ameandika kutoka kwa Ibn Abibakr kwamba Abu Qatada aliapa kwambakamwe hatapigana chini ya Khalid. Yaqubi ameandika kwamba Umar Ibn Al-Khatab alimwambia Abubakr, "Ewe mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Khalidaliangukia kwenye mapenzi na mke wa Malik, na siku hiyohiyo akamuua Malikambaye alikuwa Mwislamu." Abubakr alimwandikia Khalid kutaka maelezo, naKhalid akaja kwa Abubakr akisema, "Ewe mrithi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu,katika kumuua Malik nilifanya uamuzi wa sawasawa kabisa, lakini pia nilifanyakosa."

92

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Mutammim Ibn Nuwaira, kaka yake Malik, alitunga idadi fulani ya mashairi akiom-boleza mauaji ya ndugu yake. Alikwenda Madina na akajiunga kwenye Swala yajamaa iliyoongozwa na Abubakr. Baada ya sala hiyo Mutammim aliegemeakwenye uta wake, na akimwambia Abubakr, alisoma:

Ewe Ibn AzwarUliutupa chini mwili wa mtu mwenye daraja,Wakati upepo mwanana wa asubuhi unapapasa mlango wetu.Ulimhadaa kwa kutumia jina la Mwenyezi Mungu,Lakini muumini Malik siku zote aliheshimu neno lake.

Abulfada ameandika kwamba pale habari za Malik zilipomfikia Abubakr na Umar,Umar alimwambia Abubakr, "Khalid bila shaka amefanya zinaa; ufanye apigwemawe."

Abubakr akajibu, "Sitafanya hivyo." Umar kisha akasema kwamba Khalid ameuwaMwislamu, na kwa hiyo ahukumiwe kifo. Abubakr akasema kwamba Khalid ame-tekeleza majukumu yake na aliyaelewa - pia amefanya kosa. Umar alimuombaAbubakr amfukuze Khalid. Lakini Abubakr akasema, "Kamwe sitaufutika upangaambao Mungu ameutoa kwenye ala yake."

Tabari ameandika kutoka kwa Ibn Abibakr kwamba Khalid alitoa kisingizio kwaAbubakr akisema kwamba Malik alimwambia, "Sidhanii kwamba sahiba wako(Mtume) alisema hili na lile." Khalid alijibu, "Hakuwa (Mtume) sahiba wako wewe?"na aliamuru akatwe kichwa chake na wanaume wote waliokuwa na Malik,wakatwe vichwa vyao pia.

Habari ilipomfikia Umar, aliijadili na Abubakr akisema, "Yule adui wa Mungu ameuaMwislamu na, kama mnyama mara tu amemkera mke wake."

Khalid alirudi nyumbani, kisha akaenda Msikitini akiwa amevaa joho lenye doa lakutu iliyotoka kwenye mavazi yake ya chuma ya kivita, na unyoya kwenye helmetiyake kama askari wa Kiislam. Alimpita Umar ambaye kwa ghadhabu alimvamia,akichomoa ule unyoya kwenye helmet yake huku akisema, "Kama mnafiki, umeuaMwislamu, na kama mnyama, ukamvamia mke wake, Wallah, nitakupiga mawempaka ufe. Hicho ndiyo unachostahili."

Khalid alibaki kimya akidhani kwamba Khalifa Abubakr atasema kwamba anahatia. Lakini pale Khalid alipotoa taarifa ya mafanikio ya safari yake na kukiri kosalake, Abubakr alimsamehe. Akiwa njiani kurudi kutoka kumuona Khalifa, Khalidalimpita Umar tena na akamkemea:

"Ewe mwana wa Umma Shamlah - sasa niambie kile ulichotaka kusema." Umarakaelewa kwamba Abubakr amemsamehe Khalid, na akaondoka pale Msikitini naakaenda nyumbani kimya kimya.

Huu ndiyo mwisho wa kisa cha Khalid na Malik kwa mujibu wa rejea sahihi. Lakini

93

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Seif ameielezea ngano hiyo katika matukio saba, kila moja likisifu jingine, na Tabariameiandika na matukio ya mwaka wa 11 Hijiria kama ifuatavyo:

NGANO YA MALIK KWA MUJIBU WA SEIF

1) Tabari wakati akiandika simulizi za Seif juu ya Bani Tamim na Sajah anasema,"Wakati Mtume wa Mungu alipofariki, wawakilishi wake katika Bani Tamim wal-ihitilafiana kila mmoja juu ya ni nani wampe ile Zaka ambayo wameikusanya.Kwa kweli watu wa nchi ya Bani Tamim waligawanyika, wengine wakibakiawaaminifu, na wakibishana na wale ambao hawakumtii Abubakr. Malik alikuwammoja wa upinzani na hakulipa Zaka aliyoikusanya kwa Abubakr.

Sajah, ambaye alidai kuwa mtume, baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliandi-ka barua kwa Malik akiomba kukutana.

Malik, Sajah na Waki walikutana na kufanya mkataba wa kutoshambuliana nakuwa na ulinzi wa pamoja.

2. Seif akiandika uasi wa watu wakazi wa Bahrain anasema, "Ala Ibn Hadhramialitumwa kwenda kuwashughulikia waasi hukoYamama. Waligawanyika katikamakundi mawili - waasi na waumini, wakibishana wenyewe kwa wenyewe.Wale waumini wakaungana na Ala Ibn Hadhrami. Malik na wenzie walikuwahuko Butah, na walikuwa na mabishano na Ala Ibn Hadhrami."

3. Seif pia, kuhusiana na matukio hayo hapo juu anasema, "Wakati Sajah ali-porudi nyumbani, Malik alikuwa na mashaka na wasiwasi kidogo. Waki naSama's walikubali kwamba walifanya makosa, hivyo walitubu kwa dhati, nawakatoa ile Zaka iliyocheleweshwa mara moja kwa Khalid. Hapakuwa na cho-chote kilichovurugika katika jimbo la Bani Handhala isipokuwa tabia ya Malikna wale aliokuwa nao huko Butah. Malik hakuwa imara - siku moja alikuwasawasawa, na iliyofuatia akafanya mambo ya ajabu ajabu."

4. Seif tena anasimulia kwamba pale Khalid aliposafisha wilaya za Asad naGatafan na waasi, aliondoka kwenda Butah alikoishi Malik. Maansarihawakuwa na uhakika kuhusu Malik, na hawakufuatana naye Khalid, wakise-ma kwamba walikuwa na amri ya Khalifa ya kubakia Buzakha. Khalid akase-ma ni juu yake kuwasiliana na Khalifa, kwani alikuwa ndiye kamanda wa jeshi.Alisema pia kwamba hatamlazimisha kamwe mtu yoyote kufuatana naye kati-ka msafara wake wa kumshughulikia Malik. Kisha akaondoka zake. Maansariwakagundua kosa lao na wakiwa wanamfuata Khalid, hatimae wakamkuta.Khalid aliendelea mpaka akafika Butah, na kuona hakuna mtu pale.

5. Seif pia anasimulia kwamba Malik aliongea na watu wake kama ifuatavyo:"Enyi watu wa kabila la Bani Harbu, tuliwapinga viongozi na makamanda, laki-ni tulishindwa na kampeni yetu dhidi yao. Nawashauri msisimame kwenye njiayao. Nendeni kwenye miji yenu na majumbani kwenu. Watawala hawa

94

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

wameingia madarakani bila ridhaa ya watu." Baada ya hotuba hii watuwakatawanyika na Malik pia akaenda nyumbani. Hivyo pale Khalid alipowasilihapo Butah, hakukuta hata mtu mmoja hapo. Khalid ndipo akawatuma watuwake kama mubaligh wa kiislam, kuwakamata wale ambao hawakukubalianana mawazo yao, na kumuua yeyote yule atakayepinga kutiwa mbaroni. Kwakweli amri ya Abubakr ilitamka hivi: "Adhinini kila mtakapokwenda. Kama watuhawatajiunga na mwito wa sala, washambulieni ghafla, na wateketezeni kwamoto, au kwa njia nyingine yoyote. Kama watajiunga na mwito wa sala wapenimajaribio. Kama watakubali kulipa zaka yao, kubalini imani yao ya Kiislam,vinginevyo malipo yao ni kuangamia."

Askari wa Khalid walikuja na Malik, binamu zake na baadhi ya watu wa kabilalake, kutoka kwenye msafara wao huo. Abu Qatada na baadhi ya askari wenginewalitoa ushahidi kwamba Malik na watu wake walijiunga na mwito wa Swala, nawalisali pamoja nao. Lakini kwa sababu ya tofauti katika ngano za askari haokuhusu Malik, alifungwa kwa usiku mzima na watu wake. Lakini ulikuwa ni usikuwenye baridi kali sana, na Khalid akaamuru wafungwa wale wapashwe moto.Maneno yaliyotumiwa na Khalid katika kutoa amri hii, pia yana maana "kuua" kati-ka lugha ya baadhi ya watu wa makabila 'idfau usara-akum' Hivyo wakamuuaMalik na wenzake. Chakari (muuaji) wa Malik alikuwa Zirar Ibn Azwar. Mayowe yakufa huko yalimtoa Khalid nje ya nyumba, ambapo alijua juu ya mauaji hayo.Akasema, "Kile Mungu alichoamuru, kimefanyika."

Baada ya tukio hili Abu Qatada alibishana na Khalid, na akaenda Madina kutoataarifa kwa Khalifa. Abubakr aliisikiza habari hiyo lakini akaonyesha kutoridhishwana Abu Qatada. Umar akaingilia kati, hivyo Abubakr akamsamehe Abu Qatada, naakamrudisha kwenda kujiunga na Khalid kwenye medani ya vita. Khalid akamuoaUmma Minhal, mke wa Malik aliyeuawa, lakini hakuishi naye mpaka mwisho wakipindi cha asubuhi cha mume wake wa kwanza.

Umar akamwambia Abubakr "Kuna namna ya uasi katika upanga wa Khalid -angalau kwenye suala la Malik." Abubakr hakujali kabisa kwani hajawakaripia watuwake kamwe kwa makosa yao. Hivyo alimuomba Umar aache kumkashfu Khalidna akasema, "Khalid anaweza kuwa hakuuelewa ujumbe wake." Abubakr ndipoakalipa fidia ya damu ya Malik, na akamwandikia Khalid kumwambia aje Madina.Khalid aliliarifu tukio hili kwa Abubakr aliyesamehe kosa la Khalid, lakini akamsu-ta kwa ndoa ile kwani ilikuwa kinyume na desturi ya Kiarabu.

6. Seif, mahali pengine, anasema kwamba baadhi ya askari walimshuhudia Malikakisali lakini wengine walilikataa hili na wakahalalisha kuuawa kwake. Kakayake Malik alitunga mashairi ya maombolezo, na akadai fidia ya damu yandugu yake, na kurudishwa kwa wale wafungwa. Abubakr aliidhinisha kuachi-wa kwa wale mateka. Umar alisisitiza kufukuzwa kwa Khalid kwa vile hakuwezakudhibiti upanga wake. Lakini Abubakr akasema kwamba hataurudisha upan-ga wa Mungu, ambao ulikuwa dhidi ya makafiri, kwenye ala yake.

95

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

7. Seif katika ngano yake ya mwisho, anasema kwamba Malik alikuwa na nywelenyingi. Pale vichwa vya wale waliouawa vilipotumika kama kuni za moto wakupikia, moto ulifikia ngozi za vichwa vyote isipokuwa katika kichwa cha Malik, kwasababu ya nywele zake nyingi. Mutammim alitunga shairi, na alielezea kupen-dezwa kwake na tumbo tupu la Malik kama mfano kwa askari wake wote. Umarambaye alimuona Malik mbele ya Mtukufu Mtume pia alipendezewa na Malik.

Hii ndiyo kumbukumbu ya mwisho ambayo imepatikana katika maandishi ya Seifkuhusu Malik.

KIINI CHA NGANO ZA SEIF

Kwa mujibu wa Seif, dondoo tatu za kwanza kati ya hizo saba hapo juu, zilitokakwa Sa'ab, mtoto wa Atyya, ambaye naye alizisikia kutoka kwa baba yake, Atyyamtoto wa Balal. Hiyo dondoo ya tano na ya saba zilisimuliwa na Uthman, mtoto waSuwaid, mtoto wa Math'abah.

NI NANI HAWA SA'B, ATYYA NA UTHMAN?

Hakuna dalili katika kitabu chochote cha historia ya Sa'b, Atyya au Uthman, hawawasimulizi watatu wa asili; ambao Seif amewanukuu.

Tunaweza kusema kwa hiyo kwamba hawa watatu ni miongoni mwa masahabamia na hamsini wa Mtume waliobuniwa na Seif.

Seif katika baadhi ya mambo kwenye ngano zake, amebadilisha watu wa kubuni,kama katika suala la Uthman, ambaye ameandika kutoka kwake. Hakuna dalili yaUthman katika kitabu chochote isipokuwa kwenye kitabu cha Seif. Suwaid yulebaba, na Math'ab (Shu'bah) babu yake Uthman walikuwa ni watu hasa waliokuwe-po .

Katika ngano ya mbwa pale Hawab, yule mwanamke halisi Umma Qirfa ni mamawa mtu wa bandia. Umma Zamal, na mwanaume halisi, Hurmuzah, ni baba waQumaziban, pia mtu wa bandia aliyebuniwa na Seif.

KWA NINI NGANO ZA SEIF NI ZA UWONGO?

Waandishi wa wasifu wametayarisha orodha ya wote na msimuliaji kila walioishikutoka wakati wa Mtume, na mbele mpaka wakati wa utawala wa Bani Abbas,ambao wametawala baada ya utawala wa Amawiyah. Wale wapokezi ambao wal-imkuta Mtukufu Mtume ndiyo kundi la kwanza, wanaitwa Masahaba. Kundi la pilini wale waliowakuta Masahaba, na walipokea ngano kutoka kwao, hawa wanait-wa Wafuasi (Tabi'in), na waliishi hadi mwaka wa 126. Kundi la mwisho la Tabiinwamekusanya mambo tu kutoka kwa wale tabi'in wa mwanzo, na waliishi hadimwaka wa 132. Vilikuwepo vikundi kumi na nne kwa jumla, na cha mwishokilikuwa wakati wa Mansoor, Khalifa wa pili wa Bani Abbas.

96

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Waandishi wa wasifu wengine wameorodhesha wapokezi, waliokufa katika miakakumi kama rika moja. Hivyo hasa, kundi la kwanza ni wale wapokezi waliokufakatika muongo wa kwanza, na kundi la pili ni wale waliokufa kwenye muongo wapili, na kadhalika. Wale wapokezi waliitwa 'Wanazuoni' na wale waliowafikishiangano hizo kwao waliitwa 'Sheikh'. Maisha ya kila Sheikh mmoja na Mwanazuoniyameandikwa kwa kina, walipoishi, na kama walikuwa Shia au Sunni, kamawalikuwa wakereketwa kumpendelea Ali au dhidi ya Ali, kama walikuwa wapenziau wapinga serikali. Hivyo vitabu vilivyotayarishwa viliwekwa katika orodha tofauti- vingine kwenye mpango wa alfabeti kama Tarikh Kabir, n.k. Vingine kulingana nawakati, kama Ibn Athir, n.k. Baadhi ya waandishi wa wasifu wameyapanga majinaya wapokezi kulingana na makazi yao, Makka, Madina, n.k.

Elimu ya upokezi wa Hadithi ilikuwa ndiyo ya kuvutia sana na somo maarufu lawakati huo na waandishi mbalimbali wa wasifu wameyapanga majina ya wapokezikatika njia mbalimbali, na wametoa uangalifu wao wa hali ya juu katika kuandikahayo maelezo. Hata hivyo kuna vitabu vilivyoandikwa kusahihisha makosa yawaandishi wa wasifa, kama vile al-Mukhtalif, n.k., hivyo hakuna sababu yoyote yamashaka juu ya utambulisho wa hao wapokezi.

Kwa vile idadi ya wapokezi ilikuwa ndogo katika wakati wa Bani Umayya, na Seifaliandika vitabu vyake viwili kuwapendeza watawala wa wakati huo, Bani Umayya,ambapo hatuwezi kupata majina ya watu ambao Seif ameandika kutoka kwao,kwa msingi wa maelezo ya hapo juu, tunaweza kusema kwamba Seif amebuni haowapokezi wake, na akanukuu kutoka kwa watu hawa bandia.

MATIN YA NGANO ZA SEIF

Katika masuala mengine, Seif ametumia majina ya baadhi ya wapokezi wa kwelikatika ngano zake za uwongo, kama vile katika tukio la tano na la saba, tuliyok-wishataja kabla. Uchunguzi makini na wa utaratibu, kulingana na kanuni za elimuya ngano, unaonyesha kubatilika kwa dondoo hizo.

ULINGANISHO

Ulinganisho kati ya ngano ya Seif na masimulizi ya wapokezi wengine kuhusuKhalid unaonyesha kwamba Seif alilichezea hilo tukio kufuta shutuma za Khalid,za lile shambulio lake dhidi ya Malik, na ule uvamizi kwa mke wa Malik.Anayaandaa mandhari nyuma; kwanza kabisa kumshutumu Malik kwa kuwa namashaka juu ya Uislam; pili yale mabishano ya waumini pamoja naye na tatu kuru-di kwa Sajah, na kusita kwa Malik. Kisha kwa sababu rejea nyingine zimeelezakwamba Malik alikuwa peke yake, Seif anadokeza kwamba Malik alikuwa na vikosipamoja naye, lakini alivifuta siyo kwa sababu alitubia bali kwa sababu ya hofuyake. Seif kwa hiyo anatamka kwamba Malik alikuwa muasi.

Katika ngano zingine Seif amedokeza uasi wa Malik, bila kutaja jina la Khalid ili

97

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kuondoa mawazo ya kutoka kwenye amri ya Khalid ya kumuua Malik nauhwosiano wake na mke wa Malik.

Seif ameubuni kule kupingana kwa wale askari na amri ya Abubakr,kumuangamiza Malik, mbele ya Khalid hivyo anamsafisha Abubakr vilevile naKhalid. Seif alitaka kuonyesha kwamba Khalid hakutaka kumuua Malik, alitoa amritu ya kuwapasha moto wale wafungwa, lakini wale askari walidhani alimaanisha'ua' kwa sababu ya kutoelewana kutokana na matatizo ya lahaja, bado yulealiyetoa amri, na wale machakari (wauaji) walikuwa na lahaja moja (Quraish naBani Asad). Ukweli unabakia kwamba kuchukulia kwamba kutokuelewana kulis-ababisha mauaji, basi kwa nini vile vichwa vitumike kama kuni za moto wakupikia.?

Tabari ameandika ngano ya Malik kutoka kwa Seif na Ibn Athir, Ibn Kathir,Mirkhand wamenukuu yale 'mambo' yaliyoandikwa na Tabari. Kama nyaraka zawanahistoria wengine, kwa waandishi wengine, walioitaja ngano ya Malik kutokakwenye rejea zingine mbali na Seif zitachunguzwa, basi hitilafu kati ya 'Matendo' ya Seif na ukweli hutokea.

Zile rejea nyingine zinazoeleza kwamba Khalid alitoa amri ya dhahiri ya kumuuaMalik ni kama ifuatavyo:

Hiyo hapo juu ni moja ya vita zilizopiganwa kwa jina la Uasi (zilizopiganwa naAbubakr). Vita hii inaweza kuchukuliwa kama mfano.

Futuuhul-Buldan Cha Baladhuri Uk.105

Tahdhib Cha Ibn Asakir Uk. 105, 112

Alkhamis Cha Diyar Bakri, Juz.2 Uk. 333

an-Nihaya Cha Ibn Athir, Juz.3 Uk. 257

as-Sawaiq al-Muhriqa Cha Ibn Hajar Al- Makki (chapa ya Misri) Uk.21

Taj al-Aruus Cha Zabidi, Juz.8 Uk.75

98

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

5. NGANO YA ALA IBN HADHRAMIKUTOKA KWA SEIF

NGAMIA WANAOTOROKAMUUJIZA WA CHEMCHEMI

KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

99

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

NGANO YA ALA IBN HADHRAMI

Ala Ibn Hazrami mwana wa Abdullah, mwana wa Ibad mwana wa Akbar mwanawa Rabi'a mwana wa Malik mwana wa Uwaif Hadhrami. Abdullah, baba yake,alikuwa mwenyeji wa Makkah na rafiki wa karibu sana wa Harb Ibn Umayya.Mtume alimteua kuwa Gavana wa Bahrain. Abubakr na Umar walimruhusu kushik-ilia nafasi yake mpaka alipokufa katika mwaka wa 14 au 21 Hijiria. (al-Istiab, chapaya 3,uk.146-148 na al-Isaba, chapa ya 2,uk.491.)

SEIF ANATUELEZA KUHUSU ALA IBN HADHRAMI

Katika Tabari 2-522, 528 Seif ameandika kutoka kwa Minjab Ibn Rashid kwambaAbubakr alimwamuru Ala kuwapiga waasi wa Bahrain. Minjab alikuwa katika jeshihilo. Anasema, "Tulifika katika bonde la Dahna, ambako Mungu aliamua kutuonye-sha muujiza. Ala na sisi, tulikuwa wote tumeshuka kwenye vipando vyetu.Ghaflangamia wetu wakashtuka na wakakimbia na mahitaji yetu yote, na wakatuacha bilakitu chochote katikati ya lile jangwa la mawe tupu. Pia kabla hatujapata muda wakujenga mahema yetu. Tulihuzunika sana na kukanganyikiwa, na tukaachianawosia zetu mmoja kwa mwingine. Mwito ukaja kutoka kwa Ala tumwendee - sisiwote. Hivyo tukajiunga naye. Aliuliza sababu ya kuvunjika moyo kwetu na tukajibu:'Unategemea nini kwa kundi ambalo hakuna kitakachobakia kesho, isipokuwasehemu yao katika historia.' Alituliwaza akisema, 'Waislam wanaweka imani yaokwa Allah, ukweli Allah hatawatelekeza wale ambao wako kwenye hali kama yetu.'Siku iliyofuata baada ya sala ya alfajir, Ala alipiga magoti nasi tukafanya vivyohivyo na tukamuomba Mola atupe maji, Ala ndipo akaona viwimbi. Akamtuma mtuakaangalie kama yalikuwa ni maji, lakini ilikuwa ni mazigazi tu. Mazigazi hayohayo yalichunguzwa baadae. Mara ya tatu mjumbe alirudi na habari kwambakulikuwa na maji, hivyo vikosi vikanywa na vikaoga, kisha ghafla ngamia wetuwalionekana, na walirudi kwa kupenda kwao wenyewe pamoja na mahitaji yetusalama vilevile kama wakati kabla hawajaondoka."

Baada ya kuondoka mahali pale rafiki yangu Abu Huraira akaniuliza kamanitaweza kupajua pale mahali tena, ambapo yale maji yalipatikana. Nikajibu kwam-ba ninapajua pale mahali vizuri zaidi kuliko mtu mwingine yoyote. Aliniomba nim-peleke kwenye yale maji tena. Nikafanya hivyo; lakini palikuwa hapana maji,hapana kidimbwi, bado tukaona jagi limejaa maji. Abu Huraira akasema kwambani jagi lake ambalo aliliacha pale kwenye kidimbwi kwa makusudi kuona kamapalikuwa na kidimbwi kweli pale ama ni muujiza ulitokea. Minjab aliapia kwambahajawahi kuona maji pale kabla na Abu Huraira akamshukuru Mungu kwa muujizahuu. Kisha Seif anasema Ala alishinda vita hiyo (dhidi ya waasi) wakati wa usikuwalipokuwa waasi wote wamelewa.

100

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Baada ya Ala kuwa na uhakika wa kuangamia kwa wale waasi alitoka na vikosivyake kuelekea Darain; lakini kabla ya kuondoka alitoa hotuba kwa askari wake.Alisema kwamba Mungu ameonyesha muujiza katika nchi kuwatia moyo na yalemaji (katika uvamizi wao unaofuatia kwa waasi). Kisha akaamuru mashambuliziakisema, "Tusonge mbele na tuivuke bahari, Mungu amewazingira maadui mahalipamoja kwa ajili yenu." Wale askari wakakemea, "Wallah, hatutakuwa na wogatena kamwe madhali tumeuona ule muujiza katika jangwa la Dahna." Ala akapan-da (kipando) na pamoja na askari wake wakafika baharini. Waliingia bahariniwengine juu ya vipando na wengine kwa miguu. Walikuwa wakisoma, "Ewe Mwingiwa Rehma, Mwenye upendo, Mvumilivu, Wa-milele, Uliye Hai, Mhuishaji,Unayejitosheleza, hapana Mungu ila Wewe. Oh, Mola wetu." Maji yalionekanakwao kuwa machache, kwa kina tu cha kiwiko cha mguu wa ngamia, ingawaumbali wa kisiwa kile ulikuwa ni safari ya siku moja kwa mashua kutoka ufukweni.Walikifikia kisiwa na vita vilivyopangwa vikatokea hapo (kati ya askari wa Ala nawaasi) na maadui wakaangamizwa kabisa.

Hakuna kati ya waasi aliyebakia kurudisha taarifa kwao. Mali na familia zao vilitek-wa na kugawanywa. Askari wa kipando alipata elfu sita na wa miguu alipata elfumbili. Afif Ibn Mundhar alitunga ubeti ufuatao juu ya tukio hilo:

Mungu, Mwenye uwezo aliiweka bahari chini ya udhibiti wetu,Tukio la kushangaza mno kuliko jukumu lenyewe.Lililofanywa na Musa kwenye Bahari Nyekundu na Mto Nile.Ghadhabu ya Mungu ilimwangukia kila asiyeamini.Chemchem ilibubujika kutoka chini ya changarawe,Nasi tena, tukasikia mlio wa kengele za ngamia wetu.

Mtawa mmoja alikuwa akisafiri pamoja na jeshi la Ala ambaye aliingia Uislambaada ya vikosi hivyo viliporudi Bahrain na ushindi na nchi kufagiwa waasi. Watuwakamuuliza mtawa yule kwa nini alisilimu. Alisema ameona dalili tukufu tatu, naaliogopa kubadilishwa kuwa mnyama kama hakuingia Uislam. Aliulizwa kuhusudalili hizo tatu na alizitaja kama ifuatavyo:

1) Ile chemchem iliyotokea chini ya changarawe,2) Kugeuka kwa bahari iliyochafuka.3) Ile dua iliyosomwa na wale askari, kama ifuatavyo:

"Ewe Mola, wewe ndiye Mwingi wa Rehema. Hapana Mungu ila Wewe,Uliyejiumba, hakuna kilichokuwepo kabla Yako, Wa milele, Mtambuzi, Hai usiyek-ufa kamwe, Muumba wa Yasiyoonekana na yale Yanayoonekana. Mmiliki wakudumu. Unajua bila kujifunza."

Mtawa yule akasema wale askari walikuwa kwenye haki hivyo malaika walikuwaupande wao. Hii ngano ya mtawa imerudiwa mara kwa mara baadae. Ala aliandi-ka barua kwa Abubakr kumweleza kwamba baada ya kupata matatizo kiasi Mungu

101

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

aliwasaidia kwa kufanya chemchem kububujisha maji kutoka chini ya changarawe.Ala katika barua yake alimuomba Abubakr aviombee vikosi vya Waislam vinavy-opigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Abubakr akafanya hivyo, na kusemakwamba Mabedui wamezoea kusema, "Luqman, mwenye hekima, aliwazuia watukuchimba kisima cha maji katika jangwa la Dahna, kwa sababu hakukuwa nakamba iliyokuwa ndefu ya kutosha kuyafikia maji ambayo yangekuwa mbali sanachini ya ardhi." Abubakr ndipo akasema kwamba kule kutokea kwa maji kulikuwamoja ya ishara kubwa sana za Allah na alikuwa haijawahi kusikiwa kabla naummah mwingine, na akaongeza, "Oh Mola, usiiondoe neema ya Muhammadkutoka kwetu."Ibn Kathir katika kitabu chake (juz.6,uk.328-29), ameandika ngano hiyo hapo juukutoka kwa Seif. Abulfaraj katika kitabu chake al-Aghani amenakili kutoka kwaTabari ambaye naye ameandika kutoka kwa Seif. Wanazuoni wengine wameandi-ka ngano hiyo kutoka kwa Seif.

ASILI YA NGANO YA SEIF

Seif amesimulia ngano ya Ala kutoka kwa Sa'b mtoto wa Atyya mtoto wa Balal, hiini kwamba, ilipita kutoka kwa babu kwenda kwa baba na kwenda kwa mtoto.Tumeonyesha wakati tunajadili ngano ya Malik kwamba sanad-ya-kifamilia yawapokezi hiyo hapo juu imebuniwa na Seif.

NGANO YA ALA KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

Baladhuri katika Futuuhul Buldan (uk.92-93) anasema kwamba wakati wa utawalawa Umar Ala alipelekwa Zara na Darain. Alifanya mkataba na watu wa Zara wakuchukua theluthi moja ya dhahabu, fedha, na mali nyingine za mji huo kuongezeana nusu ya mali kutoka nje ya mji huo. Akhnas Ibn Amery, mwakilishi wa mji huoalimwambia Ala kwamba mkataba huo ulihusika tu na watu wa mji wa Zara nahaukuhusika kwa jamaa zao walioishi mji wa jirani wa Darain.

Ala alimchukua Karadhulnukri kama mwelekezaji wake, na wakavuka bahari juuya ukanda wa ardhi kwenda Darain. Huko aliwashambulia wakazi, akawaua wapi-ganaji wao na kuziteka familia zao.

VITA DHIDI YA WAASI {ULINGANISHAJI NA HITIMISHO}

Seif anaandika kwamba:

1) Chemchem ya ajabu ilitokea mahali ambapo hata Luqman, mwenyehekima, hakutegemea maji.

2) Wale ngamia walirudi kwa hiari zao wenyewe.

3) Wale askari walitembea juu ya bahari, kama juu ya ardhi, ni ajabu

102

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

zaidihata kuliko muujiza wa Musa. Kisha aliupa nguvu ukweli wa miu-

jiza hii, kwa kuelezea juu ya mtawa anayesilimu kwa kuiona miujiza

hiyo. Anatilia mkazo kwamba miujiza hii ilitokea kwa ajili ya barua ya

Ala kwa Abubakr kumwomba baraka zake.

Tabari, Hamawi, Ibn Athir, Ibn Kathir na baadhi ya waandishi wengine wanarudiangano ya Seif katika vitabu vyao, na Waislam wameikubali kama historia ya kiis-lam. Hata hivyo, hapakuwa na muujiza, mji huo ulikuwa na njia ya kufikia bara kwaukanda ambao kupitia humo askari hao ndimo walimotembea. Pia tukio hilo haliku-tokea wakati wa Abubakr, bali katika wakati wa utawala wa Umar.

Seif ndiye peke yake anayehusika na ubunifu wa ngano hizi kwani yuko peke yakekatika kuziwasilisha, kama vile tu alivyo peke yake anayesema kwamba hakunakatika maadui aliyebaki wa kupeleka habari nyumbani.

103

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

6. TUKIO LA MIBWEKO YA MBWA WA HAUW-ABKUTOKA KWA SEIF

NA KWA WENGINE

ULINGANISHO

104

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

HAUW-AB NCHI YA MIJIBWA

Tabari katika juz.3,uk.490-407, ameandika kutoka kwa Seif kwamba Umma ZemalSalma, mfungwa wa kivita wa kike, alitolewa kwa Ayisha (mke wa Mtume) kamafungu lake la ngawira ya vita. Ayisha akamwacha huru, lakini akakaa ndani yanyumba ya Ayisha.

Siku moja Mtume alirudi nyumbani na kuwakuta wanawake wamekusanyikapamoja. Mtume aliwanyooshea kidole na akasema, "Mmoja wenu anawafanyambwa wabweke katika nchi ya Hauwab." Baada ya Mtume kufariki, Umma ZemalSalma alilikusanya jeshi kulipiza kisasi juu ya Waislam waliowaua ndugu zake.Alipokuwa analikusanya jeshi lake kutoka Zafr na Hauwab, mbwa walimbwekeangamia wake hapo Hauw-ab (kutimiza utabiri wa Mtume). Khalid (aliyekuwaJenerali) alimtambua Umma Zemal Salma na akapigana dhidi yake. Askari waKhalid wakakata miguu ya ngamia wake na wakamuua (Umm Salma).

Hamawi ndani ya kitabu chake Mujamul Buldan, ameiandika ngano hiyo hapo juukutoka kwa Seif. Ibn Hajar katika Isaba, juz.2,uk.325, ameiandika kwa kifupi bilakutaja rejea yake.

CHANZO CHA NGANO YA SEIF

Seif amesimulia ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Sahl mtoto wa Yusuf na AbuYaqub, ambao utambulisho wao haukuandikwa. Ibn Hajar na Ibn Abdul-Birr wame-sema, "Siyo Sahl wala baba yake Yusuf wanaojulikana kwa mtu yoyote." AbuYaqub ndani ya ngano za Seif ni "Said Ibn Ubaid" ambaye Dhahabi anasema,"Hajulikani." Baadhi ya waandishi wengine wanasema, "Yupo Said Ibn Ubaidmmoja lakini hajulikani kama Abu Yaqub."

NI NANI ALIBWAKIWA NA MBWA HAPO HAUW-AB?

Seif katika ngano ya Hauw-ab amechanganya matukio mawili pamoja. La kwanza,tukio la Ummu Qirfa, la pili, mbwa wa Hauwab.

1) Ummu Qirfa: Kwa mujibu wa Ibn Sa'd na Ibn Hisham, msafara wa biasharawa Waislam ukiwa njiani kwenda Damascus uliporwa na kabila la FarazaWadilqura. Mwislamu aliyekuwa mkuu wa msafara, Zaid, alijeruhiwa vibaya.

Yaqubi anasema kwamba Mtume alikuwa atume jeshi ugenini chini ya uongozi waZaid kwenda kuliadhibu kabila la Fazara. UmmuQirfa, mke wa chifu wa kabila hilokatika kujua makusudio ya Mtume alituma jeshi chini ya uongozi wa arobaini katiya watoto wake mwenyewe kukutana na lile jeshi la Waislam karibu na Madina.Mapigano yaliyopangwa yakatokea hapo na wanaume wote wa kabila la Fazarawakauawa na wanawake wao wakachukuliwa mateka. Isipokuwa Ummu Qirfa na

105

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

binti mmoja aliyeitwa Jariah ukoo wote uliuawa. Hawa wawili walitekwa bilakuumizwa. Zaid aliamuru Ummu Qirfa auawe na akamchukua yule binti Jariah kwaMtume ambaye alimtoa kwa ami yake mwenyewe, na mtoto wa kiume baadaealizaliwa na akaitwa Abdur-Rahman.

Tukio hili lilitokea katika mwaka wa 6 wa Hijiria wakati wa uhai wa Mtume.

2) Mbwa wa Hauwab: Hauwab ni mahali karibu na Basra. Kwa mujibu wa IbnAbbas, Mtume aliwaambia wake zake: "Mmoja wenu atapanda ngamiamwenye manyoya mengi, mbwa watambwakia huko Hauwab, watu wengiwatauawa mkono wako wa kulia, na kushoto kwako,6 kifo kitakutisha wewe,lakini utabakia salama."7 Kwa mujibu wa Ummu Salama (mmoja wa wake zaMtume), Mtukufu Mtume alitaja uasi wa mmoja wa wake zake, wale mama wawaumini (kama wanavyoitwa), Ayisha (mmoja wa wake za Mtume) akacheka.Mtume alitoa kauli juu yake akisema, "Inanielekeza kwamba mbwa wanakub-wakia huko Hauwab ukiwa unafanya uasi kidhalimu dhidi ya Ali." KishaMtume akamwangalia Ali, akisema, "Kama jambo la Ayisha litakuja mikononimwako, kuwa mvumilivu juu yake."

Kwa mujibu wa Tabari, juz.3,uk.475, na baadhi ya wanahistoria, ngano ni kamaifuatavyo:

Urani, yule mtu aliyeuza ngamia wake kwa Ayisha alikuwa safarini akiwa amepan-da ngamia wake. Mtu alimfuata, na akataka kununua ngamia wake. "Dirham elfumoja ndiyo bei yake," Alisema Urani, "Una wazimu?" Yule mtu akasema, "Nanianayelipa Dirham elf moja kwa ajili ya ngamia?" Urani akasema, "Ngamia huyuana thamani ya Dirham elf moja kwa sababu ninaposhindana na mpandaji wanguninampita, na hakuna anayeweza kunikuta mimi ninapompanda ngamia huyu."Yule mtu akasema, "Utafanya biashara vizuri nami kama utajua ni kwa ajili ya nanininamtaka ngamia wako."

Urani: Ni kwa ajili ya nani unamtaka huyu ngamia?Mwarabu: Kwa ajili ya mama yako.Urani: Nimemwacha mama yangu taabani nyumbani.Mwarabu: Namtaka ngamia wako kwa ajili ya mama wa

waumini, Ayisha.Urani: Basi mchukue kama zawadi kutoka kwangu.Mwarabu: Hapana, fuatana nami, nitakupa ngamia na pesa vilevile.

Urani: Nilikwenda na yule mtu, alinipa ngamia jike aliyekuwa wa

6 Ibn Kathir (juz.6,uk.212).

7 Salati katika Kasais (juz.2,uk.137) na Ibn Abd Bir katika al-Istiab.

106

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Ayisha na Mtoto wake, na Dirham 400 au 600 vilevile. Kisha yule mtu aka-

niuliza kama nilizijua barabara pale, na nilimjibu kwa kumkubalia.

Aliniomba niwaongoze, na nikawaambia jina la kila jangwa na mto tulioupi-

ta. Tulikuwa tukipita maji ya Hauwab pale mbwa walipobweka. Waliniuliza,

"Jina la maji yale yanaitwaje?" Nikajibu, "Hauwab." Ndipo Ayeshah alipopi-

ga ukelele na kumfanya ngamia wake akae chini na akasema, "Wallah, ni

mimi ambaye mbwa wamenibwakia hapa Hauwab, nirudisheni." Watu

wengine waliwakalisha ngamia wao chini kumzunguka Ayishah. Ayeshah

kamwe hakusogea kutoka mahali pale mpaka siku iliyofuatia. Mpwa wake

Ibn Zubair alikuja na akamwambia, "Ondoka haraka," kwa sababu Ali

alikuwa anawafuata, na angewafikia mara tu. Urani ndipo akasema,

"Waliondoka mahali pale na wakanilaani."

Kwa mujibu wa Musnad Ibn Hanbal (juz.6,uk.97), Ibn Zubair alimwambia Ayishah,"Huu siyo wakati wa kutuangusha, pengine Mungu anakutaka wewe uingilie katibaina ya Waislam na kufanya amani miongoni mwao."

Ndani ya Ibn Kathir (juz.7,uk.230), imeandikwa kwamba Masheikh wawilihawakuiandika ngano hii kwenye vitabu vyao ingawa inazo shuruti zote zakuifanya ikubalike kama ni sahihi kwao.

Katika Tabari (juz.3,uk.485), imeandikwa kutoka kwa Zuhri kwamba wakatiAyishah alipowasikia mbwa wakibweka, aliuliza, "Mahali hapa panaitwaje?" Baadawalipomwambia kuwa ni 'Hauwab' alijuta na kusema, "Wote ni wa MwenyeziMungu na Kwake yeye tutarejea." Kisha akaendelea akisema, " Ni mimi kwa kweliambaye Mtume alinizungumzia kwa wake zake akisema angependa kujua ni naniatabwakiwa na mbwa hapo Hauwab." Ayisha alitaka kuondoka mahali pale, lakiniIbn Zubair alimshawishi kuendelea mbele.

Mahali pengine Ibn Kathir (juz.7,uk.230), na Abulfaraj (uk.173), imeandikwa kwam-ba Ayishah alijuta, akisema, "Mimi ndiye yule mwanamke," lakini Ibn Zubair akam-saliti akisema kwamba mahali pale hapakuwa Hauw-ab.

Katika Murujudh-Dhahab (juz.2,uk.248), imeandikwa kwamba Ibn Zubair na Talhawaliapa kwa Allah kwamba mahali pale hapakuwa Hauwab, na wakaleta Waarabuhamsini kuapa vivyo hivyo na huo ulikuwa uongo wa kwanza kuapiwa katikaUislam.

Katika Yaqoubi (juz.2,uk.157) na Kanzul-ummal (juz.6,uk.83-84), imeandikwakwamba Ayisha alisema, "Niacheni nirudi. Haya ni maji yaleyale Mtume aliy-ozungumzia, akinionya juu ya mbwa wanaobweka." Walileta Waarabu hamsini ili

107

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kuapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba mahali pale hapakuwa Hauw-ab. Ndani yaal-Imama wa-Siasa (juz.1,uk.59-60), imeandikwa kwamba Ayisha alipowasikiambwa wanabweka alimuuliza Muhammad Ibn Talha juu ya mahali pale na kadha-lika. Muhammad alimwambia, "Ubarikiwe moyo wako. Sahau juu ya ngano hizi."Abdullah Ibn Zubair akashuhudia kwa uwongo, na wakaleta mashahidi wanaoon-gopa. Ule ulikuwa ushahidi wa kwanza wa uwongo katika Uislam.

Wanahistoria wengine pia wameisimulia ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Mtumewa Mwenyezi Mungu, kama vile Ibn Athir ndani ya al-Nihaya; Hamawi ndani yaMujamul-Buldan, Zamakhshari katika al-Faiq; Ibn Taqtaqi katika al-Fakhri (uk.71)juzuu za Cairo; Zubaidi (juz.1,uk.195) chini ya neno Hauwab; Musnad Ahmad(juz.6,uk.52, 97); A'tham (uk.168-169); Sam'ani katika al-Ansab; Sira Halabiyyah(juz.3,uk.320-321); na Muntakhab Kanz (juz.5,uk.444-445).

HITIMISHO

Wanahistoria kwa makubaliano wameandika kwamba (mke wa Mtume) Ayishaalikuwa ndiye mtu pekee ambaye mbwa walimbwakia hapo Hauwab, kama ilivy-otabiriwa na Mtume na wamelichukulia tukio hilo kama moja ya dalili za unabii waMtume Muhammad.

Ni Seif pekee aliyelihusisha tukio la mbwa hao kwa Ummu Zemal Salma,mwanamke wa bandia kuwaridhisha wale ambao kwa sababu moja au nyingine,waliupenda uwongo wa Seif.

Tabari kwa upande wake bahati nzuri, ameiandika ngano hiyo kutoka kwawasimulizi wengine na Seif vilevile. Kwa hiyo, ile nia ya Seif ya kuzipindua nganoimefichuliwa. Kwa kuziandika ngano za Urani, yule mmiliki wa mwanzo wa ngamiaaliyepandwa na mama wa waumini, na ngano ya Zuhri juu ya mbwa wale, Tabariameudhihirisha uso halali wa Seif kwa wasomaji wake, mbali na nyakati zingineambapo Tabari ameandika kutoka kwa Seif tu na akauficha ukweli.

Mpaka hapa tumeandika baadhi ya ngano zilizosimuliwa na Seif katika wakati waAbubakr, sasa zinafuata baadhi ya ngano zake katika wakati wa Umar.

108

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

7. KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIA WA ZIAD:

KIINI CHA NGANO YA SEIF

ZIAD NA ABU SUFYANNGANO HIYO ILIVYOELEZWA NA WENGINE

MBALI NA SEIF

HITIMISHO

109

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

KUUSAHIHISHA MTI WA FAMILIAYA ZIAD

Abu Mughaira Ziad alikuwa mtoto wa mtumwa wa kike aliyekuwa akiitwaSumayya, wa mkulima wa Ki-Fursi, aliyemtoa kwa mganga mmoja aitwaye HarthThaghafi, kwa malipo ya huduma yake ya tiba. Sumayya alizaa watoto wawili wakiume Nafiia na Naafi, wakati bwana wake alipokuwa ni mganga Harth. BaadaeHarth alipanga ndoa kati ya Sumayya na mtumwa wake wa Kirumi, Ubaid. WaliishiTaif. Abu Sufyan alikwenda Taif na akamuomba muuza baa mmoja afanye ukuwa-di (ugawadi) kwa malaya kwa ajili yake. Yule muuza baa Abimaryam Selluli akam-tambulisha Sumayya kwa Abu Sufyan na akawa mjamzito usiku uleule, na baadaeakamzaa Ziad katika mwaka wa kwanza wa Hijiria, alipokuwa mke wa Ubaid.Wakati Mtume wa Allah alipoizingira Taif, mmoja wa watoto wa kiume wa Harth(yule mganga) ambae jina lake lilikuwa Nafiia alikimbilia kwa Mtume ambayealimwacha huru na akimwita Abubakra. Harth akamwambia Naafi kwamba yeyealikuwa ndiye baba yake na hivyo akamzuia asikimbilie kwa Mtume kama kakayake alivyofanya. Ndugu watatu hawa, Abubakra, Naafi na Ziad baadae waligeu-ka wakaitwa ' watumwa walioachwa huru na Mtume', Ibn Harth na Ibn Ubaid kamawalivyofuatana. Mu'awiyah alimpendelea na kumpokea Ziad kuwa ndugu yake, naakamwita Ziad Ibn Abu Sufyan. Lakini baada ya Mu'awiyah na kuanguka kwaUfalme wa Amawi, Ziad aliitwa, Ziad mtoto wa Baba Yake (ikimaanisha mwana-haramu) na wakati mwingine akiitwa Ziad mwana wa Sumayya kwa jina la mamayake.8 Wanahistoria wameandika ngano ya Mu'awiyah kutoa udugu wake kwaZiad na kumlaumu Mu'awiyah kwa kitendo chake hiki.

Seif, akidhamiria kumuondoa Mu'awiyah kwenye lawama na kuliondoa doa kuto-ka kwenye nguo ya Ziad, alibuni ngano ambayo Tabari ameiandika kwenye kitabuchake (juz.3.uk.259) miongoni mwa matukio ya mwaka wa 23 Hijiria, kama ifu-atavyo:Mwarabu anayeitwa Ganzi alimlalamikia Umar kwamba Gavana wake Abu Musaaliipeleka kesi yake kwa katibu wake Ziad Ibn Abu Sufyan, na ngano inaendelea.Umar alimuuliza Ziad alivyoitumia zawadi yake ya kwanza aliyopewa. Ziad akase-ma kwamba alinunua uungwana wa mama yake na akamwacha huru. Kuhusuzawadi yake ya pili alisema kwamba alinunua uungwana wa mlezi wake Ubaid.

Seif katika hiyo ngano ya kubuni hapo juu alinuia kuthibitisha kwamba Ziad aliit-wa 'Ziad, mwana wa Abu Sufyan', hata wakati wa Khalifa Umar, na Khalifahakukataa kumwita Ziad 'mwana wa Abu Sufyan', hivyo, alikuwa ni Mu'awiyah,

8 al-Kamil ya Ibn Athir - Matukio ya mwaka wa 44 Hijiria; al-Istiab juz.1,uk.548-555; al-Isabah ,juz.1,uk.563.

110

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

mtoto wa Abu Sufyan, aliyempa Ziad udugu wake (kama ilivyoelezwa hapo juu,Mu'awiyah alishutumiwa na wanahistoria kwa kitendo hiki.) Zaidi ya hayo, Seifanajaribu katika ngano yake kumlinda Ziad vilevile, pale Ziad anapomtaja Ubaidkama mlezi wake. Cha zaidi, Seif anaielezea ngano hiyo kutoka wakati wa KhalifaUmar, ili kuifanya izidi kukubalika kwa Waislam.

KIINI CHA NGANO YA SEIF

Seif ameiandika ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Muhammad, Talha na Muhallab.Seif ameandika ngano 216 ambazo zimeandikwa katika Tabari kutoka kwa Seif,ambaye naye ameiandika kutoka kwa Muhammad Ibn Abdullah Ibn Sawad IbnMalik Ibn Nuwaira, ambaye hajulikani katika vitabu vyote vya historia isipokuwandani ya Ikmal ambacho mwandishi wake pia ameandika kutoka kwa Seif. KunaTalha wawili. Mmoja ni Abu Sufyan, Talha Ibn Abdurahman ambaye hakuna dalilizake zinazoopatikana. Wa pili Talha Ibn A'lam aliyeishi Jian karibu na Ray (Tehran)na Seif hakumtaja bayana katika ngano yake. Seif ameandika ngano 67 kutokakwa Muhallab Ibn Uqba al-Asadi, ambazo pia zinazopatikana kwa Tabari, lakinihakuna dalili yake inayoweza kupatikana katika kitabu cha wasifa chochote.

ILIVYOELEZWA NA WENGINE MBALI NA SEIF

Al-Daynawari katika kitabu chake, The long stories, uk.14 anasema: "Abu Musaalimwona Ziad Ibn Ubaid, mtumwa wa kabila la Thaqif, ni mtu mwenye tamaa yamaendeleo ajabu na mwerevu sana, na akamwajiri kama katibu wake. Ziadalikuwa na Mughaira kabla ya hapo." Ibn Abdulbarr katika kitabu chake, al- Istiab(juz.1,uk.548), anasema, "Kabla Mu'awiyah hajampa Ziad udugu wake alikuwaakiitwa Ziad Ibn Ubaid Thaqafi." Imeandikwa pia hapo, kwamba Ziad alinunuauungwana wa baba yake Ubaid na akamwacha huru ambalo lilikuwa tendo zurisana.

Katika al-Istiab, uk. 549 kutoka kwa Ibn Abdulbarr imeandikwa hivi: "Ziad alikuwaakijulikana kama Ziad Ibn Ubaid kabla ya kuungana na Mu'awiyah," kisha inaen-delea, "Ziad alitoa hotuba mbele ya Khalifa Umar katika sherehe na hotuba yakeilimshangaza kila mtu." Mmoja wa wageni, Amr bin Al-Aas akasema, "Wallah,kama kijana huyu (mzungumzaji) angetoka kwenye kabila la Quraish, angewezakuwa ndiye mtawala.” Abu Sufyan ndipo akasema, "Ninaijua asili yake." Ali akase-ma, "Ni nani baba yake?" Abu Sufyan akasema, "Ni mimi." Ali kisha akasema,"Acha Abu Sufyan (kuelezea uhusiano wako na mama yake Ziad)." Kisha AbuSufyan akatunga ubeti ufuatao:

Kama ningekuwa simuogopi mtu(Umar) ningesema,Wallah, Sakhr Ibn Harb angesaliti,Na wewe Ali, kwa hakika ungeamua,Wewe mwenyewe, ujuzi wa hotuba wa Ziad ni wa kutoka upandewa nani.Wanahistoria wafuatao wameandika hii ngano ya udugu wa Ziad na

111

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Mu'awiya.Ibn Athir katika matukio ya mwaka wa 44 Hijiria.Ibn Abdulbarr ndani ya al-Istiab katika wasifu wa Ziad.Yaqoubi, juz.2, uk. 195.Masoud katika Muruuj al-Dhahabi, juz.2,uk.54.Suyuti katika matukio ya mwaka wa 41 Hijiria.Ibn Kathir, juz.8, uk.28.Abul Fada, uk.194.Tabari katika juz.4,uk.259, na katika matukio ya mwaka wa 44 Hijiria, piakatika matukio ya mwaka wa 160, uk.334-335.Sahih Muslim, juz.1,uk.57.Usudul Ghaba wal Isaba, kwenye wasifa wa Ziad.Ibn Asakir, juz.5,uk.409-421.Yaqubi, juz.4,uk. 160.

Wanahistoria wengine wameirejea, lakini tumeamua hapa kuifanya fupi ngano hii.

HITIMISHO

Wanahistoria wote wameandika kwamba:

a) Zaid alizaliwa kwenye kaya ya Ubaid na mke wake muasherati Sumayyaaliyepewa mimba na Abu Sufyan usiku ule alipotambulishwa kwake na mtuanayeitwa Abimaryam Selluli.

b) Abu Sufyan alimsaliti Ziad mbele ya Umar.c) Mu'awiyah alimpokea Ziad kama ndugu yake.d) Waislam walimshutumu Mu'awiyah ambaye alipuuza amri ya Mtume isemayo,

''mtoto ni wa kaya ambayo mke na mume wanaishi pamoja, hata kama mkehuyo alipewa mimba hiyo na mgeni.'

d) Baada ya kuanguka kwa utawala wa Amawi, Ziad wakati mwingine aliitwa'Mtoto wa Baba Yake', na nyakati zingine 'Mwana wa Sumayya (mama yake)'.

Seif alitaka kuondoa mzigo huo kutoka kwa Mu'awiyah, ambaye alimtunukiaudugu wake Ziad, na akabuni ngano ambamo Ziad aliitwa, 'Mwana wa Abu Sufyan'katika wakati wa Umar, nyuma kabisa kabla ya Mu'awiyah, na kwa wakati huoUbaid aliitwa mlezi wa Ziad, na bado tunajua kwamba Ziad katika moja ya hotubazake alikiri kuwa mwana wa Ubaid kama ilivyoandikwa katika Yaqubi, juz.2,uk.195.

112

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

8. NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA:KUTOKA KWA SEIF

NA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

113

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

NGANO YA MUGHAIRA IBN SHU'BA.

Mughaira alikuwa wa Kundi la Muhajirina. Umar alimfanya Gavana wa Basra naakamfukuza baada ya kushutumiwa kwa zinaa. Alikuwa Gavana wa Kufa wakatialipofariki. Seif katika ngano inayofuata alijaribu kuonyesha kwamba lile dai lazinaa halikuwa na msingi.

Tabari katika juz.3,uk.170-171, ameandika kutoka kwa Seif kwamba sababu yaMughaira kushutumiwa kwa zinaa ilikuwa ni baadhi ya tofauti kati yake naAbubakra,9 mmoja wa mashahidi dhidi yake. Abubakra na Mughaira waliishi kati-ka vyumba viwili vinavyotazamana. Siku moja upepo ulifungua dirisha la chumbacha Abubakra, alikuwa analifunga wakati alipomuona, kupitia dirisha la upande wapili, Mughaira na mwanamke mgeni. Abubakra alikuwa na wageni na aliwaita wajekuona kinachofanyika kati ya Mughaira na mwanamke yule. Abubakra aliwaambiawageni wake kwamba alikuwa ni Ummu Jamil, mhudumu wa viongozi na watu-mishi wa serikali. Wageni wa Abubakra waliona kitu, lakini walingoja mpaka waka-muona yule mwanamke sawasawa kabla ya kukata shauri kuhusu hali hiyo.

Seif sasa akizungumzia uendeshwaji wa kesi hiyo mahakamani, anasema kwam-ba Mughaira alimwomba Umar awadodose hawa mashahidi wanne ambaowalikuwa watumwa, na akawaambia, "Mmeona nini kwangu, ama nilikuwa sina siriau mlichungulia kwenye nyumba yangu bila ruksa. Hata hivyo nilikuwa pamoja namke wangu ambaye anafanana na Ummu-Jamil." Mashahidi wawili walielezangano hiyohiyo, wa tatu tofauti na wale wawili, na wa nne, Ziad akasema alionamambo tofauti kabisa. Wale mashahidi watatu walichapwa kwa kutoa ushahidi wauongo.

Umar (Khalifa) akamwambia Mughaira, "Wallah, kama ungekuwa na hatia,ningekupiga mawe mpaka ufe."

WANAHISTORIA WENGINE

Ngano iliyoelezwa na wengine mbali na Seif kama ilivyoandikwa katika Futuuhul-Buldan cha Baladhuri uk.423; Kitabul Ahkam cha Mawardi uk.280; Yaqubijuz.2,uk.124. Tabari na Ibn Athir miongoni mwa matukio ya mwaka wa 17 Hijiriailikuwa kwamba Mughaira alikuwa na uhusiano na mwanamke aliyeitwa Ummu-Jamil, binti ya Afqam Ibn Mihjan Ibn Abi Amr Ibn Shu'ba. Alikuwa mke wa Hajaji IbnAtik wa kabila la Thaqif. Sasa kisa chote kilichobakia kwa mujibu wa al-Aghani chaAbulfaraj, juz.14,uk.139-142:

9 Abubakra: jina lake ni Nafi mwana wa Masruh Habashi na inasemekana kwamba baba yake alikuwaakiitwa Harith Ibn Kelda Ibn Amr Ibn Alaj Ibn Abi Salma Ibn Abd al-Uzza Ibn Qais.

114

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Mughaira Gavana wa Basra wa wakati wa Umar alizoea kumtembelea Raqta,mwanamke wa kabila la Thaqif, kwa siri katika nyumba yake. Mume wake alikuwani Hajaji Ibn Atik kutoka kabila la Thaqif. Siku moja Abubakra alikutana naMughaira katika mtaa na akamuuliza anakokwenda. Mughaira akasema anakwen-da kumuona mtu fulani. Abubakra akasema, "Gavana anakaa nyumbani na watuwanamtembelea yeye." Abubakra mara kwa mara alikuwa akimwambia Mughairaalipokuwa akimuona nje wakati wa mchana. Wanahistoria wamesema kwambahuyo mwanamke Mughaira aliyekuwa akimtembelea alikuwa jirani yake Abubakra.

Siku moja, Abu bakra, ndugu zake wawili Naafi na Ziad na mtu mwingine anayeit-wa Shibl Ibn Ma'bad, walikutana pamoja kuongea, mara upepo ukavuma na kufun-gua dirisha na wanaume hao wakamuona Mughaira katika chumba upande wa pilina mwanamke. Abubakra akawaomba wageni wake walithibitishe hili. Abubakraakangojea mpaka Mughaira alipotoka nyumbani kwa yule mwanamke naakamwambia, "Huwezi kuwa Gavana wetu tena, tumekuona na mwanamke."10

Mchana Abubakra alitaka kumzuia Mughaira kuongoza sala lakini watu waliingiliakati na kumwambia Abubakra amuandikie Umar (Khalifa) kuhusu Mughaira.Walimuandikia Umar ambaye aliamuru Mughaira na mashahidi waende Madina.Mughaira akajiandaa kwa kuondoka, na akampeleka mtumwa wa kike wa Kiarabuna mjakazi wake kama zawadi kwa Abu Musa (mwakilishi wa Umar).

Hapo mahakamani Umar alimuuliza Abubakra kama alimuona Mughaira akifanyamapenzi na huyo mwanamke na Abubakra akatoa maelezo. Mughaira akasema,"Ulikuwa ukinipeleleza." Abubakra akasema, "Sikukikosa kile ambacho MwenyeziMungu atakuaibisha wewe." Umar alitaka maelezo zaidi, hivyo Abubakraakaelezea kile alichokiona. Pale shahidi wa pili alipoeleza kama yule wa kwanza,Umar akasema, "Mughaira nusu yako imekwenda." Shahidi wa tatu alifanya sawa-sawa na wale wengine wawili, kisha, Umar akasema, "Mughaira, robo tatu yakoimekwenda." (Mughaira alivunjika moyo na akaomba msaada kwa kila mtu.)

Mughaira alikutana na Muhajiriina na mama wa waumini (wake za Mtume) naakawaomba msaada, walimhurumia. Umar aliamuru wale mashahidi watatuwatengwe, mpaka yule shahidi wa nne Ziad afike kutoka Basra.

Viongozi wa Muhajirina na Masahaba wa Mtume walikusanyika Msikitini pale Ziadalipowasili. Mughira tayari alikuwa amekwisha andaa utetezi. Umar alipomuonaZiad anakuja, akasema, "Namuona mtu ambaye hatamuangusha jamaa wa kundila Muhajirina, kama Mungu alivyoagiza." Alisema pia, "Namuona kijana ambayehatoshuhudia chochote bali ukweli," kwa mujibu wa Muntakhab, juz.2,uk.413. Kwamujibu wa Abulfida, juz.1,uk.171, Umar alimwambia Ziad, "Namuona mtu ambaye,nategemea, hatamfedhehesha sahaba yoyote wa Mtume wa Allah."

10 Kisa cha uzinifu wa Mughaira inasimuliwa na Ibn Jarir, Ibn Athir na Abul Fida katika Matukio yamwaka wa 17 Hijiria.

115

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Katika al-Aghani imeandikwa kwamba Uthman an-Nahdi alisema kwamba uso waUmar ulibadilika rangi baada ya shahidi wa kwanza na uso wake ulionyeshamajonzi baada ya shahidi wa pili, na uso wake ulikuwa jivu baada ya shahidi watatu, na Umar alipomuona Ziad anakuja akiwa amevaa nguo nyeupe alimpigiakelele, "Unajua nini, Ewe chozi la tai." Abu Uthman alipiga kelele kwa sauti kubwasana akimuiga Umar kiasi kwamba msimuliaji alishituka sana.

Mughaira akasema, "Ewe Ziad, mkumbuke Mungu na Siku ya Qiyamah. Mungu,Mtume Wake, Kitabu Chake na Mbora wa Waumini (Umar, Khalifa), wameiokoanafsi yangu. Usiipoteze kwa kuelezea kile ambacho hukukiona." Ziad akasema,"Sikukiona walichokielezea, Ewe Mbora wa Waumini, lakini nimeona kituko chakufedhehesha, na niliona kwamba Mughaira alikuwa hana pumzi baada ya kuhu-siana na yule mwanamke." Ziad aliyakataa waliyoyaeleza wale mashahidi wenginewatatu. Umar kisha akasema, "Allah Akbar. Simama Mughaira na uwachapeviboko." Mughaira aliwachapa Abubakra na wale wengine wawili, viboko themani-ni kila mmoja.

Hakim katika Mustadrak na Dhahabi, juz.3,uk.448, wanasema, "Umar akasemaAllah Akbar, na akafurahia sana na akawachapa wale mashahidi watatu, lakini siyoZiad."

Imeandikwa katika Futuuhul-Buldan kwamba Shibl yule wa tatu alisema, "Shahidimwaminifu anapata viboko licha ya hukumu ya Mwenyezi Mungu." Abubakrabaada ya kuchapwa, alisema tena, "Nashuhudia kwamba Mughaira amefanyazinaa." Umar akaamuru aadhibiwe tena kwa kutoa ushahidi wa uongo. Ali akapin-ga akimwambia Umar, "Kama utamchapa huyo, nitampiga mawe rafiki yako(Mughaira) mpaka afe." Ali alikuwa na maana kwamba kama kauli ya pili ya Abubakra itaruhusiwa, basi kauli hizo nne zitathibitisha kosa la Mughaira. Hivyo lazi-ma apigwe mawe afe. Umar alimtaka Abubakra atubie. Abu bakr alimuuliza kamaalitaka kumuondolea mzigo wa ushahidi wa uongo ili kumtakasa, kwa kauli yakeinayofuatia, Umar alimjibu kwa kukubali. Abu bakra alisema kwamba hakutakakutoa ushahidi mwingine zaidi. Wakati adhabu zilipokwisha, Mughaira aliwaambiawale mashahidi, "Ninamshukuru Mungu aliyewaaibisheni nyie." Umarakamwambia Mughaira, "Kimya!!, Mwenyezi Mungu apafanye pachafu hapomahali walipokuona.

Abubakra aliondoka mahali hapo huku akisema, "Wallah, sitaweza kusahau kitukohicho." Wale mashahidi wengine wawili walitubia hivyo ushahidi wao ulikubalikabaadae. Abubakra alitakiwa kutoa ushahidi wake kwa ajili baadhi ya matukiomengine naye alisema, "Muombeni mtu mwingine. Abu Mughaira amevunja sifayangu."

Imeandikwa katika Al-Aghani na sherehe ya Nahj kwamba Ratqa, yule mwanamkekatika suala la Mughaira kule Basra alikuwa akimtembelea Mughaira huko Kufa

116

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

pia. Umar safari moja alimuona Ratqa wakati wa hijja huko Makkah. Mughairaalikuwepo pia. Umar alimuuliza Mughaira kama alikuwa anamfahamu yulemwanamke. Mughaira akasema kwamba alikuwa ni Ummu Kulthum (mke waUmar). Umar akamwambia Mughaira, "Ole wako, unanifanya mimi mjinga. Wallah,nina hakika Abubakra alikuwa na haki. Nina wasiwasi ninapokuona wewe, jiwehuniangukia kutoka mbinguni." Hassan Ibn Thabit alitunga beti zifuatazo:

Kuzungumzia ukatili, ninayo imani thabiti,Kwamba ukatili halisi unatokana na kabila la Thaqif.Yule mtu mwenye jicho-moja aliyeuacha Uislam na akaanguka,Asubuhi moja ndani juu ya mwanamwali aliyefunikwa shali.Alidhani kwamba yuko kwenye upeo wa urijali,Akicheza na wasichana watumwa katika hali ya uchumba.

Baladhuri katika Futuuhul-Buldan, uk.343 ameandika kwamba wakati Umaralipotaka kumfanya Mughaira kuwa Gavana wa Kufa, alimuuliza kama atarudiayale yaliyosemwa juu yake. Mughaira akasema, "Hapana." Hamawi katikajuz.1,uk.642; Mustadrak, juz.3,uk.449; Wafaiat, juz.2,uk.455 na juz.5,uk.406; naIbn Kathir, juz.7,uk.281, wameutaja ufuska wa Mughaira.

ASILI YA NGANO YA SEIF

Seif ameandika kutoka kwa Muhammad, Talha, Muhallah na Amr. Tumeelezeauongo wa hawa watatu wa kwanza katika ngano iliyopita. Seif amesimulia nganosita kutoka kwa Amr Ibn Zian au Amr Ibn Rayyan mtu bandia wa kubuniwa na Seifkwa mujibu wa Mizanul-Itidal.

HITIMISHO

Seif alitaka kumuweka huru Mughaira kutokana na ile lawama ya ufuska kwasababu aliteuliwa kuwa Gavana wa Khalifa. Ndipo akaigeuza kwa hila ile kadhiaya kweli ya ufuska iliyoandikwa na wanahistoria wengine wengi. AnasemaAbubakra aliishi kwenye chumba mkabala na kile cha Mughaira na alimuona kupi-tia dirishani Ummu-Jamil chini ya Mughaira kisha akawataka wageni wake kul-ishuhudia hilo. Waliamua kumshutumu Mughaira lakini Mughaira na Umarwakawahoji mashahidi wale na kuthibitisha kwamba ushahidi wao ulihitilafiana.Seif pia anasema kwamba Umar alimwambia Mughaira, "Kama hatia yako ingeth-ibitishwa, ningekupiga mawe mpaka ukafa." Wanahistoria mbali na Seifwameiandika ngano hii kinyume kama tulivyoandika. Kuigeuza ngano kumpende-lea Mughaira aliye Gavana, Seif aliunda wapokezi na Tabari ameandika kutokakwa Seif.

117

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

9. KIFUNGO CHA ABU MAHJANKILIVYOSIMULIWA NA SEIF

KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

118

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

KIFUNGO CHA ABU MAHJANAbu Mahjan mtoto wa Habib Ibn Amr Ibn Umar, alikuwa katoka kabila la Thaqif.Alikuwa ni mshairi na mtu mwerevu sana. Aliingia Uislam wakati kabila lakelilipoukubali Uislam. Alikuwa mlevi na Umar alimpiga viboko mara saba au tisa kwaajili ya ulevi. Kwa mujibu wa al-Aghani, juz.21,uk.142 watu wachache walipatikanawalevi na walikamatwa. Umar aliwaambia, "Mmekunywa mvinyo na mnajua kwam-ba Allah na Mtume Wake wameukataza." Wakasema kwamba Munguhajaukataza, na imeandikwa ndani ya Qur'ani kwamba waumini ambao niwachamungu na wanaofanya amali njema hawawezi kuwa na hatia ya kula amakunywa chochote. Umar aliwauliza wafuasi wake kuhusu maoni yao. Hawakuwezakufikia uamuzi wowote ule. Alimtuma mtu kwa Ali Ibn Abi Talib kutaka maoni yake.Ali alisema kwamba kulingana na watuhumiwa, tafsiri ya Qur'ani, basi si damu,mnyama mfu wala nguruwe imekatazwa. Umar alimuuliza Ali nini angewafanyahao? Ali akasema kwamba kama wanasema pombe haijakatazwa, ni lazimawauawe. Lakini kama watasema pombe imekatazwa na wameinywa, wapigweviboko. Wale watuhumiwa walikubali kwamba pombe imekatazwa, hivyo walipig-wa viboko.

Pale Abu Mahjan alipopigwa alitunga beti zifuatazo:

Katika dunia hii isiyo na uhakika mtu hawezi kupigana,Kulilia maziwa yaliyomwagika hakuwezi kuweka mambo sawa.Nimestahimili kwa uvumilivu kule kupotelewa na ndugu zangu,Lakini hata kwa siku moja sintastahimili kuipoteza pombe.Kwa kuipiga marufuku pombe, huyu bwana wa waumini ametufanyawanyonge.Tunakusanyika na kulia katika chumba ambamo zabibu inakamuliwa.

Pale Abu Mahjan aliposema kwamba hata kwa siku moja hawezi kustahimilikuacha pombe, Umar akasema, "Umeifichua siri yako. Nitakuadhibu zaidi kwasababu una shauku sana ya kunywa pombe." Ali akasema kwamba mtu asiad-hibiwe kwa kitu ambacho hajakitenda, na akasoma kifungu kifuatacho cha Qur'ani:"Wanakiri (washairi) kwa kitu ambacho hawajakifanya." Umar akasoma sehemu yaAya iliyobakia, "Ila wale walioamini na kufanya amali njema." Ali akamwambiaUmar, "Unadhani ni waumini, ambapo Mtume wa Allah amesema kwamba palemtu anapokunywa hawi muumini."

Kulingana na al-Isaba, wakati mmoja Umar alifikiri Abu Mahjan alikuwa amelewana akadai aruhusiwe kunusa pumzi zake. Abu Mahjan akasema, "Kufanyauchukunguzi kumekatazwa" na Umar akamuacha. Tabari katika juz.4,uk.152 mion-goni mwa kadhia za mwaka wa 14 Hijiria anasema kwamba Umar aliwaadhibubaadhi ya wafuasi wake, mwanae na Abu Mahjan kwa sababu walikunywa pombe.Ibn Kathir katika juz.7,uk.48 anasema, "Abu Mahjan Thaqafi alipigwa viboko mara

119

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

saba kwa kulewa." Imeandikwa ndani ya Aqdulfarid kwamba miongoni mwa watuwa daraja la juu ambao wameadhibiwa kwa kulewa alikuwa ni Abu Mahjan, mleviwa uhakika. Kwa mujibu wa al-Isaba na al-Aghani, Abu Mahjan alimpenda bibimmoja aliyeitwa Shamus. Alijaribu bila mafanikio kuonana naye. Jirani wa bibihuyo alikuwa na mkandarasi ndani ya nyumba yake, Abu Mahjan alipata kazi kwamkandarasi huyo ndipo akamuona bibi huyo kutoka juu ya ukuta. Kisha akatungabeti zifuatazo:

Nilimuangalia Shamus ingawa Mungu amekataza,Kumuangalia mwanamke ambaye alipasa awe amefichwa.Kama mkulima anayekuja mjini kwa ajili ya likizo,Baada ya kuuza mazao yake, alikuwa mwenye furaha na bashasha.

Mume wa Shamous alilalamika kwa Umar. Umar akampeleka Abu Mahjan uhamis-honi huko Hazouzi,11 chini ya uangalizi wa Jahra al-Nasri na mtu mwingine. Umaraliwaambia walinzi hao wasimruhusu Abu Mahjan kubeba upanga wake. AbuMahjan akauficha upanga wake katika mfuko wa unga, na hapo ufukweni kablahajapanda chomboni alinunua kondoo na akafanya karamu kwa ajili ya walinziwake. Kabla ya mlo, Abu Mahjan akajifanya kama anachukua unga atengenezemkate. Aliutoa upanga wake kutoka kwenye mfuko ule, Jahra akauona na akakim-bilia kwenye ngamia wake, akampanda na kwenda kwa Khalifa Umar kumuelezeakisa chake.

Kulingana na al-Isaba na Istiab baada ya kuhamishwa Abu Mahjan alikwendampakani na Uajemi chini ya uangalizi wa Sa'd Ibn Waqqas. Ilikuwa ni Vita vyaQadisyya, Muhammad mtoto wa Sa'd alisema kwamba baba yake alimuweka AbuMahjan minyororo kwa sababu alikuwa amelewa. Sa'd hakuwa mzima siku hiyo naKhalid Ibn Orfota aliliongoza jeshi, na Sa'd alikuwa amesimama juu ya kilimakuuangalia uwanja wa mapambano. Abu Mahjan ambaye alikuwa amefungwapingu alitunga ubeti ufuatao:

Ni huzuni iliyoje kufungwa katika minyororo.Na kuangalia watu wakitumia mikuki yao tena na tena.

Kisha akamuomba Salmi, mke wa kamanda Sa'd, kumfungulia na kuahidi kamaatapona, kurudi na kufungwa minyororo tena, na kama atakuwa ameuawawatakuwa wameondokana naye. Salmi akaiondoa minyororo mikononi na miguu-ni mwa Abu Mahjan. Kisha akarukia juu ya mgongo wa Balqa, farasi wa Sa'd akiwana mkuki mkononi mwake. Aliwashambulia maadui. Askari walifikiria alikuwa nimalaika. Sa'd aliyaona mashambulizi ya mpanda farasi na akasema, "Ile miruko nisawa na miruko ya farasi wangu (Balqa) na lile shambulizi la mkuki ni sawa nashambulizi la Abu Mahjan, ila kwamba Abu Mahjan amefungiwa.”

11 Hazouzi: Jina la mlima katika kisiwa ambamo watu walikuwa wakipelekwa uhamishoni wakati huo.

120

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Adui aliposhindwa, Abu Mahjan alirudi. Wakaweka tena zile nyororo mikononi namiguuni mwake. Mkewe Sa'd akamuelezea Sa'd kile kisa cha Abu Mahjan. KishaSa'd akasema, "Wallah sitamuadhibu mtu yule kwa ulevi ambapo alileta ushindikwa Waislam." Ndipo tena akaamuru Abu Mahjan aachiliwe huru. Abu Mahjanakasema, "Nilikuwa nikiipokea ile adhabu kama toba, sasa kwa sababu huniad-hibu, sitakunywa tena."

SIMULIZI YA SEIF

Tabari katika juz.3,uk.43, anasema kwamba Sa'd aliwafunga wale watu waliokun-ywa mvinyo na kufanya matata. Sa'd aliwafedhehesha kwa kusema, "Kamatusingekuwa kwenye uwanja wa vita, ningewafundisheni somo ambalo wenginewangelijifunza kutokana nalo." Abu Mahjan alikuwa mmoja wao ambaye mikonona miguu yake ilikuwa imefungwa minyororo. Tabari katika juz.3,uk.55-57, anase-ma kwamba baada ya mke wa Sa'd kumfungulia Abu Mahjan na akapigana namaadui alirudi tena kule jela, na wakamfunga minyororo. Mkewe Sa'd alimuulizaAbu Mahjan ni kwa nini alikuwa kifungoni? Alisema, "Nilikuwa nikinywa mvinyokabla ya kuingia Uislam. Sasa ninatunga beti za kuusifu mvinyo. Sa'd hapendi kwahiyo ananifunga." Salmi alimwambia mumewe Sa'd kile Abu Mahjan alichokisema,hivyo Sa'd alimtoa jela, na akamwambia, " Sitakuadhibu kwa ajili tu yakuzungumza kuhusu dhambi." Abu Mahjan akaapia kwamba hataongea mamboambayo siyo mazuri.

Abulfaraj katika al-Aghani, juz.2 ameiandika ngano hii iliyosimuliwa na Seif kutokakwa Tabari.

Ibn Hajar katika al-Isaba, juz.4,uk.175 anasema kwamba Fat'houn alimshutumuAbu Amr aliyeandika kwenye Istiab (kama ilivyotajwa kabla) kwamba Abu Mahjanmara nyingi alikuwa amelewa. Ilitosha kusema tu kwamba aliadhibiwa kwa ulevi.

Ingekuwa vizuri kusema kile ambacho Seif amekiandika. Ibn Hajar kisha anaen-delea kusema, "Seif ni dhaifu (asiyetegemewa) lakini tulichokiandika kina nguvuna kinajulikana sana." Ibn Fat'houn anakataa kwamba Sa'd alizembea kumuad-hibu mlevi yoyote, na alibadili kile alichosema Sa'd, "Sitamuadhibu Abu Mahjankwa ulevi," kuwa "Abu Mahjan hatakunywa tena kuweza kuadhibiwa." Masudi kati-ka juz.2,uk.422-424 Muruuj al-Dhahabi, amenakili alichosimulia Seif bila ya kutajajina la Seif. Lakini tunajua Masoudi ameandika kutoka kwa Tabari kwani alim-tukuza sana Tabari mwanzoni mwa kitabu chake.

ASILI YA NGANO YA SEIF

Seif ameandika ngano hii kutoka kwa Muhammad, Talha, Ziad na Ibn Mihraq.Hawa wawili wa kwanza ni wale wale watu wa uongo tuliowataja katika ngano zili-zopita. Seif amesimulia mara 53 ndani ya Tabari kutoka kwa Ziad ambaye haju-likani kwa waandishi wa wasifu kama alivyo Ibn Mihraq.

121

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

HITIMISHO

Seif alitaka kumkosha Sa'd rafiki na Gavana wa Khalifa kutokana na kutotekelezaadhabu ya kidini juu ya mlevi. Kisha alibuni yale maongezi kati ya Abu Mahjanhuyu mlevi na mke wa Sa'd aliyemfungulia kutoka kifungoni. Seif anasema kwam-ba mke wa Sa'd alimuuliza Abu Mahjan ni kwa nini Sa'd alimuweka kifungoni. AbuMahjan alijibu kwamba ni kwa sababu aliongea upuuzi, na siyo kwa sababu alikun-ywa pombe. Lakini Muhammad, mtoto wa Sa'd, ameandika kwamba Abu Mahjanalimwambia mama yake, wakati alipomfungulia kwamba kama angeuawa katikaile vita wangekuwa wameondokana naye. Inavyoonekana, huyu mke wa kamandaSa'd, aliijua rekodi ya nyuma ya Abu Mahjan, na bila shaka, na zile adhabu zamumewe zilizotolewa kwa Abu Mahjan kwa ulevi wake.

Lakini Seif amesema kwamba Sa'd alimwachia Abu Mahjan akisema hatamuad-hibu kwa kitu ambacho hakukifanya bali alikiongelea tu. Kisha Abu Mahjan anase-ma, "Sitaongea upuuzi tena." Ibn Fat'houn pia kwa kumpendelea Khalifa aliich-agua ile ngano ya Abu Mahjan iliyosimuliwa na Seif.

Masoudi yule mwanahistoria msomi anayeaminika akimfuata Tabari ameandikakile Seif alichosimulia. "Mwanadamu anaweza kufanya makosa." Hata hivyo, Seifna wale walioandika kutoka kwake hawawezi kuuficha ukweli.

122

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

10. SIKU ZA SEIFSIKU YA NG'OMBE

ARMATHAQWAS

IMASJARATHIM:

KUTOKA KWA SEIFKWA WENGINE MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

123

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

SIKU ZA SEIF

Waarabu wanaiita siku ya tukio kama vile: Siku ya Jamal, Siku ya Siffin, Siku yaHudaybia, kwa siku moja au zaidi ya moja kulingana na idadi ya siku ambazo tukiolimechukua. Kwa hiyo, Siku ya Jamal, ina maana ile kadhia ya Vita vya Jamal. Seifamebuni baadhi ya matukio ambayo ameyaandika kama "Siku ya Kadha naKadha", kama ile "Siku ya wale Ng'ombe", Siku ya Armath, Siku ya Jarathim.

A - SIKU YA NG'OMBE

Tabari katika juz.3,uk.12-14, ameandika kutoka kwa Seif kwamba Sa'd, alipokuwaakipigana na Waajemi, alifika sehemu inayoitwa Uzaibul Hijanat, karibu na MtoFurati (Euphrates). Alimtuma Asim Ibn Amr kwenda kununua kondoo au ng'ombehuko Maysan mji ulioko karibu na mto huo. Asim hakuona chochote kwa sababuwatu hao waliwaficha ng'ombe wao. Lakini alikutana na mtu karibu na msitu naakamuuliza kuhusu kondoo au ng'ombe. Yule mtu aliapa kwamba hakujua pakuwapata, ingawa alikuwa mchungaji wa kondoo. Mara ng'ombe mmoja akalia,"Wallah, anadanganya, tupo hapa." Hapo Asim akaingia kule msituni, akawaonang'ombe na akawaleta kambini. Sa'd akaiandaa karamu na akaigawa miongonimwa vikosi. Hajjaj baadae alizijua habari za kadhia hiyo na akaagizia apate mtualiyekuwepo wakati ule na mahali pale.

Nazir Ibn Abdshams na Zahir walimwambia Hajjaj kwamba walikuwepo wakatikadhia hiyo ilipotokea. Hajjaj mwanzoni hakuwaamini. Wakasema kwamba waowasingeamini pia kama wasingeiona. Ndipo Hajjaj akashawishika kwambawalikuwa wanasema kweli na akawauliza watu walisema nini wakati huo?Wakasema kwamba watu waliichukulia kama ishara kutoka kwa Mungu, waki-maanisha radhi ya Mwenyezi Mungu na ushindi dhidi ya adui. Hajjaj basi akase-ma, "Namna hii ya tukio hutokea tu kwa watu waadilifu." Seif kwa hiyo anasema,"Hii ilikuwa ni Siku ya Ng'ombe".

Mwana historia mwingine pekee mbali na Seif anayerejea kwenye tukio hili niBaladhuri ambaye katika Futuuhul-Buldan, uk.314 anaeleza kwamba, lile jeshi laSa'd lilipotaka mahitaji alituma kikosi kando ya mto kwenda kupora, mahitajimengine yalikuja kutoka kwa Khalifa Umar aliyewatumia kondoo na ng'ombe kuto-ka Madina.

VYANZO VYA NGANO YA SEIF

Seif ameiandika ngano hii kutoka kwa Abdullah Ibn Muslim al-Okli na Karb Ibn AbiKarb al-Okli ambao majina yao hayamo kwenye vitabu vyovyote vya wasifu.

124

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

HITIMISHO

Seif amebuni hii ngano ya ng'ombe na kuithibitisha kwa uchunguzi wa Hajjaj, nakubuni hilo jina kwa kuiita: Siku ya Ng'ombe. Seif hakutaka kuikosa fursa ya kubuni'Siku' sawasawa na matukio ya kweli.

B- SIKU ZA ARMATH, AQWAS NA IMAS

Kulikuwa na mapigano yaliyoandaliwa huko Qadisyya kati ya Waislam na Waajemikwa siku tatu. Seif aliita ile siku ya kwanza, Siku ya Armath, ya pili, Siku ya Aqwas,na ya tatu, Siku ya Imas. Amebuni mashujaa wa kabila lake mwenyewe la Tamim,kama vile ndugu wawili Qa'qa na Asim. Tabari ameziandika ngano za Seif nawanahistoria, Ibn Athir na Ibn Kathir wakanakili kutoka kwa Tabari. Hamawi piaamenukuu maandishi ya Tabari kuelezea maneno Armath, Aqwas na Emas. IbnAbdun katika shairi lake, "Ibn Badroon" katika sherehe yake ya mashairi haya naQalwashandi katika kitabu chake The days of Islam - siku za Uislam, ametumiaubunifu wa Seif wa siku hizo tatu hapo juu. Katika kitabu changu 'Masahaba miamoja na hamsini wa kubuni' (Masahaba wa Mtume), nimetoa maelezo zaidi juu yasiku hizo tatu chini ya majina ya Asim na Qa'qa.

CHANZO CHA NGANO YA SEIF

Seif ameziandika hizi Siku kutoka kwa Muhammad, Talha, Ziad na Ibn Mihraq wak-isimulia kutoka kwa mtu wa Kabila la Tay na Ghosn akisimulia kutoka kwa mtu waKabila la Kanana. Tumesema hapo kabla kwamba Muhammad, Talha, Mihraq naZiad walikuwa ni wapokezi bandia wa Seif. Seif ameandika ngano kumi na tatukutoka kwa Ghosn ambaye kwamba hatuwezi kuona dalili zozote katika vitabu vyawasifu, na hatujui ni nani huyu mtu asiyetajwa jina wa kutoka Kabila la Kanana.

C - SIKU YA JARATHIM

Tabari ameandika ngano kumi na tano kutoka kwa Seif kuhusu kule kuvukwa kwaMto Tigris na Sa'd. Hii ni ngano iliyoandikwa na Seif kwa ufupi:

Baada ya Vita vya Qadisyya, jeshi la Waislam lilikusudia kuiteka Madain (makaomakuu ya Uajemi). Sa'd, yule kamanda alitoa hotuba hapo kambini karibu na MtoTigris (Dajla) na akawatahadharisha Waislam juu ya mashambulizi ya maaduikutoka kule mtoni. Aliwaambia kwamba yeye aliamua kuuvuka mto ule. Akauliza,"Nani yuko tayari kuongoza mashambulizi haya?" Asim Ibn Amr akasema kwam-ba yeye atakuwa wa mwanzo kushambulia. Asim pamoja na watu sitini wakaoge-lea mtoni, na wakapigana na adui na wakauteka ule upande mwingine wa mto.Kisha jeshi lote la Waislam likavuka ule mto. Mto ulikuwa umechafuka, lakini askarihao walikuwa wakiongea mmoja na mwingine kana kwamba wanatembea katikaardhi. Wakati wowote farasi akiwa amechoka, ile ardhi chini ya mto ilinyanyukachini ya miguu yake, hivyo farasi huyo akasimama juu yake na kurudisha pumzizake. Hakuna kitu cha ajabu zaidi kuliko hiki katika hii Siku ya Vita vya Madain. Hii

125

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Siku ya Maji inayoitwa Siku ya Jarathim, ikimaanisha Siku ya Kilima Kidogo. IliitwaJarathim kwa sababu hakuna aliyechoka,na kwa sababu kilima kidogo kilinyanyu-ka chini ya miguu yake ili kwamba aweze kupata mapumziko. Seif alisimulia kuto-ka chanzo kingine kwamba askari mmoja alisema, "Tuliogelea katika mto huo namaji marefu sana yalifikia kwenye tumbo la farasi wakati wowote mpanda farasi ali-posimama kwa ajili ya mapumziko.

Mahali pengine Seif anasema kwamba wote walivuka mto huo ila mtu aliyeitwaGharqdeh (ikimaanisha kuzama maji) aliyeanguka kutoka kwenye farasi wake.Mpokezi anasema kwamba inaelekea kwamba alimuona farasi wake akikung'utamaji kutoka kwenye manyoya ya shingoni mwake na mtu huyo akielea. Qa'qaalimvutia ukingoni na kumuokoa. Baada ya kuwa ameokolewa mama yake Qa'qaalimwambia Qa'qa, "Hakuna dada aliyezaa shujaa kama wewe."

Abu Naim ametaja baadhi ya sehemu za historia hiyo hapo juu katika kitabu chakeThe Signs of the Apostleship (Ishara za Unabii), na akazihesabu kama ushahidi wautume wa Mtume wa Uislam.

CHANZO CHA NGANO YA SEIF

Seif ameandika kutoka kwa Muhammad, Talha, Muhallab, Nazr Ibn Rufail na mtuasiyejulikana. Baadhi ya wapokezi hawa tuliwataja hapo kabla. Tabari ameandikangano sitini na saba za Seif kutoka kwa Muhallab, Ibn Oghbeh Asadi, na nganoishirini na nne za Seif kutoka kwa Ibn Rufail. Hakuna dalili za wapokezi hawa zina-zoweza kuonekana katika vitabu vyovyote vya wasifu. Ngano za Seif kutoka kwamtu asiye na jina ni dhahiri kwamba sizo za kweli.

Vita ya Madain kwa mujibu wa wengine mbali na Seif. Hamawi katika juz.4,uk.33,Mu'jamul-Buldan anasema, "Wakulima wa Kiajemi walilisaidia jeshi la Waislamkwa kuwaonyesha sehemu za udhaifu wa Waajemi, kuwapa zawadi na mahitaji.Khalid Ibn Arfata aliwashambulia Waajemi bila mafanikio. Baadae Khalid Ibn Sabataliiteka Madaen. Lile jeshi la Waislam lilielekezwa kwenye sehemu nyembamba zamto huo, hivyo wakavuka kutokea hapo."

Katika Futuuhul-Buldan uk.323 anasema, "Jeshi la Waajemi liliwatupia mishaleWaislam, lakini hakuna hata mmoja aliyeuawa ila askari mmoja kutoka Kabila laTay aliyeitwa Salili Ibn Yazid Ibn Malik Sanbesya."

HITIMISHO

Seif alimfanya Asim kutoka kwenye kabila lake mwenyewe, ingawa ni wa bandia,kuwa ndiye shujaa wa ngano hii. Pia alisema, "Farasi yoyote aliyechoka, kilima kil-itokea chini ya miguu yake." Lakini mtu alianguka kutoka kwenye farasi wake, naile ardhi chini ya mto haikunyanyuka chini ya miguu yake, kwa sababu Qa'qa yulendugu yake Asim alikuwa jirani kumuokoa. Askari wale waliuvuka mto kwa muu-jiza, kwa mujibu wa Seif. Lakini kwa mujibu wa wengine muongozaji aliwaonyesha

126

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

sehemu yenye kina kifupi cha maji, ukanda mwembamba au ukanda wa ardhi.

Uharibifu mkubwa uliofanywa na Seif kwenye historia ya Uislam ni ubuniaji wakewa Masahaba (wa Mtume). Amewataja majina yao kwenye matukio ya uzushi naya kweli, yaliyopotoshwa kwa njia moja au nyingine. Wanahistoria wamenakilimajina ya Masahaba bandia wa Seif na ngano katika vitabu vyao, na Waislamwamelichukulia kwa uzito, na kuamini kwamba hawa watu wa kubuni walikuwahasa ni masahaba wa Mtume.

Ibn Abdulbirr katika kitabu chake al-Istiab, ameandika majina ya watu hawa naanasema, "Hawa ni masahaba wa Mtume baadhi yao wamekutana naye Mtume,wengine wamemuandikia au wametuma zaka zao kwake. Mtu yeyote ambaye jinalake limeandikwa katika tukio lolote linalomhusu Mtume limeorodheshwa. Hapahata wale ambao majina yao na mashina ya koo zao hayakujulikana na hakunahata mmoja aliyewajua ila kupitia kwa jamaa zao wa mbali." Seif amebuni watuwengi na amebadili majina au sifa za baadhi ya watu wanaojulikana vema, ili kupo-tosha mambo, mafundisho ya Mtume, na kuwadanganya watafiti na wanazuonikatika juhudi zao za kunakili matukio ya kweli.

Baada ya miaka mingi ya kazi ngumu na kwa utafiti katika takriban vitabu vyotevya historia ambavyo vimenakili matukio katika siku za mwanzo za Uislam,nimeweza kuja na ngano za uongo na majina yaliyobuniwa na Seif, lenye uharib-ifu zaidi ya yote, likiwa ni ule ubuniaji wa Masahaba. Majina mia moja na hamsiniya Masahaba (wa Mtume) wa uongo waliobuniwa na Seif yameorodheshwa kati-ka kile kitabu 'Hundred and Fifty Invented Sahabis' - Masahaba Mia na Hamsini waKubuni.

127

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

11. MASHAURIANO NA KIAPO CHAUTII KWA UTHMAN

KAMA ILIVYOSIMULIWA NA SEIF

NA WENGINE MBALI NA SEIFULINGANISHO

128

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

MASHAURIANO NA KIAPO CHAUTII KWA UTHMAN

Imeandikwa katika Tabari juz.3,uk.292 miongoni mwa kadhia za mwaka wa 23Hijiria ikinakiliwa kutoka kwa Seif kwamba Umar alisema, "Nina hakika kwambawatu maarufu sana miongoni mwa Waislam hawa wawili (Ali na Uthman) - Mtumewa Mwenyezi Mungu alikuwa akiwasomea wao kile ambacho Jibril alimshushiakutoka kwa Allah." Katika kurasa za 266 na 305, kuhusu matukio ya mwaka wa 24Hijiria imeandikwa hivi: "Katika siku ya tatu ya Muharram, Uthman alishinda kuraza washauri wakati wa mchana. Wakati adhana yaSwala ya mchana ilipopigwa,Uthman alitoka nje ya chumba cha mikutano na kuongoza Swala." Tabari anaandi-ka kutoka kwa Seif pia kwenye uk.305 kwamba pale wajumbe wa ushauri walipopi-ga kura kwa upande wa Uthman, alitoka nje ya ukumbi wa mikutano akionekanamwenye huzuni sana na akapanda kwenye mimbari ya Mtume, na akatoa hotuba.Baada ya kumshukuru Mungu na kumtakia rehma Mtume, alisema, "Enyi watu,mpo katika nyumba ambayo ina msingi dhaifu sana, ukiwapeni ukumbusho wawakati wa uhai wenu. Kabla kifo hakijawakuteni, fanyeni amali njema, kwa sababukifo kinakuja ghafla wakati wa mchana au usiku. Msiache shetani akawadan-ganyeni, msiyachukulie maisha kwa uhakika. Chukueni tahadhari kwa walewaliokufa kabla yenu. Msipoteze muda wenu bure. Jaribuni kadiri ya uwezo wenu.Hamtasahauliwa (mbele ya Allah). Wako wapi baba zenu na ndugu zenu walioli-ma ardhi hii kabla yenu, na wakaiacha? Lengo lenu liwe wokovu wenu. Allah ame-toa mfano kwa maisha haya ya sasa na akasema, 'Wapigie mfano kuhusu maishahaya, yako kama mvua ambayo mimea ya kijani hustawi kama matokeo ya mvua.'"Kisha akasoma mpaka mwisho wa aya hii. Ndipo watu wakaja mbele na kumpamkono kama wafuasi wake.

NGANO YA MASHAURIANO KUTOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

(Umar Khalifa wa Pili, aliteua watu sita kukutana na kuchagua Khalifa wa Tatumiongoni mwao wao wenyewe.).

Ibn Hisham katika kitabu chake As-syra juz.4,uk.334-337 amenakili kutoka kwaAbdulrahman Ibn Auf kwamba wakati wa Hijja huko Mina, mtu mmoja alimwambiaUmar kwamba mtu mmoja alimwambia, "Kama Umar atakufa atamuidhinisha mtufulani wa fulani kama Khalifa, pia uchaguzi wa Abubakr ulikuwa wa ghafla na kosaingawa ulifanikiwa." Umar alimjibu kwa hasira, "Nitalishughulikia jambo hili usikuwa leo, na kuwaonya wale wanaotaka kupora huu urithi wa Mtume, MunguAkipenda." Abdulrahman alimshauri Umar kuahirisha uamuzi wake mpaka warudiMadina kwa sababu walikuwepo watu wa aina zote katika Hija, lakini watu wakub-wa na wanazuoni waliishi Madina. Umar alikubali na walipofika Madina katikaIjumaa ya kwanza, Umar alitoa hotuba na akasema, "Nilielewa kwamba mtummoja alisema kwamba kama Umar atakufa atamuidhinisha Fulani kama Khalifa.

129

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Msiufanye ule usemi, 'uchaguzi wa Abubakr ulikuwa wa ghafla na kosa, lakini uli-fanikiwa' ukawadanganyeni. Hata hivyo ndivyo ilivyokuwa, lakini Mungu alitulinda.Kumbukeni hakuna aliyekuwa maarufu kati yenu kama Abubakr. Mtu yeyoteanayetoa mkono wa kiapo kwa mtu yeyote bila ya kushauriana na Waislam,anaonyesha kiapo chake hakina thamani, na watu wote hao ni lazima wauawe."

Sehemu ya ngano hiyo hapo juu na maoni ya Umar yametajwa kabla paletulipoelezea, "Watu walitafuta kimbilio kwenye nyumba ya Fatimah." Ibn Abil-Hadid, katika juz.2,uk.123 aliandika kutoka kwa Jahiz kwamba Ammar Ibn Yasiralisema kwamba baada ya Umar atamchagua Ali. Hii ilimfanya Umar awahutubiewatu wa Madina akisema, "Watu wengine wanasema Talha Ibn Ubaidullah ndiyemgombea. Haileti tofauti yoyote kuwa mgombea ni nani, lakini jambo ni kwambaMtume hakuwaamuru watu wake kuchagua Khalifa, na yule Khalifa wa kwanzapia, aliingia madarakani kwa uamuzi wa haraka na wenye pupa." Kwa neno mojauchaguzi wa Khalifa haukuwa ni desturi katika Uislam. Ni |Umar tu aliyeamuakuteua watu sita waliomchagua Khalifa wa tatu miongoni mwa wenyewe.

Uamuzi wa Umar ulipangwa kabla ya kupigwa kwake upanga uliomuua, . Tutaonabaadae kama Umar alikuwa na mtu mawazoni mwake kama mrithi wake au la.

USHAURI NA UMAR

Imeandikwa katika al-Ansabul Ashraf ya Baladhuri,uk.15-16 na Tabaqat ya IbnSa'd juz.3, uk.243, kwamba Umar alitoa hotuba siku ya Ijumaa, na baada yakumshukuru Mungu na kumtakia rehma Mtume akasema, "Nimeota kijogookikinidonoa. Nadhani kifo changu kimekaribia. Watu wananiomba niteue mrithi.Mungu hataipuuza dini Yake, au Khalifa na madhumuni ya kumleta Kwake Mtume.Baada ya kufa kwangu, huyo Khalifa atachaguliwa na washauri sita. Mtume ali-wafurahikia kabla hajafa. Ninajua watu wengine watanilaumu kwa kuchukuauamuzi huu. Watakuwa ni wale niliowashawishi kuukumbatia Uislam. Walewanaopinga ni maadui wa Mwenyezi Mungu."

Imeandikwa katika Iqdul-Faraid juz.3,uk.73, kwamba wakati Umar alipodungwa,watu walimtaka ateue mrithi. Yeye alisema, "Mtu bora kuliko mimi hakuchagua mtuna mwingine bora kuliko mimi hakuchagua mtu (alimaanisha Mtume na Abubakr).Abu Ubaidah asingekufa, ningemteua yeye kwani alikuwa ni mtu wa kuaminiwakama Mtume alivyosema. Pia kama Salim yule huru wa Abu Hudhaifa angekuwahai ningemteua kwa sababu alimpenda sana Mungu kiasi kwamba hakufikirikamwe kutenda dhambi, hata bila ya hofu kutoka kwa Mungu." Umar aliombwakumteua mwanae. Akasema kwamba inatosha kwamba Khatab mmoja anawajibi-ka kwa Allah. Alitamani kama angekuwa huru mbele ya Allah, kuweka sawa mazurina mabaya. Kisha akasema kwamba alitaka kuteua mtu wa kuwaongoza kwenyenjia ya haki na akamnyooshea kidole Ali, lakini akasema kwamba bora asimch-ague, kwa sababu hakutaka kuchukua jukumu katika maisha haya, na yajayo. Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.16, kwamba Amr Ibn

130

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Maimoun alisema kwamba kwa kweli alimuona Umar akichomwa upanga naakamsikia akisema, "Nileteeni Ali, Uthman, Talha, Zubair, Abdulrahman Ibn Auf naSa'd Ibn Waqqas." Akamwambia Ali, "Watu wanaweza kutambua kwamba wewe nibinamu ya Mtume na mkwe wake, na u mwenye elimu katika Uislam. Ukiwatawalawatu hawa umuogope Mungu." Akamwambia Uthman, "Watu wanaweza kutam-bua kwamba wewe ni mkwewe Mtume, na u mtu mzima. Ukiwatawala watu hawaumuogope Mungu na usiwaache (ndugu zako) ukoo wa Mu'awiyyah kuwamuduwatu." Kisha akamuita Suhaib, na akamwambia kwamba aongoze Swala kwa sikutatu na awaweke hawa watu (sita) wakiwa wamefungiwa ndani ya ukumbi wamikutano kwa mashauriano. Kama kwa kauli moja watamchagua Khalifa, yeyoteambaye hakumuunga mkono akatwe kichwa chake. Walipoondoka (wale sita naSuhaib), Umar akasema, "Kama watamuacha yule kipara (alimaanisha Ali ambayehakuwa na nywele za mbele ya kichwa chake) atawale, atawaongoza watu vizuri."Mwanae (Ibn Umar) akamwambia, "Basi mteue yeye." Akajibu kwamba hakutakakuchukua hilo jukumu.

Katika Riadhun-Nadhira juz.2,uk.72, baada ya usemi huo hapo juu wa Umarkuhusu Ali, imeandikwa kwamba Umar alisema, "Kama watu wangemuacha yulemwenye paji refu la uso refu (alimaanisha Ali) awaongoze kwenye njia ya haki,angefanya hivyo japo kwa upanga." Akaulizwa, "Kwa nini humteui yeye?"Akasema, "Yule aliyekuwa mbora kuliko mimi hakuteua (mrithi wake)."

Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.17, kwamba Waqedi amese-ma kwamba Umar alipokuwa akizungumzia mrithi, watu walimpendekezaUthuman, Zubair, Talha, Sa'd au Abdulrahman. Alisema kwamba Uthaman ange-toa nafasi za juu kwa jamaa zake. Zubair alikuwa muumin wakati wa amani, naasiyeamini anapokasirika. Talha alikuwa mkereketwa, Sa'd ni mzuri wa kuongozajeshi lakini hangeweza kutawala hata kijiji, na Abdulrahman angeweza tu kumudunyumba yake. Ibn Maimoun alisema kwamba Umar aliacha mrithi wake achaguli-we kutoka miongoni mwa watu sita, na akaomba kwamba mwanae Abdullah IbnUmar awe na hao watu sita, lakini asichaguliwe. Baladhuri ameandika katikaAbsabul Ashraf kwamba Abi Mekhnaf alisema kwamba wakati Umar alipochomwa,alimuamuru Suhaib Ibn Abdullah Jod'an awaite viongozi kutoka Muhajirina naAnsar. Walipofika, Umar akasema, "Nimeyaacha mambo yenu mikononi mwawatu sita waliokuwa watangulizi katika Uislam, na Mtume alikuwa radhi nao wakatialipokufa. Watachagua mmoja kati yao kuwa kiongozi wenu (Khalifa)." Ndipoakawataja hawa watu sita. Alimuamuru Abi Talha Ziad Ibn Sahl Khazraji kuwekatayari askari hamsini kushinikiza suala la kumuunga mkono huyo Khalifa mpya.Aliamuru kwamba uchaguzi huo umalizike ndani ya siku tatu. Alimwambia Suhailaongoze Swala mpaka hapo Khalifa atakapokuwa amechaguliwa. Talha, mmojawa wale wateuliwa sita hakuwepo Madina, Umar akasema kwamba wasimngojeebaada ya siku tatu, na kwamba yoyote yule aliyechaguliwa, awe ndiye Khalifa, namtu atakayempinga akatwe kichwa chake. Kisha Umar akamtuma mtu kwenda

131

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kumjulisha Talha. Lakini Talha alipokuja Madina, Khalifa Umar alikuwa amekufa,na Uthuman alikuwa amechaguliwa kuwa kama Khalifa mpya. Talha alibakianyumbani kwake katika kupinga. Uthuman alimwendea, Talha akasema,"Utauachia Ukhalifa nitakapokuwa sikubali." Uthuman alijibu kwa kukubali, ndipoTalha pia akashika mkono wa Uthu+-+man kama Khalifa.

Imeandikwa katika Iqdul-Faraid uk.20 kwamba Talha alimwambia Umar kwambaalikuwa tayari kumpa mkono ndani ya Msikiti au hadharani . Abdullah Ibn SaadAbisarh alisema kwamba kabla ya Talha kutoa mkono wake wa kiapo, watuwalikuwa na wasiwasi ikiwa kama asingekubali. Uthuman siku zote alimheshimuTalha mpaka alipozuiwa ndani ya nyumba yake kabla hajauawa. Ndipo Talhaalipoonyesha upinzani mwingi kwa Uthaman kuliko mtu mwingine yeyote.

Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf uk.18 kwamba Umar alisema,"Wachache lazima wawatii wengi, na yeyote atakaepinga, mkate kichwa."Imeandikwa pia katika uk.19 kwamba Umar aliwaamuru wale wajumbe wamashauriano kushauriana kwa siku tatu, na kama watu wawili watapiga kurakumpendelea mtu mmoja, na wawili wengine wakampigia mtu mwingine, basi kurazipigwe tena. Kama watu wanne watakuwa upande wa mtu mmoja, na mmoja tuakapinga, basi wanne hao watakuwa kwenye haki, kama watafungana watatu kwawatatu, watatu hao wakikubaliana na Abdulrahman watakuwa washindi kwa ajiliya kile Abdurahmani anacowachagulia Waislamu kitakuwa salama zaidi..Baladhuri katika Ansabul Ashraf juz.5,uk.15, ameandika kwamba Umar alisema,"Watu wengine wanasema kwamba uchaguzi wa Abubakr ulikuwa ni kosa laghafla, Mungu Alitulinda na madhara yake, na Umar hakuingia madarakani kwakupigiwa kura, lakini nimeamua kwamba mrithi wangu achaguliwe kwa majadil-iano. Kama wanne wako upande mmoja, na mmoja katika upande mwingine,chukueni upande wa wanne. Kama palikuwa na watatu dhidi ya watatu, kubalia-neni na wale watatu ambao Abdulrahman atakuwa miongoni mwao. KamaAbdulrahman (atajishika mikono yake miwili) pamoja, mfuateni."

Muttaqi pia ameandika katika Kanzul-Ummal juz.3,uk.160 kwamba Umar alisema,"Atakapojishika Abdulrahman mikono yake miwili pamoja basi mtamchukua yeyekama Khalifa." Muttaqi ameandika pia kutoka kwa Aslam kwamba Umar alisema,"Atakapomtaja Abdulrahman mmoja wao kama Khalifa itawabidi mumtii, na yeyoteatakayejizuia na utii lazima akatwe kichwa." Ngano hizo hapo juu zinaeleza kwam-ba Umar aliyaacha mambo ya Waislam mikononi mwa Abdulrahman, na yalemajadiliano ya wale watu sita aliowateua kumchagua Khalifa yalikuwa tu kamahatua za kiusalama za kuhakikisha mrithi wake anakalia kiti. Ali aliugundua mpan-go wa Umar kama ilivyoandikwa ndani ya Ansabul Ashraf, juz.5,uk.19, kwamba Alialimsikia Umar akipendekeza uthibitisho wa Abdulrahman kwa uchaguzi waKhalifa. Alisema kumwambia ami yake Abbas, "Wallah, tumeupoteza uchaguzi."Abbas akamuuliza, "Umejuaje?" Ali akasema, "Sa'd anampendelea Abdulrahmankwa sababu ni mabinamu. Abdulrahman ni mkwewe Uthuman, na ni rafiki yake.

132

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Hawa watatu wako upande mmoja, hata kama Zubair na Talha wanipigie kuramimi, wao watashinda, na tutapoteza kwa sababu Abdulrahman yu miongonimwao." Karibu mazungumzo hayo hayo yameandikwa katika Iqdul-Faraid,juz.13,uk.74.

Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf, juz.5,uk.20, kutoka kwa Abi Mikhnafkwamba Ali alihofia kama Sa'd, Abdulrahman na Uthuman wangekubaliana pamo-ja. Kwa hiyo alimchukua Hasan na Husein kwenda nao kwa Sa'd na akamwambia,"Ewe Aba Is'haq, sikuja kukutaka unipigie kura badala ya Abdulrahman. Bali kamaAbdulrahman atakuomba uchukue upande wa Uthuman tafadhali usikubali, kwasababu mimi ni ndugu wa karibu mno kwako kuliko Uthuman." Ali akamtajia hiliSa'd na akamkumbusha uhwosiano wake, uhwosiano wa Hasan na Husein nauhwosiano wa Amina mama yake Mtume na Sa'd. Sa'd akamwambia Ali,"Umepewa ulichokiomba." Wakati Abdulrahman alipomtaka Sa'd ushauri, Sa'dalisema, "Ninakupigia kura wewe, lakini simpigii Uthaman, kwa sababu Ali anas-tahili nafasi hii zaidi kuliko Uthuman." Abu Talha (mlinzi mkuu) alikuja kwenyeukumbi wa mikutano kuwasisitiza wafikie uamuzi na akawaambia wale wajumbewa mashauriano, "Mnaonyesha shauku ya majadiliano, lakini mnacheleweshamjadala wenyewe. Inaelekea kila mmoja wenu anatamani kuwa ndiye Khalifa."Abu Talha alipoiona ile hali alitokwa na machozi na akasema, "Niliwategemea waowasiwe na tamaa ya nafasi hiyo, na nilihofia kuwa hakuna kati yao atakayelikubalijukumu hilo la kuwa Khalifa, na kwamba kila mmoja atajaribu kumtupia mwingine."Umar alimteua mwanae kama mjumbe wa mashauriano bila ya kuwa na kura, laki-ni mwanae hakujiunga na baraza hilo kama ilivyoandikwa katika Ansabul Ashraf,juz.5,uk.21.

Abi Mikhnaf alisema kwamba Umar alizikwa siku ya Jumapili na Suhaib aliongozaSwala ya jeneza, na Abu Talha akaongoza ile Swala ya jamaa ya kila siku. Walewashauri hawakuanza kazi yao jioni ile, na asubuhi iliyofuatia walisimamia hazinakwa maombi ya Abu Talha, yule mlinzi mkuu. Abdulrahman aligundua kwambawale washauri walikuwa wakinong'onezana kuwakatisha tamaa wagombea kishaakasema, "Sa'd na mimi tulifuta madai yetu kama wagombea mradi nimchagueKhalifa, kwa sababu watu walikuwa wanangojea matokeo na walitaka kurudikwenye miji ya nyumbani kwao. Wagombea wote walikubali isipokuwa Ali ambayealisema, "Nitalifikiria hili." Abu Talha alikutana nao na Abdulrahman akamwambiaalichopendekeza, na juu ya kutokukubali kwa Ali. Abu Talha alisema kumwambiaAli, "Muamini Abdulrahman na Waislam wengine vilevile. Yeye binafsi siyomgombea kwa sababu halitaki hilo jukumu, kwa nini hukubaliani naye?" Basi Aliakamtaka Abdulrahman kuapa kwamba atakuwa muadilifu na ataupa kipaumbeleustawi wa Waislam mbele mbele kuliko mawazo ya matamanio yake binafsi,Abdulrahman akaahidi. Kisha Abdulrahman akamwambia Ali, "Usiwe nashaka."Hili lilitokea ama ndani ya nyumba ya hazina au katika nyumba ya MiswarIbn Makhrama. Kwa maombi ya Abdulrahman wajumbe wote walitoa ahadi zao

133

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

kwamba yeyote atakayemchagua atakubaliwa. Abdulrahman akauchukua mkonowa Ali na akasema, "Apa kwa Mwenyezi Mungu kwamba nikikuchagua kamaKhalifa, hutawapendelea Bani Abdulmuttalib, na utatenda kwa mujibu wa sunnahya Mtume hasa." Ali akasema, "Nani anaweza kukubali kufanya hasa kama Mtumealivyofanya? Ninaweza kukubali tu kufanya kwa juhudi zangu zote." NdipoAbdilrahman akauchukua mkono wa Uthuman na kumwambia, "Apa kwaMwenyezi Mungu kwamba kama nitakuchagua kuwa Khalifa, hutawapendeleaBani Umayya na utamfuata Mtume, Abubakr na Umar." Uthuman akaapa kutendakama hivyo, na akaahidi. Ali akamwambia Uthuman, "Umepata ulichokitaka."Kisha Abdulrahman akamwambia Ali namna hiyo hiyo. Ali akasema, "Ninaahidikufuata sunnah ya Mtume na kufanya kile ninachodhani kwamba ni sahihi kwamujibu wa Sheria za Kiislam." Wakati huo huo Uthuman aliendelea kusema, "Ninaahidi, kama Mitume walivyomuahidi Mwenyezi Mungu, kutenda kulingana nasunna ya Mtume, Abubakr na Umar."

Ndipo Abdulrahman alipoushika mkono wa Uthuman na kumtangaza kuwa Khalifa.Wajumbe wote wa mashauriano walimpa mikono Uthuman, kuonyesha kumkubalikwao kama Khalifa, isipokuwa Ali aliyebaki amekaa baada ya wengine kuwawamesimama kumthibitisha Uthuman, Abdulrahman akamwambia Ali, "Kubali amasivyo nitakukata kichwa chako." Hakuna mjumbe aliyekuwa amebeba upangaisipokuwa Abdulrahman. Ilisemekana kwamba Ali alitoka kwenye ukumbi wamikutano kwa hasira. Wajumbe wengine walimfuata akubali la sivyo wapiganenaye. Ndipo Ali aliporudi na kupeana mkono wa kiapo na Uthuman.

Baladhuri ameandika katika Ansabul Ashraf, Juz.5,uk.24 kutoka kwa Waqedikwamba baada ya Uthuman kutoka nje ya ukumbi wa mikutano akiwa Khalifa, alik-wenda kwenye mimbari. Alimshukuru Mola na kumtakia rehma Bwana Mtume, naakasema, "Enyi watu, kipando cha mwanzo ni kigumu. Tunao muda mwingi wakutosha mbele yetu. Kama nitakuwa hai nitawaandalieni hotuba. Sikuwamzungumzaji kabla, lakini Mungu atanifundisha jinsi ya kutoa hotuba."

Imeandikwa katika Iqdul-Faraid, juz.2,uk.140, kwamba Uthaman alikuwa mmojawa wale walioona vigumu kutoa hotuba. Imeandikwa pia katika albaian-wat-Tabieen kwamba Uthuman alifanya makosa fulani fulani katika mimbari pale ali-posema, "Enyi watu, Abubakr na Umar walikuwa wakitayarisha hotuba zao kabla."Abi Mekhnaf anasema kwamba Uthaman ndani ya mimbari alisema, "Sikuandaahotuba na kamwe sijawahi kutoa moja .Kwa mapenzi ya Mungu, nitarudi hivipunde na kuongea nanyi." Imesimuliwa pia kwamba Uthaman alipanda kwenyemimbari na kusema, "Hatuna uzoefu wa kuhubiria watu, kama tuko hai Inshaallah,mtasikia hotuba nzuri. Niwaambie sasa kwamba kwa sheria ya Mungu, Ubaidullahmwana wa Umar amemuua Hurmuzan. Hurmuzan alikuwa Mwislamu lakinihakuwa na mrithi, mimi kiongozi na Khalifa nitamsamehe muuaji. Je, mnamsame-he?" Wote walijibu kwa kukubali, ila Ali aliyependekeza hukumu ya kifo kwa muua-

134

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

ji na akamnyooshea kidole Ubaidullah, akisema, "Oh wewe mnafiki, kamaningekupata ningekuua katika kulipiza kisasi kwa ajili ya kumuua Hurmuzan."

Tabari katika kitabu chake juz.3,uk.292-302, ametengeneza ngano moja kutokakwenye ngano zote hapo juu, na amefupisha baadhi ya sehemu zake kiasi kwam-ba matukio hayo hayakuelezewa sawasawa. Ameandika hii hotuba ya Uthamankutoka kwa Seif peke yake. Tumeandika kidogo hapa kuhusu 'Ushauri' kuonyeshatofauti kati ya Seif na wengine katika kuyaandika matukio. Tutaelezea zaidikuhusu mjadala wa wajumbe wa ushauri katika ukumbi wa mikutano baadaye. Seifhakupotosha kadhia hiyo hapo juu, lakini amebuni mamia ya ngano kuwalindawatawala wa wakati huo, na watu mashuhuri. Tabari ameonyesha upenzi maalumwa kuandika kutoka kwa Seif. Mtu yeyote kama atakaposoma matukio ya miakaya 11-37 Hijiria kutoka kwenye kitabu cha Tabari, atagundua ni kiasi gani matukiohayo yamebuniwa na/au kugeuzwa.

135

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

12. QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZAN

KWA MUJIBU WA SEIF:

KUTOKA KWA SEIF

TOKA KWA WENGINE MBALI NA SEIF

ULINGANISHO

136

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

QUMMAZBAN MWANA WA HURMUZANKWA MUJIBU WA SEIF

Abi Mansur alimsikia Qummazban akisema, "Waajemi wanaoishi Madina walikuwawakitembeleana - safari moja baba yangu alikutana na Firuz akiwa ameshika jam-bia lenye ubapa kila upande. Baba yangu akamuuliza Firuz, 'Kwa nini unalitakajambia hili?' Firuz akasema, 'Nitakata.' Baada ya Umar kujeruhiwa, mtu mmojaakasema kwamba alimuona Hurmuzan akimpa Firuz jambia lile. Ubaidullah (mtotowa Umar) ndipo akaenda kumuua Hurmazan (baba yangu). Wakati Uthumanalipokuwa Khalifa, aliniambia nilipize kisasi juu ya Ubaidullah na nimuuwe. Kilamtu alitaka Ubaidullah auawe isipokuwa wachache walioniomba nimsamehe.Nikawauliza kama nilikuwa na haki ya kumuua (Ubaidullah), wakakubali. Kishanikawauliza, 'Mnaweza kunizuia kumuua muuaji wa baba yangu?' Walijibu kuwahawawezi na wakamuapia Ubaidullah. Hata hivyo nilimsamehe Ubaidullah, yotekumridhisha Mungu na watu wale. Ndipo watu wale wakaninyanyua na kunipele-ka nyumbani kwangu wakiwa wamenibeba juu ya mabega yao." (Mwisho wangano ya Qummazban).

Seif katika ngano ya pili ameandika kwamba Abdulrahman Ibn Abubakr alisema,"Usiku wa jana nilimuona Abu Lulu (Firouz) akiongea na Jufaina na Hurmuzan.Waliponiona wakatawanyika haraka haraka. Walidondosha jambia lenye bapambili. Lilikuwa ndiyo silaha iliyotumika kumkatia Umar. Ni watu wachache tuwalioruhusiwa kubakia pale ndani ya Msikiti baada ya kukatwa kule.

Mmoja wao mtu wa kutoka kabila la Tamimi, alimfukuza Abu Lulu, akamkamata,akamuua, na akaleta lile jambia pamoja na yeye (Abu Lulu). Lilikuwa ni lile jambialililoelezwa. Ubaidullah mtoto wa Umar alisubiri mpaka baba yake alipokufa, ndipoakamuua Hurmuzan na Jufaina ambaye alikuwa ni mwalimu wa Kikristo. Suhaib(Gavana wa muda), Gavana wa Madina alimtuma Amr Ibn Al-Aas kumtia mbaroniUbaidullah. Amr Ibn Aas alijaribu mara nyingi mpaka akilipata lile jambia na kum-tia mbaroni Ubaidullah."

NGANO KAMA ILIVYOELEZWA NA WENGINE MBALI NA SEIF

Tabari ameandika kutoka kwa Miswar Ibn Makhrama kwamba baada yaUbaidullah (mtoto wa Umar) kumuua Hurmuzan, Jufaina na binti ya Abu Lulu,alisema, "Wallah, nitawauwa wale ambao wanahusika na kifo cha baba yangu."Sa'd aliuchukua ule upanga kutoka kwa Ubaidullah na kumfunga ndani ya nyum-ba yake mpaka Uthuman alipotoka ndani ya nyumba yake na kuwaambia baadhiya Ansari na Muhajir kuhusu maoni yao juu ya Ubaidullah kama muuaji wa watuwasio na hatia. Ali akasema kwamba ni lazima auwawe. Baadhi ya Muhajirwakasema, "Umar ameuawa jana, na mwanae auawe leo?" Amr Ibn Aasakamwambia Uthuman, "Una bahati kwamba damu ilimwagwa kabla hujawa

137

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Khalifa."

Tumetaja hapo kabla kwamba Baladhuri katika ile ngano ya mashauriano alisemakwamba Khalifa Uthuman katika kutokea kwake kwa mara ya kwanza hadharanialisema, "Kwa sheria ya Allah, Ubaidullah amemuua Hurmuzan. NinamsameheUbaidullah kwa niaba ya Waislam wote kwa sababu, Hurmuzan hana mrithi."Kisha Uthuman akaomba idhini ya Waislam. Wote walikubali isipokuwa Aliambaye alisema, "Huyu mnafiki lazima auawe, kwa sababu ameua Waislam wasiona hatia." Kisha akamnyooshea kidole Ubaidullah na kusema, "Nitakuua kulipizakisasi cha Hurmuzan." Uthuman akasema, "Nitalipa fidia ya damu ya kuuawaHurmuzan." Ziad Ibn Labid Bayazi akatunga ubeti ufuatao kuhusu mauaji yaHurmuzan:

Ubaidullah, ilikuwa ni uovu kwako kumuua Hurmuzan,Mwislamu asiye na hatia, bila sababu ya maana.Uthuman alikulinda, na akaokoa damu yako,Lakini hakuna atakayekulinda kutokana na kisasi cha Mungu.

Ubaidullah alilalamika kwa Uthuman naye akamuamuru Ziad aache. Ndipo Ziadakatunga ubeti ufuatao dhidi ya Uthuman:

Aba Amr wakati Ubaidullah alipochomoa upanga wake,Alikuwa anataka kutenda kosa, Wallah.Kumsamehe mhalifu na kutenda dhambi,Hivi mashujaa wawili wanafikia mwisho kwa wakati mmoja.Huna haki ya kumsamehe muuaji,Na kama ukifanya hivyo, nina hakika unakosea.

HITIMISHO

Seif anasema kwamba Hurmuzan alikuwa na mtoto wa kiume, Qummazban. Piaanaandika ngano kutoka kwa mtoto huyo. Wanahistoria wengine wanasemakwamba kwa sababu Hurmuzan hakuwa na mrithi, Khalifa Uthuman alimsameheUbaidullah kwa niaba ya Waislam mbali na kufidia kwake damu ya Hurmuzan. Seifpia anasema mtu kutoka kabila la Tamimi alimuua Abu Lulu kuthibitisha heshimakwa ajili ya mmoja wa jamaa yake wa kikabila asiyejulikana.

138

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

13. MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF.

ULINGANISHO

139

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

MIJI ILIYOBUNIWA NA SEIF

Seif amebuni baadhi ya miji kama vile Dolouth, Tawus, Alejrana Wa Na'manaleraq,Alqordouda, Nhar-att, Thanyya Thanyyatul Rakab, Qodais, Wayakhord, Alwalajana Alhawafi, ambayo inatajwa na Hamawi ndani ya Mujamul-Buldan, na Tabari nawengineo.

Yaqut Hamawi alikuwa muangalifu sana kuandika ngano adimu na za kipekeekatika kitabu chake Mujamul-Buldan. Ameandika nyingi ya ngano za Seif katikakitabu chake anapoelezea mambo ya ajabu kuhusu mahali au mji. InavyoonekanaHamawi alikuwa na muswada wa kitabu cha Seif kama inavyoweza kuonekanawakati anaporejea kwa Jubar, Ja'rana, Shairja na Sahid katika kitabu chake chajogorafia, Mujamul-Buldan. Muswada huo uliandikwa kwa mkono na AbibakrMuhammad Ibn Ahmad Ibn Abdulbagi Albaghdadi Hafidh (kafa 489 Hijiria)12.

Alikuwa akiitwa Ibn Khaziba na ameandika baadhi ya maoni katika pambizovilevile, na amesimulia kutoka kwa Abibakr Alkhatie. Katika pambizo hizo kulikuwana maoni yaliyotolewa na Abibakr Ibn Seif. Alikuwa ama ni Abibakr Ahmad IbnBakr Ibn Seif Jessaini, ambaye wasifa wake umeandikwa na Hamawi na Sam'ani,chini ya jina Jessaini, au Abubakr Ahmad Ibn Abdullah Ibn Seif Ibn Said Sajestaniambaye kutoka kwake Ibn Asakir ameandika ngano zote za Seif, na Ibn Nadimameandika jina lake katika kitabu chake, Alfihrist, uk.119 kwa jina la UbaidullahSajestani. Hamawi ameandika baadhi ya ngano za Seif katika kitabu chake kwanamna ileile kama Tabari, lakini kuna tofauti moja kati yao. Tabari ameandikamatukio kwa namna ambayo matukio machache yanafanya ngano kamili. Pia ana-toa kama kawaida, vyanzo vyake vya habari. Lakini Hamawi wakati mwingineameandika sehemu ya tukio, kwa sababu alipenda ule mtindo wa ushairi aunathari ambayo limeandikiwa. Wala halitaji jina la Seif katika (matukio) mengi yao.Tunaweza kuona baadhi ya ngano za Seif kwa Hamawi ambazo hazikuandikwandani ya Tabari na kinyume chake. Kila mmoja wa wanahistoria hawa wawiliamechagua zile tungo za Seif zinazokidhi malengo yake mwenyewe. Hamawiameandika vipande kutoka kwa Seif chini ya majina ya miji kama ifuatavyo:

1. DOLUTH

Mtu kutoka kabila la Abdulqais anayeitwa Suhara anasema, "Katika Vita vyaHurmazan, vilivyotokea pale Ahwas, mji ulio kati ya Doluuth na Dujail, nilimkutaHarim Ibn Hayan na nikachukua kichanga cha tende toka kwake…………… n.k."

12 Tarikhul Kamil juz.10,uk.178; Shazarat-u-Dhahab, Matukio ya mwaka wa 489 Hijiria; Lisanul Mizanjuz.6,uk.57, 479; na Tadhkiratul Hafidh al-Dhahabi, uk.1224.

140

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

Tabari ameandika katika juz.1,uk.2537, mwaka wa 13 Hijiria ngano hiyo hapo juumpaka "kichanga cha tende". Ambapo Hamawi anaendelea katika kuandika kwakezaidi ya Tabari. Kwa hiyo Hamawi anaweza kuwa hakuandika kutoka kwa Tabarina lazima awe alipata ujuzi zaidi wa muswada wa Seif.

2. TAWUS

Hamawi anasema kwamba ni mahali katika jimbo la Fars (ndani ya Iran). Seifalisema kwamba Ala Ibn Hazrami alituma kikosi kwa njia ya baharini kwendaTawus bila ridhaa ya Umar. Hamawi ameiandika ngano hii ambayo pia imeandik-wa na Tabari kutoka kwa Seif katika juz.1,uk.2545-2551, mwaka wa 17 Hijiria, laki-ni Hamawi ameandika pia shairi lililotungwa na Khalid Ibn Munzir ambalo Tabariameliacha.

4. JI'RANA NA NA'MAN

Ni sehemu mbili katika Iraq kwa mujibu wa Seif, kama ilivyoandikwa na Hamawi.Hamawi amelitaja jina la Seif katika sehemu kumi au zaidi. Lakini kuna miji mingiambayo ameandika juu yake katika kitabu chake bila ya kutaja jina la Seif.Msomaji wa habari za baadae anaweza kudhani kwamba Hamawi ameelezamaoni yake mwenyewe, mfano ni Qorduda.

4. QORDUDA

Wakati Tulaiha, yule mtume wa uongo alipofika Sumeira, alipokea ujumbe kutokakwa Thamama Ibn Oas Ibn Lam Altai usemao, "Nina watu kama mia tano, kamaunataka msaada wowote. Tupo hapa Qorduda na Ansur kwenye michanga."

Hamawi amechukua ngano hiyo hapo juu kutoka kwa Tabari 13. Ibn Hajar pia ame-tumia taarifa zilizochukuliwa kutoka kwa Tabari alipokuwa akiandika wasifa waThamama. Hakuna dalili ya Qorduda na Thamama popote pale isipokuwa kwenyengano za Seif.

5. MTO UTT

Khalid Ibn Al-Walid alimtuma mmoja wa majenerali wake anayeitwa Utt Ibn Abi-Oh,aliyekuwa anatoka kwenye kabila la Bani Sa'd, kwenda Duwraqestan. Jeneralihuyo aliweka kambi kando ya mto na baadae mto huo uliitwa Mto Utt kwa jina lajenerali huyo. Msomaji tena anaweza kufikiri kwamba Hamawi ameandika hilokwa maamuzi yake mwenyewe, hata hivyo ameiazima ngano hiyo kutoka kwaTabari. Ibn Hajar pia ameandika ngano hiyohiyo ambayo inaelezea neno Utt (kuto-ka kwa Tabari).14

13 Tabari juz.1,uk.1892; Ertedad Ghetpan, mwaka wa 11 Hijiria.14 Tabari juz.1,uk.2052; habari kufuatia Hayrih.

141

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

6. IRMATH AGHWATH NA AMAS

Majina haya yaliyoelezwa na Hamawi yameazimwa kutoka kwa Tabari kama tulivy-oelezea hapo kabla kwenye vita vya Qadisyya.

7. ALTHENI, THANYA TALKERAB, AL QODAIS, AL MAQR, WAYAKHURDWALAJA NA ALHAWAFI

Ni baadhi ya majina Hamawi aliyoazima kutoka kwa Tabari, juz.1,uk.2026, 2648,2230-33, 43, 65, 88, 94, 2326-38, 2037-38 na 2618-25 na pia 2169 kimpangilio bilaya kutaja jina la mbuniaji wao Seif. Hamawi ameandika juu ya sehemu nyingine namiji katika kitabu chake Mujamul-Buldan. Amezipata kutoka kwenye kitabu chaSeif, na tunashindwa kuzipata kwenye vitabu vingine vyovyote vya jogorafia auhistoria, kwa majina:

1. Safat Jaziratul-Arab, cha Abi Muhammad Alhassan Ibn Ahmad Ibn YaqubIbnYusuf Ibn Daud, anayejulikana kama Ibn Haik (kafa 334 A.H - 945/6 A.D.).

2. Futuuhul-Buldan, cha Baladhuri.

3. Mukhtasarul-Buldan, cha Abibakr Ahmad Ibn Muhammad Hamdani anayejulikana kama Ibn Faqih aliyeishi katika karne ya 3 Hijiria.

4. Atharul-baqua anil Quruunil khaliah, cha Aburaihan Muhammad Ibn Ahmad al-Birouni Kharazmi (kafa 440 A.H.)

5. Mujam Mastu'jim, cha Abi Ubaid Abdullah Ibn Abul-Aziz Ibn Mas'ab AlbakriAlwazir (kafa 478 A.H.)

6. Taqwimul-Buldan, cha Ismail Sahib Hama (kafa 432 A.H.)

Wanajogorafia wawili wa wakati mmoja hawakumwamini Hamawi na hawakuzita-ja sehemu hizo katika vitabu vyao.

1. Lesyrenj, kitabu chake ni: Cities of East Khalifate (Miji ya Ukhalifa waMashariki)

2. Umar Reza Kehala, kitabu chake ni: Geography of Arabian Peninsula(Jogorafia ya Peninsula ya Arabia).

142

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

14. SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZO

ULINGANISHO

143

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

SEIF NA TAREHE ZA KADHIA HIZOSeif hakubuni ngano tu, bali pia amezibadili tarehe za kadhia za kweli.

1. Tabari juz.2,uk.553-56 kuhusu Vita vya Ubolla,15 ameandika kutoka kwa Seifkwamba Abubakr alimtuma Khalid kwenda Iraq. Wapagani walikuwa wamepi-ga kambi kati ya ugavi wa maji na jeshi la Khaud. Allah akatuma mawingu yamvua kuwasaidia Waislam. Waislam walipigana na kushinda Vita hivyo vyaUbolla. Khalid alipeleka moja ya tano ya ngawira (kama kodi) na Tembo mmojaMadina. Wanawake wa hali ya chini wa Madina wakauliza, "Huyu Tembo nikiumbe cha Allah au ametengenezwa na binadamu?" Kisha Tabari anasema,"Vita vya Ubolla vina tofauti kubwa sana kama ilivyoandikwa na wanahistoriawa kuaminika, vilitokea wakati wa Umar, katika mwaka wa 14 Hijiria na kaman-da alikuwa ni Utba Ibn Ghazwan na siye Khalid."

Seif ameweka tarehe isiyo sahihi ya kisa hicho na vilevile akawawasilishakinyume kamanda na Khalifa.

2. Tabari katika juz.2,uk.89 ameandika kwamba Umar alimtuma Utba IbnGhazwan kwenda Basra katika mwaka wa 14 Hijiria na Seif ameandika mwakawa 16 Hijiria. Ibn Kathir ameiandika tofauti hii katika juz.7,uk.47-48 ya kitabuchake.

3. Ile kadhia ya Yarmuuk, imeandikwa katika juz.7,uk.61 na Ibn Kathir kwambakadhia ya Yarmuuk ilitukia katika mwaka wa 15 Hijiria kwa mujibu wa Laith IbnSa'd , Ibn Lahba'a, Abima'shar, Walid Inb Muslim, Yazid Ibn Ubaida, Khalifa IbnKhayat, Ibn Kalbi, Muhammad Ibn Aiz, Ibn Asakir na msomi wetu Dhahabi, laki-ni Seif na Tabari wanasema kwamba ilitokea mwaka wa 13 Hijiria. Ibn Kathirtena ameitaja kadhia hii katika marejeo yake ya kwenye mwaka wa 13 Hijiria.Ibn Asakir juz.1,uk.159 anasema, "Seif amesema kwamba kadhia hii ilitokeakatika mwaka wa 13 Hijiria kabla ya kutekwa Damascus lakini hakuna hatammoja aliyekubaliana naye."

4. Kadhia ya Fihl. Imeandikwa katika juz.7,uk.25,ya Ibn Kathir, "Ile kadhia ya Fihlilitokea kabla ya kutekwa Damascus kwa mujibu wa wanahistoria wengi. LakiniAbujafar Ibn Jazir (Tabari), akimfuata Seif, anasema kwamba ilitokea baada yakutekwa Damascus." Baladhuri ameandika katika Futuuhul-Buldan,uk.137,"Inasemekana kwamba ile kadhia ya Fihl wa Jordan ilitokea siku mbili kabla yamwezi wa Dhilqada haujaisha, hii ni kusema, miezi mitano baada ya Umar kuwaKhalifa."

15 Ubolla ni jina la mji karibu na ule Mto Tigris na Basra. Basra ilikuja kuwa mji katika wakati wa Umarambapo Ubolla, mji wa zamani kabisa, ulikuwa makao makuu ya jeshi kwa amri ya Kasra, kutokaMujamul-Buldan.

144

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

5. Kuondoka kwa Hercules kutoka Syria . Tabari ameandika kwenye kitabu chakejuz.3,uk.99 "Hercules aliondoka Syria kwenda Constantinople katika mwaka wa15 Hijiria kwa mujibu wa Ibn Is'haq. Lakini kulingana na Seif lilikuwa ni mwakawa 16 Hijiria." Ibn Kathir ameitaja tofauti hii katika kitabu chake juz.7,uk.53.Baladhuri amekubaliana na Abu Is'haq katika Futuuhul-Buldan uk.162

6. Kutekwa kwa Orshelim: Tabari juz.3,uk.103 ameandika kutoka kwa Seif,"Mkataba kati ya Umar na Wapalestina ulikuwa katika mwaka wa 15 Hijiria." IbnKathir juz.7,uk.57ameandika kwamba kutekwa kwa Palestina kulikuwa katikamwaka wa 16 Hijiria kwa mujibu wa wanahistoria wote isipokuwa Seif. Baladhurikatika uk.165-166, anasema kwamba hii ilitokea katika mwaka wa 16-17 Hijiria.

7. Kutekwa kwa Algire: Tabari ameandika katika juz.3,uk.155: "Katika mwaka wa17 Hijiria, Algire ilitekwa kwa mujibu wa Seif." Lakini Ibn Is'haq anasema ilikuwakatika mwaka wa 19 Hijiria. Ibn Kathir katika juz.7,uk.76 na Hamawi katikaMujamul-Buldan wameitaja tofauti hii. Baladhuri katika uk.204-205amekubaliana na tarehe za Ibn Is'haq za mwaka wa 19 Hijiria.

8. Tauni ya Amawas: Tabari ameandika katika juz.3,uk.161-163, "Ibn Is'haqanasema kwamba ilikuwa kwenye mwaka wa 18 na Seif anasema kwambailikuwa katika mwaka wa 17 Hijiria." Ibn Kathir ameandika zile simulizi kuhusuTauni hii katika kitabu chake, juz.7,uk.77-79 na amelitaja kosa la Seif na katikauk.78 amasema, "Muhammad Ibn Is'haq na Abuma'shar na baadhi ya wengi-neo wanasema kwamba ilitokea katika mwaka wa 18." Baladhuri ameandikakatika Futuuhul-Buldan uk.165 kwamba ile Tauni ya Amawas ilikuwa katikamwaka wa 18 Hijiria.

9. Ile kadhia ya baina ya Waajemi na Waislam: Tabari ameandika kwamba kwamujibu wa Seif, ilitokea katika mwaka wa 15, lakini alikuwa katika mwaka wa16 kulingana na Ibn Is'haq na Waqedi. Ibn Kathir ameitaja tofauti hii katikajuz.7uk.60 wa kitabu chake.

10. Vita vya Korasani: Tabari katika juz.3,uk.244 na Ibn Kathir katika juz.7,uk.126wameandika kutoka kwa Seif kwamba ilitokea katika mwaka wa 18 Hijiria, laki-ni wengine wanasema ilitokea katika mwaka wa 22 Hijiria.

11. Vita vya Tabaristan: Waqedi, Abuma'shar na Madaini wameandika kwambaSa'd Ibn Aas alipigana huko Tabaristan katika mwaka wa 30 Hijiria. Lakini Seifanasema kwamba Suwaid Ibn Muqarran aliifanya mikataba ya Tabaristan kati-ka wakati wa Umar (nyuma kabisa kabla ya mwaka wa 30 Hijiria).

145

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

HITIMISHO

Kwa miaka mingi, nimefanya utafiti makini katika historia ya Uislam, visa naSunnah za Mtume Muhammad (s.a.w.w.). Mwaka 1949 nilizikuta ngano za Kiislamzenye kutia mashaka katika Vitabu vya Historia vya Kiislam. Nilishangazwa kwam-ba katika mifano mingi, ukweli umepuuzwa na/au kuachwa. Badala yake uongo nawatu bandia vimejitokeza katika vitabu vya historia, na hususan katika miaka yamwanzoni ya Uislam, yaani, zama za Makhalifa wanne wa mwanzo na utawala waBani Umayya (hasa Mu'awiyya).

Nimefuatilia uongo huu na hawa watu wa bandia katika vingi ya vitabu vinavy-opatikana, khususan vile maarufu, ambavyo vimekuwa kwa kawaida ndiyo vyan-zo (rejea) vikuu vya habari kwa wanahistoria wengine na (hata) wanahistoria waMagharibi waliobobea hasa kwenye Historia ya Kiislam.

Baada ya uchunguzi makini, nilitosheka, bila ya kiwingu chochote cha mashaka,kwamba baadhi yake zimeghushiwa kwa malengo maalum. Chanzo cha uongo nahawa watu bandia (wa kubuni) ni Seif Ibn Umar al-Tamimi, mwandishi wa al-Futuuh al-Kabir Wal-Riddah na al-Jamal wal Masiir Ayeshah wa Ali. Seif anato-fautiana na waandishi wa kweli siyo tu katika maandishi bali hata katika Sanadikwa kutumia simulizi za watu ambao hawapo. Seif alizibuni ngano hizi na watuwasiokuwepo ili kuwaridhisha wale waliotaka kuufunika ukweli na kuwasilishamatukio ya historia kinyume kabisa na yalivyokuwa.

Baadhi ya wanahistoria waliziona ngano za Seif zikikubaliana na hisia zao, kwasababu tu Seif amebuni katika ngano zake watu wenye fadhila ajabu, mashujaana watu wenye uzuri wa kipekee na busara kutoka kwenye watawala wa wakatihuo, magavana na makamanda wa majeshi. Amebuni pia mambo ya ajabu,kinyume kabisa na kanuni za desturi asili ili kuzifanya zionekane kama ni miujiza,kama mchanga kugeuka kuwa maji, bahari kugeuka kuwa mchanga na ng'ombekuongea na watu kuonyesha mahali walipojificha kwa jeshi la Waislam, n.k.

Zaidi ya hayo, hao watawala, magavana, makamanda na watu mashuhuri katikamiaka ya mwanzo ya Uislam, walijihusisha binafsi katika mambo ambayo yalikuwahayafai. Ngano za Seif zilizifunika dosari zile kwa visingizio dhahiri, na hivyoamezuia shutuma dhidi yao.

Kwa mfano tunayaona yafuatayo katika maandishi ya Seif:

1. Seif ameandika kwamba Ali Ibn Abi Talib, alitoa kiapo cha utii kwa Abubakr sikuileile watu wengine walipotoa viapo vyao!! Ambapo, ukweli ni kwamba Alialikataa kutoa ridhaa yake na kiapo mpaka na baada ya mke wake (binti yaMtume, Fatima) alipofariki.

146

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

2. Seif ameandika kwamba Sa'd Ibn Ubadah, bila kupenda alitoa kiapo chake!!Ambapo ukweli ni kwamba alikataa kutoa kiapo chake cha utii, na kwa matokeoya hili, aliuawa kule kwenye sehemu yake ya uhamishoni, Howran.

3. Seif ameandika kwamba wale watu wote kutoka makabila mbalimbali, walioam-riwa kuuawa, na wake zao walichukuliwa kama wafungwa wa kivita walikuwaMurtadi (waliokubali Uislam na baadae wakaukana!!). Ambapo, ukweli ni kwam-ba walikataa kutoa kiapo cha utii kwa Abubakr.

4. Seif ameandika Hadith ya Mtume, alipokuwa anajulisha juu ya mwanamkeanayepanda ngamia na kukaribia Hauwab kuwa ni Ummu Zumal !! Tunajuasasa kwamba alikuwa ni Ayishah, Ummul-Mu'minin (binti yake Abubakr na mkewa Mtume).

5. Seif ameandika kwamba Mughaira Ibn Sho'abih (yule Gavana wa wakati waUmar) alikuwa ndani ya nyumba yake, alipoonekana akijamiiana namwanamke, wale waliomuona hawakuweza kumuona huyo mwanamke naangeweza kuwa ni mke wake !! Tumegundua, kwamba maandishi ya wengineyanapingana na hili kabisa. Mughaira Ibn Sho'abih alikuwa katika nyumba yaUmmu Jamil na alikuwa akijamiiana na mwanamke huyu, pale alipoonekana.

6. Seif ameandika kwamba Abu Mahjan Thaqafi alifungwa wakati wa Umar,kutokana na shairi alilolisoma lenye kupendelea pombe !! Ukweli ni kwambaalikuwa hasa amelewa wakati wote.

Pengine baadhi ya wanahistoria wa Magharibi wamekipata pia walichokuwawanakitafuta katika ngano za kubuni za Seif, hicho ni, mauaji mengi na tabia zakikatili zinazofanywa na majeshi na askari wa Uislam. Tumeona katika ngano zaSeif kwamba Khalid Ibn Walid alishughulika kwa siku tatu usiku na mchana kuka-ta vichwa wale wafungwa wa kivita; kwa nyongeza, tumeona kwamba Khalid ali-wakata vichwa hata watu wasiokuwa na hatia, yote haya kwa sababu Khalid ali-apia kwamba 'atafanya mto kutokana na damu yao' !! Upuuzi usio shaka.

Wanahistoria wa Magharibi wamesoma katika ngano za Seif kwamba ile idadi yawatu waliouwawa katika nyingi ya vita katika siku za mwanzoni za Uislam ilikuwaimevuka zaidi ya laki moja, kudhihirisha tabia za unyama na ukatili wao wakuwaangamiza wanadamu kama Hekalu na Mongole.

Wameona katika maandishi ya Seif kwamba Waislam wengi nje ya mzunguuko waMakka na Madina walikuwa Murtadi baada ya Mtume Muhammad (SAW), nawalikuwa wasilimishwe tena kwa nguvu na kwa upanga, kuashiria kwamba Uislamuliendelea na kupanuka kwa mabavu !!

Na hatimae, hao wanahistoria wa Magharibi wamejua kupitia maandishi ya Seifkwamba Myahudi anayeitwa Abdullah Ibn Saba, alikuwa na athari sana kwawafuasi wa mara baada ya Mtume, kugeuza mawazo yao kutoka kwenye

147

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

mafundisho makuu ya Uislamu kusababisha uasi, uliowafanya kumuuwa Khalifa.Yote haya yametokea kama matokeo ya jitihada za Myahudi wa ajabu !! n.k.

Pengine, wanahistoria wa Magharibi walizipenda sana ngano za Seif kiasi kwam-ba waliegemeza kazi ya uchanganuzi wao juu ya maandishi ya Seif nahawakuhangaika kuchimbua kwenye maandishi ya wengine na hawakutaja juu yavitabu vyenye kutegemewa zaidi.

Baada ya utafiti makinifu katika maandishi ya Seif ndani ya al-Futuuh Wal-Riddahna al-Jmal wa Masiir Ayeshah wa Ali, tunafikia kwenye ukweli huu hasa, kwambamaandishi ya Seif yameathiri kwa kiasi kikubwa sana waandishi wengine wengi,pamoja na waandishi mashuhuri kama vile Tabari, Ibn Athir, Ibn Kathir na IbnKhaldun. Zaidi ya hayo, tunapolinganisha maandishi ya Seif na yale ya maandishimengine, tunafikia kwenye uamuzi huu kwamba baadhi ya wanazuoni wengi waHadithi walikuwa na haki kabisa kusema kwamba: "Seif alikuwa mdanganyifu namwandishi muongo."

Kiasi Seif alivyokuwa zindiq (zandiki, mnafiki), ambao baadhi ya wanazuoni waHadithi na wasomi wamemshutumu, kinavyohusika, tutalijadili jambo hili katika kilekitabu - 'One hundred and Fifty Sahabis Mukhtalagh' (Masahaba 150 wasiowahikuwepo). Katika kitabu cha tatu, tutajaribu kukijadili na kukichambua kitabu chaSeif, al-Jamal…Seif alikiandika kitabu hicho kwa nia ya kuelezea kile chanzo chamaasi katika wakati wa Khalifa Uthuman, kuwalinda watawala wa Bani Umayyakama vile Mu'awiyya na Abdullah Ibn Abi Sarh, na tutaelezea sababu ambazoWaislam katika nchi mbalimbali walikuwa wamechukia na kukirihishwa nawatawala wa Bani Umayyah, n.k. Tutajaribu kuzichambua Ngano hizi, vyanzo nawapokezi wake katika kitabu hicho cha tatu .

148

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO

149

ABDU`L-LAH IBN SABA`NA NGANO NYINGINEZO